Katibu wa maendeleo ya jamii katika jiji
la Abuja Nigeria, ametangaza ‘kiama’ kwa wanawake wanaofanya ‘biashara
ya kujiuza’ pamoja na wateja wao.
Taarifa iliyochapishwa na Today Internet Newspaper
imesema, katibu mkuu huyo Blessing Unoh amesema serikali imetoa amri ya
kusitisha biashara hiyo ndani ya saa 48, kwa yeyote atakayekiuka hatua
kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.
↧