Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all articles
Browse latest Browse all 45270

TAKUKURU Yarejesha Zaidi Ya Shilingi Milioni15 Zilizokuwa Zimeliwa Na Wajanja Kahama

$
0
0
SALVATORY NTANDU
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga imefanikiwa kurejesha  fedha shilingi milioni 15,056,125 kwa walimu wastaafu na halmashauri ya Msalala zilizokuwa zimetumikia kinyume na zimetumika kinyume na utaratibu ulipangwa na taasisi hizo.

Akizungumza katika hafla ya Kukabidhi fedha hizo Mjini Kahama  Julai 2,2020 Mkuu wa TAKUKURU wilaya ya Kahama Cosmas Shauri alisema kuwa fedha hizo zimegawanyika katika makundi mawili ambapo kundi la kwanza ni  shilingi milioni 7,780,625 za Kahama walimu Saccos Ltd  na kundi la pili ni shilingi milioni 7,275,500  za Halmashauri ya Msalala.

Alisema kuwa TAKUKURU ilifanya uchunguzi katika Chama cha akiba na Mikopo cha walimu kahama na kubaini kuwepo kwa madeni ya         muda mrefu ya walimu wastaafu 29 zilizotokana na kuchagia fedha kipindi wakiwa watumishi lakini baada ya kustaafu fedha hizo hazikuwahi kulipwa.

“Awamu ya kwanza tulirejesha shilingi milioni 5,815,800 kwa walimu wastaafu 13 waliokuwa wanazidai kwa muda mrefu ambapo na tutahakikisha madai yote wanayodai yanalipwa ili kuondoa malalamiko yasiyokuwa na tija yaliyosababishwa na baadhi ya viongozi wazembe,”alisema Shauri.

Shauri alifafanua kuwa katika kundi la pili TAKUKURU wamefanikiwa kurejesha fedha zilizokuwa zimetumikika kinyume na utaratibu katika ujenzi wa kituo cha afya ngaya baada ya kufanya uchunguzi na kubaini upotevu wa zaidi ya shilingi milioni saba kutokana na mtaalamu wa kitengo cha Manunuzi kutotimiza wajibu wake ipasavyo.

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Kahama Anamringi Macha aliwataka watumishi wa taasisi za umma na binafsi kuhakikisha wanatekeleza wajibu wao ipasavyo ili kuhakikisha wanazitendea haki dhamana walizokabidhiwa na watu wanao waongoza.

“Naipongeza TAKUKURU kwa kazi nzuri ya kurejesha fedha hizi kwa walimu wastaafu ambao walikuwa hawajui ni lini watapata stahiki zao,serikali ya awamu ya tano itahakikisha inawatetea wananchi wanyonge hivyo badi ni budi mkahakikisha mnawachukuli hatua kali wote watakaobaini kuhujumu fedha za Umma au sekta binafsi kwa manufaa yao binafsi,”alisema Macha.

Macha alitoa rai kwa watumishi wa umma kufanya kazi kwa uzalendo na kuepukana na vitendo vya rushwa ambavyo vinasababisha watu wengine kukosa haki zao za Msingi na kuwataka kutoa taarifa za matukio hayo kwa vyombo husika ili hatua ziweze kuchukuliwa.
Mwisho.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 45270

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>