Rais Magufuli amempongeza Dk. Lazarus Chakwera kwa kuchaguliwa kuwa Rais mpya wa Malawi.
Kupitia ukurasa wake wa Twitter; Rais Magufuli amesema, “Nakupongeza Dkt. Lazarus Chakwera kwa kuchaguliwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Malawi.
“Kwa niaba ya Serikali na Watanzania wote, naahidi kuendeleza uhusiano wetu wa kidugu, kirafiki na ujirani mwema hususani katika masuala ya uchumi na ustawi wa jamii. Hongera sana Mhe. Rais,” amesema.
Chakwera amechaguliwa na Wamalawi katika uchaguzi wa marudio uliofanyika tarehe 23 Juni 2020 kwa kupata asilimia 58 akimshinda Rais aliyekuwa madarakani Peter Mutharika.