Uongozi wa klabu ya Yanga umempiga faini ya Sh. 1.5 Milioni nyota wake raia wa Ghana, Benard Morrison kwa kufanya mahojiano na mwandishi wa habari bila kutoa taarifa kwa klabu na kuzua hali ya sintofahamu juu ya mkataba wake.
Taarifa kutoka ndani ya klabu ya Yanga imeeleza kuwa mchezaji huyo aliingia mkataba wa kwanza na timu hiyo tarehe 15 Januari, 2020, kwa muda wa miezi sita huku kukiwa na kipengele cha kuongeza kama wataridhishwa na kiwango chako.