Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all articles
Browse latest Browse all 45270

Mapenzi Ya Kichawi : Wanawake Acheni Kutumia Uchawi Kwenye Mapenzi. .... Athari Zake Ni Kubwa Sana.

$
0
0
By.  AFRICANDADAZ    BLOG
Wanawake  wengi  wa  siku  hizi  hawajiamini  katika  mapenzi  ndoa  na  mahusiano.  Ndio  maana  wengi  wao  hawawezi  kuingia  katika  mahusiano  ya  kimapenzi  bila  kutumia  uchawi.

 Yani  baadhi  ya  wanawake, akitongozwa  tu  na  bwana  ako  basi  jua  umekwisha!!!  Yani hata  kama  bwana  alikuwa  anamtamani  kwa  ajili  ya  kujifurahisha, akitembea  nae  tu  imekula  kwako  wewe  mwanamke  usiye  tumia  uchawi. 

Atalazimishwa  mapenzi  kwa  uchawi  hadi  atasahau  familia.  Baadhi  ya  wanawake  wapo  tayari  kufanya  kitu  chochote  kile  ili  wawakamate  wanaume  kimapenzi  kwa  kutumia  uchawi.  

Ukienda  makanisani  kusikiliza  shuhuda  za  wanawake  walio  amua  kuokoka  na  ambao  kabla  ya  kuokoka  walikuwa  wanajihusisha  na  uchawi  wa  mapenzi utastaajabu  kusikia  mambo  wanayo  yashuhudia.  

Wanaume  wanalishwa  vitu  vichafu  sana. Kuna  mwanamke  anasema  yeye  alienda  kwa  mganga  kumroga  bwana  ake  kimapenzi,mganga  akamwambia  aende  mahali  kwenye  msiba  wa  mwanamke, halafu afanye  mpango  kwa  gharama  yoyote  ile  aongee  na  wahusika apate  madawa   kwa  sababu  eti mtu  akiwa  anapelekwa  kaburini  kuzikwa  ananyanyuliwa   juu  na  watu ( wanaume ) , basi  na  yeye  nyota  yake  itakuwa  juu  kwa wanaume  wote, itabebwa  juu  juu  na  kila  mwanaume  na  atakuwa  juu  ya  mwanaume  wake.

Lakini  wanawake  wote  hawa  pamoja  na  kuroga  na  kufanya  kila  aina  ya  uchawi, mwisho  wao  ulikuwa  mbaya  sana  na wasinge  fanya  uamuzi  wa kumpa Yesu  maisha  yake, basi  sasa  hivi wangelikuwa  wameshaondoka  duniani.

Wanawake  uchawi  katika  mapenzi  haufai. Kumbuka  hawa  waganga  wanatumia  mapepo  na  mashetani. Hivi  jamani  hujiulizi, pepo  linakupenda  wewe   mwana wa adamu  kwa  sababu  gani  hadi  likupe  kitu  kizuri  kama mume?

Wanawake  tumwogope  Mungu. Tuache  kuvunja  ndoa  za  watu  kwa  uchawi, tuache  kuvunja  familia  za  watu  kwa  uchawi, tuwaonee  huruma  watoto  wanao  lelewa  katika  familia hizo kwani  nao  pia  wanahitaji  malezi  ya  baba  na  mama.

“Hakika hapana uchawi juu ya Yakobo, Wala hapana uganga juu ya Israeli. Sasa habari za Yakobo na Israeli zitasemwa, Ni mambo gani aliyoyatenda Mungu!.”.. HES. 23:23 SUV

Kwa  Mungu Hakuna  lisilo wezekana. Yeremia  32:27

 Unaweza  kupata  mume mwema, unaweza kuolewa  hata  bila ya  kwenda  kuroga  kwa  waganga.

 Kwa  jambo muhimu  katika maisha  ya  mwanadamu  kama ndoa  unapaswa  kumtumainia  Bwana na  sio  kwenda  kwa  waganga.

Wamtumainio BWANA ni kama mlima Sayuni, Ambao hautatikisika, watakaa milele…  Zaburi  125:1

Kusoma zaidi  shuhuda  hizo  tembelea;
 

Viewing all articles
Browse latest Browse all 45270

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>