Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all articles
Browse latest Browse all 45270

Ndayishimiye aapishwa kuwa rais mpya wa Burundi, aahidi kuliunganisha taif

$
0
0
Evariste Ndayishimiye aliyeshinda uchaguzi mkuu wa hivi karibuni nchini Burundi ameapishwa jana Alhamisi kuwa rais mpya wa nchi hiyo, kufuatia kifo cha ghafla cha Rais Pierre Nkurunziza.

Hafla ya kuapishwa jenerali huyo mstaafu wa jeshi imefanyika katika mji mkuu wa kisiasa wa Gitega, ambapo ameahidi kuliunganisha taifa hilo ambalo limekatiwa misaada na wafadhili haswa wa nchi za Magharibi kwa madai ya kukanyaga haki za binadamu.

Rais Ndiyishimiye amesema, "sitofelisha mkataba wa amani, katiba na sheria zingine za nchi, nitadhumisha umoja miongoni mwa Warundi, amani na haki kwa wote, na pia nitakabiliana na idiolojia ya mauaji ya kimbari na ubaguzi."

Awali Ndaiyishimiye alitazamiwa kula kiapo hicho cha kulitumikia taifa mwezi Agosti mwaka huu. Uamuzi wa kuapishwa mapema rais huyo mteule ulipasishwa na Mahakama ya Katiba ya Burundi. 

Alhamisi iliyopita, Baraza la Mawaziri la nchi hiyo lilifikia uamuzi wa kuikabidhidi mahakama hiyo jukumu hilo, baada ya taifa hilo kushuhudia ombwe la uongozi kufuatia kifo cha Nkurunziza.

Kwa mujibu wa Katiba ya Burundi, Spika wa Bunge ndiye aliyepaswa kushika madaraka ya nchi hadi wakati wa kuapishwa rasmi rais mteule.

Rais Nkurunziza ambaye ameiongoza Burundi kwa miaka 15 alifariki dunia kwa kile ambacho serikali ilisema ni maradhi ya moyo mnamo tarehe 9 Juni mwaka huu wa 2020.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 45270

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>