Wizara ya Afya nchini Kenya kwa mara nyingine imethibitisha idadi kubwa ya maambukizi 124 kwa muda wa saa 24 na kufikisha walioambukizwa kuwa 2340
Wizara hiyo imeeleza kuwa wagonjwa hao wametambuliwa baada ya sampuli 2640 kuchunguzwa.
Wizara hiyo imeeleza kuwa wagonjwa hao wametambuliwa baada ya sampuli 2640 kuchunguzwa.
Vilevile Kenya imesajili idadi ya wastani ya wagonjwa waliopona kwa siku moja baada ya watu 39 kuondoka hospitalini na kufikisha 592 waliopona kufikia sasa,hata hivyo idadi ya waliofariki imefikia 78 baada ya watu 4 zaidi kufariki.