Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all articles
Browse latest Browse all 45270

Watu walioambukizwa Corona nchini Kenya wafikia 2093, waliofariki 71.

$
0
0
Idadi ya wagonjwa wa Corona nchini Kenya imefikia 2093 baada ya kuwepo maambukizi mapya 72 ya Corona kutokana na kufanyiwa uchunguzi sampuli 2,892 kwa saa 24 zilizopita.

Watu waliopatikana na maambukizi ni kutoka jijini Nairobi watu 39, mpakani mwa kenya na Uganda wa Busia 13 na Mombasa maambukizi 8.

Taarifa ya Naibu waziri wa Afya Dkt.Rashid Aman ameeleza kuwa idadi ya waliofariki kutokana na COVID 19 sasa imefikia 71 baada ya watu 2 zaidi kufariki katika muda wa saa 24 zilizopita huku waliopona wakifikia 499 baada ya watu 17 kupona na kuondoka hospitalini.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 45270

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>