Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) inapenda kuujulisha Umma kuwa haihusiki kwa njia moja au nyingine na mashindano ya mbio za Heart Marathon 2020 yaliyokuwa yafanyike tarehe 19 Aprili mwaka huu jijini Dar es Salaam na Zanzibar na kuahirishwa kutokana na kuwepo kwa ugonjwa unaosababishwa na Virusi vya Corona (COVID – 19).
Mbio hizo za Heart Marathon ambazo zimepangwa kufanyika siku za mbeleni zimeandaliwa na Asasi ya kiraia ya Tanzania Health Summit na siyo Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI).
Aidha Taasisi inatoa rai kwa wananchi watakaopenda kushiriki katika mashindano hayo kuwasiliana moja kwa moja na waandaaji kama matangazo yao yanavyoonesha.