Rwanda imethibitisha visa 10 vipya vya maambukizi ya ugonjwa wa Corona siku ya Jumapili na kufikisha 70 jumla ya watu wanaougua corona, Wizara ya afya Rwanda imetangaza.
Katika hotuba yake kwa taifa usiku wa Ijumaa Rais Paul Kagame alisema idadi hiyo itaendelea kuongezeka kwasababu wale waliotangamana na waathirika wanaendelea kutafutwa.
Katika visa vya hivi punde vya maambukizi, watu sita walitokea Dubai, wawili kutoka Afrika Kusini, mmoja kutoka Nigeria na mwigine alikuwa amesafiri maeneo ya Afrika mashariki hivi karibunii, ilisema taarifa ya wizara ya afya nchini humo.