Kama ilivyo kwa magonjwa ya kawaida, maradhi ya kichawi nayo yana vyanzo vyake. Ni vyema kujua vyanzo vya maradhi haya ili uweze kujua namna ya kujiepusha nayo.
NJIA WATUMIAZO WACHAWI KUWASABABISHIA WATU MARADHI YA KISHEITWANI
Wachawi wakitaka kumsababishia mtu maradhi ya kisheitwani huwa wanatumia njia kuu zifuatazo:
1.KUMLISHA SUMU ZA KICHAWI : Hii ni miti inayo kaliwa na kumilikiwa na majini wa kisheitwani ambao kazi yao kuu ni kuwasababishia wanadamu maradhi na matatizo mbalimbali ya kimaisha.
Katika kutengeneza sumu za kichawi, wachawi hutumia miti hiyo kwa kuichanganya na mikuli ya ndege, wanyama, samaki na wadudu wenye kuhusiana na majini mbalimbali wa kisheitwani.
Bomu likisha kamilika sasa ndipo mhusika aliye kusudiwa hulishwa uchawi kwa lengo la kumsababishia maradhi ya kisheitwani.
MBINU WANAZO TUMIA WACHAWI KUWALISHA WATU SUMU ZA KICHAWI
Wachawi wakitaka kumlisha mtu sumu za kichawi hufanya hivyo kwa kuwatumia misukule kwa sababu misukule wanaweza kuingia kwenye nyumba ya mtu na kufanya au kuchukua kitu chochote walicho agizwa na kisha kutoka bila kuonekana na mtu yoyote.
Kwa hiyo misukule wakishaweka uchawi huo kwenye chakula , mhusika atakapo kula chakula hicho tayari uchawi unakuwa umeingia mwilini mwake na baada ya kipindi kilicho kusudiwa basi mhusika huyo ataanza kuonyesha dalili zote za maradhi yaliyo kusudiwa kwake.
KINGA
Kujikinga wewe pamoja na familia dhidi ya shari hii unaweza kufanya mojawapo kati ya mambo yafuatayo :
Moja : Kuchanjiwa dawa ya kutapisha sumu za kichawi mara baada ya kula ama kulishwa sumu hizo : Zipo kinga maalumu za asili zenye kumsaidia mtu kutapisha sumu za kichawi mara tu anapo kuwa amelishwa sumu hizo. Zipo dawa ambazo mhusika hutapika kupitia mdomoni na zingine mhusika hutoa sumu za kichawi kwa njia ya haja kubwa.
Hii dawa ya kutoa sumu za kichawi mwilini kwa njia ya haja kubwa hutengenezwa kwa kutumia samaki wa maji baridi ajulikanae kama Shilonge. Samaki huyu anapatikana Ziwa Victoria tu na ana sifa moja kubwa huwa hakai kwenye tumbo la samaki. Samaki wakubwa wakimmeza samaki huyu mdomoni huwa anateleza tumboni na kutokea kwenye tundu la haja kubwa hapo hapo .
Samaki huyu huchanganywa na dawa zingine za porini kutengeneza dawa ya kusaidia kuondoa sumu za kichawi kwa njia ya haja kubwa mara mtu anapokuwa amelishwa uchawi huo. Na hata kama mtu alikuwa ameshalishwa uchawi zamani, dawa hii husaidia kumuondolea uchawi. Samaki huyu pia hutumika kutengeneza dawa ya kumuchisha mtu pombe.
==>><<BOFYA HAPA >> Kuendelea na makala hii
==>><<BOFYA HAPA >> Kuendelea na makala hii