Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all articles
Browse latest Browse all 45270

Waziri Nchemba: Ni Kosa Polisi Kumkamata Mtu Mwingine kwa Kosa la Mwingine

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Ndani, Dkt. Mwigulu Nchemba amesema si sawa Jeshi la Polisi kumchukulia hatua mtu ambaye si mkosaji kwa kosa la mtu mwingine.

Dkt. Mwigulu amesema hayo bungeni leo wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum (Chadema), Devotha Minja lililohoji kumekuwa na tabia ya jeshi la polisi, wanapokwenda kumkamata mtu, wakimkosa wanamkamata mbadala, mke au mme, je jeshi la polisi wanatoa wapi mamlaka haya kwa kumkamata mtu na kumtesa?

Akijibu swali hilo, Waziri Mwigulu amesema Jeshi la polisi linafanya kazi kwa mujibu wa sheria, hakuna mtu anayeruhusiwa kuadhibiwa kwa mbadala.

“Kosa linabaki kwa muhusika na kama kuna mtu anaweza kusaidia afanye hivyo lakini si kuchukua adhabu kwa mtu mwingine”, amesema Mwigulu.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 45270


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>