TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Umechangia historia ya nchi yetu, Rais Kikwete amsifu Mzee Mkapa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemsifu na kumpongeza Rais wa tatu wa Tanzania, Mzee Benjamin William Mkapa kwa kuchangia historia ya Tanzania kupitia uamuzi wake wa kuchapisha vitabu vya hotuba zake alizozitoa wakati wa uongozi wake wa miaka 10.
↧