Wizara ya Ulinzi na
Jeshi la Kujenga Taifa, limetoa mwezi mmoja kwa watumishi wake wote
kuwasilisha vyeti vyao ili viweze kufanyiwa uhakiki ili kubaini kama
kuna vyeti feki.
Katibu Mkuu wa Wizara
hiyo, Job Masima, aliyasema hayo Dar es Salaam jana wakati wa Mafunzo ya
Elimu ya Hifadhi ya Jamii yaliyoandaliwa na Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA).
↧