Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Kutana na Maajabu ya Mtabibu CHIEF SULTAN(MAKATA WA MAKATANI) Mganga wa Waganga Sasa Yupo Mikoa Yote Tanzania

$
0
0
Kutana Maajabu ya Mtabibu CHIEF SULTAN(MAKATA WA MAKATANI) Mganga wa Waganga Sasa Yupo Mikoa Yote Tanzania
 
Pia anatoa Tiba kwa Njia ya Simu ukiwa popote Pale Tanzania au Nje ya Tanzania..
CHIEF SULTAN ni Mtabibu na Mtafiti wa Dawa za Asili ya Africa, na Duniani Katika utoaji wa Tiba za Asili..
Je unasumbulia na Mapenzi..?


(Umeachwa na Umpendae awe Mume/ Mke au mpenzi na Anaishi na Mtu Mwingine na Bado Unampenda?) Umejaribu sehemu Nyingi bila Mafanikio?Wasiliana na CHIEF SULTAN Akusaidie Kumshika Umpendae Asikusaliti(LIMBWATA) Kumtawala Mpenzi wako kwa sababu Maalum..Anauwezo wa Kusambalatisha Mahusiano yao ndani ya siku Moja tu.


Je Unasumbuliwa na Madeni?
Biashara yako Haina wateja?
Unatatizo la kutokushika Mimba na umehangaika sehemu nyingi bila mafanikio?
Wasiliana na CHIEF SULTAN Kwa Majibu ya Maswali yako..
Anasafisha NYOTA na Kutoa PETE za BAHATI kuendana na NYOTA yako. UTAJIRI USIO NA MASHARTI.(Magic Wallet_Pochi ya Maajabu Isio Isha Hela)


KUWA MAARUFU na KUJULIKANA
Kupandishwa CHEO na HESHIMA Mahala pa KAZI.
Utapewa Nguvu ya Kujilinda na MALI ZAKO zako na Mwili wako.. Huzuia Chuma Ulete katika Biashara.. Hurudisha MALI zilizo Potea au KUDHULUMIWA..
Mvuto wa Biashara na Mwili wako.
Hutibu kabisa Nguvu za Kiume na Kurefusha Uume kwa saizi Unayotaka.

Magonjwa Sugu(Miguu Kufa Ganzi, kisukari, Presha, Pumu nk.)Humaliza Kesi za Muda mrefu ndani ya siku 14 tu.


Anatoa NDAGU Zisizokuwa na Masharti.. Kwa maelezo Zaidi wasilina nae kwa 

 
whatsapp +255 0658 316 976
Call +255 755 911 233

TAKUKURU yaisaidia Serikali kuokoa Sh53 bilioni

$
0
0
WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema Serikali imefanikiwa kuokoa Sh bilioni 53.9 kutokana na uchunguzi na operesheni mbalimbali zilizofanywa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) katika mwaka 2016/2017.

Amesema kiasi hicho cha fedha ni kikubwa mno, ikilinganishwa ni Sh bilioni 7 tu zilizookolewa katika mwaka 2015/2016. Alisema hayo jana wakati akifungua semina ya Mtandao wa Wabunge wa Afrika walio katika Mapambano ya Rushwa (APNAC) Tawi la Tanzania kwenye ukumbi wa African Dream mjini Dodoma.

Akizungumzia hatua mbalimbali zinazochukuliwa na Serikali katika mapambano dhidi ya rushwa, alisema Serikali imeanza kupata mrejesho mzuri kwamba watumishi wa umma wanawajibika ipasavyo na vitendo vya rushwa vinaendelea kupungua.

“Baadhi ya hatua tulizochukua ni pamoja na kuimarisha taasisi yetu ya TAKUKURU; kuimarisha matumizi ya mashine za kielektroniki ili kupunguza mianya ya kupoteza mapato; kuanzisha mahakama ya mafisadi; kusimamia nidhamu katika utumishi wa umma na kuchukua hatua za haraka za kinidhamu na za kisheria dhidi ya watuhumiwa wote wa rushwa na ufisadi,” alisema.

Aliwaomba wabunge waendelee kuiunga mkono Serikali, kwani haina mzaha kwenye mapambano hayo. “Serikali haina mzaha kwenye mapambano dhidi ya rushwa na tutaendelea na mapambano hayo.

Hivyo, ninaomba waheshimiwa wabunge muendelee kutuunga mkono katika mapambano haya, twende kwa wananchi tukatoe wito kwao watuunge mkono kwenye vita hii,” alisisitiza.

“Tayari tumefanya tathmini na kubaini mianya ya rushwa katika sekta za ardhi, uchukuzi, biashara na maji na hivyo kuziba mianya hiyo. Tutaendelea kuiwezesha TAKUKURU ili iendelee na kazi nzuri waliyoianza ya kubaini mianya na kutoa ushauri wa kuziba mianya hiyo ya rushwa.Lengo letu ni kuwekeza zaidi kwenye kuzuia, kwa kuwa kinga ni bora kuliko tiba”. 

Mapema, akizungumza katika semina hiyo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais anayeshughulikia Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angellah Kairuki alisema Takukuru kwa kushirikiana na taasisi zilizo chini yake, wako njiani kuanzisha mtaala wa somo la rushwa ili ifundishwe tangu shuleni.

“Napenda kuwahakikishia waheshimiwa wabunge kwamba Serikali ya awamu ya tano haitakubali kuona rushwa ikiota mizizi. Tunaamini wanafunzi wakijengewa uwezo tangu utotoni, watachukia rushwa na hatimaye tutakuwa na Taifa lenye watu waadilifu,” amesema.

Alisema kutokana na kazi ya kupunguza watumishi hewa, hadi kufikia Aprili mwaka huu, Serikali imekwishapokea Sh bilioni 1.2 kwenye akaunti maalumu ya Takukuru iliyoko Hazina ambazo zinatokana na makusanyo kutoka kwa waliokuwa watumishi hewa.

Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkazi wa UNDP, Godfrey Mulisa alisema wataendelea kushirikiana na Bunge katika miradi mbalimbali ikiwemo shughuli zinazofanywa na APNAC.

Awali, Mwenyekti wa APNAC tawi la Tanzania, George Mkuchika alisema hadi sasa wabunge wapatao 148 wamekwishajiunga na mtandao huo. Kwamba anaamini hadi Bunge hili litakapomaliza muda wake, zaidi ya robo tatu ya wabunge watakuwa wamejiunga

Jela Miaka 23 Kwa Kuiba Cheti Kidato cha Nne

$
0
0
Mahakama  ya Wilaya ya Mlele mkoani Katavi imemhukumu kwenda jela miaka 23 mkazi wa kijiji cha Kalovye, Osward Mpalasinge (26).

Amepewa adhabu hiyo baada ya kupatikana na hatia ya kuvunja na kuiba vitu mbalimbali ikiwemo cheti cha kidato cha nne. Hukumu hiyo ilitolewa jana na Hakimu Mfawidhi wa mahakama hiyo, Teotimus Swai baada ya mshtakiwa kukiri kosa mahakamani.

Akitoa hukumu hiyo, Hakimu Swai alisema mtuhumiwa amekutwa na hatia pasipo shaka hivyo anahukumiwa kwenda jela miaka  23. 

Awali, Mwendesha Mashitaka, Baraka Hongoli alisema mshitakiwa alitenda makosa ya kuvunja na kuiba Mei 25 mwaka huu saa mbili usiku nyumbani kwa Veronica Crispin katika Kijiji cha Kalovye, Inyonga.

Alidai kwamba mshitakiwa alifika nyumbani hapo, akavunja na kisha kuiba nguo zenye thamani ya Sh 110,000 na cheti cha kidato cha nne cha Henreth Edward Kalamu, kilichotolewa na Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) mwaka 2015.

Hongoli aliitaka mahakama kutoa adhabu kali kwa mtu huyo ili iwe fundisho kwa kuwa wizi wa aina hiyo ndio umesababisha usumbufu na watu kupoteza ajira zao serikalini na maeneo mengine pindi uhakiki wa vyeti unapofanyika.

Akijitetea, mshitakiwa aliiomba mahakama impatie muda ili aweze kwenda Dar es Salaam kumtafutia mtu huyo cheti kingine

Meya wa Jiji la Arusha Amtaka Mkuu wa Mkoa Amuombe Radhi

$
0
0
Meya wa Jiji la Arusha, Calist Lazaro ametoa siku saba kwa  Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo amuombe radhi kwa kosa la kumuweka ndani wakati alipokuwa anakabidhi rambirambi kwa wazazi waliofiwa kwenye ajali ya gari la Shule ya Msingi Lucky Vincent.

Akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake jana Ijumaa, Lazaro alisema mpaka sasa ameshindwa kuelewa ni kwanini mkuu huyo aliagiza meya pamoja na wenzake wakiwemo viongozi wa dini, madiwani, wawakilishi waliotoa rambirambi na mwenye shule kukamatwa na Jeshi la Polisi na kuwekwa ndani.

"Mimi sikuwa na shida na RC na kitendo cha kumuweka ndani kiongozi wa dini, paroko, kiongozi wa dini ya Kiislamu ni kitendo ambacho si cha kibinadamu na anapaswa aombe radhi umma,"alisema.

Pia, alimtaka kutafakari nafasi yake na kuona kuwa anafaa kuendelea kuwa mkuu wa Mkoa wa Arusha kwasababu ameonyesha kuwatumikia wananchi ambao hawaheshimu.

"Hana heshima na mbunge, madiwani, watu wenye degree zao, haheshimu viongozi wa dini halafu bado anataka uongozi,"alisema.

Kamati ya Pili ya Mchanga wa Madini kuwasilisha ripoti yake kwa Rais Magufuli Jumatatu 12 Juni, 2017

Serikali yasaini mkataba kupanua na kuongeza kina cha Bandari ya Dar es Salaam

$
0
0
Benjamin Sawe-Maelezo
Mamlaka ya Bandari nchini (TPA), imesaini mkataba wa upanuzi na uongezaji wa kina cha bandari utakaowezesha bandari ya Dar es Salaam kupokea meli kubwa za mizigo na kushindana na bandari nyingine katika pwani ya bahari ya hindi.
 
Upanuzi huo utakaofanywa na kampuni ya China Harbor Construction ya China utagharimu kiasi cha shilingi bilioni 336 na utadumu kwa miezi 36, ambapo utahusisha uongezaji wa kina cha lango la bandari na uongezaji wa kina cha maji kati ya gati namba 0, 1 hadi 7.
 
Akizungumza katika hafla ya utiaji saini mkataba huo Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa amesema hatua hiyo inalenga kuifufua upya bandari ya Dar es Salaam ili ifanye kazi kwa ushindani na kuhudumia wateja wengi kuliko ilivyo sasa.
 
“ Kukamilika kwa upanuzi na uongezaji wa kina cha maji katika gati namba 1 hadi 7 kutoka mita 8 hadi 15 kutawezesha meli kubwa na za kisasa zenye uwezo wa kubeba hadi makontena elfu kumi na tisa kutia nanga katika bandari ya Dar es Salaam na kuongeza ufanisi na kukuza uchumi wa Tanzania”, amesema Prof. Mbarawa.
 
Aidha Prof. Mbarawa amesisitiza kuwa pamoja na upanuzi wa bandari ya Dar es Salaam Serikali inaendelea na ujenzi wa miundombinu wezeshi ya reli na barabara ili kuhakikisha mizigo haikai muda mrefu bandarini.
 
“Ujenzi wa reli ya kisasa ya Standard Gauge toka Dare s Salaam hadi Kanda ya Ziwa na Kigoma na ufufuaji wa reli ya Tazara kutawezesha bandari ya Dar e s Salaam kufanya kazi kwa ufanisi na kuvutia wafanyabiashara wengi hivyo nawataka wafanyakazi wote wa bandari kufanyakazi kwa bidii na uadilifu”, amesisitiza Prof. Mbarawa.
 
Naye Mkurugenzi Mkuu wa TPA Eng. Deusdedit Kakoko amesema kiasi cha dola za Marekani milioni 421, kitapatikana kwaajili ya ujenzi huo ambapo kati ya fedha hizo Benki ya Dunia itatoa mkopo wa masharti nafuu wa dola milioni 345.
 
Kukamilika kwa ujenzi huo kutaondoa adha ya baadhi ya meli kusubiri kwa muda mrefu kupata nafasi ya kutia nanga na kutaongeza hadhi ya bandari ya Dar es salaam na kuvutia wasafirishaji wengi kutoka ndani na nje ya nchi.

Kitimoto Chapigwa Marufuku Mkoani Dodoma

Basi la BATCO Lateketea Kwa Moto

$
0
0
Basi la BATCO lenye namba za usajili T192DHW limeteketea kwa moto hii leo katika eneo la Kirumi kata ya Bukabwa Wilayani Butama Mkoani Mara. Gari hilo lilikuwa linafanya safari zake kutoka Tarime-Sirari na Mwanza.

Chanzo cha Moto huo bado hakijafahamika.Taarifa za awali kutoka kwa baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo pamoja na abiria wameeleza kuwa baadhi ya mali za abiria zimeteketea kwa moto na hakuna mtu aliyepoteza maisha.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumapili ya June 11

Breaking News: Mkurugenzi Mkuu EWURA Asimamishwa Kazi

$
0
0
Usiku wa kumkia leo( saa saba usiku) Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa amemsimamisha kazi Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), Felix Ngalamgosi.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu imeeleza kuwa Bw. Felix amesimmisha kazi kuanzia leo Juni 11, 2017.

Maamuzi haya yamekuja siku mbili baada ya habari za kampuni ya IPTL kutaka kuongezewa mkataba wa uzalishaji umeme ambapo pia Kituo cha sheria na haki za Binadamu kilijitokeza na kusema hakikubaliani na mkataba huo kuongezwa kwani kampuni hiyo inahusishwa na kashfa ya uchotwaji wa Mabilioni kupitia account ya ESCROW.

Rais Magufuli huko nyuma amewahi kusikika akiuponda mkataba wa IPTL na kusema kuwa ni mkataba wa hovyo unaopelekea kutokuwapo kwa umeme wa uhakika kutokana na watu hao kufanyabiashara bila kujali utoaji huduma.

“Ni lazima nchi yetu tuachane na umeme usio na uhakika, umeme wa kukodishakodisha, umeme wa kutumia watu na ndiyo maana kumekuwa na matatizo mengi mara IPTL, mara nini, ni kwa sababu tulizoea maumeme ya kukodisha kodisha, ya wafanyabiashara,” alisema Rais Magufuli wakati akiweka jiwe la msingi kwenye mitambo ya kufua umeme ya Kinyerezi II.

Rais Magufuli alisema kuwa ni lazima Tanzania iachane na mitambo ya kukodi na TANESCO ijiwekee mikakati ya kuzalisha umeme wake yenyewe ili kutoa huduma ya uhakika kwa wananchi.

“Tuachane na mitambo ya kukodi, tumechoka kufanyishwa biashara na wawekezaji, tunalipia `capacity charge’ za ajabu ajabu halafu tunalipia bei ya ajabu. Tunawapa shida Watanzania wa hali ya chini, kila mmoja anahitaji umeme, lakini wengine wanashindwa kuuvuta kwa sababu umeme ni wa juu.”

Kutokana na kauli hiyo ambayo Rais Magufuli aliitoa Machi 2016 ni dhahiri kuwa serikali isingekuwa tayari kuendelea na mkataba na IPTL ambayo yeye anaamini kuwa inawanyonya watanzania.

Juni 7 mwaka huu EWURA ilitangaza kupokea maombi ya IPTL ikiomba kuongeza muda wa leseni uweze kuendana na mkataba wa mauziano ya umeme na TANESCO. 


EWURA ilisema kuwa imeyapitia maombi hayo na kuwa inadhamiria kuiongezea muda kampuni hiyo kutokana na makubaliano ya kuuziana umeme yaliyopo kati ya IPTL na TANESCO

EWURA iliwataka wanachi na wadau mbalimbali kutoa maoni yako kuhusu kusudio hilo ambapo wengi waliotoa maoni hayo walipinga kusudio la IPTL kuongezewa muda wa leseni yake.

Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kiliitaka EWURA kuondoa kusudio la kuiongezea muda IPTL na pia kuwaomba msamaha wananchi na wabunge.

IPTL ilikuwa ikiomba kuongezewa muda wa miezi 55 ya kuendelea na biashara ya kuiuzia umeme TANESCO kuanzia Julai 17, 2017 hadi Januari 15, 2022 ambapo ni miaka minne na nusu.

Mauaji Kibiti: IGP Sirro Awataka Waandishi Kuwa Wazalendo

$
0
0
Wakati  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba akisema matukio ya mauaji ya hivi karibuni mkoani Rufiji yana harufu ya kisiasa, Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP), Simon Sirro amevitaka vyombo vya habari kuwa na uzalendo, ikiwa ni pamoja na kuacha kutoa taarifa zenye kuchochea hofu kwa wananchi.

Waliyasema hayo kwa nyakati tofauti juzi na jana katika mikoa ya Singida na Morogoro. Waziri Mwigulu Akihutubia wananchi katika Kijiji cha Kaselya wilayani Iramba, Singida juzi katika siku ya kwanza ya ziara ya siku tatu kutembelea jimbo lake, Mwigulu alisema anahusisha mauaji hayo na siasa kwa kuwa mauaji ya wananchi kwenye maeneo hayo yanawakumba zaidi wafuasi na viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Alihoji; “Ujambazi gani huo wa Wana CCM tu? Hako kamchezo tumeshakagundua. Dhahiri, huo ni ushamba wa vyama vingi.” Alisema wanaodhani kuwa upinzani ni kwenye maisha wanakosea. “Naomba tupingane kwa kushindanisha sera na wala tusikunjiane ngumi kwa ajili ya siasa kwa kuwa siasa haipaswi kuwa ya uadui,” alisema.

Alisema pamoja na siasa hazipaswi kuwa ya uadui bado wapo baadhi ya wapinzani wanaotengeneza siasa ili zionekane kuwa ni za uadui.“Watu hawa wangekuwepo wakati wa vita baina ya nchi yetu na Uganda, hakika wangemsaidia Iddi Amin; bahati nzuri walikuwa bado wadogo,” alisema Waziri.

Sirro na uzalendo 
Naye Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) nchini, Sirro amevitaka vyombo vya habari nchini kuwa na uzalendo ikiwa ni pamoja na kuacha kutoa taarifa zenye kuchochea hofu kwa wananchi.

Alitoa rai hiyo jana wakati akizungumza na waandishi wa habari mjini Morogoro ambapo alisema baadhi ya vyombo vya habari vimekuwa vikitumia maneno yanayoongeza hofu kwa wananchi.

Kuhusu mauaji yanayotokea katika wilaya za Kibiti, Rufiji na Mkuranga mkoani Pwani, alisema vyombo vya dola vinaendelea kuyadhibiti na kwamba, jeshi hilo linaendelea kuchukua hatua, lakini baadhi ya vyombo vya habari vimekuwa vikitoa taarifa za kuchochea hofu.

“Taarifa zinazotolewa kwa umma hazioneshi kama kuna kazi inafanyika na vyombo vya dola kuzima mauaji hayo,” alisema 

Aidha, alisema pamoja na habari hizo kujenga hofu kwa jamii, pia zimekuwa zikiambatana na picha za watu waliojeruhiwa, picha za silaha kuonesha Pwani ni eneo la vita.

IGP Sirro aliwataka wanahabari wanapoandika masuala ya kiusalama, watafute ufafanuzi kwenye vyombo husika ili waandike taarifa sahihi, ikiwa ni pamoja na kutanguliza uzalendo mbele huku wakitambua athari zinazotokana na taarifa hizo kwa jamii.

Alisema wananchi wakijawa na hofu, watashindwa kutekeleza shughuli zao za kijamii na kiuchumi.“Epukeni sana kuandika habari zenye sura ya kishabiki kwenye suala hili, habari nyingi mnazoandika kwenye suala hili mnaonesha kama vile mnalifurahia, hili si suala la kufurahia hata kidogo,” alisema 

Alisema hayo ni mapambano hivyo kila mmoja anawajibika katika kusaidia ikiwa ni pamoja na kutoa taarifa sahihi zitakazosaidia kuzuia uhalifu na kuwakamata wahalifu.

OFA: Jipatie Riwaya Kali ya Kusisimua Ya President Wife

$
0
0
OFA KABAMBE SI YA KUKOSA MPENDWA MSOMAJI WANGU
 
Nunua kitabu cha PRESIDENT WIFE kwa sh 10000 ujipatie kitabu cha SORRY MADAM season ONE BureEEE kabisa. OFA hii ni wa watumiaji wa mtandao wa Whatsapp 0657072588 na EMAIL eddazariaM@gmail.com NDANI NA NJE YA TANZANIA 
 
Kumbuka kwamba SORRY MADAM season ONE ni mwanzo kabisa wa visa vyetu vya kusisimua cha EDDY na baba yake Mzee GODWIN

PRESIDENT WIFE
"Baada ya utawala wa mzee GODWIN na MANKA kutolewa madarakani na EDDY DODWIN, adui mkubwa wa Eddy, JOHN anachukua madaraka ya Mzee Godwin na kuapa ni lazima ataamuangamiza Eddy aliye kuwa rafiki yake wa kipindi kirefu toka wakiwa sekondari. Rahab anaongoza nchi huku kijana machachari Adrus akiwa mlinzi makini kuhakikisha maisha ya mke wa raisi yanakuwa salama, ila K2 na kaka yake wanajawa na uchu wa madaraka na kuhakikisha kwamba wanauangusha uongozi wa Raahab, ila Eddy anasimama kama ngao na kupigania uongozi wa Rahab je atafanikiwa"
 
Ungana nami muandishi wako Eddazaria G.Msulwa katika hadithi hii ya kusisimua

Wasiliana nami kwa simu 0657072588 au 0768516188
KARIBUNI SANA

Majaliwa apokea taarifa uchunguzi wa Salfa, Ni ya makontena 211 yaliyokuwa bandarini Dar

$
0
0
Waziri wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa amesema salfa iliyoingizwa nchini kwenye makontena 211 haina kasoro na inafaa kwa matumizi ya kupulizia kwenye mikorosho.

Majaliwa amesema hayo wakati akizungumza na wajumbe wa kamati maalum, waagizaji wa salfa na baadhi ya wajumbe wa Bodi ya Korosho nchini (CBT) kwenye kikao alichokiitisha kwenye makazi yake, Oysterbay, jijini Dar es Salaam.

“Bodi kaandaeni taratibu za kawaida kusambaza salfa kwa wakulima ili waanze kupuliza dawa hiyo. Wasichelewe kupuliza kwa sababu msimu umeshaanza,” amesema.

Juni 4, mwaka huu Waziri Mkuu alimuagiza Mkemia Mkuu wa Serikali, Prof. Samuel Manyele aende kuchunguza mzigo wa salfa ulioko bandari ya Dar es Salaam baada ya kutokea mkanganyiko uliosababishwa na ripoti ya TPRI kuwa ya salfa iliyoingizwa nchini na kampuni ya ETG Inputs Ltd kwa niaba ya Bodi ya Korosho haijakidhi viwango.

Waziri Mkuu alichukua hatua hiyo baada ya kubaini kuwa kuna mkanganyiko miongoni mwa wakulima juu ya matumizi ya kiuatilifu hicho licha ya kuwa Serikali ilikwishapokea taarifa ya bodi, na taarifa ya kampuni iliyotengeneza salfa hiyo na taarifa iliyoletwa na mwagizaji ambayo imethibitishwa na makampuni matatu ya kimataifa. Aliyataja makampuni hayo matatu kuwa ni InterTech, Bureau Veritas na SGS.

Akitoa taarifa ya uchunguzi wao mbele ya Waziri Mkuu, Prof. Manyele alisema walifanya uchunguzi kwenye makontena 21 ambayo ni sawa na asilimia 10 ya makontena yote 211 ili kubaini ubora wake.

“Uchunguzi ulifanyika kwenye maeneo ya purity, acidity na moisture contents kama ulivyokuwa umeelekeza. Sampuli zilichukuliwa kutoka GALCO Inland Container Depot iliyoko Chang’ombe ambako ndiko mzigo wa salfa ulioletwa na kampuni ya ya ETG Inputs Ltd unahifadhiwa,” alisema.

“Kwa kuzingatia matokeo ya kiuchunguzi wa kimaabara uliofanyika, viwango (specifications) vilivyowekwa ndani ya mkataba na viwango vya Shirika la Chakula na Kilimo Duniani (FAO) kuhusiana na kiuatilifu cha salfa ni maoni yetu kuwa mzigo wa salfa ulioko ndani ya makasha (containers) 211 unakidhi viwango,” alisema kwenye taarifa yake.

Naye, Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Korosho nchini, Bw. Maokola Majogo alisema yeye pamoja na Bodi yake watatekeleza maelekezo ya Waziri Mkuu na akawataka wakulima wasisite kutumia salfa hiyo kwani imekwishathibitishwa na Mkemia Mkuu kwamba haina matatizo.

IGP Sirro: Ni kosa Polisi Kudai Hela ya Mafuta kwa Raia

$
0
0
Mkuu wa Jeshi la polisi nchini (IGP), Simon Sirro amewataka makamanda wa polisi mikoa kuhakikisha wanatumia vizuri mafuta ya magari wanayowekewa ili kuepuka malalamiko ya wananchi kwa magari ya polisi kukosa mafuta.

Pia amesema hataki kusikia polisi hawajafika katika tukio kutokana na kisingizio cha kutokuwa na mafuta.

IGP Sirro alisema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari jana mkoani Morogoro na kuongeza kuwa ni kosa kwa mwananchi kudaiwa fedha za mafuta ya gari la polisi.

IGP Sirro yupo katika ziara ya kuangalia hali ya uhalifu katika mikoa akitokea mkoani Dodoma.

Alisema mafuta ya gari yapo katika bajeti ya Jeshi la Polisi kwa kila mkoa hivyo kinachotakiwa ni makamanda wa mikoa kuhakikisha kuwa wanayatumia vizuri.

“Ni jambo la kusikitisha mwananchi kutakiwa kuchangia mafuta ya gari la polisi,hili hatuliruhusu kabisa,” alisema Sirro

Hivi karibuni, wakazi wa Malinyi walimlalamikia Mkuu wa Wilaya hiyo Jacob Kassema kwa kuwachangisha Sh800,000 za mafuta ya gari lake. Hata hivyo, Kassema alikanusha suala hilo.

Mbali ya suala la mafuta, IGP Sirro aliwatoa hofu wananchi na kusema Serikali inaendelea na uchunguzi wa kina kuhusu mauaji yanayoendelea mkoani Pwani.

“Ni kweli kuna tatizo la mauaji Pwani lakini askari wetu wapo kazini mchana na usiku kutafuta suluhisho la tatizo,” alisema Sirro.

TFF Wakanusha Kutowalipa Posho Serengeti Boys

$
0
0
Kufuatia taarifa zilizokuwa zikienea na kusambazwa kwenye mitandao ya kijamii, zikidai kuwa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limewatelekeza wachezaji wa timu ya mpira wa miguu ya Tanzania ya vijana wenye umri wa chini ya miaka 17(Serengeti Boys), TFF imejitokeza na kukanusha taarifa hizo.

Taarifa hizo za uongo zilidai kuwa Serengeti Boys hawakulipwa posho na kushutumu viongozi wa juu wa shirikisho kuhusu jambo hilo.

“Tunapenda kuwajulisha wazazi na umma kwa ujumla kwamba vijana wetu walilipwa posho zao zote wakiwa kambini Morocco na Cameroon na zile za mashindano ya AFCON nchini Gabon.” wamesema TFF

Kwa mujibu wa Taarifa kutoka TFF, zimeeleza kuwa Shirikisho linafanya taratibu za kupeleka maombi kwenye Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (Football Development Fund FDF) ili kuweza kuwalipa vijana na benchi la ufundi sehemu ya posho zilizokuwa bado hazijakamilishwa wakati wa michuano ya kufuzu kwa AFCON 2017.

“Tumeshtushwa na taarifa hizo ambazo tafsiri yake ni kuharibu uhusiano mwema kati ya shirikisho, wazazi na wachezaji ambao wanatarajiwa kuitumikia timu ya Taifa ya Vijana wenye umri wa chini ya miaka 20 maarufu kama Ngorongoro Heroes.”

TFF wamesema kuwa wanawatambua vijana wa Serengeti Boys kwani bado ni sehemu ya kikosi cha Ngorongoro Heroes na hivyo ukifika wakati wataitwa kambini kwa ajili ya michezo ya kimataifa ya U-20.

Aidha, Wametoa shukrani kwa kuushukuru umma ambao wameendelea kuchangia Mfuko wa FDF ambao kimsingi kazi yake ni kutafuta rasilimali kwa ajili ya maendeleo ya mpira.

“Tunaomba michango iendelee kwani bado tuna changamoto za mashindano mbalimbali kwa timu za wanawake na vijana ikiwemo fainali za wanawake Afrika zitakazofanyika Ghana hapo mwakani kwa timu ya Twiga Stars na AFCON 2019 kwa Serengeti Boys ambayo itakuwa mwenyeji.”

Mfuko wa Maendeleo ya Mpira – FDF ulianzishwa kwa lengo la kutafuta rasilimali za maendeleo ya mpira wa miguu hasa kwa wanawake na vijana pamoja na miundombinu ya mchezo huo.

Zitto Kabwe Afunguka Mazito kutimuliwa kazi kwa Mkurugenzi Mkuu wa EWURA

$
0
0
Hili la Mkurugenzi Mkuu wa EWURA linahusu tangazo la leseni ya Kampuni ya kifisadi ya IPTL?

Ni muhimu sana Rais afahamu kwamba kuna kazi kubwa ya chinichini inafanywa na wasaidizi wake ( sina hakika kama yeye Rais anajua na au ameruhusu kazi hiyo ) kuendeleza wizi huu wa watu wa PAP ya Harbinder Singh Seth na IPTL.

Kwenye kesi ya Standard Chartered Bank dhidi ya TANESCO huko mahakama ya ICSID ambapo TANESCO wanatakiwa kulipa shilingi 352 bilioni kwa Benki hiyo, Wanasheria wa TANESCO na wale wa PAP/IPTL wanashirikiana kwa karibu mno. Kwenye rufaa, TANESCO wametakiwa waweke fedha hizo kwanza kwenye akaunti ya Benki ya nje kabla ya rufaa kusikilizwa.

PAP/IPTL wanalinda ufisadi wao kwa kujifanya wanashirikiana na TANESCO kwenye kesi. Kwenye Taarifa ya PAC kuhusu Tegeta Escrow Account, tuliweka wazi kuwa PAP/IPTL waliweka dhamana kuwa ikitokea madai yeyote yale dhidi ya TANESCO basi PAP/IPTL italipa.

Madai yametokea, matapeli hawa wanajifanya kushirikiana na Shirika letu na Wanasheria wa Serikali wanawasaidia matapeli hawa na sasa wanataka kuwaongezea leseni ya Biashara. Kwanini Serikali isitumie ile Indemnity kuwataka PAP kulipa hizi fedha? Kwanini Serikali inayosema inapambana na ufisadi inawakumbatia mafisadi wa PAP/IPTL?

 Kwanini Serikali iliyoonyesha ujasiri wa kupambana na Kampuni kubwa kama Acacia/Barrick inayumbishwa na matapeli hawa? Tena tapeli mmoja tu Harbinder Singh Seth?

Vyombo vya Serikali pia vinahusika na kuwalinda hawa matapeli. Kwa mfano, huko ICSID Shirika letu la TANESCO kupitia wanasheria wake wamepeleka hoja kwamba Maazimio ya Bunge kuhusu Tegeta Escrow hayana msingi wowote wa kisheria na kwamba Bunge linapiga porojo tu.

Wanasheria hawa wameomba Ofisi ya Bunge iwape barua kuthibitisha kuwa Maamuzi ya bunge hayana msingi wowote na ni maoni tu yanaweza kudharauliwa na kutupiliwa mbali. Shirika la Umma linalosimamiwa na Bunge linapeleka barua kwenye vyombo vya kibeberu kuwa Bunge porojo tupu.

Pia kwa kudanganywa na PAP/IPTL, TANESCO wamepeleka madai kuwa PAC ilihongwa kufikia maamuzi yaliyofikiwa na Bunge. Wametengeneza barua pepe za kujaribu kushawishi madai yao hayo na hata Taasisi muhimu kama PCCB waliingia kwenye mkenge huo na kuniita kunihoji.

Niliwapa ushirikiano wote na kuwapa simu na computer zangu wachunguze barua pepe zile za kuchonga wakakuta hakuna lolote. Sikuwaacha, niliwaambia kuwa wao ni mawakala wa mashetani.

Wanashirikiana na matapeli kuwaibia Watanzania. Idara ya Usalama wa Taifa, inahusika moja kwa moja na kazi hii inayofanywa na PAP/IPTL ili kufanikisha mradi huu wa kitapeli. Sina hakika kama Rais aliidhinisha haya maana TISS na PCCB wanawajibika kwa Rais moja kwa moja.

Hivyo, inawezekana kabisa mpango wa kuongeza leseni ya IPTL akawajibishwa mtu wa EWURA kwa sababu ndiye alitoa tangazo la leseni, lakini huyo mtu wa EWURA anaweza kuwa ameshinikizwa na watu wa Usalama wa Taifa kufanya hivyo. Mimi naamini Rais, kwa jinsi alivyo, hawezi kuwa anahusika na haya matapeli, lakini Rais mtumbuaji anakaaje miezi 20 kwenye Kiti za Enzi bila kumaliza suala la IPTL ilhali kuna Maazimio ya Bunge yanayopaswa kutekelezwa?

Nawapa kazi ndogo Watanzania, tazameni lile Tangazo la EWURA kuhusu IPTL nililowawekea hapa siku limetoka. Tazameni umiliki na wamiliki wa IPTL hivi sasa. Kuna hisa 16% kwa kampuni mbili zenye majina ya ujanja ujanja. Kina nani hao wamegawiwa hizo hisa tena wakati wa Uongozi wa Rais John Pombe Magufuli.

Jinsi Kitambi Kinavyopatikana na Jinsi Kinavyoondolewa na Dawa ya Mkataa Kitambi

$
0
0

Kitambi  ni  ile  hali  ya  tumbo  kuwa kubwa  na  kuchomoza  kwa  mbele  na  wakati mwingine  kufikia  hatua  ya  kunin’ginia.
JINSI  KITAMBI  KINAVYO  PATIKANA
Kwa  mujibu  wa  tafiti  mbalimbali  za  kitaalamu, mwili wa binadamu una seli kati  ya bilioni 50  hadi 200 za mafuta zilizogawanyika katika  sehemu  mbalimbali  za  mwili wa binadamu.

 Kwa wanawake  seli hizo  zipo sana katika maeneo ya matiti, kwenye  nyonga, kiunoni na kwenye makalio.

Kwa upande  wa  wanaume seli  hizo zinapatikana  sana kwenye kifua, tumboni na kwenye makalio pia.

Mafuta ya tumbo yanayofanya kitambi hukusanywa kwa njia kuu mbili:

i.Njia  ya kwanza ni mafuta kutoka kwenye tishu zilizo chini ya ngozi

ii.Na  njia  ya pili ni kutoka kwenye ogani za ndani kama moyo, kongosho n.k

SABABU ZA KUPATA KITAMBI
Sababu kubwa ya kitambi ni kukosekana ulingano wa nguvu(kalori) katika  mwili  wa  mwanadamu, hali  inayo  sababishwa  na  mtu  kula vyakula vinavyotia nguvu sana kuliko jinsi anavyoweza kutumia na kutoa kama taka mwili.

VYAKULA  VINAVYO  CHANGIA KULETA  KITAMBI

Vyakula vinavyochangia  kuleta  kitambi ni  pamoja  na :
i.Vyakula  vyenye  mafuta  mengi  kama  vile  nyama nyekundu  (iwe ni ya kuchemsha, kukaanga au kuchoma), nyama  ya  kuku  wa  kizungu  ( iwe  ya  kuchemsha, kukaanga  ama  kuchoma ), mafuta ya kupikia, (hasa yale yatokanayo na bidhaa za wanyama, kama siagi, na jibini), viazi ya kukaanga kwa  mafuta  (chips) pamoja  na  pizza.

ii.Vyakula vyenye wanga mwingi kama  vile ugali wa mahindi, mihogo, wali, mkate  mweupe.

iii. Vyakula  na  vinywaji  vyenye  sukari  nyingi  iliyo  ongezwa( added  sugar ), kama  vile  soda  na  keki.

iv. Vyakula  vilivyo  tengenezwa  kwa  ngano  na  sukari kama  vile  keki, skonzi, chapatti, maandazi, mkate  mweupe  nakadhalika

v. Pamoja  na  vinywaji  vilivyo  tengenezwa  kwa  kutumia  ngano  kama  vile  bia  za  aina  mbalimbali  na  kadhalika.

Vyakula  vilivyo  tajwa  hapo  juu, vikitumiwa  bila  kuzingatia  kanuni  za  mlo  kamili, huchangia  kuleta  tatizo  la  kitambi.

vi. Sababu nyingine ni  kutofanya  mazoezi  ya  mwili  na  viungo(  physical  exercises  )  kwa  muda  mrefu.

JINSI YA KUJUA KAMA UNA KITAMBI
Kitambi kinaweza kuonekana kirahisi kwa macho. Ila kujua ni kwa kiwango gani kitambi chako kipo inabidi kufanya vipimo vya kiuno(waist) na nyonga (hips).

Mzingo wa kiuno ukiwa >102 cm au 40  kwa wanaume na >88 cm au 35  kwa wanawake, na uwiano wa kiuno na hips(Waist-Hip Ratio) ikiwa >0.9 kwa wanaume na >0.85 kwa wanawake.

BMI ya 30 au zaidi inaashiria 'Obese' uzito kuzidi kiasi. Kuwa na mzingo uliozidi kawaida ni kiashiria hatari cha matatizo ya kimetaboliki, kuliko hata cha BMI.

Kipimo kingine cha kitambi ambacho kimeonyesha uwezo zaidi kuliko BMI katika kutabiri uwezekano mkubwa wa magonjwa ya moyo ni Index Of Central Obesity(Waist-To-Height Ratio-WHtR) ambapo uwiano ukiwa sawa na 0.5 au zaidi, hii ikimaanisha mzingo wa kiuno angalau ni nusu ya kimo cha mtu.

Kipimo kingine ni Body Volume Index, kinachopima kitambi kwa kupima umbo la mtu na mgawanyo wa uzito wake.

MAMBO  YANAYO  MUWEKA  MTU  KATIKA  HATARI  YA  KUPATWA  NA  KITAMBI
Tumekwisha  ona  hapo  juu jinsi  kitambi  kinavyo  patikana  na  vyakula  pamoja  na  sababu  nyinginezo  zinazo  sababisha  kutokea  kwa  kitambi, sasa  tutazame  mambo  yatakayo  kufanya  uwe  katika  hatari  ya  kupatwa  na  kitambi.

Kwa  mujibu  wa  tafiti  mbalimbali  za kitaalamu, mambo  yafuatayo  huwaweka  watu  katika  hatari  kubwa   ya  kupatwa  na  kitambi :

1. Ulaji  mbovu  wa  chakula; Ulaji  mbovu  wa  chakula  ni  ulaji  usio  zingatia  kanuni  za  mlo  kamili. Hapa  mtu  hufululiza  kutumia  chakula  cha  aina  fulani  pekee  bila  kuzingatia  aina  nyinginezo  za  chakula.  Mfano; mtu  anaweza  kuwa  anakula  mlo  ufuatao :

Asubuhi :  Mchemsho  ama    supu  ya  ng’ombe , chapatti  tatu  na  soda  moja.  Mchana :   Ugali  nyama  choma anashushia  kwa  maji  na  soda.

Jioni :  Mchemsho  wa  kuku  na  bia  mbili  nakuendelea.

Usiku  :  Chips  mayai  au  chips  kuku  au  chips  mishikaki  na  bia.

Mtu  huyu  akiendelea  na  utaratibu  huu  kwa  muda  mrefu, ni  lazima  atapatwa  na  kitambi.

2. Ulaji  mfululizo  wa  vyakula  vyenye  mafuta  mengi

3. Ulaji  mfululizo  wa  vyakula  vyenye wanga  mwingi  

4.Ulaji  mfululizo  wa  vyakula  vyenye  sukari  iliyo  ongezwa ( added  sugar  ).

5.Ulaji  mfululizo  wa  vyakula  vya  ngano.

6.Ulaji  mfululizo  wa   vinywaji  vyenye ngano  na  sukari.

7.Kutofanya  mazoezi  ya  mwili  na viungo  ( physical  exercises  ).

Mhusika  anapokuwa  katika  makundi  yote  yali yotajwa  hapo  juu, hali  huwa  mbaya  zaidi. 

NJIA ZA KUONDOA KITAMBI
Kuwa  na  kitambi  ni  lugha  ya  mwili  ( body-language )  inayo  leta  ujumbe  kwako  kwamba  “ Mwili    wako  haupo  salama  tena “

Kama  una  kitambi   maana  yake  una  mafuta  yasiyo  hitajika  mwilini, mwili  wako  unatumika  kuhifadhi  mafuta  usiyo  yahitaji.

Hali  hii  kitabibu  imaanisha  kwamba, ogani  nyinginezo  zilizomo  ndani  ya  mwili  wako  zinao gelea  kwenye  mafuta( fats  )  yasihotika  yaliyomo ndani  ya  mwili  wako,  jambo  linalo  kuweka  katika  hatari  kubwa  sana  ya  kushambuliwa  na  magonjwa  hatari  kama  vile  shinikizo  kubwa  la  damu, kiharusi  na kisukari  na  kwa kutaja  machache.

Hivyo  basi  ili  kuondokana  na  hatari  hiyo, yakupasa   kupambana  kuondoa  hayo  mafuta  yasiyo  hitajika  mwilini  mwako.

NJIA  ZA  KUONDOA  KITAMBI.
Unaweza  kuondokana  na  kitambi  kwa  kufanya  diet  pamoja  na  mazoezi ya  mwili  na  viungo.

Vilevile  unaweza  kuondoa  kitambi  na  kupunguza  mafuta  mwilini  kwa  kutumia  dawa  asilia  ya  kuondoa  kitambi  na  kuondoa  mafuta  yasiyo  hitajika  mwilini.

DAWA   ASILIA  YA  KUONDOA  KIAMBI  NA  MAFUTA  MWILINI.
Hii  ni  njia  ya  uhakika  kabisa  ya  kuondoa  tatizo  la  kitambi  pamoja  na  mafuta  yasiyo  hitajika  mwilini.

 Unaweza  kuondoa  tatizo  la  kitambi  pamoja  na  kupunguza  mafuta  mwilini  kwa  kutumia  DAWA  ASILIA   IITWAYO YA  MKATAA  KITAMBI.

 Dawa   hii  ni  ya asili  kabisa
“  Pure  Herbal “, ambayo  haijachanganywa  na  kemikali  yoyote, haina  side  effect kwa  mtumiaji  na  inaondoa  kabisa  tatizo  la  kitambi  ndani  ya  siku  kumi  na  nne.

JINSI  DAWA  YA  MKATAA  KITAMBI  INAVYO  FANYA  KAZI.
1.Huyeyusha  mafuta  yasiyo  hitajika  mwilini.

2.Husaidia  kupunguza  hamu  ya  chakula.

3.Inazuia  kutengenezwa  kwa  seli  za  mafuta  ( fat cells  ) katika  mwili  wa  mwanadamu. Unapokula  chakula  chenye  mafuta  mengi, dawa  hii asilia  hupambana  kuyafanya  mafuta  hayo  yasitengeneze  seli  za  mafuta  mwilini  mwako. Hali  hii  huuepusha  mwili  wako  kuhifadhi  mafuta   yasiyo  hitajika  mwilini.

4. Husaidia  kupunguza  uzito wa mwili  kwa  haraka  sana  endapo  itatumika  pamoja  na  diet  ya  kabechi.

UFANISI  WA  DAWA.
Ufanisi  wa  dawa  hii  ni  wa  asilimia  mia  moja. Dozi  ya  dawa  hii  hutumika  kwa  muda  wa  siki  ishirini  na  moja.

MATOKEO  YA  DAWA:
Dawa  hii  huondoa  kabisa  kitambi  ndani  ya  siku  kumi  na  nne.

BEI  YA  DAWA :
Dawa  hii  inaoatikana  kwa  kiasi  cha  SHILINGI  ELFU  HAMSINI  TU  (Tshs. 50,000/=)

MAHALI  TUNAPO  PATIKANA.
Tunapatikana  jijini  DAR  ES  SALAAM, katika  eneo  la  UBUNGO  karibu  na  SHULE  MSINGI  UBUNGO  NATIONAL  HOUSING  nyuma  ya  jengo  la  UBUNGO  PLAZA.

KWA  WATEJA  WASIO  WEZA  KUFIKA  OFISINI  KWETU.
Kwa  wateja  wasio  weza  kufika  ofisini  kwetu  Tabata, tunao  utaratibu  wa  kuwafikishia  dawa  mahali  popote  walipo  ndani  ya  jiji  la  Dar  Es  salaam.

KWA  WATEJA  WA  NJE  YA  DAR  ES  SALAAM.
Kwa  wateja  waliopo  nje  ya  Dar  Es  salaam, tunawatumia  dawa  kwa  njia  ya  MABASI.

Kwa  wateja  wa  ZANZIBAR  tunawatumia  dawa  kwa njia  ya  boti.

KWA  WATEJA  WA  NJE  YA  NCHI:
Kwa  wateja  wa  nje  ya  nchi, tunatumia  dawa  kwa  njia  ya  POSTA  au  DHL.

WASILIANA  NASI  KWA  SIMU  NAMBA : 0766  53 83 84

TUTEMBELEE:

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumatatu ya June 12

Fundi Mbao Atiwa Mbaroni Kwa Kuwabaka Watoto Wake Wawili

$
0
0
Fundi mbao, Japhet Lendiman (38) mkazi wa Daraja Mbili, anashikiliwa na Jeshi la Polisi, baada ya kubaka watoto wake wa kike wa darasa la sita na kidato cha kwanza.

Akizungumzia tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo alisema kuwa polisi wanaendelea na uchunguzi ili kubaini kiini cha tatizo hilo ni nini na kufuatiwa na hatua ya kufikishwa mahakamani. Mtuhumiwa huyo anashikiliwa na Jeshi la polisi tangu Juni 6, mwaka huu na upelelezi unaendelea kubaini undani wa tukio hilo.

Akimzungumzia mtuhumiwa huyo, mmoja wa majirani wa eneo hilo la Daraja Mbili (jina limehifadhiwa) alidai kuwa mzazi huyo amezoeleka kwa tabia hiyo mbaya mtaani kwao.

 Alidai kuwa mtuhumiwa huyo amezoea kubaka watoto wake mara kwa mara wakati mama yao akiwa kazini na kwamba Mei 28 majira ya saa 9:00 alasiri alimbaka tena mtoto wake (Jina tumelihifadhi) wa darasa la sita shule ya Msingi Daraja Mbili ndipo taarifa zilipoanza kuzagaa mtaani.

“Siku hiyo ya tukio lililosababisha mzazi huyo kukamatwa mtoto aliona sasa uvumilivu umefika mwisho, alikwenda kwa mama mkubwa na kutoa taarifa jinsi baba yake anavyomwingilia na kueleza kuwa anataka kunywa sumu ili afe,” alieleza jirani huyo. 

Alisema baada ya maelezo hayo mama mkubwa aliamua kuhoji watoto wote wa shemeji yake akiwemo mwingine wa umri wa miaka 14 (jina limeifadhiwa) ambaye yupo kidato cha Kwanza Sekondari ya Felix Mrema, alikiri kuingiliwa na baba yake tangu mwaka 2016. 

Aliendelea kueleza kwamba mama yao mkubwa ambaye ni muuguzi (jina limehifadhiwa ) katika moja ya hosptali mkoani Arusha, aliamua kutoa taarifa kwa mwenyekiti wa mtaa na Polisi.

EWURA Wasitisha Mchakato wa Kuiongezea Leseni Kampuni ya IPTL......Ni Baada ya Waziri Mkuu kumsimamisha kazi Mkurugenzi Mkuu

$
0
0
Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imesitisha mchakato wa kushughulikia maombi ya IPTL ya kuongezewa muda wa leseni yake ya biashara kwa miezi 55 ili iendelee kuzalisha umeme na kuiuzia TANESCO.

Mbali na kusitisha mchakato huo, EWURA imesitisha pia upokeaji wa maoni kutoka kwa umma na wadau mbalimbali kuhusu kusudio lake la kuiongezea muda wa kufanyakazi nchini Kampuni ya IPTL

Uamuzi huu wa EWURA umekuja ikiwa ni siku moja baada ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kumsimamisha kazi Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Felix Ngamlagosi bila kueleza sababu za uamuzi huo.

Hapa chini ni taarifa ya EWURA

Viewing all 45270 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>