Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Waziri Mkuu Akemea Uvuvi Haramu Ziwa Victoria

$
0
0
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mmiliki wa Pantoni ya MV Nyehunge, Said Mohammed  kwenye gati la Kirumba wakati aliposafiri  na chombo hicho kutoka jijini Mwanza kwenda Ukerewe Februari 18, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

 ***
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amekemea vitendo vya uvuvi haramu wa kutumia sumu kali ndani ya ziwa Victoria kwa sababu vinaharibu soko la samaki.

Aliyasema hayo jana jioni (Jumamosi, Februari 17, 2018) wakati akizungumza na wananchi wa kijiji cha Kisorya wilayani Bunda mkoani Mara.

Alisema kitendo cha kuvua kwa kutumia sumu kinaharibu soko la samaki la ndani na nje ya nchi kwa sababu sumu hiyo inabaki hivyo kumuathiri mlaji.

Waziri Mkuu aliwaagiza Maofisa Uvuvi katika Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwenda kutoa elimu kwa wavuvi wa eneo hilo juu ya madhara ya zana haramu za uvuvi.

Alisema baadhi ya wavuvi wanavua kwa kutumia nyavu zilizopigwa marufuku, kokoro pamoja na mabomu jambo ambalo haliwezi kuvumilika kwa sababu zana hizo zinaharibu uhai wa viumbe hai ndani ya ziwa Victoria.

Pia, Waziri Mkuu alisema Serikali tayari imeshaagiza nyavu zinazofaa kwa ajili ya uvuvi endelevu kutoka nje ya nchi ambazo zitauzwa kwa wavuvi mbalimbali.

Waziri Mkuu alisema wavuvi wote wanatakiwa kufuata sheria ikiwemo kuwa na leseni za uvuvi kwa vyombo vyao, hivyo  alimuagiza Afisa Uvuvi afanye ukaguzi.

Alisema Serikali inafanya uhakiki wa vyombo na wavuvi wote ili kubaini nani anavua wapi na kwa utaratibu upi. “Kamati ya Ulinzi na Usalama simamieni suala hili.”

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu alimuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda Bw. Amos Kusaja kuhakikisha gari la kuhudumia wagonjwa la Kituo cha Afya cha Kasahunga linakuwa na mafuta wakati wote.

Alitoa agizo hilo baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa wananchi waliodai kuchangishwa fedha za mafuta ya gari hilo mara wagonjwa wao wanapopewa rufaa kwenda katika hospitali ya wilaya.

(mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMAPILI, FEBRUARI 18, 2018.

Mtandao wa wanafunzi Tanzania (TSNP) Wamtaka Mwigulu Nchemba Ajiuzulu Sakata la Mwanafunzi wa NIT Kupigwa Risasii na Polisi

$
0
0
Mtandao wa wanafunzi Tanzania (TSNP) na Chama cha ACT-Wazalendo wamemwomba Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,  Mwigulu Nchemba kujiuzulu ili kuonyesha uwajibikaji kwa maelezo kuwa ameshindwa kusimamia amani.

TSNP imetoa kauli hiyo leo Februari 18, 2018 ikiwa ni siku moja tangu kupigwa risasi kwa  mwanafunzi wa Chuo cha Usafirishaji cha Taifa (NIT), Akwilina Akwiline aliyekuwa katika daladala wakati polisi walipowatawanya wafuasi wa Chadema.

Kauli ya mtandao huo na chama hicho imetolewa leo baada ya viongozi wao kuzungumza na waandishi wa habari.

Mwenyekiti wa TSNP Taifa, Abdul Nondo amesema iwapo Mwigulu hatajiuzulu wadhifa wake, wamemuomba Rais John Magufuli kutengua uteuzi wake.

“Kwa kuwa hivi sasa matukio haya yamekuwa yakishamiri na kushika kasi; watu kutekwa, kupotea, kupigwa risasi na kuuwawa ni muda muafaka sasa kwa Mwigulu kuchukua uamuzi wa kujiondoa katika wizara kuonyesha uwajibikaji,” amesema.

Amebainisha kuwa mwaka 1977 Rais mstaafu wa Awamu ya Pili Ali  Hassan Mwinyi wakati huo akiwa Waziri wa Mambo ya Ndani alijiuzulu baada ya polisi  kutumia nguvu dhidi ya raia.

"Tunaamini kwamba huo utakuwa ni mwanzo wa kukaribisha mabadiliko katika Jeshi la Polisi kwani kuondoka kwa mkuu kutawafanya walio chini yake kuondolewa,” amesema.

Katika hatua nyingine Mkuu wa Idara ya Sheria TSNP,  Deogratias Mahinyila amesema taasisi yao kupitia wanasheria wao na wanasheria mbalimbali watawasaidia walezi na wazazi wa mwanafunzi huyo kufungua kesi ya madai mahakamani, kutokana na uzembe uliofanywa na polisi ili iwe fundisho.

"Tunataka hatua stahiki zichukuliwe dhidi ya askari polisi waliotenda unyama huu na kukatisha haki ya kusoma na kuishi kwa mwanafunzi mwenzetu kwani wamekiuka sheria na maadili ya kazi yao, katika kulinda amani ya raia," amesema.

Chama cha ACT Wazalendo kimemtaka Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba awajibike kwa kujiuzulu wadhifa wake kwa sababu ameshindwa kukomesha mfululizo wa mauaji ya watu wasio na hatia.

Pia, wamewataka Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP Simon Sirro na Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa nao wajiuzulu kwa kushindwa kutekeleza majukumu yao ikiwamo kulinda usalama wa raia na mali zao.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Ngome ya Vijana wa ACT Wazalendo, Licapo Bakari amesema matukio mengi ya mauaji na kupotea kwa watu yanatokea na viongozi hao hawachukui hatua zozote kukomesha hali hiyo.

Amesisitiza kwamba wote wanaouawa na kutoweka katika mazingira tatanishi ni vijana ambao ndiyo nguvu kazi ya Taifa na chachu ya mabadiliko ambayo inatakiwa kulindwa kwa mustakabali wa nchi hii.

Bakari amesema vijana wa ACT Wazalendo wanalaani mauaji ya Akwilina, kwamba tukio la kuuawa kwa binti huyo siyo la kwanza, siku chache zilizopita kiongozi wa Chadema kata ya Hananasifu, Daniel John naye aliuawa na mwili wake kuokotwa kwenye fukwe za Coco.

"Tunataka uchunguzi huru ufanyike kwa kuchunguza matukio yote kuanzia hili la mwanafunzi wa NIT na mengine yote ya mauaji na utekaji," amesema.

Wakati huohuo, Bakari amewataka viongozi wote wa vyama vya siasa kukutana na kupanga mikakati na siku ambayo wanajumuika pamoja na wananchi kupaza sauti na kusema matukio hayo sasa basi.

"Wote tunaipenda nchi yetu, hatupendi kuona ikipotea. Viongozi wa dini, vijana, wanafunzi na wananchi wote tuungane pamoja kupinga ukatili unaotokea ndani ya nchi yetu wenyewe," amesema.

Polisi sita washikiliwa kwa uchunguzi kifo cha mwanafunzi NIT

$
0
0
Polisi inawashikilia askari wake sita na silaha zao kwa ajili ya uchunguzi kuhusu tukio la kuuawa kwa risasi mwanafunzi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Akwilina Akweline.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amesema hayo leo Februari 18,2018 alipozungumza na waandishi wa habari kuhusu ulinzi wakati wa kampeni, upigaji kura, na utangazaji matokeo ya uchaguzi mdogo wa ubunge jimbo la Kinondoni uliofanyika jana Februari 17,2018.

Amesema polisi iliunda timu ya upelelezi kuchunguza chanzo cha kifo cha mwanafunzi huyo kilichotokea Februari 16,2018 wakati polisi wakiwatawanya wanachama wa Chadema waliokuwa wanakwenda ofisi za mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni kushinikiza mawakala wao kupatiwa barua za viapo vyao.

Kamanda Mambosasa amesema polisi pia inawachunguza watuhumiwa 40 ili kubaini iwapo miongoni mwao walikuwepo waliokuwa na silaha za moto.

Amesema pia wanaendelea kuwatafuta wafuasi na viongozi wa Chadema walioshiriki kushawishi wafuasi wao kushiriki kwenye maandamano. 

Wakati huohuo, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole katika taarifa aliyoitoa jana Februari 17,2018 alisema chama hicho kinalitaka Jeshi la Polisi kufanya uchunguzi wa kina kuhusu aliyehusika na tukio la kuuawa kwa mwanafunzi huyo.

Polepole alisema polisi imhoji Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na viongozi wenzake walioshiriki maandamano aliyosema hayakuwa halali yaliyosababisha uhai wa Mtanzania kupotea.

Rais Magufuli Aomboleza Kifo cha Mwanafunzi wa NIT Aliyepigwa Risasi na Polisi

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli ametuma salamu za pole kwa familia ya Akwilina Akwilini aliyeuawa baada ya kupigwa na risasi katika maandamano wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Februari 16, 2017 eneo la Kinondoni jijini Dar es Salaam

Katika salamu hizo, Rais Dkt Magufuli amesema kwamba amepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo hicho na hivyo ameviagiza vyombo vya dola kufanya uchunguzi na kuwachukulia hatua za kisheria wale wote watakaobainika kuhusika na tukio hilo.

“Nimesikitishwa sana na kifo cha mwanafunzi Akwilina Akwilini wa Chuo cha Usafirishaji (NIT). Natoa pole kwa familia,ndugu,wanafunzi wa NIT na wote walioguswa na msiba huu. Nimeviagiza vyombo vya dola kufanya uchunguzi na kuwachukulia hatua za kisheria waliosababisha tukio hili.”

Akwilina alikumbwa na umauti wakati Polisi walipokuwa wakitawanya maandamano ya CHADEMA walipotaka kwenda kwenye Ofisi za Msimamizi wa uchaguzi wa Jimbo la Kinondoni kuhoji kwanini mawakala wao hawajaaapishwa.

Shy-Rose Bhanji: CCM haiwezi kukwepa lawama Mauaji ya Mwanafunzi wa NIT

$
0
0

Aliyekuwa Mbunge wa Afrika Mashariki, Shy-Rose Bhanji amefunguka na kuweka wazi msimamo wake juu ya tukio la kupigwa risasi kwa mwanafunzi wa mwaka wa kwanza Chuo cha NIT Aqulina Akwilini na kusema kuwa chama chake cha CCM hakiwezi kukwepa juu hilo.

Shy-Rose Bhanji amesema kuwa kufuatia kifo hicho cha mwanafunzi huyo ambaye alipigwa risasi na jeshi la polisi Februari 16, 2018 eneo la Mkwajuni jijini Dar es Salaam wakati jeshi la polisi likiwatawanya wafuasi wa CHADEMA ambao walikuwa wakiandamana kwenda kwa Mkurugenzi wa uchaguzi wa Kinondoni na kudai kuwa suala hilo yeye linamsuta moyoni mwake. 

"Serikali ya chama changu CCM haiwezi kukwepa lawama kwa namna yoyote ile kufuatia kupigwa risasi kwa binti ambaye hakuwa na hatia hata kidogo. Imekuwa ni siku mbaya sana kwangu, nimeshindwa kula na nashindwa kupata usingizi kutokana na kifo cha huyu binti. Nafsi yangu inanisuta. Mungu wangu naomba unisaidie" alisema Shy-Rose Bhanji

Serikali kugharimia mazishi ya mwanafunzi aliyepigwa risasi na Polisi

$
0
0
Serikali imetoa pole kwa familia ya mwanafunzi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Akwilina Akwiline aliyeuawa kwa kupigwa risasi Februari 16,2018 na kuahidi kugharimia mazishi yake.

Akizungumza leo Februari 18,2018 na vyombo vya habari, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako amesema pamoja na katibu mkuu wa wizara watahakikisha wanasimamia shughuli zote za msiba huo.

Amesema Akwilina alikuwa katika majukumu yake ya kawaida akipeleka barua yake ya mafunzo kwa vitendo Bagamoyo alipofariki dunia.

"Mafunzo yake kwa vitendo yalikuwa yanatarajiwa kuanza Februari 26, mwaka huu, hivyo kifo chake kimeleta simanzi kwa wananchi wote na Serikali kwa jumla.”

"Akwilina alikuwa ni miongoni mwa wanafunzi wa kike waliojipambanua kwa kujua umuhimu wa elimu, alihakikisha anasoma kwa bidii kwa manufaa yake na familia yake, lakini pia alinufaika na mkopo wa elimu ya juu," amesema Profesa Ndalichako.

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni amesema uchunguzi wa tukio hilo utafanyika haraka iwekezanavyo, kwa weledi na utaalamu ili haki itendeke.

"Tutafanya uchunguzi na kuwachukulia hatua kali za kisheria wote watakaobainika kuhusika na tukio hilo, Serikali tunasikitishwa na kifo cha mwanafunzi huyu, pia na kujeruhiwa raia na askari polisi wawili," amesema Masauni.

Amesema Serikali haiwezi kuyaacha matukio hayo yapite kama yalivyo, hivyo imeyachukulia kwa uzito unaostahili.

PICHA: Waziri Ndalichako,Masauni watoa mkono wa pole kwa wafiwa kifo cha Mwanafunzi aliyepigwa Risasi

$
0
0
Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi Prof Joyce Ndalichako pamoja na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ,Injinia Hamad Masauni  wakimfariji Mama Mzazi wa marehemu  Aqwilina jioni ya leo Mbezi Kimara jijini Dar.

***
Mwanafunzi  huyo wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji(NIT) amepoteza maisha baada ya kupigwa risasi Februari 16 mwaka huu eneo la Mkwajuni jijini Dar es Salaam wakati Polisi walipokuwa wakizuia maandamano ya chama cha CHADEMA.Kufuatia kifo cha Mwanafunzi huyo Serikali imesema itabeba jukumu la Mazishi yake.

Aidha Rais Dkt John Pombe Magufuli  amesema amesikitishwa sana na kifo cha mwanafunzi huyo,Aqwilina Akwilini wa Chuo cha Usafirishaji (NIT).

"Natoa pole kwa familia,ndugu,wanafunzi wa NIT na wote walioguswa na msiba huu.Nimeviagiza vyombo vya dola kufanya uchunguzi na kuwachukulia hatua za kisheria waliosababisha tukio hili",Ilisema sehemu ya taarifa yake iliyotolewa mapema leo.
Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi Prof Joyce Ndalichako (tatu kulia) akiwafariji Mama Mzazi wa marehemu  Aqwilina pamoja na ndugu jioni ya leo Mbezi Kimara jijini Dar
 Mama wa Marehemu Akwiline akilia kwa uchungu mara baada ya kuona viongozi wa Waandamizi wa serikali walipofika nyumbani kwake,Mbezi Kimara jioni ya leo kwa lengo la kutoa pole na kufahamu taratibu mbalimbali za msiba huo.

PICHA: IGP Sirro amefika katika Msiba wa Mwanafunzi Aliyepigwa Risasi

$
0
0
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Nyakoro Sirro, leo amefika kwenye msiba wa aliyekuwa mwanafunzi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Akwilina Akwilini ambaye aliuawa kwa kupigwa risasi juzi Ijumaa eneo la Mkwajuni, Kinondoni, Dar. Msiba huo upo nyumbani kwao Akwilina maneo ya Mbezi jijini Dar.

Kauli ya Waziri Mwigulu Nchemba kuhusu Mwanafunzi Aliyepigwa Risasi

$
0
0
Waziri wa Mambo ya ndani ya Nchi Dr. Mwigulu Nchemba amemuagiza Mkuu wa jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro na timu ya uchunguzi kutoka jeshi la polisi kufanya uchunguzi wa kina juu ya kupigwa risasi kwa mwanafunzi Akwilina Maftah.

Waziri Nchemba ametoa maagizo hayo akiwa mkoani Geita wilaya ya Chato wakati wa uzinduzi wa Gereza la wilaya ya Chato.

Waziri Dr. Mwigulu amelitaka jeshi la polisi kuchunguza kwa kina tukio hilo na kuchukua hatua kwa askari aliyehusika na hilo na kuwaambia wananchi nini kinachoendelea.

“Kama Waziri mwenye dhamana nalaani vikali sana tukio la kupoteza maisha ya binti wetu ambaye hakua na hatia, matukio ya namna hii naona yanaanza kujirudia tena kwa kasi matukio ya kupoteza maisha kwa watu wasiokuwa na hatia hasahasa katika masuala yanayohusu siasa ni mambo ambayo hayakubaliki na ninalaani kwa nguvu zote.” -Waziri Mwigulu

Dr. Mwigulu amewataka wananchi wote kuepuka vitendo hivi vinavyoweza kusababisha madhara kwa namna moja au nyingine na wanapoona matukio ya namna hii watoe ushirikiano kwa vyombo vya ulinzi na usalama ili wahusika wafikishwe katika vyombo vya usalama.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatatu ya February 19

Jinsi Punyeto Inavyo Sababisha Ukosefu Na Upungufu Wa Nguvu za Kiume

$
0
0
Ukosefu  na/ama  upungufu  wa  nguvu  za  kiume, ni  tatizo  linalo  wakabili  mamilioni  ya  wanaume  duniani.  Zipo  sababu  nyingi  zinazo  sababisha  tatizo  la  ukosefu  wa  nguvu  za  kiume.  

Miongoni  mwa  sababu  hizo  ni  pamoja  na  maradhi  kisukari, presha,shinikizo  la  damu, moyo, figo, matatizo  kwenye  mishipa  ya  ubongo  &  mishipa  ya  uti  wa mgongo, matatizo  kwenye  mishipa itumikayo  kusafrisha damu  mwilini, maradhi  ya  ngiri,  pamoja  na   upigaji  punyeto  kwa  muda  mrefu.

Katika  makala  yetu  ya  leo, tutaangalia  namna   suala  la  upigaji  punyeto linavyo  athiri  nguvu  za  kiume.

Kabla  hatujaangalia  namna  suala la upigaji  punyeto linavyo  maliza  nguvu  za  kiume, ni  vyema  tukafahamu  kwanza  kuhusu  SAYANSI  YA  MFUMO  WA  NGUVU  ZA  KIUME.

Kufahamu   kuhusu   SAYANSI  YA  MFUMO  WA  NGUVU  ZA  KIUME  tafadhali  tembelea :

Ukisoma  vizuri  kuhusu  mfumo  wa  nguvu  za  kiume, utagundua  kuwa   Suala  la  nguvu  za  kiume  ni  suala  la  kimfumo.  Ili  mwanaume  awe na nguvu  za  kiume, aendelee  kuwa  na  nguvu  za  kiume na  azilinde  nguvu  zake za  kiume, ni  lazima  ogani  zote zinazo  husika  na  mfumo  wa  nguvu  za  kiume  ziwe  na  afya  njema  na  ziwe  na  ushirikiano   thabiti  na  wenye  afya.

Vile  vile , utagundua  kuwa , mambo  makuu  muhimu  katika   mfumo  wa  nguvu  za  kiume  ni  kama  ifuatavyo:

i.Mishipa  imara  ya  ubongo  na  yenye  afya  njema

ii. Mishipa  imara  ya  uti  wa  mgongo  (  spinal  cords )

iii.Mishipa  imara  itumikayo  kusafirisha  damu  mwilini  (  Blood Vessels )

iv. Mfumo  imara  wa  usafirishaji  damu  mwilini

v. Mishipa  ya  uume  iliyo  imara  na  yenye  afya  njema

vi. Uhusiano  imara  na  wenye  afya  kati  ya  mishipa  ya  fahamu  iliyopo  katika  ubongo, mishipa  ya  kwenye  uti  wa  mgongo  pamoja  na  misuli & mishipa  ya  kwenye  uume.

Hivyo  basi, ili  mwanaume  aweze  kuwa  na  nguvu  imara  za  kiume, na  aendelee  kuwa  na  nguvu  hizo ni  lazima  mambo  yote  muhimu  katika  mfumo  wa  nguvu za  kiume  yawe  imara  pasi na  hitilafu  yoyote.

Hitilafu  yoyote  katika  mambo  hayo, itasababisha  ukosefu na/ama  upungufu wa  nguvu  za  kiume  kwa  mwanaume  huyo.  Pale inapotokea    hitilafu  ama  mapungufu  katika  ogani  zaidi  ya  moja  kati  ya  zilizo  tajwa hapo  juu, basi  tatizo  kwa  muhusika  huwa  kubwa  mara  dufu.

JINSI  PUNYETO  INAVYO  SABABISHA  TATIZO  LA  UKOSEFU &  UPUNGUFU  WA  NGUVU  ZA  KIUME.
Mwanaume   anapopatwa na  wazo  la  kufanya  tendo  la  ndoa, ubongo  hutoa  ishara  kwenye  mishipa  ya  uti  wa  mgongo  ambayo  nayo  husafirisha  taarifa  hadi  kwenye  mishipa &  misuli  ya  uume.

Mishipa  ya  uume inapopokea  taarifa  hiyo, hutanuka. Na  mishipa  ya  uume  inapotanuka, hufanya  mambo  mawili  muhimu  sana :

i.Husababisha  mishipa  ya  ateri  kupanuka  na  hivyo  kuruhusu  damu  kuingia kwa  kasi  sana   ndani  ya  mishipa  ya  uume  na  hivyo  kuufanya  uume  usimame  na  kuwa  imara  bara bara.

ii. Huibinya na  kuiziba  mishipa  ya  vena  na  hivyo  kuzuia  kunyonya  ama  kufyonza  damu  iliyo  ingia  ndani  ya  mishipa ya  uume.  (  KAZI  KUBWA  YA  MISHIPA  YA  VENA  ILIYO  KARIBU NA  MISHIPA  YA  UUME  NI KUHAKIKISHA  HAKUNA  DAMU NDANI YA  MISHIPA  YA  UUME. HIVYO  BASI  DAMU  INAPOINGIA  NDANI YA  MISHIPA  YA  UUME, MISHIPA  YA  VENA  HU “SENSE” JAMBO  HILO  KWA  HARAKA  NA HIVYO  KUIFYONZA  DAMU  HIYO  KUTOKA KWENYE MISHIPA  YA UUME  YA  KUITOA  NJE YA MISHIPA  YA  UUME.  NA  DAMU INAPOKOSEKANA  NDANI  YA  MISHIPA  YA  UUME, HUUFANYA  UUME  KUSINYAA  NA  KULEGEA )

Mtu  anayepiga  punyeto  husababisha  mambo  yafuatayo  katika  mwili  wake :

1. Huuwa  nguvu  ya  mishipa  & misuli ya  uume ambayo  ndio  inayo husika  na  kusimama  kwa  uume

2. Mishipa  ya   uume  inapo  sinyaa  na  kukosa  nguvu  yake  ya  asili, husababisha  mambo  yafuatayo :

i.Huondoa  uwezo  wa  mishipa  &  misuli  ya  uume  kutanuka, na  hii  ndio  sababu  inayo  wafanya  waathirika  wa  punyeto  kutumia  nguvu  nyingi  sana  katika  kuufanya  uume  usimame.

ii.Huondoa  uwezo  wa  mishipa &  misuli  ya  uume  kuibana  na  kuiziba  mishipa  ya  vena, na  hii ndio  sababu  inayo  fanya  waathirika  wa  punyeto  kufika  kileleni  haraka  sana, kwani damu  inayo  ingia  kwenye misuli  ya  uume   hufyonzwa  ndani ya  muda  mfupi sana. 
 
 Hii  hutokea  kwa  sababu  mishipa na  misuli  ya  uume inakuwa  imelegea,na  mishipa  ya  vena inakuwa  imepwaya, hivyo  msuguano wowote ule  hufanya  mishipa  ya  vena  kufunguka  na  kufyonza  damu  kutoka  kwenye mishipa  ya  uume  na hivyo  kuufanya  uume  kusinyaa  ndani ya dakika ama sekunde  chache sana.

3. Vile  vile  punyeto  hufanya  uume  kusinyaa na  kurudi ndani  na  kuufanya  uonekane kama  uume  wa  motto mdogo.

Kwa  ufupi  punyeto  husababisha  ukosefu  wa  nguvu  za  kiume  kwa  sababu  kuu  zifuatazo :

i.Kwanza   hudhoofisha  na  kuharibu  mishipa  ya  uume,  ambayo  ndio  hufanya  uume kusimama.

ii.Pili  hudhoofisha  utendaji  kazi  wa  mishipa  ya  ateri, ambayo  ndio  hutumika  kama  njia  ya  kusafirisha  damu kupeleka kwenye  misuli  ya  uume  na  ivyo  kuufanya  uume  usimame

iii. Tatu, punyeto  hupelekea  kuvuja  kwa  mishipa  ya  vena  na  hivyo  kusababisha  damu  kufyonzwa  kwa  haraka  sana  kila  iingiapo ndani  ya  misuli ya  uume  na  matokeo  yake  ni  uume   kusimama  kwa  muda  mfupi  sana  wakati wa  tendo  la  ndoa.

iv. Punyeto  huathiri  mtiririko  wa  damu  kwenda  kwenye  mishipa  ya  uume, kwa  sababu  hudhoofisha  misuli &  mishipa  ya  uume  pamoja  na mishipa ya  ateri  ambayo  ndio  hutumika  katika  kusafirisha  damu kwenda  kwenye  uume

DALILI  ZA  MTU  ALIYE  ATHIRIWA  NA  PUNYETO
Dalili  kuu  za  mtu  aliye athiriwa  na  punyeto  ni  kama  ifuatavyo:

i.           Uume  kusinyaa  na  kuwa  kama  wa  mtoto
ii.         Uume kurudi  ndani
iii.       Uume  kusimama  ukiwa  legelege
iv.       Kufika  kileleni  haraka  wakati  wa  tendo  la  ndoa.

TIBA   YA   NGUVU  ZA  KIUME  KWA MTU  ALIYE  ATHIRIKA  NA  PUNYETO.
Dawa   asilia  ya  nguvu  za  kiume iitwayo JIKO  ni tiba  bora  na  ya  uhakika  kabisa  kwa  mtu  aliye  athiriwa   na  punyeto.  Dawa  hii, pamoja  na  mambo  mengine  mengi, husaidia  kufanya  mambio  yafuatayo  katika  mwili  wa  mwanaume  aliye  athiriwa  na  punyeto :

i.Kuimarisha  mishipa  & misuli  ya  uume  ulio  legea na  hivyo  kuurejeshea  uwezo wake wa  asili

ii. Hutibu   tatizo  la  uume  kurudi  ndani

iii.Humaliza  tatizo  la  kusimama  kwa  uume  ukiwa  legelege

iv.Hutibu  na  kuponya  kabisa  tatizo  la  kufika  kieleleni  haraka.

BEI  YA  DAWA  :  Dawa  hii  inapatikana  kwa  gharama  ya  SHILINGI  ELFU  THEMANINI  TU (Tsh. 80,000/=)

MAHALI  INAPOPATIKANA :  Dawa  hii  inapatikana  katika  duka  la  dawa  asilia  liitwalo  NEEMA  HERBALIST  &  NUTRITIONAL  FOODS  CLINIC  lililopo  jijini  DAR  ES  SALAAM  katika  eneo  la  UBUNGO   nyuma  ya  jengo  la  UBUNGO  PLAZA   karibu  na SHULE  YA  MSINGI  UBUNGO  NATIONAL  HOUSING.

Kwa  wateja  wasio  weza  kufika  ofisini  kwetu. Watafikishiwa  dawa  mahali  popote  walipo  jijini  DAR  ES  SALAAM.

Kwa   wateja  waliopo  mikoani  watatumiwa  dawa  kwa  njia  ya  MABASI

Kwa  wateja  waliopo   Zanzibar  wata fikishiwa  dawa  kwa  njia  ya  usafiri  wa boti.

Na  kwa  wateja  waliopo  UGHAIBUNI  watatumiwa  dawa  kwa  njia  ya  POSTA  ama  DHL.

MAWASILIANO :  WASILIANA  NASI   KWA  SIMU  NAMBA  0766  53  83  84.

Kwa  taarifa  zaidi  kuhusu  huduma  zetu, tutembelee kila  siku  kwenye  blogu  yetu :

Waziri Mkuu Ampa Siku 3 Mkurugenzi Ajiieleze Matumizi ya Milioni 350

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ametoa siku tatu kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Ukerewe Bw. Frank Bahati aeleze amepeleka wapi zaidi ya sh milioni 350 zilizotolewa na Serikali kwa ajili ya miradi mbalimbali.

Ametoa agizo hilo jana (Jumapili, Februari 18, 2018) wakati akizungumza na madiwani na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe akiwa katika siku ya nne ya ziara yake ya kikazi mkoani Mwanza.

Waziri Mkuu amesema Serikali haiwezi kuvumia kuona fedha inazopeleka katika halmashauri hiyo kwa ajili ya kugharamia miradi na kulipa madai ya watumishi zinatumika kinyume na maelekezo.

Alisema miongoni mwa fedha hizo ni sh. milioni 451.47 za miradi ya miradi ya maendeleo (CDG), ambapo zilizotumika ni sh. milioni 221.9 tu.” Namtaka Mkurugenzi na Muweka hazina wa Halmashauri hii Bw. Peter Molel tarehe 21 waje Mwanza wanieleze walikopeleka fedha hizo.”

Waziri Mkuu amesema fedha zingine ni sh. milioni 50 za ziizotolewa na Serikali kwa ajili ya kulipa madai mbalimbali ya watumishi kama likizo ambapo zililipwa sh. milioni 13 na zingine hazijulikani zilipo.

Pia Serikali ilitoa sh. milioni 65 za kugharamia mradi wa umwagiliaji wa Bugorola ambazo nazo hazijulikani zilipo pamoja na sh. milioni 84 zilizotolewa kwa ajili ya kulipa motisha kwa walimu ambapo zilizolipwa ni sh. milioni 60 tu.

“Kama mlidhani Ukerewe ni sehemu ya kutafunia fedha za umma mmekosea kwa sababu Serikali haiwezi kuvumia haya, Mkurugenzi umeaminika na kupewa dhamana ya kusimamia rasilimali za umma lakini unafanya tofauti.”

Waziri Mkuu amesisitiza kwamba lazima viongozi hao wahakikishe fedha zinazopelekwa na Serikali katika Halmashauri zao zikiwemo za utekelezaji wa miradi ya afya, elimu, uvuvi zinatumika kama ilivyoelekezwa na si vinginevyo.

Pia Waziri Mkuu amemuagiza Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza asimamie utendaji wa viongozi na watumishi katika  wilaya zote za mkoa huo na kisha kutoa taarifa kwa Mkuu wa Mkoa, Bw. John Mongella.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amewataka watumishi wa Halmashauri hiyo wasikubali kugawanywa kwa sababu ya maslahi ya watu ambayo hayana tija kwao na hata kwa wananchi wa wilaya hiyo.

Waziri Mkuu ameyasema hayo baada ya kubaini kuwepo kwa mgogoro kati ya Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Bw. Bahari pamoja na Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Bw. George Nyamaha ambao wamekuwa wakiwagawa watumishi.

Amewataka viongozi hao kurekebisha tofauti zao kwa sababu mgogoro wao umesababisha watumishi kugawanyika, hivyo kuwaumiza wananchi wa wilaya ya Ukerewe kwa kushindwa kuwahudumia vizuri jambo ambalo halikubaliki.

(mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMAPILI, FEBRUARI 18, 2018.

Makamu wa Rais awasili mkoani Mwanza kwa ziara ya kikazi

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amewasili Jijini Mwanza jana jioni  na kupokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka.

Makamu wa Rais anategemewa kuanza ziara ya kuhamasisha shughuli za kimaendeleo leo mkoani Simiyu.

Katika ziara hiyo inayoanza leo tarehe 19/2/2018 na kumalizika tarehe 22/2/2018, Makamu wa Rais atakagua maendeleo ya ujenzi wa mradi  wa maji Kiloleli na kuweka jiwe la msingi na baada ya hapo atazungumza na wanachi Lamadi.

Pia Makamu wa Rais ataweka jiwe la msingi kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za viongozi wa mkoa  katika eneo la Nyaumata.

Miradi mingine ambayo Makamu wa Rais ataitembelea ni Kukagua Ujenzi wa Barabara za Lami Bariadi mjini chini ya Programu ya uimarishaji wa Serikali za Mitaa za Mjini.

Makamu wa Rais atakagua maendeleo ya ujenzi wa bwawa la Mwanjoro na kusalimia wananchi siku ya tarehe 20, pia atasalimia wananchi wa Mwanhuzi Mjini, Mwandoya (Meatu)

Tarehe 21, Makamu wa Rais atafungua Kongamano la Elimu ya Juu na Uchumi wa Viwanda Tanzania kisha atafungua jengo la Utawala la halmashauri ya Itilima na kusalimia wananchi, kufungua jengo la upasuaji  la Samia Suluhu  Hassan katika Hospitali ya Wilaya  ya Maswa na kuzungumza na wananchi katika viwanja vya nguzo nane.

Siku ya tarehe 22, Makamu wa Rais ataongoza Mahafali  ya 34 ya Chuo Kikuu Huria.

Waziri Mkuu Aagiza Sekondari Ya Pius Msekwa Ipewe Gari

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemtaka Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Ukerewe Bw. Frank Bahati awe amepeleka gari katika shule ya Sekondari ya bweni ya Pius Msekwa ifikapo Februari 25 mwaka huu.

Amesema shule hiyo yenye wanafunzi zaidi ya 700 lazima iwe na chombo cha usafiri kitakachotumika kwa ajili ya shughuli mbalimbali ikiwa ni pamoja na dharura za kuwapeleka hospitali wanafunzi pale wanapougua.

Waziri Mkuu alitoa agizo hilo jana (Jumapili, Februari 18, 2018) wakati alipotembelea shule hiyo na kuzindua madarasa na mabweni yaliyojengwa kupitia mradi wa Mpango wa Elimu wa lipa kulingana na Matokeo (EP4R).

“Wakurugenzi mnatakiwa kutambua shule hizi ni zenu, hivyo mnapaswa kuzihudumia. Shule hii inawafunzi zaidi ya 700 na wanalala hapa hapa hivyo lazima kuwe na gari la kuwahudumia wanafunzi hasa wakati wa dharura.”

Alisema Serikali haiwezi kuiacha shule hiyo bila ya kuwa na chombo cha usafiri, ambapo alimsisitiza Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo kuhakikisha anatoa kipaumbele kwa taasisi za umma ili ziweze kutekeleza majukumu yake ipasavyo.

Hata hivyo, Waziri Mkuu aliwwagiza Wakurugenzi wote nchini kushirikiana na uongozi wa shule mbalimbali za Serikali katika kutatua baadhi ya changamoto zinazoikabili.

Miongoni mwa changamoto hizo ni malipo ya watumishi wasaidizi wakiwemo wapishi, walinzi na madereva, ambapo aliwataka wachukue jukumu la kuwalipa watumishi hao badala ya kuacha ya kuwaachia Wakuu wa Shule.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu aliziagiza halmashauri zote nchini kuhakikisha zinamalizia ujenzi wa vyumba vya maabara katika shule zao zilizobaki na Serikali itasambaza vifaa vya maabara mara zitakapokamilika.

Waziri Mkuu alisema tayari Serikali ilishasambaza vifaa vya maabara katika shule 1,696 za sekondari nchini ambazo zilikamilisha ujenzi.

(mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMATATU, FEBRUARI 19, 2018.

Waziri Mkuu Azindua Mradi Wa Maji Ukerewe......Awataka Viongozi Wa Wilaya Wahakikishe Unakuwa Endelevu

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amezindua mradi wa maji katika kijiji cha Bwasa katika mji wa Nansio wilayani Ukerewe na kuuagiza uongozi wa wilaya hiyo kuhakikisha maji hayo yanatoka wakati wote na mradi huo unakuwa endelevu.
 
Waziri Mkuu alizindua mradi huo jana (Jumapili, Februari 18, 2018) wakati akiwa katika siku ya nne ya ziara yake ya kikazi mkoani Mwanza. Alisema Serikali imedhamiria kumaliza tatizo la upatikanaji wa maji safi na salama nchini.

Baada ya kuzindua mradi huo, Waziri Mkuu alizungumza na wananchi wa mji wa Nansio kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika Uwanja wa Getrude Mongella, ambapo alisema mradi aliouzindua katika kijiji cha Bwasa ni sehemu ya mradi wa maji wa Kazilankanda utakaohudumia vijiji 13 vya wilaya hiyo.

Alisema mradi huo unagharimu shilingi bilioni saba na unatekelezwa katika vijiji vya Muhula, Mahande, Namasabo, Namagondo, Kazilankanda, Malegea, Igalla, Kigara, Lutare, Busunda, Bwasa, Buhima, Hamuyebe  na utahudumia wakazi  68,038 pindi utakapokamilika.

Mkataba wa Mradi huo ulisainiwa Machi 2013 na unatarajiwa kukamilika ifikapo April, 2018, ambapo hadi sasa jumla ya shilingi bilioni 5.637 sawa na asilimia 78.26 tayari zimeshatumika na mradi umekamilika kwa asilimia 92 na tayari baadhi vijiji vimeanza kupata maji.

Waziri Mkuu alisema mkakati wa Serikali ni kuwahudumia wananchi kwa kutatua kero zinazowakabili ikiwemo ya upatikanaji wa maji, ambapo imedhamiria kuendelea kusambaza huduma hiyo hadi vijijini ili kuhakikisha vyote vinapata maji.

Waziri Mkuu alisema Serikali inatekeleza Kampeni ya Rais Dkt. John Magufuli ya kumtua mama ndoo kichwani, inayolenga kuwaondolea wananchi tatizo la upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama katika umbali usiozidi mita 400 kutoka kwenye makazi yao.

Waziri Mkuu aliwaambia wananchi kuwa Serikali ya Awamu ya Tano ina mikakati mizuri inayolenga kuondoa tatizo la maji kote nchini  ili kusaidia wananchi hao hasa wanawake kutumia muda mwingi kufanya kazi za maendeleo kuliko kutafuta maji.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu alimuagiza Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe, Bw. Estomihn Chang’ah apange siku maalumu kwa ajili ya kusikiliza kero mbalimbali zinazowakabili wananchi hususani za ardhi na kushirikiana nao katika kuzipatia ufumbuzi.

Pia Waziri Mkuu alimuagiza Mkuu huyo wa wilaya leo saa 3.00 asubuhi akiwa na watumishi wa Idara ya Ardhi akutane na wananchi wote wenye malalamiko ya ardhi ili ashirikiane nao katika kuyapatia ufumbuzi. Alitoa agizo hilo baada ya kupokea malalamiko mengi ya wananchi yahusuyo masuala ya ardhi yaliyowasilishwa kwake kupitia njia ya mabango.

Alisema kwa sababu ya kutotekeleza wajibu wao ipasavyo kumekuwa na kero na malalamiko mengi kutoka kwa wananchi na hivyo kusababisha wananchi kuwasilisha kero na malalamiko hayo wakati wa ziara za viongozi wakuu wa nchi.

Awali, Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Bw. Luhaga Mpina aliwaomba wananchi hao kutunza rasilimali zilizopo ndani ya ziwa Victoria na kujiepusha na uvuvi haramu kwa sababu unatishia uwepo wa samaki ndani ya ziwa hilo.

Waziri huyo alisema iwapo vitendo vya uvuvi haramu vikiachwa bila ya kuzuiwa kuna uwezekano mkubwa wa samaki kutoweka ndani ya ziwa hilo baada ya miaka miwili. Alisema tayari Serikali inaendelea na operesheni ya kupambana na uvuvi haramu.

(mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMATATU, FEBRUARI 19, 2018.

Mwanamke achomwa moto na waganga wa jadi akitafuta uzazi

$
0
0
Jeshi la Polisi Mkoa wa Kipolisi wa Tarime/Rorya, linawashikilia waganga wa jadi wawili ambapo mmoja ni mkazi wa Kijiji cha Obwere na Michael Jacob wa Omuga kwa tuhuma za kumjeruhi kwa kumuunguza moto, Emiliana Thomas anayeishi Kijiji cha Omuga wilayani Rorya.

Kamanda wa Polisi wa mkoa huo, Henry Mwaibambe alisema jana kuwa, majeruhi huyo ambaye ni mwanamke anayesumbuliwa na tatizo la kutopata ujauzito, waganga hao walimwaminisha kuwa ataupata.

Alisema walimwambia ili apate mtoto ni mpaka kuku imwagiwe mafuta ya taa na iteketezwe moto huku mama huyo akiwa ameishikilia mikononi.

Kamanda alisema baada ya waganga hao kuwasha moto ulimunguza na kumsababishia majeraha.

Mwaibambe alisema, awali waganga hao walimweleza mwanamke huyo kuwa anasumbuliwa na mashetani ndani ya tumbo na ndio yanayomfanya asizae.

Alisema walimweleza kwamba kuku ikiteketea ikiwa mikononi mwake atakuwa ameondokana na mashetani, hivyo ni lazima iteketezwe.

Kamanda huyo alisema baada ya waganga hao ‘kumsomesha’ mwanamke huyo alikubali na ndipo walipoimwagia mafuta ya taa kuku hiyo na kuwasha moto kwa kibiriti uliolipuka na kumjeruhi kifuani na mikononi.

Mwaibambe aliongeza kuwa, hali ya mama huyo ni mbaya na anaendelea na matibabu katika Hospital ya Kowak wilayani humo.

Mmoja wa waganga hao wa jadi, Jacob alisema tukio hilo ni ‘bahati mbaya’.

“Alikuja akiomba tiba, sasa kwa bahati mbaya mafuta yalikuwa yamemumwagikia mikononi na mikono ya nguo aliyokuwa amevaa ilikuwa hadi mikononi, wakati tumewasha moto ndipo ukamuunguza,” alisema Jacob.

Mwakilishi wa Chama cha Tiba Asili mkoani Mara, Jacob Matiko alilaani kitendo hicho kuwa hakiendani na taratibu za tiba na kinakiuka sheria inayozuia vitendo hivyo huku akiwataka waganga kutofanya utapeli iwapo hawawezi kufanya tiba kama matabibu asili.

TANGA RAHA- Sehemu ya Nane ( 8 )

$
0
0
MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA
ILIPOISHIA
Simu yangu ikaanza kuita nikapiga hatua za haraka kwenda kuipokea huku nikimgonga kidogo muhudumu begani kitendo cha kuinama na kuiokota suruali yangu iliyopo chini ili kuitoa simu yangu mfukoni gafla taulo langu likafunguka na kudondoka chini huku muhudumu akibaki ananishangaa.

ENDELEA
  Nikashika na bumbuwazi huku nisijue ni nini nifanye huku muhudumu akiwa hakwepeshi hata jicho katika kunitazama katika kiko yangu.Nikaitoa simu na kukuta ni Rahma anaye piga.Nikaipokea huku nikiwa ninaliokota taulo taratibu
“Baby umeshaletewa chakula”
“Ndio baby”
“Ok mimi nimeshafika kwa bibi nikitaka kuja huko nitakuambia”
“Sawa mke wangu”
Nikakata simu na kumkuta muhudumu akiwa anmenata kama amedandishwa na superglue kwani hakutingishika wala kukwepesha sura yake katika taulo ambalo limeifunika koki yangu
“Hei dada…..dada”

    Akastuka na kwa aibu akatoka pasipo kuzungumza chochote na akaufunga mlango na nikabaki nikijifikiria ni kitu gani cha ajabu alicho kiona muhudumu mpaka akawa anashangaa kiasi cha kunifanya nimshangae.Nikala chakula ambacho kimeletwa na muhudumu kwenye chumba changu.Nikamaliza na kuvaa nguo zangu na kwenda kutembelea maeneo ya hteli hiyo yenye mandhari mazuri ya kupendeza.

Nikatafuta sehemu ya kukaa iliyopo kandokando ya swimming pool na kagizia juisi baridi na kuanza kunywa huku nikimsubiri Rahma kuja kunihukua.Nikiwa ninaendelea kunywa juisi yangu kuna wasichana wawili warembo wakaja kukaa kwenye kitanda kilichopo pembeni yangu huku wakianza kuvua nguo zao kwa ajili ya kuogelea katika swimming pool hilo

    Wakabaki na nguo zao za ndani na kujitosa ndani ya maji na kuanza kuogelea.Wakiwa wanaendelea kuogelea mmoja anayeonekana si mzoefu sana katika kuogelea akaanza kupiga kelele ya kuomba msaada wa kuokolewa.Nikanyanyuka haraka haraka na kuvua viatu na kuitoa wallet yangu yenye pesa pamoja na simu mfukoni na kujitosa ndani ya maji.Nikaogelea hadi katika eneo alilo kuwepo nikamsubiria maji ya mlegeze kwanza kwa sekunde kadhaa nikihofia enedapo nikimuokoa akiwa katika hali yake ya kuwa na nguvu anaweza kunizamisha na mbaya zaidi sehemu waliyopo katika swimming pool hilo kuna kina kirefu kwenda chini.

Nikamshika vizuri na kwenda naye njee na kumlaza katika ukingo wa swimming pool hilo huku nikianza kumminya minya kifuani ili atapike maji aliyo yanywa nikaanza kumpa pumzi kwa kumpulizia mdomoni kwake.Wahudumu wa kiume wa hotel wakawa tayari wameshafika katika eneo hilo na kunisaidia katika zoezi la kumtapisha msichana huyo huku mwenzake akiwa pembeni akilia

==>Endelea Nayo <<kwa Kubofya Hapa>>

Zitto Kabwe kufanya ziara Nchi Nzima katika Kata zinazoongozwa na ACT Wazalendo

$
0
0
Viongozi wa Chama cha ACT- Wazalendo wakiongozwa na Zitto Kabwe wameanza ziara katika mikoa minane kutembelea kata ambazo zinaongozwa na chama hicho.

Taarifa kwa umma, iliyotolewa leo Jumatatu Februari 19, 2018 na Zitto, imesema katika ziara hiyo ameambatana na mwenyekiti wa kamati ya chama hicho inayoshughulia Bunge na Serikali za Mitaa, Annamarrystella Mallack, katibu wa kamati hiyo, Janeth Rithe na mwenyekiti wa Kamati ya Sera na Utafiti, Emmanuel Mvula.

Zitto ambaye pia ni mbunge wa Kigoma Mjini amesema: “Tumeanza ziara ya mikoa minane kutembelea kata mbalimbali ambazo wananchi walichagua madiwani kutoka chama chetu katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015.”

“Ziara itafanyika kwa siku 19 katika mikoa minane husika, ambako leo (Februari 19,2018) tumeanzia Kata ya Kiparang’anda, Wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani.”

Amesema lengo la ziara ni kuwashukuru wananchi, kushiriki kazi za maendeleo katika kata, kuzungumza na kamati ya maendeleo ya kata, kuzungumza na wananchi husika, kuangalia utendaji wa madiwani kutokana na matarajio ya wananchi, kuona vikwazo na changamoto za madiwani wao.

Pia, amesema watasisitiza uwazi, uwajibikaji na ushirikishwaji wa wananchi kwenye masuala yote ya kata, pamoja na kufanya tafiti juu ya masuala ya kisera na miradi ya maendeleo ambayo ACT Wazalendo Taifa wanaweza kuyabeba kusaidia madiwani.

Diamond Platnumz atangaza ziara yake ya muziki nchini Marekani

$
0
0
Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz ametangaza ziara yake ya muziki nchini Marekani ambapo atatumbuiza kwenye majiji 12 nchini humo.

Ziara hiyo inayoanza tarehe 22 June hadi 23 July 2018, Diamond atawapagawisha kwa burudani wakazi wa Majiji ya New York, Los Angeles, Minnesota, Houston, Seattle, Kansas City, Washington DC, Boston, Atlanta, Columbus, Philadephia, Dallas.

“Kuelekea kwenye Kuachiwa Rasmi kwa Albam ya #AboyFromTandale Ndugu zangu Mlio Marekani Jiandaeni kwa Ziara ya #AboyFromTandaleUSATour ndani ya State hizo 12 kuanzia tareh 22/06 hadi 23/07 Mwaka 2018!!“amesema Diamond Platnumz.

Ziara hiyo ya ‘A Boy From Tandale’ itakuja baada ya kuachiwa kwa album yake ya ‘A Boy From Tandale’ mwezi Machi 14, 2018.

Mahakama yaamuru ‘Nabii Tito’ akapimwe Mirembe.....Kesi Imeahirishwa hadi Machi 5

$
0
0
Mahakama ya Wilaya ya Dodoma imemuamuru mkuu wa Gereza la Isanga kumpeleka katika taasisi ya magonjwa ya akili mshtakiwa Onesmo Machibya maarufu Nabii Tito, ili kujua iwapo ana akili timamu au la.

Hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama hiyo, James Karayemaha ametoa agizo hilo leo Jumatatu Februari 19,2018.

Amesema Magereza wanachelewesha haki ya mshtakiwa na kwamba, anashangaa ni kwa nini wanashindwa kutekeleza agizo la kumpeleka kufanyiwa uchunguzi.

"Naagiza amri ya Mahakama itekelezwe, apelekwe taasisi ya magonjwa ya akili Isanga (Mirembe) si kama alivyoleta vielelezo kutoka Muhimbili," amesema Karayemaha.

Hakimu ameahirisha kesi hadi Machi 5,2018 itakapotajwa kwa ajili ya kupokea taarifa ya uchunguzi.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images