Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Serikali yawatoa hofu wananchi kuhusu umeme....Haya Ndo Mambo Ambayo Msemaji wa Serikali Kayasema

$
0
0
Serikali imewatoa hofu Watanzania kuhusu tatizo la umeme na utekelezaji wa mradi wa treni ya umeme nchini ambao ujenzi wake unaendelea.

Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji wa Serikali Dk Hassan Abass amesema jitihada zinaendelea kufanyika kuhakikisha umeme wa kutosha unazalishwa nchini.

Akizungumza na wanahabari leo Jumatatu jijini Dar es Salaam kuhusiana na utekelezaji wa ahadi za Serikali, Dk Abass amesema kazi ya kusanifu njia yote itakayopita reli hiyo ya umeme imeshakamilika.

"Suala la umeme sio tatizo Serikali inaendelea kutekeleza miradi zaidi ya  20 kuhakikisha nchi ina umeme wa uhakika,"

Dk Abass amesema Serikali kupitia kampuni Hodhi ya Rasilimali za Reli (Rahco) inatarajia kununua vichwa 23 vya treni ya umeme na viwili vya treni ya dizeli kwa ajili ya kuboresha usafiri wa reli.

Sambamba na hilo inatarajia pia kununua mitambo 25 ya ukarabati wa reli na mabehewa 1,590 kati ya hayo 1,530 yakiwa ya mizigo na 60 ni ya abiria.

Dk Abass amesema zabuni za manunuzi hayo zinatarajiwa kufunguliwa ndani ya mwezi huu.

Amesema kati ya mabehewa 60 ya abiria 15 ni daraja la kwanza na 45 daraja la kawaida.

Kuhusu usafiri wa majini Dk Abass amesema tayari Serikali imenunua meli mpya mbili za mizigo katika ziwa Nyasa.

Meli hizo Mv Njombe na  Mv Ruvuma na zina uwezo wa kubeba tani 1,000 kila moja na zimeanza kufanya kazi wiki iliyopita.

Serikali yatoa neno kuhusu Bombardier na Meli ya Tanzania iliyokamatwa na dawa za kulevya

$
0
0
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imetoa neno kwa mara ya kwanza kwa mwaka 2018 kuhusu ndege ya Tanzania aina ya Bombadier Q400 iliyozuliwa nchini Canada na Meli ya iliyosajiliwa kwa namba za Tanzania iliyokamatwa huko Jamhuri ya Domica na Shehena ya dawa za kulevya.

Kuhusu Bombardier Serikali kupitia kwa Msemaji wake Mkuu, Dkt. Abbas Hassan amesema bado ratiba ipo vile vile kuwa ndege hiyo ya Bombardier na ile kubwa ya Dreamliner zote zitafika nchini kati ya mwezi Juni na Julai mwaka huu.

“Ishu ya ndege tutaizungumza itakapofika wakati wake lakini mara ya mwisho nilisema ndege zote za serikali ambazo tumenunua ratiba yake ni kufikia mwezi Juni- Julai mwaka huu ndege zote nne ikiwemo ile ndege ya ndoto yetu ya Boeing Dreamliner zitakuwa zimefika nchini.“amesema Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi kwenye mkutano wake na Waandishi wa Habari.

Kwa upande mwingine Serikali imekiri kupokea taarifa za Meli yenye usajili wa Tanzania kukamatwa kwenye visiwa vya Jamhuri ya Dominika ikiwa na shehena ya dawa za kulevya aina ya Cocaine.

“Suala la meli iliyokamatwa Dominika hili nalifahamu, nimelisikia kwa hiyo wenzetu wa wizara ya mambo ya nje bado wanafuatilia kujua usahihi maanake imeripotiwa hivyo kwa hiyo wizara ya nje tumeshazungumza nao na wanalifanyia kazi kwahiyo kama kutakuwa na taarifa zitatolewa.“amesema Dkt. Hassan Abbasi.

Mnamo Desemba 31, 2017 Jeshi la Maji nchini Uholanzi liliikamata Meli yenye usajili wa Tanzania ikiwa na shehena ya dawa za kulevya aina ya Cocaine tani 1.6 ambapo Meli hiyo pamoja na wahusika waliokuwemo walishikiliwa nchini Jamhuri ya Dominika kwa uchunguzi zaidi.

Hii ndio benki mpya iliyopewa leseni ya biashara na Benki Kuu ya Tanzania

$
0
0
Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imetoa taarifa kwa kwa umma kuwa, imetoa leseni ya biashara kwa benki mpya yenye jina, Guaranty Trust Bank (Tanzania) Limited.

Leseni hiyo inatoa kibali kwa taasisi hiyo kutoa huduma za kibenki nchini Tanzania kama benki ya kibishara na imetolewa kuanzia Januari 5, 2018.

Makao Makuu ya Benki hiyo yanapatikana Kitalu namba 4, Regent Estate, Barabara ya Bagamoyo, jijini Dar es Salaam.

Hatua hiyo ya Benki Kuu imekuja siku chache tangu ilipozifutia leseni za biashara, benki 5 ambazo ni Covenant Bank, Efatha Bank, Njombe Community Bank, Kagera Farmers’ Cooperative Bank, na Meru Community Bank.

Benki Kuu ilizifungia benki hizo kutokana na kushuka kwa mtaji.

BREAKING: Mh. Edward Lowassa, Mbowe wamjulia hali Mzee Kingunge

$
0
0
Mwenyekiti CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe ameongozana na Waziri Mkuu Mstaafu na Mjumbe wa Kamati Kuu, Edward Lowassa kumjulia hali Mzee Kingunge Ngumbare Mwiru aliyelazwa katika Hospital ya Taifa ya Muhimbili anapopatiwa matibabu.

Mzee Kingunge anatibiwa majeraha baada ya kushambuliwa na mbwa nyumbani kwake.

Hivi karibuni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,alifika hospitalini hapo kumjulia hali mzee huyo.

Gigy Money akuta moto BASATA...Atakiwa Kuonana na Waziri

$
0
0
Siku moja baada ya Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza kumtaka msanii Gift Stanford  ‘Gigy Money’, kuripoti ofisini kwake, msanii huyo ameamua kwenda Baraza la Sanaa Tanzania( Basata).

Gigy ambaye alijipatia umaarufu kutokana na kupiga picha za kutatanisha  na kuzirusha katika mitandao mbalimbali ya kijamii, amesema ameamua kwenda Basata baada ya kuambiwa waziri hayupo.

Hata hivyo, amesema mpaka sasa hajui kosa analoitiwa na kama ni picha za utupu mbona ameshaacha tabia hiyo siku nyingi na sasa yupo busy kulea mimba yake.

“Najua wapo watu wanaodhani naitwa kwa ajili ya tabia zangu za kupiga picha za utupu, lakini mimi hayo mambo nishayaacha muda mrefu nadhani kwa wanaonijua Gigy wa sasa hivi sio wa kipindi kile, ila ngoja nisubiri waziri atakachoniambia japo najiona sina kosa lolote nililotenda kwa sasa tangu Rais alipotoa onyo kwa wasanii wanaovaa vibaya.

“Pia kwa wale wanaodhani labda ni kutokana na wimbo wangu wa Papa,  binafsi sina wasiwasi nayo kwa kuwa mimi nilimaanisha samaki, sasa kama kuna watu wameitafsiri kivingine ni wao,” amesema .

Kwa upande wake Katibu wa Basata, Godfrey Mngereza alikiri msanii huyo kufika katika ofisi zao zilizopo Ilala leo na kueleza kwamba hilo halimuondolei kuitikia wito wa waziri kwa kuwa yeye ndiye aliyemuita.

Mngereza amesema alichokiona kwa msanii huyo ni kwenda kwao akijua kwamba baraza hilo ndio mlezi wa wasanii na kubainisha kuwa hata wao walikuwa hawafurahishwi na aliyokuwa anayafanya msanii huyo japo hawajawahi kumuita hata siku moja.

Breaking: Kiongozi Mkubwa wa Upinzani Kesho Kutimkia CCM. ....Ni Nani Huyo? Endelea Kuwa Nasi

$
0
0
CCM kupitia kwa Katibu Mwenezi Humphrey Polepole kesho asubuhi wanasema watampokea kiongozi mkubwa wa Upinzani ambaye atajiunga na Chama cha Mapinduzi (CCM) .Je, ni nani huyo? Jibu litapatikana Kesho. 

Usikose Kuitembelea Mpekuzi Blog mapema asubuhi  kwa habari motomoto

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumanne ya January 9

Naibu Waziri Mpya wa Madini, Doto Biteko aanza kazi

$
0
0
Naibu Waziri wa Madini, Doto Mashaka Biteko ambaye ameapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli kuwa Naibu Waziri katika Wizara ya Madini tarehe 8 Januari, 2018 ameanza kazi rasmi kwa kufanya kikao na Viongozi na Watumishi wa Wizara husika.

Kikao hicho kimefanyika katika ukumbi wa Wizara jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo na Katibu Mkuu, Profesa Simon Msanjila.

Akizungumza katika kikao hicho, Naibu Waziri huyo alieleza kuhusu umuhimu wa kuwepo kwa ushirikiano kati ya viongozi na watumishi wa Wizara ili kwa pamoja wasimamie ipasavyo Rasilimali Madini na kuhakikisha kuwa inafaidisha Taifa.

“Ili kutimiza malengo ya Rais wetu ya kuhakikisha kuwa Rasimali Madini inaendelezwa ipasavyo, hatuna budi kushirikiana na kushikamana ili kuwe na umoja utakaoleta ufanisi katika utekelezaji wa majukumu kwani sisi sote ni watumishi wa watanzania,” alisema Biteko.

Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo amesema kuwa Uteuzi wa Naibu Waziri wa Pili katika Wizara ya Madini unaonesha namna Rais John Magufuli anavyoichukulia kwa umuhimu wa pekee Sekta ya Madini ambayo ni muhimu katika ukuaji wa uchumi wa nchi.

“Tutashirikiana kwa pamoja na watumishi wa Wizara ili kuweza kusukuma gurudumu la maendeleo ya Taifa mbele zaidi,” alisema Nyongo.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Profesa Simon Msanjila alisema kuwa viongozi hao na watumishi kwa pamoja watafanikisha mategemeo na malengo ya Rais John Magufuli ya kuhakikisha kuwa Rasimali Madini inalinufaisha Taifa.

Aidha alitumia fursa hiyo kuwaeleza watumishi kuhusu uamuzi wa Rais John Magufuli wa kutengua uteuzi wa Kamishna wa Madini, Mhandisi Benjamin Mchwampaka na kumteua Profesa Shukrani Elisha Manya kuwa Kamishna wa Madini na pia kukaimu nafasi ya Mtendaji Mkuu wa Kamisheni ya Madini na hivyo kuwaasa watumishi kumpa ushirikiano Kamishna huyo mpya.


Gavana mpya wa Benki Kuu ya Tanzania aanza kazi rasmi

$
0
0
Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Prof. Florens Luoga ameanza kazi jana  Januari 8, 2018 kwa kusema lugha ya kushindwa kukabiliana na changamoto haikubaliki katika taasisi hiyo.

==>Taarifa kamili iko hapo chini 

MC Pilipili Aipongeza Serkali kwa Kuwabana Wanoatupia Picha za UCHI Mitandaoni .....Aitaka Pia Imuhoji Idris na Kim Sasha

$
0
0
Baada ya Serikali kupitia Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kumuita msanii wa Bongo Fleva Gigy Money na Mwanamitindo Sanchoka kwa mahojiano maalumu kuhusu kazi zao ambazo zinaonekana zipo kinyume na maadili hususani kwenye mavazi wanayovaa, Hatimaye Mchekeshaji maarufu nchini Tanzania, MC Pilipili ameipongeza Serikali kwa hatua hiyo na kuishauri iendelee kuwasaka wengine wanaofanya hivyo.

MC Pilipili amesema amepokea taarifa hizo kwa mikono miwili ingawaje amesema kuna watu wengi mitandaoni wanafanya makosa kama hayo ya kuvaa nguo fupi au kuonesha maungo yao kwenye mitandao.

“Hiyo hatua mimi nimeipenda kwanza imeturudisha kwenye Maadili..Unajua hapa Bongo mtu anaweza akawa maarufu kwa kuposti maumbo yake tuu mtandaoni hii ni kinyume cha maadili,“amesema MC Pilipili na kuwataja watu wengine wanaokaa uchi mitandaoni

“Nilipatwa na maswali juzi Sancho ameitwa, Gigy Money kaitwa lakini pia kuna msanii mwingine alikuwa maarufu kwa kuposti picha kama hizo amejichora mitatuu anaitwa Agness, mwingine anaitwa Kim Sasha lakini wakati huo namuona Idris naye amevaa chupi hivi ile haihamasishi au naye aitwe?“amesema MC Pilipili.

Jamaa Katiwa Mbaroni Kwa Kutoboa bomba la mafuta ya Dizeli mali ya TPA na kujiunganishia bomba lake la mafuta hadi nyumbani

$
0
0
Askari wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), wakishirikiana na Jeshi la Polisi nchini, wanamshikilia Ndugu Samwel Nzagi Kilang'ani mwenye umri wa miaka (63), kwa tuhuma za kutoboa bomba la mafuta ya Dizeli la "Single Point Mooring" mali ya TPA na kujiunganishia bomba lake la mafuta hadi nyumbani kwake ambako ameweka mantaki makubwa ambayo ameyachimbia chini ya ardhi.

Msemaji wa TPA,  Janeth Ruzangi amethibitisha kukamatwa kwa mtu huyo huku polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam ikiendelea kumshikilia kwa uchunguzi zaidi.

LIVE BREAKING NEWS : Kiongozi mkubwa wa upinzani Anajiunga CCM Muda Huu.....Bofya Hapa kujionea

$
0
0
Kiongozi mkubwa wa upinzani Anajiunga CCM Muda Huu.....Bofya Hapa kujionea

Jipatie Dawa za Asili za Kupunguza Maziwa, Kutoa Michirizi, Kuondoa Chunusi, Kuongeza Maumbilie na Nguvu za Kiume

$
0
0
MAMBO MAPYA 2018
  Ktk kusajiliwa kwa kampuni ya  @natural_beauty_prod
Kwanza tunawatakia kheri ya mwaka mpya kwa wote. Pia tunakukalibisha tena kwenye kampuni yetu yenye bidhaa mpya zilizoingia kuanzia tar 01/01/2018. 

     Bidhaa hizi MPYA zimefanyiwa maboresho makubwa zaidi hivyo zina matokeo ya haraka kuliko ilivyokuwa awali.
  NI PAMOJA NA  HIZI👇🏼
☆Kutengeneza shepu (hips, makalio na mapaj) @200,000/=
☆Kurefusha nywele @130,000/=
☆Kuongeza urefu na upana wa uume @200,000/=
☆Kung'arisha mwili mzima na kuondoa sugu @150,000/=
☆Kupunguza unene na manyama uzembe @180,000/=
☆Kuongeza nguvu za kiume  hata kwa mwenye kisukari (diabetic) @180,000/=
☆Kuondoa mvi moja kwa moja na zisiludi tena milele @150,000/=
☆Kuongeza unene, uzito na hamu ya kula @150,000/=
☆Kutengeneza miguu (Chupa ya bia) na kuondoa kigimbi @150,000/=
☆Kubana uke na kuondoa uchafu @150,000/=
☆Kuongeza au Kupunguza maziwa na kuyasimamisha @140,000/=
☆Kuondoa michirizi ya uzazi  au unene @130,000/=
N.K
     Bidhaa hizi zote zimetengenezwa kwa mimea na matunda. Hazina kemikali wala madhara kwa mtumiaji.
    NB: MATOKEO NI UHAKIKA NA GARANTII NA HAKIKISHA UNAPATA RISITI YENYE MUHURI HALISI WA NATURAL BEAUTY
 
    Wasiliana nasi kwa no
         (+255) 0759029968
                0659618585
  Popote ulipo utapata huduma
   Follow us on
GOOGLE👉 natural beauty
INSTAGRAM@natural_beauty_pr
YOU TUBE 👉natural beauty
         <<WELCOME ALL>>

UPDATE: Aliyejiunganishia bomba la mafuta ni mstaafu wa Tazama

$
0
0
Aliyejiunganishia bomba la mafuta nyumbani kwake Samwel Kilanglani(63) amejulikana kuwa ni mfanyakazi mstaafu wa bomba la kusafirisha mafuta Tanzania na Zambi (Tazama).

Kilanglani anatuhumiwa kutoboa bomba la mafuta ya dizeli la Mamlaka ya Bandari Tanzania(TPA) na kujiunganishia kwenye mantaki mawili yakiwa ndani ya nyumba yake iliyopo Tungi Kigamboni.

Kaimu Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Benedict Kitalika amesema mtuhumiwa huyo alijiunganishia na bomba la TPA kwa njia ya kuchomelea na kuunganisha moja kwa moja kwenye mantaki yake mawili yaliyochimbiwa chini ndani ya nyumba yake.

Kitalika amesema mtuhumiwa alijiunganishia katikati na bomba kuu hivyo mafuta yanapopelekwa sehemu husika mengine yanaingia kwake hivyo hayafiki kama yalivyokusudiwa.

"Mafuta yanaweza yakapelekwa lita 4,000 sehemu husika lakini hayafiki yote mengine yanaenda kwa mtuhumiwa huyu matokeo yake wanajiuliza haya mengine yameenda wapi," amesema

Kamanda wa Kikosi cha Polisi Bandari, Robert Mayalla amesema inavyoonekana huyu mtuhumiwa alijiunganishia kipindi mabomba hayo yanajengwa kwa kuwa kipindi hiki isingewezekana.

Amesema bomba hilo amejiunganisha kwa utaalamu wa juu kwa kuwa hayo mabomba yamepitishwa chini ya ardhi.

Wakati hao wakisema hivyo Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Deusdedit Kakoko amesema anaandaa ripoti kuhusu tukio hilo na ataitoa saa tisa leo Jumanne.

"Hili ni suala kubwa linalohusu uchumi wa nchi. Ni sawa na mtu kuvamia kambi ya jeshi."

PICHA: Mtazame Hapa Kigogo wa CHADEMA Aliyejivua Uanachama na Kujiunga CCM Leo

$
0
0
Kiongozi mkubwa wa upinzani aliyejiunga na CCM leo ni Muslim Hassanali aliyekuwa mgombea ubunge Ilala kwa tiketi ya Chadema 2015 .

Pia alikuwa ni  Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini  na  mmoja kati ya watia saini wa ruzuku za Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)

 Kujiunga kwa Hassanali ni mwendelezo wa mfululizo wa viongozi wa upinzani wakiwemo wabunge na madiwani kuondoka na kujiunga CCM.

Tayari viongozi kadhaa wakiwemo wabunge na wapinzani wamejiunga na CCM wakitokea upinzani kwa sababu tofautitofauti ikiwemo ya kuunga mkono serikali ya Rais John Magufuli.

Kiongozi huyo amepokelewa na Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Philip Mangula akiwa na viongozi wengine wa CCM katika ukumbi wa Checkpoint Pugu jijini Dar es Salaam.



Breakimg News: Rais Magufuli Akutana Na Kufanya Mazungumzo Na Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa- Ikulu

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 09 Januari, 2018 amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Edward Ngoyai Lowassa, Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Baada ya mazungumzo hayo Mhe. Edward Ngoyai Lowassa amempongeza Mhe. Rais Magufuli kwa kazi nzuri anayoifanya na ametaja baadhi ya maeneo ambayo kazi kubwa imefanyika kuwa ni kutoa elimu bila malipo, ujenzi wa mradi wa uzalishaji wa umeme katika maporomoko ya mto Rufiji (Stiegler’s Gorge), ujenzi wa viwanda na ujenzi wa reli kwa kiwango cha kisasa (Standard Gauge) ambavyo vinazalisha ajira nyingi kwa Watanzania.

“Nimepata faraja sana kuja hapa Ikulu kuonana na Mhe. Rais, tumezungumza nae na nimempongeza kwa kazi nzuri anayoifanya, lazima tukiri anafanya kazi nzuri na anahitaji kutiwa moyo.

“Moja kubwa ambalo ni la msingi sana ni la kujenga ajira, katika kuanza ujenzi wa reli ya kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro hapo anajenga ajira, na kwenye nchi yoyote inayoendelea suala muhimu ni kujenga ajira, Stiegler;s Gorge ni kujenga ajira na mingine ya aina hiyo, lazima kuwepo na kipaumbele cha kusema kwamba tunajenga ajira, jingine ni la elimu, ni muhimu sana, hauwezi kuacha elimu katika mambo yako unayofanya, hili nalo lazima lisemwe vya kutosha, kwa kweli nakushukuru Mhe. Rais, you made my day” amesema Mhe. Lowassa.

Kwa upande wake Mhe. Rais Magufuli amempongeza Mhe. Edward Ngoyai Lowassa kwa kutambua kazi kubwa inayofanywa na Serikali na amesema Mhe. Lowassa ni mmoja wa viongozi ambaye kwa wakati wake ametoa mchango wake katika nchi.

Mhe. Rais Magufuli ameongeza kuwa Mhe. Lowassa ni mwanasiasa mzuri kwani hata wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu uliopita ambao naye aligombea kiti cha Urais, hakuwahi kumtukana.

“Mhe. Lowassa ameniomba mara nyingi nikutane nae, na leo nimekutana nae, tumezungumza mambo mengi, ameniambia ya kwake na mimi nimemwambia ya kwangu, kwa ujumla Mhe. Lowassa ni mwanasiasa mzuri na tuendelee kuwaenzi wazee hawa ambao kwa nyakati fulani walifanya mambo mazuri, na mimi napenda kumpongeza Mhe. Lowassa ambaye kama alivyosema hapa kuwa tumefanya mambo mazuri mengi.

“Ametaja miradi mbalimbali tunayotekeleza, ametaja mradi wa Stiegler’s Gorge utakaogharimu zaidi ya Shilingi Trilioni 7, amezungumzia juu ya elimu bure, amezungumzia juu ya maji ambayo kwa bahati nzuri yeye alikuwa Waziri wa Maji na anafahamu sasa tumefikia wapi, amezungumza juu ya umeme tulivyosambaza katika vijiji mbalimbali, elimu bure, huduma za hospitali na mengine” amesema Mhe. Rais Magufuli.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
09 Januari, 2018

Mrema Awapa Makavu Waliomzushia Kifo

$
0
0
Mwenyekiti wa Bodi ya Parole nchini na mwanasiasa mkongwe, Agustino Lyatonga Mrema, amekanusha taarifa za kifo ambazo zilianza kusambaa mitandaoni mapema leo.

Akizungumza na waandishi wa habari nyumbani kwake Sinza jijini Dar es salaam, Mheshimiwa Mrema amesema yeye ni mzima wa afya na hata ugonjwa amabo ulikuwa ukimsumbua kwa miaka mingi ameshapona.

“Afya yangu ni njema ni kweli nilikuwa mgonjwa tangu mwaka 2015, wakati wa kampeni na wakawa wanasema msimchague Mrema ni mgonjwa ni marehemu Mtarajiwa, ila tangu Magufuli kushika urais wake aliahidi serikali itasimamia matibabu yangu, nikapelekwa India na ile kansa iliyokuwa inanisumbua imepona kabisa”, amesema Lyatonga Mrema.

Mrema ameendelea kwa kusema kwamba...”kwa kweli naona mambo yangu ni mazuri hata sura inang'aa, ngozi ile iliyokunjamana haipo tena. Leo asubuhi nimepata taarifa kuwa kuna kikundi kile kile cha 2015 wanataka nife, wanahisi naelekea tena Vunjo kuchukua lile jimbo, lakini nataka kuwaambia mimi sio mgonjwa kansa nimepona, hajafa mtu hapa”, amesema Lyatonga Mrema.

Leo asubuhi kulikuwa na taarifa kuwa mwanasiasa hyo amefariki dunia, kitendo ambachosio mara ya kwanza kutokea kwa kiongozi huyo, ambaye sasa anashikilia wadhifa wa Mwenyekiti wa Bodi ya Parole nchini.

Wizara ya Kilimo Yahaha Kutimiza Agizo la Rais Magufuli.....Magari ya JWTZ Yatumika Kuokoa Jahazi

$
0
0
KUFUATIA agizo la Rais Dkt John Pombe Magufuli, kwa Wizara ya Kilimo, kuhakikisha ndani ya siku saba kumaliza malalamiko ya mahitaji ya mbolea kwa mikoa ya Katavi na Rukwa, Kampuni ya Taifa ya Mbolea (TFC) imeanza mara moja kuteleleza agizo hilo.

Waandishi wa Habari  jana na leo wameshuhudia watendaji wa TFC wakihaha kutafuta magari ya kukodi kwa ajili ya kusafirisha mbolea kuipeleka mkoani Rukwa na Katavi, ambapo zaidi ya tani 600 zimeanza kusafirishwa kuanzia juzi siku ya agizo hilo.

Akizungumzia hatua hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa TFC, Salum Mkumba, alisema mara baada ya taarifa ya Ikulu jana, waliamua kuanza kupakia mbolea hiyo, kwa kutumia magari makubwa (malori) ya kukodi pamoja na magari makubwa ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).

“Kwa sasa sisi TFC hatuna akiba ya mbolea, lakini hawa wenzetu wa Primium Agro Limited, wanayo akiba ya kutosha, hivyo tunachukua kwao kwa makubaliano maalum,” alisema Mkumba.

Mkumba aliongeza kusema kwamba, kutokana na uzito wa agizo hilo lililotolewa na Rais Magufuli, wameongeza nguvu ya magari, yanayoelekezwa mikoa ya Katavi na Rukwa, ambako mahitaji ya mbolea hiyo ni makubwa kwa sasa.

Alisema nusu saa baada ya tamko la Rais Magufuli, alipokea taarifa kutoka kwa Waziri wa Viwanda na Uwekezaji Charles Mwijage, akimtaka kuhakikisha wakulima kwenye maeneo husika wanatulia kwa kupokea mbolea.

“Mbolea hii inapelekwa kwa wakulima kote nchini na itauzwa kwa bei elekezi ya szerikali, na ninawashukuru hawa wenzetu wa kampuni ya Premium Agro Limited kwa kuwa tayari kushirikiana kwa maslahi ya wananchi na Taifa letu,” alkisema Mkumba.

Mkumba alisema wameamua kuingia makubaliano na kampuni binafsi ya Premium Agro Chem Limited, kupeleka mbolea hiyo kwenye maeneo hayo na mengineyo nchini yenye mahitaji, lakini akiamini kuwepo kwa unafuu kwenye maeneo mengine.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Primium Agro Chem Limited, Sargar Shah, alisema kwamba makubaliano na TFC ni kupakiwa kwa zaidi ya tani 1000 za mbolea hiyo kwenda katika mikoa ambayo wo hawana mawakala na kurahisha upatikanaji na pia kwa bei elekezi ya serikali.

Meneja Biashara wa Primium Agro Chem Limited, ambaye kwa sasa ndiye anayesimamia zoezi hilo Brijesh Barot, alisema wamejiandaa vizuri kufanya kazi hiyo mchana na usiku kwa nia ya kufikia malengo ambayo serikali imeyahitaji.

Barot alisema kampuni hiyo tayari kuanzia mwezi Septemba, imesambaza kwa wakulima kupitia kwa mawakala wao zaidi ya tani 19,500 za mbolea ya kupandia aina ya Urea, ikiwa kwenye ujazo wa kilo 25 na kilo 50.

Barot aliongeza kusema kwamba, kampuni yake imeendelea kusambza na kuuza kwa wakulima mbolea zaidi kwa bei elekezi, licha ya kuwa tayari walimaliza kuuza tani 3,500 zilizoagizwa na serikali na kutakiwa kuuzwa kwa bei elekezi.

“Sisi ni watanzania, wafanyabiashara wazalendo kwa nchi hii, hatutaki kufanyakazi kwa ajili ya kutafuta faida,badala yake tunaungana na Mheshimiwa Rais Magufuli, kuisaidia jamii kwa kufanya kazi ” alisema Barot.

Godbless Amchana Lowassa Baada ya Kwenda Ikulu na Kuonana na Rais Magufuli

$
0
0
Baada ya aliyekuwa Waziri Mkuu,Edward Lowassa ambaye ni Mjumbe wa Kamati Kuu kuonana Rais Magufuli. Hatimae Mbunge wa Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless lema ameibuka na kusema kuwa kiongozi huyo amewakosea Watanzania kwa kauli aliyoitoa baada ya kutoka Ikulu.

Mh. Lowassa alipotoka Ikulu baada ya mazungumzo alisema kuwa; “Nimepata faraja sana kuja hapa Ikulu kuonana na Mhe. Rais, tumezungumza nae na nimempongeza kwa kazi nzuri anayoifanya, lazima tukiri anafanya kazi nzuri na anahitaji kutiwa moyo, Moja kubwa ambalo ni la msingi sana ni la kujenga ajira, katika kuanza ujenzi wa reli ya kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro hapo anajenga ajira, na kwenye nchi yoyote inayoendelea suala muhimu ni kujenga ajira, Stiegler;s Gorge ni kujenga ajira na mingine ya aina hiyo, lazima kuwepo na kipaumbele cha kusema kwamba tunajenga ajira, jingine ni la elimu, ni muhimu sana, hauwezi kuacha elimu katika mambo yako unayofanya, hili nalo lazima lisemwe vya kutosha, kwa kweli nakushukuru Mhe. Rais, you made my day,” amesema Lowassa.

Hata hivyo Lema amemhoji Mh. Lowassa kuwa ni mema gani ameyaona katika serikali hii, huku akitolea mfano Mbunge wa Singida Mashariki kuwa anauguza majeraha ya risasi.

“Mh Lowassa,umeikosea Tanzania kwa kauli baada ya kutoka Ikulu,mema yapi umeyaona katika Serikali hii?Wkt Mbunge Lissu bado anauguza majeraha ya risasi,maiti zinaokotwa,Uchumi unaanguka,Benki zinafungwa ,demokrasia imekufa Bungeni /Nje ya Bunge na Sioi mkwe wako bado yuko Magereza,” ameandika Lema kupitia ukurasa wake wa Twitter.

Taarifa ya BoT ikiwataka wananchi kupuuza taarifa zinazodai kuwa, sekta ya kibenki nchini si salama.

Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images