Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Shekhe mkuu ataka viongozi wa dini waheshimiwe

$
0
0
Shekhe Mkuu wa Tanzania, Mufti Abubakar Zuberi, ametaka viongozi wa dini nchini kuheshimiwa na jamii ikiwemo kutekelezewa mahitaji yao ya msingi ili waweze kujikimu kimaisha.

Akizungumza na waumini wa dini hiyo Jumamosi Januari 6 katika mhadhara wa Maulidi  uliofanyika katika kata ya Mazingara wilayani Handeni mkoani Tanga, Mufti Zuberi amesema kila kiongozi duniani amewekwa na Mungu hivyo ni lazima aheshimiwe.

Amesema kuna baadhi ya watu wamekuwa na tabia ya kudharau viongozi wao kwa kuwatolea lugha chafu na zenye maudhi kwa kujionyesha wana uelewa kuliko viongozi.

"Viongozi  lazima waheshimiwe kwa namna yoyote ile, sisi viongozi wa dini ndio tunaosababisha kuwepo amani na utulivu pia kutoa vizazi vyenye elimu ya dini kwa kuwafundisha watoto imani," alisema na kuongeza:

"Lazima sasa tuheshimiwe, iwe shehe  au kiongozi wa dini nyingine na pia wa serikali ambao ndio wanasababisha mipango yetu ya kidunia inakwenda  sawa. Kiongozi yoyote anateuliwa na Mungu na sio binadamu hivyo kuheshimiwa ni lazima."

Mhibiri wa dini ya Kiislamu kutoka jijini Dar es Salaam, Shehe Yusuph Hossein, amesema waumini wa dini hiyo wanatakiwa kufuata maagizo na mafundisho aliyoacha Mtume Muhammad kwani bila kufanya hivyo maovu hayatakwisha.

Ameongeza kuwa maadili katika jamii yameshuka kwa sababu watu wameacha kufuata maagizo ya dini zao badala yake  wametawaliwa na Dunia ambayo imejaa maovu.

Alipokaribishwa asalimie hadhara hiyo, Mbunge wa Jimbo la Handeni Mjini, Omari Kigoda, akapendekeza kuwepo kwa utaratibu wa kudumu wa viongozi wa dini kukutana mara  kwa mara  na waumini wao ili kuweza kukumbushana mambo ya dini.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Handeni, Athumani Malunda, amewapongeza walioandaa hadhara hiyo kwa kuifanya  muda wa mchana kuliko ilivyozoeleka nyakati za usiku na kusema kuwa utaratibu huo ni mzuri kwa usalama  wa raia, mali  zao na viongozi wanaofika kuhudhuria.

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Yazijibu hoja za UKAWA

$
0
0
Tume  ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imejibu hoja mbili kati ya 14 zilizowasilishwa kwake na Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) huku ikisisitiza kuwa hoja zingine 12 hazimo ndani ya mamlaka yake.

Hata hivyo, Mwenyekiti wa Ukawa, Freeman Mbowe amesema tume kwa kutoa kauli hiyo, inakwepa wajibu wake na kuwa sehemu ya serikali.

Katika mkutano wake na vyama vya siasa jijini Dar es Salaam jana uliohudhuriwa na vyama 17 kati ya 19, Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa na Jeshi la Polisi, NEC ilisema imeamua kuuitisha kwa lengo la kupeana taarifa na kujadiliana mambo mbalimbali na uchaguzi mdogo katika majimbo matatu na madiwani katika kata sita Tanzania Bara.

Majibu ya hoja za Ukawa yalitolewa baada ya mchangiaji wa mada, Katibu Mkuu wa NCCR-Mageuzi, Juju Danda, kuhoji juu ya barua hiyo huku akiituhumu tume kunyamaza na kutoitisha mkutano wa wadau kabla ya kufanyika kwa uchaguzi mdogo.

"Ukawa tuliomba kukutana na wadau wote pamoja na tume kabla ya uchaguzi, lakini sasa mmetuita, mmeshapanga tarehe ya uchaguzi," Danda alisema.

"Wasimamizi wa uchaguzi ni makada, tunakwenda kushindana kwenye uchaguzi wa nini wakati mshindi anajulikana?” Danda alihoji.

Baada ya hoja hiyo, Mwenyekiti wa NEC, Jaji Semistocles Kaijage, alitoa barua ya Ukawa na kueleza kubainisha kuwa iliwafikia Desemba 14 na waliijibu siku nne baadaye na kurejesha majibu kwa aliyeiandika.

"Mwandishi wa barua ndiye alijibiwa, fuatilia kwenye vyama vyenu, aliyeandika alipata jibu na alijulishwa kwa maandishi, alitakiwa kufika leo kwenye kikao ili yaliyomo kwenye barua yaweze kujadiliwa, lakini hajafika,” alisema Jaji Kaijage.

Mwenyekiti wa NEC huyo alijibu hoja moja baada ya nyingine zilizowasilishwa kwao na Ukawa kupitia barua hiyo akibainisha kuwa hoja yao ya kwanza na ya pili ndiyo ziko ndani ya mamlaka ya tume, akianza na hoja ya kutolewa nje kwa mawakala wa uchaguzi na kuzuiwa kwa mikutano ya siasa nchini.

“Niwasihi sana viongozi wa vyama vya siasa, makosa yoyote yanayokiuka taratibu za kisheria, za kiuchaguzi, taratibu muhimu zinazomnyima mgombea haki ya kugombea na kupitishwa yafuate mkondo. Sheria na taratibu zetu hazijaacha ombwe, foramu imewekwa ya kuwasilisha tatizo hilo, hakuna sababu yoyote ya msingi kwa wakala kutolewa nje,” alisema na kueleza zaidi:

“Wakala anapotolewa maana yake uchaguzi haujaenda vizuri, na sheria imeweka utaratibu wa wapi malalamiko yapelekwe ili ufumbuzi upatikane."

Mwenyekiti wa NEC huyo alisema kama kuna wakala alitolewa nje, uchunguzi ufanyike na hatua zichukuliwe kwa mujibu wa sheria za nchi, maadili, taratibu na kanuni.

Jaji Kaijage alisema hoja ya pili ni madai ya Ukawa kuwa matokeo halisi hayatangazwi akifafanua kuwa kifungu cha 81 cha Sheria ya Uchaguzi na kifungu 82 cha Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, vinaeleza anayetangazwa kuwa mshindi ni ambaye amepata kura nyingi halali zaidi ya mwingine.

“Lalamiko la msingi kuwa matokeo halisi kutotangazwa, pengine ambaye siyo mshindi ndiye katangazwa, hili ni kosa kubwa sana. Sheria ya Uchaguzi na Sheria ya Serikali za Mitaa imeweka wazi kwamba malalamiko yenye ushahidi wa msingi ya kukiuka sheria na taratibu, ana haki ya kwenda mbele ya vyombo vya sheria kulalamika na ikithibitika uchaguzi unatenguliwa,” alisema na kuongeza:

“Laiti kama haya na mengine yangewasilishwa katika mamlaka za kisheria na kanuni yangekuwa yamepata majibu. Kusita au kukataa kwa sababu nyingine ndiyo kunaleta malalamiko. Tulishasema malalamiko yote yaliyopo humu (barua) hakuna ambalo haliwezi kushughulikiwa chini ya sheria za nchi."

Kuhusu kupigwa marufuku kwa mikutano ya vyama vya siasa, Jaji Kaijage alisema majukumu ya NEC yako kwenye katiba na sheria, hivyo ni suala ambalo haliko kwenye mamlaka ya tume na wanabaki kuwa wasikilizaji pekee.

Alisema hoja ya tatu ya Ukawa ni kuwapo kwa mauaji nchini ambayo alikiri kuwa ni tatizo na ni kosa kubwa la jinai, lakini akasisitiza kuwa halipo ndani ya majukumu ya NEC.

“Tume kuitisha kikao cha kujadiliana kuhusu mauaji tunaweza kushtakiwa kwa kuparamia mamlaka na madaraka ambayo tume haina," Jaji Kaijage alieleza.

Alibainisha kuwa hoja ya nne ya Ukawa ni madai ya kuminywa kwa vyombo vya habari, akieleza kuwa suala hilo pia lipo nje ya mamlaka yao na kwamba linaweza kuwaingiza kwenye matatizo.

"Uchaguzi hauwezi kutenguliwa na huwezi kuitisha kikao kujadili mambo ambayo tume haina mamlaka nayo," alisema.

Aliitaja hoja ya tano kuwa ni vituo kuvamiwa wakati wa kuhesabu kura akifafanua kuwa vifungu na maelekezo yametolewa vizuri kabla ya kuanza upigaji wa kura na wakati wa kufunga kituo kuna fomu maalum inajazwa kama kuna malalamiko yoyote yanaainishwa.

Alisema kama tatizo lilijitokeza, kanuni na taratibu zinaweka wajibu kwa msimamizi wa kituo kutoa ufafanuzi, kama hakutoa inakuwa ndiyo msingi wa kupeleka kwenye mamlaka za kisheria.

Jaji Kaijage alisema hoja zingine za Ukawa ni kutaka kuwa na tume huru, katiba mpya, mikutano ya hadhara, maandamano na kutofanya kazi za kisiasa.

"Sisi kama Tume tunafuata Katiba, sheria zilizopo, kanuni, suala la kikatiba tunajiuliza hivi tume inayo mamlaka ya kufanya marekebisho ya sheria au kuhitisha mkutano wenye lengo la kuweka sawa katiba inayolalamikiwa," Jaji Kaijage alisema na kuongeza:

"Tume inaweza ikatoa ufumbuzi juu ya kuruhusiwa au kutoruhusiwa kwa mikutano ya hadhara?

"Kuhusu katiba mpya, sisi tunaweza tukatoa maoni kama watu wengine mbele ya chombo kilichokabidhiwa jukumu la kufanya marekebisho ya katiba au sheria."

Alisema lawama kwa tume ni zinapaswa kuwa kushindwa kutekeleza mamlaka yake, kanuni na sheria zinazoongoza uchaguzi.

“Tume iko makini kuhakikisha inafuata taratibu zote za kisheria, kanuni na kimaadili. Tume itakuwa ya mwisho kukiuka sheria, taratibu na katiba ya nchi,” alisema.

Katika mkutano huo, baadhi ya wajumbe waliitaka tume kutokukwepa majukumu yake kwa kuwa ndiyo chombo mama na kwamba siyo dhambi kuishauri serikali pale wanapoona wana nafasi ya kufanya hivyo.

“Mtu anafika kituoni na mapanga anakata watu, ukilalamika unaambiwa ni suala la polisi. Tume haichukui hatua, unatuambie tukaelimishe wananchi, lakini wanajua wamezuiliwa kufanya mikutano, kazi yao ilikuwa ni kuelimisha jamii,” alisema mmoja wa wajumbe waliohudhuria mkutano huo.

Katika mkutano huo, Mkurugenzi wa NEC, Kailima Ramadhani, aliwasilisha taarifa ya maandalizi ya uchaguzi mdogo katika majimbo ya Longido, Singida Kaskazini na Songea mjini na kata sita, akibainisha kuwa Chadema na NCCR- Mageuzi wamesusa.

Mbowe Afunguka:
Akizungumza jana, Mbowe alisema katika mambo yanayohusu uchaguzi na maisha ya watu, hakutakiwi kuangalia kama lipo ndani ya mamlaka au la, bali kinachotakiwa ni kushauriana.

“Kuna mambo kadhaa wanajadiliana, jambo linahusu idara nyingine na kuishauri ni mambo ya kawaida katika uongozi, NEC kama mhusika mkuu wa uchaguzi, watendaji wengine wa idara za serikali wanapofanya mambo yaliyo kinyume ni wajibu wao kukemea,” alisema.

Mbowe alisema polisi wanapoumiza wafuasi wa chama fulani katika uchaguzi ni ngumu kusema NEC haihusiki na wanaohusika ni polisi pekee. Alisema wajibu wao ni kuhakikisha uchaguzi unakuwa huru na haki kwa njia zote za amani na haki.

“Jambo lolote linapoibuliwa halijadiliwi kwenye mkutano wa waandishi wa habari, bali wadau wakiwa na kikao cha ndani. Tuliwaandikia tukutane na NEC, polisi, usalama wa taifa na Msajili wa Vyama vya Siasa,” alisema.

Mbowe ambaye pia ni Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, alidai uchaguzi mdogo uliopita ulikuwa na kasoro mbalimbali zinazolalamikiwa na wadau, lakini inashangaza tume kusema haikuona tatizo.

Kiongozi huyo wa Ukawa pia alidai kikao kilichofanyika jana kilipangwa kufanyika mapema zaidi lakini kikaahirishwa na kwamba Chadema hawakupata barua ya tarehe mpya ya kikao.

“Tulikuwa Nairobi, Kenya kwa ajili ya kumsafirisha Tundu Lissu. Kikao kiliitwa mwezi uliopita, kikahairishwa japo hawakueleza agenda za kikao. Taarifa za uwapo wa mkutano mimi (Mwenyekiti), Makamu Mwenyekiti na Katibu Mkuu hatuna taarifa,” alisema na kuongeza:

“Tuna wajibu wa kuhakikisha nchi inakuwa na uchaguzi wa haki amani, kila mmoja aone faida ya vyama vya siasa na siyo hasara.

“Tatizo lililopo, tume inajiona wao ni serikali, wanatuangalia kama watu wa kupambana nao, kukinzana na hoja na siyo watu wa kushirikiana kutafuta suluhisho. Ndiyo maana kila tukilalamika wanajenga ‘defence’ (kujilinda), wameegemea upande wa serikali.

“Ni bahati mbaya sana iliyopo nchini kwamba vyombo vyetu vya kusimamia mambo ya kuleta umoja katika taifa wanaanza kuwa sehemu ya vyama, wanashiriki upande mmoja na kukandamiza haki ya upande wa pili na wanadanganya umma kuwa haki inatolewa kumbe haitolewi."

Awali wakati wa mkutano Mwakilishi wa ACT-Wazalendo, Msafiri Mtemelwa, alisema Chadema hakikufika kushiriki kwa kuwa imekuwa kawaida kuzungumza lakini mambo hayashughulikiwi.

“Jeshi la Polisi linatumika vibaya, magari ya polisi maana yake wapinzani wasijitokeze watakamatwa, kwanini polisi wanaenda na magari yenye bendera nyekundu, mavazi ya kutisha wananchi?" Alihoji.

Aliitaka tume kuacha kuwatumia wakurugenzi wa halmashauri kusimamia uchaguzi na wakuu wa wilaya na mikoa kuacha kufanya siasa.

“Unakuta RC na DC ambao ni wenyeviti wa kamati za ulinzi na usalama wanafanya kampeni za CCM. Ndiyo maana tunasema wapeni ushindi CCM waendelee kutawala, hakuna haja ya kufanyika uchaguzi,” alisema Mtemelwa.

Katibu Mkuu wa Sau, Jonson Mwangosi na Lulu Kimwaga wa Tadea, waliiomba tume kusaidia vyama visisivyo na uwakilishi bungeni vipate ruzuku ili viweze kushindana kwenye chaguzi mbalimbali.

“Uchaguzi wa sasa ni sawa na kumpa nyama kibogoyo ashindane na mwenye meno," alisema Kimwaga.

Mwezi uliopita Ukawa kupitia kwa Mbowe ulitangaza kususa kushiriki uchaguzi mdogo wa majimbo matatu na kata sita uliopangwa kufanyika Jumamosi ukitaka uitishwe kwanza mkutano wa NEC na wadau wa uchaguzi kujadili na kuzitafutia ufumbuzi changamoto zilizojitokeza katika uchaguzi mdogo wa madiwani wa kata 43 Tanzania Bara uliofanyika Novemba 26.

Mchungaji Peter Msigwa adai kuna njama za Kumwangamiza

$
0
0
Mbunge wa Jimbo la Iringa Mjini Chadema  Mchungaji Peter Msigwa amesema mbinu inayotumika  kuwashawishi na kuwanunua madiwani wa Chama hicho imelenga kupunguza nguvu zake katika kuikosoa Serikali.

Amesema taarifa hizo amepewa na viongozi wa CCM ambao wamemthibitishia  kuwa hawana shida nao.

"CCM hawana shida na madiwani, wanachama wanashida na wale wakosoaji wakubwa wa Serikali Kuu"amesema Msigwa

Msigwa amewataja wabunge wengine wa upinzani aliodai watapitia kipindi hicho kuwa ni Mbunge wa Jimbo la Hai  Freeman Mbowe, Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki Tundu Lisu, Mbunge wa Jimbo la Mbeya Joseph Mbilinyi, Mbunge wa Kawe Halima Mdee na Mbunge wa Arusha Mjini Godbles Lema.

Serikali Yataifisha Tani 65 za Samaki zenye Thamani ya Milioni 300

$
0
0
Waziri wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Luhaga Joelson Mpina amekamata kilo 65600 za samaki wachanga aina ya Sangara waliokaushwa kwa chumvi wenye thamani ya shilingi milioni mia tatu katika Kisiwa cha Lubili wilayani Muleba kwenye Mkoa wa Kagera baada ya wamiliki wa samaki hao kukimbia.
 
Akizungumza jana na Waandishi wa Habari katika Ofisi ya  Kitengo cha Doria na Udhibiti wa Uvuvi wa mpakani katika Mkoa wa Kagera, Mpina alisema  tukio la kukamatwa kwa samaki hao lilifanikiwa baada ya yeye kupata taarifa kutoka  kwa raia mwema ambapo aliagiza mamlaka za Wilaya ya Muleba kufuatilia kwa karibu hatimaye kuwakuta  samaki hao wakiwa wameanikwa chini katika kisiwa hicho.
 
Waziri  Mpina alisema Sheria ya Uvuvi namba 22 ya Mwaka 2003  na Kanuni zake za mwaka 2009 kifungu cha 90(1) inataka samaki wanaovuliwa waandaliwe katika mazingira yanayokidhi vigezo vya usalama  kwa mlaji na  kwamba ni kosa kisheria kuwavua au kuchakata samaki aina ya Sangara walio chini ya sentimeta 50 kwa kuwa ni wachanga na sentimita 25 kwa Samaki aina ya Sato. Pia sentimita 85 kwa Sangara kwa kuwa ni wazazi wanaotakiwa kundelea kuzaa.
 
Aidha Waziri aliongeza kwamba Sheria hiyo imetoa  mamlaka kwa watendaji wa Serikali kutaifisha mali zote zilitumika katika uvuvi haramu kupitia  kifungu cha 37(a) (ii) na (iii) pamoja na   Sheria ya Hifadhi za Bahari na Maeneo Tengefu namba 29 ya mwaka 1994.
 
Waziri Mpina  ameagiza  watendaji kufuata taratibu zote za kisheria ili samaki hao wauzwe kwa njia ya mnada  na mapato hayo yaingie Serikalini mara moja.Aidha  aliwaonya wafanyabiashara na wavuvi kuachana na uvuvi haramu kwa kuwa ni kuhujumu raslimali za taifa  ambazo zingetumika kwa kizazi cha sasa  na baadaye.
“Mfanyabiashara yoyote wa samaki na mazao yake anayetaka kufilisika  na kutafuta matatizo katika maisha yake aendelee na biashara ya uvuvi haramu”alisisitiza Mpina
 
Kufuatia tukio hili, Waziri Mpina  amewapa wiki mbili wafanyabiashara na wasafirishaji wote wa samaki na mazao yake waliopewa leseni  ya kufanya  biashara hiyo kwa mwaka 2018 kuleta cheti cha uthibitisho cha ulipaji kodi ambapo amesema kama watashindwa kufanya hivyo hawataruhusiwa kufanya biashara hiyo.
 
Alisema kuanzia sasa wafanyabiashara wote wote wataruhusiwa  kupata leseni hiyo baada ya kuwasilisha cheti cha uthibitisho wa ulipaji kodi, cheti cha usajili wa kampuni na mahesabu ya kibiashara  yaliyohakikiwa ili kuepuka utaratibu wa sasa ambao unatoa mwanya kwa mawakala wa ndani na nje ya nchi kujiingiza katika biashara hiyo kinyemela  na kuikosesha Serikali mapato kwa  kukwepa kulipa kodi mbalimbali.
 
Naye Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Meja Jenerali Mstaafu Salum Mustapha Kijuu alisema  Serikali  itahakikisha kwamba uvuvi haramu unakuwa historia katika Mkoa wa Kagera na kuwataka wananchi kuwafichua wavuvi  haramu  ili vyombo vya Serikali viwakamate na kuwafikisha katika  mikondo ya sheria.
 
Alisema  sekta ya uvuvi inaweza kuchangia kwa kiasi kikubwa  katika kuinua hali ya uchumi kwenye mkoa wake na taifa kwa ujumla kama  wadau wote watashiriki kikamilifu katika  vita dhidi ya  uvuvi haramu ambapo alisema  jumla ya wananchi 26,272 wameajiriwa kutokana na shughuli za uvuvi katika mkoa huo.
 
Alisema mkoa utaendelea na kupambana na uvuvi haramu ambapo  kwa mwaka 2016/17 jumla ya doria 65 zilifanyika na kuwezesha kukamatwa kwa makokoro ya Sangara 422, nyavu ndogo za dagaa 57,nyavu za timba 3,231, nyavu za makila 14,141, ndoano 711, katuli 16,mitumbwi 133 samaki wachanga kilo 5,621 na watuhumiwa 86.
 
Hata hivyo Mkuu  huyo alisema  katika kuongeza uzalishaji wa samaki jumla ya mabwawa 584 yamechimbwa kwa mwaka 2016/2017 kutoka mabwawa 181 mwaka 2005/2006 sawa na ongezeko la mabwawa 403.
 
Kwa upande mwingine Mkuu wa Mkoa alisema hivi karibuni Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Ngara ilikamata gari lenye namba za uasajili T 614 CLQ aina ya Mitsubishi Canter likiwa limepakia samaki kilo 2,000 aina ya Sangara na kilo 530 wa aina ya Sato kwenye mpaka wa Murusagamba wilayani Ngara.
 
 Alisema Afisa wa Kitengo cha Doria na Udhibiti wa Uvuvi wa mpakani katika Mkoa wa Kagera bwana  Ayoub Ngoma na dereva  wa gari hilo Ayoub Sanga  walishikiliwa na polisi kwa hatua za kisheria kwa tuhuma za  kushiriki katika utoroshaji wa samaki wenye kilo 2530 kwenda nchini Burundi zenye thamani ya shilingi 20,850,000/= ambapo Ngoma
ameshasimamishwa kazi kupisha uchunguzi.
 
Pia Mshauri wa Uvuvi wa Mkuu wa Mkoa, Efrazi Mkama na  maafisa Uvuvi wa Halmashauri ya Muleba Wilfred Tibendelana na Maengo Nchimani na Afisa Uvuvi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba vijijini Renus Ruhuzi wanaendelea kuripoti katika kituo cha polisi Bukoba kwa mahojiano ya kisheria juu ya utoroshwaji wa samaki hao.
 
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Uvuvi, Mwanaidi  Mlolwa alisema Serikali ina mkono mrefu  na kwamba  hakuna mtu atakayebaki salama iwapo atajihusisha  na uvuvi haramu.
 
Aidha alisema maafisa uvuvi wanawajibu wa kuhifadhi na kutunza takwimu mbalimbali za sekta ya uvuvi ili kutoa picha halisi ya jinsi sekta inavyochangia katika uchumi wa nchi kwa ujumla.
 
“Kimsingi sekta ya uvuvi ina mchango mkubwa katika uchumi wa nchi yetu lakini tatizo kubwa ni ukosefu wa takwimu sahihi

Ratiba Rasmi Ya Mazishi Ya Mke Wa Mzee Kingunge Ngombale Mwiru

$
0
0
Mazishi ya mke wa mwanasiasa mkongwe nchini, Mzee Kingunge Ngombale Mwiru, Marehemu Peras Kingunge, yamepangwa kufanyika siku ya Alhamisi Janury 11, 2018 katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar es salaam, msemaji wa familia Bw. Omari Kimbau ametangaza. 
 
Bw. Kimbau amesema kuwa ratiba ya mazishi hayo itaanza rasmi siku ya Jumatano jioni wakati mwili wa marehemu utawasili nyumbani  kwake mtaa wa Kingunge eneo la Victoria (njia ya kuelekea Mwananyamala, jirani na ilipokuwa Istana Restaurant) kutoka hospitali ya Taifa ya Muhimbili unakohifadhiwa, na kwamba baada ya hapo kutakuwa na mkesha wa maombi. 
 
Amesema siku ya pili, Alhamisi, shughuli zitakuwa kama ifuatavyo:
*Saa moja hadi za mbili na nusu asubuhi – Kifungua kinywa kwa waombolezaji
*Saa Tatu hadi saa Sita na nusu – Waombolezaji wataaga mwili wa marehemu
*Saa saba mchana – Misa ya marehemu kufanyika katika kanisa la St. Peters, Oysterbay.
*Baada ya misa mwili utapelekwa makaburini Kinondoni kwa mazishi. 
 
 Baada ya mazishi Bw. Kimbau ameomba waombolezaji warejee nyumbani kwa marehemu kwa ajili ya chakula na kuanua tanga. 
 
Marehemu Peras Kingunge alifariki dunia siku ya Alhamisi katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili alipokuwa akipatiwa matibabu. 

Mume wake, Mzee Kingunge, kwa hivi sasa amelazwa hospitalini hapo akiuguza majeraha yaliyotokana na kuumwa na mbwa nyumbani kwake. 

Hali yake inazidi kuimarika na anatarajiwa kurudi nyumbani kushiriki katika mazishi ya mkewe wakati wowote kuanzia sasa.

Serikali Kuendelea Kushirikiana Na TUCTA Kuongeza Tija Na Ufanisi Sekta Ya Kazi

$
0
0
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira,Vijana  na watu wenye ulemavu) Mhe.  Jenista Mhagama amesema serikali itaendelea  kushirikiana na Shirikisho la Vyama vya  Wafanyakazi Nchini (TUCTA) katika kuleta tija na ufanisi katika sekta ya kazi kwa kushughulikia masualaya wafanyakazi nchini

Waziri Mhagama ameyasema hayo jana tarehe 7 Januari 2018, jijini Dar es salaam wakati wa mkutano wake na viongozi hao wa TUCTA, walipokutana kwa ajili ya kujadiliana na kushauriana juu ya mazingira bora na wezeshi ya wafanyakazi, sekta ya kazi na ajira  nchini .

“Hatuwezi kupata tija na ufanisi katika sekta ya kazi bila vyama vya wafanyakazi  kushughulikia  malalamiko na manunguniko ya wafanyakazi katika maeneo yao ya kazi hasa katika mikataba  ya ajira na stahiki zao kwa mujibu wa sheria .

"TUCTA msipo simamia haya hata serikali tutashindwa kutimiza wajibu wetu kikamilifu. Serikali itaendelea kushughulikia masuala  ya wafanyakazi na sekta ya kazi kwa kuzingatia miongozo, kanuni na sheria za kazi  na ajira katika kutafuta suluhu ya masuala  ya kazi” alisema Mhagama.

Mhagama aliwahakikishia TUCTA kuwa serikali itayashughulikia madai yote ya wafanyakazi ambayo yanazingatia  sheria. 

Aidha Mhagama aliwataka TUCTA kuvitaka vyama vya wafanyakazi kufanya vikao na wafanyakazi katika maeneo yao ya kazi  na wawapatie elimu juu ya masuala ya kazi ikiwa ni pamoja na kuwaelimisha juu ya tafsiri sahihi ya sheria za kazi  tulizonazo nchini.

Kwa upande wake Rais wa TUCTA, Tumaini  Nyamghokya ameishukuru serikali kwa ushirikiano wanaoupata toka serikalini  kupitia majadiliano ambayo yamesaidia  migogoro ya wafanyakazi kupungua katika maeneo ya kazi.  ushirikiano huo umekuwa ni mhimili mkubwa kati ya serikali, waajiri na wafanyakazi.

Mkutano huo  ulihudhuriwa  na Waziri wa Nchi Ofisi ya Raisi  utawala bora, George Mkuchika, Naibu waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazina Ajira), Anthony Mavunde na Katibu Mkuu Tawala za mikoa na Serikali za mitaa  na Katibu Mkuu ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi na Ajira)  Erick Shitindi.

Msingi wa serkali na Shirikisho la Vyama vya  Wafanyakazi Nchini (TUCTA) kukutana kwa majadiliano na mashauriano unatokana na nchi ya Tanzania kusaini mikataba ya Shirika la Kazi Duniani (ILO), ukiwemo mkataba namba 98 wa mwaka  1949,ndio uliweka mazingira hayo  ya serikali,waajiri na wafanyakazi kukutana ili kuweka dhana ya kuaminiana na  kuleta tija na ufanisi katika sekta ya kazi na ajira.

Ukikutwa wamesimama na wanafunzi wa kike, viboko 12

$
0
0
Uongozi wa kata ya Nyehunge wilayani Sengerema umepitisha sheria ya kuwacharaza viboko 12 au faini ya Sh10,000 wanaume watakaokutwa wamesimama na wanafunzi wa kike.

Sheria hiyo ndogo imepitishwa juzi kwenye kikao cha maendeleo ya kata (WODC) baada ya tatizo la wanafunzi kukatisha masomo kutokana na kupata uja uzito kuzidi kuwa sugu.

Ofisa mtendaji wa Kata ya Nyehunge, Mabula Enock alisema sheria hiyo itasaidia kudhibiti vitendo vya wanaume wanaoshawishi wasichana kufanya nao mapenzi na baadaye kuwapa ujauzito unaokatisha ndoto zao.

“Tumelazimika kupitisha sheria hiyo ili kuungana na mkuu wa wilaya yetu, Emmanuel Kipole aliyeagiza wanaume watakaokutwa wamesimama na wanafunzi wacharazwe viboko au kutozwa faini ya Sh10, 000 ama vyote kwa pamoja,” alisema Enock.

Agizo la mkuu huyo wa wilaya alilitoa Oktoba mwaka 2017 wakati akikaribisha wanafunzi 81 kujiunga na masomo ya kidato cha tano katika Shule ya Sekondari ya Nyehunge.

Diwani wa kata hiyo, Charles Mbogo alisema kitendo cha kukatiza masomo si cha kuungwa mkono, hivyo adhabu inapaswa kuongezwa na kuitaka jamii kuachana na suala hilo.

Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na ofisa elimu ya sekondari wa Buchosa, Benjamini Siperato halmashauri hiyo ina jumla ya wanafunzi 1,136 katika shule 20 za sekondari 20 na mwaka 2016/17 wanafunzi 18 wa kike walipata ujauzito, hivyo jamii inapaswa kuacha tabia ya kuwarubuni watoto wa kike.

Waziri Mkuu Aweka Jiwe La Msingi Kituo Cha Kupozea Umeme Njia Ya Makambako – Songea

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameweka jiwe la msingi kwenye mradi wa njia ya kusafirisha umeme wa kilovoti 220 kutoka Makambako hadi Songea na kuahidi kuwa Serikali itaendelelea kuwasambazia umeme wananchi wote.

Ametoa ahadi hiyo jana Jumapili, Januari 7, 2018 wakati Akizungumza na wananchi wa eneo la Unangwa nje kidogo ya mji wa Songea, mara bada ya kuweka jiwe la msingi kwenye mradi wa ujenzi wa kituo cha kupozea umeme.

Waziri Mkuu alisema ujenzi huo unaenda sambamba na ahadi ya Mheshimiwa Rais, Dk. John Joseph Magufuli ya kuwataka Watanzania wapate umeme kwa urahisi.

 “Mheshimiwa Rais ameshusha gharama za umeme kutoka sh. 380,000 hadi sh. 27,000. Zamani ulikuwa unalipia fomu za kuomba umeme, sasa hivi nazo amesema zitolewe bure. Nguzo za umeme zilikuwa zinatozwa sh. 150,000, sasa hivi amesema zitolewe bure,” alisema.

Waziri Mkuu amesema zamani mikoa ya Njombe, Iringa, Ruvuma, Songwe, Mtwara na Lindi ilikuwa na matatizo sufu ya kupata umeme lakini hivi sasa mikoa ya Mbeya na Iringa imepata suluhisho baada ya kukamilika kwa mradi wa umeme wa kilovoti 400 wa kutoka Iringa hadi Shinyanga.

“Sasa hivi tunaingia Njombe na Ruvuma na baadaye tutaenda Mtwara na Lindi,” alisema.

Alitumia fursa hiyo kuwaomba wakazi wanaoishi jirani na mahali kituo hicho kinapojengwa, wawe walinzi wakuu wa mali za mkandarasi ili mradi huo uweze kukamilika mapema. “Eneo hili lina saruji, nyanya na nondo, si vema watu wachache wjiokeze na kuiba vifaa vya ujenzi. Saidieni kulinda eneo hili, na mali za mkandarasi ili mradi ukamilike kwa wakati,” alisisitiza.

Akitoa taarifa ya ujenzi wa mradi huo, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Dk. Titus Mwinuka alisema mradi huo utakapokamilika utaunganisha vijiji 120 na wateja 22,700.

Wakati huohuo, Waziri Mkuu ameweka jiwe la msingi la ujenzi wa ofisi za TANESCO mjini Songea ambalo litagharimu sh. bilioni 2.27. Ujenzi wa jengo hilo unatarajiwa kukamilika mwishoni mwa Machi, 2018.

Akimkaribisha kuzungumza na watumishi wa TANESCO na wananchi waliohudhuria hafla hiyo, Waziri wa Madini, Dk. Medard Kalemani alisema jengo hilo ni moja ya majengo makubwa saba nchini ambayo yatakuwa makao makuu ya kimkoa ya TANESCO.

Majengo mengine yatajengwa kwenye mikoa ya Singida, Kilimanjaro, Mtwara, Njombe, Pwani, Geita na Kigoma. “Kukamilika kwa ofisi hizi haimaanishi wafanyakazi wakae ofisini na kufaidi viyoyozi. Ni lazima waende nje kuwafuata wateja,” alisisitiza.

Dk. Kalemani alisema chini ya mradi wa kusafirisha umeme wa kilovoti 220 kutoka Makambako hadi Songea, Serikali imeamua kujenga vituo vya kupozea umeme huko Makambako, Madaba na Songea ambavyo vitakamilika Agosti 30, 2018.

“Kukamilika kwa mradi huo kutaiepusha TANESCO na mzigo mkubwa wa kutumia fedha nyingi kununua mafuta mazito ambao pia utapunguza gharama za umeme kwa watumiaji. Kabla ya hapa, TANESCO ilikuwa inatumia sh. milioni 900 kwa siku kugharimia mafuta hayo,” alisema.

Mapema, akitoa taarifa ya ujenzi wa jengo hilo, Kaimu MKurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Dk. Titus Mwinuka alisema ujenzi wa jengo hilo ambao umefikia asilimia 78, unatarajiwa kukamilika ifikapo Machi 31, mwaka huu.

“Gharama za ujenzi kwa jengo zima ni sh. bilioni 2.198 na gharama za mshauri ni sh. milioni 78 na gharama zote zinafikia sh. bilioni 2.276. Fedha hizi zimetolewa na Serikali,” alisema.

Majaliwa awatolea uvivu mkuu wa wilaya, mkurugenzi

$
0
0
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amemtolea uvivu mkuu wa wilaya ya Nyasa, Isabella Chilumba na mkurugenzi wa halmashauri hiyo, Dk Oscar Mbyuzi, ambao wamekuwa wakivurugana, akisema tofauti zao zinaathiri watendaji walio chini yao na kuumiza wananchi.

Taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Waziri Mkuu inasema kuwa Majaliwa alisema hayo alipokuwa katika ziara yake Wilaya ya Nyasa.

Waziri Mkuu alisema katika ziara zote za mikoani, amekuwa akipata malalamiko mengi kwenye halmashauri na mabaraza ya madiwani, lakini amekuta hali si shwari Wilaya ya Nyasa kwa kuwa kuna migogoro midogo kwenye uongozi wa juu.

“Tatizo ni dogo huku juu, bado mnavurugana mkuu wa wilaya na mkurugenzi. Ninyi ni viongozi wa juu, acheni kuvurugana, fanyeni kazi. Mkigombana wanaoumia ni wananchi,” alisema.

“Mkuu wa wilaya anaweza kuingia kwenye kikao chochote cha halmashauri na kudai apewe taarifa, mpeni. Yeye siyo mjumbe wa kikao hicho, lakini anayo mamlaka ya kushiriki.

“Mkurugenzi ni mtendaji mkuu, tumekukabidhi watumishi uwaongoze. Tumekukabidhi fedha kwa ajili ya maendeleo ya wilaya hii. Mtu akizitamani, mwambie hizi fedha zina maelekezo rasmi, hazipaswi kwenda kokote.”

Aliwataka madiwani wasijenge tabia ya kuongeza siku za vikao kwa makusudi ili tu wapate posho za ziada. 

“Msitengeneze siku za ziada na kumpa presha Mkurugenzi. Kama kikao ni cha siku moja, basi kiishe. Siyo kulaza ajenda ili mmalizie kesho yake. Mkurugenzi akiwanyima fedha, msianze kugombana naye kwa sababu yeye hana fedha za kumgawia mtu,” alisisitiza.

BREAKING: Rais Magufuli Abaini Madudu Tena Bandarini...... Ateua Kamishna MPYA wa Madini

$
0
0
Rais Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Prof. Shukrani Elisha Manya Mhadhiri wa Chuo Kikuu Dar es Salaam (UDSM) kuwa Kamishna wa Madini.

Rais ametangaza uteuzi huo leo Jumatatu Januari 8, 2018 alipokuwa akitoa hotuba fupi mara baada ya kumuapisha Mhe. Dotto Mashaka Biteko kuwa Naibu Waziri wa Madini.

“Nimesikia tatizo ni kamishna wa madini, sasa nimeamua kumteua kamishna mpya wa madini, jina lake linaanza na Prof. Shukrani Elisha, huyo atakuwa ndiye mtendaji na msimamizi mkuu wa madini.

“Mambo ya hovyo ni mengi mno, nilipotembelea bandarini niliunda katume kasirisiri hivi, kwa kulihusisha Jeshi la Wananchi, TISS na Polisi. Yanayogundulika huko ni ya ajabu, kuna hadi simenti za zamani sana, yapo makontena bandarini na pale Ubungo.

“Mimi sio mwanasiasa mzuri wa kubembelezabembeleza, nikitoka mimi mtapata wakubembeleza, ila mimi nataka kabla ya Ijumaa regulations (kanuni za sheria ya madini) ziwe zimesainiwa. Pro Kabudi nendeni mkazifanyie kazi, tafuta watu wa kukusaidia na mkamalize hayo,” alisema Magufuli.

Kamishna aliyekuwepo,  Mhandisi Benjamin Mchwampaka amehudumu katika nafasi hiyo kwa siku 263 tangu alipoteuliwa mpaka leo uteuzi wake ulipotenguliwa na Rais magufuli.

Aidha rais Magufuli amewataka watendaji wote wa Wizara ya Madini kuchapa kazi kwa bidii kwani mpaka sasa bado utendaji wao bado unasuasua.

Breaking News: Matokeo ya darasa la nne na kidato cha pili yatangazwa. Bofya Hapa Kuyatazama

$
0
0
Baraza la Mitihani Tanzania (Necta) limetangaza matokeo ya mitihani ya upimaji wa darasa nne na kidato cha pili iliyofanyika Novemba 22 na 23 mwaka jana, huku idadi kubwa ya wanafunzi wakifanya vyema katika mitihani hiyo.

Akitangaza matokeo hayo leo Jumatatu Januari 8, Katibu Mtendaji wa Necta,  Dk Charles Msonde amesema jumla ya wanafunzi 1,086,156 waliofanya mtihani wa darasa la nne wamefaulu  kati ya 1,158,444 waliofanya upimaji huo.

Amesema  wanafunzi hao wamefaulu kwa kupata alama zenye madaraja ya A,B,C na D wakati wanafunzi 72,288 sawa na asilimilia 6.24 wamepata alama za daraja E, ambao ni ufaulu usioridhisha.

Kuhusu matokea ya upimaji wa kidato cha pili, Dk Msonde  amesema jumla ya wanafunzi 433,453 sawa na asilimia 82.32 kati ya 486,742 waliosajiliwa  kufanya mtihani huo wamepata ujuzi wa maarifa ya kuwawezesha kuendelea  na kidato cha tatu.

Dk Msonde alisema wanafunzi wa kidato cha pili  51,807 sawa na asilimia 10.68 wameshindwa kupata alama za kuwawezesha kuendelea na kidato cha tatu.


Mwendokasi ( UDART ) wasitisha shughuli zao kwa muda Kutokana na Mafuriko Jijini Dar

$
0
0
Kufuatia barabara, madaraja na mitaro kujaa maji jijini Dar es Salaam kutokana na mvua kubwa inayoendelea kunyesha  jijini Dar es Salaam, kampuni inayotoa huduma katika mradi wa mabasi yaendayo haraka (Udart) imesitisha kwa muda huduma za mabasi yake.

Taarifa iliyotolewa leo Jumatatu Januari 8 Mkuu wa mitengo cha mawasiliano wa kampuni hiyo, Deus Bugaywa imesema huduma hizo zitarejea mara baada ya hali kutengamaa.

“Kutokana na maji kupita juu ya daraja la Mto Msimbazi kwenye barabara ya Morogoro na kusababishwa kufungwa kwa muda kwa barabara hiyo, kampuni ina uarifu umma kuwa huduma za mabasi hayo zimesitishwa kwa muda,” imesema taarifa hiyo na kuongeza,

“Imesitishwa kuanzia saa 3:00 asubuhi, mara  baada ya hali kutengemaa na mamlaka husika kuruhusu barabara hiyo kuendelea kutumika, huduma zitarejea mara moja.”

Serikali yaitaka Stamigold ijiendeshe kibiashara

$
0
0
Na Veronica Simba – Biharamulo
Serikali imetoa siku 14 kwa kampuni ya Stamigold, inayomiliki Mgodi wa Dhahabu uliopo Biharamulo mkoani Kagera, kuandaa mpango mkakati wa kibiashara, utakaobainisha namna itakavyojiendesha pasipo kuitegemea Serikali.

Agizo hilo lilitolewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Profesa Simon Msanjila alipotembelea Mgodi huo na kuzungumza na Menejimenti pamoja na wafanyakazi wake.

Profesa Msanjila alisema kuwa lengo la Serikali kupitia Wizara ya Madini, ni kuona Kampuni tanzu hiyo ya Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), inajiendesha kibiashara na kiushindani ili ipate faida stahiki na kulinufaisha Taifa kama ilivyo dhamira ya kuanzishwa kwake, na siyo vinginevyo.

“Menejimenti ya Kampuni, Bodi pamoja na Menejimenti ya STAMICO, nawapa hadi tarehe 21 mwezi huu, kila upande uwe umewasilisha mapendekezo ya kimkakati yanayobainisha namna gani Stamigold itaweza kusimama yenyewe na kujiendesha kiushindani kama zilivyo kampuni nyingine za kibiashara. Kwa upande wetu, Kamishna wa Madini na mimi Katibu Mkuu pia tutakuja na mapendekezo yetu.” alisema Profesa Msanjila.

Akifafanua zaidi, Katibu Mkuu alisema Serikali imewekeza kwa kiasi kikubwa katika kampuni ya Stamigold hivyo haitakubali kuona mgodi huo unaendeshwa kwa hasara. “Kila mtu awajibike kwenye eneo lake,” alisisitiza.

Alisema, pamoja na kuwa Stamigold ni kampuni ya Serikali lakini imesajiliwa na Taasisi inayotoa leseni za biashara ya Brela, hivyo inapaswa kujiendesha kama kampuni nyingine za kibiashara. 

“Kampuni ya serikali ambayo haifanyi biashara haiendi kujiandikisha Brela. Ninyi mnafanya biashara hivyo lazima mfanye kazi kibiashara.”

Aidha, Profesa Msanjila aliutaka uongozi wa kampuni kuhakikisha unaweka wazi taarifa zote za mapato na matumizi kwa wafanyakazi wote ili waelewe wanazalisha kiasi gani, wanapata faida kiasi gani, matumizi ni kiasi gani na kama kuna hasara ibainishwe wazi.

Alifafanua kuwa utaratibu wa kuweka wazi mapato na matumizi kwa wafanyakazi wote utaondoa manung’uniko kwani utaratibu wa kibiashara unamtaka mwajiri amlipe mfanyakazi kulingana na mapato. 

“Huwezi kumlipa mtu mshahara hata pale ambapo hazalishi. Hii siyo sawa kibiashara maana lazima utapata hasara. Huu ndiyo ukweli ndugu zangu. Tubadilike. Hakuna hela ya kuchezea.”

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO Mhandisi John Nayopa alimhakikishia Katibu Mkuu kuwa maagizo yote aliyoyatoa yatatekelezwa ndani ya muda alioelekeza. 

Aidha, aliwataka wafanyakazi wa Stamigold kutoa ushirikiano kwa kutoa maoni na ushauri wao wakati wa kuandaa mpango mkakati huo utakaoiwezesha Kampuni kujiendesha kibiashara.

Katika ziara hiyo, Katibu Mkuu aliambatana na viongozi wengine wa Wizara akiwemo Mkurugenzi Msaidizi wa Rasilimaliwatu, Miriam Mbaga, Kamishna Msaidizi wa Madini Kanda ya Ziwa Viktoria Magharibi, Mhandisi Yahaya Samamba, Kaimu Afisa Madini wa Mkoa wa Kagera, Paschal Bundala na Mhandisi Migodi kutoka wizarani, Kungulu Kasongi.


Rais Magufuli Aibua Madudu Zaidi.....Akerwa na Utendaji wa Viongozi wa Wizara ya Madini

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ameanika madudu mengine ya Wizara ya Madini akisema kuwa baadhi ya wateule wake katika wizara hiyo wamekuwa wazembe katika kutekeleza maagizo na kutimiza majukumu yao kama watendaji wa serikali.

Magufuli ameyasema hayo leo Jumatatu wakati akimwapisha Mhe. Dotto Mashaka Biteko kuwa Naibu Waziri wa Madini Ikulu jijini Dar es Salaam. 

Rais ametolea mfano wa sheria mpya ya madini iliyopitishwa bungeni mwezi Julai mwaka jana, ambapo amesema mpaka sasa wizara hiyo haijapitisha kanuni (regulations) ili sheria hiyo iweze kufanya kazi jambo ambalo amesema ni uzembe usiovumilika huku akimwagiza Waziri wa Sheria, Prof. Palamagamba Kabudi kukamilisha kanuni hizo na kuzisaini kufikia Ijumaa ya wiki hii.

“Nakushukuru Mhe spika kwa kutoa ushauri kwa serikali na sisi tumekuwa tukiufuata sana. Wizara ya madini ina changamoto sana na hata sasa ina changamoto na haifanyi kazi vizuri. Spika utakumbuka mwezi wa saba mlifanya marekebisho ya sheria ya madini.

" Na ilipokuja kwa kwangu siku hiyo hiyo nilisaini na kuipitisha, lakini tangu Julai mpaka sasa regulations (kanuni) hazijasainiwa lakini sheria imepitishwa na bunge, hivyo sisi Watanzania watumishi hatupo serious.

“Nasikitika kusema baadhi ya ninaowateua hawajajua nataka nini. Ndiyo maana nikamteua aliyekuwa kwenye kamati ya madini, labda atatoa changamoto kwa wenzake maana huenda yeye anaelewa zaidi. 

"Na mnada wa Tanzanite hautafanyika tena mpaka regulations zitakaposainiwa. Sasa mpo manaibu wawili na waziri wa sheria yupo hapa nataka regulations hizi zisainiwe kabla ya Ijumaa, tumeibiwa mno, sasa nimesema imetosha,” alisema Rais Magufuli kwa uchungu.

LIVE | Mkutano wa Msemaji wa Serikali kuhusu utekelezaji wa ahadi za serikali

$
0
0
Msikilize hapo chini Msemaji wa Serikali akizungumza na waandishi wa habari.. Kuna nini???  Bofya apo umsikie

Spika Ndugai Ammwagia Sifa Rais Magufuli

$
0
0
Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai amempa pongezi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuweza kusikiliza maoni ya Bunge na wabunge kwa kutekeleza moja ya maombi yao kuigawa Wizara ya Nishati na Madini.

Ndugai ametoa pongezi hizo leo Januari 8, 2018 akiwa Ikulu jijini Dar es Salaam katika hafla ya kuapishwa kwa Naibu Waziri wa Madini, Mhe. Doto Mashaka Biteko na kusema kwa miaka mingi walikuwa wakitaka Wizara hizo kugawanywa lakini ilikuwa inashindikana ila katika awamu ya tano Rais Magufuli ndiyo ameweza kufanya hivyo.

"Sisi Bunge tulikuwa tukishauri toka miaka ya nyuma kwa Serikali kwamba Wizara iliyokuwa inaitwa Wizara ya Nishati na Madini ilikuwa ni nzito mno, ilikuwa imejaza mambo mengi sana kwa wakati mmoja ushauri wetu ulikuwa ni vizuri kuzitenganisha na kuzisimika kila moja kivyake. 

"Jambo hili Mhe. Rais umelitekeleza kabisaa kwenye awamu ya tano umeunda wizara mbili na hata tendo la leo linadhirisha kabisa jinsi ambavyo unazidi kuimarisha sekta ya Nishati na Madini kwa hili tunakushukuru sana kwani linaonesha dhamira yako ilivyo" alisema Ndugai

Mbali na hilo Ndugai amesema kuwa katika miaka ya nyuma katika sekta ya madini na nishati kama nchi tumeliwa sana hivyo anaamini kuwa katika Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Magufuli na wateule wake jambo hilo halitaweza kuendelea tena.

Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania linatarajiwa kuanza mnamo Januari 30, 2018 Makao Makuu ya nchi mjini Dodoma.

TRA Yakusanya Zaidi Ya Trilioni 7.87 Kwa Kipindi Cha Nusu Mwaka 2017/2018

$
0
0
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imeeleza kuwa, katika kipindi cha kuanzia Julai hadi Disemba, 2017, imekusanya jumla ya shilingi trilioni 7.87, ikilinganishwa na shilingi 7.27 zilizokusanywa katika kipindi kama hicho kwa mwaka wa fedha wa 2016/17.

Sumatra yajipanga kuruhusu mabasi kusafiri kwa saa 24

$
0
0
Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Majini na Nchi Kavu (SUMATRA), imeeleza kuwa ina mpango wa kufunga mfumo wa kuratibu mwenendo wa mabasi (VTS), katika mabasi yote ili kuweza kukusanya taarifa za mwenendo wa mabasi yanayosafirisha abiria kwenda mikoa mbali mbali hapa nchini.

Mkurugenzi Mtendaji wa Sumatra, Williard Ngewe, alieleza hayo jana, Jumapili, Januari 7, 2018, jijini Mbeya wakati wa mkutano wa kutoa elimu kwa wadau wa usafirishaji mkoani humo juu ya sheria mpya ya usimamizi wa usafiri wa mabasi.

Mkurugenzi Ngewe aliongeza kuwa wameamua kufunga mfumo huo ili kupima mwenendo wa mabasi ya mikoani na kisha baadae kuruhusu mabasi hayo yawe yanafanya safari zake muda wowote (mchana na usiku) ili kuongeza tija katika sekta ya usafiri nchini.

Alisema mfumo huo unasaidia mamlaka hizo mbili kutambua matatizo kwenye mabasi pindi inapotokea na hivyo hatua za haraka kuchukuliwa ili kudhibiti madhara.

“Kuna kitufe maalumu kwenye mfumo huo ambacho dereva anapopata tatizo, ikiwamo basi kutekwa, kupata ajali ama basi linapoharibika katika sehemu ambayo inayotakiwa ulinzi, anabonyeza kisha taarifa zinafika Sumatra na Polisi…(halafu) tunachukua hatua za haraka kuokoa,” alisema Ngewe.

Aliongeza kuwa lengo kubwa la kufunga mfumo huo kwenye mabasi ya abiria yaendayo mikoani, ni katika kuhakikisha kuwa wanapunguza ajali kwa kuratibu mwenendo wa madereva, kondakta pamoja na usalama mzima wa basi  linapokuwa safarini.

Kwa upande wake, Meneja wa Huduma za Sheria wa Sumatra, Leticia Mutaki, alisema kwa mujibu wa sheria mpya ya usafirishaji, miongoni mwa makosa yaliyoainishwa kuwa yanaweza kulifungia basi ni kuchezea mfumo huo wa VTS.

Meneja Mutaki, alisema kutokana na malalamiko ya wadau na maoni mbalimbali yaliyotolewa, sheria hiyo imeshafanyiwa marekebisho na kwamba makosa ya mmiliki na dereva yametofautishwa na kila mmoja wao ana nafasi yake katika basi husika.

Alisema dereva pamoja na kondakta watawajibika kwa vitendo vyote vya utovu wa nidhamu wakati wakiendelea na safari ikiwamo kuonyesha video ambazo zipo kinyume cha maadili zikiwamo za watu wanaoonekana wakiwa watupu.

“Lengo la kuanzisha mfumo huu ni kuongeza tija kwenye sekta yetu hii ya usafirishaji, sasa sheria imeweka wazi kuwa endapo mfumo huo utabainika kuwa umechezewa, basi husika litafungiwa kufanya kazi kwa siku 30,” alisema Mutaki.

Rais Magufuli Aipa Siku 5 Wizara ya Kilimo

$
0
0
Rais Magufuli ameiagiza Wizara ya Kilimo kuhakikisha mbolea inafikishwa katika mikoa yote ya uzalishaji wa chakula ukiwemo Mkoa wa Rukwa ifikapo Ijumaa Januari 12, 2018.

Magufuli ameyasema hayo leo Jumatatu wakati akimwapisha Mhe. Dotto Mashaka Biteko kuwa Naibu Waziri wa Madini Ikulu jijini Dar es Salaam. 

Amemuelekeza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kufuatilia jambo hilo na amebainisha kuwa endapo mbolea haitafikishwa katika maeneo hayo ifikapo Ijumaa wahusika waachie ngazi.

“Wakulima wanataka mbolea na muda ni huu, inasikitisha sana, fedha kwenye bajeti zimetengwa lakini mpaka leo mbolea haijawafikia wakulima, sasa mkoa kama Rukwa ndio tunaoutegemea kwa chakula, waziri yupo na watendaji wake wapo lakini mpaka leo mbolea haijapelekwa, wakulima watazalishaje chakula?

Rais Magufuli amewataka watendaji wote wa Serikali kutekeleza majukumu yao ipasavyo na ameonya kuwa hatosita kumfukuza kazi mtendaji yeyote atakayeshindwa kutekeleza wajibu wake kwa maslahi ya Watanzania.

“Nataka kila mmoja afanye kazi, Watanzania wanataka maendeleo, hakuna muda wa kubembelezana, kila mmoja afanyie kazi mambo yanayomhusu asisubiri kuambiwa, kule bandarini niliunda timu za kuchunguza madudu yaliyopo huko naambiwa kuna makontena 178 ya makinikia hayana mwenyewe, mengine yapo Ubungo, mengine bandari” ameongeza  Rais Magufuli.

VIDEO: Hotuba Ya Rais Magufuli alipomuapisha Naibu Waziri Wa Wizara Ya Madini.

$
0
0
Rais Dkt. John Pombe Magufuli ameamuapisha Mhe. Doto Mashaka Biteko kuwa Naibu Waziri wa Madini, Ikulu Jijini Dar es Salaam leo Jumatatu, Januari 8, 2018

==>Msikilize hapo chini Rais Magufuli akiongea baada ya kumuapisha Mhe. Dotto Mashaka Biteko
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images