Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Polisi Yasema Makosa ya Jinai Yamepungua.....Mauaji na Ubakaji Yameongezeka

$
0
0
Jeshi la Polisi nchini limetamba kushinda vita dhidi ya uhalifu baada ya kupunguza matukio ya aina hiyo huku likikiri kuongezeka kwa vitendo vya ubakaji na kunajisi.

Wakati hali ikiwa hivyo, jeshi hilo limetoa tahadhari kwa watu ambao hujihusisha na uhalifu hasa katika kipindi cha sikukuu za mwisho wa mwaka kwa lengo la kutaka kujipatia kipato kwa njia zisizo halali kuwa watachukuliwa hatua kali kwa kuwa limejipanga kupambana nao.

Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Robert Boaz, alisema hayo jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na hali ya usalama nchini.

Alisema hali ya usalama wa nchi kwa ujumla ni ya kuridhisha na kwamba takwimu zinaonyesha kuwa kuanzia Januari hadi Novemba, mwaka jana, makosa makubwa ya jinai yalikuwa 68,204 ikilinganishwa na makosa 61,794 yaliyoripotiwa mwaka huu.

Hali hiyo imesababisha upungufu wa makosa 6,410 ambayo ni sawa na asilimia 9.4.

Ubakaji Waongezeka
Hata hivyo, Kamishna Boaz alisema makosa ya ubakaji na kunajisi yanaonekana kuongezeka kwa kuwa kwa mwaka 2016 hadi kufikia Novemba, yaliyoripotiwa yalikuwa 6,935 kulinganisha na makosa 7,460 ambayo yaliripotiwa mwaka huu.

“Hili ni ongezeko la makosa 478 sawa na asilimia 6.8 wakati makosa ya kunajisi yalikuwa 16 mwaka 2016 ikilinganishwa na makosa 25 ambayo yametokea mwaka huu na kufanya ongezeko la makosa tisa sawa na asililimia 56.3,” alisema.

Alisema kuna sababu tatu ambazo zimechangia kuongezeka kwa matukio hayo ikiwamo mmomonyoko wa maadili kwa kuwa kuna watu wanaparamia watoto wadogo. Pia alisema hali hiyo inachangiwa na ushirikina kutokana na baadhi ya watu kuambiwa kuwa wakitembea na watoto wadogo wanaweza kufanikiwa katika mambo fulani, lakini wakati mwingine hiyo inatokana na tamaa za mwili.

“Sasa sababu hizo ni kwamba tiba yake ipo kwenye jamii na sisi tutaweka msisitizo sana mwakani na pengine mwisho wa mwaka kuhusiana na matukio hayo,” alisema Boaz.

Makosa dhidi ya Binadamu
Alisema makosa dhidi ya binadamu ambayo yanajumuisha mauaji, kubaka, kulawiti wizi wa watoto, kutupa watoto, kunajisi na kusafirisha binadamu yaliyoripotiwa katika kipindi cha Januari hadi Novemba, 2016 yalikuwa 11,513 kulinganisha na 11,620 yaliyoripotiwa mwaka jana ambayo ni ongezeko la makosa 107 sawa na asilimia 0.9.

Pia alisema makosa ya wizi wa silaha, unyang’anyi katika barabara kuu, unyang’anyi wa kutumia silaha, unyang’anyi wa kutumia nguvu, uvunjaji, wizi, wizi wa pikipiki, wizi wa magari, mifugo pamoja na kuchoma nyumba moto mwaka jana yaliripotiwa 34,830 wakati mwaka huu yameripotiwa makosa 29,677 ambayo ni pungufu kwa makosa 5,153 sawa na asilimia 14.8.

Makosa ya uhalifu wa kifedha
Boaz alisema makosa ya noti bandia , wizi katika mabenki, wizi katika mashirika ya umma, wizi katika vyama vya ushirika na makosa ya kughushi jumla ya yaliripotiwa makosa 1,861 kwa mwaka jana ukilinganisha na mwaka huu yaliripotiwa makosa 1,526 ikiwa ni pungufu ya makosa 335 sawa na asilimia 18.0.

Kwa upande wa uhalifu katika jamii, alisema makosa hayo ni yale ambayo yanahusisha kupatikana na silaha, dawa za kulevya, bangi, mashamba ya bangi, mirungi, nyaraka za serikali, magendo, rushwa, uvuvi haramu, kupatikana na mazao ya bahari na wahamiaji haramu.

Alisema makosa ya aina hiyo yaliyoripotiwa kwa kipindi cha Januari hadi Novemba, mwaka huu yalikuwa 20,000 kulinganisha na makosa 18,971 yaliyoripotiwa mwaka jana.

Makosa ya Barabarani
Kuhusu makosa ya usalama barabarani, alisema mwaka jana kuanzia Januari hadi Desemba yaliripotiwa matukio 9,550 ikilinganishwa na 5,537 yaliyoripotiwa katika kipindi kama hicho mwaka huu ikiwa pungufu ya matukio 4,013 sawa na asilimia 42.

Boaz alisema ajali hizo zilisababisha vifo vya watu 3,108 na majeruhi 8,898 kwa mwaka 2016 wakati mwaka huu watu waliokufa ni 2,491 na majeruhi 5,696.

“Uchunguzi umebaini kuwa kiasi kikubwa, ajali zinasababishwa na vyanzo vikuu vitatu ambavyo ni sababu za kibinadamu, ubovu wa vyombo vya usafiri na sababu za kimazingira.

“Sababu za kibinadamu ni pamoja na uendeshaji wa hatari, uzembe wa madereva, uzembe wa abiria, mwendokasi, uzembe wa watembea kwa miguu, ulevi, mifugo isiyochungwa na uzembe wa waendesha pikipiki,” alisema.

Aidha, alisema katika msimu wa sikukuu ya Krismasi na Mwaka Mpya, wamejipanga vyema kudhibiti vitendo vyote vya uhalifu vitakavyojitokeza kwa kuwa ulinzi utaimarishwa katika maeneo yote ikiwamo kwenye nyumba za ibada, fukwe za bahari, sehemu za starehe na mengine ya mikusanyiko mikubwa ya watu.

DCI azungumzia tukio la Tundu Lissu ,Ben Sanane na mwandishi wa habari Azory Gwanda

$
0
0
Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), amefunguka na kusema wao wanaendelea na upelelezi juu ya taarifa ya kutekwa kwa Ben Saanane na kudai hawawezi kusema kila hatua wanayochukua pia amedai polisi wanachukulia 'serious' shambulio la Lissu

DCI Boaz amesema hayo jan Disemba 20, 2017 wakati akiongea na waandishi wa habari na kusema kuwa amepata taarifa juu ya kupotea kwa mwandishi wa habari Azory Gwanda, Ben Saanane na kudai hawawezi kuwa wanatoa taarifa kwa kila hatua ambayo wamefikia.

"Tumepata taarifa za huyo mwandishi kupotea na kwa taratibu zetu tunachukua kila hatua inayostahili kuchukuliwa wakati wa utafutaji wa mtu aliyepotea.

"Zipo taratibu ambazo tunapaswa kuzichukua sisi kama polisi, suala la Ben Sanane tumeshalisema sana sisi kama upepelezi hatuwezi kusema kila hatua tunayochukua, hairuhusiwa kisheria na katika kanuni zetu za upelelezi lakini niwathibitishie kwamba kila hatua inayostahili kufanywa ili kutrace mtu imeshafanyika" alisema DCI Boaz na kuongeza;

”Pengine nitoe rai kwa wananchi na waandishi wa habari taarifa kwetu ni muhimu sana na huwa tunazifuatilia. Tunaendelea kuwaomba kama mna taarifa ambazo ni za uhakika watuletee tutazifanyia kazi.”

Akizungumzia tukio la Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu ambaye alipigwa risasi na watu wasiojulikana, Boaz alisema jambo hilo limezungumzwa sana na viongozi, hivyo asingependa kulizungumzia na kwamba Jeshi la Polisi linachukulia tukio hilo kwa umakini na hawawezi kujibishana na watu katika magazeti.

“Tunachukua hatua zote ambazo zinatuwezesha kutambua ni nani katenda tukio hilo,” alisema Boaz.

Ajali Yaua 7 Na Kujeruhi 12

$
0
0
Wakati Jeshi la Polisi likiendelea kutoa tahadhari ya mara kwa mara kwa madereva kuwataka waongeze umakini hasa katika kipindi hiki cha kuelekea msimu wa sikukuu za mwisho wa mwaka.

Ajali mbaya ya mabasi la abiria ilitokea jana na kusababisha vifo vya watu saba huku wengine 12 wakijeruhiwa vibaya.

Kwa mujibu wa mashuhuda, saba waliofariki dunia ni wanaume watano akiwamo dereva wa Toyota Hiace aliyetajwa kwa jina la Hassan na wengine wakiwa ni mtoto mdogo na mwanamke anayedhaniwa kuwa ni wa mtoto aliyefariki dunia.

Tukio hilo lililotokea jana majira ya saa 11:00 alfajiri, ikiwa ni siku nne tu kabla ya siku ya sikukuu ya Krismasi, lilitokea katika Kijiji Cha Kabeba, Kata ya Mwakizega, Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza mkoani Kigoma baada ya basi kubwa la abiria aina ya Scania la kampuni ya Saratonga (namba T384 BMG) kugongana uso kwa uso na basi dogo aina ya Toyota Hiace ‘kipanya’, lenye namba za usajili T237BCE.

Taarifa zilizothibitishwa na Polisi kupitia kwa Kaimu Kamanda wake mkoani humo, Sweatbert Njewike, abiria wote waliofariki dunia walikuwa katika basi dogo lililokuwa likisafiri kutoka Kigoma Mjini kwenda katika Kijiji cha Lilagala, Wilaya ya Uvinza mkoani humo.

Majeruhi walipelekwa kwenye Hospitali ya Rufani ya Mkoa wa Kigoma wakiwa ni wa kutoka mabasi yote mawili. Basi kubwa lilikuwa likitokea eneo la kijiji cha Lilagala kwenda Kigoma Mjini.

Kwa mujibu wa Kaimu Kamanda Njewike, uchunguzi kuhusiana na ajali hiyo bado unaendelea kabla hatua zaidi hazijachukuliwa.

Hata hivyo, kamanda huyo aliongeza kuwa taarifa za awali zinaonyesha kuwa chanzo ni uzembe na ubabe wa madereva wa magari hayo baada ya wote wawili kukataa kupeana nafasi ya kupita kwa zamu kwenye daraja jembamba katika eneo hilo na mwishowe kugongana uso kwa uso wakati kila mmoja akijaribu kupita kwa kasi.

Kutokana na ajali hiyo, Kamanda huyo aliwataka madereva mkoani humo kuzingatia sheria za barabarani ili kujiweka mbali na ajali zinazoepukika na pia kutumia busara kwa kupeana nafasi wakati wanapokatiza kwenye maeneo tata kama ya kwenye madaraja madogo na kona kali.

Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufani ya Mkoa wa Kigoma, Maweni Kibaya, alisema jana kuwa waliwapokea watu waliojeruhiwa katika ajali hiyo na kwamba walikuwa wakiendelea kuwatibia huku baadhi yao wakiwa na majeraha makubwa katika sehemu mbalimbali za miili yao.

Kauli Ya Albert Msando Baada ya Kuteuliwa na Rais Magufuli

$
0
0
Mwanasheria Albert Msando amemshukuru Rais Magufuli kwa kumuamini na kumteua kuwa miongoni mwa watu 9 ambao watakuwa na jukumu la kufuatilia na kuhakiki mali za Chama Cha Mapinduzi (CCM) kote nchini.

Albert Msando ameandika ujumbe huo wa shukrani kwenye ukurasa wake wa instagram, na kusema kwamba anaamini kazi hiyo itafanyika kwa weledi.

“Namshukuru Mh. Dkt. John Pombe Magufuli, Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa uteuzi wa kuwa mjumbe wa Tume ya Kufuatilia Mali za Chama. Chini ya uenyekiti wa Dkt. Bashiru Ally Kakurwa na wajumbe wengine wa tume.Nnaamini kwa dhati kazi hii itafanyika kwa weledi ili kukiwezesha chama cha Mapinduzi kujitegemea kupitia mali zake”, ameandika Albert Msando

Hapo jana Rais Magufuli ameteuwa timu ya watu 9 ambao wataunda tume ya kufuatilia na kuhakiki mali za CCM nchini kote, baada ya kubaini kuna baadhi ya mali haziingizi kipato stahiki.

Korea Kaskazini Yapiga Marufuku Sherehe za Krismass

$
0
0
Kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong Un amepiga marufuku mikusanyiko inayoashiria kusherehekea sikukuu ya Krismasi kama vile inayohusu unywaji na uimbaji.

Ametaka wananchi kutosherehekea sikukuu hiyo na wanaopenda kufanya hivyo, waitumie Desemba 24 kusherehekea siku ya kuzaliwa kwa bibi yake aliyezaliwa siku kama hiyo mwaka 1919.

Kiongozi huyo ameviagiza vyombo vya ulinzi na usalama kuhakikisha vinadhibiti mikusanyiko yote ambayo inaendana na maadhimisho ya Krismasi.

“Ni marufuku watu kukusanyika na kufanya mambo kama ya unywaji au kuimba katika sikukuu ya Krismasi,” chanzo kimoja cha habari kimenukuu taarifa ya kiongozi huyo.

Kim Jong Un amekuwa akichukua hatua kuzua kuenea kwa utamaduni kwa kigeni na amedhibiti vyombo vya habari kutotangaza taarifa zozote zinazoienzi sikukuu hiyo kama hatua ya kupiga marufuku Krismasi.

Ingawa sikukuu ya Krismasi si tukio kubwa nchini humo, lakini baadhi ya wananchi wamekuwa wakiisherekea na kufuata misingi ya Kikristo.

SORRY MADAM -Sehemu ya 84 & 85 (Destination of my enemies)

$
0
0
MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA
ILIPOISHIA

 “Eddy…yu…..”
Sa Yoo hakumalizia sentensi yake kwa maana aliweza kumona Eddy akiwa amekumbatiwa na mwanamke wengine, tena mwanamke huyo akionekana kumpiga mabusu mfululizo kila sehemu ya uso wake. Madam Mery akafanikiwa kuona tukio hilo.
“Yupo wapi?”
Phidaya aliuliza, huku akitazama sehemu aliyo kuwa ameangalia Sa Yoo, Phidaya na Shamsa wote wakastuka kwa kumuona Eddy akiwa anadendeka na mwanamke mwengine, wote wawili kwa pamoja wakaanza kutembea kwa mwendo wa haraka kuelekea katika eno alilo simama Eddy na Agnes, wanao dendeka pasipo kujali wingi wa watu walio kuwa katika eneo hilo.  

ENDELEA
   Sa Yoo na Madam Mery wote kwa pamoja wakawawahi Phidaya na Shamsa ambao kwa pamoja wanaonekana kujawa na hasira ya kumuona Eddy akiwa anafanya uchafu huo mbele yao.
“Munatuzuia nini?”
Shamsa alizungumza kwa hasira huku akijaribu kutaka kumpita Sa Yoo aliye simama mbele yake.
“Munataka mufanye nini sasa?”
 
Sa Yoo aliwauliza kwa sauti ya juu hadi baadhi ya askari wakawatazama. Wanajeshi wanne walio valia vitambaa vilivyo andikwa MP, wakawafwata Shamsa na wezake walipo simama.
“Hamruhusiwi kuingia katika eneo hili”
Mwanjeshi mmoja alizungumza huku akiwa amewakazia macho Shamsa na Phidaya ambao wanaonekana kwamba ni vigego wanao taka kwennda katika eneo ambalo limesha zungushiwa utepe wa alama ya njao wenye maandishi meusi yaliyo andikwa ‘DANGER’    
“Sisi tunataka kumuona Ed…..”
Shamsa alijikuta akiropoka ila kwa haraka Sa Yoo akawahi kumzimba mdomo.
“Waheshimiwa tumewaelewa, kidogo wezetu wamechanganyikiwa na hili tukio”
Madam Mery alizungumza huku akimshika mkono Phidaya, wakaondoka eneo hilo huku wakisindikiwa na wanajeshi hao wenye mitutu ya bunduki. Mara kwa mara Shamsa aligeuka nyuma na kumuangalia Eddy anaye onekana kusahau kabisa kama ana mke wake.
 
“Ndio mumefanya nini sasa?”
Shamsa alizungumza kwa kufoka huku akimtazama Sa Yoo kwa macho ya hasira, Sa Yoo hakulijali hilo zaidi ya kutafuta sehemu na kukaa, kwani wote hawakujua ni nini kilicho tokea hadi wakamuona Eddy akiangua kilio akiwa katika eneo hilo.
“Tunatakiwa kujua ni kitu gani kinacho endelea, na si muda wa kakaa na kugombana”
“Madam Mery nakuheshimu sana, ila wewe umekuwa chanzo cha Eddy kuwa na yule mwanamke na bado munaendelea kumtetea tetea, inabidi yule mwanamke tumshike tumbamize hadi akome”
Shamsa alizidi kuzingumza kwa hasira, madam Mery hakumjibu kitu cha aina yoyote kwa maana anatambua hiyo ni hasira na baada ya muda fulani itakwenda kupotea.  Phidaya alikaa kimya huku akiendelea kuumia kimoyo moyo. Picha ya mwanamke ambaye yupo na Eddy, mara kadhaa ikawa inamrudia kichwani mwake. Hakuweza kuyazuia machozi yake kwa maana maumivu aliyo nayo ni makali sana japo anatambua mume wake yupo hapo kwa kazi fulani.
‘Inakuwaje wapigane mabusu hadharani?’
Hilo ni swali alilo liwaza Phidaya mara kadhaa kichwani mwake, akijaribu kutazama ndani kama anaweza kumuona Eddy na huyo mwake, ila hakuweza kuwaona kutokana na wingi wa watu wanao zidi kumiminika kutoka maeneo mbalimbali kujua kushuhudia tukio hilo la kutisha.
                                                                                                               ***
“Erickson haupo sawa mume wangu madaktari wamekuja kukuchukua wakuwahishe hospitalini”
“Nipo sawa Agnes”
 
“No haupo sawa, madaktari mchukueni”
Agnes aliwaambia madaktari ambao wamefika sehemu hiyo kwa ajili ya kuwachukua majeruhi kama Eddy. Eddy akatazama pende zote haswa sehemu ulipo mwili wa raisi Praygod, ili utambulisho wake usijulikane, taratibu akaondoka na kuongozana na madaktari huku Agnes akifwata kwa nyuma. Eddy akalala kwenye kitanda kidogo cha wagonjwa, kikanyanyuliwa na kuingizwa kwenye gari ya wagonjwa. Madaktari hao wawili wakaingia kwenye gari hilo huku wakifwatiwa na Agnes aliye kaa karibu sana na Eddy.
   Wakafika katika hospitali ya Muhimbili. Eddy akashushwa kwenye kitanda na moja kwa moja akapelekwa kwenye chumba cha  kupatiwa huduma ya kwanza.
“Dokta mimi nipo salama, naomba niondoke zangu”
Eddy alizungumza huku akikaa kwenye kitanda hicho, daktari akabaki amemtumbulia macho. Eddy akasimama wima, akapiga hatua hadi mlangoni, akafungua na kuondoka zake na kumuacha daktari akiwa bado ameduwaa.
 
“Honey vipi mbona umetoka?”
“Nipo salama”
“Kweli mpenzi wangu?”
“Ndio, nahitaji kuelekea nyumbani muda huu”
“Ok basi twende pamoja nikapafahamu kwako”
“Hapana tutakwenda siku nyingine kwa leo ninakumba niende peke yangu na sinto hitaji unifwate”
Eddy alizungumza kwa sauti yenye msisitizo hadi Agnes mwenyewe akajikuta akimuogopa. Eddy ahakutaka kupoteza muda. Moja kwa moja akatoka eneo la hospitali huku Agnes akimfwata kwa nyuma. Eddy bila yakujali, akamuita bodaboda mmoja wa pikipiki, akapanda na kuondoka.
“Nipeleke bahari beack hoteli”
“Sawa”
Dereva bodaboda akaondoa pikipiki na kumuacha Agnes akiwa anashangaa shangaa asijua ni nini cha kufanya.

<<Endelea Nayo Kwa Kubofya Hapa>>

Orodha ya Mikoa iliyotahadharishwa kuwa na mvua kubwa msimu wa sikukuu

$
0
0
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), imesema wakati wa kuelekea sikukuu za Krismasi na mwisho wa mwaka, mvua kubwa zinatarajiwa kunyesha katika mikoa ya Mbeya, Songwe, rukwa na Kigoma.

Meneja wa kituo Kikuu cha Utabiri wa Hali ya Hewa wa TMA, SAmuel Mbuya, alieleza kuwa mvua zinazoendelea kunyesha katika maeneo ya ukanda wa Pwani ni zile za kumalizika kwa msimu wa vuli.

Mkurugenzi Mbuya alieleza kuwa Mikoa hiyo minne iliyotajwa ndiyo inayotarajiwa kuwa na mvua wakati wa sikukuu na ifikapo mwisho wa mwezi huu, mvua zinazoendelea kunyesha katika mikoa mbalimbali ikiwamo Dar es Salaam zitakuwa zimefikia ukingoni.

“Mvua zinazonyesha maeneo ya ukanda wa Pwani ni zile za vuli na zilianza Oktoba na zinaisha mwisho wa mwezi huu, si mvua zinazoendelea isipokuwa tu katika mikoa ya Mbeya, Songwe Rukwa na Kigoma ambako katika msimu huu wa sikukuu kutakuwa na mvua,” alisema.

Aliongeza kuwa TMA inatarajia mvua zitaendele kunyesha katika mikoa ya. Kigoma, tabora, Katavi, Rukwa, Songwe, Mbeya, Ruvuma, Lindi, Dodoma na Singida. Alisema mvua katika mikoa hiyo zilianza kunyesha Novemba na zinatarajiwakumalizika mwezi Aprili.

Mbuya aliwataka wananchi kuendelea kufuatilia taarifa zinazotolewa na TMA mara kwa mara, ili kupata mwelekeo wa hali ya hewa pamoja na kuchukua tahadhari mapema.

Breaking News: Kiwanda Cha Pombe Bandia Chanaswa Jijini Mwanza

$
0
0
Wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihimiza ulipaji wa kodi wapo wahujumu uchumi na wanaotumia vibaya Sera ya Tanzania ya viwanda.

Kupitia oparesheni iliyofanyika jana  usiku, Jeshi la Polisi mkoani Mwanza limefanikiwa kubaini Kiwanda bubu cha pombe bandia  kilichokuwa kinazalisha pombe kali iliyopewa jina la 'kubumba'

Polisi wamekifunga kiwanda hicho na kumkamata mmiliki wake, Emanuel George Munisi maarufu kama CCM pamoja na wenzake wanne.

Pombe hizo zilikuwa zikitumia stempu ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), na meneja msaidizi wa TRA Mwanza amesema wanafuatilia kujua mtuhumiwa alipataje stempu hiyo bila kuwa na kibali

Kanisa Katoliki kufanya misa ya Krismasi kitaifa Zanzibar

$
0
0
Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) limesema misa ya Krismasi kitaifa itaadhimishwa katika Jimbo Katoliki Zanzibar katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Joseph, Minara Miwili.

Taarifa iliyotolewa leo Alhamisi Desemba 21,2017 na Mkuu wa Idara ya Mawasiliano Jamii ya baraza hilo, Bernard James imesema misa hiyo itaongozwa na Askofu wa jimbo hilo, Mhashamu Augustino Shao.

Katika sikukuu hiyo inayoadhimishwa Desemba 25 ya kila mwaka, Wakristo duniani huadhimisha kuzaliwa kwa Yesu Kristo.

Awali, mratibu wa matukio ya kanisa Tumaini Media, John Leveti amesema Kardinali Polycarp Pengo ataongoza misa ya mkesha wa Krismasi katika Kanisa Katoliki la Mtakatifu Maurus, Kurasini jijini Dar es Salaam.

"Askofu msaidizi wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Eusebius Nzigilwa yeye siku hiyo ya mkesha, Desemba 24 ataongoza ibada katika Kanisa la Mtakatifu Joseph," alisema Leveti.

"Siku ya sikukuu Kardinali Pengo atafanya ibada katika Kanisa la Mtakatifu Joseph na Nzigilwa atakuwa St Peters," amesema.

Breaking News: TTCL Makao Makuu Wanatoa Ufafazi Kuhusu Kauli ya Rais Magufuli

$
0
0
Kufuatia kauli ya Rais Magufuli kutaka kuchunguzwa kwa kampuni ya simu ya Airtel kuwa ni mali ya kampuni ya simu ya TTCL, kampuni hiyo ya TTCL leo inatoa ufafanuzi juu ya swala hilo.

==>Tazama apo chini

Walichojadili Zitto Kabwe na Freeman Mbowe baada ya kukutana leo.

$
0
0
Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo na Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe amekutana na Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe kwa ajili ya kujadili masuala ya uchaguzi wa haki nchini baada ya vyama hivyo kutangaza kutoshiriki uchaguzi wa marudio.

Leo December 21, 2107 Zitto amekutana na Mbowe ikiwa ni siku chache baada ya kutoa taarifa kwamba watavizungukia vyama vyote vya siasa ili kujadilia masuala ya uchaguzi.

Kwa mujibu wa Afisa Habari wa chama hicho, Abdallah Hamis kikao cha chama hicho kilichoketi hivi karibuni na kuamua kugomea kushiriki uchaguzi wa marudio katika Kata na Majimbo mbalimbali nchini unaotarajiwa kufanyika mapema mwakani.

“Kamati Kuu ya ACT iliuagiza Uongozi wa Taifa wa Chama kuwafikia wadau wote wa Demokrasia nchini na kuweka mikakati ya pamoja ya hatua za ziada za kuchukua ili kuboresha mazingira ya chaguzi za haki nchini kwetu, kwa kuanzisha mazungumzo na vyama vyote vya Upinzani.

“Lengo ni kuona njia bora zaidi ya mapambano ya pamoja ya kukabiliana na vitendo vya chama tawala za kuvuruga chaguzi huru na za haki nchini,” – Abdallah

Zitto ameanza mazungumzo hayo na Mbowe, wakati Katibu Mkuu wa chama hicho, Dorothy Semu, akiwa anaendelea na utaratibu rasmi wa kulitekeleza suala hilo.

“Nilipewa wajibu wa kuanzisha mazungumzo ya Viongozi wa Juu wa vyama, jana nimezungumza na Mwenyekiti wa Taifa wa NCCR Mageuzi, ndugu James Mbatia aliyeko hospitalini KCMC baada ya hapo nimekutana na Mbowe na kujadili kuhusu mazingira ya chaguzi za haki nchini,”– Zitto

Aidha Zitto amesema mazungumzo na viongozi hao yameenda vizuri.

'Selfie' yamponza mbunge wa CHADEMA

$
0
0
Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro Urich Matei ameweka wazi sababu za kukamatwa kwa mbunge wa Kilombero kwa tiketi ya CHADEMA, Peter Lijualikali, mara tu baada ya kuachiwa leo na polisi ambapo alikuwa rumande.

Kamanda Matei amesema sababu iliyopelekea mbunge huyo kukamatwa tena leo hii ni picha aliyopiga na kuposti mtandaoni huku ikimuonesha akiwa na Afisa mmoja wa Polisi

"Kuna picha alipiga na ofisa mmoja akaiweka mtandaoni, sasa unajua haya masuala ya mitandao unapoweka picha ya mtu, na mwenyewe amekiri kweli ni yake na yeye ndiye ameposti, sasa bado tupo naye kwa mahojiano zaidi", amesema Kamanda Matei.

Leo asubuhi mbunge huyo alikamatwa na polisi muda mfupi baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro kuahirisha kesi inayomkabili.

Waziri Mkuu Majaliwa Azindua Mpango wa Pili Jumuishi wa Huduma za Kifedha.....Asema bado kuna fursa nyingi za kukuza uchumi

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema uwepo wa uchumi imara na unaokua kwa kasi ni miongoni mwa vigezo vinavyochangia ukuaji wa haraka wa sekta ya fedha nchini.
 
Ametoa kauli hiyo leo mchana (Alhamisi, Desemba 21, 2017) wakati akizindua Mpango wa Pili wa Taifa wa Huduma Jumuishi za Kifedha katika ukumbi wa Benki Kuu jijini Dar es Salaam.

Akizindua mpango huo unaotarajiwa kutekelezwa kuanzia mwaka 2018 hadi 2022, Waziri Mkuu alisema uwepo wa miundombinu muhimu iliyojengwa na inayojengwa na Serikali; na sekta binafsi katika maeneo mbalimbali yakiwemo ya vijijini; na ongezeko la watumiaji wa mitandao ya simu na huduma za mawasiliano ni kati ya fursa nzuri iliyotajwa kwenye mpango huo.

“Kati ya fursa nzuri iliyotajwa kwenye mpango huo ni uwepo wa uchumi imara na unaokua kwa kasi. Tukijenga vizuri juu ya misingi hii tunaweza kupiga haraka hatua za maendeleo katika sekta ya fedha na uchumi kwa ujumla wake,” alisema.

Alisema ameupitia mpango huo na kubaini kuwa umeainisha changamoto mbalimbali zinazoikabili nchi hii katika harakati zake za kuongeza matumizi ya huduma za kifedha. Hata hivyo, Waziri Mkuu alikiri kuwa mpango huo umeainisha fursa ambazo zinaweza kutumika ili kukabiliana na changamoto hizo na hatimaye kuongeza matumizi ya huduma za kifedha.

“Changamoto zilizoainishwa ni pamoja na kuimarisha utawala wa matumizi ya fedha taslimu kwa ajili ya malipo badala ya matumizi ya mifumo ya kielektroniki ya malipo; kukosekana kwa utambulisho wa kipekee (unique identification) kwa Watanzania walio wengi; uhalifu kwa njia za mtandao (cyber-crime); kukosekana kwa mifumo madhubuti ya taarifa za kutosha za watumiaji wa huduma za fedha na dhamana zao; na uelewa mdogo wa masuala ya kifedha,” alisema.

Aliwataka wajumbe wa Baraza la Taifa la Huduma Jumuishi za kifedha waaandae mpango mahsusi wa kutoa elimu vijijini kuhusu faida na umuhimu wa huduma jumuishi za kifedha Tanzania, na akasisitiza kuwa kipaumbele kitolewe kwa makundi maalum ya vijana na wanawake.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu alisema wataalam wa uchumi duniani wanaeleza kwamba jamii ambayo imejijengea utamaduni wa kujiwekea akiba katika asasi za kifedha ina fursa kubwa ya kupata maendeleo endelevu na ya haraka.

“Hii ni kwa sababu uwekaji akiba ndiyo kiini na nguzo ya uwekezaji wa miradi ya maendeleo, na bila uwekezaji wa miradi ya maendeleo, hakuna maendeleo. Nchi zote zilizoendelea zimejijengea utamaduni huu wa wananchi wake wa kujiwekea akiba,” alisisitiza.

Alitoa wito kwa wajumbe hao kuhakikisha kuwa mpango huo unajikita zaidi katika kuimarisha utamaduni wa Watanzania kujiwekea akiba kwa kila aina ya mapato ambayo mwananchi anapata, iwe katika kilimo au biashara au ufugaji au uvuvi au shughuli nyingine yeyote anayofanya ya maendeleo.

“Taarifa ya Mpango wa Pili wa Huduma Jumuishi za Kifedha inaonyesha kuwa asilimia kubwa ya Watanzania (watu wazima) wanamiliki simu za mkononi na wanatumia simu hizo kufanya miamala ya kifedha. Kwa msingi huo, nashauri kuwepo kwa ushirikiano wa karibu baina ya wadau wa taasisi za fedha na wadau wa TEHAMA ili kuimarisha matumizi na mtandao wa kifedha vijijini ili iwe kichocheo cha uchumi,” alisema.

Mapema, Gavana wa Benki Kuu, Prof. Benno Ndulu alisema matokeo ya tathmini iliyofanyika yanaonyesha kwamba wananchi walio karibu na huduma za fedha wameongezeka kufikia asilimia 86 mwaka 2017 ya Watanzania (watu wazima) ikilinganishwa na asilimia 29 ya mwaka 2012.

Pia alisema Watanzania wanaotumia huduma za fedha hasa kupitia asasi za kifedha na mitandao ya simu wameongezeka kutoka asilimia 17 mwaka 2009 hadi asilimia 11 mwaka 2006, na hadi sasa (2017) takwimu zinaonyesha kwamba wananchi asilimia 65 wanatumia huduma za kifedha nchini.

“Kutokana na mafanikio haya makubwa, Tanzania imekuwa nchi ya kwanza barani Afrika na ya sita duniani kwa kuweka mazingira bora ya utoaji na upatikanaji wa huduma za kifedha kwa wananchi,” alisema.

Naye Mwenyekiti wa Jumuiya ya Mabenki Tanzania ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya CRDB, Dk, Charles Kimei alisema wenye mabenki wana haja ya kubadili mtazamo na kujikita kwenye ngazi ya chini ambako kuna watumiaji wengi zaidi.

“Wenye kampuni za simu wameonyesha kuwa inawezekana kufikisha huduma kwa watu wa chini kupitia simu zao, nasi tukitumia vifaa hivyo tunaweza kuwafikia wananchi wengi kwa kuwapa huduma zetu,” alisema.

Alitumia fursa hiyo kuwaomba viongozi wa ngazi zote wakiwemo wa mikoa, wilaya na wabunge walifanye suala la uwekaji akiba liwe ajenda kuu ya mikutano yao kwa kuwaelezea wananchi umuhimu wa suala hilo.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
ALHAMISI, DESEMBA 21, 2017   

Sugu Awapiga Mkwara CCM

$
0
0
Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi maarufu kama Sugu amefunguka na kusema kuwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) hawawezi kulikomboa jimbo la Mbeya Mjini hata kwa mabavu kwani anasema watu wa Mbeya hawajaribiwI hata Kikwete na Magufuli wanatambua hilo.

Sugu amesema hayo alipokuwa akihojiwa na MCL na kudai kuwa amesikia CCM wanasema wanataka kukomboa jimbo la Mbeya Mjini na kudai kuwa hawataweza kwa kuwa hata wao CHADEMA hawajalala.

"Wananchi bado wanaridhika na sisi kwa hiyo njia pekee watakayofanya labda watumie mabavu na kwa kutumia mabavu CCM Mbeya wanajua, Kikwete anajua, Magufuli anajua kwamba kwa mabavu kwa Mbeya uwezo huo hawana kwa sababu watu wa Mbeya hawajaribiwi na hilo tunalithibitisha hata kwenye Kata ya Ibighi wameleta mchezo mchezo wao kote walikoleta kwenye kata 42 lakini walipofika Ibighi tuliwapiga 'Stop' tukawathibiti" alisema Sugu

Sugu aliendelea kusema kuwa "Kama kwenye uchaguzi mdogo wa Ibighi ambao kulikuwa na resources zote za mkoa ziliwepo pale na wakashindwa kutumia mabavu watawezaje kwenye uchaguzi mkuu ambao resources zinakuwa mbalimbali, majimbo yanakuwa saba huko kote hao polisi wa kuwapeleka hawana kama ambavyo waliweza kukusanya polisi wa mkoa mzima kuwapeleka kwenye Kata ya Ibighi na bado wakashindwa" alisisitiza Sugu

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Ijumaa ya Disemba 22


Waziri Lukuvi amaliza mgogoro wa ardhi Vingunguti

$
0
0
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mheshimiwa William Lukuvi ameumaliza mgogoro wa ardhi wa muda mrefu kati ya wakazi wa Mtaa wa Mtambani Vingunguti na mwekezaji wa kampuni ya PMM jijini Dar es salaam.

Mwekezaji huyo wa Kampuni ya PMM inayojihusisha na uhifadhi wa mizigo alitaka kuchukua eneo la hekari 228 lenye nyumba 4,000 na wakazi 70,000 wa Mtaa wa Mtambani Vingunguti.

Waziri Lukuvi amesema Serikali haitambui uwekezaji uliokuwa ufanyike na kwamba, mwekezaji hakufuata utaratibu uliyowekwa na Serikali, hivyo kusababisha mgogoro huo kuwa mkubwa.

Kwa mujibu wa wananchi wa eneo hilo tangu mwaka 2012 mwekezaji huyo aliwazuia kufanya shughuli zozote za uendelezaji kwa kile alichodai ameshafanya tathmini na anaisubiri Wizara ya Ardhi ambayo inamchelewesha, jambo ambalo Waziri Lukuvi amekanusha.

Mwekezaji huyo ametakiwa kurejesha nyaraka alizozichukua kwa wananchi hao kinyume na utaratibu na ametakiwa kuwalipa fidia wananchi kwakuwa aliwazuia wakazi hao kufanya shughuli zozote za uendelezaji kwa kile alichodai ameshafanya tathmini. Hata hivyo, hadi sasa hakuna kinachoendelea na malipo hayajafanyika.

Waziri lukuvi aliwaambia wananchi hao kuwa kuanzia leo haya maeneo ni mali ya wananchi kama anataka kununua aanze upya kufuata utaratibu uliowekwa, na haiwezekani mtu anakuja kuwanunua watu 70,000 kienyeji.

“Hatuzuii mtu kuuza mali yake, tunachosimamia sisi ni haki itendeke na utaratibu ufuatwe, lakini katika mchakato huu mambo yamekwenda ndivyo sivyo,” amesema Waziri Lukuvi.

Kwa upande wa meneja wa mradi wa PPM Bwana Deogratius Chacha amesema wapo katika hatua za mwisho na malipo yangefanyika ndani ya siku 90 zijazo ambapo wananchi hao hawakukubaliana na hilo.

Wakazi wa eneo hilo wamemwambia waziri Lukuvi kuwa mwekezaji amechukua pia leseni zao za makazi kwa muda mrefu na kushindwa kuendeleza makazi yao. Hata hivyo, hadi sasa hakuna kinachoendelea na malipo hayajafanyika zaidi ya ahadi na kwamba anasema Wizara ya Ardhi ndio inayomchelewesha.

Kauli hiyo imemfanya waziri Lukuvi kutoa agizo kwa meneja huyo kuwarudishia nyaraka zao wakazi wote hadi ifikapo kesho saa tano asubuhi. “OCD chukua vielelezo vya meneja, hakikisha hadi kufikia kesho saa tano awe amewarudishia wananchi nyaraka zao, kinyume cha hapo mkamate mweke ndani,” amesema waziri Lukuvi.

Na Hassan Mabuye, Wizara ya Ardhi

Dr.kigwangalla ateua wajumbe wengine kamati ya urithi wa tanzania

$
0
0
Waziri wa Maliasili na Utalii  Dk.Hamisi Kigwangalla   jan Desemba 21, 2017 aliteua majina mengine ya Kamati ya Kitaifa ya kuandaa mwezi maalum wa maadhimisho ya Urithi wa Tanzania.

Makamu wa Rais Azindua Kampeni ya Kuifanya Dodoma Kuwa ya Kijani

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ameagiza kuwa kampeni ya kupanda na ustawishaji miti isiishie Dodoma mjini tu bali ienee katika Wilaya zote za mkoa wa huo na hatimaye nchi nzima.

Makamu wa Rais aliyasema hayo kwenye uzinduzi wa kampeni ya kuufanya mji wa Dodoma kuwa wa kijani.

Makamu wa Rais alisema upandaji miti si kwa ajili ya kuhifadhi mazingira tu bali ni fursa ya kiuchumi, kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi ambapo alitolea mfano mti mmoja uliokomaa unaweza kunyonya hadi kiasi cha kilo 150 za gesi ya hewa ya ukaa kwa mwaka,husaidia kupunguza joto, kusaidia kuboresha afya zetu za mwili na akili kama tafiti zinavyoonyesha .

“Ni dhahiri, kampeni hii ya kuifanya mji wa Dodoma kuwa wa kijani ni kuunga mkono uamuzi wa Rais wetu, Dkt. John Pombe Magufuli wa kuhamishia Makamo Makuu ya Nchi kutoka Dar es Salaam kuja Dodoma kwa vitendo.” alisema Makamu wa Rais.

Makamu wa Rais amewataka Viongozi na Wana Dodoma kuipokea kampeni hii kwa mikono miwili na kutoa kila aina ya ushirikiano ili kufikia lengo zuri lililokusudiwa.

Makamu wa Rais ambaye alihamia rasmi mjini Dodoma siku ya ijumaa tarehe 15 Desemba, 2017 alitoa pongezi kwa Waziri wa Nchi ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba na Ofisi yake kwa kuja na wazo zuri .

Makamu wa Rais alisisitiza kuwa hategemei kuona zoezi la upandaji miti lianze na kuisha leo, na badala yake liwe la kudumu, pia alizitaka manisapaa zitunge sheria ndogo zitakazoelekeza shule, chuo, taasisi na familia kuanzisha bustani ndogo za miti zitakayomudu mazingira husika,Makamu wa Rais aliendelea kusema kuwa ni vyema kupunguza ukataji wa miti kiholela ambapo alizitaka sheria, kanuni na taratibu zizingatiwe kabla ya kukata miti na kusema tupande miti kabla ya kukata mti.

Makamu wa Rais alimalizia kwa kutoa shukrani kwa kampuni ya TATU Mzuka kwa kujitoa na kuhakikisha kampeni hii inatekelezwa na kutoa wito kwa Bodi ya Bahati Nasibu ya Taifa ya Tanzania iige mfano na kuelekeza makampuni mengine ya bahati nasibu yaweze kutoa mchango wake katika shughuli za kijamii hususan kwenye suala la hifadhi ya mazingira.

Pia Makamu wa Rais alitoa shukrani kwa Jeshi la Kujenga Taifa Makotopora, DUWASA, Magereza na Tanzania Forest Services (TFS) kwa kujitoa na kushiriki kikamilifu kwenye zoezi hili.
 
Mwisho, Makamu wa Rais aliwataka Wanawake wa mkoa wa Dodoma kuanzisha vikundi mbali mbali vya upandaji.

Sakata la Airtel: TTCL Yamwaga Mboga.....Yasimulia Masaa 24 Yalivyotumika Kuwaliza Watanzania

$
0
0
IKIWA imepita siku moja tangu Rais John Magufuli amwagize Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango, kuchunguza undani wa suala la umiliki wa kampuni ya simu ya Airtel, siri zaidi kuhusiana na kile kilichofanyika katika ‘dili’ za mauziano zimeanza kuanikwa.

Akizungumza mjini Dodoma juzi, Rais Magufuli alimtaka Dk. Mpango kuchunguza  undani wa kampuni ya Airtel baada ya kuwapo kwa taarifa kuwa kampuni hiyo inapaswa kuwa chini ya umiliki wa Kampuni ya Simu (TTCL),  ambayo ni ya serikali. Pia Rais Magufuli alieleza wazi kuwa kuna ‘mchezo mchafu’ uliofanywa na baadhi ya watu katika suala hilo.

Kutokana na agizo hilo la Rais Magufuli, jana, TTCL, kupitia kwa mwenyekiti wake wa sasa wa bodi ya wakurugenzi, Omar Nundu, na Ofisa Mtendaji Mkuu, Waziri Kindamba, iliibuka na kuanika undani wa mambo kadhaa kuhusiana na kampuni hiyo, mojawapo ikiwa namna vigogo watano walivyoketi kwa siku moja na kufanya uamuzi unaoibua maswali mengi kwa sasa kuhusiana na umiliki wa kampuni ya Airtel. Kimahesabu, siku moja ina saa 24.

Alipoulizwa jana kuhusiana na suala hilo linaloambatana na madai kwamba TTCL ndiyo inayoimiliki Airtel Tanzania, Meneja Uhusiano wa kampuni hiyo, Jackoson Mbando, alisema jambo hilo hawawezi kulizungumzia kama watendaji bali wamiliki wa hisa walio nje ya nchi ndio wenye wajibu huo.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Nundu alisema  chanzo cha yote kilianzia Agosti 5, 2005, wakati aliyekuwa Mwenyekiti wa Bodi za TTCL na Celtel wakati huo na wajumbe watano ambao majina yao hakuwa tayari kuyataja, walipokutana siku hiyo moja na kubariki uamuzi mzito uliofikisha jambo hilo lilipo sasa.

Nundu alisema bodi hiyo ilikuwa na watu tisa, lakini siku hiyo moja waliketi watano kati yao na kufanya uamuzi huo mazito huku wakiongozwa na mwenyekiti ambaye wakati huo alikuwa amekabidhiwa asilimia moja ya hisa zilizokuwa zikimilikiwa na ‘mtu asiyejulikana’.

Nundu alisema Celnet ilianzishwa na TTCL Mei 7, 2001 kwa mtaji wa Sh. bilioni moja na thamani ya hisa ikiwa Sh. milioni moja.

Alibainisha kuwa TTCL ilikuwa ikimiliki hisa moja huku thamani ya hisa ilikuwa Sh. 1,000 na mtu asiyejulikana alikuwa akimiliki hisa moja yenye thamani pia ya Sh. 1,000, kuanza baishara kwa jina la Celtel.

Hata hivyo, Nundu alisema hisa moja ya mtu asiyejulikana ikashikiliwa na raia wa kigeni na kwamba baadaye, TTCL ilitoa bilioni tano kwa ajili ya mtaji ili kampuni ianze kufanya kazi.

"Ilianzishwa kampuni inaitwa Celnet…imeanzishwa na TTCL,…ikapewa masafa megawati 900. Ilipofika wakati wa kufanya kazi, ikabadilishwa na kuwa Celtel, kampuni hii ilianzishwa na TTCL Mei 7, 2007 mtaji wake ukiwa Sh. bilioni moja, maana yake hisa milioni moja na kila hisa ina thamani Sh. 1,000,” alisema Nundu.

“Lakini wanahisa wakawa wawili, TTCL yenyewe ikachukua hisa moja, mtu asiyejulikana akachukua hisa moja, lakini akaishika raia wa kigeni. Kwa maana hiyo, kampuni ikaanzishwa kwa fedha Sh. 2,000," alisema Nundu.

Aidha, Nundu alisema TTCL ilitoa pia fedha zaidi ya Sh. bilioni 82 kwa ajili ya biashara huku cha kushangaza, mtu asiyejulikana akiwa hajatoa kitu chochote.  

"Kama si TTCL kutoa Sh. bilioni tano,  hakuna ambacho kingefanyika. Hakukuwa  na uhitaji wa mwekezaji…. isitoshe TTCL iliweka Sh. bilioni 82 na ushee kuikopesha Celtel…sasa hapo unaona ni kampuni ya TTCL," alisema Nundu.

Alisema baadaye, raia wa kigeni aliyekuwa akishikilia hisa moja ya mtu asiyejulikana aliikabidhi kwa Mtanzania ambaye alikuwa miongoni mwa wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya TTCL na pia Celtel. 

“Siku ya kikao hicho, mwenyekiti wa bodi (ambaye ndiye aliyekabidhiwa hisa hiyo moja ya mtu asiyejulikana) na wajumbe wengine watano walifanya maamuzi (uamuzi) magumu (mgumu) ya kuirudisha hisa hiyo moja na kuikabidhi TTCL, hivyo TTCL ikawa inamiliki Celtel kwa hisa zote kwa asilimia 100,” alisema.

Akieleza zaidi kuhusiana na ‘mchezo’ uliofanyika, Nundu alisema thamani ya hisa asilimia 100 za TTCL ilikuwa Sh. bilioni moja, lakini wakakubaliana siku hiyo kuongeza thamani ya hisa hizo hadi kufikia Sh. bilioni 50 katika kampuni ya Celtel.

Alisema mpaka Mei 7, 2001, hisa 999,998 zisizo na mtu ilipewa TTCL kwa sababu ilishaweka Sh. bilioni tano, hivyo kuwa na jumla ya hisa 999,999 huku mtu asiyejulikana akiwa bado anamiliki hisa moja.

Nundu alisema ilipofika Novemba 27, 2001, raia wa kigeni aliyeshikilia hisa ya mtu asiyejulikana alimpa mtu mwingine ashikilie ambaye ni Mtanzania, na mtu huyo aliyepewa ashikilie ndiye aliyekuwa mwenyeki wa bodi ya TTCL na Celtel.

Nundu aliongeza kuwa baada ya hapo, zilichukuliwa Sh. bilioni 40 za TTCL na kuwekwa katika mfuko wa Celtel kama mtaji wake, hivyo kuifanya kumilikiwa kwa asilimia 100 kwa mtaji wa Sh. bilioni 41, huku Sh. bilioni tisa zikiwa hazina mmiliki.

“Siku hiyo hiyo moja, baada ya muda TTCL ikanyang’anywa hisa zake zote  na hapo ndipo tunapojiuliza uhalali wa Celtel,” alisema Nundu.

Nundu alisema kama  hiyo haitoshi, hisa hizo zilianza kugawanywa kwa watu ambao hawapo katika mlolongo wa Celtel kutokana na ukweli kuwa wakati huo,  waliokuwa wakitambulika ni wawili tu, yaani TTCL na ‘mtu asiyejulikana’.

Aidha, alisema ilikubaliwa kuwa serikali ipewe asilimia 65 na ‘mtu asiyejulikana’ apewe asimilia 35.Alisema kwa hesabu za kawaida, haikupaswa watu wengine kugaiwa hisa kwa sababu hawakuwa na hisa tangu awali lakini wakapewa hisa zote.

Alisema kama haitoshi, siku hiyo hiyo ya kikao cha bodi yenye watu watano, serikali ikapewa hisa milioni 26.650, ikiwa ni uwiano wa asilimia 65 ya umiliki na mwingine (mtu asiyejulikana) alipewa hisa milioni 14.350, sawa na asilimia 35.

Baada ya hapo, alisema serikali ilichukua tena hisa milioni 10 zingine na kumpa mwekezaji, hivyo kumfanya afikishe milioni 24.350 na kuifanya serikali kubakiwa na hisa milioni 16.650.

Alisema uwiano huo ndio unaoendelea hadi leo na kwamba umiliki wa Celtel upo mikononi mwa Airtel ‘kimagumashi’ (kijanjaujanja).

Kadhalika, Nundu alisema jambo la kushangaza ni kwamba ilipofika Juni 23, mwaka jana, Airtel ilitangaza kujitoa kwenye umiliki wa TTCL ambao walikuwa wamiliki na wameshajitoa.

Nundu alisema baada ya kufanyika ‘mchezo’ huo,  TTCL ilikopeshwa dola za Marekani milioni 28 na kuwekewa riba ya asilimia 18 na kusababisha deni kukua hadi kufikia Sh. bilioni 76.6.

“Mimi na wenzangu baada ya kuja TTCL, ndiyo tukaanza kuchimba chimba ili kujua mbivu na mbichi kwa sababu kuna mambo mazito zaidi,” alisema.

Bosi TTCL Ajilipua
Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Waziri Kindamba, alisema wanachotaka kutoka kwa Airtel ni kampuni yao.

Alisema wanaamini na kutarajia kuwa watarejeshewa kampuni yao bila kukwaruzana na wamikili wa kampuni ya Airtel na kwamba wamejipanga kwa ushahidi wa asilimia 100.

“Tumeamua kujitoa sadaka za nafsi na miili yetu kwa ajili ya kutetea wanyonge katika vita hii kubwa ya uchumi inayoongozwa na Rais Magufuli,” alisema Kindamba.

Pia alisema wanatarajia kufanya biashara ya huduma za simu kwa gharama nafuu zaidi watakaporejeshewa kampuni yao na pia kuiwezesha kulipa kodi zaidi serikalini

Times Radio FM yakanusha kusambaza taarifa inayomuhusu Benard Membe

Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images