Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Mh. Rais Kikwete Aalikwa Nigeria na Rais Jonathan

$
0
0
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mazungumzo na Rais Goodluck Jonathan wa Nigeria wakati viongozi hao wawili walipokutana na kufanya mazungumzo Alhamisi, Januari 23, 2014, kwenye Hoteli ya Intercontinental, Davos, Uswisi, ambako  walikuwa wakihudhuria  Mkutano wa Mwaka huu wa Taasisi ya Uchumi Duniani –WEF.   (PICHA NA IKULU) RAIS KIKWETE AALIKWA NIGERIA NA RAIS JONATHAN

Ajabu,,,,,, Wakati Mafuriko yanaendelea Dumila, Mke wa Mtu Afumaniwa Akisaliti Ndoa Yake Guest House

$
0
0
   Jambo limezua jambo! Mvua zilizonyesha na kusababisha mafuriko maeneo ya Dumila mkoani hapa, zimemuumbua mke wa mtu ambaye jina lake halikupatikana, akiwa anasaliti ndoa gesti. Mafuriko hayo yalisababishwa na mvua kubwa zilizoanza kunyesha Jumatano iliyopita na kusababisha maafa makubwa yakiwamo kuharibiwa kwa makazi ya watu, majengo ya serikali zikiwamo shule, vyuo na mahakama.

Slaa; 2015 Maamuzi Magumu na Makini ni muhimu kwa maslahi ya Watanzania

$
0
0
 KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Wilbrod Slaa, amesema ili nchi iondokane na hali ya umaskini, wananchi wanatakiwa kufanya uamuzi mgumu wa kutoirudisha CCM madarakani, katika uchaguzi mkuu ujao, utakaofanyika mwakani.Dk. Slaa alisema misingi mibovu ya CCM ndiyo sababu ya nchi kuyumba na kwamba hali hiyo imechangia Tanzania kuwa ya pili kutoka mwisho kwa

Rais Obama amwalika Rais JK Kwenye Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika

$
0
0
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI Rais wa Marekani Mheshimiwa Barack Obama amemwalika Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete kuhudhuria Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika ambao anauandaa katika mji mkuu wa Marekani, Washington baadaye mwaka huu.Mkuu wa Shirika la Misaada ya Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID), Bwana Rajiv Shah amewasilisha mwaliko

Chama Cha Mapinduzi Bukoba Mjini Chatoa Tamko Juu ya Ripoti ya CAG

$
0
0
TAMKO LA CHAMA CHA MAPINDUZI WILAYA BUKOBA MJINI TAREHE 24/01/2014 KWA  VYOMBO VYA HABARI Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Bukoba Mjini kupitia kikao chake cha kawaida cha Kamati ya Siasa ya H/Kuu ya Wilaya iliyoketi leo tarehe 24/01/2014.Kimepokea na kujadili taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (GAG) kuhusu Ukaguzi maalum uliofanyika katika Halmashauri ya Manispaa

Ukatili Jamani..... Mwalimu Mkuu Atuhumiwa Kumlawiti Mtoto Yatima na Kumsababishia Kushindwa Kuendelea Na Masomo

$
0
0
MWANAFUNZI mmoja (Jina limehifadhiwa) wa Darasa la Saba katika  Shule ya Msingi Mkombozi iliyopo katika mji mdogo Mbalizi Wilaya ya Mbeya Mkoani hapa ameshindwa kuendelea na masomo tangu shule zifunguliwe akiogopa kuzomewa na wenzie baada ya kuhisiwa kulawitiwa na Mwalimu Mkuu wake.Hatua ya mwanafunzi huyo kushindwa kufika shuleni kuungana na wenzie kumetokana na madai ya kuzagaa kwa

Baba Mzazi Aamua Kumshtaki Mwanawe kwa Kosa la Kuoa Mwanamke Masikini

$
0
0
PATNA, India -- MWANAMUME nchini India amemshtaki mwanawe wa pekee wa kiume katika mahakama kwa kumharibia sifa, alipoamua kumuoa mwanamke wa tabaka la chini. Alisema kwamba kitendo hicho kimemharibia sifa na hadhi yake katika jamii.Mzee Sidhnath Sharma anataka alipwe rupia 10,000,000 (KSh13,638,900) na mwanawe Sushant Jasu, na anataka mahakama iamuru kwamba kijana huyo asitumie tena

Waliofeli kidato cha pili watarudia darasa

$
0
0
IMEELEZWA kuwa, licha ya matokeo ya kidato cha pili kutolewa `kimyakimya’ kupitia ofisi za Elimu za Kanda na kubandikwa shuleni, hatua hiyo haimaanishi kuwa waliofeli wamenusurika kutorudia darasa.   Hayo yameelezwa na Msemaji wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Ntambi Bunyazu alipozungumza na gazeti la Habari leo  jana.   Alisema kwa sasa Wizara inaendelea kujumuisha matokeo hayo

Picha za Rais Kikwete alivyoongoza mazishi ya aliyekuwa mbunge wa Chalinze Ramadhan Bwanamdogo

$
0
0
 Rais Kikwete alivyoongoza mazishi ya aliyekuwa mbunge wa Chalinze Ramadhan Bwanamdogo   Rais Jakaya Kikwete akiweka udongo katika kaburi la aliyekuwa Mbunge wa Chalinze kwa tiketi ya CCM Ramadhan Bwanamdogo aliyefariki dunia juzi. Maziko ya marehemu Bwanamdogo, yamefanyika kijijini kwake Chalinze Mion, wilaya ya Bagamoyo.    Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa

Freeman Mbowe anusurika kufa jijini Mwanza

$
0
0
Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe, amenusurika kifo baada ya gari alilokuwa akisafiria kutoka jijini Mwanza kwenda wilayani Ngara, Kagera kupata ajali.   Ajali hiyo ilitokea jana saa 6 mchana, umbali wa kilometa mbili kutoka Kata ya Katoro, Geita na inadaiwa kuwa gari alilokuwa akitumia limeharibika sehemu ya mbele.   Taarifa za uhakika kutoka eneo la tukio

Waziri wa Fedha akiri serikali kuwa katika hali ngumu kifedha....

$
0
0
Waziri wa Fedha, Saada Mkuya amekiri Serikali kuwa katika hali ngumu, lakini akasema kuwa mkakati uliopo ni kudhibiti matumizi ili yaendane na fedha iliyopo.    Waziri Saada alisema hayo kwa njia ya simu, alipotakiwa na Mwananchi  kujibu madai ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG) juu ya kauli yake ya hivi karibuni aliyoitoa katika mkutano mjini Dodoma.  

Mchungaji Mtikila kufungua kesi kupinga kuendelea kwa mchakato wa mabadiliko ya Katiba Mpya.

$
0
0
Mwenyekiti wa Chama cha Demokratic (DP), Mchungaji Christopher Mtikila anatarajia kufungua kesi Mahakama Kuu ya Tanzania kupinga kuendelea kwa mchakato wa mabadiliko ya Katiba Mpya.    Mchungaji Mtikila akizungumza na Mwananchi alisema, madhumuni ya kufungua kesi hiyo ni mchakato huo kukiuka hatua mbalimbali muhimu wakati wa kuiandaa ikiwamo kutoa elimu kwa wananchi kipi wanatakiwa

Wanafunzi wa sekondari ya wasichana iliyopo wilayani Bagamoyo mkoani Pwani wadaiwa kujihusisha na mapenzi ya jinsia moja ( Usagaji )

$
0
0
Picha  ya  mtandao ** Shule moja ya sekondari ya wasichana iliyopo wilayani Bagamoyo mkoani Pwani,  imelalamikiwa na wanafunzi pamoja na wazazi kuwa mabinti wanajihusisha na vitendo vya ngono vya jinsia moja (usagaji). Akizungumza na NIPASHE mmoja wa wazazi (jina linahifadhiwa)  alisema shule hiyo imepoteza sifa kwa kuwa kuna wimbi kubwa la wanafunzi wanaojihusisha na vitendo hivyo vya

Profesa Mwesiga Baregu afichua siri ya kutwangana ngumi na kusalitiana ndani ya CHADEMA

$
0
0
MJUMBE wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Profesa Mwesiga Baregu, amefichua siri ya madai ya usaliti ndani ya chama hicho. Akizungumza na Mtanzania katika mahojiano maalumu yaliyofanyika jijini Dar es Salaam wiki hii, Profesa Baregu alisema kiini cha tuhuma na madai ya usaliti ndani ya Chadema ni kutoaminiana na kukosekana kwa uvumilivu.  Alisema kitendo cha

Serikali ya Tanzania yaiomba Uingereza msaada wa mabehewa na injini za treni ambazo haizitumii lakini ni nzima.

$
0
0
SERIKALI ya Uingereza inatafakari ombi la Tanzania la mabehewa na injini za treni, ambayo nchi hiyo haizitumii tena, lakini bado ni nzima kwa ajili ya kusaidia kuimarisha usafiri wa reli katika Tanzania na hasa wa Jiji la Dar es Salaam.Ahadi hiyo ya Uingereza ilitolewa na Naibu Waziri Mkuu wa Uingereza, Nick Clegg wakati wa mazungumzo yake na Rais Jakaya Kikwete kwenye hoteli ya

Ufoo Saro wa ITV amwaga machozi kanisani wakati akimshukuru Mwenyezi Mungu kwa kumnusuru alipopigwa Risasi na mchumba wake...

$
0
0
Ufoo saro jana  amefanya ibada na kusema "Namshukuru Mungu kwa kuniponya"... Hiii ni mara ya kwanza kwa Saro kuzungumza tukio hilo tangu aliporuhusiwa kutoka Taasisi ya Mifupa na Mishipa ya Fahamu MOI ya Hospitali ya Taifa Muhimbili alikokuwa amelazwa.   Katika ibada hiyo iliyofanyika katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheli Tanzania (KKKT) Usharika wa Kibamba Jimbo la Magharibi Ufoo

WAZIRI Mkuu, Mizengo Pinda, akiri kwamba Serikali ilifanya uzembe katika kutatua taarifa za uchochezi zilizosababisha vurugu za Mtwara

$
0
0
WAZIRI Mkuu, Mizengo Pinda, amekiri kwamba Serikali ilifanya uzembe katika kutatua taarifa za uchochezi zilizosababisha vurugu za Mtwara. Kauli hiyo aliitoa mjini Mtwara  jana alipozungumza na wananchi wa Masasi akiwa njiani kuelekea wilayani Nanyumbu kufungua mradi wa umeme. Alisema baada ya kutokea kwa uzembe huo wako wajanja wachache waliotumia nafasi hiyo kufanikisha malengo yao.

Tuhuma nzito Baraza la Mawaziri ....Profesa Ibrahim Lipumba atilia shaka elimu ya waziri wa fedha, Waziri naye afunguka kwa kutoa vielelezo lukuki

$
0
0
MWENYEKITI wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, amelishushia tuhuma nzito Baraza la Mawaziri, baada ya kudai baadhi ya mawaziri walioteuliwa hawana elimu ya kutosha. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Profesa Lipumba alisema mmoja wa mawaziri hao ni Waziri wa Fedha, Saada Mkuya. Alisema chama chake, kina wasiwasi na elimu ya Waziri Mkuya,

Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Asha-Rose Migiro aitembelea tume ya mabadiliko ya katiba

$
0
0
Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Asha-Rose Migiro (kushoto) akipokea nakala za ripoti za Tume ya Mabadiliko ya Katiba ikiwemo Rasimu ya Katiba kutoka kwa Mwenyekiti wa Tume hiyo, Jaji Joseph Warioba wakati wa ziara yake ya kutembelea na kuzungumza na Watendaji wa Tume hiyo aliyoifanya mwishoni mwa wiki Jijini Dar es Saalam. Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji Joseph

Tanzania kuisaidia Madagascar kuondolewa vikwazo ilivyowekewa na jumuiya za kimataifa.

$
0
0
  Rais mpya wa Madagascar Hery Rajaonarimampianina akiapishwa rasmi rais wa nchi hiyo mjini Antananarivo kufuatia ushindi mkubwa alioupata katika uchaguzi mkuu uliofanyika nchini humo mwezi Desemba 2013. Rais mpya wa Madagascar Hery Rajaonarimampianina akisani kiapo chake tayari kuanza kazi ya kuwatumikia wananchi wa Madagascar mbele ya Jaji Mkuu wan chi hiyo Jean –Michael
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live


Latest Images