Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Wizara ya Mambo ya Nje yatoa tamko Sakata la Madareva 24 waliotekwa DRC

$
0
0
Juni 29, 2017 madereva 24 wa malori wametekwa na kikundi cha waasi cha Mai Mai nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).

Akizungumzia tukio hilo Msemaji wa Wizara ya mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashairiki, Mindi Kasiga, amesema kuwa madereva hao wametekwa wakiwa wanelekea katika mgodi wa dhahabu wa Namoyo katika jimbo la Mainiema unaomilikiwa na kampuni ya Banro Gold ya Canada.

Amesema kati ya madereva 24 waliotekwa, 21 ni Watanzania na 3 ni Wakenya hivyo Serikali inafanya jitihada za kuwaokoa madevera hao.

Mindi amesema kuwa kwa mujibu wa taarifa kutoka Ubalozi wa Tanzania nchini DRC, madereva hao wametekwa na waasi wa kikundi cha Mai Mai, kilishambulia msafara wa malori hayo uliokuwa ukisindikizwa na askari wa jeshi la DRC (FARDC) na kufanikiwa kupora mali zao zote zikiwemo fedha na kuharibu malori hayo.

Amesema hadi sasa Serikali kupitia Ubalozi wake nchini DRC umechukua hatua kadhaa kuhakikisha madereva hao wanapatikana na wakiwa salama. 

==>Hatua hizo ni;
1.Kuwasilisha  rasmi tukio hili  kwa  serikali ya  DRC  na kuwaomba  wasaidie kuwapata hawa watanzania. 

2.Tumeomba Oparesheni  inayoendelea dhidi ya waasi huko DRC  itambue uwepo wa raia wa tanzania msituni ili wawasaidie haraka

3. Mawasiliano na madereva yanafanyika kujua hali zao

4.Mgodi wa Banro umetoa ushirikiano mkubwa ikiwemo  kuwahamisha kwa muda wafanyakazi wa mgodi huo ikiwemo watanzania had hali itulie

5. Ubalozi unafatilia  maombi ya kukutana na waziri wa ulinzi wa nchi hiyo ili kuomba wasaidie madereva hao wapatikane salama

Mbowe Alaani Wabunge wa CHADEMA Kukamatwa......Aiomba Mahakama Itende Haki

$
0
0
Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Mh. Freeman Mbowe amelaani kitendo cha wabunge 8 wa upinzani kukamatwa na jeshi la polisi kwa madai yakutaka kumpiga mbunge wa CCM Juliana Shonza, na kusema hawajapeleka mabondia bungeni.

Freeman Mbowe aliyasema hayo  jana mjini Dodoma baada ya kutoka mahakamani na kudai kuwa wao wanaamini kuwa mahakama itatenda haki kwa wabunge hao.

"Kama ambavyo mnajua kwa masaa zaidi ya 48 wabunge wa CHADEMA wameshinda polisi, jana siku nzima wameshinda polisi na leo wameshinda polisi mpaka mchana huu.

"Kwa maana hiyo wawakilishi hawa wa wananchi wameshindwa kuwajibika kwa ajili ya wananchi kwa makosa ambayo kimsingi kabisa hayakutakiwa kupewa uzito huu yanaopewa.

"Inasemakana kuwa wabunge hawa walimfanyia fujo Mbunge wa viti maalum (CCM) Juliana Shonza, jambo hili linafedhehesha sana, sisi tuna wabunge ambao wanajiheshimu na kuheshimu sheria za nchi, hatukupeleka wapiganaji bungeni bali tumepeleka viongozi wa kutunga sheria" alisisitiza Freeman Mbowe

Mbali na hilo Mbowe anasema kitendo cha Spika wa Bunge Mh. Job Ndugai kulivalia njuga suala hilo ni jambo ambalo yeye limemsikitisha.

"Kitendo cha kuwapeleka polisi na kuwashtaki wabunge wetu na Spika wa Bunge kushadadia jambo hili limenisikitisha sana

" Spika kusema ametoa ruhusa wahukumiwe kwa kesi za jinai ni mwendelezo wa kutaka kutunyamazisha, ila hatutayumba na tunaamini kuwa jopo la majaji litatenda haki katika jambo hili, maana hakuna mbunge yoyote wa CHADEMA wala UKAWA ambaye amemshambulia mbunge yoyote yule bungeni" alisisitiza Mbowe.

Katika watuhumiwa wote nane, mtuhumiwa mmoja ambaye ni Mbunge wa jimbo la Ubungo, Mbunge Saed Kubenea jana  alipandishwa mahakamani na kushtakiwa kwa kosa moja la shambulio la kawaida hivyo alidhaminiwa na shauri hilo upelelezi wake bado haujakamilika hivyo kesi itatajwa tena tarehe 26, Julai 2017 Dodoma.

Waziri Mkuu: Wanafunzi wenye mimba kutoruhusiwa kurudi shule si jambo jipya

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema msimamo wa Serikali wa kutoruhusu wanafunzi waliopata ujauzito kuendelea na masomo katika mfumo rasmi wa elimu umetolewa kwa mujibu wa Sheria na sio utaratibu mpya kama inavyopotoshwa na baadhi ya wanaharakati.

Waziri Mkuu ametoa ufafanuzi huo jana (Jumatano, Julai 5, 2017) katika hotuba yake ya kuahirisha Mkutano wa Saba wa Bunge mjini Dodoma.

Alisema msimamo huo wa kisheria unalenga kuwafanya watoto wa kike wajishughulishe na masomo yao zaidi badala ya kushiriki kwenye vitendo vya ukiukwaji wa maadili.

Kwa mujibu wa takwimu za mwaka 2015, jumla ya wanafunzi 3,637 waliacha masomo kutokana na kupata ujauzito.

“Kuwaachisha masomo wanafunzi waliopata ujauzito ni utekelezaji wa Waraka na Kanuni za Elimu za mwaka 2002, zinazoruhusu kufukuza na kuondoa wanafunzi shuleni kutokana na makosa mbalimbali ikiwemo uasherati, wizi, ulevi, kutumia dawa za kulevya pamoja na utoro.”

“Lengo hili lina nia ya kuwahimiza wazazi wawafundishe watoto wao mambo mema ndani ya familia na wawakataze kushiriki vitendo vya ngono katika umri dhamira ya Serikali ni kumlinda mtoto wa kike ili apate elimu kwa ajili ya manufaa yake na Taifa kwa ujumla.”

Waziri Mkuu alisema kila Mtanzania ana wajibu wa kuhakikisha kuwa watoto wote wanapata elimu. Hivyo ni lazima tuhakikishe mtoto wa kike anapata elimu stahiki na masomo yake hayakatizwi kwa kupata ujauzito.”

Alisema Serikali imewekeza kwenye mtoto wa kike, ambapo kifungu Na. 60 (b) cha Sheria ya Elimu Sura ya 353, kinatoa adhabu ya miaka 30 jela kwa yeyote atakayeoa au kumpa ujauzito mwanafunzi.

Pia, sheria inatoa adhabu ya kifungo cha miaka mitano jela au faini ya shilingi milioni tano, au vyote kwa pamoja kwa anayeshiriki kumuozesha mtoto wa shule.

“Natoa wito kwa Wakuu wa Wilaya kusimamia utekelezaji wa Sheria za nchi zenye lengo la kumlinda mtoto wa kike. Aidha, nawashauri Waheshimiwa Wabunge, mshirikiane na Halmashauri zenu kuweka mikakati ya kudhibiti ujauzito kwa watoto wa shule.”

Wahamasisheni wananchi watoe ushirikiano kwa vyombo vya dola, ili wanaowapa wanafunzi ujauzito au kuwakatisha masomo ili waozeshwe wapate adhabu stahiki.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU

Mwanamuziki mkongwe wa Msondo Ngoma Shaaban Dede amefariki

$
0
0
Mwanamuziki mkongwe kutoka Msondo Ngoma Music Band, Shaaban Dede amefariki dunia leo saa mbili asubuhi katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili alikokuwa amelazwa kwa matibabu.

Taarifa hizo zimethibitishwa na mtoto wake wa kiume aliyetambulika kwa jina la Hamad Dede na kusema mipango ya mazishi inafanyika nyumbani kwa marehemu Mbagala jijini Dar es salaam, na kwamba ratiba na taratibu zote zitatangazwa mara zitapokamilika kupangwa.

Marehemu Dede atakumbukwa kama mmoja wa wanamuziki nguli kutokea nchini Tanzania kwa uwezo wa kucheza na sauti yake pamoja na kuwa mtunzi mahili wa nyimbo mbalimbali  enzi za uhai wake alipokuwa anaimbia bendi tofauti tofauti ni Jazz, Bima Lee, Tabora Mlimani Park na Msondo Ngoma ambako alikuwa anatumikia hadi mauti yanamkuta.

Kutana Maajabu ya Mtabibu CHIEF SULTAN(MAKATA WA MAKATANI) Mganga wa Waganga Sasa Yupo Mikoa Yote Tanzania

$
0
0
Kutana Maajabu ya Mtabibu CHIEF SULTAN(MAKATA WA MAKATANI) Mganga wa Waganga Sasa Yupo Mikoa Yote Tanzania

Pia anatoa Tiba kwa Njia ya Simu ukiwa popote Pale Tanzania au Nje ya Tanzania..

CHIEF SULTAN ni Mtabibu na Mtafiti wa Dawa za Asili ya Africa, na Duniani Katika utoaji wa Tiba za Asili..
 
Je unasumbulia na Mapenzi..?
(Umeachwa na Umpendae awe Mume/ Mke au mpenzi na Anaishi na Mtu Mwingine na Bado Unampenda?) Umejaribu sehemu Nyingi bila Mafanikio?Wasiliana na CHIEF SULTAN Akusaidie Kumshika Umpendae Asikusaliti(LIMBWATA) Kumtawala Mpenzi wako kwa sababu Maalum..Anauwezo wa Kusambalatisha Mahusiano yao ndani ya siku Moja tu.
Je Unasumbuliwa na Madeni?
Biashara yako Haina wateja?
Unatatizo la kutokushika Mimba na umehangaika sehemu nyingi bila mafanikio?
 
Wasiliana na CHIEF SULTAN Kwa Majibu ya Maswali yako..
Anasafisha NYOTA na Kutoa PETE za BAHATI kuendana na NYOTA yako. UTAJIRI USIO NA MASHARTI.(Magic Wallet_Pochi ya Maajabu Isio Isha Hela)
KUWA MAARUFU na KUJULIKANA
Kupandishwa CHEO na HESHIMA Mahala pa KAZI.
Utapewa Nguvu ya Kujilinda na MALI ZAKO zako na Mwili wako.. Huzuia Chuma Ulete katika Biashara.. Hurudisha MALI zilizo Potea au KUDHULUMIWA..
Mvuto wa Biashara na Mwili wako.
Hutibu kabisa Nguvu za Kiume na Kurefusha Uume kwa saizi Unayotaka.
 
Magonjwa Sugu(Miguu Kufa Ganzi, kisukari, Presha, Pumu nk.)Humaliza Kesi za Muda mrefu ndani ya siku 14 tu.
Anatoa NDAGU Zisizokuwa na Masharti.. Kwa maelezo Zaidi wasilina nae kwa

whatsapp +255 0658 316 976
Call +255 755 911 233

China Yaikingia Kifua Korea Kaskazini.....

$
0
0
Balozi wa China katika Umoja wa Mataifa, Liu Jieyi amesema kwamba suluhu ya nguvu za kijeshi inayotaka kufanywa na Marekani dhidi ya Korea Kaskazini haifai kupewa kipaumbele.

Liu Jieyi amesema hayo katika kikao cha dharura cha baraza la usalama la Umoja wa Mataifa akijibu hatua ya Korea Kaskazini kufanyia majaribio kombora lake la masafa marefu.

Hayo yamejiri baada ya Marekani kutangaza kuwa itatumia nguvu za kijeshi dhidi ya Korea Kaskazini ‘iwapo ni lazima’ kufuatia jaribio la kombora la masafa marefu lilotekelezwa na taifa hilo.

Liu Jieyi alirejelea wito wa China na Urusi kwa mazungumzo ya Korea Kaskazini kusitisha majaribio ya makombora iwapo Marekani na Korea Kusini zitasitisha mazoezi ya pamoja ya kijeshi.

Awali balozi wa Marekani katika Umoja wa mataifa Nikki Haley alisema kuwa vikwazo vya kimataifa vilivyowekewa Pyongyang kwa miaka kadhaa havitoshi.

Amesema kuwa vitendo vya Korea Kaskazini ni ishara za kuzuka kwa mgogoro duniani.

Mahakama ya Rufaa yakubali rufaa ya DPP Dhidi ya Masheikh wa Uamsho

$
0
0
 Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) ameshinda rufaa dhidi ya viongozi wa Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar (Jumiki), Sheikh Farid Hadi Ahmed na wenzake 21 wanaokabiliwa na mashtaka ya ugaidi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

DPP alikata rufaa Mahakama ya Rufaa akipinga uamuzi wa Mahakama Kuu, kuhusu mamlaka ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kusikiliza na kutoa uamuzi wa hoja walizoziibua washtakiwa kupitia kwa mawakili wanaowatetea, baada ya kusomewa mashtaka yanayowakabili.

Siku waliposomewa mashtaka, washtakiwa kupitia mawakili, Juma Nassoro na Abubakar Salim pamoja na mambo mengine walihoji uhalali wa Mahakama ya Kisutu kusikiliza shauri lao, pia waliiomba mahakama iwafutie mashtaka wakidai kulikuwa na kasoro za kisheria.

Mahakama ya Kisutu katika uamuzi wake ilikataa kusikiliza hoja za washtakiwa hao, ikisema haina uwezo wa kisheria kusikiliza hoja zozote kutoka kwao kwa kuwa mashtaka yanayowakabili yanasikilizwa na Mahakama Kuu tu, hivyo ikawaelekeza kuwasilisha hoja hizo Mahakama Kuu.

Washtakiwa hawakuridhika na uamuzi wa Mahakama ya Kisutu, hivyo walifungua maombi ya mapitio Mahakama Kuu, wakiiomba mahakama iitishe na kuchunguza kumbukumbu za mwenendo wa kesi hiyo ili kujiridhisha na uhalali na usahihi wake.

Walidai Mahakama ya Kisutu ina mamlaka ya kusikiliza na kutoa uamuzi wa hoja walizoziibua baada ya kusomewa mashtaka.

Mahakama Kuu katika uamuzi uliotolewa na Jaji Fauz Twaib ilikubali hoja za mawakili wa washtakiwa kuwa Mahakama ya Kisutu ina uwezo wa kusikiliza na kutoa uamuzi wa hoja zao na alielekeza mahakama hiyo kuendelea na usikilizwaji wa uamuzi wa hoja za washtakiwa hao.

DPP hakuridhika na uamuzi huo hivyo alikata rufaa Mahakama ya Rufaa, akipinga uamuzi wa Mahakama Kuu.

Mahakama ya Rufaa katika hukumu iliyoandikwa na Jaji Bethuel Mmila kwa niaba ya wenzake, Jaji Kipenka Mussa na Jaji Rehema Mkuye waliounda jopo lililosikiliza rufaa hiyo, imetengua uamuzi wa Mahakama Kuu.

Hukumu hiyo imesomwa leo  na Naibu Msajili Mwandamizi wa Mahakama ya Rufaa, Phocus Bampikya ikisema Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu haina uwezo wa kusikiliza na kuamua hoja zilizoibuliwa na washtakiwa hao kupitia kwa mawakili wao.

Mahakama ya Rufaa imesema hakuna sharti lolote kisheria linaloipa mamlaka mahakama hiyo kusikiliza na kutoa uamuzi wa hoja hizo na kwamba, mahakama hiyo ina uwezo wa kuwezesha mshtakiwa/washtakiwa kusomewa au kuwezesha kusomewa maelezo ya mashahidi tu kabla ya kwenda kusikilizwa na Mahakama Kuu.

Imesema manufaa ya matakwa hayo ya mahakama kuwezesha mshtakiwa kusomewa maelezo ya mashahidi ni kuwafanya kujua mapema aina ya ushahidi utakaotolewa dhidi yake wakati wa usikilizwaji Mahakama Kuu na watakaotoa ushahidi huo ili kupata nafasi nzuri ya kuandaa utetezi wake.

“Ni mtazamo wetu kwamba mambo/hoja zilizoibuliwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ni za kisheria ambazo Mahakama ya Hakimu Mkazi haina mamlaka kuyaamua. Masuala hayo yanapaswa kusubiri na kuibuliwa Mahakama Kuu wakati wa usikilizwaji wa shauri hilo,” inasema hukumu hiyo.

Mahakama hiyo imeelekeza Mahakama ya Kisutu kuendelea na shauri hilo kuanzia pale lilipokuwa limeishia kabla ya kufunguliwa kwa mapitio Mahakama Kuu.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Ijumaa ya July 7


Hakimu mwingine anayesikiliza ya Lema ajitoa

$
0
0
Hakimu Patricia Kisinda aliyekuwa akisikiliza kesi ya uchochezi inayomkabili Mbunge wa Arusha Mjini kwa tiketi ya CHADEMA, Godbless Lema dhidi ya Rais Dkt Magufuli amejitoa baada ya upande wa Jamhuri kusema kuwa hawana imani naye.

Wakili wa Serikali Sabina Silayo alisema kuwa hawawezi kusoma hoja za awali za kesi hiyo kwani hawana imani na  hakimu huyo kutokana na kuwa na urafiki na mke wa mtuhumiwa, Godbless Lema jambo ambalo linaweza kuathiri mwenendo wa kesi na haki isitendeke.

Licha ya kuwa upande wa utetezi ulilipinga hilo wakisema kuwa haina uzito na kwamba watanzania wote ni marafiki na ndugu, lakini hakimu huyo aliridhia kujiondoa katika kesi hiyo ambayo inatarajiwa kuendelea tena Agosti 8 mwaka huu ambapo hoja za awali zitasomwa huku jalada likipelekwa kwa Hakimu Mfawidhi ili apangiwe hakimu mwingine.

Hakimu huyo ni wa pili kujitoa katika kesi hiyo, kwani Mei 29, Hakimu Mkazi wa Mkoa wa  Arusha, Desderi Kamugisha pia alijitoa kwa maelezo kuwa hawezi kusikiliza kesi zote nne zinazomkabili Lema  hivyo kuwaeleza mahakimu wengine watapangiwa kesi hiyo.

Wakili wa Lema, Shedrack Mfinanga aliiomba mahakama kuahirisha kesi hiyo kutokana na mteja wake kutokuwapo mahakamani kwani anaumwa.

Jinsi Ya Kuandaa Na Kutayarisha Lishe Maalumu Ya Kuongeza Na Kunenepesha Mwili

$
0
0
Kama umekonda  na  kudhoofika  mwili  kutokana  na  sababu  mbalimbali  kama  vile kuugua  magonjwa  na  maradhi  mbalimbali  au  kupatwa  na  msongo  mawazo, basi  fuata  maelekezo  yafuatayo  ili  upate  kujua  namna  ya  kuandaa  na  kutayarishe  lishe  maalumu  ya  asili  itakayo  kusaidia kunenepa  na  kurejesha  afya  ya  mwili  wako  katika  hali  yake  ya  kawaida.

MAHITAJI:
1.    Dawa  Lishe  ya  kuongeza  na  kunenepesha  mwili

2.   Asali  ya  tende

3.   Ufuta

4.     Ukwaju

5.    Kitunguu  swaumu

6.   Giligiliani

7.    Juisi  ya  Komamanga na  Asali

MATAYARISHO  NA  MATUMIZI
Matumizi  ya  lishe  hii, yame  gawanyika  katika  awamu  kuu  mbili. Awamu  ya  kwanza, itachukua  siku thelathini  na  awamu  ya  pili  itachukua  siku  thelathini pia.

Katika  awamu  ya  kwanza , mgonjwa  atatumia  DAWA  LISHE  YA  KUNENEPESHA  MWILI, ASALI  YA  TENDE  NA  UFUTA  na  awamu  ya  pili, mgonjwa  atatumia   UKWAJU, KITUNGUU  SWAUMU, GILIGILIANI  na  JUISI  YA  KOMAMANGA  & ASALI  kwa  kufuata  utaratibu  utakao  elezwa  hapo  chini.

AWAMU   YA   KWANZA
SIKU   THELATHINI  ZA  KWANZA

Mahitaji

1.   Dawa  lishe  ya  kuongeza  na  kunenepesha  mwili

2.   Ufuta

3.   Asali  ya  Tende  (   Dates  Syrup )

MATAYARISHO  , MAELEKEZO  NA  MATUMIZI
1.   Dawa –Lishe  ya  Kunenepesha  Mwili

Chukua  vijiko   vitatu vikubwa  vyenye  dawa  yako, kisha  changanya  na  maji  nusu  lita halafu chemsha  hadi  itokote, Ikiisha  tokota, ipua  acha  ipoe  kidogo kisha  tumia  kunywa  pamoja  na  machicha  yake.  Utafanya  hivyo  mara  mbili  kwa  siku  asubuhi  na  jioni  kwa  muda wa  siku  thelathini.

2.   Ufuta : Matayarisho : Chukua  vijiko  vikubwa  vinane  vyenye  ufuta, kisha  changanya  na  lita  moja  na  nusu  ya  maji. Kama  hauna  tatizo  na  sukari, unaweza  kuongeza  na  sukari  kiasi ili  kuipa  ladha.  Ikisha  tokota, ipua iache  ipoe  kiasi  kisha  tumia  kula  ufuta wote  pamoja  na  supu  yake  ama  juisi  yake. Utafanya  hivyo mara  mbili  kwa siku  asubuhi  na  jioni  kwa  muda  wa  siku  thelathini.

(N.B:   KAMA  UNA  NAFASI,  BADALA  YA  KUTUMIA  VIJIKO  VINANE  TU VYA  UFUTA  KWENYE LITA  MOJA  NA  NUSU  YA  MAJI, WEWE  TUMIA  ROBO KILO  YA  UFUTA  KWENYE  LITA  TATU  YA  MAJI, CHEMSHA  HADI  ITOKOTE,  IACHE  IPOE, KISHA  TUMIA  KULA . FANYA  HIVYO  MARA  MBILI  KWA  SIKU  ASUBUHI NA  JIONI  KWA  MUDA  WA SIKU  THELATHINI )

2.   ASALI  YA  TENDE
3.   Tumia  kula  vijiko vikubwa  vinne  vya  tende  mara  mbili  kwa siku  asubuhi  na  usiku   kwa  muda  wa  siku  thelathini. Yaani  asubuhi  kula  vijiko  vikubwa vinne  na  usiku  kula  vijiko  vikubwa vinne  vya  asali  ya  tende.

( HABARI  NJEMA  KWA  WATEJA  WETU  NI  KWAMBA, ASALI  YA  TENDE  SASA  INAPATIKANA  MOJA  KWA  MOJA  DUKANI   KWETU . UTAPATIWA  DAWA  LISHE  PAMOJA  NA  ASALI  YA  TENDE  UTAKAYO  ITUMIA  KWA  MUDA  WA  SIKU  THELATHINI  KWA  UTARATIBU  WA  MAELEKEZO  HAYO  HAPO  JUU )
AWAMU   YA  PILI
Awamu  ya  pili  ya  lishe  hii, itaanza  baada  ya  kukamilika  kwa  siku  thelathini  za  kutumia  dawa  lishe, ufuta  pamoja  na  asali  ya  tende. Kama  ilivyo  kuwa  kwa  awamu  ya  kwanza, awamu  ya  pili  pia  itachukua  muda  wa  siku  thelathini

MAHITAJI, MATAYARISHO   NA  MATUMIZI

1.  UKWAJU
Matayarisho na  Maandalizi
Chukua ukwaju  kiasi  cha  robo kilo , weka  kwenye  maji  kiasi  cha  lita  moja, ongeza pilipili  manga kiasi cha  kijiko kimoja kidogo  ( tea spoon ) halafu ongeza sukari  vijiko  vitatu vikubwa, ongeza karafuu  ya unga  kijiko kimoja kidogo, pamoja  na hiriki vijiko  vikubwa  viwili.

Ukisha  fanya  hivyo, chemsha  hadi  mchanganyiko  wako  utokote. Ukisha  tokota, ipua  na  kuchuja  kisha  weka  kwenye  chombo  kisafi.

MATUMIZI :
Tumia  kunywa  mchanganyiko  huu kila  siku  asubuhi  baada  ya  kunywa  chai. Utafanya  hivyo  kwa  muda  wa  siku  thelathini  mfululizo.

2.   JUISI   YA  KOMAMANGA  NA  ASALI
Matayarisho  na  Matumizi

Tayarisha  juisi  ya  komamanga  kiasi  cha  nusu  lita, changanya  na asali ya  kawaida  vijiko vikubwa    vinane, kisha  ongeza  chumvi kijiko kidogo( tea spoon)

Koroga  mchanganyiko  wako  halafu  tumia  kunywa. Utafanya  hivyo  mara  moja   kwa  siku kwa  muda  wa  siku thelathini.

Matunda  ya  makomamanga  yanapatikana  masokoni, ingawa  mara  nyingi  hupatikana  kwa  uchache. Kama  utabahatika  kupata matunda  mengi, basi  unashauriwa  kuyachukua  kwa  wingi  na  kuyahifadhi, sehemu  salama ili usipate  usumbufu  wakati  wa  kutumia  tiba  yako.

Mbali  na  kutumika  katika lishe  ya  kuongeza  na  kunenepesha  mwili, tunda  la  komamanga, linasaidia  kuondoa  harufu  mbaya  ya  kinywa. Kwa  kuondoa  harufu  mbaya  ya  kinywa, kula  walau  tunda  moja  la  komamanga  kwa  siku  kwa  muda  wa  siku  thelathini  mfululizo. Utapata  matokeo  mazuri . ( HII  ITAWASAIDIA  ZAIDI  WALE  AMBAO  TATIZO  LAO  LA  KUTOKWA  NA  HARUFU  MBAYA  YA  KINYWA  LIMEANZIA  KINYWANI  NA  SIO  TUMBONI

ALTERNATIVE (MBADALA )  WA JUISI  YA  KOMAMANGA  ILIYO  UNGWA  NA  ASALI.

Kama  utashindwa  kupata makoma manga, basi  utafanya  kama  ifuatavyo :

KITUNGUU  SWAUMU
Chukua punje  nne  za  vitunguu  swaumu, zitwange kisha  tia  kwenye  maji nusu lita halafu ongeza  juisi  ya  ndimu  moja  au  limao  moja kisha  chemsha hadi mchanganyiko  wako  uchemke.

Matumizi :  Tumia  hivyo kila  siku  usiku baada  ya  kula  chakula cha  usiku. Utafanya  hivyo  kwa  muda  wa  siku  thelathini mfululizo.

AU
Vile vile , mbadala  mwingine wa  kutumia  juisi  ya komamanga  iliyo  changanywa  na  asali, unaweza  kutumia  JUISI  YA  GILIGILIANI  kwa  kufuata  utaratibu  ufuatao :

JUISI   YA   GILIGILIANI
MATAYARISHO   NA   MATUMIZI YA  JUISI  YA  GILI GILIANI

Chukua giligiliani  fresh, kisha zi -blend ( ZISAGE ) ili  kupata  juice  yake  kiasi  cha  robo  lita.

 Ndani  ya  juisi  yako  ya  giligiliani, kamuliamo ndimu fresh moja, halafu  ongeza  chumvi  kiasi robo  kijiko  kidogo ( tea spoon), koroga  kisha  tumia  kunywa.  Utakunywa  usiku  baada  ya  kula  chakula  cha  usiku. Utafanya  hivyo mara   moja  kwa  siku  kwa  muda  wa  siku  thelathini  mfululizo.

PIA : Jenga  utaratibu  wa  kuwa  unakula    giligiliani kwa wingi. Hakikisha  katika  kila  mlo  wako, inakuwepo  mboga  ya  giligiliani  pembeni.

VITU   VINGINE VYA   KUZINGATIA..
Pamoja na kutumia  lishe  hii  ya  asili  kwa  kufuata  utaratibu  huo  hapo  juu, unashauriwa  kuzingatia  matumizi  ya  vyakula  vifuatavyo:

TANGAWIZI
Jenga  tabia  ya  kuwa  una tumia  tangawizi, kila  mara  upatapo  nafasi.  Utaratibu  wa  jinsi  ya  kutayarisha  tangawizi ni  kama  ifuatavyo :

Chukua kipande  kimoja  cha  tangawizi, kisha  kitwange  halafu ongeza  vikombe  viwili vya  maji  vyenye  ujazo  wa  milimita  mia  mbili  na  hamsini ( 250 mills). Chemsha pamoja  kisha ongeza  maziwa  kiasi cha  robo lita  na  sukari ili kupata  ladha.  Fanya  hivi  kila  mara  uapatapo  nafasi. Ukiweza kufanya  hivyo walau  mara  mbili  kwa  siku, itakuwa  vizuri  zaidi.

  AU  chukua  kipande  kimoja  cha  tangawizi, kitwange kisha  chemsha pamoja  na  chumvi nusu  kijiko  kidogo  kwenye  maji kiasi  cha  nusu   lita  halafu tumia  kunywa  kikombe  kimoja  nusu  saa  kabla  ya  kula  chakula chako  cha  asubuhi, mchana  na usiku.

HIRIKI
Jenga utaratibu  wa  kuwa  unakunywa  mara  kwa  mara  chai  iliyo  changanywa  na  hiriki.

MACHUNGWA
Jenga utaratibu  wa  kuwa  unakula  machungwa kwa  wingi,  kwa  kadri utakavyo  weza. Unashauriwa  kuwa  unachanganya na  chumvi  kidogo  pamoja  na  pilipili  manga.

KWA  MAHITAJI  YAKO  YA  DAWA-LISHE  YA  KUNENEPESHA  & KUONGEZA  MWILI  PAMOJA  NA  ASALI  YA  TENDE.

Kwa  mahitaji  yako  ya  DAWA-LISHE ya  kuongeza & kunenepesha  mwili, pamoja  na  asali  ya  tende, fika  katika  duka  la  NEEMA  HERBALIST.

Tunapatikana  UBUNGO  jijini  DAR  ES  SALAAM, jirani  na  SHULE  YA  MSINGI   UBUNGO  NATIONAL  HOUSING  nyuma  ya  jengo  la  UBUNGO  PLAZA.

WASILIANA  NASI  KWA  SIMU  NAMBA  0766 53 83 84.

Kwa wateja  wetu  waliopo  jijini  Dar  Es  Salaam, ambao  hawana  nafasi  ya  kufika  dukani  kwetu  Ubungo, tunayo  huduma  ya  kuwapelekea  dawa  mahali  walipo ( HOME & OFFICE  DELIVERY  )

Kwa wateja  waliopo  nje  ya  mkoa   wa  Dar  Es  Salaam,  watatumiwa  dawa  kwa  kutumia  mabasi  mbalimbali.

Kwa  wateja  waliopo  Zanzibar, watatumiwa  dawa  kwa  njia  ya  usafiri  wa  boti.

Kwa  wateja  waliopo  ughaibuni, watatumiwa  dawa  kwa  njia  ya  POSTA  au  DHL.

Na kwa  taarifa  zaidi  kuhusu  huduma  zetu, tutembelee  kila  siku  katika  blogu  yetu :

Mahakama Kuu yaitosa Bodi ya Lipumba

$
0
0
Bodi ya Wadhamini iliyo chini ya Mwenyekiti wa CUF anayetambuliwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Profesa Ibrahim Lipumba, imeiomba Mahakama Kuu iitendee haki kwa kuithibitisha kama bodi halali ya chama hicho, ili iweze kufuta kesi zilizofunguliwa dhidi ya Lipumba na wenzake, kwa madai zilifunguliwa na Bodi isiyo halali.

Wakati akizungumza na waandishi wa habari, jana Julai 6, 2017 katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Slaam , Katibu wa Bodi hiyo, Thomas Malima alidai kuwa mahakama hiyo haikuwatendea haki kwa kutothibitisha uhalali wa bodi hiyo pamoja na kutowatambua mawakili wake.

“Mahakama haikutupa haki ya kutusilikiliza na kuithibitisha bodi yetu ambayo ni halali, mawakili wanaojiita wa bodi ya CUF ndiyo wale tuliowafukuza kazi, ambao kwa sasa ni sawa na mawakili wa mahakama na si wa chama chetu hatuwatambui, sisi ndio wenye mamlaka ya kufuta kesi,” alisema Malima.

Aidha, Bodi ya Wadhamini iliyo chini ya Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Shariff Hamad imefungua mashauri takribani sita dhidi ya Lipumba na wenzake ikiwemo shauri la kuzuia utolewaji wa fedha za rudhuku ya chama hicho kwa Lipumba.

Na kwamba Bodi ya Lipumba inadai kuwa kesi hizo zimefunguliwa kinyume na sheria kwa kuwa yenyewe ndiyo yenye uhalali wa kufungua kesi za chama hicho.


Jaji Mwingine Aomba Kustaafu Kabla ya Wakati.....Rais Magufuli Aridhia

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ameridhia maombi ya kustaafu mapema kwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mhe. Prof. John Eudes Ruhangisa.

Taarifa iliyotolewa  na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa Mhe. Rais Magufuli ameridhia maombi ya kustaafu mapema kwa Prof. John Eudes Ruhangisa kuanzia  06 Julai, 2017.

Mhe. Prof. John Eudes Ruhangisa alikuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya  Tanzania kanda ya Shinyanga.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam

Jeshi la Polisi Laua Wahalifu Wawili Kibiti

$
0
0
Jeshi la Polisi nchini limewaua watu wawili wanaodaiwa kufanya mauaji katika Wilaya za Mkuranga, Kibiti na Rufiji, mkoani Pwani.

Akielezea tukio hilo jana (Alhamisi Julai 6) ,   Mkuu wa Operesheni Maalumu  za Jeshi la Polisi,  Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Liberatus Sabas alisema tukio hilo lilitokea Jumatano  saa nne usiku  katika msitu wa Ngomboroni Kata ya Ikwiriri, Wilaya ya Ikwiriri.

Wahalifu hao waliuawa na askari wa operesheni maalumu wakiwa katika doria za ufuatiliaji wahalifu sugu wanaojihusisha na mauaji yanayoendelea katika kanda hiyo ya kipolisi.

Alisema askari wakiwa na mtuhumiwa mmoja muhimu anayeshiriki katika mauaji hayo  ambaye alikamatwa, alikubali kwenda kuwaonyesha polisi mahali  ambapo ni maficho ya wenzake.

“Baada ya kufika  eneo la msitu wa Ngomboroni  kikundi cha watu wanaokadiriwa kufikia watano walikurupuka  kutoka kwenye kichaka na kuanza kukimbia ndipo polisi kwa tahadhari kubwa walianzisha mashambulizi na kufanikiwa kumjeruhi mhalifu mmoja kwa risasi, katika  mashambulizi hayo  mtuhumiwa aliyekuwa mkononi mwa polisi  naye alijaribu kutoroka  na hivyo kupelekea kumjeruhi kwa risasi hivyo idadi yao kufikia wawili,” alisema.

Aliongeza;“majeruhi hao wawili  walifariki dunia njiani wakati wakipelekwa hospitali  kwa matibabu kutokana na kuvuja damu nyingi iliyosababishwa na majeraha ya risasi waliyoyapata. Miili ya marehemu imehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.”

Kamishna Sabas alisema katika tukio hilo wamefanikiwa kupokonya silaha mbili  aina ya SMG  na Shotgun moja pamoja na  risasi tisa.

Kamishina Sabas  amewataka wananchi kutoa taarifa zitakazowezesha kupatikana kwa wahalifu wengine waliosalia  na kwamba zawadi nono bado ipo pale pale  na itatolewa kwa mtu yeyote atakayetoa taarifa sahihi kuhusiana na wahalifu  wanaojihusisha na mauaji katika kanda maalumu ya Rufiji.

Wateja Wa Vodacom Waichangamkia RED RLX Katika Maonesho Ya Sabasaba

$
0
0
Kampuni ya simu za mkononi inayoongoza nchini, Vodacom Tanzania inashiriki Maonesho ya 41 ya Viwanda na Biashara maarufu kama “Sabasaba” ambapo mamia ya wateja wameoneshwa kufurahishwa na kujiunga na huduma mpya inayojulikana kama “RED RLX” ikiwa ni miongoni mwa huduma nyingi zinatolewa bandani hapo. 


Huduma hii ni mpango unaojumuisha vifurushi na kulipa kadri mteja atumiavyo na lengo ni kuwafanya wateja wa Vodacom waishi bila wasiwasi linapokuja suala la mawasiliano. Vifurushi hivi vina dakika nyingi, MB za intaneti nyingi, SMS nyingi na pia dakika za kupiga simu nje ya nchi.

Wakati mteja anaponunua kifurushi cha RED, anaweza kuchagua huduma ya kifurushi cha kujirudia (kujinunua tena) kila kinapoisha muda wake au kununua mara moja tu.
 
Mteja wa Vodacom akinunua bando ya RED, atapata nafasi na kipaumbele ya kuhudumiwa bila kukaa kwenye foleni wakati akitembelea duka lolote la kampuni hiyo, atapata huduma ya SOKONI App BURE, taarifa fupi ya M-Pesa BURE pindi anapohitaji na huduma ya kipekee pindi atakapowasiliana na huduma kwa wateja. Ili mtejaajiunge na kunufaika na kifurushi hiki anatakiwa kupiga *149*01# na Chagua RED na ataona vifurushi hivi vya RED.
 
Kifurushi cha Silver
  • TZS 30,000
  • 600 Dakika (Mitandao Yote)
  • 3GB Data
  • 3,000 SMS
Kifurushi cha Gold
  • TZS 50,000
  • 1,000 Dakika (Mitandao Yote)
  • 7GB Data
  • 7,000 SMS
Kifurushi cha Platinum
  • TZS 95,000
  • 2,500 Dakika (Mitandao Yote)
  • 30 Dakika (Kimataifa)
  • 20GB Data
  • 15,000 SMS

Kutana Maajabu ya Mtabibu CHIEF SULTAN(MAKATA WA MAKATANI) Mganga wa Waganga Sasa Yupo Mikoa Yote Tanzania

$
0
0
Kutana Maajabu ya Mtabibu CHIEF SULTAN(MAKATA WA MAKATANI) Mganga wa Waganga Sasa Yupo Mikoa Yote Tanzania

Pia anatoa Tiba kwa Njia ya Simu ukiwa popote Pale Tanzania au Nje ya Tanzania..

CHIEF SULTAN ni Mtabibu na Mtafiti wa Dawa za Asili ya Africa, na Duniani Katika utoaji wa Tiba za Asili..
 
Je unasumbulia na Mapenzi..?
(Umeachwa na Umpendae awe Mume/ Mke au mpenzi na Anaishi na Mtu Mwingine na Bado Unampenda?) Umejaribu sehemu Nyingi bila Mafanikio?Wasiliana na CHIEF SULTAN Akusaidie Kumshika Umpendae Asikusaliti(LIMBWATA) Kumtawala Mpenzi wako kwa sababu Maalum..Anauwezo wa Kusambalatisha Mahusiano yao ndani ya siku Moja tu.
Je Unasumbuliwa na Madeni?
Biashara yako Haina wateja?
Unatatizo la kutokushika Mimba na umehangaika sehemu nyingi bila mafanikio?
 
Wasiliana na CHIEF SULTAN Kwa Majibu ya Maswali yako..
Anasafisha NYOTA na Kutoa PETE za BAHATI kuendana na NYOTA yako. UTAJIRI USIO NA MASHARTI.(Magic Wallet_Pochi ya Maajabu Isio Isha Hela)
KUWA MAARUFU na KUJULIKANA
Kupandishwa CHEO na HESHIMA Mahala pa KAZI.
Utapewa Nguvu ya Kujilinda na MALI ZAKO zako na Mwili wako.. Huzuia Chuma Ulete katika Biashara.. Hurudisha MALI zilizo Potea au KUDHULUMIWA..
Mvuto wa Biashara na Mwili wako.
Hutibu kabisa Nguvu za Kiume na Kurefusha Uume kwa saizi Unayotaka.
 
Magonjwa Sugu(Miguu Kufa Ganzi, kisukari, Presha, Pumu nk.)Humaliza Kesi za Muda mrefu ndani ya siku 14 tu.
Anatoa NDAGU Zisizokuwa na Masharti.. Kwa maelezo Zaidi wasilina nae kwa

whatsapp +255 0658 316 976
Call +255 755 911 233

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumamosi ya July 8

Urusi yadaiwa kudukua vitalu vya nyuklia vya Marekani

$
0
0
Wadukuzi wanaosadikika kuwa ni kutoka Urusi wamejaribu kudukua makumi ya vitalu vya nyuklia vya Marekani katika mwezi Mei na Juni, kwa mujibu wa ripoti ya vyombo vya usalama vya Marekani.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Idara ya Ulinzi ya Homeland ya Marekani (DHS), wadukuzi hao waliweka hatari kubwa kwenye vitalu hivyo vilivyopo Kansas.

Hata hivyo, vyombo vya ulinzi vya marekani na idara hiyo vilikataa kueleza kwa undani endapo vitalu hivyo vya nyuklia vilidukuliwa au udukuzi uliishia kwenye majaribio.

DHS wamesema wanalihusisha tukio hilo na wadukuzi wa Urusi kwani mbinu iliyotumika ni sawa na ile iliyotumika katika uchaguzi wa marekani pamoja na udukuzi wa vitalu vya nyuklia vilivyoleta madhara makubwa nchini Ukraine.

Idara hiyo ilieleza kuwa wadukuzi waliwatumia barua pepe maafisa wa ngazi za juu wa idara hiyo zilizosomeka ‘maombi ya kazi’, lakini zilikuwa zimebeba ‘codes’ ambazo zingewawezesha kufanya udukuzi huo baada ya maafisa hao kuzifungua.

Hata hivyo, msemaji wa DHS, Jenny Hageman alisema kuwa wadukuzi hao hawakuathiri utendaji wa vitalu hivyo.

“Ni kweli kwamba hawakuleta madhara kwa sababu mfumo wa kompyuta zinazotumika kwenye utendaji ni tofauti kabisa na mfumo mkuu,” Reuters imemkariri Hageman.

Marekani iliwahi kuituhumu Urusi kwa kufanya udukuaji kwenye vitalu mwaka 2015 vilivyopelekea kukatika kwa umeme katika nchi yote ya Ukraine.

Tuhuma za udukuzi dhidi ya Urusi zimetolewa saa chache baada ya Rais wa Marekani, Donald Trump kukutana kwa mara ya kwanza na Rais wa Urusi, Vladimir Putin nchini Ujerumani walipokuwa wakihudhuria kikao cha G20.

Serikali yapunguza gharama za dawa, vifaa tiba na huduma za afya

$
0
0
Serikali imesema kuwa imepunguza bei ya vifaa mbalimbali vinavyotumika katika sekta ya afya zikiwemo bei za dawa, vitendea kazi na vifaa tiba vya maabara vinavyonunuliwa na kusambazwa na Bohari ya Dawa(MSD) kwa asilimia 15
 
Hayo yamesmwa jana na Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto  Ummy Mwalimu  jijini Dar es salaam alipokuwa akizungumza na wafanyakazi wa Bahari ya Dawa (MSD) ambapo alisema kuwa hayo ni matokeo ya utaratibu wa kuanza ununuzi wa moja kwa moja kutoka kwa wazalishaji kama Rais Dkt. John Magufuli alivyoagiza.
 
Alisema kuwa kwa sasa Halmashauri, Hospitali na Vituo vya Afya vianapaswa kutumia bei elekezi ya dawa iliyotolewa na Wizara ya Afya ambayo ipo kwenye kitabu ya orodha ya bei cha MSD.
 
“MSD  kwasasa inaagiza dawa moja kwa moja kutoka kwa wazalishaji wanchizipatazo 20 ambazonipamojana Kenya, Uganda, Afrika Kusini, India, Bangladesh, Pakistan, Jamhuri ya Watu wa Korea, China, Ujerumani, Uingereza, Uswisi, Denmark, Ufaransa, Ubelgiji, Italia, Romania, Marekani, Cyprus, Falme za Kiarabu, na Tanzania,”alisema Ummy Mwalimu.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Laurean Bwanakunu alisema tayari wametoa mikataba 73 kwa wazalishaji ambapo kati ya hiyo 46 ni ya wazalishaji wa dawa ambao wanatoka nchi za Uganda, Denmark, Ufaransa, Ujerumani, China, Afrika Kusini, Nchi za Falme za Kiarabu,Bangladesh, India, Kenya na Tanzania ambao wanazalishia aina 178 za dawa.
 
Hata hivyo, kwa upande wa vifaa tiba alisema jumla ya wazalishaji 18 wamepata mikataba ambao wanatoka Uingereza, Ujerumani, India, Kenya na Tanzania, kwa ajili ya aina 195 za vifaa tiba.Aidha, kwa upande wa vitendanishi vya maabara, jumla ya wazalishaji 9 kutoka nchi za Uingereza, Ujerumani, Ubelgiji, Romania, China, India na Kenya wamepata mikataba kwa ajili ya aina 178 za vitendanishi vya maabara.

Lowassa Amlilia Waziri wa Usalama Kenya

$
0
0
Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa ametuma salamu la rambirambi kufuatia kifo cha Waziri wa usalama wa Kenya, Meja mstaafu Joseph Nkaissery aliyefariki ghafla katika hospitali ya Karen iliyopo Nairobi muda mfupi baada ya kupelekwa kwa uchunguzi.

Meja Joseph Nkaissery alipelekwa hospitali kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi wa kiafya kabla ya umauti kumkuta, Mkuu wa Utumishi wa Umma wa Kenya Joseph Kinyua amethibitisha kutokea kwa kifo cha Waziri wa Ulinzi wa Kenya.

Baada ya taarifa hizo kusambaa Waziri Mstaafu Edward Lowassa amesema Nkaissery alikuwa ni rafiki mzuri na kiongozi mzuri na wakupigiwa mfano

"Natuma salamu zangu za pole kwa familia na watu wa Kenya kwa kumpoteza Waziri Joseph Nkaissery, alikuwa ni rafiki mzuri na kiongozi mzuri wa kupigiwa mfano, Mungu amumlaze mahali pema peponi" alisema Lowassa

Joseph Kasaine Ole Nkaissery alikuwa ni mwanasiasa wa Kenya, Mbunge kutoka mwaka 2002 mpaka 2014 na baadaye aliteuliwa kuwa Waziri wa usalama wa Kenya mpaka kifo chake, mbali na hilo Nkaissery alikuwa kiongozi Mkuu wa jamii ya Maasai nchini Kenya.

Bodi ya mikopo yajipanga kutangaza vigezo vya wanufaika

$
0
0
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imesema hivi karibuni itatangaza sifa na vigezo vitakavyotumika kuwapangia wanafunzi mikopo ya elimu ya juu kwa mwaka wa masomo 2017/2018 unaotarajia kuanza miezi michache ijayo.

Ufafanuzi huo umetolewa jaa (Ijumaa, Julai 7, 2017) jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Msaidizi wa Habari, Elimu na Mawasiliano wa HESLB, Dk Cosmas Mwaisobwa wakati akijibu maswali ya baadhi ya wateja waliotembelea Banda la HESLB katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere ambako HESLB inashiriki katika Maonyesho ya 41 ya Kimataifa ya Biashara.

“Tunakamilisha mwongozo wa utoaji mikopo kwa mwaka ujao wa masomo na tumepanga kabla ya mwisho wa mwezi huu wa Julai tuwe tumeutangaza na tumefungua mtandao wetu ili waombaji wenye sifa waombe,” alisema Dk Mwaisobwa.

Dk Mwaisobwa amewataka waombaji wa mikopo watarajiwa wawe watulivu na kufuatilia kwa karibu vyombo vya habari na tovuti ya HESLB (www.heslb.go.tz) ambayo huwa na kiunganishi (link) cha mfumo wa kuombea mkopo.

Awali, katika maonesho hayo, baadhi ya wananchi wanaotarajia kuomba mikopo ya elimu ya juu wamepata fursa ya kuuliza maswali mbalimbali yakiwemo tarehe ambayo Bodi itaanza kupokea maombi ya mikopo kwa mwaka wa masomo 2017/2018.

Maswali mengine yaliyoulizwa ni kama utaratibu wa udahili kupitia vyuoni moja kwa moja utaathiri upatikanaji mikopo, wengine walitaka kupata elimu zaidi kuhusu taratibu za urejeshaji wa mikopo.

Akifafanua kuhusu maswali hayo, Dkt. Mwaisobwa alisema Sheria iliyoanzisha HESLB, pamoja na mambo mengine, inamtaka mnufaika kuanza kurejesha mkopo wake miezi 24 baada ya kuhitimu masomo.

Mkurugenzi huyo wa HESLB alisema kuwa sheria hiyo inamtaka mwajiri yeyote kuwasilisha kwa HESLB majina ya waajiriwa wake wote ambao ni wahitimu wa taasisi za elimu ya juu ndani ya siku 28 baada ya kuwaajiri na Bodi itamjulisha kama ni wanufaika au hapana pamoja na utaratibu na kiwango cha kumkata mnufaika. 

Dk Mwaisobwa aliwataka wananchi kutembelea banda la HESLB kwa kuwa Bodi ya Mikopo itaendelea kuonyesha shughuli zake kwenye banda lake lililopo ndani, Banda la Benjamin Mkapa (Namba 19&20) hadi mwisho wa maonyesho hayo, tarehe 13 Julai, 2017.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images