MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWAILIPOISHIA
ILIPOISHIA
"Unajua nini nataka"
Paulina akafungua kifungo cha tatu cha shati lake, maziwa yake pamoja na tumbo lake vikaonekana vizuri. Paulina akauchukua mkono wa kulia wa meneja na kuukandamiza kifuani mwake, akamshikisha maziwa meneja, akabaki akiwa ameduwaa huku akihema. Gafla Paulina akamshika meneja Shingo yake, akamgandamiza kichwa chake kwenye meza kwa nguvu na kumuachia. Paji zima la uso wa meneja likawa linavuja damu nyingi na kumfanya atoe kilio cha maumivu.
ENDELEA
"Unajisikiaje?"
Paulina alimuuliza meneja wa benki ambaye kichwa chake kilisha anza kuvuma milio ambayo ni ya ajabu ajabu ambayo yanatokana na maumivu makali sana ya kubamizwa kwenye meza yake. Paulina akajifunga vifungo vya shati lake na kujiweka sawa. Akazunguka upande wa pili wa meza na kumshika shati meneja, akamnyanyua juu na kumsogeza karibu na uso wake.
"Nahitaji pesa"
Paulina alizungumza kwa kujiamini sana.
"Pesa! Pesa gani?"
"Priscar fanya kazi iliyo kupeleka hapo"
Sauti ya Rahab ilisikika kupitia kinasa sauti alicho kivaa masikioni make. Hakuwa Paulina kama alivyo jitambulisha ila ni Priscar aliye panga mpango na Rahab kufanya uvamizi wa kimya kimnya. Huku Priscar akiwa amevaa sura ya bandia ambayo si rahisi kwa mtu kuweza kumfahamu.
Kwa amri aliyo pewa na Rahab, Moja kwa moja, akamuamrisha meneja kuelekea kwenye chumba ambacho kinahifadhiwa mali nyingi za benki ikiwemo pesa nyingi sana. Pasipo mtu yoyote kuweza kufahamu ni kitu gani kinacho endelea huku damu zilizo kuwa zimejaa usoni make zikiwa zimefutwa na Paulina au Priscar.
Chumba kilicho jaa droo nyingi za chuma zenye mamba kwa kila droo meneja akaanza kufungua droo moja hadi nyingine. Huku mapigo ya moyo yakimuenda kasi sana, kwa vitisho ambayo aliweza kuvipata.
Priscar akawa na kazi ya kukusanya madini yenye thamani kubwa, hakuhitaji Kuchukua pesa kutokana na kuhofia kustukiwa.
"Nakuomba mumuachie mwangu tafadhali"
Meneja alizungumza katika hali ya majonzi kwani kwa kipindi alipo kuwa ofisini kabla ya kutolewa kwenye ofisi hiyo. Alipewa simu na kuzungumza na mtu ambaye amemteka mwanae wa kike kipenzi na wapekee.
"Nilazima kutoka hapa tuondoke pamoja"
"Nipo tayari katika hilo"
Priscar alipo hakikisha amechukua madini yenye thamani si chinj ya bilioni moja ya kitanzania. Akaifunga pochi yake, wakatoka katika chumba hicho ambacho mara nyingi huingia watu .atajiri wanao sadikika kuweka thamani ya pesa zao katika mfumo wa madini ambayo huwa na thamani sawa na pesa ambazo wanaziweka.
Wakatoka nje pasipo mtu yoyote kuweza kustukia swala lililo tokea. Wakaingia katika gari la Priscar na kuondoka naye kuelekea katika eneo ambalo yupo Rahab akiwa amemshikilia mtoto wa kike wa meneja wa benki.
***
Msako wa kumtafuta mke wa raisi ukazidi kuendelea kufanyika, hapakuwa namkuu wa jeshi aliye weza kulala. Kila mmoja alihakikisha kwamba anakiamrisha kikosi chake katika kuwatafuta watu ambao wamemteka mme wa raisi.
Uvumilivu ukawashinda jeshi na kuamua kutangaza hadharani zawadi nono kwa mtu ambaye atafanikisha kukamatwa kwa watekaji walio mchukua mke wa raisi. Hapakuwa na aliye kuwa na hisia kwamba mke wa raisi hajatekwa na yupo kwenye maficho ya handaki ambalo siku za nyuma alikuwa akilitumia yeye na wezake wakiwa katika kujificha kipindi wakifanya shuhuli za kijambazi.
Mawazo yakazidi kumkondesha raisi Praygod, uchangamfu wake ulipotea kwa watu wake wa karibu. Hapakuwa na mtu aliye weza kuzungumza jambo la kumfurahisha, akili yake yote ipo kwa mke wake kipenzi. Hata baadhi ya kazi za kiserikali zikaanza kumshinda kufanya. Ikamlazimu makamu wa raisi kuweza musimamia baadhi ya amjukumu.
"Muheshimiwa kuna mgeni anahitaji kukuona"
Sekretaari wake alimuambia raisi Praygod aliye jiinamia kwenye meza yake mawazo yakizidi kumpelekesha puta.
"Sihitaji kuonana na mtu kwa wakati hu"
"Ila amesema ni muhimu sana"
Kwa jicho alilo mtazama sekretari wake lilimtosha kufahamu kwamba rahisi haitaji kuzungumza naye. Taratibu mama huyo akatoka ofisini kwa raisi Praygod na kurudisha jibu kwa mkemia mkuu, bwana Ingnatus Mkama.
Jibu hilo likafedhesha mkemia wa serikali kwani alihitaji kumjulisha juu ya mazishi ya Lukuman ambaye ana wiki kadhaa akiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti, huku watu wengi wakiamini kwamba ndio Eddy.
"Nitafanya ninacho kifahanu"
Mkemia mkuu akizungumza na kuamua kuondoka akiwa amechoshwa sana skendo ambayo rafiki yake wa karibu bwana Eddy Godwin, zinaendelea kumtafuna kwenye jamii akioneka si mtu mwema kwao.
***
Shamsa hakuwa na jinsi yoyote zaidi, ya kuendelea kujitahidi kuogelea kuyaokoa maisha yake. Hakuhitaji kufia baharini. Ni bora kufili mbali na si kwenye bahari. Chuki dhidi ya Tanzania ikaanza kumjaa moyoni make. Furha ya maisha aliyo kuwa nayo kipindi cha nyuma imepotea. Akazidi kukumbuka Eddy kwa msaada alioweza kumpatia. Akimchukulia na kumpenda kama mwanae
Kadri jinsi alivyo zidi kwenda ndivyo jinsi Shamsa alijikuta akichoka. Njaa kali ikazidi kumtesa tumboni make, uwezo na kasi ambayo alikuwa anaitumia katika kuogelea ikaanza kupungua taratibu. Hali ikazidi kuwa mbaya zaidi na ndani ya dakika kumi mbele akajikuta akipoteza fahamu kabisa. Boti moja iliyo jaa watu wembamba kasi huku nywelie zao zikiwa zimenyongorotana, wakasimama karibu na ulipo mwili wa Shamsa unao elea juu ya maji. Mmoja wao akamkabidhi mwenzake bunduki yake, kisha yeye akajitosa ndani ya maji.
Wakamuokoa Shamsa na kumuingiza ndani ya boti na kuondoka naye.
Kila mmoja wao ndani ya boti hiyo aliweza kumtambua binti huyo, moja kwa moja wakampeleka kwenye makao makuu yao ha Al-Shabab. Moja kwa moja wakampeleka kwa Kiongozi wao bwana Mohammed Abdulah.
"Briton hamujampata?"
"Hatujampata kiongozi, huyu amekuwa kama bahati kwani kwenye patrol yetu ndio tumeweza kumpata Shamsa"
Kwa upande mmoja ikawa ni furaha kwa bwana Mohamed Abdulah na kwa upande mwingine imawa ni huzuni, kubwa kwa kumpoteza kijana wake aliye mtegemea kuliko yoyote, japo habari za vijana wake wengine alio watuma nchini Tanzania alizipata kwamba wamepoteza maisha. Shamsa akapatia watibabu yote ya muhimu huku daktari akitoa majibu yaliyo mridhisha bwana Abdulah Mohammed.
"Kwahiyo umesema kwamba hali yake itakuwa nzuri"
"Ndio muheshimiwa atakuwa salama, akizinduka hapa kila kitu kitakuwa sawa"
Wakamuacha Shamsa katika chumba maalumu cha matibabu kisha yeye na daktari wakatoka ndani ya chumba hicho.
***
Hali ya Eddy ikazidi kuhimarika siku hadi siku, huku dokta William akizidi kumuhudumia jeraha lake hadi likapona kabisa. Dokta William akamtafutia Eddy, mwalimu wa kumfundisha maswala ya kujilinda katika maisha yake ya baadaye.
Eddy akazidi kupiga tizi na kujifunza mbinu mbalimbali za kuweza kupambana kwanza kutumia mwili wake ikiwa akipatiwa ujuzi wa kareti pamoja na mafuzo ya judo. Alipo weza kuhitimu kwa wakati mfupi tu, akaingia katika mafunzo ya taikondo ambayo aliweza kufundishwa na .walimu mwengine kutoka nchi ya Thailand.
Mafunzo hayo Eddy aliweza kujifunza kwa juhudi zote, huku akilini mwake kukiwa na hali moja tu ya kipiza kisasi kwa mzee Godwin aliye weza kuhusika katika kumuulia familia yake.
Mazoezi hayo yakazidi kuuimarisha mwili wa Eddy. Haukuwa kama awali alivyo kuwa bali aliweza kupungua kwa kiasi kikubwa. Kifua chake hadi tumboni kuliweza kugawanyika katika miraba sita.
Misuli ya mikono yake iliweza kugawanyika kwa kiasi cha kumfanya muonekano wa mwili wake kubadilika kwa kiasi kikubwa. Hakuwa Eddy waziri tena ambaye hapo awali mwili wame ulisha anza kunenepa na kutokwa na kitambi. Ila huyu ni Black Shadow, umri wake wa miaka ishirini na saba ulimfanya aweze kujitahidi kuhakikisha anafanya kila jambo katika kuhakikisha kisasi chake kinakamilika kwa asilimia mia.
"Itabidi usafiri kwenda Japan"
Dokta William alizungumza mara baada ya Eddy kukamilisha kufanya mazoezi yake katika ukumbi maalumu ambao ndio anao fanyia mazoezi.
"Kufanya nini dokta?"
"Kule kuna baadhi ya mazoezi ninahitaji uende kuyafanya kuna mzee mmoja nirafiki yangu wa kipindi kirefu nahitaji akakupatie mazoezi hayo ambayo yatakusaidia"
"Sawa dokta, ila ni kwanini usisitishe mpango wa kuishambulia Tanzania na umshambulie Raisi Praygod peke yake"
"Hilo pia ninaliwaza kichwani mwangu, ila sintk hitaji kumuona anaingia katika awamu ya pili ya uongozi wake hata kama wananchi wake wanampenda sana.
"Ila unampango gani na Mzee Godwin?"
"Nahitaji kujiweka sawa ndio niweze kuliliza kisasi japo ni baba yangu ila yeye ndio chanzo cha mimi kuwa hivi."
Hapakuwa na jambo jengine ambalo dokta William, alilizunguza zaidi ya kuhakikisha mpango wa Eddy unakamilika. Siku mbili mbele Eddy akaanza safari ya kwenda Japan ambapo alipewa maagizo yoye ya kukutana na mzee huyo ambaye lengo la dokta William ni Eddy kujifunza mafunzo ya kininja ili kupapambana na kila mtu ambaye atakuwa ni adui yake.
***
Serikali ya Marekani iliamini kwamba wanajeshi wake pamoja na magaidi watatu ambao wikuwa wakiwasafirsha katika ndege hiyo kubwa ya wafungwa, wamefariki dunia kwa mlipuko mkubwa ulio weza kutokea. Hapakuwa na masalia yaliyo baki ya ndege hiyo kwani kila kitu kilisha potelea angani. Hapakuwa na aliyeeweza kufahamu kwamba kuna mchezo wa akili sana ulio weza kuchhezwa na marubani hao ambao ni miongoni mwa wanachama wa D.F.E.
Kitu kilicho weza kutokea kipindi ndege hiyo ilipo kuwa ikipasua mawingu juu angani umbali mrefu sana kutoka usawa wa bahari.
Kati ya askari ambao walikuja kuwachukua Fetty, Halima na Anna. Alikuwemo Agnes, Jaquline na Manka. Wote watatu waliweza kuzifunika sura zao na kuingia kisiri katika mpango wa kuwasafirisha magaidi hao, huku wakiwaua askari watatu wanawake ambao walikuwa kwenye mpangu huo kisha nafasi zao wakazichukua wao.
Ulikuwa ni mpango wa siri sana wakishirikiana na mkuu wa kikosi cha FBI, ambaye aliweza mutoa siri zote za mpango mzima wa tukio hilo lilivyo kuwa limepangwa, ndio maana alijitahidi kadri ya uwezo wake kuishawishi serikali kuweza kukiruhusu kikosi chake kusimamjia jukumu lote la wao kuwasafirisha magaidi hao.
Hata mlipuko wa helcoptar ambayo ilitegeshwa bomu linalo ongonjwa kwa romoti, ulikuwa ni mpango wame akishirikiana karibu na Mzee Godwin mwenye matawi mengi sana duniani na hapakuwa na jambo alilo weza kupinga na kushindika.
Ikawabidi Agnes na wezame kuvua kofia ambazo zilificha sura zao na kubakisha macho yao. Wakawavua na kina Fetty vigunia vizito vyeusi walivyo wavisha. Hapakuwa na mtu kati ya Fetty aliye weza kuyaamini macho yake kumuona mwenzao waliye potezana naye kwa kipindi kirefu akiwa amesimama mbele ya macho yao. Wakanyanyuka kwa furaha na kumkumbatia Agnes. Machozi yaliyo changanyikana na uchungu yakawatoka wote wanne.