Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Serikali yatakiwa kujibu kiapo kesi ya Uraia wa Yusuf Manji

0
0
Maombi ya mfanyabiashara maarufu nchini, Yusuph Manji dhidi Idara ya Uhamiaji yamechukua sura mpya baada ya Serikali kutakiwa iwasilishe kiapo kinzani za majibu.

Mahakama imeagiza Serikali ifanye hivyo ifakapo Jumatatu ijayo na imepanga kusikiliza maombi hayo siku hiyo.

Manji amefungua maombi hayo katika Mahakama Kuu akihoji uhalali wa kushikiliwa na idara hiyo huku akiwa bado amelazwa katika Hospitali ya Aga Khan, jijini Dar es Salaam kwa matibabu.

Uhamiaji inamtuhumu mfanyabiashara huyo kuwa siyo raia wa Tanzania.

Agizo dhidi ya Serikali la kuwasilisha hati ya kiapo kinzani ikiwa ni majibu limetolewa na Jaji Ama-Isario Munisi anayesikiliza maombi hayo.

Katika maombi hayo aliyoyafungua kupitia Wakili wake, Hudson Ndusyepo, Manji anaiomba Mahakama Kuu iiagize Uhamiaji imfikishe mahakamani ili iamue uhalali wa kushikiliwa kwake na kisha iamuru aachiwe huru.

Mwalimu atiwa mbaroni kwa kumwadhibu mwanafunzi

0
0
Jeshi la Polisi Mkoani Tanga linamshikilia Mwalimu wa Shule ya Sekondari Mkwakwani kwa kumpiga na kumsababishia madhara ya kiafya mwanafunzi, Suleiman Mohamed (18).
 
Mwanafunzi huyo inadaiwa alichapwa viboko juzi asubuhi na mwalimu huyo wa zamu aliyekuwa akiwaadhibu wanafunzi waliochelewa na waliokuwa wakipiga kelele darasani.
 
Aidha, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Benedict Wakulyamba amesema tayari mwalimu huyo yuko mikononi mwa Jeshi hilo na upelelezi wa suala hilo unaendelea.
 
Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Thobias Mwilapwa amewataka walimu kuwa waangalifu wakati wakiwaadhibu wanafunzi ili kukwepa madhara kwa wanafunzi.
 
“Tunalifuatilia kwa karibu tukio hili. Niseme kwamba tutachukua hatua stahiki ikithibitika kuwa umefanyika uzembe,” amesema Mwilapwa.
 
Hata hivyo, Baada ya kuchwapwa  mwanafunzi huyo alikimbizwa katika Hospitali ya Rufani ya Bombo kwaajili ya matibabu ikielezwa kwamba tayari amepatiwa rufaa kuhamishiwa Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa ajili ya matibabu zaidi.

Mchungaji Atiwa Mbaroni Kwa Tuhuma za Kumbaka na Kumlawiti Mtoto

0
0
Mchungaji wa Kanisa la Pentekoste Ipagala Manispaa ya Dodoma, Joshua Warioba, anashikiliwa na jeshi la polisi mkoani Dodoma kwa tuhuma za kumbaka na kumlawiti mtoto mwenye umri wa miaka mitano.

Tukio hilo linaripotiwa kutokea Machi 2, mwaka huu, majira ya jioni katika kituo cha chekechea cha Efretha English Medium Pre & Primary School, kinachomilikiwa na mchungaji huyo.

Kamanda wa Polisi mkoani Dodoma, Lazaro Mambosasa, alisema kuwa Mchungaji huyo anashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kumuingilia mtoto huyo kila siku alipokuwa akienda masomo ya ziada (tuition) na jalada la kesi hiyo lipo kwa mwanasheria wa serikali ambae muda wowote atapeleka hati ya mashtaka polisi ili afikishwe mahakamani.

Mama wa mtoto huyo anasema kuwa alimwandikisha mwanae kusoma chekechea katika shule ya kanisa hilo Februari 2. Baada ya mdogo wake kuja nyumbani kwake na kuuliza kama mwanae nae huwa anahudhuria masomo ya ziada na kujibiwa kuwa hajui kama kuna masomo hayo. Ndipo alipoamua kufuatilia kwa majirani wengine pia kuubaini ukweli.

Walipomuuliza mtoto huyo alisema japo kwa woga vitendo alivyokuwa akifanyiwa na mchungaji huyo. Ndipo walipoweka mtego na kumfuma mchungaji huyo akiwa na mtoto huyo kwenye chumba huku nguo zake za ndani zikiwa zimeshushwa.

Wananchi walikusanyika wakitaka kumpiga mchungaji huyo lakini aliokolewa na mwanajeshi mmoja na kukimbizwa polisi. 

Baada ya mzazi huyo kufika polisi aliandikiwa mtoto aende kupimwa hospitali na majibu ya daktari yalionyesha kuwa mtoto ana michubuko. Alipoulizwa mtoto huyo alisema kuwa mchungaji alikuwa akimbaka kila alipoenda kusoma.

Kamanda Mambosasa aliwataka wazazi kutowaruhusu watoto kwenda kusoma masomo ya ziada (Tuition) pasipo kuwa na uangalizi wa karibu na pia aliitaka jamii kuendelea kupiga vita dhidhi ya matendo ya udhalilishaji kwa kutoa taarifa ili hatua za kisheria zichukuliwe.

Breaking News: Rais Magufuli Afuta Agizo La Kufunga Ndoa Kwa Sharti La Kuwa Na Cheti Cha Kuzaliwa

0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amelifuta agizo lililotolewa jana tarehe 16 Machi, 2017 na Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Harrison Mwakyembe linalotoa sharti la kuwa na cheti cha kuzaliwa kwa watu wote watakaofunga ndoa kuanzia tarehe 01 Mei, 2017.

Rais Magufuli amefuta agizo hilo leo wakati akizungumza na Waandishi wa Habari muda mfupi kabla ya kuondoka katika Ikulu ya Chamwino Mkoani Dodoma na kurejea Jijini Dar es Salaam.

Rais Magufuli amesema Serikali haiwezi kuruhusu sharti hilo kutumika kwa kuwa litawanyima haki ya kuoa na kuolewa Watanzania wengi ambao hawana vyeti vya kuzaliwa, huku utaratibu wa kupata vyeti hivyo ukiwa bado unakabiliwa na changamoto nyingi kwa wanaohitaji.

Amesema mpaka sasa idadi ya Watanzania walio na vyeti vya kuzaliwa ni chini ya asilimia 20 huku wengi wao wakiwa ni wananchi waishio vijijini ambako ni vigumu kupata vyeti hivyo, na wengine wakiwa ni waliozaliwa kabla ya kuanza kutolewa kwa vyeti vya kuzaliwa nchini mwaka 1961.

“Kwa hiyo ndugu zangu Watanzania msiwe na wasiwasi wowote, endeleeni na utaratibu wenu wa kuoa na kuolewa kama kawaida na kama kuna kifungu chochote cha sheria kinachomlazimisha mtu awe na cheti cha kuzaliwa ndipo aoe ama aolewe nitamuelekeza Waziri wa Katiba na Sheria Harrison Mwakyembe apeleke Bungeni kikarekebishwe” Amesema Rais Magufuli.

Rais Magufuli ametoa wito kwa wanasheria kuziangalia vizuri sheria zinazohusiana na kuzaliwa na kifo na kuoa na kuolewa ili zisilete mkanganyiko kwa wananchi. 

Hata hivyo Mhe. Rais Magufuli ametoa wito kwa Watanzania kuendelea kupata vyeti vyao vya kuzaliwa kama kawaida na amewataka viongozi wote kuwahamasisha wananchi kuwa na vyeti hivyo.

Jinsi Mababu Zetu Walivyotumia Njia ya Kiini Macho Kuongeza Ukubwa na Urefu wa Maumbile ya Kiume

0
0
Imesimuluiwa  na  DOKTA  MUNGWA  KABILI…0744 000 473

Suala la udogo wa  maumbile  ya  kiume lipo tangu  enzi  za  mababu  zetu. Enzi  za  mababu  zetu, suala  la  udogo  wa maumbile  ya  kiume  lilikuwa  linatibiwa  kwa  kutumia  njia  kuu  mbili.  Njia  hizo ni  kama  ifuatavyo :

1.   KUCHANJIWA AMA  KUNYWESHWA  DAWA  YENYE  KUONGEZA  UKUBWA WA  MAUMBILE

 Hapa  mwanaume  mwenye  tatizo  la kuwa  na  maumbile  madogo  ya  kiume  alichanjiwa  au  kunyweshwa  dawa  ya  asili  yenye  uwezo  wa kurefusha  na   kuongeza  urefu na  ukubwa  wa  maumbile  ye  kiume.  Kama  iligundulika  kuwa, tatizo  la  mwanaume  husika  lilitokana  na  mkono  wa  mtu ( kurogwa ), basi  zoezi  la  kumchanja  au  kumnywesha  dawa  mwanaume  huyo lilienda  pamoja  na  tambiko  maalumu  la  kuua  nguvu  ya  uchawi  ulio  tumika  kufunga  ukuaji  wa  maumbile  ya  kiume  ya  mwanaume  huyo

Sababu  zilizo  wafanya  watu  wawafunge  watoto  wa  kiume  au  wanaume  maumbile  yao  yawe  madogo  ni  pamoja  na ; Kwenye  ndoa  za  mitaala, mke  anawafunga  watoto  wa  kiume  wa  mke  mwenzake  ili  waishie  kuwa  na  maisha    yenye  mateso  na  mahangiko ( SIKU NYINGINE  NITAELEZEA  JINSI   WATOTO  WA  KIUME  NA WANAUME  WANAVYO  FUNGWA   KUWA  NA  MAUMBILE  MADOGO  YALIYO SINYAA  )

Mwanamke  anamfunga  mwanaume  aliye mkataa  nakadhalika. Sababu  ni  nyingi  sana.

Kwa  bahati nzuri, nimeshaelezea  jinsi  na  namna  ya  kuongeza  na  kurefusha  ukubwa  wa  maumbile  ya  kiume  kwa  njia  ya  kuchanjia  au  kunywa  dawa.

Leo  nitaelezea  kuhusu  njia  ya  pili, ambayo  ni  KUONGEZA  UREFU  NA  UKUBWA  WA  MAUMBILE  YA  KIUME  KWA  NJIA  YA  KIINI  MACHO.  Njia  hii  haijulikani  na  watu  wengi.

Tiba  hii  hutumiwa na  mtu  ambaye  amethibitika  kuwa  suala  la  udogo  ama  ufupi  wa  maumbile  yake  ya  kiume, unatokana  na  maumbile  ya  asili. Yaani  amerithi  vinasaba  vya  maumbile  yake  kutoka  kwa  wazazi  wake na  wala  hajarogwa   na  mtu  yoyote.

Njia  hii  hutumiwa  na  magwiji  wa  tiba  za  jadi  tangu  enzi za  mabibi  na  mababu  wa  mababu, leo  nitaielezea  kwa  ufupi.

JINSI  YA  KUONGEZA  UKUBWA  NA  UREFU WA  MAUMBILE  YA  KIUME  KWA  NJIA YA  KIINI  MACHO

Kiini  macho  ni  uchawi  unao tumika  kufunga  na  kuyamiliki macho  ya  mtu  pamoja  na  kuyaelekeza  ama  kuyaamuru  yaone  na  kuamini  kile  ambacho  wewe  unataka   yakione  na  kukiamini.

  Katika  tiba  hii, mwanaume  anachanjiwa  dawa  kwenye  uume  wake  pamoja na  sehemu  nyinginezo za  mwilini mwake  kwa  lengo  la  kuyafunga, na kuyaamuru  macho  na  akili  ya  mwanamke  atakae  kutana  nae  faragha  kumuona  kama  mwanaume  mwenye maumbile makubwa  ya  kiume.

Kabla  ya  mwanaume  kuchanjiwa  dawa  hii, kwanza  unaandaliwa  huo  uchawi  wa  kiini  macho.

JINSI  UCHAWI  WA  KIINI  MACHO  UNAVYO TENGENEZWA.

Anachukuliwa  paka  mweusi  aliye  asi  nyumbani (  Paka  wa  aina  hii  katika  ulimwengu  wa  wachawi  huwa  wanajulikana kama  “  KIMBURU” ,    paka  huyo  anapelekwa  njia  panda  saa  sita za usiku, kisha  anatobolewa  macho, halafu  kwenye  macho  yake  zinawekwa  mbegu  za  mti  wa   mnyonyo.

Baada  ya  hapo, litachimbwa  shimo , kisha  paka  huyo  atazikwa  humo.

Huyo paka  akisha  zikwa , litaanza  zoezi  la   kumwagilizia  sehemu  aliyo  zikwa  paka  huyo.  Eneo  hilo  litakuwa linamwagiliziwa  mara  saba  kwa  siku, asubuhi  mara  tatu, mchana  mara  mbili  na  usiku  mara  tatu.

Eneo  hilo  litamwagiliziwa  hadi  uote  mti  wa  mnyonyo na  kukomaa.

Mti  wa  mnyonyo  ukishaota  na  kukomaa , itachukuliwa  ile  mizizi  ya  huo  mnyonyo  na  kupondwa  pondwa   pamoja  na  dawa  ya  asili  inaitwa  nkwesi.

Zoezi  la  kuponda  ponda  hiyo  mizizi  ya  mnyonyo  pamoja  na  hizo nkwesi likikamilika,   mhusika    ataenda  kwenye  eneo  lenye  mkutano  au  onyesho  lolote  kisha  atachukua  uchafu au takataka  za  eneo  hilo  wakati  watu  hao wakiwa  bize  wanasikiliza  mkutano, atazichoma  hadi  ziwe  unga unga.

Baada  ya  hapo  atachanganya  dawa  hizo  nilizo  zitaja  mwanzo,yaani mizizi  ya  mnyonyo  na  nkwesi  pamoja  na  madawa  mengine  ya  asili.

Zoezi  la  kuchanganya  mizizi  ya  mnyonyo  iliyo  sagwa  pamoja  na  kwesi , takataka  & uchafu  uliochukuliwa kwenye  mkutano  na  kuchomwa  pamoja  na  dawa  nyingine  za  porini, litafuata  zoezi  la kuchinja  punda.

Watachukuliwa  punda  saba  (YOTE  MADUME  YALIYO KOMAA ), Punda  hawa  watachinjwa  kwa  tambiko  rasmi.  Punda  hawa  watachinjwa  kwa  muda  wa  siku saba  mfululizo, kila  punda  mmoja  atachinjwa  kwa  siku  moja.

Kila  punda  atakae  chinjwa, itachukuliwa  DHAKARI  yake  ama  uume  wake kwa  wale  wasio elewa  dhakari  maana yake  nini, dhakari  za  hawa  punda zitaunganishwa  zote  kwa  pamoja, zitachanganywa  na  majivu  ya  kondoo  mweusi  aliye  pita  duniani  bila  kuonekana, utukakanga  wa  baharini  au  wa  porini  pamoja  na  dawa  nyingine  za  porini..  Baadae   litafanyika  tambiko  rasmi  la  kuchanganya  dawa ama  vizimba  vyote  nilivyo  vitaja  hapo  hapo  juu.

Dawa  hii  watapewa  wanaume  wenye  tatizo la  maumbile  mafupi  na  madogo  ya  kiume,  watajichanja  wenyewe   katika maeneo  Fulani  Fulani  mwilini  huku  wakitamka  maneno  Fulani 

Basi  kila  mwanamke  atakae  kutana  na  mwanaume  huyu ataenda  kusimulia,  kwa  wenzake  kuwa amekutana  na  mwanaume  wa  ukweli  na  anae  ijua  kazi  ambayo  iliwaleta  wanaume  duniani.


IMESIMULIWA  NA  DOKTA  MUNGWA  KABILI. ANAPATIKANA  KWA  SIMU  NAMBA  0744 – 000 473.
 
Kwa  makala  zenye  kuelimisha kutoka  kwa  Dokta. Mungwa  Kabili, tembelea.
 

Tundu Lissu afikishwa mahakamani ......Asomewa mashitaka Matano na Kuachiwa Kwa Dhamana

0
0
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemuachia kwa dhamana Mbunge Tundu Lissu aliyefikishwa mahakamani hapo na kusomewa mashtaka matano.

Lissu amesomewa Mashitaka matano(5)  ambayo ni yale yale aliyofutiwa hapo awali kuhusu maneno ya Uchochezi kwenye Uchaguzi wa Dimani,Zanzibar.

Serikali imesema upelelezi umekamilika na   ikaomba kesi ianze kusikilizwa leo.Lissu aliiomba mahakama isisikilize  kesi hii  leo ili akashiriki Uchaguzi wa TLS utakaofanyika kesho mkoani Arusha.

Mahakama imekubali maombi ya Tundu Lissu na kumwachia huru kwa dhamana ya milioni 10 ambapo tayari amekwishapanda ndege kuelekea jijini Arusha Kushiriki Uchaguzi huo

Lawrence Masha Ajitoa katika mbio za kugombea urais wa TLS .....Atangaza kumuunga mkono Tundu Lissu.

0
0
Wakati kesho kukitarajiwa kufanyika uchaguzi wa Rais wa chama cha wanasheria wa Tanganyika, leo wanasheria hao wamekuatana Arusha kwenye mkutano mkuu wa chama cha wanasheria hao.

Katika mkutano huo,  aliyekuwa mgombea wa Urais wa TLS, Mwanasheria Lawrance Masha ametangaza kujiondoa kuwania Urais huo na  amesema anamuunga mkono Tundu Lissu na kura zake apigiwe Tundu Lissu.

Rais Magufuli Amuagiza Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo kuwafikisha katika vyombo vya sheria wafugaji wote waliowashambulia wanakijiji.

0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amemuagiza Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Mkoani Pwani Alhaji Majid Mwanga kuwasaka, kuwakamata na kuwafikisha katika vyombo vya sheria wafugaji wote wanaodaiwa kuhusika katika matukio ya kuwashambulia kwa viboko wananchi wa Kijiji cha Fukayosi kilichopo Wilayani humo.

Mhe. Dkt. Magufuli aliyekuwa akisafiri kwa gari kutoka Dodoma kwenda Jijini Dar es Salaam ametoa agizo hilo leo tarehe 17 Machi, 2017 aliposimama katika kijiji hicho baada ya kuona wananchi wengi wakiwa wamekusanyika kando ya Ofisi ya Kata.

Baada ya kusimamisha msafara wake, Mhe. Rais Magufuli aliwaita wananchi waliokuwa wamekusanyika huku wakiwa wameshika mabango yaliyoandikwa ujumbe wa kutaka wafugaji wa jamii ya Wamang’ati waondolewe na kisha akatoa nafasi kwa baadhi yao kueleza dukuduku lao.

Wananchi hao ambao ni wakulima na mfugaji mmoja aliyejitokeza wakaeleza kuwa Wamang’ati wamekuwa wakiwanyanyasa kwa kuingiza mifugo katika mashamba yao ya mazao na wakithubutu kuwakataza wamekuwa wakichapwa viboko na baadhi kuuawa.

Katika majibu yake, pamoja na kutaka wote wanaodaiwa kuwashambulia wananchi kwa viboko wakamatwe Mhe. Rais Magufuli amemtaka Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo kukomesha mara moja vitendo vya wafugaji kuwapiga wakulima na wakulima kuwapiga wafugaji, na pia kukomesha vitendo vya wafugaji kulisha mifugo yao katika mashamba ya wakulima.

“Kuanzia leo isitokee mfugaji kumpiga mkulima, mkulima kumpiga mfugaji wala mfugaji kulisha mifugo yake kwenye mashamba ya wakulima, na suala hili nitalifuatilia mimi mwenyewe.

“Kwa hiyo Mkuu wa Wilaya na Viongozi mlishughulikie hili kabla mimi sijawashughulikia nyinyi, wale waliopiga watu, nataka wote wakamatwe na wafikishwe kwenye vyombo vya sheria” amesema Mhe. Dkt. Magufuli.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam

17 Machi, 2017

Taarifa ya TANESCO kuhusu kuzimwa kwa mfumo wa LUKU nchi nzima

Taarifa ya CCM kuhusu mchakato wa kupata wagombea ubunge watakaoiwakilisha Tanzania katika Bunge la Afrika Mashariki.

AUDIO: Lowassa amtaka Rais Dkt Magufuli kufuta kauli yake

0
0
Aliyekuwa Waziri Mkuu na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA, Edward Lowassa, amemtaka Rais Dkt. John Magufuli kuifuta kauli yake ya kuwataka wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wasishirikiane na wabunge wa vyama vya upinzani.

Alizungumza hayo jana kwenye ziara ya viongozi wa CHADEMA katika mkoa wa Pwani na Dar es Salaam. Lowassa alidai kuwa kauli hiyo ya Rais Dkt. Magufuli inabomoa misingi ya amani iliyowekwa na waasisi wa taifa letu. 

Alisema “Namuomba Rais aisahihishe kauli hiyo na nawaomba watanzania tukatae kugawanywa… Tusikuballi, nchi hii ni yetu sote hakuna mtu mwenye haki miliki hapa. Ikienda vibaya tutaangamia wote na ikienda vizuri tutafaidi wote, kwahiyo tukatae.”

Aliongeza kuwa watanzania wamekuwa wakiishi bila kubaguana kwa misingi ya dini, rangi au ukabila na kukumbushia kauli iliyowahi kutolewa na baba wa taifa kuwa ubaguzi ni sawa na kula nyama ya mtu, ukishakula hutotaka kuiacha.

Katika kikao hicho alizungumzia pia juu ya hali ya maisha na uchumi kuwa mgumu, bei za bidhaa kupanda  na mipango mibovu ilivyosababisha sekta binafsi kuyumba hali iliyosababisha kuongezeka kwa watu wasio na ajira nchini.

==>Msikilize Lowassa hapo chini akiongea

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumamosi ya March 18

Ridhiwani Afunguka Tena Tuhuma Dawa Za Kulevya

0
0
Mbunge wa Chalinze, Ridhiwani Kikwete, amezungumzia suala la marafiki zake kuhusishwa na biashara ya dawa za kulevya huku akisisitiza kwamba wanaodaiwa kuwa ni marafiki zake sio bali ni watu anaokutana nao katika maeneo anayotembelea.

Mbunge huyo amezungumza hayo jana jijini Dar es Salaam baada ya kuhojiwa na Mamlaka ya kudhibiti na Kupambana na Dawa za kulevya nchini, ambapo alisema roho yake imesuuzika kwani jamii imeamini kwamba hahusiki kwa namna yoyote ile na biashara hiyo haramu.

Ridhiwani alieleza kufurahishwa kwake baada ya kuhojiwa na Mamlaka hiyo nchini.

“Nashukuru kwa kuhojiwa huku nimepata nafasi ya kueleza ukweli juu ya jambo hili ambalo lilishaanza kuleta taharuki katika jamii, sasa umma umejua kuwa siuzi wala sihusiki na dawa za kulevya, roho yangu imesuuzika,” alisema Ridhiwani.

Alisema vita ya dawa ya kulevya ni kubwa na inapaswa kupigwa na kila mmoja ili kuokoa kundi kubwa la vijana ambao wanaathirika kutokana na suala hilo na kwamba kuhojiwa kwake kumemfanya awe na amani.

“Naunga mkono vita hii ya dawa za kulevya nchini kwani itasaidia kurudisha nguvu kazi inayopotea kutokana na matumizi ya dawa hizo za kulevya kwa mzazi ambaye mtoto wake ameathirika na matumizi ya dawa hizo anajua uchungu wake na hasara zake,” alisema Ridhiwani.

Aidha, aliongeza kuwa jamii inapaswa kusimama kwa kauli moja ili kuliokoa Taifa na nguvu kazi inayopotea ili Taifa liwe na vijana wanaojitambua na kutimiza wajibu wao katika kulitumikia taifa.

Ridhiwani alisema mchakato huo wa kupambana na dawa za kulenya nchini umekuwa ukiwachanganya wananchi kwani haieleweki ni nani anayehusika na kushugulikia suala hilo.

“Huu mchakato umekua ukichanganya, kuna watu wanaitwa kwa Kamanda Sirro na wengine wanaitwa kwa Kamishna Sianga (Rogers), mfano msanii Vanessa Mdee ambaye ameitwa kwa Kamanda Sirro badala ya kwa Kamishna Sianga,” alisema Ridhiwani.

Alisema watu wanahoji kwanini wengine watangazwe hadharani na wengine kuitwa kimya kimya na ameongeza kuwa ni vyema mamlaka zikajipanga ili kufanikisha vita hii na kufikia malengo yake ya kumaliza tatizo la dawa za kulevya nchini

Rais Magufuli Afanya Mazungumzo Na Waziri Wa Afya Wa Kenya Kuhusu Tanzania Kupeleka Madaktari 500(Wasio Na Ajira Serikalini) Kwenda Kufanya Kazi Nchini Kenya

0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Waziri wa Afya kutoka nchini Kenya Dkt. Cleopa Mailu aliyefika Ikulu pamoja na ujumbe wake kwa ajili ya mazungumzo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Waziri wa Afya kutoka nchini Kenya Dkt. Cleopa Mailu kuhusu Tanzania kupeleka madaktari 500 nchini Kenya, Ajira za Madaktari hao zitatangazwa mara moja na Waziri wa Afya Ummy Mwalimu na zitawahusu Madaktari ambao hawajaajiriwa Serikalini(hawapo katika utumishi wa umma au taasisi za serikali) waliomaliza mafunzo kwa vitendo na ambao wamesajiliwa na Baraza la Madaktari la Tanganyika.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na ujumbe kutoka nchini Kenya uliongozwa na Waziri wa Afya kutoka nchini Kenya Dkt. Cleopa Mailu Ikulu jijini Dar es Salaam.

VIDEO: Rais Magufuli akitolea ufafanuzi uamuzi wa Tanzania kuepeleka madaktari 500 nchini Kenya.


Breaking News: Tundu Lissu Achaguliwa Kuwa Rais wa TLS Kwa Ushindi wa Asilimia 88

0
0
Wajumbe wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS), leo wamefanya uchaguzi wa kumchagua rais pamoja na wajumbe wa ngazi mbalimbali za uongozi wa chama chao.

Uchaguzi huo umefanyika mjini Arusha ambako wanachama  wa TLS wamekutana kutekeleza ratiba hiyo pamoja na kupanga mipango mbalimbali ya utendaji kazi wa chama hicho.

Matokeo ni kama ifuatavyo:
 
Urais: Kura zilizopigwa 1682
  1.     Tundu Lissu 1411  sawa na asilimia 88
  2.     Francis Stolla 64
  3.     Victoria Mandari 176
  4.     Godwin Mwapongo 64
==>Kwa upande wa nafasi ya Makamu wa Rais (TLS) mshindi ni Godwin Ngwilimi aliyekuwa Mwanasheria wa Tanesco na kutimuliwa kwa kupinga Escrow.

Council Members
  1.     Jeremiah Motebesya
  2.     Gida Lambaji
  3.     Hussein Mtembwa
  4.     Aisha Sinda
  5.     Steven Axweso
  6.     David Shilatu
  7.     Daniel Bushele

Rais Magufuli kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa barabara ya juu katika makutano ya Ubungo.

0
0
Na. Immaculate Makilika –MAELEZO
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa kushirikiana na Rais wa Benki ya Dunia, Dkt. Jim Yong Kim wanatarajiwa kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa barabara za juu (Ubungo interchange) eneo la Ubungo jijini Dar es Salaam Machi 20 mwaka huu.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kitengo cha Habari na Mawasiliano, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano inasema kuwa mradi wa ujenzi wa barabara za juu katika makutano ya Ubungo yatagharimu takribani shilingi bilioni 188.71 ambapo una lengo kupunguza msongamano wa magari katika barabara za Morogoro, Nelson Mandela na Sam Nujoma.

“Mradi huo ni sehemu ya uboreshaji usafiri Jijini Dar es Salaam yaani (Dar es salaam Urban Transport Improvement Project), utakaogharimiwa kwa mkopo kutoka Benki ya Dunia na mchango wa Serikali ya Tanzania”

Aidha, taarifa hiyo ilisema kuwa, mradi huo utahusisha pia awamu ya tatu na ya nne ya ujenzi wa miundombinu ya mabasi yaendayo haraka (Bus Rapid Transit- BRT), katika barabara ya Nyerere kutoka katikati ya jiji la Dar es Salaam hadi Gongo la mboto na barabara ya Bagamoyo kutoka katikati ya jiji hadi Tegeta.

Waziri Mkuu amwakilisha Rais Magufuli Uzinduzi wa Jukwaa la uchumi Afrika

0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amekutana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda wakati akiwa uwanja wa ndege wa Julius Nyerere akielekea Port Louis, Mauritius.
 
Waziri Mkuu, anakwenda Mauritius kumwakilisha Rais John Magufuli, katika uzinduzi wa Jukwaa la Uchumi la Afrika(The inaugural session of The African Economic Platform).
 
Mauritius inakuwa mwenyeji wa mkutano huo utakaofanyika kuanzia Machi 20 hadi 22 katika hoteli ya Turtle Bay, jijini Balaclava.
 
Waziri Mkuu wa Mauritius, Pravid Jugnauth atafungua mkutano huo ambao pia utahudhuriwa na viongozi wakuu wa kisiasa wa Afrika, wafanyabiashara, vyuo vikuu, sekta binafsi na wasomi.

Wizara ya Afya yatangaza nafasi 500 za kazi kwa Madaktari Wanaotaka Kufanya Kazi Kenya

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumapili ya March 19

Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images