Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatatu Ya Octoba 3


SIKIKA Yaitaka Serikali Iache Siasa Upatikanaji wa Dawa.....Yatoa Mapendekezo 6 Kutatua Tatizo

$
0
0
Wiki iliyopita Sikika ilikutana na vyombo vya habari kujadili uhaba wa dawa unaoikabili Bohari Kuu ya Dawa (MSD). Vyombo vya habari kwa nyakati tofauti vilitoa taarifa sahihi kuhusu tatizo hili.

Hata hivyo, majibu kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto na Bohari Kuu ya Dawa hayakuonesha kutoa kipaumbele kwa tatizo hili. Kwa kuwa taarifa za uhaba wa dawa zilipatikana kutoka kwenye tovuti ya Bohari Kuu ya Dawa, tulitegemea majibu yenye ukweli,weledi na kuonesha ukubwa wa tatizo kutoka kwa wahusika. Taarifa hizo zingesaidia Ofisi ya Rais kupitia Wizara ya Fedha na Mipango kuona uharaka na umuhimu wa kutatua tatizo hili ili kuwasaidia wananchi kwa wakati. Badala yake majibu ya Wizara na Bohari Kuu yalipoteza msingi wa tatizo kama ifuatavyo;

(i)  Vyombo vya habari vilitumia takwimu kutoka katika tovuti rasmi ya Bohari Kuu ya Dawa kwamba kuna upungufu wa asilimia 47 ya aina mbalimbali za dawa zilizotakiwa kuwepo kwenye orodha ya dawa MSD. Tarehe 27 Septemba 2016, Wizara ya Afya ilikanusha kwa kudai kwamba aina ya dawa zilizokuwepo ni asilimia 53. Hata hivyo, mtu akisema uhaba ni asilimia 47 ya aina ya dawa na mwingine akasema uwepo ni asilimia 53 wote wanamaanisha kitu kile kile.

(ii)Taarifa za vyombo vya habari zilionesha uhaba wa baadhi ya dawa muhimu ambazo zilitarajiwa kupatikana MSD muda wote Taarifa hizi zilikusudia kuonesha mifano ya kiwango cha ukubwa wa upungufu wa dawa. Badala ya kujibu hoja ya msingi, yaani upungufu wa dawa nchini kwa ujumla; Wizara iliamua kujikita kwenye kutaja uwepo wa baadhi ya dawa kama vidonge vya paracetamol na zingine chache.

(iii)Bohari Kuu ya Dawa ilinukuliwa na vyombo vya habari ikikanusha uwepo wa upungufu wa dawa na kusema kwamba serikali imefanya maajabu kwa kuipatia MSD jumla ya Shilingi bilioni 20 kwa robo ya 2016/2017. Hata hivyo, bilioni 20 ni pungufu ya kiwango halisi ambacho kingehitajika (Shilingi bilioni 62.5), kwa robo ya kwanza ya mwaka iwapo bajeti iliyotengwa ya shilingi bilioni 251 ingegawanya sawa na kutolewa katika awamu nne. Je, Bohari Kuu ya Dawa inaposema serikali imefanya maajabu ina maana haihitaji fedha zaidi kwa ajili ya kutatua tatizo la dawa nchini?

(iv)Wizara ya Afya imeahidi kuongeza akiba ya baadhi ya dawa kuanzia mwezi Oktoba, 2016. Hii ni sawa na kukiri kwamba kulikuwa na upungufu wa dawa. Ingawa tunaipongeza wizara kwa hili, Wizara haikueleza ni lini itapata fedha zilizobaki na iwapo ongezeko hilo la dawa litakidhi mahitaji halisi.

Katika kufafanua suala hili, Sikika ingependa kuelezea umma na wadau wa sekta ya afya ukweli kuhusu upungufu huu sugu wa dawa na vifaatiba kwenye Bohari Kuu ya Dawa na katika vituo vya kutolea huduma za afya:

(i)  Uhaba wa dawa na vifaa tiba katika Bohari Kuu ya Dawa siyo tatizo jipya, bali ni la muda mrefu, ambalo serikali yenyewe imekuwa ikikiri kupitia taarifa zake mbali mbali. Isipokuwa sasa limefikia kiwango kikubwa, hata kupelekea uhaba wa dawa kama za chanjo kwa kipindi cha zaidi ya miezi mitatu.
(ii)Kila mwaka, Wizara ya Afya wamekuwa wakiahidi Bungeni kutatua upungufu na uhaba wa dawa muhimu na vifaatiba. Pia Wizara ya Afya imekuwa ikiahidi bungeni kila mwaka kulipa deni inalodaiwa na MSD ili kuboresha ufanisi wa bohari. Hata hivyo uhaba wa dawa umeendelea kuwepo na deni la MSD limekuwa likikua kila mwaka.

(iii)Uhaba ukitokea MSD moja kwa moja unaathiri upatikanaji wa dawa muhimu na vifaa tiba katika vituo vya kutolea huduma za afya vya umma, kwa sababu mfumo wa sasa unalazimisha vituo kuagiza dawa kutoka MSD kwanza kabla ya kuruhusiwa kununua mahali pengine. Pamoja na hilo, mgao wa fedha za dawa kwa vituo hivyo hupelekwa moja kwa moja MSD ambapo vituo haviwezi kuzichukua kuagiza dawa pengine pale wanapokosa dawa MSD.

(iv)Mnamo Septemba 16, 2016, tovuti ya MSD ilionesha ukosefu wa asilimia 47 wa aina mbali mbali za dawa. Miongoni mwa dawa na vifaatiba vilivyokosekana ni vile vinavyotumika katika matibabu muhimu ya kupunguza vifo, mfano dawa za kuharisha kwa watoto (ORS+Zinc), vifaa vya kujifungulia (Delivery kits), dawa za maumivu, dawa za magonjwa ya moyo na chanjo kama vile za surua, homa ya manjano na kichaa cha mbwa.

(v)  Mojawapo ya sababu za uhaba huu ni serikali kushindwa kutenga na kutoa fedha za kutosha kukidhi mahitaji ya nchi ya dawa muhimu na vifaatiba. Kwa mfano, mahitaji ya sasa ya dawa na vifaatiba ni zaidi ya shilingi bilioni 577 lakini bajeti iliyotengwa kwa mwaka huu ni shilingi bilioni 251, ambapo kati ya hizo, shilingi bilioni 108 ni zakulipa deni la MSD.

(vi)  Vituo vya afya vya umma vinapata usumbufu mkubwa kutokana na utaratibu unaovilazimisha kutuma maombi ya dawa MSD licha ya kufahamu ukweli kwamba hazipo. Baada ya vituo kupata uthibitisho wa maandishi wa kutokuwepo dawa MSD, ndipo vinaruhusiwa kufanya taratibu zingine. Pamoja na usumbufu huu, baadhi ya vituo vimemudu kukabiliana na uhaba wa dawa kwa kutumia vyanzo mbadala vya fedha kununua dawa kutoka kwa wauzaji binafsi. Mfano halisi ni katika vituo vya afya vya wilaya za Kondoa na Kilolo ambapo Sikika ilifuatilia kwa kina.

Kutokana na uzoefu wa Sikika wa kufanya kazi katika sekta ya afya kwa takribani miaka kumi, tunashauri mapendekezo yafuatayo yafanyiwe kazi:
(i)  Bohari Kuu ya Dawa iachwe iwe taasisi au kampuni huru itakayofanya maamuzi yake yenyewe na kukusanya mtaji kushindana na wauzaji wengine binafsi wa dawa nchini.
(ii)Serikali ifute ulazima wa vituo vya kutolea huduma za afya vya umma kuagiza dawa MSD kwanza, badala yake viachwe huru kuamua kununua kutoka kwa muuzaji yeyote mwenye dawa ambaye anadhibitiwa na kuhakikiwa na serikali.

(iii)Serikali ihakikishe kuwa fedha zinazotengwa kwa ajili ya dawa muhimu na vifaatiba zinapelekwa moja kwa moja kwenye akaunti za vituo au Halmashauri badala ya utaratibu wa sasa ambapo zinapelekwa kwenye akaunti za vituo zilizopo MSD.

(iv)TAMISEMI iimarishe na kusimamia uwezo wa vituo vya kutolea huduma za afya katika halmashauri ili kujiendesha vyenyewe, na Wizara ya Afya ijikite katika kusimamia ubora na udhibiti wa bei za dawa.

(v)  Tunaomba watendaji na viongozi katika sekta ya Afya wafanye kazi kitaalam zaidi badala ya kisiasa.
(vi)Mwisho, wakati Wizara ya Afya ikifanyia kazi mapendekezo haya. tunaiomba Ofisi ya Rais kuagiza fedha zitolewe kama mpango wa dharura kutatua tatizo lililopo la dawa, ikiwa ni pamoja na kulipa deni lote la MSD.

ACT-Wazalendo waitisha mkutano wa kidemokrasia Kupigania Upatikanaji wa Katiba Mpya

$
0
0

Chama cha ACT- Wazalendo kimepanga kuwasha moto mjadala wa Katiba mpya katika mkutano wake kidemokrasia kilioitisha jijini Dar es Salaam Oktoba 8. 

Mkutano huo unalenga kufufua mchakato wa Katiba Mpya kwa kuzingatia michakato ya katiba za nchi nyingine za Afrika, alisema Katibu wa itikadi na uenezi wa ACT Wazalendo, Ado Shaibu alipozungumza na waandishi jijini Dar es Salaam  jana. 

Alisema katika kupata uzoefu, ACT Wazalendo imemualika Adabu Namwamba, ambaye ni kiongozi wa Chama cha Labour cha Kenya kilichofanikiwa kubadilisha katiba yake baada ya mchakato mrefu. 

 Aliwataja wageni wengine kuwa ni mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba Tanzania, Deus Kibamba ambaye naye atatoa mada kuhusu suala hilo. 

Mchakato wa kuandika Katiba mpya nchini umekwama katika hatua ya kupiga Kura ya Maoni baada ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kushindwa kukamilisha uandikishaji wapigakura kwa muda uliotakiwa. 

Mchakato huo uligubikwa na vikwazo kadhaa, ikiwa ni pamoja na vyama vinne vya upinzani na baadhi ya wajumbe kususia kwa maelezo kuwa Bunge liliacha Rasimu ya Katiba iliyokuwa na maoni ya wananchi na kuingiza sera za CCM. 

Katika mkutano huo, kiongozi wa ACT Wazalendo, Zitto Kabwe atawasilisha mada kuhusu hali ya nchi kwa mtazamo wa chama hicho. 

“Kiongozi wetu atawasilisha uchambuzi mpana wa kina zaidi kuhusu hali ya nchi yetu kiuchumi, kisiasa na kijamii tangu Serikali ya Awamu ya Tano ilipoingia madarakani,” alisema. 

Pia, mwenyekiti wa ACT Wazalendo, Anna Mghwira, ambaye aligombea urais mwaka jana, ataeleza uzoefu wake katika uchaguzi, wakati mshauri wa chama hicho, Profesa Kitila Mkumbo atachambua mwelekeo wa chama hadi mwaka 2020. 

“Chama kinatoa wito kwa wananchi wanaotaka kushiriki katika mkutano huo kuwasiliana na ofisi ili kujiandikisha,” alisema. 

RIWAYA: She is My Wife- Sehemu ya 19 & 20

$
0
0

MWANDISHI : EDDAZARIA G.MSULWA

ILIPOISHIA...
“NDUGU ABIRIA, NIFURAHA YANGU KUWA NANYI KATIKA SAFARI HII, NIMETOA LISAA MOJA KWA KILA ABIRIA KUSALI SALA YAKE YA MWISHO KWANI NDEGE INAKWENDA KULIPUKA NDANI YA LISAA HILO KUTIMIA KAMA HUAMINI, TIZAMA HII”

Samson akaishika camera na kuigeuzia kwenye computer aliyo iietega mwendo kasi wa saa, unao onyesha dakika zake zikirudi nyuma, kwani ikifika ndani ya muda alio upanga, mfumo mzima wa ndege unakwenda kuzima, na litakalo tokea hapo ni ndege kulipuka, jambo lililo anza kumuogopesha kila mmoja aliyomo ndani ya ndege hadi raisi mwenyewe

ENDELEA...
Samson akaigeuzia kamera alipo na kuznedelea kuzungumza kwa sauti iliyo jaa msisitizo
“NAJUA MUTASHANGAA, ILA NI KWAMBA NITAHITAJI RAISI KUFANYA HAYA YOTE AMBAYO NITAMUAGIZA KUFANYA LA SIVYO PUUUUUUU, SOTE TUTAKUFA HAHAHAAAAA”
Samson akaanza kucheka kicheko kilicho muacha mdomo wazi Rahab ambaye hadi sasa hivi amuelewi Samson anamalengo gani na roho yake

Fetty, Anna, Agnes na Halima hawatambui ni wapi wanapo elekea, kila mmoja akabaki akiwa na wasiwasi moyoni mwake kwani, nyuso zao bado zimefunikwa na vitu mifuko mnyeusi, isiyo wapa uwezi wa kuona kinacho endelea zaidi ya pumzi zinazo ingia kwenye pua zao.Kila mmoja anahofu ya kuuliza ni wapi wanakwenda kutokana kila jibu walilo pewa apo awali ni kwamba wanaelekea kuzimu.Wakasikia mlango wa chuma ukifunguliwa kwenye chumba walichopo.
“Yupi mkuu”

Sauti ya mwanaume ilisikika kwenye masikio yao, na hawakujua ni nani anaye uliziwa
“Huyu mwenye mahipsi makubwa”
Mkuu wa askari alijibu kupitia redia ya upepo, huku akitazama kwenye moja ya Tv iiyopo kwenye chumba chake, ikionyesha video za kamera za ulinzi zilizopo kwenye chumba walichopo Fetty na wezake

“Ahaa sawa mkuu”
Askari aliye agizwa na mkuu wake wa kikosi, akamkamata Anna, na kumnyanyua juu
“Jamani munanipeleka wapi?”
Anna alizungumza huku akijitahidi kujitoa mikononi mwa askari huyo
“Tulia wewe, nitakuua malaya mkubwa wewe”
Askari huyo akamnyanyua Anna na kumuweka begani mwake, na kutoka kwenye chumba na kuuamiza mlango kwa nguvu
“Hakikisheni hatoki mtu hapa”

Askari huyo aliwaagiza askari wengine wawili, walio simama kwenye malango wakilinda chumba walichopo majambazi hawa wa kike.Askari aakendelea kumbeba Anna ambaye anaendelea kufurukuta kwenye bega lake alipo muweka, kutokana na ukubwa wa misuli yake iliyo jengeka vizuri kutokana na mazoezi ya kijeshi anayo yafanya, Anna hakumsumbua kabisa kuchomoka kwenye mikono yake.Wakafika kwenye moja ya chumba ambacho yupo mkuu wake wa kikosi bwana Mathiasi Reymond na kumuingiza Anna na kumkalisha kwenye kiti
“Tulia kama ulivyo la sivyo tutakunyonga”

Anna aliendelea kupokea vitisho kutoka kwa askari aliye mtoa kwenye chumba alicho kuwepo na wezake.Mathiasi Reymond, tayari amesha vua ngua zake na kubaki na bukta yake ya ndani kwa ajili ya kufanya kazi moja tu, yakumuingilia kimwili Anna, msichana mzuri aliye umbika kila idara ya mwili wake.

Fetty akanyanyuka kwenye kwenye sehemu aliyo kaa, lengo lake ni kusikiliza kama atapokea amri yoyote ya kuambiwa kukaa kwenye sehemu yake, ila ukimya ukatawala.Akapiga hatua za taratibu akizunguka kwenye chumba akijaribu kujua ni kitu gani kinacho endela ila hakusikia chochote.

“Jamani mupo”
Fetty alizungumza kwa sauti ya chini
“Ndio, ila tupo wa tatu”
Halima alijibu kwa sauti ya kunong’oneza
“Nalijua hilo, Anna atakuwa amepelekwa wapi?”
“Yaani hata mimi mwenyewe sielewi?” Agnes alijibu
“Sijui hapa ni wapi jamani” Agens aliiuliza
“Cha msingi ni kujua nini tunatakiwa kukifanya na amini mumenielewa”

Fetty alizungumza huku akijiegemeza kwenye ukuta wa chumba alichopo, kutokana na mikono yake kufungwa kwa nyuma kwa pingu na kugundua si ukuta wa kawaida

Mathiasi Reymond akamuamuru mlizi wake, kumfungua  vipingu za mikononi na minyororo aliyo fungwa Anna kwenye miguu yake na mlinzi wake akafanya kama alivyo agizwa na bosi wake.Baada ya mlinzi wake kumfungua Anna akatoka ndani ya chamba na kumuacha bosi wake na Anna
                                                                                            
Vichwa vya viongozi wa pande zote mbili Tanzania na Marekani vinazidi kuuma, kila mmoja akijaribu kutafuta mbinu na njia za kuweza kuipata ndege yenye thamanini sana aina ya Air Force inayomilikiwa na serikali ya nchini Tanzania huku ndani mwake ikiwa imembeba raisi pamoja na viongozi wapambe wake.Juhudi za Satelait katika kuinasa ndege ya raisi na kutambua ni wapi ilipo inafua dafu, jambo linalo zidi kuwachanganya sana viongozi wa pende zote mbili.

Wanacho kihofia viongozi wa nchini Tanzania ni kumpoteza raisi wao mpendwa bwana Praygod Makuya, huku serikali ya Marekani ikihofia kupoteza moja ya ndege zake ambazo ina uwezo mkubwa wa kuhimili mikiki mikiki ya vita ya anga japo imetengenezwa kistarehe zaidi kwa ajili ya kumbeba raisi huyu wa Tanzania aliye jijengea umaarufu mkubwa sana kutokana na ucheshi wake na ushirikiano wake kwa wananchi na vingozi mbali mbali duniani, katika mataifa tajiri na mataifa masikini

“Inatuazimu kutumia, mpango namba mbili(Plan B)”
Mkuu wa jeshi la anga alizungumza na mkuu wa jeshi la anga nchini Tanzania kwa kupitia mtandao wa kuonana moja kwa moja katika vioo vya Tv zao kubwa zilizopo kwenye maofisi yao ya jeshi.

Rais MagufuliJP amteua Prof. Lawrence Mujungu Museru kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

$
0
0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe 03 Oktoba, 2016 amemteua Prof. Lawrence Mujungu Museru kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, Ikulu Jijini Dar es Salaam imeeleza kuwa uteuzi wa Prof. Lawrence Mujungu Museru umeanza jana tarehe 02 Oktoba, 2016.

Kabla ya Uteuzi huo Prof. Lawrence Mujungu Museru alikuwa akikaimu nafasi hiyo.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam

03 Oktoba, 2016

Rais Magufuli Akutana Na Makamu Wa Rais Wa Jamhuri Ya Cuba, Ikulu Jijini Dar Leo

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe 03 Oktoba, 2016 amekutana na kufanya mazungumzo na Makamu wa Rais wa Cuba Mhe. Salvador Antonio Valdes Mesa ambapo viongozi hao wamekubaliana kuimarisha na kuongeza uhusiano na ushirikiano kati ya nchi hizi mbili kwa manufaa ya wananchi wake.

Katika Mazungumzo hayo Rais Magufuli amesema anatambua uhusiano na ushirikiano mzuri na wa kihistoria uliopo kati ya Tanzania na Cuba na kwamba Serikali yake imejipanga kuhakikisha uhusiano huu unaelekezwa katika maeneo yenye manufaa ya kiuchumi na ustawi wa jamii.

Rais Magufuli amemuomba Makamu huyo wa Rais wa Cuba kuwashawishi wawekezaji wa kutoka nchini mwake kuja hapa nchini kujenga viwanda vya kutengeneza dawa za binadamu ili kurahisisha upatikanaji wa dawa na kupunguza gharama.

Pia, Rais Magufuli amemuomba Makamu wa Rais wa Cuba Mhe. Salvador Antonio Valdes Mesa kuwashawishi wafanyabiashara wa Cuba kuja kuwekeza katika uzalishaji wa sukari na amewahakikishia kuwa wakiwa tayari Serikali ya Tanzania ipo tayari kuwapa ardhi kwa ajili ya kuendesha uzalishaji huo.

"Mhe. Salvador Antonio Valdes Mesa najua kuwa nchi yenu ina utaalamu wa kutosha katika uzalishaji wa sukari, uzalishaji wa dawa za binadamu na masuala mengine mengi yanayohusu matumizi ya teknolojia katika shughuli mbalimbali za uzalishaji, nakuomba uwaambie wafanyabiashara wa Cuba kuwa tunawakaribisha waje Tanzania kuwekeza na Serikali itawapa ushirikiano wa kutosha" amesema Rais Magufuli.

Kwa upande wake Makamu wa Rais wa Cuba Mhe. Salvador Antonio Valdes Mesa amempongeza Rais Magufuli kwa juhudi kubwa zinazofanywa na Serikali yake katika kuinua uchumi wa Tanzania na amemhakikishia kuwa Cuba ipo tayari kushirikiana na Tanzania kwa kutumia utaalamu na uzoefu wake.

Amesema kwa kuanzia Cuba italeta wataalamu kwa ajili ya kuangalia namna itakavyotekeleza ombi la kujenga viwanda vya kutengeneza dawa za binadamu na pia atazungumza na Jumuiya ya Wafanyabiashara wa Cuba na kuwashawishi kuja hapa nchini kuwekeza katika uzalishaji wa sukari.

"Mhe. Rais Magufuli natambua kuwa uhusiano wetu na Tanzania na Afrika ni wa kihistoria, sisi Cuba tumepiga hatua kubwa katika maendeleo ya uchumi na teknolojia, nimekuja kukuhakikishia kuwa tutauendeleza uhusiano huu ili ulete manufaa kwenu na kwa wananchi wa Cuba" amesema Mhe. Mesa.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
03 Oktoba, 2016

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumanne ya October 4

Profesa Lipumba Apata Pigo........Baraza la Wadhamini CUF Lagoma Kumtambua, Lapanga Kufunga Jengo la Chama

$
0
0

TAMKO LA BODI YA WADHAMINI YA THE CIVIC UNITED FRONT (CUF – CHAMA CHA WANANCHI) KUFUATIA KIKAO CHAKE KILICHOFANYIKA JANA, TAREHE 2 OKTOBA, 2016

Kwa kuzingatia hali iliojitokeza katika chama chetu cha THE CIVIC UNITED FRONT (CUF – Chama Cha Wananchi) kufuatia hatua ya makusudi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi, kutupandikizia vurugu na fujo kwa kujipa mamlaka asiyokuwa nayo ya kutuamulia nani awe Mwenyekiti wa Chama, hatua ambayo imesababisha mtu anayeitwa Ibrahim Haruna Lipumba na genge lake tarehe 24 Septemba, 2016 kuvamia na kuhodhi jengo la Ofisi Kuu ya Chama iliyopo Buguruni, Dar es Salaam, Bodi ya Wadhamini ya Chama iliona kuna haja ya kukutana na kuchukua hatua za kukabiliana na matukio hayo.

Bodi ya Wadhamini ya The Civic United Front (CUF – Chama Cha Wananchi) imefanya kikao chake, tarehe 2 Oktoba, 2016 katika Makao Makuu ya Chama, mjini Zanzibar chini ya Mwenyekiti wake, Mhe. Abdallah Said Khatau.

Tumefanya hivyo kwa kutambua wajibu wetu kwa mujibu wa Sheria ya Vyama vya Siasa, Sura 258 ya Sheria za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (Political Parties Act, Cap 258) na Katiba ya CUF ya 1992 (Toleo la 2014).

Ni vyema ieleweke kwamba kwa mujibu wa Sheria ya Vyama vya Siasa, kila chama cha siasa chenye usajili wa kudumu kinapaswa kuunda Bodi ya Wadhamini ambayo ndiyo inayokuwa mmiliki na msimamizi wa mali zote za chama cha siasa husika. Kifungu cha 21 cha Sheria ya Vyama vya Siasa kinalieleza hilo kama ifuatavyo:

“21. —(1) Every political party which has obtained a certificate of full registration shall appoint a board of trustees to manage the properties and any business or investment of the party.

(2) Every board of trustees shall be duly incorporated under the Trustees Incorporation Act and every party shall, not later than sixty days from the date of full registration, submit to the Registrar—
a) the names and addresses of the members of ther board of trustees; and
b) a copy of the certificate of incorporation.”

CUF kilitimiza masharti hayo ya kisheria kwa kuunda Bodi ya Wadhamini, na Katiba ya Chama ya 1992 (Toleo la 2014), Ibara ya 98 ikafafanua zaidi namna inavyopatikana, pamoja na nguvu na uwezo wake kichama, kama ifuatavyo:

“98._ (1) Kutakuwa na Bodi ya Wadhamini ya Chama itakayoteuliwa na Baraza Kuu la Uongozi la Taifa kwa mujibu wa sheria za nchi kwa kipindi cha miaka mitano (5) na mjumbe anaweza kuteuliwa tena baada ya muda wake kumalizika.

(2) Bodi itakuwa na wajumbe wasiozidi tisa (9), watano (5) kutoka Bara angalau wawili (2) wakiwa ni wanawake na wanne (4) kutoka Zanzibar angalau mmoja (1) akiwa ni mwanamke ambao watateuliwa kwa masharti yanayohitajika ya Sheria ya Bodi ya Wadhamini na utaratibu uliowekwa na Baraza Kuu la Uongozi la Taifa.

(3) Bodi ya Wadhamini itakuwa ndiyo mdhamini pekee wa fedha na mali za Chama pamoja na madeni na itafanya shughuli zake kwa mujibu wa sheria na taratibu zilizowekwa na sheria ya nchi inayohusu Wadhamini.

(4) Bodi inaweza kushitaki au kushitakiwa kwa niaba ya Chama.

(5) Bodi itawajibika kwa Baraza Kuu la Uongozi la Taifa la Chama ambalo linaweza kuweka utaratibu unaofaa wa kuendesha shughuli za Bodi hiyo, na itafanya vikao vyake angalau mara mbili kwa mwaka.

(6) Mwenyekiti na Naibu Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini watachaguliwa na Wajumbe wa Bodi kutoka miongoni mwao, kwa sharti kwamba Mwenyekiti akitoka upande mmoja wa Jamhuri ya Muungano, Naibu Mwenyekiti atatoka upande mwengine wa Jamhuri ya Muungano.”

MAAMUZI YA BODI YA WADHAMINI:
Kufuatana na uwezo wake uliotajwa hapo juu na kwa kuzingatia nafasi yake kama mdhamini pekee wa fedha na mali za Chama (rejea Ibara ya 98(3) iliyotajwa hapo juu, Bodi ya Wadhamini imefikia maamuzi yafuatayo:

1. Imepuuza wito wa mtu anayeitwa Ibrahim Haruna Lipumba alioutangaza jana kwamba eti amemtaka mtu mwengine anayeitwa Thomas Malima kuitisha kikao cha Bodi ya Wadhamini. Lipumba kwa sasa si Mwenyekiti tena wa CUF na pia si mwanachama wa CUF baada ya kufukuzwa uanachama na Baraza Kuu la Uongozi la Taifa.

2. Itaendelea kuwajibika kwa Baraza Kuu la Uongozi la Taifa la Chama kama inavyotakiwa na Ibara ya 98(5) ambalo ndilo linaloiteua Bodi na litaheshimu maamuzi yote ya Baraza Kuu la Uongozi la Taifa likiwa ndiyo chombo chenye dhamana ya kusimamia uongozi na uendeshaji wa Chama.

3. Itachukua hatua za kisheria chini ya uwezo wake iliopewa na Ibara ya 98(3) na 98(4) kurejesha chini ya dhamana yake mali zote za Chama zilizovamiwa, kuporwa na kuhodhiwa na Ibrahim Lipumba na genge lake ikiwemo jengo la Ofisi Kuu ya Chama iliopo Buguruni, Dar es Salaam.

4. Itachukua hatua za kisheria chini ya uwezo wake iliopewa na Ibara ya 98(4) dhidi ya Ibrahim Lipumba kumtaka alipe gharama na hasara zote alizozisababisha kwa kuvamia Mkutano Mkuu Maalum wa Taifa wa Chama, tarehe 21 Agosti, 2016 katika Ukumbi wa Blue Pearl, Ubungo Plaza na genge lake kufanya vurugu, ghasia na uharibifu wa mali za hoteli na hatimaye kuvuruga Mkutano Mkuu jambo lililosababisha hasara ya takriban Sh. 600 milioni; na kisha kuvamia Ofisi Kuu ya Chama, Buguruni, Dar es Salaam, tarehe 24 Septemba, 2016 ambapo alisababisha hasara ya takriban Sh. 50 milioni.

5. Itachukua hatua za kisheria chini ya uwezo wake iliopewa na Ibara ya 98(4) kwa kumshtaki Msajili wa Vyama vya Siasa kwa kuingilia maamuzi halali ya vikao halali vya Chama na kulazimisha kukichagulia Chama chetu Mwenyekiti kinyume na onyo lililowahi kutolewa na Mahakama Kuu dhidi ya Ofisi yake kutokuwa na mamlaka ya aina hiyo.

6. Inawahakikishia wanachama wote wa CUF wa Tanzania Bara na Zanzibar kwamba Bodi yao ya Wadhamini iko makini na itasimama pamoja nao kulinda mali zote za Chama.

7. Inaionya Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa iwache kuingilia mambo ya ndani ya uongozi na uendeshaji wa Chama cha CUF.

HAKI SAWA KWA WOTE

Abdallah Said Khatau
MWENYEKITI WA BODI

Joran Lwehabura Bashange
KATIBU WA BODI

Rais Magufuli Amkabidhi Vifaa Vya Ujenzi Mjane Mkoani Kagera.

$
0
0
Na Eleuteri Mangi-MAELEZO.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemchangia vifaa vya ujenzi Mjane Agripina Angelo Mkazi wa Kitoma Wilayani Karagwe Mkoani Kagera.

Akimkabidi vifaa hivyo kwa niaba ya Rais, Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali (Mst) Salum Kijuu alisema kuwa Rais Dkt. Magufuli amefanya hivyo baada ya kuona kupitia vyombo vya habari jitihada za Mjane huyo kuanza kuijenga nyumba yake upya kutokana na kuharibika baada ya tetemeko la ardhi lililotokea mkoani humo mapema mwezi septemba.

Aidha Mkuu wa Mkoa Kijuu alitoa wito kwa wananchi ambao hawajaanza juhudi za kurejesha makazi yao waige mfano wa mjane huyo kwa kuanza ujenzi wa nyumba zao.

Akizungumza baada ya kukabidhiwa vifaa hivyo Bi. Agripina alisema kuwa anamshukuru Rais kwa mchango huo kwani vifaa hivyo vitamsaidia kukamilisha ujenzi wa nyumba yake na hatimaye kupata mahali pa kuishi yeye na familia yake baada ya nyumba yake ya awali kuharibiwa na tetemeko la ardhi.

Vifaa alivyokabidhiwa mjane huyo ni pamoja na Mbao pisi 30, Mabati 35 ya futi kumi ,Saruji mifuko 25 ,Misumari ya mabati kilo 4, Misumari ya kenchi kg 7 na waya za kufungia makenchi kilo 3.
Mjane Agripina Angelo mkazi wa Kitoma Mkoani Kagera akimuonesha Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali (Mst) Salum Kijuu nyumba aliyoijenga baada ya nyumba yake ya awali kuharibiwa na tetemeko la ardhi

Rais wa DRC Joseph Kabila awasili nchini Kwa Ziara ya Siku Tatu

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) Mhe. Joseph Kabila Kabange, amewasili hapa nchini jana tarehe 03 Oktoba, 2016 kwa ziara rasmi ya kiserikali ya siku tatu na kupokelewa na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.

Pamoja na Rais Magufuli viongozi wengine waliompokea Rais Joseph Kabila Kabange ni Makamu wa Rais Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama, viongozi mbalimbali wa Serikali, Mabalozi na wananchi.

Katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam, Rais Joseph Kabila Kabange alipokea heshima ya kupigiwa mizinga 21 na kukagua gwaride rasmi lililoandaliwa kwa ajili yake na baadaye kushuhudia burudani ya vikundi vya ngoma.

Leo tarehe 04 Oktoba, 2016 Rais Joseph Kabila Kabange atafanya mazungumzo rasmi na mwenyeji wake Rais John Pombe Magufuli, ataweka jiwe la msingi la jengo la Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) na baadaye kushiriki dhifa ya kitaifa iliyoandaliwa na Mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na mgeni wake wake Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Joseph Kabila wakati nyimbo za Taifa za mataifa yote mawili zikipigwa kabla ya ukaguzi wa gwaride lililoandaliwa kwa ajili ya heshima yake.

UPDATED!: List Ya Vyuo Vilivyotoa Selection Ya Majina Ya Wanafunzi Waliochaguliwa Vyuo Vikuu Mbalimbali 2016/2017

$
0
0

Kuona Majina Ya Wanafunzi Waliochaguliwa Chuo Kikuu 2016/2017,
 
 ==>Chuo Kikuu Arusha    <<bonyeza Hapa>>

==>Chuo Cha Mipango Dodoma   <<bonyeza Hapa>>


==> Sokoine University- SUA   <<Bofya Hapa>>

==>Chuo Kikuu Suza-zanzbar  <<bonyeza Hapa>>

==>Chuo Kikuu Saut-mbeya      <<bonyeza Hapa>>


==>Chuo Kikuu Saut-arusha     <<bonyeza Hapa>>
 
==>Chuo Cha MUM-Morogoro(2nd Round)   <<bonyeza Hapa>>

==>Chuo Cha Ushirika-moshi MUCCOBS(MoCU)   <<bonyeza Hapa>>

==>Chuo Cha Maji-ubungo   <<bonyeza Hapa>>

==>Chuo Cha Tumaini- Dar  << bonyeza Hapa>>

==>Chuo Kikuu Ardhi    <<bonyeza Hapa>>

==>Chuo Kikuu Sekomu     <<bonyeza Hapa>>

==>Chuo Cha Mweka-moshi      <<bonyeza Hapa>>

 ==> 
Chuo Kikuu St. John's Dodoma   <<Bonyeza  Hapa>>

==> Chuo cha Tax Management- ITA  <<Bonyeza Hapa>>

==> Chuo Kikuu Huria -OUT  <<Bonyeza Hapa>>
 
==> TEKU     <<Bonyeza Hapa>>
 
 ==>Chuo Kikuu Ruaha   <<Bonyeza Hapa>>
 
==> Chuo Kikuu Iringa    << Bonyeza Hapa>>
 
==> Chuo kikuu Bugando  <<Bonyeza Hapa>>
 
==>Chuo  Kikuu Cha Mwalimu Nyerere  <<bonyeza Hapa>> 

==>Chuo  Kikuu Cha  Udsm,duce Na Muce   <<bonyeza Hapa>> 

==>Chuo  Kikuu Cha  Tumaini Makumira    <<Bonyeza Hapa>>   

==>Chuo  Kikuu Cha Udom  <<bonyeza Hapa>>

 ==>Chuo  Kikuu Cha Ifm <<bonyeza Hapa>>

==>Chuo Kikuu Marian << Bonyeza Hapa>>

 ==>Chuo Kikuu Cbe        << Bonyeza Hapa>>

==>Tumaini-mbeya     << Bonyeza Hapa>>& <<hapa>>

 ==>Chuo Kikuu Mum         << Bonyeza Hapa>>

==>Chuo Mum(Diploma) <<Bonyeza Hapa>>

 ==>Chuo- Stella Maris  << Bonyeza Hapa>>

 ==>Chuo- Kampala-kiu  << Bonyeza Hapa>>

Benki Ya NMB Yadhamini Timu Ya Mashua Kwenye Mashindano Ya Mashua Afrika

$
0
0

Kwa kutambua umuhimu wa michezo kwa vijana nchini, benki ya NMB imedhamini vijana watano kutoka nchini kwa ajili ya kwenda kushiriki mashindano ya mashua ya Afrika yanayotarajiwa kufanyika Luanda, Angola kuanzia Oktoba 6 - 13, mwaka huu.Akizungumzia udhamini huo wa Milioni 10 na jezi kwa vijana hao. 

Mkurugenzi Mtendaji wa NMB nchini, Ineke Bussemaker amesema NMB kama benki ya kitanzania inawathamini watanzania wote na inajivunia kuwa sehemu ya makampuni ambao yameidhamini timu hiyo ili ikaiwakilishe nchi katika mashindano ya mashua.
Mkurugenzi Mtendaji wa NMB nchini, Ineke Bussemaker akizungumzia udhamini wa NMB kwa timu ya vijana ya mashua ambayo inataraji kushiriki Mashindano ya Afrika ya Mashua.

“NMB ni benki ambayo inaongoza Tanzania na ipo kwa ajili ya watanzania, moja ya sehemu ambayo tunaihudumia ni vijana, tunadhamini michezo mingi na tunaamini ni sehemu nzuri kwa vijana wadogo maana wanatakiwa kuandaliwa mapema,

“Mchezo wa mashua una wachezaji wengi, NMB inajivunia kuwa sehemu ya wadhamini kwa vijana hawa ambao watawakilishi nchi, na tunaamini watarudi kutoka Angola wakiwa na medali,” alisema Ineke.

Nae Makamu Mwenyekiti wa Chama Mashua Tanzania (TSA), Philimon Nassari aliishukuru NMB kwa msaada ambao imewapatia na kuelezea changamoto mbalimbali ambazo zimekuwa zikiukabili mchezo huo kutokana na kutokuwa na wadhamini wanaowasimamia na kuwaomba NMB kuendeleza udhamini huo kwa kipindi kirefu zaidi.
Makamu Mwenyekiti wa Chama Mashua Tanzania (TSA), Philimon Nassari akiishukuru NMB kwa kuipa timu ya vijana udhamini na kuelezea changamoto ambazo zinawakabili.

“Chama chetu ndiyo kina dhamana ya kuongoza mchezo wa mashua nchini, mchezo huu sio mgeni hata watu wanaovua ngalawa wanatumia mashua, mchezo wetu unadumaa kwasababu hatuna udhamini na kama mnavyojua mchezo huu unachezwa sehemu ya wazi kwahiyo hakuna anayelipa pesa, muda wote niwa kujitolea,

“Mchezo huu kwa sasa nchini unakuwa kama unashuka, tulianza kushiriki na watoto 12 lakini kwa sasa tunakwenda na watoto watano, mwanzo mgumu lakini sisi tunaongeza juhudi na tunawashukuru NMB kwa hili wamelolifanya,” alisema Nassari.
Mwakilishi wa Dar es Salaam Yacht Club, Robert Cunnane akizungumzia jinsi klabu yao inavyoisaidia timu ya mashua.

Kwa upande wa Mwakilishi wa Dar es Salaam Yacht Club, Robert Cunnane alisema klabu yao imekuwa ikiwasaidia watoto mbalimbali ambao wanacheza mchezo wa mashua kwa kuwapa nafasi ya kujifunza lakini pia muda mwingine kuwalipia fedha kwa ajili ya kwenda kujifunza mchezo huo na matarajio ya klabu hiyo ni kuona mchezo wa mashua unakuwa maarufu nchini.

“Tumekuwa tukisaidia mchezo wa mashua lakini kutoa udhamini kwa kutumia Milioni 24 kila mwaka kwa watoto kwenda kujifunza mchezo wa mashua na kwenda kushiriki mashindano mbalimbali, tunajivunia kuwa na hii timu na tunataka kuona timu hii inapata mafaikio,” alisema Cunnane.
Mkurugenzi Mtendaji wa NMB nchini, Ineke Bussemaker akimkabidhi jezi Kocha wa Timu ya Mashua, Penny Alson.

Vodacom Tanzania Kuendelea Na Gulio La Simu-Janja Kwa Bei Nafuu Kupitia Kampeni Mpya Ya #Bandukakijanja

$
0
0
Kampuni ya simu za mkononi chini, Vodacom Tanzania baada ya kufanya gulio mwisho wa wiki iliyopita ambapo simu imara ziliuzwa kwa bei nafuu kuwahi kutokea. Kampuni hiyo inaendelea kuwawezesha Watanzania kumiliki simu imara kwa bei nafuu kwa kuendelea na gulio katika maduka yao 

“Hatutoacha hadi kila Mtanzania awe ameunganishwa” kauli ya Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Ian Ferrao.


Kwa taarifa tulizonazo ni kwamba simu zinazopatikana ni pamoja na Smart 7, SmartKicka, Tecno, Itel na Huawei. 

Mteja akifika dukani kwa ajili ya kununua simu mojawapo ya simu hizi anatakiwa kununua kifurushi tu atapatiwa simu ya kijanja na orijino kulingana na kifurushi alichonunua. 

Mfano, mteja akinunua kifurushi chenye dakika 1,400, SMS 10,000 na 5GB za intaneti atapewa Smart 7 BURE kabisa.
Simu zote zitakuwa zimeunganishwa na intaneti ambapo mitandao kama Facebook, Twitter, WhatsApp, Snapchat na Instagram tayari zimeingizwa kwenye simu. Unaweza kutembelea kurasa za Vodacom Tanzania za mitandao ya kijamii kufahamu zaidi au duka la Vodacom lililo karibu yako

Facebook: https://www.facebook.com/tzvodacom
Twitter: https://www.twitter.com/VodacomTanzania
Instagram: www.instagram.com/vodacomtanzania
 

Aliyetoa taarifa za maiti kufufuka ikiwa mochwari Singida ashikiliwa na Polisi

$
0
0
Jeshi la polisi mkoa wa Singida, linamshikilia askari mgambo mwajiriwa hospitali ya mkoa, MG 7822 Emmanuel Daghau (42) kwa tuhuma ya kutoa taarifa za uongo juu ya maiti kufufuka ikiwa kwenye chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali ya mkoa.

Imedaiwa kuwa uongo huo ulizua mtafaruku mkubwa kwa ndugu na jamaa wa merehemu Rahel Erasto (28), aliyekuwa mkazi wa Minga manispaa ya Singida.

Kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Singida, SSP Mayala Towo, alisema tukio hilo limetokea Septemba, 30 mwaka huu, majira ya alasiri huko katika hospitali ya mkoa mjini hapa.

Akifafanua, kaimu kamanda huyo alisema kuwa Septemba, 29 mwaka huu Rahel (marehemu) alifikishwa katika hospitali hiyo ya mkoa, kwa ajili ya kupata huduma za kujifungua salama.

“Kutokana na sababu za kitabibu Rahel, alishindwa kujifungua kwa njia ya kawaida na hivyo ililazimika kufanyiwa upasuaji ambapo mtoto wa kiume alitolewa akiwa hai, Lakini mama kwa bahati mbaya alifariki dunia usiku saa saba Septemba, 30. Mimba hiyo ilikuwa ya kwanza kwa marehemu Rahel,” alisema kaimu kamanda huyo.

Akifafanua zaidi, alisema kuwa baada ya Rahel kufariki dunia, mwili wake ulipelekwa mochwari ambapo kesho yake, ndugu walijikusanya eneo hilo wakijadiliana namna kuuchukua mwili kwa ajili ya kwenda kuzika.

Alisema kuwa wakati ndugu wakiendelea kuzungumzia masuala ya mazishi, alijitokeza mlinzi Daghau na kuwaeleza kuwa ndugu yao huyo, alifariki kutokana na uzembe na kwamba usiku akiwa kwenye doria za kawaida, alisikia marehemu akipiga chafya na aliposogelea dirishani, alimwona akiwa amefufuka.

Towo alisema kuwa awali mgambo huyo baada ya kuhojiwa na Polisi, alikiri kumwona marehemu huyo akiwa amefufuka na alisikia akipiga chafya. Alikiri kwa maandishi na kuweka saini yake.

Alisema lakini baada ya Emmanuel kubaini kuwa baadhi ya ndugu wa marehemu na watoa huduma za afya hospitali ya mkoa kudai kuwa Rahel amefariki dunia kutokana na matatizo ya kawaida ya uzazi na wala hakufa na kufufuka, alipohojiwa mara ya pili, alikana maelezo yake ya awali aliyotoa kwa Polisi.

Wifi wa marehemu Rahel, Mary Mpaki, alikiri kuwa alimsikia mlinzi Emmanuel wakati akiwatangazia waombolezaji kuwa marehemu amefariki dunia kutoka na uzembe wa madaktari, na kwamba alipelekwa chumba cha kuhifadhia maiti akiwa hai.

“Kama ndugu wa marehemu ambao baada ya kufanyiwa upasuaji kuna ndugu ambao walitaka kulala wodini lakini hawakuruhusiwa.Tuliposikia maneno ya mlinzi huyo, tuliamini kwa asilimia mia moja maneno yake kwamba Rahel alipelekwa mochwari akiwa bado yu hai,” alisema kwa masikitiko.

Mary alisema baada ya taarifa ya mlinzi huyo, walienda moja kwa moja kituo cha Polisi kutoa taarifa hizo za kusikitisha.

Ndugu wa marehemu ambaye hakutaka jina lake litajwe, alisema taarifa iliyotolewa na mlinzi kuwa Rahel alifufuka na kupiga chafya, zitakuwa ni za ukweli kwa sababu Ni mtu mwenye akili, hawezi kudanganya jambo hilo.

“Tunasikia kwamba mlinzi kala matapishi yake kwa kitendo cha kukanusha taarifa alizotoa awali kituo cha Polisi. Kama amefanya hivyo, itakuwa kuna shinikizo amepata hivyo anatafuta njia ya kujiokoa,” alisema.

Kaimu mganga mkuu wa mkoa, Dk.Ramadhani Kabala, alikiri kuwepo kwa taarifa hizo na kudai kwa sasa mwili wa marehemu unaendelea kufanyiwa uchunguzi, ili kutambua kama kweli Rahel alifufuka na kupiga chafya akiwa ndani ya chumba cha kuhifadhia maiti.

“Ingawa si rahisi binadamu kufufuka baada ya kufariki dunia, lakini hatuwezi kuzipuuza taarifa hizi za mlinzi. Ipo timu inaongozwa na daktari bingwa kutoka wiraza ya mambo ya ndani, Dk.Ahmed Makata inaendelea na uchunguzi wa kina. Kwa hiyo baada ya kumalizika kwa uchunguzi, tutawaita waandishi wa habari kuwaeleza ukweli ili muweze kuitaarifu jamii,” alisema Dk.Kabala.

Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Singida, Mhandisi Mathew Mtigumwe, alikiri kupokea taarifa hiyo ya aina yake, na kwamba zipo timu mbili zinaendelea na kuchunguzi ili ukweli uweze kubainika.

Na Nathaniel Limu, Singida

Wananchi Walioua Watafiti Wakimbia Kijiji Wakihofia kukamatwa na Jeshi la Polisi........Miili Ya Marehemu Yaagwa Jijini Arusha

$
0
0
Baada  ya baadhi ya wakazi wa Kijiji cha Iringa Mvumi katika  Wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma kuwaua watafiti wa Kituo cha Udongo na Maendeleo cha Selian Arusha, wakazi wa kijiji hicho wamehama makazi yao wakihofia kukamatwa na Jeshi la Polisi.

Waandishi wa habari waliofika kijijini hapo jana na walishuhudia hali ya utulivu kijijini hapo tofauti na ilivyozoeleka.

Pamoja na wananchi hao kukimbia makazi yao, taarifa zinasema viongozi wote wa Serikali ya Kijiji hicho  wamekamatwa na polisi wakiwamo Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji, Albert Chimanga na Diwani wa Kata ya Iringa Mvumi, Robert Chikole.

Mmoja wa wakazi wa kijiji hicho aliyejitambulisha kwa jina la Michael Kagisi, alisema kitendo cha wananchi kukimbia kijiji hicho kimesababisha shughuli nyingi za  jamii kusimama   na maduka kufungwa.

Kwa mujibu wa Kagisi, hata wananchi   waliobaki kijijini hapo wakisema    hawakushiriki mauaji hayo, ikifika jioni wanakwenda porini kulala.

“Sehemu kubwa ya watu wameyakimbia makazi yao kwa sababu wanaogopa kukamatwa na polisi, yaani hata shule hazina wanafunzi kwa sababu wengi wamekimbia na wazazi wao.

“Yaani waliouawa waliuawa kwa makosa kwa sababu  kabla ya kuwapiga, walijitetea na kujitambulisha, lakini wananchi hawakutaka kuwasikiliza…   baada ya kuwaua, waliwawekea majani na kuwachoma moto ili wafe haraka,” alisema Kagisi.

Akifafanua, mwananchi huyo alisema siku ya tukio ulikuwapo mkutano kijijini hapo na mwenyekiti wa kijiji alipata taarifa kwamba katika eneo la kutengeneza chumvi, kuna gari ambalo walilitilia shaka kwamba huenda ni majambazi.

“Siku hiyo tulikuwa kwenye mkutano na baadaye tulimuona mwenyekiti akiwaita baadhi ya vijana na kuwaagiza waende eneo la tukio.

“Wale vijana walikwenda huko  walipiga simu kijijini kuwaeleza wananchi, kwamba kuna gari la watu ambao hawaeleweki.

“Taarifa hizo ziliposambaa, wananchi walihamasishana na kuelekea eneo la tukio.

“Walipofika tu, walianza kuwapiga, lakini wale watafiti walijieleza kwamba wao siyo majambazi, huku wakiwaomba wananchi wawapeleke katika ofisi zao za kijiji, lakini wananchi walikataa na kuendelea kuwapiga hadi walipowaua,” alisema.

Naye  Mchungaji wa Kanisa la Biblia kijijini hapo, Donald Nyambuya, alisema kwa sasa maisha kijijini hapo ni ya shida kwa sababu huduma nyingi za  jamii zimefungwa baada ya watu kukimbia makazi yao.

Mwinjilisti wa Kanisa la Waadventista Wasabato (SDA), Jacob Foda, alisema kitendo cha watu kukimbia makazi yao  kimeathiri huduma ya  roho kwa kuwa huwa na kawaida kuwatembelea waumini wake.

Wakati huohuo, simanzi na majonzi, jana, vilitawala wakati wa kuaga miili ya Watafiti wa Kituo cha Utafiti wa Udongo na Maendeleo cha Selian mjini hapa.

Watafiti hao waliuawa juzi na wananchi wa Kijiji cha Iringa Mvumi, wilayani Chamwino, Mkoa wa Dodoma kwa kukatwakatwa mapanga na kuchomwa moto.

Miili hiyo iliwasili mjini hapa jana asubuhi kwa gari ikitokea Dodoma na kuingizwa kwenye eneo la wazi la kituo hicho kilichopo pembeni mwa Uwanja mdogo wa Ndege wa Arusha kwa ajili ya wafanyakazi kutoa heshima za mwisho.

Shughuli ya kuaga miili hiyo ilifanyika asubuhi kwa wafanyakazi, jamaa na marafiki kutoa heshima za mwisho bila majeneza kufunguliwa kwa kuwa imeharibika.

Baadaye  ilipelekwa katika Hospitali ya Mkoa wa Arusha ya Mount Meru kwa ajili ya kufanyiwa maandalizi ya kusafirishwa.

Waliouawa katika tukio hilo  walitambuliwa kuwa ni Jaffari Mafuru aliyesafirishwa jana kwenda Mara kwa mazishi, Theresia Ngume, aliyetarajiwa kuzikwa jana mjini Arusha na dereva wa gari walilokuwamo,       STJ 9570 aina ya Toyota Hilux, mali ya Kituo cha Utafiti cha Selian, Nikas Magazine, aliyesafirishwa kwenda Ifakara, Morogoro kwa mazishi.

Watafiti hao  waliuawa wakiwa katika kazi ya mradi unaoandaa taarifa za hali ya udogo kwa nchi nzima.

Akizungumza baada ya kutoa heshima za mwisho, Mkurugenzi wa Kituo hicho, Januari Mafuru ambaye ni baba mzazi wa marehemu Jaffari, alisema tukio hilo limemuumiza sana.

Alisema kituo hicho kimekuwa kikiendesha mradi huo kwa lengo la kuwasilisha taarifa hizo kwa wakulima wadogo na wataalamu wa kilimo  ziweze kuwasaidia wananchi katika kilimo na hatimaye kuongeza mazao.

“Mradi huu umemaliza utafiti katika Mikoa ya Kanda ya Kaskazini ya Kilimanjaro, Arusha na Manyara. Baada ya hapo kazi nyingine ilikuwa imeanza Kanda ya Kati Dodoma na Singida.

“Wiki iliyopita, tuliandaa watafiti wanane na magari yao manne kwa ajili ya kwenda mkoani Dodoma kukusanya udongo kwa ajili ya kuuleta hapa kwenye maabara za Seliani kufanyiwa utafiti kisha kutoa matokeo yatakayowarudia wakulima,” alisema Mafuru.

Akizungumzia kuwasili kwa watafiti hao katika Kijiji cha Iringa Mvumi, wilayani Chamwino yalikotokea mauaji hayo, Mafuru alisema timu zote zilikuwa na barua za utambulisho pamoja na vifaa vya kazi.

“Timu iliyokuwa Chamwino katika Kijiji cha Iringa Mvumi, iliwakuta wanawake wakiendelea na shughuli za kukusanya chumvi  na watafiti waliwasilimia na kujitambulisha wametokea wapi.

“Taarifa tulizonazo ni kwamba, baada ya kusalimia, watafiti waliacha gari pembeni na kutembelea maeneo   kuchagua udogo.

“Huku nyuma kundi la wale wanawake lilitoa taarifa kwa viongozi wao kuwa wamevamiwa na wanyonya damu, ndipo walipotokea watu wakiwa na mashoka na mapanga na   kuwashambulia kabla ya kuwachoma moto,” alisema.

Mtafiti Mwandamizi wa Kituo cha Selian, Dk. Lameck Makoye, alilaani mauaji hayo na kusema hajawahi kuona wala kusikia watafiti wakivamiwa   wanapokuwa   vijijini.

“Naamini Serikali imeona, binafsi sijawahi kuona tukio la aina hii kwa sababu  watafiti wale walikuwa na vielelezo vyote vinavyowatambulisha.

“Hata mradi waliokwenda kufanya ulikuwa ni kwa faida ya wananchi wa Kijiji cha Iringa Mvumi kwa vile umelenga maeneo ya nchi nzima.

“Sisi Kituo cha Utafiti cha Selian ndiyo tunaoleta maendeleo ya mkulima kwa nchi nzima kwa kufanya utafiti wa udongo unaomwezesha mkulima alime vipi na atumie mbolea kwa kiwango gani na ya aina gani,” alisema Dk. Makoye.

Mume wa marehemu Theresia, Jonas Mjema, akizungumza kwa huzuni kuhusu  kuondokewa na mkewe, alisema kabla ya tukio la mkewe kuchomwa moto, alizungumza naye asubuhi kujua anaendeleaje.

“Niliwasiliana naye asubuhi Jumamosi tukatakiana kazi njema, ilipofika jioni nilimtafuta lakini simu yake haikupatikana.

“Nilijipa matumaini labda mawasiliano hayakuwa mazuri kwa vile shughuli zao ni za porini.

“Ilipofika Jumapili, nilipigiwa simu na shemeji yangu akinipa taarifa za tukio la kuchomwa moto mke wangu,” alisema Mjema aliyeachwa na watoto wawili.

Rais Magufuli ampongeza Balozi Prof. Joram Mukama Biswaro kwa uteuzi wa AULOSS.

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, amempongeza Balozi Prof. Joram Mukama Biswaro kwa kuteuliwa kuwa Mwakilishi Maalum wa Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika na Mkuu wa Ofisi ya Umoja huo Sudan Kusini.

Balozi Prof. Joram Mukama Biswaro ameteuliwa na Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika (AU) Dkt. Nkosazana Dlamini-Zuma na anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Brigedia Jenerali Sara Thomas Rwambali ambaye amemaliza muda wake.

Katika pongezi hizo Rais Magufuli amesema Tanzania imepokea uteuzi huo kwa heshima kubwa na ipo tayari kutoa ushirikiano wowote utakaohitaji kwa Balozi Joram Mukama Biswaro katika utekelezaji wa majukumu yake.

“Natambua kazi kubwa iliyopo mbele yako katika nafasi hiyo muhimu ndani ya Umoja wa Afrika (AU), hata hivyo kwa kutambua uwezo wako, uzoefu wako na uchapakazi wako naamini kuwa utatekeleza majukumu yako kwa viwango vya hali ya juu na Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika Dkt. Nkosazana Dlamini-Zuma hatajutia uamuzi wake wa kukuteua katika nafasi hiyo” amesema Rais Magufuli.

Dkt. Magufuli amemtakia heri Balozi Prof. Joram Mukama Biswaro katika majukumu hayo mapya, na amemshukuru na kumpongeza Brigedia Jenerali Sara Thomas Rwambali aliyemaliza muda wake kwa uwakilishi mzuri katika kipindi chake.

Aidha, Rais Magufuli ambaye ndiye aliyempendekeza Balozi Prof. Joram Mukama Biswaro kushika nafasi hiyo, amemshukuru Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika Dkt. Nkosazana Dlamini-Zuma kwa kuridhia mapendekezo yake.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam

04 Oktoba, 2016
-----
 

Polisi Aliyerekodiwa Akipokea Rushwa Kuchukuliwa Hatua

$
0
0
Jeshi  la Polisi visiwani Zanzibar, limesema litamchukulia hatua za kinidhamu ofisa wake mwenyewe cheo cha Sajenti ambaye alionekana hivi karibuni akipokea rushwa kutoka kwa raia wa kigeni.

Hatua hiyo, imekuja baada ya picha za video kusambaa katika mitandao ya kijamii, zinazomwonyesha askari huyo akipokea fedha ambazo hadi sasa hazijajulikana kiwango chake kutoka kwa raia huyo wa kigeni, ambaye alikuwa na kosa la kutofunga mkanda.

Katika video hiyo, raia huyo anaokana kutoa fedha na kumkabidhi askari huyo huku akiahidi kumsaidia ili asikamatwe mbele ya safari.

Tukio hilo lilitokea eneo la Mkokotoni Mkoa wa Kaskazini Unguja, ingawa askari huyo alitaja eneo la Mahonda akionyesha nia ovu ya kutenda kosa hilo bila kujijua kama anachukuliwa video.

Kamishna wa Jeshi la Polisi Zanzibar, Hamdani Omar Makame alisema jeshi hilo linampongeza raia huyo wa kigeni kwa kutoa taarifa hiyo.

“Jeshi la polisi linachukua nafasi hii kulaani kosa hili, licha ya kua ni kosa la jinai linalifedhehesha jeshi na kulitia doa kutokana na dhamana kubwa lililokabidhiwa,” alisema.

Alisema kwa mujibu  wa taratibu za jeshi hilo, tayari limeanza uchunguzi mara moja na kwamba litachukua hatua zinazostahili.

Kutokana na hali hiyo, Kamishina Hamdani amewataka wamiliki wa makampuni ya simu za mikononi kufufua mfumo wa upigaji simu kutumia namba za dharura ambazo ni 111 na 112 ili kuwarahisishia wananchi kutoa taarifa.

Video iko hapo chini

Tiba Ya Asili Ya Kuacha Punyeto Kwa Wanaume

$
0
0
Punyeto  ( kwa  wanaume  )  ni  kitendo   cha  mwanaume, kujifikisha  mwenyewe  kileleni  kwa  kujichua  uume  hadi  kumwaga  mbegu  za  kiume.  


Uchunguzi  unaonyesha  katika  watu  wa  jinsia  ya  kiume  kumi  wenye  umri  wa  kuanzia  miaka  16  hadi  45, angalau  wanne  kati  yao  wamewahi  kupiga  punyeto  katika  kipindi  fulani  cha  maisha  yao, na  wawili  kati  yao  wanajihusisha  na  upigaji  punyeto. 

Uzoefu  unaonyesha, asilimia  kubwa  ya  wanaume  wanao  piga  punyeto  huanza  katika  umri  wa  kubalehe  ( miaka  14-16  ), wengine  huachana  na  tabia  hiyo  mara  baada  ya  kupata  wapenzi  wa  kike  ama  kuoa  na  wengine  huendelea  na  tabia  hiyo  hata  baada  ya  kuoa .

 Zipo  sababu  mbalimbali  zinazo  wapelekea  wanaume  kupiga  punyeto, ila  kubwa  kati  ya  hizo  ni  pamoja  na  kutokuwa  na  wapenzi, kutokuwa  na  wapenzi  wanao  kidhi vigezo  vyao, kuwa  katika  mazingira  yasiyokuwa  na  wanawake  ( mfano  katika  shule  za  sekondari  za  bweni  za  wavulana  tu ), kujiepusha  na  hatari  ya  kupata  maambukizi  ya  v.v.u  nakadhalika

  ATHARI  ZA  PUNYETO    KWA  WAVULANA.
Punyeto  ina  athari  nyingi  na  kubwa  sana  kwa  wanaume  wanao  jihusisha  nayo, lakini  kwa  leo, tutaangalia  athari  moja  kubwa  kati  ya  nyingi. Athari  hii  si  nyingine  bali  na 
 KUUA  NGUVU  ZA  KIUME.  Mwanaume  anayepiga  punyeto  hutumia  nguvu  nyingi  kuibana  mishipa  inayo  fanya  uume  usimame. Mwisho  wa  siku  uume  hulegea  na  kusinyaa, na  kukosa  nguvu  kabisa  na  hatimaye  mhusika  kuwa  khanithi. Uchunguzi  unaoonyesha, kuna  idadi  kubwa  sana  ya  wanaume  wanao  sumbuliwa  na  tatizo  la  upungufu  wa  nguvu  za  kiume  kama  matokeo  ya  kupiga  punyeto  kwa  muda  mrefu. Athari  za  mwanaume  kutokuwa  na  nguvu  za  kiume, nadhani  zinajulikana, ila  kwa  faida  ya  wote  tutazizungumzia  kwa  kina  siku  za  mbele, lakini  kwa  ufupi  ni  aibu  kubwa  sana   kwa  mwanaume  kukubali  kuua  ufanisi  wa  uume  wake  kwa  sababu  ya  kupiga  punyeto.

MUNGU  HAPENDI  PUNYETO  :  (
 MIONGONI  MWA  WANANZUONI  WA  MASOMO  YA  BIBLIA  DHAMBI  YA  KUPIGA  PUNYETO  HUJULIKANA  KAMA  ONANISM  )

Kwa  mujibu  wa  maandiko  matakatifu, upigaji  punyeto  ni  moja  kati  ya  matendo  yanayo  muudhi  Mwenyezi  Mungu, kwa  sababu  yanapigana  na  utaratibu  aliouweka . Kwenye   kitabu  cha  MWANZO  38:9, Onan  mwana  wa  Yuda  aliagizwa  na  baba  yake  ( Yuda )  kwenda  kumjua  mke  wa  kaka  yake  ( Onan )  ili  aweze  kumzalia  watoto.   (  Kwa  mujibu  wa  mila  na  desturi  za  kiyahudi  wakati  huo, kaka  anapofariki  bila  kucaha  mtoto, ndugu  wa  kiume  wa  marehemu  hutakiwa  kwenda  kumuoa   mjane  aliye  achwa  na  kaka  yake, na  watoto  watakao  zaliwa  watabeba  jina  la  marehemu  kaka  yake..., aina  hii    ya  ndoa  hujulikana  kama   LEVIRATE  MARRIAGE  )Biblia  inasema, Onan  hakutaka  kumpa  mimba  mjane  wa  kaka  yake  ilihali  akijua  watoto  watakao  zaliwa  hawatakuwa  warithi  wake, hivyo  basi  kila  mara  alipokutana  kimwili  na  mjane  wa  kaka  yake, alimwaga  mbegu  zake  pembeni. Biblia  inasema  katika   kitabu  kile  cha  Mwanzo  38: 10  " 
 

" Alicho  kifanya  kilikuwa  ni    chukizo  kubwa  mbele  za  Mwenyezi  Mungu  hivyo  Mwenyezi  Mungu  akampa  adhabu  ya  kifo! " 



Umeona!  Kumbe  basi  adhabu  ya  kiroho  ya  tendo  la  masturbation  ni  “umauti!”. Umauti  huo  unaweza  usiwe  kama  ulio  mpata  Onan, ila  unaweza  kuja  katika  sura  tofauti. Mfano  kufa  kwa  nguvu  za  kiume, ni   adhabu  tosha  sana    kwa  mwanaume    yoyote  yule  duniani  na  inaweza  kuwa  kali  kuliko  hata  ile  aliyopewa  Onan.



DAWA    YA  ASILI  NA  YA  UHAKIKA  YA   KUKUFANYA  UACHE  KUFANYA  PUNYETO.

Uzoefu  unaonyesha, mtu  anayepiga  punyeto, hata  kama  ameathiriwa  na  tatizo  la  punyeto  kwa  kiwango  gani, endapo  atafanikiwa  kutopiga  punyeto  kwa  muda  wa  siku  arobaini  mfululizo, mtu  huyo  hatopiga  tena  punyeto  katika  siku  zote  za  maisha  yake  kwani  tayari  mtu  huyo  atakuwa  amerudia  katika  hali  yake  ya  kuto  kuwa  addicted  tena  na  upigaji  punyeto, na  atalichukia  kabisa  hata  jina  la  tendo  hilo  achilia  mbali  tendo  lenyewe.



UFANYE  NINI  ILI  USIPIGE  PUNYETO  KWA  MUDA  WA  SIKU  AROBAINI MFULULIZO!



Sio  rahisi  kwa  mtu  aliyekuwa  addicted  na  punyeto  kustahimili  kujizuia  kupiga  punyeto   kwa  muda  wa  siku  arobaini  mfululizo. Anaweza  kujizuia  kupiga  punyeto  kwa  siku  mbili  lakini  baada  ya  hapo  ataendelea  tena  na  mchezo  wako.


ATUMIE  DAWA  IPI?



PILIPILI

Pilipili  inayo  hitajika  hapa  ni  yoyote  ile  ili  mradi  iwe  kali  sana,  (  Ila  inayo  pendekezwa  ni  pilipili  mbuzi  ama  pilipili  kichaa, pilipili  hoho  haihusiki  hapa  ).



MATUMIZI

Kwanza  kabla  ya  kujua  matumizi  ni  vyema  ukatambua  muda  ambao  huwa  unapiga  punyeto  (  Mara  nyingi  huwa  ni  asubuhi  baada  ya  kuamka,wakati  wa  kuoga  ama  usiku  kabla  ya  kulala  ).



Chukua  pilipili  zako, zipasulie  kwenye   viganja  vya  vidole  vyako  na  kujipakaza  katika  viganja  vya  vidole  vyako.  Unaweza   kutumia  pili  moja  kwa  kila  kiganja, na  kwa  kila  muda  ambao  huwa  unapiga  punyeto  lakini   unaruhusiwa  kujipakaza  zaidi  ya  pilipili  moja.



Ukishajipaka  pilipili  kwenye  viganja  vya  vidole  vyako, moja  kwa  moja  unakuwa  umekwisha  jilazimisha  kutokufanya  punyeto, kwa  sababu  ukipiga  punyeto  kwa  viganja  ambavyo  vina  pilipili  utawashwa  sana  wala  hautaweza  kufurahia  tendo  hilo.



JAMBO  LA  KUZINGATIA  : Hakikisha  unakuwa  na  walau  pilipili mbili  mpaka  nne  kila  unapokuwa   katika  maeneo  ambayo  yanaweza  kukuchochea  kufanya  punyeto.



UFANISI  WA DAWA  HII : Dawa  hii  inawafaa  wale  tu  ambao  wamedhamiria  kutoka  mioyoni  mwao  kuacha   kufanya  punyeto. Kwa  wale  ambao  hawajadhamiria  haitaweza  kuwasaidia. 



MWISHO,TUNAWATAKIA  KILA  LA  HERI  WATU  WOTE  WATAKAO  AMUA  KUJARIBU  KUTUMIA  NJIA  HII  KUACHANA  NA   SUALA  LA  UPIGAJI  PUNYETO. TUTAFURAHI  SANA ENDAPO  MTATUPA    FEEDBACK  BAADA  YA  HIZO  SIKU  AROBAINI  TANGU  MUANZE  KUFANYA  ZOEZI  HILI. MUNGU AWAPE  NGUVU  NA  AWABARIKI. 



JINSI  PUNYETO  INAVYO  SABABISHA  TATIZO  LA  UKOSEFU  NA  UPUNGUFU  WA  NGUVU  ZA  KIUME.

Upigaji  punyeto  ni  miongoni  mwa  vyanzo  vikuu  vya  tatizo la ukosefu  na  upungufu  wa  nguvu  za  kiume.  Idadi  kubwa  ya  vijana  wenye  tatizo  la  ukosefu  na  upungufu  wa  nguvu  za  kiume, tatizo  lao  limesababishwa  na  suala  la  upigaji  wa  punyeto.

Ukitaka  kufahamu  jinsi  suala  la  upigaji  wa  punyeto  linavyo  sababisha  tatizo la  ukosefu  na  upungufu  wa nguvu , tembelea  link hii  hapa  chini:




TIBA  ASILIA  YA  NGUVU  ZA  KIUME  KWA  MWANAUME  ALIYE ATHIRIKA  NA  PUNYETO.

Dawa  asilia  iitwayo  JIKO, ni  dawa  inayo  tibu  na  kuponyesha  kabisa  tatizo  la UKOSEFU na  UPUNGUFU  wa  NGUVU ZA KIUME .


Dawa  hii  ni  ya asili  kabisa  na  IMETHIBITISHWA   na  MKEMIA  MKUU  WA  SERIKALI.

Dawa  hii  inatokana  na  mimea  iliyo  kwenye  orodha  ya  mimea  inayo  tambuliwa  na  Shirika  la  Afya  Duniani  ( W.H.O)

Dawa  hii  hutumika  pamoja  na  lishe  maalumu  inayo  tokana  na  mimea iliyo fanyiwa  tafiti  na kuthibitishwa  kisayansi.


JINSI  DAWA ASILIA  YA   JIKO  INAVYO  TIBU  NA KUPONYESHA  KABISA  TATIZO  LA  UKOSEFU  NA  UPUNGUFU  WA  NGUVU  ZA  KIUME.

Dawa  asilia  ya  JIKO, hutumika pamoja  na  lishe maalumu  kwa  ajili  ya kutibu  tatizo  la  ukosefu na  upungufu  wa  nguvu  za  kiume.

Jiko  pamoja  na  lishe  yake  maalumu, hufanya  mambo  yafuatayo :



1.Inasaidia   kuimarisha  mishipa  ya  uume  ulio legea  na  hivyo  kuufanya  uume  uwe  na uwezo  wa  kusimama  barabara  kama msumari  wakati  wa  tendo  la  ndoa.

2. Inasaidia  kusafisha  mishipa  na  misuli   ya  kwenye uume  na  hivyo  kusaidia  katika  kuongeza kasi  ya  msukumo  wa  damu kwenye mishipa  ya    uume.



3. Husaidia  kuongeza  damu  mwilini



4. Husaidia  kuongeza  msukumo(pressure)  wa damu  kwenye  mishipa  ya  uume  na  hivyo kuufanya  uume  kuwa  na  nguvu thabiti.



5. Huipa  misuli  ya  uume  uwezo  wa  kuziba na kuizuia  mishipa  ya  vena   kunyonya  damu kwenye  

mishipa  ya  uume  wakati  wa  tendo la  ndoa  na matokeo  yake  kukupa  uwezo wa  kufanya  tendo  

la  ndoa  kwa  muda  mrefu

               ( Kuzuia  hali  ya  kufika  kileleni haraka  )



6. Husaidia  kurelax  mind  na  hivyo  kumfanya mtu  awe  na  uwezo  wa  kuconcentrate  wakati wa tendo la  ndoa   bila  kuathiriwa  na msongo  wa  mawazo



7.  Hurejesha,kuimarisha  na  kuboresha ushirikiano  kati  ya  mishipa  ya  fahamu  ya  kwenye  ubongo  (nerves), mishipa  ya  kwenye  uti  wa  mgongo  pamoja  na  mishipa  ya  kwenye  uume



8. Humfanya  mwanaume  awe  na  uwezo  wa kurudia  tendo  la  ndoa  mara  nyingi  zaidi bila  kuchoka.



9. Husaidia  kuongeza  hamu  ya  tendo  la  ndoa.



10.            Husaidia kuurudisha  nje  uume ulioingia ndani.

. 11.Husaidia  kutibu  sideeffects  za  punyeto na  matumizi  ya  muda  mrefu  ya dawa  kali   (za  kizungu ) za  kuongeza  nguvu  za kiume.



12.                Husaidia  kutibu  chango  la  kiume.



13.  Husaidia  kuimarisha  mzunguko  wa  damu mwilini



14.  Husaidia  kutibu  maradhi  ya  moyo



15.      Husaidia  kuondoa  sumu  mwilini



16. Tiba  hii  ina   faida  kubwa

sana  kwa wagonjwa  wa  kisukari,kwani

husaidia  katika kusawazisha  kiwango  cha  

sukari  katika  damu.

17. Tiba  hii husaidia  kutia  nguvu  kwenye mishipa mwilini.

       18.   Husaidia  kuondoa  uchafu tumboni

19.          Husaidia kutibu  matatizo  katika  figo.

20.         Husaidia  kuimarishana na   kuongeza  homoni  za kiume.

21.   Husaidia  kudhibiti  kiwango  cha sukari  katika  damu

22.             Husaidia  kuzuia  kusanyiko la chembe  sahani,zinazo  sababisha  kuganda  kwa  damu.

23.      Husaidia  kupunguza  kolestrol  na mafuta  yasiyo faa  mwilini

24.        Husaidia  kushusha  vizuri  kiwango cha  shinikiz la  damu

25. Tiba hii  husaidia kutanuka  kwa mishipa  ya  damu.

26.  Husaidia  kuondoa  sumu  mwilini

27.Husaidia  kuweka  mlinganyo  sawa  wa  Homoni

28.  Tiba  hii         Husaidia  kutibu shinikizo  la  damu

29.Tiba  hii  husaidia  kuimarisha  msukumo  wa  damu mwilini

30.     Husaidia  kutibu  matatizo  ya  moyo

31.           Husaidia  kutibu  matatizo ya  ubongo

32.    Husaidia  kuboresha  utendaji  kazi  wa ini

33.      Husaidia  kuondoa sumu mwilini

34.  Husaidia  kutibu  tatizo  la  presha

35. Husaidia       kuongeza  stamina  mwilini

36.   Husawazisha  kiasi  cha acid aina  ya  Uric katika  damu

37. Husaidia   kuimarisha  mishipa  ya  damu

38. Husaidia kupunguza  kiasi  cha  mafuta  kwenye ini

39.Husaidia      kuzuia  magonjwa  ya  moy na  kiharusi

40. Husaidia   kumarisha  mishipa  ya  ubongo

BEI  YA  DAWA:  Dozi  ya  dawa  ya  JIKO inapatikana  kwa  gharama  ya  SHILINGI ELFU  THEMANINI  TU  (Tshs.80,000/=)





MAHALI  TUNAPOPATIKANA :

Dozi  ya  dawa  ya  JIKO, inatolewa  na  duka  la dawa  asilia  la  NEEMA  HERBALIST   NUTRITIONAL  FOODS  CLINIC. Tunapatikana jijini  DAR ES  SALAAM, katika  eneo  laUBUNGO   jirani  na   SHULE  YA MSINGI  UBUNGO  NATIONAL  HOUSING  nyuma  ya  jengo  la  UBUNGO  PLAZA.
 

Kwa  wasio  weza  kufika  ofisini  kwetu, tunatoa huduma  ya kuwapelekea  dawa  mahali  walipo ( DELIVERY )



Kwa  wateja  waliopo  nje  ya  DAR  ES  SALAAM, watatumiwa  dawa  kwa  njia  y mabasi, wateja  waliopo  Zanzibar, watatumiwa  dawa kwa   njia  y boti  na  kwa  wateja  waliopo Ulaya, America  na  Arabuni, watatumiwa dawa  kwa  njia  ya  DHL  au POSTA.



        WASILIANA  NASI  KWA  SIMU  NAMBA 



                           0766  53  83  84.



Na  kwa  maelezo  zaidi  kuhus huduma  zetu, endelea  kutembelea:
www.neemaherbalist.blogspot.com

Jeshi La Polisi Nchini Latoa Onyo Kali Kwa Wananchi Wanaojichukulia Sheria Mkononi.

$
0
0

JESHI la Polisi  nchini linatoa onyo kali kwa wote wenye tabia ya kujichukulia sheria mkononi kuacha mara moja, kwani takwimu za makosa ya kujichukulia sheria mkononi yaliyoripotiwa katika vituo vya Polisi katika kipindi cha Januari hadi Agosti 2016 ni matukio 705.

Katika matukio hayo yaliyoripotiwa, Jeshi la Polisi nchini limefanikiwa kuwakamata na kuwafikisha mahakamani watuhumiwa 393.

Hayo yametolewa katika taarifa kwa waandishi wa habari na Msemaji wa Jeshi la Polisi  Makao Makuu ya Polisi, ACP Advera Bulimba jijini Dar es Salaam leo.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa ni kosa  kuzipuuza sheria za nchi zilizopo na wakati mwingine kuzikiuka kwa makusudi na mbaya zaidi baadhi yao kufikia hatua ya kuwaua watu wasio na hatia kwa hisia.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa Mwananchi yeyote anapaswa kutoa taarifa kwa vyombo vya dola ili hatua za kisheria ziweze kuchukuliwa dhidi ya mhalifu au mtu yeyote wanayemtilia mashaka katika maeneo yao.
 
Aidha, Jeshi la Polisi nchini, litaendelea kuchukua hatua kali za kisheria kwa kufuatilia na kuwakamata watu wote wanaojihusisha na tabia za kujichukulia sheria mkononi.

Jeshi la Polisi linatoa wito kwa watu wote wakiwemo wenye ushawishi mkubwa katika jamii kuendelea kukemea na kutoa elimu juu ya madhara ya kujichukulia sheria mkononi

Tanzania na Congo DRC zimesaini mkataba wa makubaliano kutafuta mafuta Ziwa Tanganyika

$
0
0
Serikali ya Tanzania na nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC), wametiliana saini makubaliano ya kuimarisha ushirikiano wao katika nyanja mbalimbali ikiwemo suala la ulinzi na usalama pamoja uchimbaji wa mafuta katika ziwa Tanganyika.

Akiongea leo Ikulu Jijini Dar es Salaam mara baada ya kufanya mazungumzo na Rais Joseph Kabila, Rais wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amesema kuwa pamoja na mambo mengine wamekubaliana ushirikiano wa kimaendeleo katika uwekezaji pamoja na jinsi ya kusimamia uchaguzi ujao wa nchi hiyo kupitia uongozi wake katika nchi za Jumuiya ya nchi za SADC.

Aidha Rais Magufuli amesema kuwa mbali ya kuangalia masuala ya kiusalama nchini humo pia amemuomba wafanyabiashara kutoka nchini Congo kuja kuwekeza nchini pamoja kutumia bandari ya Dar es Salaam kwa katika usafirishaji wa bidhaa.

Rais Magufuli amesema kuwa wamekubaliana na mamlaka ya bandari kuongeza muda wa mizigo inayokaa bandarini mpaka muda wa siku 30 badala ya siku 14 kama ilivyo awali huku akiongeza kwa kusema kuwa hata ujenzi wa reli ya Standard Geuge utaifaidisha Congo katika usafirishaji wa mizigo.

Kwa upande wake Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC), Joseph Laurent Kabila amesema kuwa anaamini ushirikiano huo utakuza maendeleo ya pande zote mbili pamoja na nchi za jumuiya ya SADC ikiwa ni pamoja na kufanya uchaguzi utakaozingatia demokrasia nchini humo.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images