Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

TCRA yakipa onyo kali kituo cha runinga cha Clouds.........Yakifungia kwa miezi 3 kipindi cha 'Take One' kwa kukiuka kanuni za utangazaji.

$
0
0
Kamati ya Maudhui ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imetoa onyo kali kwa kituo cha Televisheni cha Clouds sambamba na kukifungia kwa kipindi kwa miezi mitatu kipindi cha Take One kinachorushwa na Kituo hicho.
 
Makamu mwenyekiti wa kamati hiyo Method Mapunda amesema sababu ya kukifungia kipindi hicho ni kutokana na ukiukwaji wa kanuni za utangazaji za mwaka 2005, kwa kumhoji na kurusha kipindi cha mtu kinachohamasisha biashara ya ngono, kuingilia faragha ya mtu na kutolinda maadili ya watoto.

“Clouds tv inapaswa kukitathimini upya kipindi hicho kwa lengo la kupata njia bora ya kukiendesha na kupeleka mapendekezo TCRA kwa ajili ya kujiridhisha kabla ya kipindi hicho kufunguliwa,”alisema mapunda.
 
Mahojiano yaliyopekea kipindi hicho kufungiwa ni kati ya mtangazaji wa kipindi hicho Zamaradi Mketema na Gift Stanford Maarufu kama ‘Gigy Money’ na yalirushwa Agost 09 saa 3.00 usiku na kurudiwa kesho yake saa 7.00

Waziri atolea maelezo taarifa ya serikali kuhakiki watumishi wanavyotumia mishahara yao

$
0
0
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora,  Angellah J. Kairuki amekanusha taarifa inayosambazwa kwenye mitandao ya kijamii kuwa serikali ina mpango ya kuhakiki namna watumishi wake wanavyotumia mishahara yao.

Waziri Kairuki kupitia akaunti yake ya matandao wa Twitter amesema kuwa taarifa hiyo ni ya uongo na kuwataka wananchi kuipuuza kwani ina lengo la kupotosha umma.

“Kuna taarifa ya uongo inayosambazwa mtandaoni kwamba “kutakuwa na zoezi la kuhakiki watumishi wa umma wanavyotumia mishahara yao”.Ipuuzieni.”

“Si dhamira wala desturi ya Serikali yetu kuingilia maisha binafsi ya watumishi wa umma hususan matumizi ya mishahara yao.Puuzieni uzushi huo.”

Taarifa hiyo imemnukuu Waziri Kairuki kuwa serikali baada ya kukamilisha uhakiki wa vyeti kwa watumishi wake, wataanza uhakiki wa jinsi watumishi wa umma wanavyotumia mishahara yao ili kurejesha maadili kwa watumishi wa umma.

Kuhusu uhakiki wa vyeti kwa watumishi wa serikali, Rais Magufulii alisema kuwa lengo la zoezi hilo si kuwafukuza watumishi lakini ni kujiridhidha kama malipo yanayofanyika kwa watumishi hao yanalandana na viwango vya elimu wanavyoeleza kuwa wanavyo.

Mambo Muhimu Waliyoyajadili Rais Magufuli na Rais wa Congo DRC Joseph Kabila wakati wa mkutano na Waandishi wa Habari Ikulu

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Mhe. Joseph Kabila Kabange leo tarehe 04 Oktoba, 2016 wamefanya mazungumzo rasmi Ikulu Jijini Dar es Salaam na kisha kuzungumza na wananchi kupitia vyombo vya habari ambapo viongozi hao wawili wamekubaliana kuendeleza na kuimarisha uhusiano na ushirikiano wa kidugu na kihistoria katika nchi hizi mbili marafiki na majirani.

Katika Mazungumzo hayo Rais John Pombe Magufuli amemuhakikishia Rais Joseph Kabila Kabange kuwa Serikali ya Tanzania imechukua hatua kadhaa za kuimarisha huduma katika bandari ya Dar es Salaam na kupunguza vizuizi vya barabarani hadi kubaki vitatu ili nchi ya Kongo na nchi nyingine za kusini na magharibi mwa Tanzania ziitumie bandari hiyo bila vikwazo.
 
Dkt. Magufuli amesema Tanzania imejiwekea malengo ya kuhakikisha uchumi wake unakua kwa asilimia 7.2 na kwamba kutokana na hali hiyo anawakaribisha wafanyabiashara wa Kongo kuja kuwekeza nchini Tanzania na wafanyabiashara wa Tanzania kwenda kuwekeza nchini Kongo.
 
“Mhe. Rais Joseph Kabila Kabange takwimu zinaonesha nchi zetu zinafanya biashara kubwa kwani katika mwaka 2009 tulifanya biashara iliyofikia Shilingi Bilioni 23.1 na imekuwa ikikua mwaka hadi mwaka na hivi sasa tunafanya biashara yenye thamani ya shilingi Bilioni 393.6 kwa mwaka.
 
“Mimi ningependa kuona sisi ndugu na majirani tunafanya biashara zaidi, wafanyabiashara wa Kongo waje Tanzania kuwekeza na Serikali yangu itawaunga mkono” amesema Rais Magufuli.
 
Aidha, Rais Magufuli amezungumzia mikakati ya kuimarisha mawasiliano ya barabara na ujenzi wa reli ya kati kwa kiwango cha kisasa (Standard Gauge) ambapo Tanzania imetenga Shilingi Trilioni 1 kwa ajili ya kuanza ujenzi huo na kwamba hatua hiyo itarahisisha zaidi usafirishaji wa mizigo ya kwenda na kutoka Kongo kupitia bandari ya Dar es Salaam.
 
Kuhusu mradi wa ujenzi wa Bomba la mafuta ghafi kutoka Hoima nchini Uganda hadi bandari ya Tanga nchini Tanzania, Rais Magufuli amesema ni matarajio kuwa Kongo ambayo pia imegundua mafuta katika ziwa Albert itatumia bomba hilo kama ambavyo Tanzania pia inatarajia kulitumia kufuatia tafiti kuonesha uwepo wa mafuta katika maeneo ya ziwa Eyasi na Ziwa Tanganyika.
 
Kwa Upande wake Rais Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo Mhe. Jospeh Kabila Kabange amemshukuru Rais Magufuli kwa mwaliko huu wa ziara ya kiserikali na amemhakikishia kuwa Kongo itaendeleza na kuimarisha zaidi uhusiano wake na Tanzania kwa kuwa nchi hizi ni majirani na ndugu tangu enzi ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
 
Mhe. Kabila amesema Kongo inatambua umuhimu wa kushirikiana na Tanzania katika biashara na uwekezaji na kwamba amefurahishwa na hatua ambazo Serikali ya Tanzania imezichukua kuboresha huduma katika bandari ya Dar es Salaam ambayo ni tegemeo kwa usafirishaji wa mizigo ya Kongo Mashariki na sehemu nyingine za nchi hiyo.
 
Ameahidi kuwa pamoja na kuwahasisha wafanyabishara wa Kongo kuitumia bandari ya Dar es Salaam, Serikali yake itachukua hatua za kurekebisha kasoro zinazolalamikiwa na wafanyabiashara dhidi ya maafisa wa forodha wa Kongo waliopo hapa nchini.
 
Rais Kabila amezungumzia mradi wa ujenzi wa bomba la mafuta ghafi kutoka Hoima nchini Uganda hadi bandari ya Tanga nchini Tanzania akisema nchi yake pia imeamua kutumia bomba hilo kusafirisha mafuta yake iliyoyagundua katika ziwa Albert upande wa Kongo na pia juhudi zinazoendelea kupata mafuta katika ziwa Tanganyika na amesisitiza kuwa ili kufanikisha hilo ushirikiano ni muhimu.
 
Kuhusu hali ya usalama nchini Kongo, Rais Kabila amesema kwa asilimia 97 nchi hiyo ina usalama na kwamba ni maeneo machache tu ya mashariki mwa Kongo ndiko kuna vikundi vinavyoendesha vurugu.
 
“Mhe. Rais Magufuli hivi karibuni tutaanza mazungumzo ya kutafuta amani ya kudumu nchini Kongo, na lengo letu ni kuhakikisha nchi inakuwa na amani kabla, wakati na baada ya uchaguzi mkuu utakaofanyika mwezi Desemba ama baada ya mwezi Desemba” amesema Rais Kabila.
 
Mhe. Rais Kabila amekubali kuupokea ujumbe wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi za Tanzania, Angola na Msumbiji ambao Mwenyekiti wa asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC – Organ Trioka) Rais John Pombe Magufuli ataituma hivi karibuni kwa ajili kufuatilia hali ilivyo nchini Kongo.
 
Baada ya mazungumzo rasmi na kuzungumza na wananchi kupitia vyombo vya habari, Rais Kabila anatarajiwa kuweka jiwe la msingi la jengo la Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA) lililopo kando ya Bandari ya Dar es Salaam na jioni atashiriki dhifa ya kitaifa iliyoandaliwa na mwenyeji wake Rais John Pombe Magufuli.
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitambulisha viongozi kwa Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC)  Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 4, 2016
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC)  Ikulu jijini Dar es salaam Oktoba 4, 2016

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
04 Oktoba, 2016

Kauli ya Makamu wa Rais kufuatia mauaji ya watafiti wawili na dereva wao waliouawa kwa kuchomwa moto

$
0
0

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amelaani vikali mauaji ya watafiti wawili wa kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Selian cha Arusha na dereva mmoja waliokuwa kazini katika kijiji cha Mvumi Makulu, wilayani Chamwino mkoa wa Dodoma.

Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan ametoa kauli hiyo leo 4-Oct-2016 wakati akifungua kongamano ya 30 la Kimataifa la Wanasayansi lililoandaliwa na Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) katika ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

Makamu wa Rais amesema kuwa tukio hilo ni baya na amewahakikishia watafiti wanaoshiriki kongamano hilo kuwa Serikali itachukua hatua stahiki kwa watu  waliofanya kitendo hicho cha kinyama ili kukomesha tabia hiyo.

“Haiwezekani hata kidogo watu kufanya mauaji hayo ya kikatili na waachwe bila kuchukuliwa hatua kali za kisheria alisisitiza Makamu wa Rais”

Akizungumzia masuala ya utafiti, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amesema serikali inatambua kazi nzuri inayofanywa na watafiti hao hivyo Serikali itaendelea kutoa mchango wake wa hali na mali ili kuhakikisha watafiti hao wanafanya kazi zao kwa ufanisi unaotakiwa.

Makamu wa Rais pia amewahimiza wafadhili waendelee kusaidia watafiti hasa wanaofanya tafiti za afya nchini kwa sababu tafiti hizo zitasaidia kwa kiasi kikubwa namna ya kukabiliana na magonjwa mbalimbali.

Amesema kuwa watafiti wanamchango mkubwa katika kuleta maendeleo kupitia matokeo ya tafiti zao nchini hivyo jitihada hizo ni muhimu zikaimarishwa ipasavyo.

Kongamano hilo la 30 la Kimataifa la Wanasayansi lililoandaliwa na Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu -NIMR- linajumuisha watafiti mbalimbali kutoka Ulaya, Afrika na Amerika.

Katika kongamano hilo, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ameshiriki katika zoezi utoaji wa tuzo kwa wanasayansi waliofanya tafiti mbalimbali za afya nchini.

Imetolewa na
Ofisi ya Makamu wa Rais
Dar es Salaam.

4-Oct-2016.

Taarifa Kwa Umma Kuhusu Kuwasili Kwa Chanjo Nchini

Rais Kabila Wa Congo-DRC Aweka Jiwe La Msingi Bandarini Jijini Dar Es Salaam .......Kasema Nchi Yake Itaendelea Kutumia Bandari Yetu Kupitisha Mizigo

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Mhe. Joseph Kabila Kabange ameweka jiwe la msingi la jengo la Kituo cha Pamoja cha Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) ambalo limejengwa kwa lengo la kuwaweka pamoja wadau wote wanaotoa huduma katika bandari ya Dar es Salaam ikiwa ni juhudi za kuboresha huduma na kupunguza gharama kwa watumiaji wa bandari hiyo.

Hafla ya uwekaji jiwe la msingi la jengo hilo refu kuliko yote Afrika Mashariki na kati imefanyika leo tarehe 04 Oktoba, 2016 na kushuhudiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.

Akizungumza kabla ya kuwekwa jiwe hilo la msingi Rais Magufuli ameishukuru Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kwa kuwa mteja mkubwa wa bandari ya Dar es Salaam na amesema aliamua jiwe la msingi la jengo hilo liwekwe na Rais wa Kongo kwa kutambua umuhimu wa nchi yake katika biashara ya bandari ya Dar es Salaam na pia undugu na urafiki wa kihistoria uliopo kati ya nchi hizi mbili.

Rais Magufuli amemhakikishia Rais Kabila kuwa kama ambavyo Serikali yake imechukua hatua kadhaa za kurekebisha kasoro zilizokuwepo katika bandari hiyo, itaendelea kujenga mazingira mazuri zaidi kwa wafanyabiashara wa Kongo kutumia bandari hiyo ikiwa ni pamoja na kudhibiti vitendo vya rushwa, kuongeza muda wa kutunza mizigo inayoshushwa kutoka siku 14 hadi siku 30, kuanzisha bandari kavu katika eneo la Ruvu mkoani Pwani na kuinua ari ya wafanyakazi wa bandari kutoa huduma bora.

"Mhe. Rais Kabila bandari yetu ilifikia mahali pa kuandika rekodi ya kupotea kwa meli kwenye taarifa za bandari, kuna wakati hapa zilipotea meli 60, lakini pia mizigo ya watu ilikuwa inapotea na wafanyabiashara walikuwa wanaombwa rushwa.

"Kuna baadhi ya wafanyakazi wa bandari waliifanya hii bandari kama mali yao, walikuwa wanaondoka na fedha za rushwa kwenye buti za magari, naomba nikuhakikishie kuwa haya hayatatokea tena, na yakitokea Mhe. Balozi wa Kongo upo hapa njoo unieleze mimi au mwambie Makamu wa Rais au Waziri Mkuu"amesisitiza Rais Magufuli.

Dkt. Magufuli pia amempongeza Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kwa kuanzisha ujenzi wa jengo hilo la Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania na kwamba anaamini litasaidia kuimarisha biashara kati ya Tanzania na Kongo na nchi nyingine zinazotumia bandari ya Dar es Salaam.

Kwa upande wake Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Mhe. Joseph Kabila Kabange amemshukuru Rais Magufuli kwa heshimu kubwa aliyompa yeye na nchi ya Kongo ya kuweka jiwe la msingi la jengo hilo na amesema kutokana na Tanzania kuchukua hatua madhubuti za kuimarisha huduma za bandari ya Dar es Salaam mizigo ya Kongo itapitia bandari hiyo.

"Mhe. Rais Magufuli bandari hii ipo Dar es Salaam lakini bandari hii ni ya kwetu sote, mashariki ya Kongo inapakana na nchi nne za Tanzania, Rwanda, Burundi na Uganda lakini asilimia 50 ya mizigo inatoka Tanzania hususani katika bandari ya Dar es Salaam.

"Nimefurahi pia kuwa katika juhudi za Tanzania kuboresha bandari pia mnaboresha barabara na bandari ndogo ndogo za ziwa Tanganyika, hili ni jambo muhimu kwa sababu sasa mizigo ya Kongo itasafiri kwa urahisi na wafanyabishara wa Kongo waliokuwa wameacha kutumia bandari ya Dar es Salaam watarudi" amesema Rais Kabila.

Mhe. Joseph Kabila Kabange amesema katika miaka ya 70 na 80 Kongo ilikuwa ikizalisha shaba kiasi cha tani laki 1 lakini hivi sasa inazalisha hadi tani Milioni 1.2 na zote hizi zinategemewa kusafirishwa nje ya nchi kupitia bandari ya Dar es Salaam.

Ameipongeza Serikali ya Tanzania kwa kununua ndege mbili aina ya Bombardier Q400 na ameunga mkono mpango wa kuanzisha safari za moja kwa moja kati ya Tanzania na Kongo huku akibainisha kuwa nchi yake pia itanunua ndege kwa ajili ya kuimarisha zaidi usafiri wa anga kati ya nchi hizi mbili.

Mapema kabla ya Marais wote wawili kuzungumza, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) Mhandisi Deodatus Kakoko alisema jengo hilo lina ghorofa 35, urefu wa meta 157, ukubwa wa meta za mraba 65,115 na ujenzi wake unatarajiwa kukamilika tarehe 31 Desemba, 2016 kwa gharama ya Shilingi Bilioni 130.

Rais Kabila ambaye aliingia hapa nchini jana tarehe 03 Oktoba, 2016 kwa ziara ya kiserikali ya siku tatu, jioni ya leo atahudhuria dhifa ya kitaifa katika ukumbi wa Ikulu Jijini Dar es Salaam iliyoandaliwa kwa ajili yake na Mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam

04 Oktoba, 2016

PICHA 5: Tingatinga Lilivyofukua mamilioni yaliyokuwa Yamefichwa ardhini

$
0
0
Kama wewe unadhani huna fedha, basi kuna wengine ambao wamezichimbia ardhini, tena kwa mamilioni. Benki ya chini ya ardhi iliyosheheni mamilioni ya fedha, zilizoswekwa ndani ya mifuko myeusi ya plastiki na kufukiwa mchangani, imechimbuliwa na matrekta ya kutengeneza barabara jijini Arusha huku noti nyekundu zikitawanywa kila kona na kufanyika kuwa 'Sadakalawe - Amina,' kwa kila mpita njia ambaye angeweza kujitwalia fungu.

Ilikuwa ni mshikemshike katika eneo la Mianzini mjini Arusha , ambako kuna mradi mkubwa wa upanuzi wa barabara ya kutoka Mianzini Mataa hadi Ilkiding'a unaoendelea.

Watu walipigana vikumbo katika harakati za kujineemesha na fedha zilizokuwa zimetapakaa eneo hilo. Ikiwa imesheheni noti tupu, tena nyekundu na mpya, kufumuliwa kwa akaunti hiyo ya benki ya chini ya ardhi pamoja na kuwa neema kwa wapita njia na wakazi wa eneo hilo, kuligeuka pia kuwa kilio kwa mmiliki wa hazina hiyo, Christopher Akoonay maarufu kama 'Mmbulu' ambaye sasa amejipatia jina jingine la 'Mabulungutu.'

Akonaay ni mkulima, lakini hasa akijishughulisha na ufugaji wa ng'ombe wa maziwa. Yeye hudamka asubuhi kukamua mifugo hao na kisha kusambaza bidhaa hiyo ya maziwa katika maeneo mengi ya jiji katika kuwauzia wakazi wa Arusha.

Na katika siku ya tukio, Akonaay alikuwa yuko kwenye shughuli zake za kuwapelekea maziwa wateja wake, ndipo watengeneza barabara walipofika eneo hilo la Mianzini na tingatinga zao na kuanza kuichimba njia hiyo ya kutoka Mianzini hadi Ilkiding'a katika kata ya Ilboru, inayotenganisha Jiji la Arusha na wilaya ya Arumeru.

Ikiwa imejengwa kwa fito na matope, nyumba ya 'Mmbulu' ilikuwa miongoni mwa zile zilizobomolewa na ni baada ya wamiliki wake, kugoma kuzibomoa wenyewe ili kupisha upanuzi wa barabara hiyo.

“Shauri letu tulilipeleka mahakamani kudai fidia kabla ya mradi wa barabara haujapita hapa,” alisema Akonaay na kuongeza kuwa mara baada ya kesi yao kutupiliwa mbali na chombo hicho cha sheria, wajenzi hawakusubiri hata saa moja ipite, bali walikwenda moja kwa moja eneo hilo na kuanza kazi.

Baadhi ya wakazi wa Mianzini, wakizungumzia suala hilo kwa masharti ya kutotajwa majina, walisema ni ajabu kwa Mzee Akonaay kuwa na kiasi kikubwa cha fedha na kuzifukia ardhini huku mwenyewe akiishi kwenye nyumba duni ya matope.

Lakini Akonaay ambaye kwa sasa anaitwa 'Mabulungutu,' anasema kuwa alikosa imani na benki maana wakati akifanya kazi serikalini miaka ya 1980, alifungua akaunti na akawa anaweka fedha zake zote benki.

Baada ya kustaafu mwaka 1994 na kuamua kushughulika na ufugaji, hakuzifuatilia tena fedha zake benki hadi mwaka 2000, ambako alipokwenda kuangalia fedha zake aliambiwa kuwa kwa sababu akaunti yake haikuguswa kwa zaidi ya miaka 10, alitakiwa aende Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kujieleza. Hata hivyo, aliona huo ni usumbufu na kuamua kuanza kuweka fedha zake nyumbani.

Lakini hii pia ilimtokea puani baada ya mmoja wa ndugu zake kuzikwapua zote mara baada ya kuzifuma katika vitita vyenye thamani ya Sh milioni 20 na zaidi. Sasa Akonaay akaja na mkakati mpya wa kuhifadhi fedha kwa kuchimba shimo katikati ya chumba chake cha kulala, kilichokuwa upande wa barabara ya Mianzini na kuanza kuweka hazina yake humo.

Lakini tena, bahati mbaya ikiendelea kumuandama, makatapila ya wachonga barabara, yakaifukua benki yake hiyo ya ardhini na kutawanya fedha zaidi ya Sh milioni 35 zilizoishia kuokotwa na wapita njia pamoja na majirani, ambao kwa hofu hawakupenda hata kulizungumzia sakata hilo.

Taarifa Kwa Wataalamu Wa Afya Wanaotarajia Kuanza Mafunzo Kwa Vintendo (Internship).


Waziri Mkuu Alaani Mauaji Ya Watafiti Chamwino, Dodoma

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amelaani kitendo cha wanakijiji kuwaua watumishi wa Serikali waliokuwa wakifanya utafiti wilayani Chamwino mkoani Dodoma.

Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo (Jumanne, Oktoba 3, 2016) wakati akizungumza na waandishi wa habari wa mkoa wa Dodoma ikiwa ni sehemu ya utaratibu wake wa kukutana na makundi mbalimbali.

Mauaji ya watafiti hao, Teddy Nguma, Jafari Mafuru na dereva wao Bw. Nicas Magazine yalitokea Oktoba Mosi, 2016 baada ya kushambuliwa na wakazi wa kijiji cha Makang’wa wilayani Chamwino mkoani Dodoma.

Amesema Serikali imesikitishwa na mauaji ya watu watatu wakiwemo watafiti wawili kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Seliani (SARI) kilichopo mkoani Arusha ambao walikuwa kazini kuchunguza sampuli za udongo ili kubaini kama matetemeko yataendelea kutokea.

“Kutokana na tetemeko lilitokea mkoani Kagera, Serikali iliamua kushirikisha watalaamu mbalimbali kufanya uchunguzi kuona kama tetemeko hilo ni endelevu au la katika maeneo mengine. Kitendo cha watu kujichukulia hatua mkononi na kukatisha uhai wa watumishi ambao walikuwa kazini hakikubaliki,” amesema

. Amesema watalaamu hao walifika katika Wilaya ya Chamwino na kufanya kazi kwa siku tano na siku ya sita ndipo walipoenda eneo la kijiji cha Iringa Mvumi kuendelea na kazi ambapo waliuawa wakiwa kazini.

“Serikali kupitia kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa inaendelea na uchunguzi wa kuwabaini watu waliofanya kitendo hicho’’ amesema. Hata hivyo, Waziri Mkuu amewatoa wasiwasi watumishi wanaohamia Dodoma kuwa Dodoma ni salama na kila anayekuja yupo salama. “Dodoma ipo salama na tunatarajia kila anayehamia hapa atakuwa salama na hata wakazi wa hapa wataendelea kuwa salama,’’ amesema.

Akizungumzia kuhusu migogoro ya ardhi inayojitokeza katika maeneo mbalimbali nchini, Waziri Mkuu amesema hali hiyo inajitokeza hivi sasa baada ya wananchi wengi kutambua thamani ya ardhi.

Amesema miaka ya nyuma watu wachache walitambua thamani ardhi hivyo kuchukua maeneo makubwa na kuyamiliki. Serikali imeendelea kuhakikisha kuwa migogoro hiyo inamalizika kwa kuweka kuweka msisitizo kuwe mipango ya matumizi bora ya ardhi ikiwa ni pamoja na kupima ardhi yote na kutoa hati kwa wananchi.

“Tunataka ardhi yote ipimwe na kila mtu anayepewa ardhi apewe hati ya kumiliki na si vinginevyo’’ amesema. Wakati huohuo, Waziri Mkuu aliwaasa waandishi wa habari wawe makini na kazi yao na wajiepushe na upotoshaji kwenye taarifa wanazozitoa kwa wananchi. Amesema vyombo vya habari ni kiungo muhimu baina ya Serikali na wananchi, hivyo aliwataka viongozi wote wa umma washirikiane na vyombo vya habari kwa kutoa habari za utekelezaji wa kazi za Serikali.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amepokea msaada wa sh. milioni 11.42 kutoka kwa taasisi na wadau mbalimbali mkoani Dodoma zikiwa ni kwa ajili ya kusaidia waathirika wa tetemeko lililotokea mkoani Kagera Septemba 10, 2016 na kusababisha vifo vya watu 17.

Michango aliyopokea leo imetolewa na Mzee Thakar Singh na familia yake sh. milioni 5; NSSF Dodoma (sh. milioni 1.2); Shirika la Bima ya Taifa tawi la Dodoma (sh. milioni moja); Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo (sh. milioni moja) na Ofisi Rais TAMISEMI (sh. milioni 2). Wengine ni TRA-Dodoma (sh. milioni moja); Dodoma FM (sh. 200,000) na Mwalimu Mstaafu, Mama Amina Mafuru aliyetoa sh. 20,000/-.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU
S. L. P. 980,
DODOMA. JUMANNE, OKTOBA 04, 2016

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumatano Ya Octobar 5

Sinema ya CUF Yazidi Kunoga.......Bodi ya Wadhamini Nayo Yagawanyika Viipandevipande

$
0
0
Bodi ya wadhamini ya Chama cha Wananchi (CUF), imegawanyika vipande viwili  kutokana na mgogoro wa uongozi unaoendelea ndani ya chama hicho.

Kugawanyika kwa bodi hiyo kumekuja siku moja baada ya Mwenyekiti wake, Abdallah Katau kutangaza kutomtambua Profesa Lipumba, huku baadhi ya wajumbe wakipinga tamko hilo wakiliita ni batili kwa mujibu wa katiba ya CUF.

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam kwa niaba ya wajumbe wenzake, mjumbe wa bodi ya chama hicho, Peter Malebo, alisema hawatambui tamko lililotolewa na mwenyekiti wao kwani bodi hiyo inajiandaa kuwakutanisha mwenyeki wa chama hicho, Profesa Ibrahim Lipumba na Katibu Mkuu wake, Maalim Seif Sharif Hamad ili kuweza kutafuta suluhu ya mgogoro huo.

Alisema kutokana na hali hiyo, watakaa na wajumbe wenzao na kujadili suala hilo kabla ya kuwaita viongozi hao ikiwa ni pamoja na kujadili ushauri wa Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi.

“Tutakaa na wajumbe wenzetu ili tuweze kujadiliana mgogoro wa viongozi wetu pamoja na kupitia maazimio ya Msajili wa Vyama Vya Siasa ili tuweze kupata hoja ya kuwahoji kwenye kikao hicho.

“Lengo letu ni kuhakikisha kuwa chama chetu kinarudi kwenye hadhi yake kama ilivyokua awali kuliko hivi sasa ambapo kimegubikwa na mgogoro wa uongozi wa kitaifa,” alisema Malebo.

Alisema ikiwa watashindwa kupata mwafaka wataitisha Mkutano Mkuu wa dharura  ili waweze kuwaeleza wajumbe wa mkutano huo hali ya chama na hatua za kuchukua.

“Kama mwafaka hautapatikana katika kikao hicho, tutalazimika kuitisha Mkutano Mkuu Maalumu ambao pamoja na mambo mengine, tutawaeleza mgogoro wa viongozi wetu ili wajumbe waweze kutoa uamuzi,” alisema.

Alisema Bodi ya Wadhamini wa CUF inaundwa na wajumbe wanane ambapo kutoka upande wa bara ni watano na Zanzibar watatu.

Aliwataja wajumbe hao kuwa ni pamoja na Abdalah Katau, Peter Malebo, Ally Mbarouk, Amin Mrisha, Zacharia Kwangu, Yohana Mbelwa na Dk. Juma Muchi.

Alisema mpaka sasa bodi hiyo imegawanyika ambapo wajumbe kutoka Zanzibar wanamwunga mkono Maalim Seif huku wale wa bara wakimwunga mkono Profesa Lipumba hali inayozidi kupandisha joto ndani ya chama hicho.

“Kinachotutafuna  ndani ya CUF ni ubaguzi unaoonyeshwa waziwazi kutoka kwa viongozi wa Zanzibar jambo ambalo limechangia kila mtu kuwa upande wake, lakini tutaitana na kujadiliana suala hili ili tuweze kupata mwafaka,” alisema.

Alisema bodi hiyo inafanya kazi ndani ya kipindi cha miaka mitano ambapo iliteuliwa mwaka 2011 na itamaliza muda wake, Desemba mwaka huu.

Atoa onyo Chadema
Katika hatua nyingine, Malebo aliwataka viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kutoingilia mgogoro huo kwa madai hauwahusu.

Alisema, kitendo cha Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe kujitokeza hadharani na kudai hamtambui Profesa Lipumba inaonyesha wazi kuwa ameshiriki kuongeza mgogoro ndani ya chama hicho.

“Mbowe haumhusu mgogoro wa viongozi wa CUF, huu ni mgogoro wa ndani ya chama, tunamshangaa kujitokeza hadharani na kudai hamtambui Lipumba, yeye ni nani ndani ya chama?, tunamuonya asirudie,” alisema.

Alisema, chama hicho kimejipanga kupambana na watu wanaoingilia mgogoro wao wakati si wanachama wa chama hicho, jambo ambalo limechangia kuendelea kuchochea vurugu hizo.

Saed Kubenea kizimbani tena kwa kupotosha

$
0
0

Mbunge wa Ubungo, Saed Kubenea amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam akikabiliwa na mashitaka ya kuandika makala ya kupotosha na kusababisha hofu kwa jamii.

Kubenea, ambaye ni mbunge kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), alifikishwa mahakamani hapo jana na kusomewa mashitaka na Wakili wa Serikali, Dereck Mukabatunzi mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri.

Wakili Mukabatunzi alidai kuwa Julai 25, mwaka huu katika Mtaa wa Kasaba, Manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, Kubenea alichapisha habari ya uongo inayoweza kusababisha hofu na taharuki kwa jamii au kuondoa amani.

Inadaiwa Kubenea alichapisha makala hiyo kwenye gazeti la Mwanahalisi la Julai 25 hadi 31, mwaka huu, lenye namba 349 ISSN: 1832-5432 ikiwa na kichwa cha habari “Yuko wapi atakayeiokoa Zanzibar”.

Baada ya kusomewa mashitaka, Kubenea alikana kutenda kosa hilo na upande wa Jamhuri ulidai upelelezi wa kesi hiyo umekamilika na kuomba tarehe nyingine kwa ajili ya kumsomea mshitakiwa maelezo ya awali.

Tundu Lissu akosekana Tena Mahakamani Kisutu, aibukia Mwanza

$
0
0
Tundu Lissu, Mbunge wa Singida Mashariki, jana alishindwa kufika katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ili kujibu mashitaka ya uchochezi huku mdhamini wake akiieleza mahakama kuwa, yupo jijini Mwanza akisimamia kesi ya Esther Bulaya, Mbunge wa Bunda katika Mahakama Kuu ya Mwanza.

Lissu ambaye pia ni wakili wa Mahakama Kuu na mwansheria mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo anashitakiwa kwa uchochezi pamoja na washitakiwa wengine ambao ni ni Jabir Idrissa, mwandishi mwandamizi wa Gazeti la MAWIO, Simon Mkina, mhariri wa Gazeti hilo na Ismail Mehboob, meneja wa kampuni ya uchapishaji magazeti ya Flint.

Mdhamini wa Lissu, Ibrahim Hemed, alitoa taarifa ya kutofika kwa mdhamana wake mahakamani hapo, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba.

Ibrahim alidai kwamba Lissu amempatia taarifa kuwa ameshindwa kufika kwa sababu yupo kwenye kesi ya uchaguzi huku Peter Kibatala wakili wa utetezi akiiomba mahakama ipokee taarifa za Lissu na ikubali kuhairisha kesi hiyo.

“Lissu ni wakili  pekee wa mlalamikiwa Esther Bulaya katika kesi ya uchaguzi,” alisema Kibatala.

Baada ya kutolewa kwa maelezo hayo, Hakimu Simba aliiahirisha kesi hiyo hadi Oktoba 31 mwaka huu.

Katika kesi hiyo Lissu anaunganishwa kama mshitakiwa kufuatia kunukuliwa akitoa maoni yake katika habari iliyochapishwa na gazeti la MAWIO ikiwa na kichwa cha habari “Machafuko yaja Zanzibar.”

Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi atoa ONYO kwa wanaotumia jina la cheo chake vibaya

RIWAYA: Sorry Madam - Sehemu ya 63 & 64 (Riwaya inawafaa kuanzia miaka 18 na kuendelea )

$
0
0
Mtunzi : Eddazaria g.Msulwa

Ilioishia...
Risasi zao nyingi zikafanikiwa kutoboa kioo cha nyuma cha gari na kuzidi kunichanganya akili yangu, nikazidi kukanyaga mafuta hadi mshale wa spidi mita ukagota kwenye spidi ya mwisho ambayo ni mia mbili na hamsini.Nikazidi kwenda mbele, gafla nikakutana na kona ambayo kwa mwendo ambao ninao nikashindwa kukunja na kuisababisha gari kupiga kweney ukuta na kuvunja ukuta huu wa udongo, kufumba na kufumbua nikajikuta gari ikielea hewani, na kuanza kwenda chini kwenye miamba mikubwa ya mawe jambo ambalo lilinifanya niaanze kusali sala yangu ya mwisho kwani, ikitua chini mimi na dorecy wote tutakuwa maiti

Endelea...
Gari ikazidi kwenda chini kwa kasi, gafla nikastukia gari ikiwa imekwama huku, tawi kubwa la mti likiwa limeingia dirishani la nyuma la gari na kuifnya iendelee kuninginia kwenye mti, nikashusha pumzi taratibu huku nikitazama chini, cha kumshukuru mungu, kutoka sehemu tulipo ning’inia hadi chini si mbali sana, nikaufungua mkanda wa gari nilio jifunga, nikamtazama dorecy na kumuoana akiwa anainyanyua nyanyua shingo yake, akizinduka kutoka usingizini.Akanitazama kwa macho yakuchoka

“eddy”
“nini?’
“yupo wapi khalid?”
“wee mwehu nini, jiulize mwenyewe”
Nilizungumza kwa hasira huku nikiufungua mlango wa gari, kuna tawi lipo karibu na mlango wangu, nikapiga makadirio ya macho na kuona ninaweza kuruka na kulikanyaga pasipo na wasiwasi wa aina yoyote
“eddy unataka kwenda wapi, kwani hapa wapi?”
Dorecy alizungumza huku akitazama chini
“hapa tupo mbinguni mama yangu”
“mbinguni……!!?”
“unauliza tena, hapa ukifungua mlango tuu umeshafika kwa sir god”

Nilizungumza kwa dharau, nikaruka kwenye tawi la mti, kwa bahati nzuri nikatua vizuri na kujiweka sawa mwili wangu, nikashuka kwenye mti taratibu na kufika chini pasipo shida ya aina yoyote, gafla nikasikia kelele za dorecy akiniita jina langu, ikanilazimu nimtazame nikamuona akiwa ananing’inia, huku ameushikilia mlango wa gari uliopo upande wa siti yake
“eddy niokoe mwenziooo, ninakufa mimi”

“ukijiachia tuu unafika mbnguni, hapo tulikuwa kwenye geti la kuingilia mbinguni”
Nilizungumza huku nikimtazama dorecy jinsi anavyo ning’inia huku akiirusha rusha miguu yake hewani
“eddy nakufa mimi”

Dorecy aliendelea kuzungumza kwa sauti ya kilio, huku akiendelea kuning’inia hewani, nikatafuta sehemu yenye jiwe lililo kaa vizuri, nikakaa na kuendelea kumtazama dorecy anaye endelea kuninginia hewani
“eddy niokooe”
“nikuulize kitu dorecy?”
“ehee” alijibu huku akiwa amening’inia
“hivi huku ulifikaje?”
“nikuulize wewe, tumefikaje huku?”

“ahaa unaniuliza mimi tena kwamba tumefikaje huku, unadhani kwamba mimi nilikuwa ni ndege iliyo kufikisha kwenye hii nchi?”
“eddy tuachane na hayo, ninakuomba unisaidiea”
Dorecy alizungumza kwa sauti ya unyong, akiashiria kwamba amechoka sana
“madini yangu yapo wapi?”
“edd siwezi kukujibu hadi nishuke”

“basi wewe si mjeda wa mzee godwin, jishushe mwenyewe”
Nilizungumza huku nikinyanyuka kwenye jiwe, nikiendelea kulichunguza aneo zima la hii sehemu, nilipo hakikisha lipo salama na hakuna uwezekana na watu wa khalid kufika katika sehemu tulipo nikarudi sehemu alipo dorecy akiendelea kuning’inia huku akitoa kilio kwa mbali akilalamika kwamba anakufa

“jiachie”
Nilizungumza huku nikiwa nimesimama chini yake nikimtazama
“ehee?”
“hujasikia, jiachie nitakudaka na hilo jitumbo lako”
“kweli eddy?”
“kama hutaki basi bwana”
“basi najiachia”

Nikaitega mikono yangu usawa wa sehemu anayo ning’inia dorecy, nikahesabu moja hadi tatu, dorecy akajiachia na kutua kwenye mikono yangu, cha kushukuru mungu ametua vizuri kwenye mikono yangu, nikamsimamisha chini na kumuacha akiendelea kuhema kwa nguvu, kama bata mzinga.Nikaanza kupiga hatua za kuondoka katika eneo hili pasipo kusubiria asante ya dorecy huku moyoni mwangu nikijikuta nikianza kusamehe kuhusiana na madini yangu, kwani hakuna uwezekano wowote wa mimi kuyapata kutokana na khalid kujizatiti vizuri katika swala la ulinzi
“edd….Y”

Nilisikia sauti ya dorecy ikiniita kwa unyonge nyuma yangu, nikasimama pasipo kutazama nyuma, nikashusha pumzi nyingi na kugeuka taratibu, nikamuona dorecy akianza kukaa chini taratibu huku akiwa amelishika tumbo lake
“eddy nakufa mimi, tumbo langu”

Dorecy alilalamika huku akiwa amelishika rumbo lake, nikaanza kupata mstuko baada ya kagauni kake ka kulalia alicho kivaa kukiona kikiwa kimelowa kwa damu sehemu zake za siri.Machozi ya uchungu yakaendelea kumtoka dorecy, vilio vya dorecy vikazidi kuongezeka, ikanilazimu kurudi kwa haraka katika sehemu alipo
“eddy mtoto anatoka”

Dorecy alizungumza huku akipanua mapaja yake, wazo la kwanza kunijia kichwani mwangu, ni kukata nguo ya ndani aliyo ivaa dorecy, macho yangu yakaendelea kumtazama dorecy jinsi anavyo toa mayowe ya uchungu
“eddy mwanangu uwiiiiiii”
“yupo wapi?”

Nikastukia kofi zito ikitua kwenye shavu langu, kutoka kwa dorecy ambaye anaonekana kukasirika, macho yake ameyatoa huku jasho jingi likimwagika kutoka na maumivu makali anayo yapata.
“jikaze uzae”

Nilizungumza huku nikiishikilia miguu ya dorecy ambayo ameichanua kwa kiasi fulani, nikaendelea kumuhimiza ajitahidi kumsukuma mtoto, kwani nilisha anza kuona dalili ya majimaji yanayotangulia kabla ya mtoto kuzaliwa.Taratibu nikaanza kuona kichwa cha mtoto kikianza kuchomoza
“push kwa nguvu”(sukuma……)

Nikaendelea kumuhimiza dorecy kwa sauti ya juu, akaendelea kujitahidi kumsukuma mtoto wake atoke nje, nikaiweka mikono yangu karibu na kichwa cha mtoto na kuanza kukipokea kichwa chake taratibu
“endelea mama, mabega yameshaanza kuchomoza”
Hadi mimi mwenyewe jasho likaanza kunitoka kwani si kazi ndogo ya kumzalisha mwanamke
“eddyyyyyyyyyyyyyyyy”


Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Alhamisi ya Oc toba 6

Rais Magufuli Aagana na Rais Kabila na kufanya ziara ya kushtukiza uwanja wa ndege

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Mhe. Joseph Kabila Kabange  jana tarehe 05 Oktoba, 2016 amemaliza ziara yake ya kiserikali ya siku tatu hapa nchini na kurejea nchini kwake.

Katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam Rais Kabila aliagwa na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.

Viongozi wengine walioungana na Rais Magufuli wakati wa kumuaga Rais Kabila ni Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Mawaziri, Mabalozi wa nchi mbalimbali, Wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Bw. Paul Makonda na Viongozi wa Dini.

Katika hatua nyingine, mara baada ya kuondoka kwa Rais Kabila, Rais Magufuli alifanya ukaguzi wa kushitukiza katika sehemu ya kukagulia mizigo na abiria ya uwanja huo upande wa Terminal One ambako Mwezi Mei mwaka huu alitembelea kwa kushitukiza na kubaini kuwa mashine za ukaguzi (Scanners) zilikuwa hazifanyi kazi.

Mara hii Rais Magufuli amebaini kuwa mashine hizo zinafanya kazi, baada ya kujionea yeye mwenyewe uhalisia wa namna mizigo inavyokaguliwa.

Hata hivyo amemuagiza Mkurugenzi wa uwanja wa ndege wa Julius Nyerere Bw. Paul Rwegasha kuwachukulia hatua za kinidhamu maafisa wawili  waliotoa taarifa za uongo pindi alipofanya ukaguzi wa kushitukiza mara ya kwanza.


"Leo kweli mashine zinafanya kazi na mimi nimeona lakini wale walionidanganya mara ya kwanza nilipokuja, Mkurugenzi hakikisha unawachukulia hatua" alisisitiza Dkt. Magufuli.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na mgeni  wake Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Joseph Kabila katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) mara baada ya kumaliza ziara yake ya siku tatu nchini na kurejea DRC.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na  Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan wakipunga mkono kuagana na Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Joseph Kabila (hayupo pichani) katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA).
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Makamu wa Rais Samia Suluhu akikagua mashine ya ukaguzi wa mizigo katika uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere (JNIA) Terminal One kuangalia ufanisi wa mashine hizo.

Majina Ya Wanafunzi Waliochaguliwa Kujiunga Chuo Kikuu St.Augustine - SAUT 2016/2017

$
0
0
Majina Ya Wanafunzi Waliochaguliwa Kujiunga Chuo Kikuu St.Augustine - SAUT   2016/2017

==> Kuaona Majina << Bofya Hapa>>

Scorpion ‘Mtoboa macho’ Apandishwa Kizimbani .........Anyimwa Dhamana, Apelekwa Rumande

$
0
0
Mkazi  wa Machimbo Yombo jijini Dar es Salaam, Salum Njwele (34) maarufu kama Scorpion, amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala kujibu mashitaka ya unyang’anyi wa kutumia silaha na kumtoboa macho yote mawili Said Mrisho.

Scorpion alifikishwa mahakamani hapo jana mbele ya Hakimu Mkazi, Adelf Sachore na kusomewa mashitaka na Wakili wa Serikali, Munde Kalombola.

Akisoma mashitaka hayo, Kalombola alidai kuwa mshitakiwa alitenda kosa hilo Septemba 6, mwaka huu eneo la Buguruni Sheli wilaya ya Ilala.

Munde alidai, Njwele aliiba mkufu rangi ya fedha wenye uzito wa gramu 34 ikiwa na thamani ya Sh 60,000, bangili na fedha taslimu Sh 331,000 vyote kwa pamoja vikiwa na thamani ya Sh 476,000 mali ya Mrisho.

Kalombola alidai kuwa mshitakiwa kabla na baada ya wizi huo, alimchoma kisu machoni, tumboni na mabegani mlalamikaji ili ajipatie mali hizo.

Hata hivyo, upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika na upande wa mashitaka uliomba tarehe nyingine kwa ajili ya kutaja.

Hakimu Sachore aliahirisha kesi hiyo hadi Oktoba 19, mwaka huu kesi hiyo itakapotajwa tena. Mshitakiwa alirudishwa rumande kutokana na mashitaka yanayomkabili kutokuwa na dhamana.

CHADEMA Wazua Balaa Umeya wa Kinondoni

$
0
0

Wakati mchakato wa uchaguzi wa meya na naibu wake ukiendelea, suala la idadi ya madiwani wa viti maalumu wa Chadema katika Manispaa ya Kinondoni limeibua mvutano mpya kati ya chama hicho na ofisi ya mkurugenzi mtendaji.

Mvutano huo umejitokeza baada ya Mkurugenzi wa Kinondoni, Aron Kagurumjuli kutoa barua inayoeleza kuwa kutakuwa na madiwani viti maalumu wanawake wasiopungua theluthi moja ya madiwani wa kuchaguliwa wa Chadema. 

Kwa mantiki hiyo, Chadema ambayo ina madiwani wa kuchaguliwa saba itakuwa na madiwani watatu wa viti maalumu. Kwa hiyo majina yasiyopungua matatu ndiyo yatakayowasilishwa kuunda baraza jipya la madiwani.

Hata hivyo, Katibu wa Chadema Mkoa wa Dar es Salaam, Henry Kilewo alipinga maelezo hayo ya mkurugenzi akisema: “Tayari nimeshamwandikia barua mkurugenzi kumweleza. Tungekuwa tunatoka katika uchaguzi mkuu ningekubaliana na hoja ya Kagurumjuli, lakini kwa hali ilivyo sasa siwezi kukubaliana naye kwa sababu baraza likiitishwa madiwani hawatakula kiapo kama awali.”

Kuhusu madai hayo Kagurumjuli alisema: “Nasimamia sheria, sifuati matakwa ya mtu. Nadhani wao wanapingana na sheria. Sielewi presha inatoka wapi. Wa kushinda atashinda na wa kukosa atakosa kulingana na idadi ya wajumbe wake na hakuna atakayeonewa.”

Alisisitiza kuwa kulingana na sheria hiyo na idadi ya madiwani wa kuchaguliwa wa Chadema, chama hicho hakiruhusiwi kuongeza diwani mwingine. Kagurumjuli hakuwa tayari kutaja idadi ya wajumbe watakaounda baraza la madiwani na kusema kwamba anasubiri majina ya madiwani kutoka CUF, Chadema na CCM.

Lakini Kilewo alisema msimamo wa Chadema uko palepale wa kuhakikisha madiwani wanne wanabaki Kinondoni na kwamba hakuna mwenye mamlaka ya kuengua mjumbe isipokuwa kifo na mahakama.

“Ubungo hakuna tatizo. Ingawa maelezo yanafanana ya wajumbe watatu kutakiwa kulingana na idadi ya madiwani wa kuchaguliwa. Ishu ipo Kinondoni kwa sababu madiwani wetu wa viti maalumu wengi walikubaliwa,” alisema Kilewo.

Kuhusu umeya baada ya manispaa hizo kugawanywa, Kilewo alisema jina la Mustafa Muro, Diwani wa Kinondoni, ndilo lililopendekezwa na kupelekwa kwa ajili ya kugombea umeya wa Kinondoni huku Boniface Jacob akiteuliwa kugombea Ubungo.

Wakati Kilewo akisema hayo, Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kinondoni, Salum Madenge alisema mchakato wa kuwapata wagombea wa nafasi ya umeya na naibu meya katika manispaa hizo ulitarajiwa kukamilika jana jioni.

“Mchakato huu ulianza muda mrefu lakini leo (jana), jioni ndiyo kilele chake. Wagombea watakaopatikana ni mahiri na CCM ipo fiti tunasubiri mechi uwanjani,” alisema Madenge.

Kwa nyakati tofauti, Manispaa za Kinondoni na Temeke zilifanya mgawanyo wa madiwani baada ya Serikali kuzigawanya na kuunda halmashauri za Ubungo na Kigamboni.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images