Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Lowassa, Mbowe Watakiwa Kuripoti Polisi Leo

$
0
0
Viongozi waandamizi wa Chadema akiwamo Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa jana walikamatwa na Jeshi la Polisi wakati wakiwa katika kikao cha ndani katika Hoteli ya Giraffe mkoani Dar es Salam

Lowassa, ambaye alikaa kituoni hapo kwa takribani saa tatu anaweza kuwa kiongozi wa kwanza aliyewahi kushika nafasi ya Waziri Mkuu kuhojiwa na polisi.

Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu aliwataja viongozi wengine waliokamatwa kuwa ni Mwenyekiti, Freeman Mbowe, Katibu Mkuu, Dk Vincent Mashinji, Naibu Katibu Mkuu Bara, John Mnyika na Makamu Mwenyekiti Zanzibar, Said Issa.

Mara baada ya kukamatwa, walipelekwa katika Kituo Kikuu cha Polisi ambako baadhi ya wajumbe na wabunge waliwafuata na kuwasubiri nje ya kituo hicho kujua hatima yao. 

Viongozi hao walionekana wakiingia Polisi saa 10.30 jioni na kutoka saa 1.25 usiku, jambo ambalo liliwafanya wakae kituoni hapo kwa saa tatu. 

Lissu alisema polisi walivamia kikao hicho kilichokuwa na wajumbe 170, wakiwamo baadhi ya wabunge wa chama hicho na kuwakamata viongozi hao kwa maelezo kuwa wamekaidi amri ya Jeshi la Polisi ya kuzuia mikutano ya ndani na nje ya vyama vya siasa. 

Imeelezwa kuwa viongozi hao wa Chadema walikuwa na mkutano uliotanguliwa na kikao cha viongozi wakuu na kufuatiwa na cha viongozi hao kikijumuisha wabunge, mameya na wenyeviti wa halmashauri. 

Wakiwa katika kikao hicho, ilielezwa kuwa watu wanne waliingia wakiwa wamevalia kiraia na kuwaeleza kuwa viongozi wao wanahitajika kituo kikuu cha polisi kutokana na kufanya mkutano kinyume cha sheria. 

Mbunge wa Viti Maalumu, Upendo Peneza ambaye  alikuwa kwenye mkutano huo alisema pamoja na mambo mengine ya chama, walikuwa wakijadili suala la operesheni Ukuta la Septemba Mosi kama liendelee au lisiendelee kutokana na hali ilivyo.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Simon Sirro alipoulizwa kuhusu kukamatwa kwao, alisema viongozi hao walikamatwa kwa kukukaidi amri ya polisi ya kuzuia mikusanyiko ya kisiasa na kuchochea wananchi kuandamana kinyume cha sheria Septemba Mosi. 

Alisema baada ya kuachiwa kwa dhamana, viongozi hao wametakiwa kuripoti kituoni hapo leo. 

Wiki iliyopita, Jeshi la Polisi kupitia kwa Kamishana wa Operesheni na Mafunzo, Nsato Marijani lilipiga marufuku mikutano ya ndani likisema inatumika kuhamasisha watu kuvunja sheria za nchi na kupambana na askari. 

Hatua hiyo ilikuja huku jeshi hilo likiwa limepiga marufuku mikutano ya hadhara na maandamano kufuatia uamuzi wa Rais John Magufuli kuzuia shughuli  za kisiasa hadi 2020. 


Madiwani Watatu wa Chadema Wafikishwa Mahakamani Kwa Kuhamasisha Maandamano ya UKUTA

$
0
0
Madiwani watatu wa Chadema na mfuasi mmoja wa chama hicho wamefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Rombo kwa makosa ya kufanya uchochezi. 

Madiwani hao, Nicolaus Kimario (Kirio), Anasia Kimario (Viti Maalumu), Daud Tarimo (Leto ) na mfuasi wa Chadema, Rogath Kanje walikana mashtaka hayo. 

Mwendesha mashtaka, Bernard Machivya alieleza mahakama kuwa washtakiwa walitenda kosa hilo Agosti 25, wakiwa nyumbani kwa mmoja wa washtakiwa Nicolaus Kimario. 

Aliieleza Mahakama kuwa washtakiwa wote wanne walitenda kosa hilo kwa pamoja wakifanya vikao vya kuhamasisha wananchi wajitokeze kwenye maandamano ya Ukuta Septemba Mosi. 

Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Rombo, Naomi Mwerinde aliahirisha kesi hiyo hadi Septemba 5 na watuhumiwa wote wataendelea kukaa rumande.

Wakili Apinga Tundu Lissu Kusomewa Mashitaka Mapya........ Hakimu aahirisha kesi hadi mwezi ujao

$
0
0
Upande wa Jamhuri katika kesi inayomkabili Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu na wahariri wa Gazeti la Mawio iliyopo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu umeshindwa kuwasomea washtakiwa hao mashtaka mapya baada ya wakili anayewatetea, Peter Kibatala kudai kuwa yaliyofutwa yamerudishwa kwa ‘staili’ tofauti. 

Hatua hiyo ilifikiwa baada ya Kibatala kuwasilisha hoja mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba za kupinga washtakiwa hao kusomewa mashtaka hayo mapya. 

Wakili wa Serikali Mkuu, Kishenyi Mutalemwa aliwasilisha maombi mahakamani hapo akiomba kuwasomea hati mpya ya mashtaka washtakiwa hao na Mahakama iliipokea na kuruhusu isomwe, lakini Wakili Kibatala alipinga kwa madai kuwa hayatofautiani na yale yaliyofutwa Juni 28, 2016.

Kibatala alidai katika hati mpya shtaka la kwanza na la tano ni sawa na yale yaliyokuwamo kwenye hati iliyofutwa mahakamani hapo baada ya kupingwa na kuonekana hayakustahili kwa mujibu wa sheria. 

Baada ya Kibatala kuwasilisha hoja hizo, Wakili Kishenyi aliiomba Mahakama hiyo kuiahirisha kesi hiyo kwa muda ili aweze kujibu hoja zilizotolewa na upande wa utetezi na hakimu aliridhia na kuiahirisha hadi saa sita mchana. 

Ilipofika mchana, Kishenyi alidai shtaka la kwanza na la tano ni kama hayakuwapo mahakamani na kwamba kufutwa kwake haikatazwi kuyarudisha tena na mashtaka hayo ya awali yalifunguliwa bila ya kuwa na kibali cha Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), lakini hivi sasa yamerudishwa yakiwa na kibali hicho. 

Kuhusu kukata rufaa, Kishenyi alidai wanakata rufaa kwenye kesi ambayo ilisikilizwa na kumalizika. Baada ya kusikiliza hoja za pande zote, Hakimu Simba aliiahirisha kesi hiyo na kuwa atatoa uamuzi wa hoja hizo mwezi ujao. 

Washtakiwa wanaokabiliwa na kesi hiyo ni Mhariri wa gazeti hilo, Simon Mkina, Jabir Idrisa, Mchapishaji wa Kampuni ya Jamana, Ismail Mehboob na Lissu ambao kwa pamoja walikuwa wanakabiliwa na mashtaka matano yakiwamo ya kuandika habari za uchochezi kinyume na Sheria ya Magazeti ya Mwaka 2002

UVCCM Waahirisha Maandamano Yao,watii Agizo La Jeshi La Polisi

$
0
0

Agosti 22, 2016 Umoja wa Vijana wa CCM tuliutangazia umma na dunia kwamba ifikapo Agosti 31 mwaka huu tutaitisha maandamano ya amani nchi nzima yenye lengo la kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dk John Pombe Magufuli kwa utendaji wenye tija, ufanisi na uliorudisha imani na matumaini kwa wananchi.

Msimamo na dhamira ya kufanya maandamano hayo ya amani yenye maudhui na kusudio hilo, bado uko pale pale ingawaje si kwa tarehe tuliopanga na kutangaza awali yaani Agosti 31 mwaka huu.

Jumuiya yetu kama mjuavyo ni ya Vijana wa CCM, (UVCCM) inapata malezi kwa karibu mno na Jumuiya ya Wazazi ya CCM. Wiki ya jana Mwenyekiti wa Wazazi Taifa Nd. Abdallah Bulembo alikutana na waandishi wa habari akitutaka UVCCM tuahirishe maandamano ya Agosti 31 mwaka huu hadi wakati mwingine.

Kwa mujibu wa Katiba ya Chama Cha Mapinduzi, Jumuiya ya Wazazi ndiyo Msimamizi wa Malezi, Maadili na Adabu kwa Vijana wote nchini, sisi UVCCM tunaamini kuwa sikio halishindani na kichwa, mtoto ni mtoto kwa Wazazi wake hakui, hana jeuri wala ubishi.

Mtoto au watoto wanaokaidi amri, ushauri au maelekezo ya Wazazi wao huitwa watukutu, wenye viburi, manunda na wasioambilika. UVCCM si watukutu, hatukufunzwa tuwe wabishi, wakaidi na wenye viburi. Tumezingatia kutii maelekezo, makatazo na maonyo , tumeambiwa tuahirishe maandamano yetu nasi tumekubali na kuheshimu mambo tuliyoaswa.

Sambamba na hilo tumepata majibu ya barua yetu tuliyomwandikia Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP Ernes Mangu) inayotutaka tuache kufanya maandamano yetu kwa sababu Polisi wamezuia mikutano ya hadhara ya Vyama vya Siasa na maandamano nchi nzima.

Jambo jingine ambalo limetufanya pia tuahirishe maandamano yetu ya Amani ni taarifa ya kintelejinsia iliowasilishwa na Kamati yetu ya Usalama na Maadili ya UVCCM mbele ya kikao cha Sekreteriet yetu, nayo ilipendekeza  suala hilo liahirishwe kwa wakati huu hadi muda mwingine.

Pia jambo jingine ambalo limefanya maandamano hayo tuyabatilishe ni kulipisha Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ ) ambalo litakuwa katika shughuli za maadhimisho miaka 52 tokea kuanzishwa kwake.

Wanajeshi wetu watakuwa katika kazi mbalimbali za kijeshi kwenye kambi zao na mitaani kufanya usafi wa mazingira, hivyo isingependeza na wala si heshima wakati sisi tukiandamana, wao wakifanya kazi muhimu kila mmoja wetu zinazomgusa badala yake ni vyema kuwaunga mkono jambo wanalolifanya la usafi wa mazingira.

UVCCM tumekubali, hatutaki kuingia katika uvunjaji wa sheria hasa baaada ya kutakiwa kuahirisha na mamlaka za Kisheria hadi wakati mwingine muafaka na si wakati huu.

Tunaelewa kwamba uamuzi wetu wa awali wa kutaka kuandamana kwa amani hata kama tungenyimwa kibali ungetugharimu, ungetusababishia madhara na pengine hasara, kwa wakati huu na kuona jambo lenyewe ni la kuipa Ari serikali katika kuhimiza Uwajibikaji, Utendaji na Usimamizi bora wa Uendeshaji wa masuala ya kiutawala.

Tulishusha maagizo kwa Makatibu wetu wote wa Mikoa yote 32 na Wilaya 171 ya Kichama tukiwataka waandike barua katika Ofisi za Ma RPC na OCD, washirikiane ili kuratibu maandamano na kuyafanikisha kama tulivyokusudia.

Watendaji wetu wa ngazi husika wamefuata maelekezo, wametii taratibu zetu za kiutendaji na leo tumewajulisha tena wasitishe maandamano hadi tutakapowapa tena maelekezo mengine. Tunawahimiza na kuwataka ni vyema kutii mamlaka za Kikanuni na Kisheria.

UVCCM kwa wakati huu tumeamua kuachana na maandamano badala yake tunajikita katika matayarisho ya kuwapeleka Vijana wetu wakashiriki katika Mafunzo ya Siasa, Utawala, Uongozi, Ufundi na Ujasiriamali yatakayoanza kufanyika katika Chuo chetu kilichopo huko Ihemi Mkoani Iringa ambapo kitakuwa kielelezo na alama nzuri ya kumuunga mkono Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli kwa vitendo.

Tumewataka Makatibu wetu wa Mikoa na Wilaya kuendelea na zoezi la Uratibu na Uhakiki kwa Vijana ambao watateuliwa kushiriki Mafunzo hayo huko Ihemi.

UVCCM tunarejea kusema tena kwamba dhamira ya maandamano yetu ya kusifu Utendaji wa Serikali ya awamu ya tano iko pale pale ila tutapanga tarehe nyingine katika wakati ujao badala ya kufanyika Agosti 31 mwaka huu kama tulivyotangaza hapo awali.

UVCCM tunawataka Vijana wote kuendelea kuheshimu Tunu ya Amani Umoja na Mshikamo wetu kwa Taifa.


KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI
Shaka Hamdu Shaka (MNEC)
KAIMU KATIBU MKUU.

Serikali Kutoa Ajira Mpya 71,496 Hivi Karibuni

$
0
0
Serikali inatarajia kutoa ajira mpya zipatazo71,496 kwa mwaka huu wa fedha baada ya kukamilika kwa zoezi la kuwaondoa wafanyakazi hewa ambapo hadi sasa watumishi wapatao 839, tayari wapo katika hatua mbalimbali wakiwepoo waliopelekwa katika Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU).

Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais,(Utumishi na Utawala Bora),Angela Kairuki aliyasema hayo wakati akizungumzia juu ya utekelezaji na mikakati katika Wizara yake katika kipindi cha “Utekelezaji” kinacho rushwa kupitia Shirika la Utangazaji Tanzania(TBC1).

“Mpaka sasa kuna baadhi ya watumishi hewa waliofanyiwa mahojiano na polisi na kama upelelezi ukikamilika sheria kali zitachukuliwa ikiwepo kufikishwa mahakani kwa mtumishi atakaye bainika kukutwa na makosa “ Alisema Kairuki


Alisema kuwa kuna baadhi ya Maofisa Utumishi pamoja na Wahasibu ambao wameonekana kuwa si waaminifu kwani baadhi yao wameonekana kuelekeza fedha kwa ndugu zao na miradi yao na wengine walishastaafu lakini majina yao yameonekana bado kuendelea kuwepo katika mfumo wa kupokea.

Kairuki aliongeza kuwa katika kipindi cha Machi mosi mpaka kufikia Agosti 20 mwaka huu, Watumishi hewa wapatao 16,127 walibainika ambapo walikuwa wakisababishi hasara ya mabilioni kwa serikali ambapo serikali kama ingewalipa ingesababisha hasara ya zaidi ya bilioni 16.

“Uhakiki huu ni endelevu kwani baadhi ya Maofisa Utumishi pamoja na Wahasibu si waaminifu hivyo tunawataka waajiri wao kuweka mkazo katika swala hili, kwani tunajua wahasibu wengi wamepewa madaraka lakini si waamiifu”Alisema Kiruki.

Kairuki aliwatoa hofu baadhi ya Watanzani ambao walikuwa wakisubiria ajira mpya kutoka Serikali, alisema kuwa kilichokuwa kikisubiriwa ni takwimu halisi ambazo zitasaidia kuonesha ni watumishi wangapi wameweza kuondolewa.

“hii ni neema kwa wanafunzi waliomaliza vyuo kwani kuna nafasi zipatazo 71,496 kwa mwaka huu wa fedha hivyo napenda kuwahauri vijana kuwa na subira kwa kuto kujiingiza katika makundi yasiyo faa” Alisema kairuki.

Pia aliwataka Maofisa Utumishi kuwa hudumia vizuri watumishi kwa kuwapa haki zao ikiwemo kuwa pandisha madaraja kwa wakati stahili na si vema kwa baadhi ya watu kughushi taarifa za Utumishi wa umma na kusisitiza kuwa kufanya hivyo ni kosa kuibwa sana.

Rais Magufuli kufungua maadhimisho ya wahandisi

$
0
0

Msajili wa Bodi ya Wahandisi nchini (ERB), Eng. Steven Mlote akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani), kuhusu maadhimisho ya 14 ya Siku ya Wahandisi Tanzania itakayoadhimishwa Septemba mosi jijini Dar es Salaam.(Picha Zote Na Benjamin Sawe – Maelezo).
****

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye maadhimisho ya kumi na nne ya Siku ya Wahandisi yatakayofanyika Septemba mosi hadi pili jijini Dar es Salaam.

Maadhimisho hayo ya siku mbili yanatarajiwa kukutanisha zaidi ya wahandisi elfu mbili kutoka ndani na nje ya nchi ili kupata fursa ya kufanya majadiliano ya kitaaluma, kufanya maonesho ya kiufundi na kibiashara, kuwatambua na kuwazawadia wahandisi wahitimu waliofanya vizuri katika mafunzo yao ya mwisho na kuwaapisha wahandisi waliokidhi vigezo.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Msajili wa Bodi ya Wahandisi nchini (ERB), Eng. Steven Mlote amesema mada kuu katika maadhimisho hayo itakuwa ni “TANZANIA KUELEKEA KUWA NCHI YA UCHUMI WA KATI NA KUWA NCHI YA VIWANDA: NINI JUKUMU LA WAHANDISI”.

“Tumejipanga Siku ya Wahandisi mwaka huu iwe na mvuto wa pekee kwa sababu mada yake ni ya kitaifa ikiangalia Dira ya Maendeleo ya Taifa na mwelekeo wa nchi kuwa nchi ya viwanda” amesema Eng. Mlote.

Maadhimisho ya wahandisi Tanzania yamekuwa yakifanyika tangu mwaka 2013, lengo likiwa ni kuiwezesha jumuiya ya wahandisi nchini kuionesha jamii kile ambacho wahandisi wanaweza kukifanya katika kuleta maendeleo ya nchi.

Takribani wahandisi elfu 17 wanakadiriwa kuwepo nchini katika sekta mbalimbali, lengo likiwa ni kuwa na wahandisi elfu 83 ili kukidhi mahitaji ya nchi kuwa ya kipato cha kati ifikapo mwaka 2025.

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.

Tamko La Mtandao Wa Watetezi Wa Haki Za Binadamu Dhidi Ya Mauaji Ya Askari Wa Jeshi La Polisi

$
0
0
Mtandao wa Watetezi wa Waki za Binadamu (THRDC) kwa niaba ya wanachama wake tunalani vikali maujai ya askari wa jeshi la polisi huku tukisisitiza kwamba askari wa jeshi la polisi wanaofanya kazi katika misingi na sheria ni watetezi wa haki za binadamu kama walivyo watetezi wengine. 

Kutokana na taarifa rasmi ya jeshi la polisi ni kwamba mnamo tarehe 23/08/2016 saa moja usiku maeneo ya Mbagala Mbande kata ya Mbande Temeke, majambazi ambao idadi yao haikuweza kufahamika wakiwa na silaha za moto walivamia benki ya CRDB tawi la Mbande ambapo waliwashambulia na kuwaua askari wanne wa Jeshi la Polisi waliokuwa kazini na kuwajeruhi raia wawili waliokuwa jirani na eneo hilo. 
 
Askari waliofariki katika tukio hilo ni E,5761 CPL Yahaya, F,4660 CPL Hatibu, G9524 PC Tito na G.9996 PC Gastone na raia waliojeruhiwa ni Ally Chiponda na Azizi Yahaya wote wakazi wa Mbande. 

Katika tukio hilo, majambazi hayo yalifanikiwa kupora silaha mbili za SMG na risasi sitini (60) na hakuna pesa au mali za benki iliyoibiwa, ni dhahiri kwamba walikuwa na kusudio la kujipatia silaha kwa ajili ya kufanya uhalifu na si vinginevyo kama baadhi walivyotaka kupotosha. 

Ikumbukwe kuwa majambazi mara kadhaa mwaka jana katika maeneo mbalimbali chini, mfano Kituo cha Stakishari Dar es Salaam na Kituo cha Polisi Ikwiriri , vilivyamiwa na majambazi kwa lengo la kuchukua silaha kwa ajili ya uhalifu.
 
Aidha, Tunalipongoza Jeshi la Polisi kwa kuweza kuwafikia majambazi hao huko Mkuranga bila kuumiza raia. Pia tunatoa pole kwa familia za askari wote watano waliopoteza maisha wakiwa kazini. 

Askari anaekamilsha idadi ya askari waliouwawa kufika watano ni Askari Thomas Njiku,Mkuu wa Kitengo cha Kuzuia Ujambazi alieuwa Vikindu wilayani Mkuranga wakati akiongoza kikosi maalum cha kuwasaka watu waliosadikiwa kuwa ni majambazi waliotekeleza tukio la kihalifu la Mbade,Mbagala.
 
Tunawasihi Watanzania kutoipokea dhana inayotaka kujengwa na wanasiasa kuwa hatukemei matukio haya dhidi ya polisi. 

Kumbukeni kuwa Mtandao wa Watetezi umekuwa ukitoa matamko mbali mbali kukemea mauaji ya askari wa jeshi la polisi, na tumekuwa mara kwa mara tukisisitiza kwamba askari wa jeshi la polisi ni watetezi wa haki za binadamu, kwa kuwa jukumu lao la kwanza ni kulinda mali za watu na usalama wa binadamu. 

Mtandao unatambua kuwa askari wa jeshi la polisi pia ni ndugu zetu, kaka zetu na baba zetu hivyo madhila wanayokumbana nayo ni yetu sote.
 
Mfano, katika repoti ya hali ya watetezi wa haki za binadamu kwa mwaka jana(2015) , Mtandao uliweza kuwa na kipengele maalumu kilichozungumzia haki za polisi na hali ya usalama kwa polisi wakiwa kama watetezi wa haki za binadamu.

 Katika ukarasa wa 18 wa repoti hiyo Mtandao uliweza kurekodi matukio ya uvamizi na mauaji ya jeshi la polisi zaidi ya kumi (10) na wengine watano (5) wakiachwa wamejeruhiwa. Kwa maana hii tukio lilitokea Mbagala ni muendelezo wa matukio ya kiuhalifu yanayoendelea nchini. 
 
Kumekuwa na changamoto kutoka kwa Jamii kuwatambua askari wa jeshi la polisi kama watetezi wa haki za binadamu, na hii ni kutokana na ukweli kwamba baadhi ya askari wamekuwa wakitumia vibaya madaraka yao kukandamiza haki za wananchi. 

Hali ilivyo sasa inaweza kuharibu dhana nzima ya polisi kuwa ni walinzi wa raia na mali zao, kwani vitendo wanavyofanya polisi dhidi ya raia hasa wafuasi wa vyama vya siasa na viongozi wao ni sababu kubwa ya kuharibu uhusiano mzuri kati ya polisi na raia.
 
Mtandao unatambua kwamba jeshi la polisi ni mamlaka muhimu sana katika kustawisha amani na ulinzi wa nchi kama litakuwa huru, bila kuingiliwa na wanasiasa na kuegemea upande wowote. 

Mtandao unapenda kuona kwamba Jeshi la Polisi linafanya kazi kwa weledi na kwa mujibu wa sharia na katiba ya nchi. Aidha, Mtandao unaona pamoja na migongano mbali mbali ya kazi za polisi na za wanasiasa ( hasa nafasi za wakuu wa mikoa na wilaya), ni vyema polisi wakaangalia misingi ya kimataifa ya haki za binadamu ili kuhakikisha usawa mbele ya jamii ili kurudisha mahusiano mazuri baina ya polisi na jamii wanayoitumikia.
 
Sambamba na hayo, Mtandao pia umesikikitishwa na kauli ya Mkuu wa mkoa wa Dar Es Salaam Mhe Paul Makonda aliyotoa tarehe 25 agosti 2016 wakati wa kuaga miili ya askari wanne waliouwawa huko Mbande Mkoani Dar es Salaam. Mtandao unakemea matamshi ya aina hiyo kutoka kwa kiongozi yoyote Yule, kwakuwa matamshi kama haya yanakwenda kinyume na misingi ya utawala bora na haki za binadamu na yanaweza kuwa sehemu ya kupoteza amani ya Taifa. Kitendo cha kukejeli haki za binadamu na kuamuru askari polisi wapige tu bila kujali taratibu za kisheria kinakwenda kinyume na misingi ya utawala bora.
 
Tunapenda viongozi wa serikali watambue kwamba kazi ya kulinda na kutetea haki za binadamu ni ya kikatiba na ndiyo maana kupitia Katiba yetu tuna Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora iliyoundwa kwa lengo la kuhakikisha viongozi wanaheshimu misingi ya utawala bora na haki za binadamu. Watetezi wa haki za binadamu wanatambulika kote duniani na wanalindwa kisheria mfano, kimataifa tuna Tamko la watetezi wa haki za binadamu la mwaka 1998. 
 
Madhara ya Uhusiano Mbaya kati ya Polisi na Raia
Ili Jeshi la Polisi liweze kufanya kazi yake vizuri ya kupambana na uhalifu hawana budi kuhakikisha wanakuwa karibu na wananchi. Madhara ya kutokuwa na mahusiano mazuri kati ya Jeshi la Polisi na raia ni makubwa. 
 
• Mojawapo ya madhara ni pamoja na kukua kwa makosa ya jinai na polisi kukosa taarifa za waalifu toka maoneo mbalimbali.
• Hali ya makosa ya jinai Tanzania imezidi kukua katika kiwango kikubwa. Kukua kwa makosa ya jinai ni zao la kutokuwa na mahisiano mazuri kati ya raia na polisi.
Wito wetu;
• Mtandao unatoa pole kwa Jeshi la Polisi pamoja na familia za askari hao na tunatoa wito kwa askari wengine wa jeshi la polisi kuendelea na kazi zao kwa weledi huku wakiboresha mahusiano mazuri na wananchi.
• Tunaishauri serikali kuliongezea nguvu Jeshi la polisi na kuboresh utalaamu katika kufanya kazi zao
• Tunawasihi askari wa Jeshi la wananchi kuheshimu mipaka ya kazi zao na kuheshimu haki za binadamu na katiba ya nchi katika kutekeleza kazi zao za kila siku
• Tunaishauri serkali kuwe na mabadiliko katika mfumo wa jeshi la polisi kuanzia kwenye mfumo wa kisheria ambao utatoa wajibu na uwajibikaji na kuheshimu haki za binadamu
• Tunaomba umma kutoa taarifa kwa jeshi la polisi na vyombo vya usalama hasa pale wanapohisi kuna tukio linalo ashiria uvunjaji wa amani na usalama.
• Tunaiomba serikali yetu kuipa kipaumbele jeshi la polisi katika kuboresha vitendea kazi vyao,nyumba za kuishi na mishahara bora ili kukidhi hali ya maisha ya sasa.
• Tunawaomba wadau wengine wa Haki za Binadamu pamoja na mashirika mengine ya maendeleo kukemea vikali tukio hilo. Tunashauri viongozi wa siasa waache kuingilia kazi za polisi ili kuepuka migogoro
 
PICHANI  JUU :Wakili wa THRDC akiwaonyesha waandishi wa habari(hawapo pichani) repoti ambayo ilitolewa na THRDC juu ya hali ya Watetezi wa Haki za Binadamu kwa mwaka jana(2015) ,ambayo ina kipengele maalumu kilichozungumzia haki za polisi na hali ya usalama kwa polisi wakiwa kama watetezi wa haki za binadamu katika ukarasa wa 18 wa repoti hiyo, http://thrdc.or.tz/download/situation-report-2015/

 
Imetolewa na Onesmo Olengurumwa
Mratibu wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC)
 
Imewasilishwa na Bennedict Ishabakaki
Wakili wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC)
 
30/08/2016

RIWAYA: Mwanafunzi Mchawi - (A Wizard Student) - Sehemu ya 36 & 38

$
0
0
MTUNZI:ENEA FAIDY


...Mama Eddy alitazama juu ili kuona kama kuna chochote lakini hakuona kitu. Ilimbidi atumie nguvu zake za uchawi alizokuwa Nazo ili kujilinda kwani aliziona dalili za kuvamiwa katika mazingira ya kutatanisha.

Mama Eddy ambaye jina lake halisi alijulikana kama Maimuna hakuwa Mtu wa kawaida Bali alitumwa na uongozi mkuu wa himaya aliyotokea Doreen ili kumsaidia kupata vitu alivyovihitaji.

Alitumia mbinu ya kujifanya mke wa Mr Aloyce ili kuweza kumteka vizuri na kumfanya asihangaike sana kuhusu mwanae kwani kulikuwa na uwezekano mkubwa sana wa kuharibu kazi.  Maimuna alikuwa ni kijakazi mkongwe wa Bi Tatile na alikuwa akiaminika sana katika himaya ya Wanatatile kwani ni mtu pekee aliyewahi kufanikisha ajali kubwa ya mabasi mawili iliyoua abiria wote kisha wakafanywa kitoweo katika sikukuu ya   kumpongeza Bi Tatile kama kiongozi bora wa wachawi wote Afrika Mashariki. Bi Maimuna alikuwa akiaminika sana kwa kila kazi anayoagizwa kwani hakuwahi kufanya makosa zaidi ya tukio moja tu la kuanguka kanisani akiwa katika harakati za kuwanga mchana.

"Maimuna! Maimuna! Hapa sio kwako na Leo ndio mwisho wa ubaya wako kwenye familia hii" ilisikika sauti nyororo isiyo na mkwaruzo hata kidogo huku ikijirudia rudia. Maimuna alibaki na mshangao wa ajabu sana, akataharuki huku akihema kwa nguvu. Akaaangaza macho kila upande pasipo kumuona mtu yeyote.

Akazidi kuchanganyikiwa sana. Ghafla wazo likamjia akilini mwake, bila kuchelewa akaamua kulifanyia kazi. Akanyoosha mkono wake wake wa kulia kisha nguvu nyingi zikamjia kama radi mkononi mwake. Bi Maimuna akaachia tabasamu mwanana akiamini hakuna kitakachomdhuru kwa wakati ule wala wakati mwingine wowote. akatulia kimya akimsubiri adui yake, lakini hakuona chochote zaidi ya ukimya mzito uliokuwa umetawala.
"Kumbe unaniogopa eeeh!" Alisema Maimuna.

"Ha ha ha! Sikuogopi Maimuna... Nakuvutia pumzi tu maana sina papara" sauti ile iliyojaa dharau ilisikika. Bi Maimuna hakutushika hata kidogo kwani  alikuwa anajiamini kupita kiasi. Ghafla sura yake ikabadilika sana na kuwa sura ya kutisha sana.

Meno yakawa marefu kama mnyama mkali, kucha zikawa ndefu na Kali kama za chui anayemvamia swala, macho yake yakawa meusi huku mboni yake ikiwa nyekundu kama moto. Lengo lake lilikuwa ni kuonesha nguvu zake  mbele ya adui yake ambaye hakujua ni nani. Ghafla kicheko kikali cha kutisha kilichojaa dhauri na jeuri kikasikika na kumfanya Maimuna ajione mdogo kama simimizi ilihali hamjui nana aliyemcheka.

Wakati huo huo Mlango ulifunguliwa na Mr Aloyce aliingia sebuleni pale.
"Mamaaaa" Mr Aloyce alipiga ukunga wa nguvu baada ya kumkuta mkewe akiwa na umbile la kutisha sana. Uvumilivu ulimshinda alijikuta anakimbia nje kama chizi huku akihema kwa nguvu. Mlinzi alimshangaa Mr Aloyce bila kuelewa kinachoendelea.

"Vipi bosi?" Aliuliza mlinzi huku akicheka sana. Mr Aloyce alianguka chini kama mzigo huku akihema kama Mtu aliyepanda mlima mrefu kwa kasi. Mlinzi alimsogelea na kumuuliza kilichojiri.
"Kuna maajabu humo ndani"
"Maajabu gani?"
"Mke.. Mke wangu...Ame..."

"Amefanyaje tena?" Aliuliza mlinzi kwa woga kwani alishapewa onto Kali na mwanamke yule kuwa asimfatilie kwa lolote. Lakini kabla hajasema chochote kuna kitu kiliwashtua Mr Aloyce na mlinzi wakabaki wameduwaa kwa mshangao.


Waziri Mkuu Apokea Hundi Ya Sh. Mil. 50 Kutoka NSSF

$
0
0
WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amepokea msaada wa sh. milioni 50 kutoka Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) ili kusaidia ujenzi wa shule ya sekondari Lindi iliyoungua moto usiku wa kuamkia Julai 10 mwaka huu.

NSSF imetoa msaada huo ikiwa ni utekelezaji wa ahadi yake iliyoitoa  Julai 17, 2016 katika harambee ya kuchangisha fedha za ujenzi wa majengo ya shule ya hiyo iliyoendeshwa na Waziri Mkuu .

Katika ajali hiyo, shule ya sekondari Lindi iliathirika kwa asilimia 34 ambapo vyumba tisa vya madarasa, jengo lenye matundu 26 ya vyoo na jengo la maabara ya kemia na fizikia yaliungua na kusababishia hasara ya sh. milioni 682.78.
 
Akipokea msaada huo leo (Jumanne, Agosti 30, 2016) Waziri Mkuu ameushukuru uongozi wa shirika hilo na kuwaomba wadau wengine waliotoa ahadi wazitekeleze ili waweze kukamilizsha ujenzi wa majengo hayo.

“Naamini fedha hizi zitakwenda kufanya kazi ambayo NSSF wameikusudia. Na leo hii naikabidhi kwa Meya wa Manispaa ya Lindi pamoja na  Mkurugenzi wake ili waende kuzifanyia kazi,” amesema.

Baada ya kukabidhiwa hundi hiyo na Waziri Mkuu, Meya wa Manispaa ya Lindi, Mohamed Lihumbo amelishukuru shirika hilo kwa kutimiza ahadi waliyoitoa siku ya harambee na kwamba fedha hizo hazitapotea kwa sababu zinaenda kutumika katika malengo yaliyokusudiwa.

Meya huyo amesema baada ya kukamilisha ujenzi wa shule hiyo wataanda hafla na kuwaita wadau wote waliotoa michango yao kwa ajili ya ujenzi huo ili wakaone matumizi ya michango waliyoitoa.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Prof. Godius Kahyarara amesema msaada huo ni sehemu ya mpango wa shirika hilo wa kusaidia jamii katika mambo mbalimbali kwa mujibu wa sera iliyowekwa na shirika hilo.

“NSSF imekuwa kinara kwenye Mifuko ya Hifadhi ya Jamii kwa kutoa misaada mbalimbali ya kijamii ambapo imejiwekea sera ya kusaidia katika sekta za elimu, afya na huduma nyingine muhimu za kijamii,” amesema.

Prof. Kahyarara amesema misaada hiyo haiathiri michango ya wanachama wa mfuko huo na mafao yatolewayo kwani hutokana na faida inayopatikana kwa uwekezaji makini wa mfuko huo.

Habari na Ofisi ya Waziri Mkuu

Profesa Mbarawa: Serikali haijakurupuka kununua ndege za Bombadier Q400

$
0
0
Na Abushehe Nondo na Sheila Simba-Maelezo
Serikali imesema kuwa iliamua kununua ndege mbili za abiria aina ya Bombadier Q400 kutoka nchini Canada kutokana na uhitaji wa huduma ya usafiri wa anga kwa safari za ndani ya nchi na mazingira halisi ya viwanja vya ndege vilivyopo nchini.

Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es Salaam na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya wakufunzi wa marubani katika chuo cha Taifa cha usafirishaji(NIT) 

Mbarawa alisema kuwa Serikali haikukurupuka katika kufanya maamuzi ya aina ya ndege za kununua badala yake imezingatia vigezo na malengo mahsusi ya kuhudumia usafiri wa ndani na kuboresha usafiri wa anga kupitia Shirika la Ndege Tanzania (ATCL).

“Serikali imeamua kununua aina hii ya ndege za Bombadier Q400 kutokana na hali halisi ya Viwanja vya ndege nchini kuwa vya Changarawe na lami kwa baadhi, huku lengo ni kutoa huduma za usafiri wa ndani” Alisema Profesa Mbarawa.

Mbarawa aliwataka Watanzania kuelewa nia ya Serikali yao ni kuhudumia wananchi hivyo watu wasipotoshe ukweli kuhusu ndege hizo kwani zimezingatia mambo mbalimbali ikiwemo suala la usalama na ufanisi katika uendeshaji wake.

Aliongeza kuwa ndege hizo zina uwezo wa kutua katika viwanja vingi hapa nchini kwani zinaweza kutua katika viwanja vyenye urefu wa kilomita 1.5 ambavyo ndio vingi nchini tofauti na aina nyingine ambazo hutua kwenye viwanja vyenye urefu zaidi ya kilomita mbili.

Prof. Mbarawa alibainisha sababu nyingine kuwa ni aliongeza uwezo mdogo wa ndege hizo katika kutumia mafuta ukilinganisha na aina zingine ambapo kwa safari ya kutoka Dar es Salaam hadi Mwanza zitakuwa zikitumia Tani 1.7 za mafuta tofauti na aina nyingine zinazotumia hadi Tani 2.8 kwa safari moja.

Waziri Mbarawa pia alitumia fursa hiyo kukanusha uvumi ulionezwa kuwa ndege hizo zimenunuliwa katika kampuni ndogo isiyokuwa na sifa na kubainisha kuwa suala hilo siyo la kweli kwani kampuni hiyo imefanya biashara na nchini nyingi ikiwemo Ethiopia yenye ndege t19 aina ya Bombadier Q400 zilizotengezwa na  Kampuni hiyo.

Mpaka sasa tayari Serikali imeshafanya malipo ya ununuzi wa ndege hizo kwa asilimia 40 ambapo ndege hizo zinatarajiwa kuwasili nchi tarehe 19 septemba mwaka huu ambapo zitaanza safari ya kutoka nchini Canada tarehe 15 septemba mwaka huu kupitia nchini Uingereza.

Akizindua mafunzo hayo ya wakufunzi wa  marubani, Waziri Mbarawa aliwaasa Marubani ambao watahitimu mafunzo hayo  kuhakikisha wanazingatia suala na nidhamu na uadilifu katika sekta hiyo ya usafiri wa anga.

“Hatutaki kuwa na marubani ambao wana uwezo wa kazi lakini sio waadilifu,hakikisheni mnawafundisha marubani wanafunzi kuzingatia nidhamu na uadilifu katika sekta hiyo ya anga ambapo wakati mwingine Rubani anajijua anakasoro lakini bado anang’ang’ania kurusha ndege” alisema Prof.Mbarawa.

Aidha amesema kuwa Serikali itashirikiana na chuo hicho katika kutoa kozi za urubani ili kuakabiliana na changamoto ya ukosefu wa marubani nchini. 
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akiendesha ndege kwa kutumia kifaa maalum cha kufundishia marubani (simulator) kwenye chumba cha mafunzo kwenye Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT).
Mkuu wa chuo cha Taifa cha Usafirishaji Profesa Zacharia Mganilwa akizungumza na wadau wa sekta ya usafiri wa anga (hawapo pichani) katika uzinduzi wa mafunzo ya wakufunzi wa marubani uliofanyika jijini Dar es salaam.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akifafanua jambo kwa wadau wa sekta ya usafiri wa anga (hawapo pichani) katika uzinduzi wa mafunzo ya wakufunzi wa marubani uliofanyika jijini Dar es salaam.
Wadau wa sekta ya usafiri wa anga wakimsikiliza Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa katika uzinduzi wa mafunzo ya wakufunzi wa marubani uliofanyika jijini Dar es salaam.

Safari Lager kuliteka soko na bia mpya ya kopo yenye ujazo wa 500ml

$
0
0
Kampuni ya Bia ya TBL kupitia bia yake ya Safari lager imezindua bia ya kopo ya kwanza yenye ujazo wa mililita 500 kwa bia ya Kitanzania. 

Akizungumza katika uzinduzi uliofanyika jijini Dar, Meneja Bidhaa wa Safari Lager, Edith Bebwa Nasuwa alisema “Ni bia ya kwanza ya Kitanzania ya kopo yenye ujazo wa mililita 500 ambayo italeta urahisi, unafuu na ladha nzuri ya aina yake kwa wapenzi wote wa bia ya Safari Lager”

Bia hii ya kopo tayari imeshaanza kupatikana maeneo yote nchini kuanzia tarehe 26 Agosti 2016 na imeelezewa kuwa ni bia ya wajanja wenye kujiamini.

“Bia mpya ya kopo ya Safari ni dhahiri kwamba imetengezwa kumpa umahiri Mtanzania katika safari ya maisha yake. Inapatikana kwa urahisi na kwa wakati muafaka hata wakati mtu anakwenda kwenye mihangaiko yake au kubeba akiwa anakwenda kwenye matembezi au safarini” alimalizia Edith Bebwa.

Fuatilia kurasa za Safari Lager kupata habari zaidi





Jukwaa la wahariri lalaani Serikali kufungia redio

Taarifa kutoka SADC: Ukuaji wa demokrasia unaendelea kuimarika katika nchi wanachama.

$
0
0


Mwenyekiti anayemaliza muda wake wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika -SADC- ambaye pia ni Rais wa Botswana Luteni Jenerali Dkt Seretse Khama Ian Khama amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli kwa kuchaguliwa kwake kwa kishindo katika uchaguzi mkuu uliofanyika mwaka jana.

Rais huyo wa Botswana ametoa kauli hiyo ya pongezi katika hotuba yake kwenye ufunguzi wa Mkutano wa 36 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa SADC unaofanyika Mbabane- Swaziland ambapo Katika Mkutano huo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli anawakilishwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.

Rais huyo wa Botswana amesema ukuaji wa demokrasia katika nchi wanachama wa jumuiya ya SADC unaendelea kuimarika hivyo ni muhimu jitihada hizo zikaendelezwa zaidi.

Amesema ana Imani  kubwa na Viongozi waliochaguliwa kwa njia ya amani,uhuru  na haki katika ukanda wa SADC akiwemo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Jamhuri ya Visiwa shelisheli kwamba watafanya kazi kwa bidii ili kuharakisha maendeleo kwa wananchi wao.

Wakuu wa nchi na Serikali wa SADC katika mkutano huo wameshuhudia utoaji wa zawadi mbalimbali kwa wanafunzi waliofanya vizuri katika utunzi wa insha na kwa wanahabari ambao wameandika habari mbalimbali kuhusu SADC ikiwemo masuala ya huduma ya maji.

Aidha Katika Mkutano huo wa 36 wa SADC viongozi wanaohudhuria watafanya uchaguzi wa Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa SADC na Uchaguzi wa Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa Asasi ya SADC ya Siasa, Ulinzi na Usalama ( SADC Troika)

Katika mkutano huo Wakuu wa nchi na serikali pia watapokea rasimu za maboresho ya mikataba mbalimbali kutoka kwenye Baraza la Mawaziri kwa ajili ya kutia saini. Miongoni mwa rasimu hizo ni mkataba wa kuboresha itifaki ya SADC dhidi ya rushwa, maboresho ya itifaki ya ushirikiano wa siasa, ulinzi na usalama ya SADC na maboresho ya itifaki ya biashara.

    Imetolewa na

    Ofisi ya Makamu wa Rais

    Mbabane- Swaziland

    30-Aug-16

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa afanya mazungumzo na Mfanyabiashara Mohammed ‘MO’ Dewji

$
0
0


WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amesema wafanyabiashara wanaokwepa kulipa kodi wanaiathiri Serikali katika juhudi zake za kuboresha maisha ya Watanzania.

Amesema Serikali haina mgogoro na wafanyabiashara bali inawataka walipe kodi na kama kuna wanaonewa na watendaji wa chini kwa kubambikiziwa kodi watoe taarifa juu ya jambo hilo.

Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo (Jumanne, 30 Agost, 2016) wakati akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa Makampuni ya Mohamed Enterprises Tanzania Limited (MeTL), Mohamed Dewji, ofisini kwake jijini Dar es Salaam.

Amesema Serikali imedhamiria kuwaunga mkono wafanyabiashara katika shughuli zao ili waweze kulipa kodi itakayoifanya imudu kuwahudumia wananchi katika huduma mbalimbali za jamii.

“Sisi msisitizo wetu ni ulipaji kodi, wakwepa kodi wanatuathiri. Sekta nyingine zinashindwa kuendelea kwa sababu hazina mtaji na kodi hazipatikani vizuri,” amesema.

Amesema “Ninyi timizeni wajibu wenu kwa kulipa kodi stahiki, tutawasaidia katika kufanya biashara zenu. Tutawasaidia katika kusimamia mambo yenu ila mjue kwamba nchi hii bila viwanda hatuwezi kwenda,”.

Pia amewataka wafanyabiashara kwenda kujenga viwanda katika maeneo ambayo malighafi zinazalishwa ili kuwahamasisha wakulima kuzalisha zaidi na kuwapunguzia mzigo wa kusafirisha malighali hizo.

Kwa upande wake Dewji amemuhakikishia Waziri Mkuu kwamba wafanyabiashara wanaiunga mkono Serikali ya Awamu ya Tano na hawana mpango wowote wa kuhamishia mitaji yao nje ya nchi kama inavyodaiwa na baadhi ya watu.

“Huu ni uongo na uzushi tu ambao watu wameamua kuusambaza, mfano mimi mwenyewe nimeanza kuongeza mitaji katika biashara zangu. Nimefufua kiwanda cha kuchambua pamba cha Chato. Nafungua biashara zingine mpya kubwa ikiwemo ya kufufua kiwanda cha nguo cha Musoma ambacho kitakuwa kinatengeneza jeans za kuuza nje ya nchi,” amesema.

Amesema yuko tayari kuwekeza kwenye ujenzi wa kiwanda cha sukari katika wilaya ya Rufiji mkoani Pwani. Kiwanda hicho kitakuwa na uwezo wa kununua miwa tani milioni 1.2 zitakazozalisha tani 120,000 za sukari kwa mwaka.

Mkurugenzi huyo amesema amepanga kuwekeza sh. bilioni 40 kwa ajili ya kukuza uzalishaji katika mashamba yake ya mkonge kwenye mikoa ya Pwani, Tanga na Morogoro.

Pia amewekeza sh. bilioni 70 katika viwanda vya kusaga unga wa ngano na sembe na anatarajia kununua tani laki moja za mahindi katika msimu wa mwaka huu.

Mbali na kuwekeza katika viwanda hivyo Dewji amesema anatarajia kujenga kiwanda kikubwa cha kutengeneza sabuni ya unga ambacho kitakuwa ni kikubwa kuliko vyote katika nchi za Afrika Mashariki na Kati.

“Tumeamua kuongeza uwekezaji katika viwanda ili kuunga mkono mkakati wa Serikali wa kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda. Vile vile nimefanikiwa kuishawishi kampuni kubwa na maarufu ya kutengeneza sigara duniani ya Marlboro kuingia nayo ubia na sasa tunajenga kiwanda cha sigara hizo mjini Mrogoro,” amesema.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
2 MTAA WA MAGOGONI,
S. L. P. 3021,
11410 DAR ES SALAAM.
JUMANNE, AGOSTI 30, 2016.

Rais Magufuli Awaalika Wafanyabiashara wa Cuba Kuja Kuwekeza Nchini

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amewaalika wafanyabiashara wa Cuba na Serikali ya nchi hiyo kuja hapa nchini kuwekeza katika uzalishaji wa sukari na kujenga viwanda vya kutengeneza dawa za binadamu.

Rais Magufuli ametoa mwaliko huo leo tarehe 30 Agosti, 2016 Ikulu Jijini Dar es Salaam alipokutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Cuba hapa nchini Mhe. Jorge Lopez Tormo.

Dkt. Magufuli amemhakikishia Balozi Jorge Lopez Tormo kuwa Serikali yake itatoa ushirikiano wa kutosha endapo mfanyabiashara yeyote wa Cuba au Serikali yenyewe ya Cuba itajitokeza kuwekeza katika uzalishaji wa sukari na utengenezaji wa dawa za binadamu, na kwamba licha ya Tanzania kuwa na mahitaji makubwa ya bidhaa hizo kuna nchi nyingi jirani na Tanzania zitanufaika.

"Mhe. Balozi ukiniletea huyo mwekezaji hata kesho nitamkabidhi shamba la kuzalisha miwa na kujenga kiwanda cha kuzalisha sukari mara moja ili uzalishaji uanze, tunataka kumaliza tatizo la sukari, uzalishaji wa sasa wa sukari hautoshelezi mahitaji yote ya Tanzania na pia majirani zetu wana upungufu wa sukari" Amesema Rais Magufuli na kuongeza kuwa yapo maeneo mengi yanayofaa kwa kilimo cha miwa likiwemo eneo la Bagamoyo ambako kuna hekta takribani 10,000.

Hali kadhalika Rais Magufuli amesema Serikali ipo tayari kutoa ardhi kwa mwekezaji yeyote kutoka Cuba atakayekuwa tayari kujenga kiwanda cha kutengeneza dawa za binadamu na vifaa tiba hapa nchini.

Kwa upande wake Balozi Jorge Lopez Tormo amempongeza Rais Magufuli kwa juhudi kubwa anazozifanya katika uendeshaji wa Serikali na amemhakikishia kuwa Cuba itaendeleza na kuimarisha uhusiano na ushirikiano mzuri na wa kihistoria uliopo kati yake na Tanzania, na ameahidi kufanyia kazi yote waliyoyazungumza.

Wakati huo huo, Rais Magufuli amekutana na kufanya Mazungumzo na Balozi wa India hapa Nchini Mhe. Sandeep Arya ambapo Balozi huyo ametoa taarifa ya hatua zinazoendelea kuchukuliwa baada ya ziara ya Waziri Mkuu wa India Mhe. Narendra Modi iliyofanyika Mwezi Julai mwaka huu.

Katika mazungumzo hayo Balozi Sandeep Arya amesema wawekezaji kutoka India wanaendelea na majadiliano na Shirika la Maendeleo ya Petroli (TPDC) juu ya utekelezaji wa mradi wa kusambaza gesi majumbani kwa ajili ya matumizi ya wananchi na pia wanajadiliana na Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi juu ya kuongeza uzalishaji wa mazao ya jamii ya kunde ili kulisha soko kubwa la mazao hayo nchini India.

Kuhusu ujenzi wa kiwanda cha magari cha Tata, Balozi Sandeep Arya amesema mchakato unaendelea na kwamba tayari wameoneshwa eneo la kujenga kiwanda hicho lililopo Kibaha Mkoani Pwani na matarajio ni kuwa ujenzi wa kiwanda hicho utakamilika mwaka ujao.

Kwa upande wake Rais Magufuli ameelezea kufurahishwa na uwepo wa miradi hiyo itakayoleta manufaa kwa pande zote mbili yaani Tanzania na India na ametoa wito kwa pande zote kuharakisha majadiliano ili utekelezaji wa miradi hiyo uanze haraka.

Aidha, Rais Magufuli amewakaribisha wawekezaji wa India kuja kujenga hospitali kubwa za matibabu ya binaadamu na kujenga viwanda vya kutengeneza dawa za binadamu huku akibainisha kuwa hatua hiyo itasaidia kupunguza gharama za matibabu kwa watanzania na wananchi wa nchi nyingine jirani na Tanzania wanaolazimika kusafiri hadi nchini India kufuata matibabu.

"Wambie wafanyabiashara wa India walio tayari kujenga hospitali kubwa, waje na mimi nitawapa ardhi ya kujenga hospitali, wasipoteze muda waje sasa" Amesisitiza Rais Magufuli.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es Salaam

30 Agosti, 2016


Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumatano ya Agosti 31

Lowassa Aandika Waraka Mzito Kuhusu Oparesheni UKUTA.....Asimulia Kilichomfanya Akutane na Rais Magufuli

$
0
0
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Edward Lowassa ameandika barua kuhusu operesheni ya chama chake iliyopewa jina la Ukuta na jinsi ambavyo jeshi la Polisi na Serikali lilivyopanga ‘kuubomoa’.

Katika waraka huo, Lowassa ameeleza kuwa ameamua kushika kalamu na kuandika masikitiko yake kuhusu hali ya amani nchini akidai Serikali imekata mkono wa amani.

Ameeleza kuwa Serikali imekandamiza upinzani na demokrasia na ndio chanzo cha wao kuanzisha UKUTA kupinga ukandamizaji huo.

“Binafsi nafurahishwa na kutiwa moyo na jinsi watanzania walivyoipokea Operesheni hii, pamoja na vitisho vya dola,” ameandika. “Siku zote sisi Chadema na Ukawa kwa ujumla ni wenye kulitakia amani na utulivu Taifa letu. Maandamano haya ya Septemba 1 ni ya amani, lakini vitendo vya jeshi la polisi vimewapa wasiwasi Watanzania,” Lowassa ameongeza.

Katika andiko hilo, Lowassa amedai kuwa amekuwa akipigiwa simu na viongozi wastaafu pamoja na watu mashuhuri wakimshauri kushawishi wakae na Serikali kuzungumza ili kuepusha taifa kujiingiza katika machafuko. Aliongeza kuwa kukutana na Rais John Magufuli katika Jubilee ya miaka 50 ya ndoa ya Rais Mstaafu, Benjamini Mkapa ni sehemu ya juhudi hizo.

“Nyote ni mashahidi wa tukio la kukutana na Rais Magufuli katika Jubilei ya miaka 50 ya ndoa ya mzee Mkapa. Ulikuwa ni mwanzo wa juhudi zetu za kuwanyooshea mkono wa amani. Lakini tunashangazwa wenzetu hawako tayari kuupokea mkono huo,” ameandika.

Aliongeza kuwa katika kikao cha juzi cha ndani cha chama hicho kilichofanyika katika Hotel ya Giraffe jijini Dar es Salaam walipanga kuzungumzia jinsi ya kuunyosha zaidi mkono wa amani lakini Jeshi la Polisi ‘liliukata’.

“Kitendo kile kwangu binafsi kimezidi kuniimarisha na kunipa nguvu zaidi ya kudai demokrasia na kuheshimu katiba ambayo viongozi wetu waliapa kuifuata na kuitetea,” unasomeka waraka wa Waziri Mkuu wa zamani, Lowassa.

Makusanyo Kodi za Simu Yapanda Maradufu

$
0
0
Sheria ya Fedha ya Mwaka 2016 iliyopitishwa kuhusu utozaji ushuru kwenye ada ya kutuma na kupokea fedha kwenye miamala ya benki na simu, imeanza kuzaa matunda kutokana na ongezeko la mapato lililoanza kushuhudiwa kutoka kampuni za simu.

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu iliyokutana jana na Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA), iliambiwa kutokana na sheria hiyo iliyopitishwa Bunge baada ya kupitisha bajeti ya mwaka huu, mwezi uliopita serikali imeshuhudia ongezeko kubwa la mapato, yaliyotolewa na kampuni za simu.

Taarifa hiyo ilitolewa jana kwenye Kamati ya Kudumu ya Miundombinu, imeonesha Kampuni ya Vodacom ilikuwa ikitoa kodi ya ushuru wa bidhaa kwa fedha zinazotumwa kwa wastani wa Sh milioni 360 kwa mwezi, lakini baada ya mabadiliko ya sheria, Julai pekee mwaka huu imelipa Sh bilioni 1.9.

Mwakilishi wa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato (TRA), Godwin Barongo aliiambia kamati hiyo kuwa kwa upande wa Kampuni ya Tigo, walikuwa wanatoa wastani wa Sh milioni 250 kwa mwezi, lakini sasa wametoa Sh bilioni 1.48.

Barongo ambaye ni Meneja Msaidizi, Kitengo cha Walipa Kodi Wakubwa TRA alikuwa akizungumzia namna Mtambo Maalumu wa Kusimamia Mawasiliano na Udhibiti wa Mapato yatokanayo na Simu (TTMS) unaosimamiwa na Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA) ulivyowezesha kufanikisha ukusanyaji mapato.

“Pamoja na mabadiliko ya sheria yaliyoanza mwezi Julai mwaka huu, kampuni za simu zilikuwa zikitoza transfer, lakini sheria ilikuwa haigusi kwenye kutoa, Baada ya hiyo, tuligundua kuwa sasa kamisheni nyingi zilipelekwa kwenye kutoa kwa sababu hakuna tozo na kwenye transfer zinapungua,” alisema Barongo.

Aliendelea kusema, “Kwa hiyo mabadiliko haya ya sheria ya sasa hivi ambayo tunatoza kwenye kuweka na kutoa, yametusaidia.” 

Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, Selemani Kakoso alisisitiza kuwa wabunge wanategemea Wizara ya Miundombinu kupitia sekta ya mawasiliano, ichangie mapato mengi kwa serikali.

Baada ya Bunge kupitisha mabadiliko ya sheria ya fedha yaliyopitisha utozaji kodi ya ushuru wa bidhaa katika miamala ya benki na simu za mkononi, ulijitokeza mjadala ambao baadhi ya watu walidai ushuru huo utaathiri wateja wa kampuni za simu na benki.

Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango alifafanua kwamba serikali imeamua kutoza ushuru kwenye ada ya kutuma na kupokea fedha au vyote kwa kadri itakavyotozwa akisisitiza kwamba utalipwa na benki na kampuni na si mtumiaji au mpokeaji wa fedha katika miamala itakayofanyika.

Ndege za Kivita Kutawala Anga la Dar Septemba 1

$
0
0
Septemba mosi mwaka huu inataraji kuingia katika histori ya Tanzania kutokana na matukio ambayo yanataraji kufanyika siku hiyo, matukio hayo ni pamoja na sherehe za miaka 52 ya Jeshi la Wananchi la Tanzania (JWTZ), maandamano ambayo yamepangwa kufanywa ya UKUTA na tukio la kupatwa kwa jua.

Akizungumza na Waandishi wa Habari wakati alipokutana na Maafisa wa Jeshi la JWTZ Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda alisema JWTZ inapotimiza miaka 52 ni fahari kubwa hivyo tunapaswa kuwapongeza kwa kudumisha amani na mshikamano.

Alisema Jeshi hilo limejipanga kurusha angani ndege zake za kivita katika anga la Dar es Salaam, Septemba 1 mwaka huu, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 52 ya kuanzishwa kwake.

Makonda aliwataka wananchi kutokuwa na hofu wanaposikia ngurumo za ndege hizo bali wafurahie kwani ni ndege zao.

“Mnaposikia milio ya ndege zetu mbalimbali, mfurahie kwa sababu hizo ni ndege za wananchi. Usisikie muungurumo ukashtuka. Hakuna jambo lolote lile zaidi ya kuonesha vifaa vyetu na jinsi ambavyo wanajeshi wetu kwa miaka 52 wamaeendelea kuwa imara na vifaa vizuri,” alisema Makonda.

Aidha, Mkuu huyo wa Mkoa waliwataka wananchi waliojipanga katika vikundi mbalimbali kuripoti kwa wakuu wao wa wilaya kujiandikisha ili waweze kushiriki pamoja na Jeshi hilo katika zoezi la usafi jijini humo.

Aliwataka wakazi wa mkoa huo pia kujitokeza kuchangia damu katika vituo mbalimbali ambavyo vimeanishwa ili kuunga mkono juhudi za uchangiaji damu zitakazofanywa na wanajeshi wa JWTZ.

“Hii ni sehemu ya amani, tufanye usafi kwa amani. Tujitolee damu zetu kwa amani na mwisho wa siku tuwaenzi na kuwapongeza wanajeshi wetu kwa kazi kubwa wanayoifanya,” Makonda alieleza.

Katika hatua nyingine, Mkuu huyo wa Mkoa aliendelea kutoa onyo kwa watu watakaotaka kufanya maandamano yaliyopigwa marufuku ya oparesheni UKUTA akiwataka kutii sheria.

“Mimi ninavyojua UKUTA ni kuwa mtu amefika mwisho wa kufikiri sasa kama watakuwa wamefika mwisho wa kufikiria basi sisi tutawasaidia … watu wapo wanapanga kufanya mambo ya kusaidia jamii wao wanapanga maandamano nawashauri wananchi waungane na Polisi,” alisema Makonda.

Lowassa, Mbowe Watakiwa Kuripoti Polisi Keshoi Septemba 1

$
0
0
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama hicho, Edward Lowassa na viongozi wengine waandamizi wameitwa na Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam kwenda kuripoti kesho Septemba Mosi.

Hatua hiyo inatokana na viongozi hao kukamatwa juzi, baada ya kufanya mkutano maalumu wa ndani wa Kamati Kuu, na walipelekwa Kituo Kikuu cha Polisi cha Kanda hiyo na kuhojiwa kabla ya kuachiwa.

Mbali na Mbowe na Lowassa, viongozi wengine wa Chadema waliokamatwa na kutakiwa kwenda Polisi kesho ni Katibu Mkuu, Vincent Mashinji, Naibu wake, John Mnyika na Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho, Said Issa Mohammed.

“Wameitwa Polisi waende Septemba mosi kuripoti baada ya jana kukamatwa na kuhojiwa wakituhumiwa kukiuka maagizo ya Polisi,” alisema Msemaji wa Chadema, Tumaini Makene na kufafanua:

“Lakini wanaweza kwenda au wakaanzia kwenye maandamano kisha wakaenda Polisi kuripoti.”

Alisema maandamano hayo yatakuwapo kama yalivyopangwa kwani maandalizi yake yamekamilika.

Habari zaidi zilieleza, kwamba jana mchana viongozi hao walikuwa wakifanya kikao Makao Makuu ya chama hicho Kinondoni Dar es Salaam, ambapo pia walikutana na wabunge wote wa chama hicho kwa makundi tofauti.

Kwa mujibu wa mtoa habari ndani ya Chadema makao makuu katika kikao hicho walijadili mambo mengi ikiwa ni pamoja na suala la utekelezaji wa Ukuta kesho.

Mmoja wa wabunge wa Chadema alisemai kwamba walikuwa wakiwekana sawa kuhusu maandamano yao.

Alibainisha kwamba katika mkutano huo ambao Mbowe hakuwepo pia walijadili maombi ya viongozi wa dini kuwataka kusitisha maandamano hayo Septemba mosi.

“Viongozi wa dini wamekuwa wakituomba tusitishe maandamano ya Ukuta Septemba mosi, tusubiri hadi baada ya mkutano wa vyama vya siasa Septemba tatu,” alisema Mbunge huyo wa Kanda ya Ziwa.

Aliongeza: Katika mkutano huo, Lowassa na viongozi wengine walijadili hayo na ikikubalika kwa heshima ya viongozi wa dini maandamano ya Ukuta yafanyike baada ya Septemba tatu.”

Hata hivyo, mwandishi alishuhudia wabunge wengi wa chama hicho wakitoka katika mkutano huo kimya kimya bila kutaka kuzungumza na kabla muda uliopangwa kwisha, huku taarifa zikieleza kwamba mkutano huo uliahirishwa baada ya kuwepo taarifa za kutaka kuvamiwa na Polisi.

“Tumeambiwa tusambaratike, tutajulishwa wapi tutakutana tena, kama hapa au wapi,” alidokeza mmoja wa wabunge hao.

Baada ya mkutano huo kuahirishwa, Lowassa alitoka eneo hilo huku taarifa zikieleza alikuwa akielekea kwenye moja ya hoteli jijini humo kuungana na Mbowe ambapo walikuwa na mazungumzo na baadhi ya viongozi wa dini.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images