Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Bado wiki tatu Mbowe atimuliwe Bilicanas

$
0
0
Zimebaki wiki tatu kabla Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kuchukua jengo la Bilicanas lililokodiwa na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, kuendesha biashara ya ukumbi wa starehe.

Jengo hilo lipo eneo la Posta jijini Dar es Salaam.Awali, NHC ilikuwa imetoa notisi ya siku 60 kwa wadaiwa sugu ambao wamepanga katika majengo yake akiwamo Mbowe.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Nehemia Mchechu, alisema pamoja na Bilicanas, shirika linazidai taasisi za umma, binafsi na watu binafsi jumla ya Sh. bilioni 15.

Notisi ya siku 60 ya kuondoka Bilicanas pamoja na majengo ya wadaiwa wengine ilishatolewa, Mchechu alisema na kwamba sasa zimesalia wiki tatu.

Alisema baada ya muda huo kumalizika, utekelezaji wa kuondolewa katika majengo hayo utaanza ukiambatana na uchukuaji wa hatua za kisheria.

Mchechu alisema mbali ya Bilicanas, wadaiwa wengine ni Wizara ya Mawasiliano na Uchukuzi inayodaiwa Sh. bilioni mbili, Benki ya Azania (Sh. milioni 161) na Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa (Sh. milioni 631).

Wadaiwa wengine walitajwa kuwa ni Wizara ya Afya na Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Sh. bilioni 1.3), Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sh. bilioni mbili), Tume ya Utumishi (Sh. milioni 109) na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Sh. bilioni moja.

Mchechu alisema ukusanyaji wa madeni hayo kwa nguvu ni mkakati wa shirika hilo kukusanya fedha ili kusaidia ujenzi wa nyumba za watumishi wanaohamia Dodoma.

Alipoulizwa iwapo mkakati huo una uhusiano wowote na masuala ya kisiasa kutokana na kumtaja Mbowe kuwa ni kati ya wadaiwa sugu, Mchechu alisisitiza hakuna uhusiano wa siasa na zoezi hilo kwani wateja wote wanachukuliwa sawa.

“Mwaka huu ujenzi unaanza Dodoma," alisema Mchechu, hivyo fedha tunazodai zitatusaidia kukamilisha uwekezaji mjini humo."

“Ndiyo maana tumetoa kwa tunaowadai notisi ya miezi miwili, vinginevyo wataondolewa katika majengo ya shirika kama kanuni zinavyotaka.

“Hakuna uhusiano wowote kati ya shirika kukusanya fedha linazodai na watu binafsi akiwamo Mbowe, taasisi za umma na binafsi.

“Lengo ni kukusanya madeni ambayo baadhi yake yalisimama kutokana na mengine kuwa na kesi mahakamani.”

Alisema kuwa fedha hizo zitatumika kwa ujenzi wa nyumba za watumishi 300 hadi 500 mkoani Dodoma.

Alisema ujenzi huo unatarajia kuanza mara moja na utachukua miezi 12.

Kwa mujibu wa Mchechu, Sh. bilioni 60 za ujenzi wa nyumba hizo zitatokana na fedha za ndani.

Alisema shirika hilo limenunua ekari 240 eneo la Iyumbu, ekari saba Chamwino, nne Bahi na Chemba ekari nne pia ikiwa ni kuunga mkono azma ya Serikali ya Awamu ya Tano kuhamia Dodoma.

Alisema fedha nyingine zitapatikana baada ya nyumba 97 za shirika hilo zilizopo Medeli mjini Dodoma kuuzwa.

Aidha, Mchechu alisema kitendo cha Serikali kuhamia Dodoma kitatoa fursa kwa Jiji la Dar es Salaam kujiimarisha kibiashara tofauti na ilivyo sasa ambapo linakwamishwa na foleni kubwa za magari kutokana na shughuli nyingi za serikali kufanyika.

“Dar es Salaam kuna bandari, uwanja wa ndege," alisema na kuongeza: “Hivyo suala la kiuchumi litaimarika zaidi kutokana na shughuli nyingi za Serikali kuhamia Dodoma. Hii itasaidia uchumi wa nchi kusambaa katika maeneo tofauti nchini.”

Uwekezaji wa NHC jijini Dar es Salaam upo kwa asilimia 70, alisema na kwamba ufanisi wa Jiji utaongezeka hususani katika usafiri na sekta nyingine kiuchumi.


Taarifa Kwa Wateja Wa Nmb Na Umma Kwa Ujumla

Waziri Mkuu Atoa Siku Mbili Kwa Maofisa Ardhi Kumaliza Kero Za Wananchi

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ametoa siku mbili kwa Mkuu wa Idara ya Ardhi na Miundombinu wa mkoa wa Rukwa pamoja na Ofisa Ardhi wa Manispaa ya Sumbawanga kutatua matatizo ya ardhi yanayowakabili wakazi wa Manispaa hiyo.

“Ijumaa kuanzia saa 3.00 asubuhi wenye kero za ardhi wote waende kwenye ukumbi wa Manispaa mkuu wa idara atakuwa na watumishi wote na hapa mtasikilizwa kero zenu na kupatiwa ufumbuzi. Nasiku hiyo hakuna kazi nyingine ni kusikiliza wananchi tu,” alisema.

Waziri Mkuu ametoa agizo hilo jana jioni (Jumatano, Agosti 24, 2016) wakati akizungumza na maelfu ya wakazi Mji wa Sumbawanga waliojitokeza katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye kiwanja cha Mandela katika jimbo la Sumbawanga mjini ambapo aliwasisitiza watendaji hao kuwasikiliza wananchi na kutatua kero zao.

Alisema tangu alivyoanza ziara yake katika mikoa ya Rukwa na Katavi kila eneo alilopita amekutana na wananchi wakiwa na mabango yanaeleza changamoto na hii inatokana na viongozi wa mikoa hiyo kushindwa kutenga siku maalumu kwa ajili ya kusikiliza kero hizo.

Waziri Mkuu alibainisha kwamba baadhi ya mikoa na halmashauri mbalimbali nchini zimeshaanza utaratibu huo wa kutenga siku maalumu katika wiki na kusikiliza matatizo yanayowakabili wananchi jambo ambalo limeanza kuonesha mafanikio ya utatuzi wa kero hizo.

Awali akizungumza katika mkutano huo mbunge wa jimbo la Sumbawanga Mjini Aeshi Hilaly alisema wakazi wa Manispaa ya Sumbawanga wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ya migogoro mikubwa ya ardhi, hivyo alimuomba Waziri Mkuu kuwasaidia katika kuipatia ufumbuzi.

Mbunge huyo alisema migogoro hiyo ambayo imedumu kwa muda mrefu imewasababishia usumbufu mkubwa wakazi wa jimbo hilo kukosa haki  zao na muda mwingi wamekuwa wakiutumia kufuatilia hatma ya ardhi yao bila ya mafanikio hivyo kurudi nyuma kimaendeleo.

Pia mbunge huyo alimuomba Waziri Mkuu kuwaondolea zuio la kuuza mazao yao nje ya nchi kwa sababu kitendo hicho kimesababisha kushuka bei ya mahindi na kusababisha hasara kubwa kwa wakulima ambao wametumia gharama kubwa katika kuandaa mashamba.

Akizungumzia zuio hilo Waziri Mkuu alisema lengo la Serikali kuzuia uuzwaji wa mazao nje ni kutaka kujiridhisha na uwepo wa chakula cha  kutosha nchini ili kuepuka kukumbwa na baa la njaa na kisha kwenda kuomba msaada kwenye nchi tuliowauzia.

 Kuhusu suala la soko la mahindi Waziri Mkuu alisema Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) watanunua kwa bei ya soko na kwamba wataruhusiwa kuuza nje ya nchi baada ya Serikali kujaza maghala yake huku wataalam wakimalizia kufanya tathmini ya hali ya chakula nchini

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
.

Taarifa kuhusu uteuzi wa Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) Uliofanywa na Rais Magufuli Leo

$
0
0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 25 Agosti, 2016 amemteua Bw. Andrew Wilson Massawe kuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA).

Kabla ya uteuzi huo Bw. Andrew Wilson Massawe alikuwa Mkurugenzi wa Mifumo ya Kompyuta katika Benki Kuu Tanzania (BOT).

Bw. Andrew Wilson Massawe anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Dkt. Modestus Francis Kipilimba ambaye ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa.

Uteuzi wa Bw. Andrew Wilson Massawe unaanza mara moja.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es Salaam
25 Agosti, 2016

Waziri Mkuu: Tatizo La Maji Sumbawanga Kuwa Historia.

$
0
0

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary wakifurahia ngoma ya asili ya kabila la Wafipa wakati walipowasili kwenye kijiji cha Mtowisa mkoani Rukwa kuzungumza na wanachi Agosti 24, 2016.

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Manispaa ya Sumbawanga mkoani Rukwa inatarajiwa kupata huduma ya maji safi na salama kuanzia mwezi ujao baada ya kukamilika kwa mradi mkubwa wa maji uliokuwa unajengwa.

Mradi huo unajengwa kwa usimamizi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira, Manispaa ya Sumbawanga (SUWASA), kwa ufadhili wa nchi za Umoja wa Ulaya (EU) na Serikali ya Ujerumani kupitia benki yake ya Maendeleo (KfW), sh. bilioni 31 utakapokamilika.

Waziri Mkuu alitoa kauli hiyo jana  (Jumatano, Agosti 24, 2016) wakati na akiweka jiwe la msingi la mradi wa maji safi na usafi wa mazingira katika Manispaa ya Sumbawanga na kuitaka kampuni ya kampuni ya Techno Fab Gammon Joint Venture ya India kumaliza ujenzi wa mradi huo haraka iwezekanavyo.

Amesema mradi huo ambao tayari umekamilika kwa asilimia 85 unatarajiwa kukamilika Septemba mwaka huu, hivyo aliwataka wananchi kuhakikisha wanashirikiana na Manispaa katika kulinda miundombinu ya mradi huo mara utakapokamilika pamoja na kutunza vyanzo vya maji.

“Pamoja na Serikali kutumia fedha nyingi kwa ajili ya kugharamia miradi ya maji inayojengwa katika maeneo mbalimbali nchini,changamoto ya upatikanaji wa huduma hiyo imekuwa kubwa kutokana na baadhi ya visima vimeanza kukauka hali inayosababishwa na uharibifu wa mazingira,” amesema.

Amesema kumekuwa na uvamizi mkubwa katika maeneo ya vyanzo vya maji ambapo wananchi wanajishughulisha na shughuli za ulimaji, uchungaji wa mifugo, ujenzi wa nyumba za makazi na uchomaji misitu hivyo kusababisha uchafuzi wa mazingira na hatimaye vyanzo hivyo hukauka.

Kufuatia hali hiyo Waziri Mkuu amewaagiza wakuu wote wa wilaya na wenyeviti wa vijiji nchini kuyasimamia maeneo yenye vyanzo vya maji na kuwaondoa watu wotewalioyavamia kwa kuwachukulia hatua kali za kisheria pamoja na kuwafikisha mahakamani.

Naye Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Isack Kamwelwe ambaye alimuwakilisha Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Gerson Lwenge katika hafla hiyo alisema aliishukuru Serikali ya Ujerumani na Umoja wa nchi za Ulaya kwa kufadhili mradi huo.

Hata hivyo Mhandisi Kamwelwe alisema suala la kuhifadhi mazingira ni msingi endelevu wa upatikanaji wa maji safi na salama, hivyo aliwaomba wananchi kujiepusha na uchafuzi wa vyanzo vya maji na uharibifu wa mazingira ili kuepuka athari ya Taifa kukubwa na janga la ukame.

“Wananchi wanatakiwa kuacha kufanya shughuli za maendeleo ikiwemo kulima, kufuga ndani ya mita 60 kutoka katika mito, maziwa na vyanzo vingine vya maji ili kuepusha uharibifu wa mazingira ambao madhara yake ni makubwa kwa viumbe wote,” alisema.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
ALHAMIS, AGOSTI 25, 2016.

Waziri Mkuu Awataka Wakurugenzi Wasiowaondoe Walimu Wakuu Wasio na Shahada au Diploma badala yake wawahamasishe kwenda kusoma.

$
0
0

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka Wakurugenzi wa halmashauri na Maofisa Elimu nchini kutowaondoa katika nyadhifa zao Waratibu wa Elimu Kata na Wakuu wa shule za sekondari wasiokuwa na shahada, walimu wakuu wa shule za msingi wasiokuwa na diploma badala yake wawahamasishe kwenda kusoma.

“Maofisa Elimu na Wakurugenzi msije mkawaondoa wale walimu wakuu kwa zile sifa nilizosema bado muda ukifika tutatangaza.Msije mkawakurupusha sasa hivi waacheni waendelee na kazi zao tutatoa muda ili wajipange viziri,” aliema.

 Agosti 20 mwaka huu Waziri Mkuu alisema Waratibu wa Elimu katika ngazi ya Kata na Wakuu wa shule za sekondari wanatakiwa kuwa na shahada huku walimu wakuu kwenye shule wanatakiwa kuwa na diploma.

Waziri Mkuu ametoa agizo hilo jana jioni (Jumatano, Agosti 24, 2016) wakati akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye kiwanja cha Mandela katika jimbo la Sumbawanga mjini.

Alisema Mratibu wa Elimu katika ngazi ya Kata ni lazima awe na shahada ili aweze kutekeleza majukumu yake ya kusimamia utolewaji wa elimu katika shule za sekondari na msingi.

“Wakuu wa shule za sekondari na waratibu wa elimu kata wasiokuwa na shahada wasiondolewe katika nafasi zao kabla ya kupewa nafasi ya kwenda kujiendeleza kwa masomo ili waweze kuwa na vigezo vya kuendelea kushika nyadhifa hizo,” alisema.

Alisema katika kuboresha maslahi ya walimu Serikali imetenga zaidi ya sh. bilioni tano kwa mwezi ambazo ni posho ya madaraka. Waratibu Elimu Kata wanapewa sh 250,000 kwa mwezi huku Wakuu wa shule za sekondari na walimu wakuu katika shule za msingi wanapewa sh. 200,000.

Waziri Mkuu alisema badala ya kuwaondoa kwenye nyadhifa hizo ni vema Wakurugenzi wakawahamasisha walimu hao kwenda kusoma ili na wao wanufaike na posho ya madaraka iliyoanza kutolewa na Serikali hivi karibuni.

Katika hatua nyingine Waziri Mkuu amewataka wazazi na walezi kwenda kuwaandisha watoto wenye umri wa miaka mitano katika shule za awali ambapo watapata fursa ya kujengewa msingi mzuri wa masomo kabla ya kuanza darasa la kwanza.

Pia aliagiza shule zote za msingi nchini zisizokuwa na madarasa ya awali kuhakikisha wanaanzisha madarasa hayo haraka na kuanza kutoa elimu hiyo.
 
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
ALHAMIS, AGOSTI 25, 2016.

Zitto Kabwe afunguka yake kuhusu Oparesheni UKUTA

$
0
0

Wakati viongozi wa dini wakiendelea na jitihanda za kusaka suluhu kati ya upande wa Serikali na Chadema kuhusu namna ya kuzuia kwa amani kufanyika kwa Operesheni ya chama hicho iliyopewa jina la UKUTA, Septemba 1, Kiongozi Mkuu wa Chama Cha ACT-Wazalendo Zitto Kabwe ametoa maoni yake.

Zitto ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Mjini amesema kuwa haoni haja ya kufanyika kwa vikao hivyo vya kusaka maridhiano kwani Chadema wanachotaka kufanya kiko kikatiba.

“Sioni ni kwanini tunahangaika na vikao vya maridhiano na tahariri nyingi kuhusu shughuli ya CHADEMA kufanya operesheni yao ya UKUTA. Kuandamana ni Haki ya KIKATIBA. Tuache watu watimize Haki yao Kwa amani. Kuzuia watu kufanya jambo lao la kikatiba ndio kuvunja amani. Wanaotaka kuandamana waandamane na wanaotaka kufanya Kazi zao nyingine tuendelee na Kazi zetu. Kwanini kutekeleza Haki ya kikatiba iwe ni kuvunja amani? Kwanini?,” Zitto ameandika kwenye ukurasa wake wa Facebook.

Hata hivyo, vikao vya maridhiano vinavyoendelea tayari vimeonesha kuzaa matunda kwenye suala la mgogoro wa Bunge ambapo wabunge wa vyama vya upinzani wameridhia kurejea Bungeni katika vikao vitakavyoanza mapema mwezi ujao.

Serikali imeendelea kuwaonya watu wote wanaopanga kuandamana Septemba 1 huku viongozi wa Chadema wakisisitiza kuwa siku hiyo watafanya maandamano kama walivyopanga.

Hali hiyo imepelekea kumtoa hadharani Kingunge Ngombale Mwiru ambaye ameomba marais wastaafu kumshauri Rais Magufuli ili kuruhusu Serikali kukaa na Chadema kusaka muafaka wa masuala ya kisiasa nchini.

Wanafunzi Wa Ualimu Waliokosa Chuo Cha UDOM Wapangiwa Vyuo Vya Ualimu Vya Serikali.

$
0
0
Na: Lilian Lundo - MAELEZO
SERIKALI kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imewapangia vyuo wanafunzi   wa programu maalum ya ualimu chuo kikuu cha Dodoma (UDOM) ambao hawakupata nafasi ya vyuo katika awamu ya kwanza, walioagizwa kuomba mafunzo kulingana na sifa zao kupitia Baraza la Taifa la Mafunzo ya Ufundi (NACTE).

Hayo yamesemwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Leonard Akwilapo leo, jijini Dar es Salaam alipokuwa akitoa taarifa kuhusu wanafunzi wanaosoma stashahada maalum ya ualimu wa sayansi chuo kikuu cha Dodoma.

“Mtakumbuka tuliagiza kwamba wanafunzi ambao walikosa sifa za kujiunga na ualimu wa sayansi waliombwa kuomba mafunzo yanayolingana na ufaulu wao kupitia NACTE,  Lakini baada ya taarifa hiyo tulipokea maombi mengi kutoka kwa vijana hawa wakiomba kupangiwa vyuo moja kwa moja na Wizara, wizara imetafakari na kuamua nao wapangiwe vyuo vya Serikali,” alifafanua Dkt. Akwilapo.

Aliendelea kusema kuwa, wanafunzi ambao waliachwa awamu ya kwanza na kupangiwa katika awamu ya pili ni wanafunzi 290 ambao walikuwa wakisomea programu ya stashahada ya ualimu wa sekondari na wanafunzi 1,181 ambao walikuwa wakisomea stashahada ya ualimu wa msingi.

Dkt. Akwilapo amesema kuwa Wizara imeamua kuwapangia wanafunzi hao vyuo kutokana na kuonyesha nia ya dhati ya kusomea ualimu ambapo wanafunzi hao wamepangiwa vyuo vya ualimu vya Marangu na Tabora.

Aidha, Dkt. Akwilapo ameeleza kuwa wanafunzi hao watajigharamia masomo yao kulingana na viwango vya ada vilivyowekwa na Serikali. Pia amewataka kutembelea tovuti ya wizara ya hiyo ambayo ni www.moe.go.tz ili kuona vyuo walivyopangiwa.

Mnamo tarehe Mei 28, 2016 Serikali iliwarejesha nyumbani wanafunzi 7,805 waliokuwa wanasoma Stashahada Maalum ya Ualimu wa Sayansi na Hisabati katika Chuo Kikuu cha Dodoma. Katika mchujo wa awamu ya kwanza wanafunzi 382 ndio waliokuwa na sifa ya kuendelea na masomo chuo kikuu cha UDOM na wengine 4,586 walipangiwa vyuo vya ualimu vya Serikali.

Mitihani ya Taifa Darasa la 4 na Kidato cha 2 kufanyika kama kawaida.

$
0
0
Na: Lilian Lundo
Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia inaukumbusha Umma kuwa mitihani ya Taifa ya Darasa la 4 na Kidato cha 2 itaendelea kuwepo na mwaka huu itafanyika kama kawaida.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Leonard Akwilapo ameyasema hayo leo, jijini Dar es Salaam alipokuwa akikanusha taarifa za kutokuwepo kwa mitihani hiyo kwa mwaka 2016.

“Napenda niukumbushe Umma kuwa mitihani hii ni muhimu sana katika ufuatiliji wa maendeleo ya wanafunzi wetu. Kwa hiyo mitihani yote miwili itaendelea kuwepo na mwaka huu itafanyika kama kawaida. Kama kuna watu wanawaambia kuwa haitafanyika wawapuuze kabisa,” alifafanua Dkt. Akwilapo.
 
Dkt. Akwilapo aliendelea kwa kusema kuwa, mitihani hiyo ina umuhimu mkubwa katika kupima maendeleo ya mwanafunzi kwa lengo la kufanya maendeleo ya kitaaluma. Aidha kwa wanafunzi ambao watakuwa hawajafikia viwango vya ufaulu vilivyowekwa watatakiwa kukariri darasa au kidato.

Amebainisha kuwa Baraza la Mitihani ndilo lenye jukumu la kushughulikia maandalizi ya mitihani hiyo ikiwa ni pamoja na utungaji, uchapaji, ufungaji na usafirishaji hadi ngazi ya Mkoa na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) ikiwa na majukumu ya kuhakikisha kuwa uendeshaji na usahihishaji wa mitihani hiyo unafanyika kikamilifu.

Mwakyembe Asema Jeshi la Polisi Liko Sahihi Kuzuia Mikutano ya Ndani ya Vyama Vya Siasa........Awataka Watanzania Wasishiriki Maandamano ya UKUTA

$
0
0

Waziri wa Mambo ya  Katiba na Sheria Mhe. Dkt Harrison Mwakyembe  amesema amri ya Jeshi la Polisi ya kuzuia mikutano ya nje na ndani ya vyama vya siasa ni halali ambayo kila Mtanzania na mwanachama wa chama chochote cha siasa anapaswa kuitii na kuizingatia na kwamba kutokufanya hivyo ni kuvunja sheria za nchi.

Amesema amri hiyo ni ya kudumu ambayo imelenga kuangalia na kufanya tathmini ya hali ya nchi kutokana na viashiria mbalimbali vya uvunjifu wa amani nchini ambavyo vimeanza kuonekana.

Dkt Mwakyembe alikuwa akijibu swali kutoka kwa Kituo cha Televisheni cha Taifa TBC 1 ambacho kilitaka kupata ufafanuzi  kuhusiana na uhalali wa kauli ya Jeshi la Polisi ya kuzuia mikutano ya ndani na ya hadhara kwa vyama vya siasa nchini.

“Jeshi  la Polisi ni chombo halali cha cha dola kilichoanzishwa kisheria chenye wajibu wa kulinda usalama wa raia na mali zake ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na kuongeza kuwa  uamuzi huo una lengo la kulinda amani ya nchi na endapo kutakuwa na viashiria vya kutishia amani ya nchi yetu lazima hatua za kisheria na kinidhamu zichukuliwe. Ni amri halali na kila Mtanzania na mwanachama wa chama chochote nchini anapaswa kuitii na kuizingatia na kwamba kwenda kinyume ni  kukiuka sheria, ” alisisitiza Mhe. Mwakyembe.

Mhe. Waziri amesema ni haki ya vyama vya siasa kufanya mikutano ila wanatakiwa kutoa taarifa Polisi ili waweze kutoa ulinzi wakati wa mkutano huo na kuongeza kuwa Jeshi la Polisi linaweza kuzuia mikutano hiyo kwa sababu za kiusalama.

Mhe. Waziri pia alisema sio kweli kuwa Mhe. Rais amezuia mikutano ya siasa, bali alichofanya ni kudhibiti uendeshaji wa holela au huria wa shughuli za siasa nje ya maeneo ya uchaguzi ya wanasiasa na kuongeza kuwa Mhe. Rais amefanya hivyo kutokana na kiapo chake cha kuilinda, kuihifadhi  na kuitetea Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Taifa kwa ujumla.

“Mhe. Rais hajapiga marufuku siasa, alichofanya ni kudhibiti uendeshaji holela au huria wa shughuli za siasa nje ya maeneo ya uchaguzi ya wanasiasa husika kuepusha shari na chuki na amefanya hivyo kutokana na kiapo chake cha kuilinda, kuihifadhi na kuitetea Katiba ya Tanzania na taifa kwa ujumla wake. Kwa hatua hiyo Mhe. Rais hajafunga milango ya majadiliano. Milango iko wazi na tulitegemea wenzetu wangekuja na njia mbadala na kulizungumzia hilo badala ya kuitisha maandamano ya nchi nzima," alisema.

Mhe Mhe. Waziri amevitaka vyama vya upinzani nchini kukaa na kuzungumza na Serikali na kuacha kufanya vitendo vya kutishia uvunjifu wa amani kama kuitisha maandamano kwa nchi nzima.

 “Njooni tukae tuzungumze tupime ushauri wenu, hili ni taifa letu sote na milango iko wazi, tuache kuchochea vitendo vya uvunjifu wa amani kama ambavyo inavyoonekana nchini hivi sasa,” alisisitiza.

Amasema Sheria ya Vyama vya siasa hairuhusu kufanyika kwa maandamano kwa nchi nzima, kufanya hivyo ni kuchochea wananchi kuasi “civil disobedience” ni kinyume cha sheria na serikali haiwezi kuivumilia hali hiyo. 

 Mhe. Waziri ametoa wito kwa Watanzania wote kutoshiriki maandamano ya Ukuta ambayo alisema hayatakuwa na tija kwa nchi bali kuleta vurugu katika jamii.

Miili Ya Askari Waliouawa Na Majambazi Yaagwa Leo Kupelekwa Mikoani Kwa Mazishi.

$
0
0
Waziri wa Wizara ya  Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba, akizungumza wakati wa  kuaga miili ya askari waliouawa katika eneo la Mbande, Temeke baada ya kuvamiwa na majambazi .Ibada hiyo ya kuaga  ilifanyika katika Viwanja vya  Polisi  vilivyopo  barabara ya Kilwa,jijini Dar es Salaam.

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Ernest Mangu, akizungumza wakati wa maombolezo na kuaga miili ya askari waliouawa katika eneo la Mbande, Temeke baada ya kuvamiwa na majambazi.Ibada hiyo ya kuaga  ilifanyika katika Viwanja vya  polisi vilivyopo barabara ya Kilwa,jijini Dar es Salaam.
Waziri wa  Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba, akipita kutoa heshima za mwisho mbele ya majeneza yaliyobeba  miili ya askari waliouawa baada ya kuvamiwa na majambazi    katika eneo la Mbande, Temeke ,bada hiyo ya kuaga miili ilifanyika katika viwanja vya polisi  vilivyopo barabara ya Kilwa,jijini Dar es Salaam.
Waziri wa  Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba, akitoa mkono wa pole kwa mmoja wa ndugu wa  askari waliouawa baada ya kuvamiwa na majambazi  katika eneo la Mbande, Temeke ibada hiyo ya kuaga miili  ilifanyika katika viwanja vya  polisi vilivyopo barabara ya Kilwa,jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa   Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni , akitoa mkono wa pole kwa mmoja wa ndugu wa  askari waliouawa baada ya kuvamiwa na majambazi  katika eneo la Mbande, Temeke ,ibada hiyo ya kuaga miili  ilifanyika katika Viwanja vya Kambi Kuu ya Polisi iliyopo barabara ya Kilwa,jijini Dar es Salaam.
Askari wakimsaidia mzazi wa mmoja wa askari waliouawa baada ya kuvamiwa na majambazi  katika eneo la Mbande, Temeke, ibada hiyo ya kuaga miili  ilifanyika katika viwanja vya  polisi vilivyopo barabara ya Kilwa,jijini Dar es Salaam.(Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)

UKAWA Wakubali Kurudi Bungeni....Wamshauri Rais Magufuli Avifute Vyama Vyote Vya Upinzani ili Aongoze Nchi Bila Kukosolewa

$
0
0
Viongozi wa vyama vya upinzani nchini vimemshauri Rais John Pombe Magufuli kuvifuta vyama vya upinzani kama anaona vinamsumbua anapofanya mambo yake.

Hayo yamesemwa leo na mwenyekiti mwenza wa UKAWA, James Mbatia ambapo amesema kuwa kama Rais Magufuli anaona vyama vya upinzania vinamkera na kumkwamisha anapotaka kufanya jambo basi serikali yake ipelekea mswada kwa hati ya dharura bungeni ili kufanya mabadiliko katika sheria ya vyama vya siasa na kuvifuta vyote.

Mbatia amesema kuwa jambo hilo amelitafakari na kuwashirikisha viongozi wenzake na huenda ikasaidia kwa sababu Rais Magufuli anaonekana kutaka kuongoza kwa kutumia akili yake na hataki kukosolewa na mtu yeyote wala chama chochote.

Katika hatua nyingine, viongozi wa vyama vya upinzani wameitikia wito wa viongozi wa dini uliowataka kurudi bungeni na wameahidi kuwa watajadiliana na wanaamini watafikia muafaka na kurudi bungeni katika mkutano ujao mwezi wa tisa.

Tazama video hapo chini


Hapa wanamshauri Rais avifute vyama vya upinzani

CHADEMA Wapinga Kauli ya Jeshi la Polisi Kuzuia Mikutano ya Ndani ya Vyama vya Siasa

$
0
0
Wakati Jeshi la Polisi likisisitiza kupiga marufuku mikutano na maandamano ya Chadema chini ya mwavuli wa Umoja wa Kupinga Udikteta nchini (Ukuta), chama hicho kimepinga katazo hilo nakudai kuwa liko kinyume na Katiba ya nchi.

Kauli hiyo imetolewa leo na Tundu Lissu, Mwanasheria Mkuu wa Chadema katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika kwenye Makao Makuu ya chama hicho Mtaa wa Ufipa, jijini Dar es Salaam.

Kwenye mkutano huo akiwa na Lawrance Masha, aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani (2005-2010) Lissu amesema, rais anayo nafasi ya kuzuia mikutano ya hadhara kwa sharti la kupeleka hoja bungeni na kisha kujadiliwa na si vinginevyo.

“Ipo sheria ya kutangaza hali ya dharura, iliyotungwa mwaka 1995, hii inamruhusu rais kupeleka hoja bungeni ya kutaka kutangaza hali ya dharura kwa kipindi kisichozidi miezi mitatu na kama Bunge likiridhia, basi rais anatangaza, namshauri Magufuli afanye hivyo.

“Aitangazie Tanzania na dunia kwa ujumla kuwa, nchi hii ipo katika hali ya hatari na katika hali ya dharura, na kwamba mikutano yote itakuwa marufuku.

“Na miezi mitatu ikiisha aende tena bungeni kuomba aongeze mingine. Akifanya hivyo atakuwa hajavunja sheria na hata sisi tutamtii,” amesema Lissu.

Lissu ambaye pia ni Mbunge wa Singida Mashariki amelitaka Jeshi la Polisi kuacha kutoa matamko yanayoiingiza nchi katika utawala wa kidikteta.

Kauli hiyo inakuja ikiwa ni siku moja tu, tangu jeshi hilo kupitia Nsato Marijani, Kamishina wa Polisi, Operesheni na Mafunzo, litangaze kupiga marufuku mikutano yote ya vyama vya siasa nchini, ikiwemo vikao vya ndani vya vyama.

Katika mkutano na wanahabari, makao makuu ya chama hicho, akiwa ameambatana na Dk. Vincent Mashinji, Katibu Mkuu wa chama hicho, Profesa Mwesiga Baregu, Mjumbe wa Kamati Kuu, pamoja na Masha amesema, Lissu amesema, kamwe Chadema hakiwezi kuruhusu ukiukwaji wa katiba na sheria za nchi.

“Amri ya jana ya polisi, wakipiga marufuku mikutano yote ya vyama vya siasa ikiwemo vikao vya ndani ni muendelezo wa amri haramu na kitendo hicho cha jana na vingine vilivyopita, ni mfano hai ya kwamba, nchi yetu imeingia katika mfumo wa udikteta.

"Kwani, kwa mujibu wa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere mwaka 1967; udikteta ni utawala wa mtu mmoja au kikundi cha watu wachache wanaofikiria kwamba, amri zao ndiyo sheria na wote wanaowapinga, hukiona cha mtema kuni,” amesema Lissu.

Lissu amesema kuwa, kwa mujibu wa Katiba ya sasa pamoja na sheria zote ikiwemo Sheria Na. 5 ya mwaka 1992 ya vyama vya siasa, Sheria ya Maadili ya Vyama vya Siasa ya mwaka 2007 pia sheria za Jeshi la Polisi, hakuna mahali ambapo polisi au rais anaruhusiwa kupiga marufuku mikutano ya kisiasa.

“Anayetakiwa kujulishwa kuhusu uwepo wa maandamano na mikutano ya hadhara ni Mkuu wa Polisi Wilaya (OCD) na kama kuna tatizo kwa muda huo, anaweza kuelekeza isifanyike kwa muda fulani lakini siyo Rais Magufuli wala Nsato,” amesema.

Wakati Lissu akisema hayo, Masha amesema,“nimekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani kwa miaka mitano, lakini sikuwahi kupiga marufuku mikutano ya hadhara wala ile ya ndani. Nilifahamu kuwa, kuna umuhimu wa watu kuzungumza, kukosoana na kuelimishana.

"Ni vyema Rais Magufuli akajua, hii ni nchi ya kidemokrasia na kuna Katiba na sheria ambazo kila mtu ni lazima afuate akiwemo yeye, matamko ya kibabe ya Rais, Waziri wa Mambo ya Ndani na Jeshi la polisi ni kinyume na sheria pamoja na Katiba yetu.”

Dk. Mashinji, amesisitiza kuwa, Chadema kipo tayari kwa mazungumzo na mamlaka yoyote ya serikali juu ya azma ya kufanya mikutano na maandamano, ili mradi tu sheria na katiba ya nchi izingatiwe katika mazungumzo hayo.

“Hatujafunga milango ya mazungumzo na serikali, tunachosisitiza sisi ni kuwa hata kama kuna mazungumzo yatafanyika, Katiba na sheria za nchi yetu lazima zizingatiwe,” amesema Dk. Mashinji.

Umoja wa Wanawake Wapinga Maandamano UKUTA Ya Chadema

$
0
0
Umoja wa Wanawake Viongozi wa Vyama vya Siasa Tanzania (UWASATA), umepinga maandamano yasiyo na ukomo yaliyotanganzwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kwa kuwa hayana tija kwa wananchi na Tifa kwa ujumla.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa umoja huo Cecilia Augustino, alisema maandamano hayo yanaashiria uvunjifu wa amani ambayo ni urithi wa Taifa la Tanzania.

Alisema wamefikisha tamko lao kwa Msajili wa Vyama vya Siasa Jaji Francis Mutungi na kumtaka msajili kutoacha chokochocko hizo ziendelee kwani zitasababisha kutoweka kwa amani nchini.

“Sisi wanawake viongozi wa vyama vya Siasa Tanzania tunapinga azimio la maandamano yasiyo na kikomo yanayoandaliwa na chama cha Chadema, hakika maandamano hayo hayana tija kwa wananchi na Taifa kwa ujumla” alisema Hokororo na kuongeza:

“Mheshimiwa Msajili, chokochocko hizi zinazofanywa na baadhi ya viongozi wa kisiasa zikiachwa tu bila ya kukemewa tunaamini tunu yetu ya amani ambayo ni urithi wetu tulioachiwa na waasisi wetu itatoweka”

Aliongeza kuwa hatma ya maandamano hayo ni kuingia kwenye machafuko na hatimaye mauaji na mateso kwa wanawake, watoto na walemavu, mambo ambayo hawatakubali yatokee.

Alibainisha kuwa wanawake viongozi wa vyama vya siasa wanaamini kuwa siasa ni kushindana kwa hoja na si uvunjifu wa sheria kwa njia ya maandamano yasiyo na tija kwa wananchi na Taifa.

Aliliomba Baraza la Vyama vya Siasa kuhakikisha linawajibika katika kulinda demokrasia, amani na ustawi wa jamii nzima ya Watanzania.

Katika hatua nyingine, umoja huo unaojumuisha wanawake viongozi wa vyama 22 vya siasa nchini, umeomba kufanya kongamano la amani lenye lengo la kuhamasisha amani na utulivu nchini.

Hivyo, Hokororo aliwaomba viongozi wakuu wa nchi kuanzia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Makamu wa Rais, Waziri Mkuu, wadau wa amani na mashirika binafsi kushirikiana na umoja huo kufanikisha kongamano hilo.

“Hakika tunaumia wanasiasa wanapokuwa chanzo cha migogoro na vurugu kwa Taifa letu.Hivyo tunamuomba Rais wetu tunajua ni msikivu  aweze kuona namna nzuri ya kutafuta suluhu ya mgogoro huu wa kisiasa” alisema Mwenyekiti Cecilia Hokororo.

Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi, tayari ameitisha Baraza la Vyama vya Siasa Agost 30, mwaka huu ili kutoa fursa kwa pande vyama husika kukaa meza moja na kujadili tofauti zilizopo na kuzipatia ufumbuzi.

Naye Makamu Mwenyekiti wa umoja huo Ziada Athumani alisema wanaunga mkono hatua hiyo kwani ndio njia muwafaka ya pande husika ili kufikia muwafaka kwa njia ya amani.

Katika mkutano huo na waandishi wa habari, wanawake viongozi wa vyama vya siasa waliwakilishwa na wenzao kutoka vyama vya Demokrasi Makini, ADA TADEA na Chama cha Umoja wa Demokrasi ya Vyama Vingi (UMD).

Wasanii Wapenda Amani Waungana Kupinga Maandamano UKUTA Ya Chadema

$
0
0
WASANII mbalimbali wanaopenda amani wameungana kwa pamoja kupinga maandamano ya UKUTA yanayotarajiwa kufanyika Septemba Mosi, mwaka huu.
 
Akizungumza jana mbele ya Waandishi wa Habari, Mwenyekiti wa Wasanii hao wapenda amani, Steve Nyerere alisema hamna haja ya maandamano bali tunahaja ya kufanya kazi hususan kwa vijana.
 
"Vijana ndio muhimili mkubwa kulinda amani ya nchi,tusiwaze maandamano bali tuwaze je Akinamama na Watoto wanapata huduma hospitali"alihoji Steve Nyerere.
 
Kwa Upande wa Makamu Mwenyekiti wa Wasanii hao, Asha Baraka alisema wameamua kupaza sauti zao kwa niaba ya Wasanii wote wanaopenda amani.
 
Alisema Tanzania ni nchi ya Amani sio nchi ya vita hivyo wanapofanya shughuli za UKUTA shughuli zote za kijamii zitasimama.
 
Hatahivyo aliomba Septemba 1,  UKUTA wasimamishe maandamano hayo, pia watafute njia muafaka ya kuweza kuongea Vyama kwa Vyama na wakapata muafaka ili nchi iweze kwenda mbele.

Rais Magufuli atoa milioni 10 za rambirambi kwa familia za polisi waliouawa

$
0
0
RAIS John Magufuli ametoa ubani wa Sh milioni 10 kwa familia za askari wanne waliouawa katika shambulio la ujambazi Mbande wilayani Temeke mkoani Dar es Salaaam, huku akiwataka askari kutokuvunjika moyo katika utendaji wao wa kazi kutokana na mauaji ya wenzao, bali walitumie kama kigezo cha kufanya kazi kwa bidii.

Aidha, Rais Magufuli amemtumia salamu za rambirambi Mkuu wa Jeshi la Polisi, Inspekta Jenerali Ernest Mangu na wanafamilia wa askari wote waliopoteza maisha.

Askari watatu kati ya wanne waliofariki katika shambulio hilo la Jumanne usiku katika eneo la benki ya CRDB Mbande, Dar es Salaam ambalo watu wenye silaha waliwavamia wakiwa kazini na kuwaua na kupora bunduki mbili aina ya SMG na risasi 60, waliagwa jana katika Viwanja vya Polisi Barabara ya Kilwa.

Akizungumza wakati wa kuaga miili hiyo katika shughuli iliyoongozwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba, IGP Mangu alisema baada ya tukio hilo kutokea, aliwasiliana na Rais Magufuli ambaye alionesha kusikitishwa sana na tukio hilo na kumpa pole yeye, askari pamoja na familia za marehemu.

Miili ya askari walioagwa jana ni Koplo Yahaya Malima aliyesafirishwa kwenda kuzikwa kijiji cha Kibuta, wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani, Tito Mapunda aliyesafirishwa kwenda kijiji cha Migoli, wilaya ya Iringa Vijijini mkoani Iringa na Gaston Lupanga aliyesafirishwa kwenda mjini Songea mkoani Ruvuma kwa maziko.

Askari mwingine Koplo Khatib Ame Pandu alisafirishwa Jumatano jioni kwenda kwao Zanzibar ambako maziko yalifanyika siku hiyo hiyo usiku.

Viongozi mbalimbali wa serikali walipata fursa ya kutoa salamu za rambirambi katika msiba huo, na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda aliamuru wale wote waliofanya uhalifu huo pamoja na wale wanaofanya vitendo vya uhalifu jijini Dar es Salaam kushughulikiwa ipasavyo.

“Katika hili ninaomba wale wa haki za binadamu wanisamehe, kitendo hiki si cha kuvumilika hata kidogo kwa kuona wale ambao wamekula kiapo kutulinda sisi, leo sisi tunakwenda kuwaua wao halafu tunyamaze, mimi nasema hapa hadharani …Afande Sirro twanga tu yeyote mtakayekutana naye msituni,”alisema Makonda.

Makonda alisema kazi ya amani ya vyombo vya ulinzi ni kubwa hivyo ipo haja ya kuangaliwa upya kwa taratibu na sheria kuona ni namna gani askari kama hao wanaopoteza maisha wakiwa bado vijana wadogo kuwajengea hata nyumba ili kuwapa faraja wale wanaowaacha nyuma yao.

Naye Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishna wa Polisi Simon Sirro alisema kitendo walichofanya wahalifu hao kuua askari ni sawa na kuwasha moto hivyo na wao watajibu mapigo na kuhakikisha wahalifu hao wanapatikana.

“Wameuwasha moto na sisi tutauwasha moto kwelikweli na katika hili tutaomba watu wa Tume za Haki za Binadamu kutosimama upande wowote,” alisema Sirro.

Aidha, Waziri Mwigulu aliagiza Jeshi la Polisi kuendelea bila kukoma kuwasaka majambazi na wahalifu wote na kuhakikisha wanakamata waliofanya tukio hilo.

Mwigulu pia ameagiza viongozi wa Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na wizara yake kuangalia upya sheria na kuona namna bora ya kuwasaidia askari kuwa na bima za maisha, huku akiwataka kuhakikisha wanaharakisha mafao kwa familia za marehemu yanaandaliwa mapema.

“Mara nyingi kumekuwa na tabia ya usumbufu kwa ndugu na jamaa za wafiwa kusumbuliwa na maandalizi ya mirathi kuchukua muda mrefu na wakati mwingine tukio kama hili tumeshuhudia wote lilivyotokea na askari wetu kufa wakiwa kazini lakini bado itaundwa tume kuchunguza ili mafao yalipwe kwa wafiwa,”alisema Mwigulu.

Naye Mwanasheria Mkuu wa Serikali, George Masaju alisema kitendo cha kushambulia askari na kuwaua ni kuichokoza mamlaka ya nchi na kulaani wote walioshabikia mauaji hayo kwa namna yeyote ile.

“Kitendo hiki si cha kushabikia na tuache kabisa kushabikia vitendo vya uvunjifu wa sheria, lakini pia tutambue kuwa sheria au Katiba ya Nchi haina mjadala,” alieleza Masaju.

Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB), Bahame Nyanduga alilaani na kupinga mauaji ya kikatili na kusema kuwa ni kinyume cha haki za binadamu na haki ya kuishi ya kila mtu ipo ndani ya Katiba.

Mbali na Mwigulu, viongozi wengine wa serikali waliotoa heshima za mwisho kwa miili ya marehemu ni Waziri wa Katiba na Sheria, Dk Harison Mwakyembe, Masaju, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Yussuf Masauni na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira.

Pia IGP Mangu, Makonda, Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Felix Lyaniva, Meya wa Manispaa ya Temeke, Abdallah Chaurembo, Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) Biswalo Mganga, Mkuu wa Makosa ya Jinai, DCI, Diwani Athuman pamoja na makamishna mbalimbali wa Polisi, mahakimu na wanasheria.

Katika hatua nyingine, mmoja wa majeruhi katika tukio hilo, Said Ally (36) aliyelazwa katika Hospitali ya Temeke, amefanyiwa upasuaji na kutolewa risasi aliyopigwa.

Ally ambaye ni mfanyabiashara katika eneo la Mbande Magengeni karibu na benki ya CRDB ambako tukio hilo lilitokea, alijeruhiwa kwa risasi hiyo wakati alipotoka nje ya duka lake kuangalia kuna nini baada ya kusikia milio ya risasi.

Akizungumzia hali ya Ally, Ofisa Habari wa Manispaa ya Temeke, Joyce Msumba alisema kwa mujibu wa taarifa alizopewa na madaktari ni kwamba majeruhi huyo alifanyiwa upasuaji huo jana. 

“Taarifa nilizopewa ni kwamba amefanyiwa upasuaji leo (jana) na ametolewa risasi ambayo ilikuwa mguuni kwake pamoja na ganda la risasi, lakini anaendelea vizuri,” alisema Msumba.

Majeruhi mwingine ni Azizi Ally aliyekuwa akiuza chipsi katika mgahawa jirani na benki hiyo, alijeruhiwa na risasi mkono wake wa kushoto wakati akikimbia kuokoa uhai wake. 

Azizi ambaye alishonwa nyuzi sita katika mkono huo, alisema anaendelea vizuri kwa kuwa alipata matibabu muda mfupi baada ya tukio hilo na aliruhusiwa kurejea nyumbani.

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Ijumaa ya Agosti 26

RC Makonda: Polisi Mkikuta Mtu Yeyote Msituni Pigeni bila Huruma.......Haki za binadamu Wakiwauliza Waambieni waje Kwangu

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ameliagiza Jeshi la Polisi kuwagonga na kuwapiga wahalifu wowote wakiwamo majambazi pindi wanapowakamata. 

Akizungumza wakati wa kuaga miili ya askari watatu kati ya wanne wa Jeshi la Polisi waliouawa wiki hii katika tawi la benki ya CRDB lililopo Mbande wilayani Temeke jijini Dar es Salaam, Makonda alisema jambazi atakapokutwa popote iwe msituni iwe wapi agongwe na apigwe. 

Alisema alipopata taarifa ya vifo vya askari hao wanne alifungua pazia za madirisha nyumbani kwake na kuwaangalia askari wanaolinda na kulia kwa uchungu na kwamba usiendelezwe ukichaa wa haki za binadamu kwani ni uendawazimu ambao hauwezi kuvumilika. 

“Kamanda Sirro (Simon) mimi ndiyo mkuu wako wa mkoa nasema ukikamata hao watu popote gonga, piga na watu wa haki za binadamu wakija waambie waje kwangu, hatuwezi kukaa kwenye mkoa ambao haupo salama,” alisema Makonda aliyedai hana maneno mazuri ya kusema kwa sababu hakuumbwa kumfurahisha mtu, bali anafanya kazi ya Mungu na wakati wake ukiisha ataondoka.

 “Kama kuna haki za binadamu nataka haki za askari wangu kwanza. Kama hao watu wa haki za binadamu wapo nataka kuona wakiandamana kukilaani kitendo hiki, ”alisema Makonda. 

Msikilize hapo chini akiongea

Polisi Yapambana na majambazi Mkuranga.....Difenda zaidi ya 16 Zipo Eneo la tukio Asubuhi hii

$
0
0

Mapigano makali yanaendelea kati ya polisi na watu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi eneo la Vikindu, wilaya ya Mkuranga, mkoa wa Pwani asubuhi hii.
 
Magari ya polisi (defenda) zaidi ya 16 yamefika eneo la tukio huku polisi wakiwa wameshika silaha zao kwa umakini mkubwa.
 
Kadhalika, magari yanayokwenda maeneo ya Vianzi Mkurang, Malela, Pemba Mnazi, Mfuru yamefungwa kutokana na mapambano hayo.

RIWAYA: Sorry Madam - Sehemu ya 29 & 30 (Riwaya inawafaa kuanzia miaka 18 na kuendelea )

$
0
0
Mtunzi : Eddazaria g.Msulwa
Ilipoishia...
Kwa nguvu zungu zote nikarusha teke lililo mpiga kwenye miguu yake kwa nyuma na kumfanya aanguke kama mzigo wa kuni na akaangukia pua kitendo kiliho shuhudiwa na watu wengi ikiwemo askari walio anza kukimbia wakija kwenye eneo tulilopo huku bunduki zao zikiwa mikononi mwao huku wakinimrisha nisifanye kitu cha iana yoyote na john akabaki akiwa haamini kitu alicho kiona

Endelea...
Nikamnyanyua mwanasheria wa  serikali  na kumuamrisha kuelekea lilipo gari lake na askari walio kuwa wakinifwata wakajikuta wakisimama huku wakionekana kunishangaa.Ila mmoja wao akanifwata akiwa na bunduki yake na kumbukumbu zikanikumbusha kuwa ni askari wa getini ambaye mara ya mwisho alinisaidia katika kotoroka mikononi mwa baba
“eddy vipi tena?”
“safi”

Nilizungumza huku nikumuongoza mwanasheria hadi kwenye gari lake nikamuomba funguo yake kilazima na akaitoa kabla sijaingia kwenye gari nikastukia nikiguswa bega na nikageuka nikakutana na sura ya askari wa getini
“kaka eddy huyo mkuu ana nini?”

“si unamkumbuka yule binti niliye kuwa naye siku ile tulivyo kuwa tunatoroka home?”
“ndio si amehukumiwa kifuno cha maisha tayari?”
“ndio ila kwa kosa la kuonewa sasa ndio huyu fala ninamuomba anipeleke alipo anakazi ya kunizingua hapa”
“ahaa mimi ninapajua tunaweza kwenda pamoja”

Tukaingia ndani ya gari na kumkabidhi askari wetu wa getini funguo ya gari na safari ikaanza.Kitu ambacho ninakishukuru kutoka kwa askari wetu wa getini ni kuwa mtu muelewa japo ni askari wa jeshi la polisi ila mama alipendekaza kuwa askari wa kuilinda nyumba yetu kutokana na upole na hekima aliyo nayo ni tofauti na maaskari wengine ambao wana dharau kiasi kwamba mtu unashindwa kuwadhamini katika maisha.

“kaka eddy unajua hata mimi niliamini kuwa umefariki dunia?”
“sijakufa ndugu yangu ila wee acha tuu”
“basi unajua habari za kifo chako zilinistua kiasi kwamba nikawa nipo njia panda kwa maana yule binti kwa muonekano anaonekana anakupenda kiasi kwamba hasikii la mtu juu yako sasa sikuelewa nilipo ambiwa kuwa amesababisha kifo chako”

“najua zote ni mbinu za mzee ila zitafikia mwisho”
“jamani ninaomba munisikilize”
Mwanasheria wa serikali alizungumza na kutufanya sote tukae kimya na kumsikila kitu anacho taka kutuambia
“jamani ukweli ni kwamba sheila hajanyongwa japo mahakama ilitoa hukumu ya namna hiyo”
Sote tukajikuta tukiguna kila mmoja kwa mtindo anao ujua yeye mwenyewe kiasi kwamba tukabaki tukimsikilizia kitua atakacho kizungumza.

“ukweli ni kwamba mr godwin alitokea kumpenda yule binti na akahitaji tuweze kumhukumu hivyo ila yeye amepanga safari ya kwenda naye kuishi visiwa vya komoro na hapa ninavyo zungumza amenitumia meseji akidai yupo uwanja wa ndege kwa ajili ya safari ya kuelekea visiwa vya comoro”

Nikajihisi nguvu za mwili zikiniiishia kiasi kwamba nikabaki nikiwa kimya nisijue nini cha kufanya na hasira kali dhidi ya baba yangu ikanipanda na kujikuta nikinyang’ata meno yangu kiasi kwamba sauti ya msuguano wake ikasikika kwa kila mtu.
“muheshimiwa amekuambia kuwa anaondoka na ndege ya saa ngapi?”
“ngoja niwaonyeshe meseji aliyo nitumia”

Mwanasheria akatoa meseji aliyo tumiwa na baba na kuanza kumuonyesha john ambaye nikamshuhudia akishusha pumzi nyingi kiasi kwamba akionekana kuchoka na kile alicho kisoma na kabla hajamuonyesha askari wetu wa getini nikampokonya simu na kuisoma meseji iliyopo kwenye simu yake.

{mr kilongo mimi nipo nipo uwanja wa ndege ninaelekea visiwa vya comoro kula raha na huyu mtoto,jana nimemuonja ni mtamu sana.Ile pesa nimekuingizia kwenye akaunti yako asante kwa kazi nzuri uliyo ifanya na hakikisha unamalizia juhudi za kuzibinafsisha mali za mke wangu nitakupa robo ya utajiri wangu}

Nikabaki nikiwa ninatetemeka kwa hasira kiasi kwamba nikajihisi michuruziko ikinitoka puani kwangu na matone baadhi yakadondoka kwenye mapaja juu ya nguo za wauguzi nilizo zivaa na kugundua kuwa ni damu ndio zimenitoka puani na sikujua zimesababishwa na nini kwani ndio mara yangu ya kwanza kutokwa na damu za puani.John akanipa kiatambaa chake na kujifuta damu zinazo nitoka na askari akasimamisha gari pembeni ya barabara na wakaniomba nishuke nipigwe na upepo wa wa halisi kulilo ic iliyo tawala ndani ya gari.

Nikashuka na kuinama chini na damu zikanitoka kidogo na chakumshukuru mungu zikakata japo kichwa nikaanza kukihisi kikiwa kimetaliwa na maumivu makali
“unajisikiaje?”
“kichwa kidogo kina gonga”
“noja tukakutafutie dawa”
”hapana twendeni air port”
“utaweza kweli eddy?”
“john usijali kwa hilo nitaweza tu”


==>Endelea Nayo <<Kwa Kubofya Hapa>>
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images