Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Serikali Yaamua Kuwarudisha Wanafunzi 382 kati ya 7805 Waliofukuzwa Chuo Kikuu cha Dodoma

$
0
0
May 28 2016 Serikali iliwarejesha nyumbani wanafunzi 7,805 waliokuwa wanasoma Stashahada Maalum ya Ualimu wa Sayansi na Hisabati Chuo Kikuu Dodoma.
 
Wanafunzi waliosimamishwa masomo walikuwa wamegawanyika katika makundi makuu mawili. Kundi la kwanza lilikuwa ni wanafunzi 6,595 waliodahiliwa katika Stashahada Maalumu ya Ualimu wa Elimu ya Sekondari na kundi la pili lilikuwa na wanafunzi 1,210 waliodahiliwa katika mafunzo ya Stashahada ya Ualimu wa Elimu ya Msingi. 
 
Taarifa iliyotolewa leo na waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Joyce Ndalichako amesema kwamba baada ya hatua ya kuwaondoa wanafunzi chuoni kuchukuliwa, Serikali ilifanya  Uchambuzi wa wanafunzi hao kwa lengo la kujiridhisha na sifa zao.  Baada ya uchambuzi huo leo July 19 2016 Serikali imetangaza maamuzi haya…….
 
Kundi la Stashahada Maalumu ya Ualimu wa Elimu ya Sekondari
Serikali imesema kwa kuwa uchambuzi umebainisha kuwa Wanafunzi wenye ufaulu wa Daraja la I na la II ambao pia wamefaulu masomo mawili ya Sayansi kwa kiwango cha C-A ni 382 (mwaka wa I -134 na mwaka wa II – 248), wanafunzi hao ndiyo pekee watakaorudishwa katika Chuo Kikuu cha Dodoma ili wakamalizie mafunzo yao katika Chuo hicho.
 
Wanafunzi 4,586 wa mwaka wa I wa Programu Maalum ya Stashahada ya Ualimu wa Elimu ya Sekondari waliokidhi vigezo vya ufaulu watahamishiwa katika Vyuo vya Ualimu vya Morogoro, Butimba, Mpwapwa, Songea na Tukuyu kuendelea na masomo yao.
 
Wanafunzi 1,337 wa Mwaka II watahamishiwa kwenye Vyuo vya Ualimu vya Korogwe na Kasulu kumalizia masomo yao.
 
Wanafunzi 290 waliokuwa wamedahiliwa kusoma Programu Maalum ya Stashahada ya Ualimu wa Elimu ya Sekondari Masomo ya Sayansi na Hisabati ambao hawana sifa stahiki wanashauriwa kuomba mafunzo yanayolingana na sifa walizo nazo kwenye chuo chochote wanachotaka wao.
 
Kundi la Programu ya Ualimu wa Elimu ya Msingi
Serikali imesema wanafunzi katika kundi hili hawakuwa sehemu ya program maalum ya kupunguza uhaba wa walimu wa Sekondari wa Sayansi na Hisabati. Walikuwa wanaandaliwa kufundisha shule za msingi wakati lengo la Programu Maalum ilikuwa ni kukabiliana na tatizo za uhaba wa walimu wa Sekondari. Maudhui ya program waliyokuwa wanasoma hayakuwa sawasawa na yale ya Programu ya Ualimu wa Sekondari wa Sayansi na Hisabati. 
 
Wanafunzi 29 wa mwaka wa II wenye Cheti cha Daraja IIIA waliodahiliwa kusoma Stashahada ya Ualimu wa Shule za Msingi watahamishiwa katika Chuo cha Ualimu Kasulu wamalizie masomo yao kwa gharama zao wenyewe.
 
Wanafunzi 1,181 waliodahiliwa kusoma Stashahada ya Kawaida ya Ualimu wa Elimu ya Msingi waombe mafunzo yanayolingana na sifa walizonazo mahali popote watakapotaka wao.
 
Aidha Serikali imesema itaendelea kuwapatia mikopo wanafunzi watakaorejeshwa UDOM na wanafunzi watakaohamishiwa kwenye Vyuo vya Ualimu vya Serikali watapewa mkopo wa kiasi cha Sh. 600,000/= kwa mwaka ambayo ni ada ya Mafunzo ya Ualimu itakayolipwa moja kwa moja Chuoni.

Fedha za Mafunzo kwa vitendo kwa wanafunzi wa vyuo vikuu kutoka Bodi ya Mikopo kutolewa baada ya uhakiki wa wanafunzi hewa

$
0
0

Na: Lilian Lundo – MAELEZO
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Prof. Joyce Ndalichako ameeleza kuwa fedha kwa ajili ya mafunzo kwa vitendo zitatolewa mara baada ya kukamilika kwa zoezi la uhakiki wa wanafunzi waliombewa  fedha hizo toka vyuo mbalimbali hapa nchini.

Prof. Ndalichako aliyasema hayo leo katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika jijini Dar es Salaam alipokuwa akitoa ufafanuzi juu ya ucheleweshwaji wa fedha hizo kwa wanafunzi wa vyuo vikuu.

“Kuna zaidi ya wanafunzi 2,736 hewa ambao majina yao yamewasilishwa  Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) kwa ajili ya kulipwa fedha za mafunzo kwa vitendo, yakiwemo majina ya wanafunzi waliofariki na waliofukuzwa chuo,” alifafanua Prof. Ndalichako.

Aliendelea kwa kusema kuwa, kuna chuo ambacho kilituma ripoti ya wanafunzi waliofukuzwa chuo mwaka 2013/2014 lakini majina hayo yametumwa tena kwa ajili ya kupewa fedha za mafunzo kwa vitendo kwa mwaka huu.

Kutokana na kasoro zilizojitokeza katika majina ya wanafunzi wanaotakiwa kupewa fedha kwa ajili ya mafunzo kwa vitendo Prof. Ndalichako amesema kuwa Serikali haitatoa fedha mpaka uhakiki wa wanafunzi wanaotakiwa kupata fedha hizo utakapo kamilika kwa vyuo vyote nchini.

Aidha, Mhe. Ndalichako amesema kuwa majina ya wanafunzi hao hewa yamewekwa katika mitandao wakitakiwa kujihakiki TCU ili kujiridhisha kama kweli ni wanafunzi na wanaendelea na masomo.

Vile vile, Prof. Ndalichako amevitaka vyuo vikuu kutoa ushirikiano kwa timu zilizotumwa katika vyuo vyao kufanya uhakiki wa wanafunzi wanaotakiwa kupata fedha hizo kwani kuna baadhi ya vyuo vimekuwa havitoi ushirikiano kwa kisingizio cha kuwepo kwenye mitihani.

Aliongeza kwa kusema kuwa, vyuo kutotoa ushirikiano kwa timu zilizotumwa kufanya uhakiki wa wanafunzi hao kutazidi kuchelewesha fedha hizo kutoka mapema.

Ufafanuzi Kuhusu Taarifa Iliyoandikwa Na Gazeti La Jamhuri Kuhusu Ofisi Ya Bunge.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatano ya July 20

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kuzindua upanuzi Uwanja wa Ndege Dodoma

$
0
0

WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa leo atazindua awamu ya kwanza ya upanuzi wa Uwanja wa Ndege wa Dodoma ili uweze kupokea ndege kubwa za mizigo, abiria na viongozi wa kitaifa na kimataifa.

Uzinduzi huo ni miongoni mwa maandalizi ya kutimiza azma ya kuufanya mkoa wa Dodoma kuwa Makao Makuu ya Tanzania. Ujenzi huo unatarajia kugharimu Sh bilioni 11.5 ambazo ni fedha za ndani na utatoa fursa kwa mashirika ya ndege kuanza huduma Dodoma, ikiwemo ndege ambazo zitanunuliwa na serikali.

Katika mkutano wake na waandishi wa habari jana, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Jordan Rugimbana alisema, leo Waziri Mkuu atazindua awamu ya kwanza ya ukarabati wa uwanja huo kwa niaba ya Rais John Magufuli, na kuongeza kuwa uzinduzi huo hautaathiri mchakato wa kujenga Uwanja wa Ndege wa Kimataifa eneo la Msalato.

“Mchakato wa ujenzi wa uwanja wa ndege Msalato uko pale pale,” alisema Rugimbana na kuongeza kuwa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano imeamua kufanya upanuzi wa uwanja huo ili ndege kubwa zitue mkoani humo.

‘’Wizara ya Ujenzi imeamua kufanya upanuzi wa uwanja wetu wa ndege wa Dodoma ili ndege kubwa ziweze kutua na sisi tunamshukuru Rais kwa kutupa uwanja huo kwani utazidi kufungua fursa katika mkoa wetu,” alieleza Rugimbana.

Rugimbana alisema sababu ya kupanuliwa uwanja huo ni nia ya dhati ya Rais Magufuli ya serikali yake kuhamia Dodoma.

Alisema baada ya uzinduzi huo wa awamu ya kwanza, awamu ya pili itafanyika kwa haraka ili uwanja huo uweze kukamilika kama ilivyopangwa.

Upanuzi wa uwanja wa ndege wa Dodoma unahusisha njia ya kuruka na kutua kwa ndege, yenye urefu wa kilometa 2.5 na mita 500 za taa za kuongozea ndege na usalama wa kuruka kwa ndege.

Waziri Mkuu Aagiza Mauzo Ya Vitalu Vya Uvunaji Wa Miti Yafanyike Kwa Njia Ya Mnada

$
0
0

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa ameuagiza uongozi wa Wizara ya Maliasili na Utalii kubadilisha mfumo wa uvunaji wa vitatlu vya miti kwenye mashamba ya Serikali ili kuweka uwazi kwenye biashara hiyo na kuipatia zaidi Serikali mapato.

Mhe. Majaliwa alisema hayo jana kwenye Mkutano na Viongozi pamoja na Watumishi wa Wizara ya Maliasili na Utalii uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Kisenga uliopo Kijitonayama Jijini Dar es Salaam.

Akizungumzia mabadiliko hayo, Mhe. Majaliwa alisema kuwa utaratibu uliokuwa ukitumika hapo awali wa kuuza miti kwenye mashamba ya Serikali kwa njia ya vibali hauna tija kwakuwa umekuwa ukiikosesha Serikali mapato na kuwanufaisha wafanyabiashara wachache.

“Utaratibu wa sasa wa kutumia vibali unatuletea migongano ndani ya Wizara na kuikosesha Serikali mapato, hivyo ni lazima tuubadilishe” Aliongeza Majaliwa.

Aliuagiza Uongozi wa Wizara kufanya marekebisho kwenye utaratibu huo na kuweka utaratibu wa mnada ili kuweka uwazi zaidi na kuondoa manung’uniko kwenye biashara hiyo. “vibali visitishwe, mnada uanze  kama inavyofanyika kwenye mitiki” Alisema Waziri Mkuu Majaliwa.

Hivi karibuni Mhe. Majaliwa alisitisha utoaji wa vibali vya uvunaji wa miti kwenye mashamba matano yanayomilikiwa na Serikali kutokana na kupokea malalamiko mengi kutoka kwa wananchi.

Katika hatua nyingine, Mhe. Majaliwa aliagiza mabadiliko ya haraka katika vizuizi vya ukaguzi wa Maliasili ambavyo amesema vimekuwa havina tija na kuagiza baadhi yake vifutwe kabisa. Miongoni vya vizuizi alivyoagiza vifutwe ni Kibaha Stendi, Kimanzichana na Mbagala, pia aliagiza kuimarishwa kwa kituo cha Vikindu, Kibiti na Vigwaza.

Mhe. Majaliwa aliwaagiza wataalamu wa Wizara ya Maliasili na Utalii kushirikiana na Tamisemi kwa ajili ya kuweka mfumo mzuri wa kuhifadhi na kuvuna mazao ya misitu yaliyopo katika Halmashauri na kutenga Misitu ya Asili tofauti na ilivyo hivi sasa ambapo kumekuwepo muingiliano katika kutekeleza majukumu hayo jambo linalopelekea uharibifu wa misitu.

Hapo awali Mhe. Majaliwa alieleza lengo kuu la Mkutano huo kuwa ni katika utaratibu wake wa kawaida aliojiwekea wa kutembelea Wizara na kuzungumza na watumishi kwa ajili kukumbushana majukumu yao, kuangalia changamoto mbalimbali na kuzitafutia ufumbuzi. 

Aliwaasa watumishi wa Wizara ya Maliasili kuwa wazalendo, waadilifu, waaminifu na kuongeza uwajibikaji ili kuiwezesha Serikali kufikia malengo yake ya kuwahudumia vizuri wananchi.

“Ninyi ni watu muhimu sana katika utoaji wa huduma kwa wananchi, tekelezeni majukumu yenu kwa uadilifu wa hali ya juu. Kamilisheni malengo yenu kulingana na mpangokazi wenu mliojiwekea” Alisema Mhe. Majaliwa.

Kwa upande wake Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe alisisitiza watumishi wa Wizara hiyo kuhakikisha kuwa wanalinda misitu kule iliko na sio kusubiri katika vituo na kukamata rasilimali zake ambazo zimevunwa isivyo halali na kuzitoza faini, kinyume chake rasilimali hizo zilipiwe kihalali kabla ya kuvunwa. Aliahidi pia kuisuka upya Idara ya Misitu.

Mahakama Yatoa Hati ya Kukamatwa Meneja wa Diamond ‘Babu Tale’

$
0
0

MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam imetoa hati ya kukamatwa kwa Hamis Tale ‘Babu Tale,’ ambaye ni meneja wa mwanamuziki wa bongo fleva,Diamond Platnumz.

Mahakama imetoa hati hiyo kutokana na Babu Tale kutotii amri ya mahakama iliyomtaka amlipe Shekhe Hamis Mbonde Sh. 250 milioni.

Babu Tale anatakiwa alipe fedha hizo kutokana na kuvunja mkataba kati yake na Shekhe Mbonde, kwa kuuza na kusambaza nakala za mawaidha (DVDs) bila ridhaa ya shekhe huyo, jambo ambalo ni kinyume na haki miliki.

Kutokana na Babu Tale na mwenzake Iddi Tale kushindwa kulipa fedha hizo kama ilivyoamriwa tarehe 18, Februari  mwaka huu, mahakama ilitoa hati ya kukamatwa kwa wadaiwa hao tarehe 8 Julai mwaka huu.

Katika hati hiyo, mahakama ilimuelekeza Kamanda wa Polisi Kanda ya Ilala kuwa, hadi jana tarehe 19 Julai mwaka huu awe amewakamata wadaiwa hao ili wafike mahakamani kueleza kwanini wasipewe adhabu kwa kukiuka amri ya mahakama.

Shauri hilo limetajwa tena jana mbele ya Juma Hassan, Kaimu Msajili wa Wilaya wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, ambapo alitoa hati nyingine kumuelekeza Kamanda wa Polisi Kanda ya Kinondoni kuwakamata wadaiwa hao.

Msajili Juma alitoa hati hiyo baada ya Mwesigwa Muhingo, Wakili wa Shekhe Mbonde,  kuomba hati hiyo ipelekwe Kinondoni kwa kuwa Babu Tale anaishi huko na si Wilaya ya Ilala kama hati ya kwanza ilivyoeleza.

Tarehe 18 Februari mwaka huu, Jaji Augustine Shangwa, aliwaamuru wadaiwa kulipa Sh. 200 milioni  kama fidia ya kuvunja haki miliki ya Shekhe Mbonde na Sh. 50 milioni kama fidia ya hasara aliyoipata kutokana na kuvunja makubaliano.

Katika uamuzi wake Jaji Shangwa alisema, Juni 16, 2013, Mbonde aliingia makubaliano na wadaiwa hao na wenzake ya kufanya biashara ya kurekodi mawaidha na kutengeneza nakala DVDs kwa ajili ya kuziuza nchini.

Wadaiwa hao waliahidi kumjengea nyumba, kumnunulia gari na kuitangaza kazi yake pia walimpa Sh milioni mbili na kumnunulia kanzu na kofia (baraghashia) na kurekodi DVDs zenye ujumbe Uzito wa Kifo, Fitina Juu ya Wanawake, Umuhimu wa Swala, Mwanadamu Yumo Ndani ya Hasara na Maadui wa Uislam.

Alisema, makubaliano ya awali yalikuwa kurekodi halafu baadaye wakubaliane kuhusu bei na jinsi ya kuziuza, badala yake waliziuza na kuzisambaza nakala hizo na kujipatia faida bila kumshirikisha Mbonde ambaye alitumia ujuzi wake.

Mbonde kupitia wakili wake Muhingo, Gwamaka Mwaikugile na Clement Kihoko,  alifungua kesi ya madai namba 185/2013 akiiomba mahakama iamuru wadaiwa wamlipe Sh. 700 milioni kama  fidia ya kuvunja makubaliano na Sh. 50 milioni kama fidia ya hasara aliyoipata kutokana na kuvunjwa kwa makubaliano.

Nyayo za Lowassa kutikisa Kikao cha CCM Dodoma

$
0
0
Wakati CCM ikijiandaa kumkabidhi Rais John Magufuli uenyekiti, suala la masalia ya Edward Lowassa linaweza kuchukua nafasi kubwa katika vikao vitatu vya juu vinavyofanyika kwa mara ya kwanza tangu kumalizika Uchaguzi Mkuu mwaka jana.

Ni dhahiri kuwa Mkutano Mkuu Maalumu ulio na ajenda moja tu ya kumchagua mwenyekiti mpya hautakuwa na nafasi ya kujadili ajenda nyingine, lakini Halmashauri Kuu iliyogawanyika baada ya Lowassa kuenguliwa kwenye mbio za urais, inaweza kuchukua muda kujadili CCM mpya baada ya waziri huyo mkuu wa zamani kujiondoa Julai 28 mwaka jana.

CCM itaanzia mikutano yake kwa kikao cha Kamati Kuu, ambayo hufanya maandalizi ya kikao cha Halmashauri Kuu kitakachofanyika Ijumaa na kumalizia na Mkutano Mkuu Jumamosi wiki hii.

Pia kutakuwa na kikao kingine cha Halmashauri Kuu kitakachofanyika Jumapili ambacho kwa sehemu kubwa kinatarajiwa kujadili taarifa za wasaliti zilizoandaliwa na kamati za siasa za mikoa na huenda kikatoa maamuzi mazito yanayobeba mustakbali wa kuijenga “CCM ya Magufuli”.

Lakini makada wengi waliohojiwa  kuhusu suala la masalia ya Lowassa kuibuka kwenye vikao hivyo, walipinga wakisema waliomuunga mkono mwanasiasa huyo maarufu, walifanya hivyo wakati akiwa CCM na kwa kuwa hawakumfuata hawatarajii suala hilo kuibuka tena.

“Makundi ndani ya CCM yalikwisha baada ya Magufuli kupitishwa kukabidhiwa kijiti,” alisema mwenyekiti wa CCM wa mkoa wa Geita na mbunge wa Geita Vijijini, Joseph Kasheku Msukuma alipoulizwa kuhusu suala la Lowassa kuibuka kwenye vikao hivyo vya juu.

Msukuma, ambaye alifanya mbwembwe za kuhama kambi ya Bernard Membe kwa kutua na helikopta kwenye mkutano wa Lowassa mjini Arusha, alisema wakati CCM ikisaka mgombea wake wa urais, kulikuwa na makundi zaidi ya 40.

“Wakati ule kila mgombea alikuwa na kundi. Ila kwa sasa sidhani kama hali hiyo bado ipo maana baada ya mgombea kupatikana kila mmoja alimuunga mkono,” alisema Msukuma.

Kauli kama hiyo ilitolewa na mwenyekiti wa chama hicho Mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhan Madabida ambaye alisema kila mwenyekiti huja na timu yake, hivyo kama kutakuwa na mageuzi, si kitu kinachohitaji mjadala. 

“(Rais wa Awamu ya Tatu, Benjamin) Mkapa alipomuachia uenyekiti (Rais wa Awamu ya Nne, Jakaya) Kikwete alikuja na timu yake mpya. Kama utakumbuka katibu mkuu wake alikuwa Yusuf Makamba,” alisema Madabida ambaye naye alikuwa miongoni mwa wenyeviti waliomuunga mkono Lowassa.

“Nina matarajio na rais. Naamini atakifanya chama kuwa imara zaidi na kuleta mageuzi ya kisiasa na kiuchumi. Mabadiliko ni kawaida na wenyeviti wapya huja na kamati kuu na sekretarieti mpya.”

Hata hivyo, kuanzia Januari mwaka huu kamati za siasa za mikoa zimekuwa zikikutana kujadili watu wanaoitwa ni wasaliti na kupeleka mapendekezo ya hatua dhidi yao kwenye vikao vya juu.

Rais Magufuli, ambaye hajawahi kushika uongozi wa chama, anaaminika kuwa ataifanya CCM kuwa na sura, mwelekeo na ushawishi mpya, hali itakayochangia kukata mizizi iliyojengwa na wanasiasa mashuhuri.

Kutokana na hali ilivyokuwa wakati Lowassa akiondoka CCM na mtikisiko aliouacha, chama hicho hakitaweza kujipapatua bila kumtaja Lowassa na mtandao wake wakati kikijadili jinsi ya kusonga mbele.

Mbunge huyo wa zamani wa Monduli amekuwa akijadiliwa kwa ushabiki mkubwa ndani na nje ya vikao halali vya CCM tangu alipojitokeza kwa mara ya kwanza mwaka 1995 kuwania urais akiwa na umri wa miaka 42.

Kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2015, mwanasiasa huyo aliwagawa makada wa CCM na alipohamia Chadema kuna kundi lilimfuata na jingine kubakia, huku baadhi ya wanachama kwenye kundi hilo wakituhumiwa kwa usaliti.

Baada ya kujiondoa CCM Julai 28, 2015 na kujiunga Chadema alikoteuliwa kuwa mgombea urais na kuungwa mkono na vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), mashambulizi mengi kutoka CCM yalielekezwa kwake.
 
Vikao vinavyosubiriwa kutia muhuri mapendekezo ya kamati za siasa za mikoa ndivyo vinavyofanyika wiki hii mjini Dodoma baada ya CCM kuitisha mkutano mkuu maalumu ili kukamilisha taratibu za kumkabidhi Rais Magufuli usukani wa chama hicho.

 Halmashauri Kuu ya JPM 
Halmashauri Kuu ya JPM inatarajiwa kutumbua watendaji wazembe, goigoi, wasiokwenda na kasi yake, wabadhirifu wa fedha za chama na wengine ambao uwapo wao ni mzigo kwa CCM.

Hivyo, Halmashauri Kuu itasuka upya chama, pia kwa kujaza nafasi za watendaji waliojiuzulu kutokana na desturi ya chama hicho.

Kwa kawaida, CCM inapopata mwenyekiti mpya, sekretarieti yote hujiuzulu ili kumpa nafasi kiongozi huyo kupanga safu yake, alisema msemaji wa chama hicho, Christopher Ole Sendeka juzi alipoongea na waandishi wa habari mjini Dodoma.

Sekretarieti inaongozwa na katibu mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, ambaye anaaminika kuwa alifanya kazi kubwa ya kukirudishia chama hicho nguvu wakati wa kuelekea Uchaguzi Mkuu uliopita ambao ulikuwa na ushindani mkubwa.

Wengine ni Vuai Ali Vuai (Naibu Katibu Mkuu Zanzibar), Rajab Luhavi (Naibu Katibu Mkuu Bara), Mohamed Seif Khatib (Katibu wa Oganaizesheni) na Nape Nnauye (Katibu wa Itikadi na Uenezi).

Wengine ni Dk Asha-Rose Migiro (Katibu wa Idara ya Mambo ya Nje), na Zakia Meghji (Katibu wa Uchumi na Fedha).

Halmashauri Kuu ya JPM inatarajiwa pia kujadili hali ya hewa ya kisiasa ndani ya chama, kupanga mikakati ya kuimarisha uchumi na kutekeleza mapendekezo ya kuwafukuza wasaliti, ambao wanatuhumiwa kuwa waliendelea kumuunga mkono Lowassa wakati wa kampeni na kusababisha chama kupoteza baadhi ya majimbo.

 Oktoba 30, 2015 baada ya kukabidhiwa cheti cha ushindi wa urais na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi (NEC), Jaji Damian Lubuva iliandaliwa hafla fupi makao makuu ya CCM Lumumba, ambako Dk Magufuli alimwambia mwenyekiti wake akisema:“Umezungukwa na wanafiki na watu ambao ulidhani watakusaidia kwenye chama, lakini wamekuangusha” 

Miongoni mwa watu ambao hata wakati wa kampeni alikuwa anawashutumu ni waliowahi kushika nyadhifa za juu serikalini, lakini wakahamia upinzani na kuibezaSerikali.

 Dk Magufuli anaonekana alikuwa anawalenga Lowassa na mwenzake Frederick Sumaye ambao waliunda safu kabambe ndani ya Chadema kuisakama CCM.

Orodha ya watakaotumbuliwa na NEC ya JPM ni ndefu. Baadhi yao ni makada waliojitokeza hadharani kupinga utaratibu uliotumiwa na wazee kukata jina la Lowassa kugombea urais. 

Hata baada ya CCM kumteua Dk Magufuli kuwa mgombea urais, bado wapo waliompinga wakidai hana mizizi katika chama.

Wengine wanaoweza kutumbuliwa ni walioanzisha wimbo wa “Tuna imani na Lowassa” ndani ya kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM wakionyesha utiifu wao kwa Lowassa badala ya Mwenyekiti Kikwete aliyeongoza kikao cha Kamati Kuu kilichotoa majina matano ya waliopitishwa kugombea urais bila ya jina la Lowassa kuwamo.

Wengine wanaoweza kutupiwa virago ni makada waliosusa kumpigia debe Dk Magufuli pamoja na waliodaiwa kukitelekeza chama.

Habari nyingine zinasema waliopendekezwa kufukuzwa na vikao vya wilayani ni wanaodaiwa kubadilika usiku na kusaidia Ukawa, wakiwamo wenyeviti wa mikoa na makatibu.

Pia, wamo baadhi ya wabunge na wafanyabiashara waliokuwa wanawabeba mamia kwa makumi ya wanachama kwenda nyumbani kwa Lowassa mjini Dodoma kuonyesha kumuunga mkono

Bodi ya Utalii yasisitiza Mlima Kilimanjaro upo Tanzania

$
0
0
Bodi ya Utalii nchini imetoa taarifa kufafanua kuhusu mlima Kilimanjaro baada ya shirika moja la habari la Marekani kudaiwa kuchapisha taarifa iliyoonekana kuashiria mlima huo unapatikana Kenya.

Taarifa hiyo imekuja baada ya kutokea kwa kifo cha dereva wa kimataifa wa mbio za magari Guguleth Zulu, aliyefariki dunia wakati akipanda Mlima Kilimanjaro.

Kwa mujibu wa taarifa ya bodi ya utalii kwa vyombo vya habari imekanusha taarifa iliyochapishwa na mwandishi wa shirika la AP kwamba milma huo upo Kenya.

‘’Tungependa kusahihisha habari za kupotosha kwamba mlima Kilimanjaro unapatikana Tanzania na si Kenya,”

Aidha Bodi ya Utalii Tanzania imeandika barua kwa chombo cha habari kilichofanya makosa hayo na kutaka wafanye marekebisho.

Miezi michache iliyopita mtoto wa aliyekuwa Waziri Mkuu wa Kenya Raila Odinga, Rose Mary Odinga akihutubia vijana nchini Marekani aliwaambia Olduvai Gorge ipo Kenya na baadaye alikanusha taarifa hiyo.

Mikoa ya Dar es Salaam na Dodoma Yaongoza Kwa Mapenzi ya Jinsia Moja

$
0
0
Takwimu zilizotolewa na wizara ya afya, maendeleo ya jamii jinsia , watoto na wazee nchini zinaonyesha kuwa mkoa wa Dar es salaam na Dodoma inaongoza kwa vitendo vya mapenzi ya jinsia moja

Akiongea na waandishi wa habari jana jijini Dar es salaam waziri wa wizara hiyo Mhe. Ummy Mwalimu alisema kutokana na hali hiyo wizara imepiga marufuku matumizi ya vilainishi vinavyotumiwa na baadhi ya makundi yanayo jihusisha na vitendo hivyo.

Mhe. Ummy Mwalimu alisisitiza kuwa serikali imeamua kuzuia vilainishi hivyo kwani vimetajwa kuchochea vitendo hivyo ambavyo nikinyume na sheria na taratibu za nchi nakuongeza kuwa vitendo hivyo nimiongoni mwa sababu inayochangia ongezeko la VVU.

Aidha Mhe. Ummy alisema kuwa kwa sasa serikali inajikita kuhakikisha kuwa inajenga wodi za wazai, kununua vifaa tiba, madawa ya kutosha katika hosptali zake na sio ununuzi wa vilainishi hivyo.

Bodi ya Wadhamini ya Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) Yagoma Kuzungumzia Hatima ya aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo, Dk Ramadhani Dau

$
0
0
Bodi ya Wadhamini ya Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) imesema kuwa haiwezi kuzungumzia lolote kuhusu hatma ya aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo, Dk Ramadhani Dau kwa vile si mwajiriwa wao. 

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi jana kwa simu, Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Profesa Samwel Wangwe alisema bodi inashughulika na wafanyakazi wa sasa katika shirika hilo na siyo walioondoka. 

“Bodi haiwezi kuchukua hatua dhidi yake (Dk Dau).Vyombo husika ndivyo vitaamua kuhusu hilo,” alisema Profesa Wangwe alipoulizwa kuhusu hatma ya Dk Dau ambaye alikuwa bosi na msimamizi mkuu wa menejimenti iliyosimamishwa kazi. 

Pia, katika kipindi ambacho Dk Dau alikuwa mkurugenzi mkuu, aliyekuwa Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi iliyopaswa kutoa idhini ya ujenzi wa kila mradi uliopangwa alikuwa Abubakar Rajabu. 

Profesa Wangwe alisema hayo alipoulizwa kuhusu hatma ya Dk Dau baada ya bodi hiyo juzi kuwasimamisha wakurugenzi sita wa shirika hilo na mameneja sita kupisha uchunguzi wa tuhuma za ubadhirifu na matumizi mabaya ya ofisi. 

Dk Dau amekuwa mkurugenzi mkuu wa NSSF kwa miaka kadhaa hadi Februari mwaka huu alipoondolewa baada ya kuteuliwa na Rais John Magufuli kuwa balozi, ingawa bado hajapangiwa nchi. 

Katika kipindi alichoondolewa NSSF, ripoti ya ukaguzi uliofanywa na kampuni ya Ernst & Young kwa hisani ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ilivuja ikionyesha ubadhirifu wa fedha katika miradi mikubwa ya ujenzi wa majengo ya kisasa yakiwemo ya mji mpya wa Kigamboni jijini Dar es Salaam uitwao Dege Eco Village.

Miradi mingine ambayo ilichunguzwa na CAG akatilia shaka ni ujenzi mradi wa Arumeru, Arusha ambapo NSSF ilikubali kujenga majengo ya kisasa katika viwanja vya mbia mwenzake kampuni ya Azimio Housing Estate Limited ambavyo ekari moja ilithaminishwa kwa Sh1.8 bilioni.

Hata hivyo, mradi huo wenye thamani ya Sh7.2 trilioni ulisimamishwa Januri mwaka huu. 

Machi 19, Rais John Magufuli alimteua Profesa Godius Kahyarara kuchukua nafasi ya Dk Dau na Juni 28, Profesa Wangwe aliteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi. Uteuzi wake ulianza Mei 30. 

Bodi ya NSSF, katika kikao cha 106 kilichoketi Julai 15, chini ya Profesa Wangwe ilijadili ripoti mbalimbali na kufikia hatua ya kuwasimamisha vigogo hao ikisema mbali ya ubadhirifu na matumizi mabaya ya ofisi pia wanakabiliwa na tuhuma za kutofuata kanuni, sheria na taratibu za manunuzi katika uwekezaji na usimamizi wa miradi, manunuzi ya ardhi na ajira. 

Wakurugenzi waliosimamishwa ni Yacoub Kidula (Mipango, Uwekezaji na Miradi), Ludovick Mrosso (Fedha), Chiku Matessa (Rasimali Watu na Utawala), Sadi Shemliwa (Udhibiti Hadhara na Majanga), Paulin Mtunda (Ukaguzi wa Mahesabu ya Ndani) na Crescentius Magori (Uendeshaji).

 Mameneja waliosimamishwa ni Amina Abdallah (Utawala), Abdallah Mseli (Uwekezaji), John Msemo (Miradi), Davis Kalanje (Mhasibu Mkuu), Chedrick Komba (Meneja Kiongozi Temeke) na Mhandisi John Ndazi ambaye ni meneja mradi.

Taarifa zaidi zilizopatikana zilieleza kuwa baadhi ya maofisa wa shirika hilo walifikishwa juzi katika Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (Takukuru) kwa tuhuma ambazo hadi jana hazikuwa zimewekwa wazi. 

Mkurugenzi wa Mawasiliano Takukuru Mussa Misalaba alipoulizwa alisema hawezi kusema ndiyo au hapana, lakini hiyo ipo chini ya taasisi hiyo. 

“Siwezi kukutajia majina kwamba nani na nani wanachunguzwa na Takukuru, sababu kufanya hivyo ni kuwadhalilisha. Kwa kifupi hiyo ni kazi yetu,” alisema. 

Aidha, Profesa Wangwe alisema maofisa hao waliosimamishwa kazi juzi kupisha uchunguzi wa tuhuma za ubadhirifu na matumizi mabaya ya ofisi, watachunguzwa na vyombo kulingana na aina ya makosa yao. 

Alipoulizwa kuhusu vyombo vinavyowachunguza maofisa hao alisema hafahamu ni vipi na ni vingapi. 

“Vyombo vinavyohusika vitafanya uchunguzi kulingana na aina ya tuhuma zinazowakabili. Siwezi kusema ni vingapi,”alisema Profesa Wangwe. 

Kwa mujibu wa ripoti kamili ya CAG, Profesa Mussa Assad iliyowasilishwa bungeni mjini Dodoma Aprili mwaka huu, kuna utata wa ardhi ya mradi mpya wa mji wa Kigamboni unaojengwa na NSSF kwa ubia na kampuni ya Azimio Housing Estate. 

Ramani ya mradi huo wenye thamani ya Dola za Marekani 653.44 milioni (Sh1.254 trilioni) inaonyesha utakapokamilika utachangia kubadili sura ya jiji la Dar es Salaam kwani kutakuwa na nyumba za kifahari, majengo ya hoteli, maduka makubwa, eneo la wazi la mapumziko, baa, shule, hospitali, kumbi za mikutano, nyumba za ibada na migahawa. 

Profesa Assad katika ripoti hiyo alitilia shaka uhalali wa Azimio kumiliki ekari 20,000 za ardhi ambazo imetoa kama sehemu ya asilimia 20 ya mchango wake katika mradi huo na kwa kuanzia imetoa ekari 300. 

“Ukaguzi wa hatimiliki umeonyesha kuwa Azimio inamiliki viwanja viwili, kiwanja chenye hatimiliki Na. 81828 chenye ukubwa wa hekta 1.98 na chenye hatimiliki Na. 105091 chenye ukubwa wa hekta 114.11,” anasema CAG. 

“Viwanja vyote vinapatikana katika eneo la Rasi Dege ambavyo kwa pamoja vilihamishiwa kwa Hifadhi Builders kutoka kwa Azimio kwa ajili ya Awamu ya Kwanza ya mradi. 

"Kwa kutumia kizio cha ekari 2.47 kwa hekta, hatimiliki hizi zitakuwa na ukubwa wa jumla wa ekari 286.74, pungufu ya ekari 13.26 kutoka kwenye ekari 300 ambazo zilipangwa kwa ajili ya awamu ya kwanza ya mradi,” anafafanua CAG. 

CAG anasema katika kipindi chote cha ukaguzi wa mradi huo ulioanzishwa mwaka 2014, hakuwahi kupatiwa hatimiliki za ardhi ambayo Azimio aliahidi kutoa kama uchangiaji wa mtaji. 

Vilevile, CAG aliitaka NSSF kuhakikisha inakirejesha katika muda uliopangwa kiasi cha Dola za Marekani milioni 20.1 (Sh43.9 bilioni) ambazo iliilipa Azimio kwa ushauri wa ujenzi wa mradi wa mji wa Arumeru, Arusha.

“Katika ukaguzi imeonekana Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii limepokea upembuzi yakinifu wa mradi pendekezwa kutoka Azimio Housing Estate Ltd kupitia barua yake ya Mei 16, 2013 yenye kumbukumbu Na. Azimio/NSSF/Arumeru/13/5. Bodi ya Wadhamini iliidhinisha kuingiza katika ubia ardhi iliyotolewa na kampuni ya Azimio katika mikoa ya Lindi, Mtwara, Mwanza na Arusha kwa ajili ya uwekezaji unaofanana na huu,” anasema. 

“Ada ya ushauri kwa ajili ya kubuni mradi huo ni Dola za Marekani milioni 218.09 (Sh 468.9 bilioni) na ilipangwa Sh 2.4 bilioni zitumike katika awamu ya upangaji wa mradi. Hata hivyo, kiasi hicho kiliongezwa hadi kufikia Sh 102 bilioni bila ya idhini ya Bodi,” anaeleza.
 
Kwa kuwa baadaye NSSF na Azimio walikubaliana kufuta mradi wa Arumeru wenye thamani ya Sh 7.2 trilioni huku Sh43.9 bilioni zikiwa zimetolewa, CAG ameitaka NSSF kuhakikisha mbia huyo anazirejesha katika muda wa miaka mitatu kwa kuangalia riba iliyoko katika soko la wakati huo. 

Orodha ya wanachuo wanaorudi kusoma stashahada maalum ya ualimu UDOM

$
0
0
==> Kuona Majina ya Waliohamishiwa Vyuo vingine << BOFYA  HAPA>>

==> Kuona majina ya ambao hawajakidhi vigezo vya kurudishwa  << BOFYA HAPA>> 

Majina ya wanachuo waliokuwa wanasoma stashahada maalum ya ualimu chuo kikuu cha Dodoma waliopangiwa kurudi kwenye chuo hicho.  Ibonyeze Picha Kifanya iwe Kubwa zaidi  ili usome vizuri


==> Kuona Majina ya Waliohamishiwa Vyuo vingine << BOFYA  HAPA>>

==> Kuona majina ya ambao hawajakidhi vigezo vya kurudishwa  << BOFYA HAPA>>

Serikali Kununua RADA Mbili Mpya

$
0
0
SERIKALI imetangaza kununua rada mbili mpya kwa ajili ya kusaidia kukusanya mapato, zaidi ya Sh bilioni 18 ambazo zinapotea kila mwaka kutokana na kukosekana udhibiti katika anga la Tanzania.

Kauli hiyo ilitolewa jana Dar es Salaam na Naibu Waziri wa Mawasiliano, Ujenzi na Teknolojia, Edwin Ngonyani,  kwenye mkutano uliowakutanisha wataalamu wa masuala ya anga pamoja na wamiliki wa kampuni za ndege barani Afrika.

Alisema katika awamu ya kwanza, Serikali imetenga bajeti kwa ajili ya kununua rada mbili ambazo zitafungwa kwenye viwanja vya ndege vya Mwalimu Julius Nyerere na Kilimanjaro (KIA), huku awamu ya pili ikifungwa katika viwanja vya Mwanza na Songwe.

“Serikali tayari imeshatenga bajeti kwa ajili ya kuhakikisha kuwa inanunua rada mbili, ili kuokoa kiasi cha takribani bilioni 18/- ambazo zimekuwa zikipotea kila mwaka, jambo ambalo linafanya nchi kupoteza mapato, kwani inakuwa haiwezi kulisimamia anga lake lote na hivyo kufanya ndege, hata zile zisizotua nchini huku zikitumia anga hilo, kushindwa kulipa ushuru.

“Kwa sasa Kenya na Rwanda ndiyo nchi zenye rada hizo licha ya kuwa nchi hizo ni ndogo ukilinganisha na Tanzania, rada hizi kila moja inauzwa dola za Marekani milioni 24. Unapoagiza unatakiwa kulipia nusu ya gharama na pindi inapokamilika unamalizia nusu iliyobaki,” alisema Naibu Waziri Ngonyani.

Kwa upande wake, Mkurungezi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TCAA), Hamza Johari, alisema kuwa ununuzi wa rada hizo utasaidia kuongeza mapato na hivyo kufanya viwanja vya ndege kujiendesha vyenyewe bila kusubiri msaada kutoka serikalini.

Katika hatua nyingine, Johari alisema kuwa mamlaka hiyo imesema Tanzania bado haijafikia kiwango cha utengenezaji ndege na hivyo kuwapiga marufuku wanaofikiria kuzitengeneza bila kuwa na kibali cha mamlaka hiyo.

“Ili kuunda ndege unatakiwa kuwa na zana za kisasa… Kwa Tanzania bado hatujafikia uwezo huo, hivyo kama TCAA tunatoa wito kwa wale wote wanaotaka kufanya hivyo bila kushirikisha mamlaka, kuacha mara koja mpango huo kwani ndege hizo wanazotengeneza bila kufuata taratibu, ni hatari na zinaweza zisimudu kukaa hewani muda mrefu na hivyo kusababisha hatari kubwa.

“Hivyo kama mtu anafikiri kuwa ana mawazo ya kutaka kutengeneza ndege, ni lazima aanzie kwetu ili tumshauri kupitia wataalamu wetu na si vinginevyo,” alisema Johari.

Mkutano huo ulikuwa ukikutanisha wamiliki wa ndege zilizokidhi vigezo na wadau mbalimbali wa masuala ya anga kutoka kote Afrika, ukiwa na lengo la kujadili changamoto zilizopo kwenye sekta hiyo.

RIWAYA: Mwanafunzi Mchawi - (A Wizard Student) - Sehemu ya 17

$
0
0
Mtunzi: Enea Faidy

..... MANSOOR alimtazama Dorice kwa jicho la kiulizo lililomtaka azungumze chochote lakini Dorice hakusema neno zaidi ya kuangua kilio cha huzuni baada ya kukosa msaada kwa Mansoor. Dorice alilia sana kwani alijua kurudi tena duniani sasa ni ndoto.

"Mansoor naomba unisaidie!" Dorice alipiga magoti akamsihi Mansoor aweze kumsaidia ili arudi kwao pia amsaidie kumwokoa Eddy ili furaha ya penzi lake irudi.

"Dorice! Naweza kukusaidia kwa yote hayo... Ila inabidi ukubali kuolewa na Mimi maana bila hivyo mama yangu hatonielewa...!" Mansoor alisisitiza.
"Siwezi kuolewa na wewe..!"

"Kwanini? Au kwa vile Mimi sio binadamu mwenzio? Jua nakupenda na nitakuruhusu kuendelea na Eddy.. Nielewe Dorice!" Mansoor alizidi kumweka Dorice katika wakati mgumu sana kwani kiukweli Dorice aliuhitaji msaada wa Mansoor ila masharti yake yalikuwa kikwazo sana. 

Dorice alishindwa kung'amua juu ya mtihani ule mzito. Alijua fika wazazi wake wataumia sana endapo wakijua kuwa Hayupo duniani, aliyafikiria maumivu ambayo mama yake angeyapata kama yeye angepotelea kule kwenye ulimwengu wa majini.

"Sijui nimkubali halafu akinirudisha duniani nimkatae?" Dorice Alizidi kuwa na utitiri wa mawazo kichwani mwake. Ghafla akashtushwa na sauti nzuri ya mahaba ya Mansoor akizidi kumshawishi kuwa amkubalie ili aweze kumsaidia kutatua matatizo yake.

"Dorice! Nifanye nifurahi tafadhali.. Nilipendwa na wengi ambao si chaguo langu.. Nasikitika chaguo langu linakuwa mwiba moyoni mwangu! Kwanini lakini?"

Dorice alivuta pumzi ndefu na kuishusha taratibu, huku akiwa ameinamisha kichwa chake. Taratibu akanyanyua kichwa chake na kumtazama Mansoor. Macho yake yalistaajabu uzuri wa asili aliokuwa nao kijana yule. Hata kama majini ni wazuri lakini Mansoor alizidi kipimo, kuanzia macho yake, pua yake na midomo mizuri ya kupendeza sana.

"Nimekubali Mansoor! Ila kabla ya yote naomba uniahidi kama utanisaidia!" Alisema Dorice kwa sauti iliyotulia sana. Maneno hayo yalifungua ukurasa mpya moyoni kwa Mansoor, alifurahi kupita kiasi akamkumbatia kwa nguvu Dorice.

"Nakuahidi kukusaidia Dorice!" Alisema Mansoor akiwa amemkumbatia Dorice.
Walikumbatiana kwa muda kisha wakaachiana. Mansoor akamtazama Dorice huku akitabasamu.
"Nataka uvae vizuri nikupeleke kwa mama yangu muda huu!"
"Nitavaa nini? Sina nguo!"
Alisema Dorice kwa woga huku moyo wake ukimsuta kwa kumsaliti Eddy kwani alikwisha muahidi kuwa hatokuwa na mwanaume mwingine yeyote zaidi yake."lakini ni kwa sababu yake..!" Alijipa Jibu Dorice.
"Unapenda nguo gani?" Aliuliza Mansoor.
"Nguo yoyote itakayonifaa!" Alijibu Dorice.

Mansoor alinyoosha mkono juu ghafla ukatokea mfuko mmoja wenye ukubwa kiasi kisha akamkabidhi Dorice. Dorice aliogopa sana, akasita kupokea.
"Usiogope.. Chukua!"
Dorice akapokea mfuko ule japo kwa woga kisha akaufungua ili atazame kilichomo. Akapigwa na bumbuwazi.

Taarifa Kwa Umma Kutoka MSD Juu Ya Uamuzi Wa Bodi Ya Wadhamini Kuhusu Wakurugenzi Waliosimamishwa


Mlinzi wa Kampuni ya Ulinzi Ajinyonga Baada ya Kugundulika ana Virusi Vya UKIMWI

$
0
0
Mlinzi wa Kampuni ya Ulinzi ya Imara, Samwel Arcado (39) amejinyonga ndani ya chumba chake kwa madai ya kugundulika kuwa na maambukizi ya virusi vya Ukimwi (VVU). 

Mlinzi huyo ambaye ni mkazi wa Mtaa wa Mji wa Zamani, Manispaa ya Mpanda alikutwa amejinyonga kwa kutumia shati. 

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi, Damas Nyanda alisema jana kuwa uchunguzi kuhusu tukio hilo unaendelea.

 Mwenyekiti wa mtaa huo, Margaret John alisema tukio hilo lilitokea jana saa kumi na moja alfajiri ndani ya chumba alichokuwa akiishi Arcado. 

Alisema Samwel alikuwa akisumbuliwa na maradhi ya mara kwa mara, hali iliyosababisha kwenda hospitali kufanyiwa uchunguzi wa afya yake, ambako aligundulika kuwa na VVU. 

John alisema baada ya kupatiwa majibu hayo alichanganyikiwa, hali iliyosababisha utendaji wake wa kazi kuzorota. 

Alisema kutokana na kushindwa kufanya kazi kwa ufanisi, mwajiri wake alitaka kumrejesha nyumbani kwao mjini Sumbawanga mkoani Rukwa. 

Hata hivyo, taarifa zinadai kuwa siku ya safari ilipofika, mmoja wa wafanyakazi wenzake alifika kwenye nyumba aliyokuwa amepanga kwa lengo la kumwamsha ili ajiandae, lakini alipomgongea mlango hakujibiwa hali iliyompa shaka na kuwaamsha wapangaji wengine. 

Mwenyekiti huyo alisema mfanyakazi huyo na wapangaji wenzake, walitoa taarifa kwa uongozi wa serikali ya mtaa na ulipofika uliamuru mlango uvujwe na kukuta amejinyonga. Alisema walitoa taarifa polisi ambao walifika na kuchukua mwili. 

Daktari FEKI adaiwa kuua mgonjwa Singida Baada ya Kumfanyia Upasuaji wa Tezi Dume

$
0
0
Mkazi mmoja mkoani Singida anayedaiwa kuwa daktari feki anatuhumiwa kusababisha kifo cha mgonjwa, Israel Shabani (68) baada ya kumfanyia upasuaji wa tezi dume. 

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, Thobias Sedoyeka alisema jana kuwa tukio hilo lilitokea Alhamisi iliyopita saa mbili usiku nyumbani kwa mtuhumiwa baada ya kumfanyia Shabani upasuaji.

Alisema mtuhumiwa huyo anadaiwa alikuwa akifanya kazi katika vituo vya afya serikalini, lakini baada ya kuacha alijiita daktari na kuamua kutoa tiba ikiwamo ya upasuaji nyumbani kwake kinyume na sheria.

Baada ya kumfanyia upasuaji huo wa kienyeji, mgonjwa huyo alitokwa damu nyingi na kuwa katika hali mbaya.Mtuhumiwa alipobaini hali hiyo, alimtelekeza na kukimbilia kusikojulikana.

Alidai kuwa baada ya polisi kufanya upekuzi kwenye nyumba ya mtuhumiwa huyo, walikamata vifaa vingi vya tiba zikiwamo dawa za kutibu binadamu.

BAVICHA Waikimbia Dodoma......Waamua Kuhamishia Mkutano wao Dar es Salaam

$
0
0
Wakati kukiwa na ulinzi mkali mjini Dodoma kuelekea Mkutano Mkuu Maalumu wa CCM, Baraza la Vijana la Chadema (Bavicha) limehamishia mkutano wake wa kamati ya utendaji jijini Dar es Salaam.

Jana, sekretareti ya CCM ilianza maandalizi kusafisha njia kwa ajili ya kikao cha Kamati Kuu, Halmashauri Kuu na baadaye Mkutano Mkuu uliopangwa kufanyika Jumamosi.

Awali, Bavicha ilikuwa imehamasisha vijana wa chama hicho kuja kwa wingi mjini hapa kwa ajili ya “kutekeleza agizo la Rais John Magufuli kuzuia mikutano ya kisiasa”, lakini Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe alifuta mpango huo akisema: “Waache wafu wawazike wafu wao”.

Pamoja na Mbowe kuzuia, Mwenyekiti wa Bavicha, Patrobas Katambi alisema wiki iliyopita kuwa wameandaa mkutano wa Kamati ya Utendaji wa Baraza hilo leo mjini Dodoma na ungefunguliwa na Mbowe.

Huku ulinzi ukizidi kuimarishwa, jana kulikuwa na uamuzi tofauti.

Mwenyekiti wa Bavicha Mkoa wa Dodoma, Malambaya Manyanya jana alisema wameamua kuuhamishia mkutano huo Dar es Salaam baada ya kuona mzozo umekuwa mkali.

"Tumeona mzozo ni mkali sana. Tumeona imeshakuwa shida, tukaona ngoja tukafanyie Dar,” alisema Manyanya.

Alisema wajumbe waliokuwa waingie Dodoma jana, wameambiwa wote waelekee Dar es Salaam  kwenye jengo la makao makuu

Msemaji wa CCM, Christopher Ole Sendeka yeye anasema kutakuwa ulinzi mkali na hakuna atakayeweza kujaribu kuvuruga mkutano huo ambao utashuhudia Rais John Magufuli akichaguliwa kuwa mwenyekiti mpya wa chama hicho.

Ole Sendeka alisema kwenye ukumbi mpya wa CCM ambako ndiko mkutano huo utakafanyika, kutakuwa na kamera maalumu zitakazofungwa ndani na nje ya ukumbi ili kuwezesha kuona kila kitu kinachoendelea.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Jordan Rugimbana ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wa mkoa, alisema ameona kwenye mitandao ya kijamii kwamba baadhi ya vyama vinatoa vitisho na kuwataka wananchi wavipuuze.

 “Na kama kuna mtu anadhani kuwa anaweza kukwamisha mkutano mkuu wa CCM, nimwambie Dodoma si salama kwake. Afikirie mahali pengine, lakini si Dodoma,” alisema.

“Nitumie fursa hii kuwaomba wananchi pale wanapoona mtu wasiyemwelewa au dalili waripoti haraka kwenye vyombo vya habari na dola au kwa viongozi popote pale ambapo wanaweza kushirikiana kuliondoa hilo tatizo. Lakini kwa ujumla hali iko shwari mpaka sasa,” alisema Rugimbana.

 Wakati Rugimbana akisema hayo Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Mayalla Towo amesema wameweka miundombinu ya kuweza kuwabaini wahalifu, lakini hawezi kuitaja.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Alhamisi ya July 21

Taarifa kutoka Ikulu: Uamuzi wa China kuhusu ujenzi wa Reli ya kati kwa kiwango cha kisasa Tanzania

$
0
0
Benki ya Exim ya China imekubali kutoa mkopo wenye masharti nafuu wa dola za Marekani Bilioni 7.6  sawa na zaidi ya Shilingi Trilioni 16 za kitanzania kwa ajili ya kugharamia ujenzi wa mradi mkubwa wa reli ya kati hapa nchini kwa kiwango cha kisasa (Standard Gauge) unaotarajiwa kuanza katika mwaka huu wa fedha.

Rais wa Benki ya Exim ya China Bw. Liu Liang amemueleza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli jana tarehe 20 Julai, 2016 katika Ikulu ndogo ya Chamwino Mkoani Dodoma, kuwa pamoja na kutoa fedha hizo zitakazofanikisha ujenzi wa kilometa 2,190 za reli ya kati benki hiyo itashirikiana na Tanzania  katika kubadilishana uzoefu na utaalamu katika ujenzi na uendeshaji wa reli.

Pamoja na kukubali kutoa fedha hizo, Rais huyo wa Benki ya Exim ya China amempongeza Rais Magufuli na serikali yake kwa dhamira ya dhati ya kuiletea nchi maendeleo ikiwemo kuharakisha ujenzi wa reli ya kati na ameahidi kuwa benki yake itatoa ushirikiano wa karibu katika kufanikisha mradi huo na miradi mingine ya maendeleo.

“Kuhusu huu mradi wa reli ya kati tuna mtazamo chanya, tunauona ni mradi mzuri na tutatoa ushirikiano wowote utakaohitajika. Tunaamini kuwa kwa ushirikiano na serikali ya Tanzania mchakato wa utekelezaji wa mradi huu utafanyika kwa mafanikio na kwa kuzingatia muda” Amesema Rais Magufuli.

Kwa upande wake Rais Magufuli amemshukuru Rais wa Benki ya Exim ya China Bw. Liu Liang kwa kukubali kutoa fedha hizo na amemuhakikishia kuwa Tanzania imedhamiria kutekeleza mradi huo ambao tayari ujenzi wake umepangwa kuanza katika mwaka huu wa fedha kwa kutumia fedha za ndani kiasi cha shilingi Trilioni 1 zilizotengwa katika bajeti.

Rais Magufuli amebainisha kuwa kutekelezwa kwa mradi huo kutasaidia kuinua uchumi wa Tanzania na nchi jirani zisizopakana na bahari zikiwemo Uganda, Rwanda, Burundi, na Congo.

“Kwa hiyo kukubali kwao ambako ilikuwa ni kitu kikubwa, inaonesha kwamba juhudi za Tanzania kwenda haraka haraka zinakubalika kimataifa, na wenzetu hawa wachina wana pesa nyingi.

“Na kule kuaminika kwamba tunakopeshwa kwa masharti nafuu, riba yake ni ndogo na huku kwetu ni mafanikio makubwa, kwa hiyo mizigo mingi tutakuwa tunaisafirisha, tutaendeleza reli yetu na bandari zetu” Amesema Rais Magufuli.

Mradi wa ujenzi wa reli ya kati utahusisha ujenzi wa reli kwa kiwango cha kisasa (Standard Gauge) kutoka Dar es salaam-Tabora-Isaka-Mwanza, Tabora-Mpanda-Kalemela, Tabora-Uvinza-Kigoma na Isaka-Keza-Msongati.

Mazungumzo kati ya Rais Magufuli na Rais wa benki ya Exim ya China yamehudhuriwa na Balozi wa China hapa nchini Dkt. Lu Youqing, Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa Mnyaa, Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Suzan Kolimba.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam
20 Julai, 2016
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images