Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Tuhuma za Ubadhirifu wa Sh bilioni 1.4 za Uchaguzi Mkuu wa Oktoba mwaka jana Zatua TAKUKURU

$
0
0

TUHUMA za ubadhirifu wa Sh bilioni 1.4 za Uchaguzi Mkuu wa Oktoba mwaka jana, zilizotolewa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kwa Halmashauri ya wilaya Mbinga mkoani Ruvuma, zimefikishwa kwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru).

Mkuu wa Wilaya ya Mbinga, Senyi Ngaga, alisema Takukuru inakamilisha uchunguzi wa kina ili wahusika waliofanya ubadhirifu huo wachukuliwe hatua za kisheria. 

Alisema hayo juzi alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake.

Alisema upo ukiukwaji mkubwa wa taratibu za manunuzi uliofanywa na wahusika waliopewa dhamana ya kusimamia matumizi yake. 

Ngaga alisema, ofisi yake baada ya kuunda tume ndogo na kubaini hilo, uchunguzi wa awali unaonesha Sh milioni 513 zimefanyiwa ubadhirifu .

Alisema, aliona ni vyema achukue hatua ya kukabidhi tuhuma hizo kwa Takukuru wafanye uchunguzi wa kina kutambua ni nani aliyehusika na ubadhirifu huo.

 Alisema, taarifa na majina ya wahusika waliofanya hivyo itatolewa baadaye Takukuru ikikamilisha kazi yake.

“Takukuru inaendelea na uchunguzi, ikikamilisha taarifa itatolewa. Katika maelezo yangu ya awali kwenye Baraza la Madiwani lililokaa juzi sikuhukumu mtu wala kusema amehusika, hivyo tusubiri tutajulishwa,” alisema.

Aliongeza kuwa, uchunguzi huo utakapokamilika, taarifa husika zitapelekwa kwa Mwenyekiti wa Baraza la Ulinzi na Usalama mkoa wa Ruvuma, Said Mwambungu awasilishe kwa Waziri mwenye dhamana.

Awali, tuhuma za ubadhirifu huo, zilitolewa na Mkuu wa Wilaya kwenye kikao cha Baraza la Madiwani wa wilaya hiyo, Mei 11, mwaka huu.

CUF Waishitaki Serikali Mahakama ya Kimataifa (ICC)

$
0
0
Chama cha Wananchi (CUF) kimesema kitawashtaki Mahakama ya Kimataifa (ICC) viongozi wa Serikali ambao walitumia mamlaka yao vibaya wakati wa Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana, wakiwamo Waziri wa Mambo ya Ndani na Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Ernest Mangu. 

CUF, chama kikuu cha upinzani visiwani Zanzibar kinachodai kuwa mgombea wake wa urais alishinda kwenye uchaguzi huo uliofanyika Oktoba 25, 2015, kimesema kwa sasa kinatumia kampuni mbili za kisheria, moja ya ndani na nyingine ya nje, kuwasaidia katika kushughulikia suala hilo. 

Mbali na vigogo hao wawili wa Serikali, chama hicho kimesema hatua hiyo pia itawahusisha viongozi na watumishi wa umma ambao hawakuchukua hatua kwa dhuluma iliyofanywa kwa Wazanzibari wakati na baada ya uchaguzi. 

CUF imesema hatua hiyo itachukuliwa baada ya jana kuzindua ripoti yake ya uvunjwaji wa haki za binadamu visiwani humo wakati wa uchaguzi huo. 

Mbali na kuwafikisha ICC, Mazrui alisema tayari chama hicho kimeanza kuchukua hatua stahiki ili kuwafikisha viongozi hao kwanza mbele ya Mahakama Kuu ya Tanzania kwa kutochukua hatua dhidi ya uovu uliokuwa unafanywa Zanzibar wakati wa kipindi hicho. 

Iwapo CUF itatekeleza azima hiyo, itakuwa tukio la kwanza kwa Tanzania kupeleka viongozi wake kwenye mahakama hiyo inayopingwa na viongozi wa Afrika wanaodai kuwa wana vyombo vyao vya kushughulikia haki za binadamu.

Tayari viongozi wawili wa Kenya, Rais na makamu wake wameshafikishwa kwenye mahakama hiyo, lakini kesi dhidi yao ilikosa nguvu baada ya mashahidi kukataa kwenda kutoa ushahidi.

Katika Uchaguzi Mkuu uliopita, mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi (ZEC), Salim Jecha Salim alifuta matokeo ya urais, wawakilishi na madiwani Oktoba 28, mwaka jana siku ambayo alitakiwa atangaze mshindi wa mbio za urais.

Alifuta wakati matokeo ya majimbo 31 kati ya 40 yameshatangazwa na kubakia majimbo tisa ambayo matokeo yalishabandikwa vituoni. 

CUF ilidai kuwa ilishinda na Jecha alipotangaza uchaguzi wa marudio, chama hicho kilijitoa na hivyo CCM kushinda viti vyote. 

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Naibu katibu mkuu wa CUF Zanzibar, Nassor Ahmed Mazrui alisema chama chake kinakamilisha ripoti ya ukiukwaji wa wa haki za binadamu uliofanywa wakati wa mchakato huo ambao chama hicho kina ushahidi wa kutosha. 

Alisema ripoti hiyo ina matukio yote yaliyotokea kuanzia uandikishaji, kampeni, kuahirishwa kwa uchaguzi na hata kurudiwa.

“Hakuna mtu aliyechukuliwa hatua za kisheria ili kutenda haki kwa waathirika,” alisema akizungumzia vitendo vya wananchi kupigwa na askari, kurushiwa risasi za moto, kubambikiwa kesi, mashambulizi yaliyofanywa na mazombi na uchomaji nyumba za wafuasi na ofisi za wafuasi wa chama. 

Shaweji Mketo, Mkurugenzi wa Uchaguzi wa CUF alifafanua kuwa licha ya viongozi hao wa wizara na Jeshi la Polisi kuanza kushtakiwa kwenye mahakama za ndani, ICC itawahusisha watu wengi zaidi. 

Alisema juhudi za makusudi zimechukuliwa na chama hicho  kuwatafuta washauri wa masuala ya kisheria na uendeshaji wa ICC ili kukusanya ushahidi wa kutosha utakaowatia hatiani wahusika wote. 

 “Waziri, IGP na baadhi ya askari watahusika. Tunayo majina yao na uchunguzi wetu utakapokamilika tutawataja,” alisema Mketo. 

Kuhusu waziri atakayehusika kwenye mashtaka yatakayofunguliwa ICC endapo vigezo vitatosha ni wale waliokuwa kwenye nafasi hiyo wakati hayo yakitokea. 

“Zipo kampuni mbili zinatushauri na kutusaidia kukusanya ushahidi,” alisema bila kuzitaja, lakini akafafanua kuwa moja ni ya nje na nyingine ya ndani. 

Alisema hazitaji majina kwa kuwa Serikali inaweza ikaingilia kati na kukwamisha mchakato mzima. 

Baada ya uzinduzi wa ripoti hiyo uliofanyika jana, Mazrui alisema wamepanga kumuandikia barua Rais John Magufuli na kumkabidhi nakala kwa kuwa ni Amiri Jeshi Mkuu, ajue kinachoendelea ndani ya utawala wake.

Alisema ripoti hiyo pia itapelekwa kwenye jumuiya, taasisi na mashirika ya kimataifa yanayotetea haki za binadamu ulimwenguni. 

Alisema CUF imebaini mipango ya Serikali ya kutaka kuwakamata viongozi wake wa Zanzibar na “kuwaweka kwenye magereza ya Bara ili kuwanyamazisha Wazanzibar”. 

Ili kuongeza uwazi kwa wanaharakati wa ndani, alisema ripoti ya chama chake sambamba na vielelezo vyote muhimu, itapelekwa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar (ZLSC) na taasisi nyingine zinazojishughulisha na masuala ya haki za binadamu nchini. 

Ili kuongeza uwajibikaji, alisema jopo la mawakili wa chama chake linashirikiana na wanasheria wabobezi wa kimataifa ili kukamilisha taratibu zitakazowezesha kuchukuliwa hatua kwa watu wote ambao walichochea au walitoa maagizo yaliyosababisha makosa dhidi ya binadamu.

“Tumeshamuandikia barua IGP na waziri. Hiyo ni moja ya hatua muhimu kabla hujawashtaki,” alisema. 

Waziri hakupatikana kuthibitisha kupokea barua hiyo. IGP alisema hajaipata ripoti hiyo, hivyo hawezi kusema chochote juu ya madai yaliyosemwa na CUF. “Nikiipata nitaijibu,” alisema kwa kifupi. 

Naibu katibu mkuu wa CCM-Zanzibar, Vuai Ali Vuai alisema hujuma ni sehemu ya siasa za kila siku visiwani humo. 

Alibainisha kuwa chama chake ambacho kimekuwa kikitangazwa mshindi tangu siasa za ushindani ziliporejeshwa mwaka 1992, kimekuwa kikihujumiwa tangu kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi na kutoa rai kwa CUF kuchukua hatua kama ina uthibitisho. 

“Makosa yote ya jinai yanashughulikiwa na vyombo vya dola. Kinachohitajika ni ushahidi wa kutosha,” alisema Vuai. 

Pia alitahadharisha dhidi ya siasa za chuki ambazo alisema zinaenezwa visiwani humo licha ya kuwa pazia la Uchaguzi Mkuu limeshafungwa.“Wapo viongozi wanaenda misikitini kuhubiri uongo… hii si sawa,” alisema. 

Kuhusu hatua za zinazotarajiwa kuchukuliwa na CUF alisema viongozi wa chama hicho wanajua kuwa wamekosea, hivyo wanajaribu kutafuta namna ya kuwatuliza wanachama wao hasa wale waliopoteza nafasi zao za uwakilishi kwenye Baraza la Wawakilishi.

“Viongozi wanahangaika. Jinamizi la kususia uchaguzi bado linawaandama. Hawaeleweki na ndiyo maana wanajaribu kote kote, Mahakamani na misikitini. Huko ni kutapatapa,” alisisitiza Vuai. 

Spika Asema Baadhi ya Wabunge Huvuta bangi na Unga, asema vifaa maalum Vitafungwa ili Kuwabaini

$
0
0

Kama unashangaa kusikia kwamba aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga, ametimuliwa kwa kuingia bungeni akiwa amelewa.

Bila shaka utachoka zaidi ukisikia kuna wabunge kadhaa huingia kwenye ukumbi wa Bunge wakiwa wametumia vilevi vikali zaidi vikiwamo bangi, viroba na dawa za kulevya.
 
Spika wa Bunge, Job Ndugai, ndiye aliyefichua siri hiyo jana.
Kutokana na hali hiyo, Ndugai alisema sasa wanafikiria kuweka vifaa maalumu vya kupima ulevi kwa watunga sheria hao na kutafuta wataalamu wa ushauri nasaha watakaowapa msaada wa kisaikolojia.
 
“Kikubwa tunataka kuweka mkakati wa kujaribu kumtambua (mbunge) mmoja mmoja na kujaribu kuwatafuta wale watu wanaotoa ushauri nasaha au watu wa mambo ya saikolojia.

“Tunajaribu ku-identify (kuwatambua) watu maalum wanaoweza kutusaidia kuzungumza na hawa watu ili waondokane na matatizo yale ambayo tutaweza kuyagundua… lakini wale wanaofanya kwa kificho itakuwa tabu kidogo. Lakini huko mbele tutakwenda kwenye vifaa,” alisema Ndugai na kuongeza:
 
“Maana siyo ulevi tu, kuna sigara kubwa (bangi), unga (dawa za kulevya)… watu wanapiga konyagi hadi mchana, kimsingi mambo ni mengi,” alisema Ndugai.
 
Hata hivyo, alisisitiza kuwa kwa taarifa hiyo asieleweke vibaya kuwa ni wabunge wote hutumia vilevi kabla ya kuingia bungeni, bali wapo wachache wenye kawaida hiyo na kwamba hao ndiyo wanaostahili kusaidiwa na wataalamu wa saikolojia na pia kufunga vifaa maalum vya kuwabaini.
 
“Simaanishi wote (wabunge), maana mtu anaweza kufikiri ni wabunge wote… hapana. Hili ni kundi dogo mno la wabunge (na) hawajai hata mkononi. Lakini wabunge walio wengi ndiyo wazuri sana, hawanywi pombe wala nini. Kikundi hiki kinahitaji msaada wa ushauri,” alisema. 
 
Akiendelea kufafanua, Ndugai alisema: “Tatizo ni kubwa kiasi… na siyo la kulewa peke yake, lazima kuangalia namna gani ya kumbana mtu yeyote ambaye amelewa, (kama) ametumia madawa ya kulevya.
 
“Kwa hiyo linatakiwa suala la kubadili kanuni litazamwe kwa mapana, siyo leo unadhibiti aliyelewa, kesho unadhibiti hali hii… ni lazima kuliangalia (suala hili) kwa mapana yake,” alisema Ndugai.
 
Alisema tofauti na kikao cha asubuhi ambacho ndicho Kitwanga aliingia akiwa amelewa (Ijumaa Mei 20, 2016), kile cha jioni ndiyo huwa kibaya zaidi.
 
“Nakubaliana ipo haja ya kuwa na vifaa, hasa bunge la mchana ndiyo huwa (na tatizo) zaidi, maana kuna baadhi ya wabunge wanakuja pale mchana wameshalewa,” alisema.
 
Alisema wabunge hao ambao huingia bungeni wakiwa wameutwika, kubwia unga ama bangi, wakati mwingine hutibua vikao vya Bunge.
 
“Huyo mbunge mmoja au wawili, wanaweza kutibua Bunge …ukajikuta Bunge zima linatibuka kumbe wenzenu hawapo `normal’ (kawaida). Kwa hiyo tunaendelea kuangalia (namna ya kudhibiti hali hiyo) kwa kupewa mawazo na Watanzania,” alisema Ndugai.
 
Alisema wakati mwingine Kamati ya Bunge ya Maadili inakaa na kufanya maazimio juu ya mbunge fulani, kumbe ukweli ni kwamba mhusika hakuwa sawa wakati akifanya tukio hilo la kukiuka kanuni bali anakabiliwa na msukumo ‘fulani’.
 
Akieleza kuhusu hatua watakazozichukua dhidi ya Kitwanga ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Misungwi, Ndugai alisema hawafikirii kumpa adhabu yoyote baada ya ile ya kuondolewa uwaziri.
 
“Kuhusu Kitwanga, hatuwezi kumchukulia hatua yoyote ile. Kama ni mlevi sana, anatakiwa kufanyiwa `counseling’ (kupewa ushauri nasaha) ili kuondokana na hilo tatizo. Mimi siwezi kujiunga na wale ambao wanamsakama, mimi ni baba na mama wa wabunge wote… kwa yule ambaye ameteleza, mimi ni wajibu wangu kumrudisha kwenye mstari. Ndiyo kazi nitakayofanya.”

Tangazo la Nafasi za Kazi Wizara ya Afya...... Wanahitajika Watu 192, Mwisho wa Kutuma Maombi ni Tarehe 6 Juni

Watanzania Kuanza Kunufaika na Hati Fungani ya NMB

$
0
0
  • Wateja na wasio wateja wa NMB kunufaika kwa Kiwango cha uwekezaji cha kuanzia Kiwango TZS 500,000 
  • Hati fungani ya NMB inapatikana katika matawi yote ya NMB na kwa mawakala.
Benki ya NMB PLC imeanza kutoa hati fungani ya NMB yenye riba ya 13% kwa yeyote mwenye nia ya kuwekeza na kupata faida nzuri. 

Hii ni mara ya kwanza kwa NMB kutoa hati fungani ya namna hii na inaweza kununuliwa kupitia matawi yote ya NMB au kwa mawakala wanaotambulika kwa kiasi cha chini cha shilingi 500,000 (laki tano tu). 

Kufunguliwa kwa hati fungani ya NMB kwa wananchi ni matokeo ya kupata kibali kutoka mamlaka ya masoko ya mitaji nchini - Capital Markets & Securities Authority (CMSA).

Wawekezaki wa hati fungani ya NMB watapata riba ya asilimia 13 kwa mwaka itakayolipwa kila baada ya miezi sita kwa miaka mitatu mpaka mwezi Juni 2019; Riba itakayotolewa itakatwa kodi ya mapato.

Hati fungani ya NMB inauzika pia, na mteja anaweza kuiuza kwa mnunuaji mwingine na kupata fedha yake kabla ya kmukomaa kwa hati fungani – yaani miaka mitatu. 

Wawekezaji wanaweza kuiuza hati fungani hiyo kabla ya kukomaa katika soko la wazi kupitia mawakala wa soko la mitaji – kwa kufuata misingi ya soko la hisa la Dar es Salaam.

Hati fungani ya NMB itauzwa kuanzia tarehe 10 Mei, 2016 mpaka June 8 2016 na riba itaanza kulimbikizwa kuanzia tarehe hii. Kununua hati fungani ya NMB, mteja anatakiwa kutembelea tawi lolote la NMB kati ya matawi 175 nchini kote au kwa mawakala wanaotambuliwa.

Tembelea tawi na NMB kunua hati fungani hii na hakikisha umebeba viambatanishi vifuatavyo;
  • Fomu ya bondi iliyokamilika na kusainiwa
  • Nakala ya kitambulisho
  • Akaunti ya CDS
  • Kianzio cha fedha cha shilingi 500,000
  • Taarifa za akaunti yako ya benki.

Naibu Waziri Ajibu swali Lililomponza Kitwanga.....Asema Serikali Imekusudia Kujenga Nyumba 9500 Kwa Ajili Ya Askari Magereza

$
0
0
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Hamad Yusufu amejibu upya swali lililomponza bosi wake wa zamani, Charles Kitwanga.

Uamuzi wa kurudia swali hilo ulitolewa juzi na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisema swali hilo lilijibiwa katika hali ya ulevi na aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani na wabunge wakaomba mwongozo kuhusu majibu yaliyotolewa.

Kitwanga aliondolewa katika nafasi yake na Rais John Magufuli baada ya kujibu ya swali hilo akiwa amelewa.

Leo, Masauni amejibu swali hilo namba 211 la Mbunge wa Viti Maalumu Devota Minja (Chadema) na kuonyesha utofauti mkubwa kati ya majibu yake na yale yaliyotolewa mwishoni mwa wiki na aliyekuwa Waziri wake.

Swali hilo ambalo awali lilikuwa namba 205, liliulizwa na Devota Minja akitaka kujua Serikali ina mpango gani wa kuboresha makazi ya polisi na askari magereza wanaoishi katika nyumba chakavu zisizokuwa na hadhi ukilinganisha na kazi zao kwa jamii.

Nyakati zote hizo, swali hilo limeulizwa na wabunge tofauti wa Chadema kutokana na Minja kutokuwapo, mara ya kwanza likiulizwa na Suzan Kiwanga (Mlimba) na leo Joseph Selasini wa Jimbo la Rombo.

Tofauti ya majibu ya Kitwanga, Masauni ametoa takwimu katika ujenzi wa nyumba 9,500 za Magereza nchi nzima ambapo amesema  tayari serikali imekwisha ingia mkataba na
Kampuni ya Poly Technologies ya China kujenga nyumba hizo.
 
Mhe. Masauni alibainisha kuwa  kupitia mkataba huo Serikali itapunguza kwa kiasi kikubwa changamoto iliyopo ya uhaba wa nyumba kwa ajili ya askari wa jeshi hilo ambapo mahitaji kwa sasa ni nyumba 14,500 wakati zilizopo ni nyumba 4,221 hivyo kupelekea upungufu wa nyumba 10,279.

“Serikali inafahamu kuwa lipo tatizo la baadhi ya askari wa Jeshi la Magereza na Polisi kuishi katika nyumba chakavu zisizokuwa na hadhi, hivyo katika kukabiliana na tatizo hili Serikali imeendelea kuzifanyia ukarabati mkubwa baadhi ya nyumba na pia kujenga nyumba mpya”. Alisema Masauni.

Mhe. Masauni alifafanua  kuwa mgawanyo wa ujenzi wa nyumba hizo mpya ni Makao Makuu ya Magereza nyumba 472, Arusha nyumba 377, Dar es Salaam nyumba 952, Dodoma 356, Kagera 364, Kigoma 272, Kilimanjaro 390, Lindi 233, Manyara 206, Mara 378, Mbeya 622, Iringa 336, Morogoro 669, Mtwara 215, Mwanza 398, Pwani 384, Rukwa 358, Ruvuma 320, Shinyanga 337, Singida 299, Tabora 408, Tanga 382, KMKGM Dar es Salaam 219, Chuo cha Ukonga 115, Chuo cha Kiwira 183, Chuo cha Ruanda 62, Chuo KPF 27, Bohari Kuu 82 na Bwawani nyumba 84.

Aidha, Mhe. Masauni aliongeza kuwa kwa upande wa Jeshi la Polisi, Serikali inakusudia kujenga nyumba 4,136 katika mikoa 17 ya Tanzania Bara na Zanzibar zitakazosaidia kupunguza tatizo la makazi kwa askari wa jeshi hilo.

Mhe. Masauni alilieleza bunge kuwa Serikali itaendelea kutatua changamoto ya uhaba wa nyumba kwa kutumia njia mbalimbali ikiwemo mikopo yenye riba nafuu, Miradi Shirikishi (PPP) na kwa kutumia fedha za bajeti ya Serikali kadri hali ya uchumi itakavyokuwa inaimarika.

Rais Magufuli Akutana Na Waziri Mkuu, Jaji Mkuu Na Kamishna Mkuu Wa TRA Ikulu Jijini Dar Es Salaam Mei 23,2016

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa aliyefika Ikulu kwa ajili ya mazungumzo na Rais Dkt. Magufuli.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa mara baada ya kumaliza mazungumzo Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Jaji Mkuu wa Tanzania Mohamed Chande Othman Ikulu jijini Dar es Salaam
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Jaji Mkuu wa Tanzania Mohamed Chande Othman mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA, Alphayo Kidata Ikulu jijini Dar es Salaam

Waziri Mkuu Anaondoka Leo Nchini Kuhudhuria Mkutano Wa ADB Zambia Kwa Niaba ya Rais Magufuli

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa anaondoka nchini leo (Jumatatu, Mei 23, 2016) kwenda Lusaka, Zambia kuhudhuria Mkutano wa 51 wa Mwaka wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (51st Annual Meeting of the Board of Governors of the African Development Bank – AfDB) utakaofanyika kesho (Jumanne, Mei  24, 2016).

Waziri Mkuu anahudhuria mkutano huo kwa niaba ya Mheshimiwa Rais, Dk. John Pombe Magufuli.

Mkutano huo ambao utafunguliwa na Rais wa Zambia, Edgar Lungu utajadili masuala ya Nishati na Mabadiliko ya TabiaNchi. 

Pia utahudhuriwa na Marais Idriss Deby wa Chad, Paul Kagame wa Rwanda na Uhuru Kenyatta wa Kenya. Nigeria itawakilishwa na Makamu wake wa Rais, Yemi Osinbajo huku Msumbiji ikiwazilishwa na Waziri wake Mkuu, Carlos Agostinho do Rosário.

Watu maarufu waliothibitisha kuhudhuria mkutano huo ni pamoja na Kofi Annan, Ashish Thakkar, John Kufuor, Mary Robinson, Mo Ibrahim, Nancy Lee, Ngozi Okonjo-Iweala na Tony Elumelu.

Mkutano huo utakaofanyika kwenye kituo cha mikutano cha kimataifa cha Mulungushi (Mulungushi International Conference Centre) utahudhuriwa na washiriki zaidi ya 5,000 kutoka nchi  54 ambao ni wanachama wa benki hiyo, washiriki kutoka nchi 26 ambazo si za bara la Afrika (non-regional member countries), wawakilishi wa mashirika ya kimataifa, wadau wa maendeleo na wawakilishi wa asasi za kiraia. Wengine ni Mawaziri wa fedha, biashara na uchumi na wataalamu kutoka vyuo vikuu.

Waziri Mkuu amefuatana na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Asantu Kijaji, wachumi kadhaa pamoja na wataalamu wa sekta ya fedha.

Rais wa Zanzibar Dr Shein Afanya Uteuzi Wa Wakuu Wa Wilaya Na Mikoa

$
0
0

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dk. Ali Mohamed Shein amefanya uteuzi wa Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya kama ifuatavyo:

1. UTEUZI WA WAKUU WA MIKOA
Kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya Kifungu 61(1) cha Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dk. Ali Mohamed Shein amefanya uteuzi wa Wakuu wa Mikoa kama ifuatavyo:
 
i. Mkuu wa Mkoa wa Mjini na Magharibi – Mheshimiwa Ayoub Mohamed Mahmoud
ii. Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini, Unguja – Mheshimiwa Vuai Mwinyi Mohamed
 
Aidha Wakuu wa Mikoa ambao Mikoa yao haikutajwa katika taarifa hii wanaendelea na dhamana zao kama kawaida.
Uteuzi huo umeanza tarehe 23 Mei 2016.
 
2. UTEUZI WA WAKUU WA WILAYA
Kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya Kifungu 61(2) cha Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dk. Ali Mohamed Shein amefanya uteuzi wa Wakuu wa Wilaya kama ifuatavyo:
 
i. Mkuu wa Wilaya ya Mjini – Mheshimiwa Marina Joel Thomas.
ii. Mkuu wa Wilaya ya Magharibi “B” – Mheshimiwa Silima Haji Haji
iii. Mkuu wa Wilaya ya Kaskazini “A”– Mheshimiwa Hassan Ali Kombo
iv. Mkuu wa Wilaya ya Kaskazini “B” – Mheshimiwa Issa Juma Ali
v. Mkuu wa Wilaya ya Kati – Mheshimiwa Mashavu Sukwa Said
vi. Mkuu wa Wilaya ya Kusini – Mheshimiwa Idrissa Kitwana Mustafa
vii. Mkuu wa Wilaya ya Chakechake – Mheshimiwa Salama Mbarouk Khatib
 
Aidha Wakuu wa Wilaya ambao Wilaya zao hazikutajwa katika taarifa hii wanaendelea na dhamana zao kama kawaida.
 
Uteuzi huo umeanza leo tarehe 23 Mei 2016.
 
Viongozi wote waliotajwa wanatakiwa waripoti Ikulu, Mjini – Unguja, siku ya Jumanne tarehe 24 Mei 2016 saa 8 za mchana tayari kwa kuapishwa.

Rais Magufuli Afanya Uteuzi wa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Mshauri wa Rais Katika Masuala ya Uchumi

$
0
0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Bw. Gerson J. Mdemu kuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Kabla ya Uteuzi huo, Bw. Gerson J. Mdemu alikuwa Karani wa Baraza la Mawaziri (Cabinet Clerk).

Bw. Mdemu anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Dkt. Tulia Ackson ambaye amechuguliwa kuwa Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Wakati huo huo, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Profesa Longinus Rutasitara kuwa Mshauri wa Rais, masuala ya uchumi.

Kabla ya uteuzi huo Profesa Longinus Rutasitara alikuwa Mhadhiri wa Uchumi katika Chuo Kikuu cha Dar es salaam.

Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi leo tarehe 23 Mei, 2016 imeeleza kuwa uteuzi huu unaanza mara moja.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam
23 Mei, 2016

Mwenyekiti Wa Mtaa Wa Babale Uliopo Wilaya Ya Nyamagana Jijini Mwanza Auawa Kwa Kupigwa Risasi Na Watu Wasiofahamika

$
0
0
MWENYEKITI wa Mtaa wa Bulale wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza, Alphonce  Nyinzi  (48) ameuawa kwa kupigwa risasi na watu wasiofahamika wakati akielekea nyumbani kwake.

Akizungumza na waandishi wa habari, Kamanda wa  Polisi Mkoa wa Mwanza, SACP Ahmed Msangi amesema kuwa tukio hilo lilitokea Aprili 22 mwaka  huu majira ya  saa 2 usiku.

Msangi amesema kuwa marehemu aliekuwa akifahamika  kwa jina maarufu "msukuma" mfanyabiashara na mkazi wa bulale aliuawa kwa kupigwa risasi kifuani na kutokea chini ya kwapa upande wa kulia na watu wawili wasio fahamika pamoja na risasi hiyo kumjeruhi  Neema Marangula (23) Mkazi wa Bulale katika Kiganja cha mkono wa kulia.

Amesema kuwa wakati Mwenyekiti huyo akitoka  kwenye kikao alichofanya na wajumbe wa kamati ya Ulinzi na Usalama wa Mtaa wa Bulale akiongozana na wajumbe wawili alikutana na Neema Marangula akiwa na mume wake ambao walikua wanawafuata marehemu na Balozi kwa ajili ya kuzungumzia mzozo wa ndani ya ndoa yao kwa hiyo walikua wanahitaji kusuluhishwa.

Mwenyekiti  huyo (marehemu) na wajumbe wake wawili wakiwa pamoja na Neema pamoja na mumewe wakiwa wanajadili tatizo hilo hapo barabarani mara ghafla wakatokea watu wawili ambao walikua wakipita barabarani na kuwaambia mko chini ya ulinzi na mmoja wao akatoa bunduki na kumpiga risasi mwenyekiti huyo  ambaye alianguka chini huku wenzake wakikimbia kujiokoa kutoka eneo hilo lakini pia wale wahalifu  wakakimbia na kutokomea gizani vichakani.

Amesema wananchi wa eneo hilo  ambapo mwenyekiti aliuawa walijitokeza kwa msaada wa kumsaidia walimchukua na kumkimbiza hospitali kwa matibabu lakini alifariki dunia wakiwa njiani. majeruhi Neema Marangula amelazwa Hospitali ya Mkoa wa Mwanza Sekou Toure kwa matibabu na hali yake inaendelea vizuri.

Mwili wa marehemu  umehifadhiwa katika  Hospitali Mkoa wa Mwanza Sekou Toure kwa ajili ya uchunguzi wa daktari, chanzo cha mauaji hayo bado hakijafahamika pamoja na  uchunguzi tukio hilo bado unaendelea.

Msangi  amewaomba  wananchi wenye taarifa zozote kuhusiana na tukio hilo zitakazo saidia kufanikisha kukamata wahusika wazitoe  polisi lakini pia kutoa ushirikiano kwa viongozi wao na kuhakikisha wanatengeneza makazi salama huko wanapoishi na maeneo ya shughuli zao na  msako mkali unafanyika na kuhakikisha wahusika wa tukio hilo wanakamatwa.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumanne ya May 24

Profesa Anna Tibaijuka kitanzini Tena......Katuhumiwia Kujimilikisha Shamba la Hekari 4,000

$
0
0
Mbunge wa Muleba Kusini, Profesa Anna Tibaijuka na Mkuu wa Wilaya ya Siha, Dk Charles Mlingwa wamelipuliwa bungeni wakidaiwa  kutumia madaraka yao vibaya.

Tuhuma hizo zilitolewa jana na wabunge wa upinzani Conchesta Rwamlaza (Viti Maalum - Chadema) na Dk Godwin Mollel (Siha - Chadema) walipokuwa wakichangia hotuba ya bajeti ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.

Rwamlaza alidai kuwa katika Kijiji cha Kamwila wilayani Muleba, Profesa Tibaijuka akiwa serikalini, aliomba eka 1,098 lakini hivi sasa anamiliki eka 4,000 jambo ambalo linazua mgogoro na wananchi.

“Hili linaleta matatizo kwa kuwa haiwezekani mtu awe na eneo hilo lote halafu anakodisha kwa wananchi,” alisema Rwamlaza.

Alisema kuna haja ya kwenda kupima ardhi hiyo na kama Profesa Tibaijuka aliomba heka 1,098 apewe hizo na si kumiliki eka 4,000 alizonazo hivi sasa.

Dk Mollel alimtaka Waziri Mkuu amhamishe Dk Mlingwa akidai ni tatizo katika wilaya hiyo.

Alisema juzi ulitokea mgogoro kati ya wananchi wa Arumeru na Siha katika mpaka jambo lilisababisha kubomoleana nyumba.

“Mkuu wa Wilaya alifika pale akiwa amelewa na kusababisha wananchi kuchukua hatua hizo wakati ilitakiwa tu tutumie akili,” alisema Dk Mollel.

Dk Mollel alisema kama DC huyo ataendelea kuwa na tabia hiyo, migogoro haitaisha na wawekezaji hawatawaheshimu wananchi kwa kuwa kiongozi wao anawaaibisha.

“Kama hamtamtoa huyu DC ambaye anatuaibisha kwa kuomba vitu vidogovidogo kwa wawekezaji basi sisi tutamtoa kwa kuwa hatuhitaji aibu.”

Alisema kuna haja ya kwenda kupima ardhi hiyo na kama Profesa Tibaijuka aliomba eka 1,098 apewe hizo na si kumiliki eka 4,000 alizo nazo hivi sasa.

Dk Mlingwa ajibu tuhuma
Akizungumzia tuhuma hizo, Dk Mlingwa alisema tangu kipindi cha kampeni, mbunge huyo alikuwa akimshambulia kwa maneno ya uongo ili kupata kura za huruma.

“Hata hii leo (jana) asubuhi alinitumia meseji akisema ooh nakwenda kukushtaki kwa Rais na Waziri Mkuu, akaweka na maneno ya vitisho mimi nikamwambia nenda kwa vile yote ni uongo,” alisema.

“Nadhani kwa sababu ya ahadi za uongo alizokuwa nazo kuwa akichaguliwa yeye mashamba yote ya wawekezaji yaliyoko Siha, yatakuwa mikononi mwa wananchi jambo ambalo haliwezekani.”

Dk Mlingwa alisema wawekezaji hao wana hati za kumiliki mashamba hayo na hilo ndilo ambalo Serikali imekuwa ikiwaeleza wananchi ukweli ili kuepuka propaganda za uongo za mbunge.

“Hiyo ndiyo imemfanya aendelee kumsema vibaya mkuu wa wilaya na mkurugenzi katika kila nafasi anayoipata hata hayo aliyoyasema bungeni ameniambia kwa meseji leo atayasema,” alisema.

“Mkuu wa wilaya kwa bahati nzuri hawezi kujificha tabia na matendo yake kama ningekuwa mlevi wananchi wangeshasema.”

Wabunge wamemshushia ‘zigo’ la migogoro ya ardhi, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi wakimtaka atatue migogoro hiyo kwa kasi ambayo ameanza nayo.

Akichangia hotuba ya bajeti ya wizara hiyo, jana, Mbunge wa Arumeru Mashariki (Chadema), Joshua Nassari alizungumzia mgogoro wa ardhi katika Wilaya ya Arumeru na kusema mgogoro huo umekuwapo tangu mwaka 1993.

Nassari alinukuu tangazo katika gazeti la Serikali na kusema Rais alitangaza kufuta umiliki wa shamba hilo. Hata hivyo, alisema mwekezaji huyo aliendelea kumiliki shamba hilo na kuwakataza wananchi kulima.

“Huyu Mzungu ni nani? Kwa nini anakuwa na nguvu kuliko Serikali? Rais alitangaza kufuta umiliki wa shamba hilo tangu mwaka 1993, lakini mpaka leo anaendelea kumiliki eneo hilo wakati halitumii,” alisema.

Alisema wananchi wanapodai ardhi yao wanafunguliwa kesi za kusingiziwa na kufungwa.

Mbunge wa Viti Maalumu (CCM), Bupe Mwakanata alimtaka waziri Lukuvi kushughulikia mgogoro wa shamba la Efatha, uliodumu kwa muda mrefu bila kutatuliwa.

“Serikali iwasaidie wananchi wake kwa kuwarudishia ardhi yao ambayo haitumiki kikamilifu. Wananchi wa eneo hilo wanategemea kilimo, ukiwanyang’anya ardhi unawasababishia ugumu wa maisha,” alisema.

Mbunge wa Rombo (Chadema), Joseph Selasini alizungumzia mgogoro katika eneo linalozunguka Ziwa Chala. Alisema eneo hilo amepewa mwekezaji ambaye anawazuia wananchi kutumia maji na kusababisha mgogoro kati ya wananchi na mwekezaji na kati ya wananchi na Serikali.

“Ziwa Chala ndiyo pekee ambalo asilimia 85 ya maji yake ni safi na salama na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam wako pale kufanya utafiti. Tunaomba umalize mgogoro huo, ili wananchi watumie ziwa hilo na ardhi kwa ajili ya kilimo,” alisema Selasini.

Mbunge wa Mpanda Vijijini (CCM), Moshi Kakoso alisema Mkoa wa Katavi una migogoro mingi ambayo inasababishwa na mipaka kati ya vijiji hivyo na Hifadhi ya Taifa ya Katavi.

Alisema vijiji vya Kapanga, Lugonesi, Kabage na Nkungwi vinakabiliwa na mgogoro ya ardhi ambayo inawafanya wananchi wa maeneo hayo kushindwa kufanya shughuli za uzalishaji.

“Ninaomba wakati waziri anashughulikia migogoro ya ardhi atuangalie na sisi mikoa ya pembezoni. Tuna migogoro mingi ambayo haijapatiwa ufumbuzi na Serikali haijafanya jitihada zozote,” alisema.

Mbunge wa Morogoro Kusini Mashariki (CCM), Omary Mgumba alisema kumekuwa na mgogoro kati ya Mkoa wa Morogoro na Pwani kwenye vijiji vya mpakani.

Alimtaka Waziri Lukuvi kutembelea eneo hilo ili mgogoro uishe na wananchi wafanye kazi ya uzalishaji.

Mbunge wa Karatu (Chadema), Willy Quambalo alisema kuna mwekezaji katika wilaya hiyo ambaye amepewa ekari 3,850 huku wananchi wakipata shida kwa sababu ameziba njia ambayo inapita katika eneo hilo.

Wakati huo huo, Lukuvi amepiga marufuku watu wote wenye mashamba makubwa ambao wanayapima na kuuza viwanja, waache kwa kuwa haliruhusiwi kuanzia sasa.

“Kama ni shamba litabaki kuwa shamba kama mtu alinunua shamba anataka kubadilisha liwe kiwanja imekula kwake,” alisema Lukuvi na kuongeza kama kuna mtu anataka kufanya hivyo akabidhi shamba kwa halmashauri ili ligawiwe au kuuzwa.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Awasili Lusaka, Zambia, Kwenye Mkutano Wa Benki Ya Maendeleo Ya Afrika

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Naibu Waziri wa Ulinzi wa Zambia, Christopher Mulenga baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Keneth Kaunda uliopo Lusaka Mei 23, may 2016 ambako leo atamwakilisha Rais John Magufuli kwenye mkutano wa Benki ya Maendeleo ya Afrika ADB. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na baadhi ya Watanzania bada ya kuwasili kwenye hoteli ya Intercontinental iliyopo Lusaka baada ya kuwsili Mei 23, 2016 amabako leo atamwakilisha Rais John Magufuli kwenye mkutano wa Benki ya Maendeleo ya Afrika ADB.

Maalim Seif Sharif Hamad Aitwa Polisi Kuhojiwa

$
0
0
Jeshi la Polisi Zanzibar litamhoji Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad Ijumaa ya wiki hii kuhusu masuala mbalimbali ambayo hata hivyo, hayakuwekwa wazi.

Kamishna wa Polisi Zanzibar, Hamdani Makame alisema jana: “Natambua kuwa wasaidizi wangu watazungumza naye Ijumaa. Wao ndiyo wanajua watamhoji nini.”

Alipoulizwa kuhusu mahojiano hayo, Naibu Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Zanzibar, Salum Msangi naye hakuweka wazi badala yake alisema kuna masuala mengi ambayo ofisi yake inahitaji kuyafahamu kutoka kwa Maalim Seif.

Hii ni mara ya kwanza kwa Maalim Seif kuhojiwa na polisi tangu kumalizika kwa Uchaguzi Mkuu ambao kwa Zanzibar ulirejewa Machi 20, baada ya ule wa Oktoba 25 mwaka jana kufutwa.

Maalim Seif ambaye kabla ya uchaguzi huo alikuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, alipinga kurudiwa kwa uchaguzi huo msimamo ambao pia ulichukuliwa na chama chake.

Kiongozi huyo amekuwa akitoa matamko kadhaa ya kuwashawishi wananchi kupinga utawala wa Serikali iliyopo madarakani.

Akiwahutubia wafuasi wake huko Pemba hivi karibuni, Maalim Seif alisema Serikali ya CCM imeanza kutikisika kutokana na vikwazo vinavyoendelea kuwekwa na wahisani pamoja na hatua ya chama chake CUF kutowatambua viongozi wake pamoja na Serikali. 

“CCM wajue wamekalia kuti kavu, siku yoyote wataanguka... tufanye kazi mpaka haki yetu tuhakikishe imerudi na wenzetu hawana safari ya kudumu,” alisema.

Aliwataka wanachama wake kuonyesha kwa vitendo kutoitambua Serikali ikiwamo kukataa kulipishwa kodi za ovyovyo pamoja na kujitenga na viongozi wa Serikali katika utekelezaji wa majukumu yao.

“Mfano tunaweza kuamua siku fulani kuanzia saa sita, tunasimamisha vyombo vyote vya usafiri na siku nyingine tunaamua kupiga honi Zanzibar nzima kuonyesha hatuitaki Serikali ya CCM,” alisema huku akishangiliwa na umati uliofurika katika ofisi za chama hicho.

Mapema jana, Mkurugenzi wa Uchaguzi wa CUF, Shaweji Mketo alisema kuwa amesikia juu ya wito huo lakini hakuwa amepata taarifa rasmi kutoka kwa mkuu wake.

“Nimesikia kama mlivyosikia ninyi,” alisema na kuongeza: “Nimeelezwa pia hata leo Kamishna wa Polisi Zanzibar alikuwa na mahojiano naye.”

Kuhusu hilo Kamishna Makame alisema:“Sijaonana wala kuzungumza naye leo. Hiyo si kweli.”

Juzi, wakati akizindua ripoti ya Uvunjifu wa Haki za Binadamu uliofanyika visiwani humo kipindi cha Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana, Naibu Katibu Mkuu wa CUF Zanzibar, Nassor Ahmed Mazrui alisema wanazo taarifa za Serikali kutaka kuwakamata viongozi waandamizi wa chama hicho na kuwashikilia.

Alisema wamebaini mpango wa kukamatwa kwao na kuwekwa kwenye Mahakama za bara ili kuwanyamazisha Wazanzibari.

Waliokosa Ubunge Walipuliwa Bungeni........Mbunge Adai NHC Imepoteza Mwelekeo

$
0
0
Mbunge wa Korogwe Vijijini, Steven Ngonyani (CCM), maarufu kwa jina la ‘Maji Marefu’ amewalipua wabunge waliokosa ubunge katika kipindi hiki na vilivyopita kwa kuhodhi nyumba za Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) mjini Dodoma na kupangisha watu wengine kinyume cha utaratibu wa shirika hilo.

Alisema hali hiyo imefanya wabunge wapya, ambao ni asilimia 70 ya wabunge wote kwa sasa, kukaa nyumba za kulala wageni wakati zipo nyumba hizo kwa wabunge kulingana na mkataba na NHC.

Mbunge alisema wapo watu wamepangishwa na wabunge hao wa zamani, ambao wamegeuza nyumba hizo kama kitega uchumi kinyume na taratibu. 

Ngonyani alisema hayo bungeni mjini hapa jana wakati akichangia mjadala wa Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa mwaka wa fedha 2016/17.

Alimuomba Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi, kufuatilia suala hilo na shirika kwa ujumla, aondoe wapangaji hao waliowapangishia wengine kinyume cha utaratibu na kuwapatia nyumba wabunge wapya ambao hawana nyumba za kuishi.

Alisema wabunge hao waliokosa nafasi ya kurudi jimboni miaka tofauti, mkataba wao wa kupangishwa nyumba hizo umekwisha, kwani ukishakosa ubunge hauna dhamana tena mpaka utakaporudi.

“ Kuna wapangaji wengi ambao ni wabunge waliokosa nafasi hiyo ambao wamepangishwa na shirika na badala yake hadi leo wamezishikilia nyumba hizo hawataki kuziachia, ”alisema Ngonyani.

Alieleza kuwa baada ya kukosa nafasi za ubunge na kushindwa kurudi bungeni, wabunge hao walipaswa kurejesha nyumba hizo kwa shirika, ambalo ndilo lenye mamlaka ya kupangisha na si wao kupangisha wapangaji wengine kupitia mikataba yao.

Hata hivyo, taarifa kutoka NHC, Dar es Salaam jana kuhusu nyumba hizo zilifafanua kuwa hazikutengwa kwa ajili ya wabunge pekee, bali hata watu wa kawaida na kila mtu anaingia mkataba binafsi na shirika.

Pia zilieleza kuwa, nyumba hizo zilikodishwa awali kutokana na mahitaji ya wabunge uliokuwapo na wapo walionunua, hivyo wana dhamana nazo. 

Aidha ilieleza kuwa ikiwa kuna mpangaji aliyepangisha mtu mwingine bila kujali alikuwa mbunge au la, anakwenda kinyume cha utaratibu, watafuatilia suala hilo.

Katika hatua nyingine, Ngonyani alisema bungeni kuwa NHC imebadilisha dhana na kutoka kwenye kujenga nyumba za bei nafuu, kusaidia wananchi wenye uwezo mdogo sasa inafanya biashara, kwani inajiendesha kibiashara na si kwa lengo la kuundwa kwake.

Mbunge wa Kinondoni, Maulid Mtulya (CUF) alisema nyumba za shirika hilo zimejengwa kwa ajili ya mabepari kwa sababu wananchi wa kawaida kutozimudu kutokana na bei zake za kati ya Sh milioni 40 hadi milioni 60.

Mbunge wa Mpanda Vijijini, Moshi Kakoso (CCM) alitaka shirika lijenge nyumba kulingana na uwezo wa watu wa eneo husika kutokana na kuwa wanajenga nyumba za gharama kubwa. 

Alisema ujenzi huo uzingatie katika miji inayokua kuiweka katika mandhari nzuri na wakazi wa maeneo husika kumudu kupanga na kununua.

Madiwani wa Misungwi Watoa Tamko Zito Kuhusu Kutumbuliwa kwa Mbunge Wao Charles Kitwanga...........Wanataka Bunge Limuombe Radhi

$
0
0
UTANGULIZI
Ndugu Waandishi wa habari, Karibuni kwenye mkutano huu mfupi ambao lengo lake ni kutoa taarifa yetu fupi kuhusu ukweli uliojificha kuhusu kitendo kilichopelekea Mh. Rais Dk. John Pombe Magufuli kutengua uteuzi wa Waziri wa Mambo ya Ndani, Charles Kitwanga.

Tunaamini kwa uwezo mliona kama waandishi wa habari, taarifa hii itafikia umma wa Watanzania kama ilivyokusudiwa.

UFAFANUZI
Kama mnakumbuka mnamo tarehe 20 Mei mwaka huu, Rais Dk John Pombe Magufuli alichukuwa uamuzi wa kutengua uteuzi wa Waziri wa Mambo ya Ndani, Charles Kitwanga ambaye pia ni Mbunge wa Misungwi kwa kosa la kwamba Mhe. Kitwanga aliingia bungeni akiwa amelewa.

Sisi wananchi wa Jimbo la Misungwi tumesikitishwa sana na taarifa na uamuzi huu kwa kuwa tunaamini kuwa kuna dhamira iliyojifika iliyopelekea Mhe Rais kufanya maamuzi haya. 

Ukweli ni kwamba huu ulikuwa mpango wenye dhamira ovu na uliogubikwa na uongo mwingi ukilenga kumchonganisha Mbunge wetu na Mhe. Raisi uliopangwa na waovu wachache ambao wamebanwa na Serikali hii ya Awamu ya tano kupitia wizara hiyo nyeti kwa usalama wa nchi.
 
Itakumbukwa kuwa, Mhe Charles kitwanga alinadiwa na Mhe Rais na wanaCCM na baadae kupigiwa kura kwa wingi na wananchi wa Misungwi kwa ajili ya uwezo wake na dhamira yake njema ya kulinda taifa letu. 

Sisi wananchi wake, tunaamini katika uwexo wake, uadilifu wake na nidhamu ya kazi aliyonayo, hatuna mashaka na hili.

Baada ya kuteuliwa na Mhe Raisi kama Waziri wa mambo ya ndani, amekuwa muadilifu na kafanya mengi katika kuimarisha usalama na kufanya maamuzi yengi mazuri kwa maslahi ya taifa. 

Hili lilimtengenezea maadui wengi ndani ya serikali, ndani na nje ya CCM, mtandao wa dawa za kulevya, walioachishwa kazi NIDA na Uhamiaji. 

Watu hawa ndio waliochochea na kutengeneza mkakati wa kumchafua Mhe Kitwanga na walikuja dodoma kuhakikisha dhamira yao ovu inatimia.

USHAHIDI WETU
Miongoni mwetu tulikuwa mjini Dodoma pamoja na madiwani wa Jimbo la Misungwi ambao tulikwenda kumtembelea Mbunge wetu bungeni, tulizungumza mengi kwa ajili ya jimbo letu na katika kikao chetu hapakuwa na chembe ya kilevi chochote na hata kesho yake alipoinga bungeni alikuwa mzima wa afya ya kimwili na akili timamu na tunawahakikishieni kuwa Kitwanga hakuwa amelewa.

Ndugu waandishi wa habari asubuhi ya tarehe 20 tulielekea bungeni kwa mwaliko wa Charles Kitwanga, tukiwa sehemu ya mualiko uliowajumuisha Madiwani wa jimbo lake tukiwa tumeambatana naye tukaingia ndani ya ukumbi wa bunge,tukashuhudia anajibu swali,baada ya kujibu swali la mbunge Sakaya,tulitoka nje na kupiga picha na madiwani wote wa Misungwi waliokuja kumtembelea Dodoma.

Baada ya zoezi la kupiga picha kukamilika pale nje ya ukumbi wa Bunge, tulitoka na kuelekea Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) kwa lengo la kututembeza maeneo yote ya Dodoma , lakini ilipofika jioni wakati tukirejea nyumbani tukiwa naye, ghafla tukaona habari zikisambazwa kwenye mitandao ya kijamii kuwa Waziri Kitwanga amevuliwa uongozi kwa kuwa alionekana na Waziri Mkuu akiwa amelewa.

Ndugu wanahabari , tulishangazwa wote kwani tulikuwa tumekaa naye pale nyumbani kwake Dodoma (site 2) tukipata chakula cha usiku ,alionekana kutoaamini na hata madiwani pia na wengine ambao tulikuwepo hapa nyumbani kwake hatukuamini.

Tunachosema ni kwamba waziri Kitwanga hakulewa kama ambavyo imepotoshwa, bali ulikuwa ni mkakati wa kumchafua na kuhakikisha anavuliwa wadhifa wake ili watu hawa waendelee kufanya maovu yao. 

Mtandao wa dawa za kulevya, pamoja na wale waliokuwa wanamshutumu kwamba amehusika kuondolewa kwao kazini wakiwemo Watu wa NIDA, Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete, Mfanyabiashara Said Lugumi pamoja na kundi mafisadi waliokwapua mabilioni ya fedha NSSF. 

Pia na baadhi ya wabunge wa CCM na Upinzani ambao walikuwa hawafurahishwi na kasi ya utendaji kazi wa Kitwanga katika Wizara ya Mambo ya ndani.

Kwa niaba ya wananchi wenzetu tunamuomba na kumtahadharisha Mhe. Rais awe makini na makundi la wafanyabiashara wa madawa ya kulevya, pamoja na lile kundi la wanamtandao masalia ndani ya CCM na serikalini na kwenye vyombo nyeti vya ulinzi na usalama, ambayo kwa ujumla yalikuwa na mkakati kabambe wa kuhakikisha wanamtenganisha na kumpotosha Mhe Raisin a kumjaza habari zisizo za kweli.

Ndugu waandishi wa habari, kilichotushangaza zaidi baada tu ya Kitwanga kuvuliwa madaraka yake ya uwaziri, kuna watu walianza kufanya sherehe wakishangilia hususani wale waliovuliwa madaraka NIDA pamoja na NSSF,Uhamiaji na wale wanaotuhumiwa kuhusika na madawa ya kulevya.

Ndugu waandishi wa habari, tunajua namna kundi la Said Lugumi, Ridhiwani Kikwete na kampuni yao walivyokuwa wanadhamini kwa mbinu za kifedha katika vita hii ya kitwanga ili aondolewe, lakini baada ya kuondolewa, wakajifanya kutoa taarifa ya kushangazwa kuondolewa kwake,

Kitwanga amekuwa mtumishi wa serikali akiwa mtumishi mwandamizi benki kuu Tanzania (BOT),amekuwa mbunge na Naibu waziri kwa miaka 10,lakini hata siku moja hakuwahi kuonekana amelewa. Ni muadilifu na ana nidhamu ya kazi, na nidhamu hii ndiyo iliyomfanya aaminiwe na kupewa dhamana hii.

MAAZIMIO YETU
=Tunaliomba Bunge kumuomba radhi Mhe. Charles Kitwanga kwa kumdharirisha mbele ya wapiga kura wake wa Jimbo la Misungwi familia yake pamoja na watanzania wote waliokuwa wanaamini utendaji wake kupitia video iliyochezewa na wataalamu wa IT katika studio za Bunge ili kufanikisha lengo la kumuonyesha Kitwanga kuwa alikuwa amelewa bungeni.

=Tunamuomba Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ambaye ndiye Kiongozi Mkuu wa Serikali bungeni atoe uthibitisho wa kikemia unaotanabaisha wazi kama Kitwanga alikuwa katumia kilevi wakati akiwa bungeni maana hakuna kipimo chochote kilichofanyika kudhibitisha uvumi huu.

=Tunaliomba Bunge lifanye uchunguzi na kubaini wale wote waliosambaza ile video inayoonyesha Kitwanga akiwa anaongea na kuonekana amelewa wakati kiuhalisia hakulewa na alijibu maswali yote vizuri

=Tunaliomba Bunge kuchunguza idara ya habari ya Bunge pamoja na studio ile ya Bunge ambao wamehusika na kuhariri ile picha ya video iliyokuwa inasambazwa kwenye mitandao ya kijamii.

=Tunahoji uhalali wa kumvua mtu madaraka kwa sababu ya ulevi bila uthibitisho wa daktari ambaye kisheria ndiye mwenye mamlaka hayo kugundua kilevi cha mtu.

= Tunaomba Watanzania wote waliosikitishwa na taarifa hizi wajue tu kwamba ile video ambayo imemtia hatiani Kitwanga ilihaririwa kwa ustadi mkubwa kupitia wafanyakazi wa Bunge ambao wanapitia zile asadi za bunge pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa serikali kwenye vyombo vya ulinzi na usalama ambao hawakupenda kitwanga aendelee kuwa pale ,kwa nia ya kumhujumu na sasa wanasema kwenye vyombo vya habari ili kuhalalisha uhujumu huo.

=Tunaomba mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA) kuangalia picha zinazosambazwa kwenye mitandao ya kijamii dhidi ya Mhe Mbunge wa Misungwi ambazo zinaonekana kumchafua wachukue hatua dhidi ya watu hao kwani kisiasa zinaendelea kumchafua na kumharibia kwa wapigakura wake,familia yake,mama yake mzazi ,ndugu zake .

=Tunajiandaa kuchukua hatua kwa Bunge za kisheria kama watashindwa kuthibitisha tuhuma hizo dhidi ya Charles Kitwanga ambazo tunaamini zimetengenezwa kwa maslahi ya makundi yanayompinga ndani ya Serikali wakiwemo mtandao wa dawa za kulevya.

Pia tunamuomba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa makini kundi la wanamtandao walio ndani ya serikali ambalo linaongozwa wahafidhina wasio taka mabadiliko ndani ya serikali .

Imeandaliwa na madiwani wa Jimbo la Misungwi pamoja na wakereketwa wa jimbo hilo.Baraka Kingamkono,Gaudency Tungaraza na IDDY Majumuisho.

Asanteni na Mungu awabariki

Nape Nnauye Ashindwa Kuhutubia Kwenye Tamasha la Muziki Jijini Mwanza Kutokana na Zomeazomea Ya Wananchi Wanaotaka Bunge Lionyeshwe Live

$
0
0
Mzimu wa kuzuia shughuli za Bunge kuonyeshwa moja kwa moja na vituo vya televisheni uliopachikwa jina la ‘Bunge Live’, umeendelea kumwandama Waziri wa Habari, Nape Nnauye baada ya juzi kupokewa kwa kelele kiasi cha kushindwa kuhutubia wapenzi wa muziki jijini Mwanza.

Nape alitangaza uamuzi wa kusitisha kurusha moja kwa moja baadhi ya shughuli za Bunge, akisema Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) linashindwa kumudu gharama, lakini wabunge, hasa kutoka vyama vya upinzani wamepinga hatua hiyo wakisema inawanyima wananchi haki yao ya kikatiba ya kupata habari kuhusu chombo chao cha kutunga sheria.

Lakini Serikali imeshikilia msimamo wake, ikitoa sababu tofauti na kwenda mbali zaidi kuzuia vituo binafsi vya televisheni kurusha matangazo, huku TBC1 ikirusha kipindi cha maswali na majibu pekee ikielezwa kuwa huo ni uamuzi uliopitishwa katika Bunge la 10.

Juzi, Nape aliyekuwa mgeni rasmi katika tamasha la Jembeka Festival lililofanyika kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, alipokewa na kelele za maneno “Bunge Live” wakati akikaribishwa kuhutubia mamia ya wapenzi wa burudani waliohudhuria tamasha hilo, ambalo lilijumuisha wasanii nyota kama Shaffer Chimere Smith a.k.a Ne-Yo kutoka Marekani na Diamond Platnum.

Baada ya mkurugenzi wa kampuni ya Jembe ni Jembe, Sebastian Ndege kumkaribisha waziri huyo kuzungumza na wananchi hao, Nape alisimama lakini akapokewa kwa kelele.

“Bunge live, Bunge live, Bunge live,” walipiga kelele mashabiki waliohudhuria tamasha hilo.

Kelele za “Bunge Live” zilisababisha Waziri Nape kushindwa kuhutubia na kulazimika kuketi chini na Mbunge wa Nyamagana, Stanslaus Mabula alisimama kujaribu kuokoa jahazi, lakini naye akakumbana na kimbunga cha sauti za wananchi walioamua kulitaja jina la mbunge wa zamani wa jimbo hilo, Ezekia Wenje.

“Wenje, Wenje, Wenje,” wananchi hao waliimba kwa sauti wakati Mabula akijaribu kuwatuliza ili Nape ahutubie.

Akizungumzia tukio hilo, Nape alisema wananchi waliompigia kelele za “Bunge Live” walisukumwa na masuala ya kisiasa, ndiyo maana aliepuka kuendelea kuzungumza ili kutochafua hali ya hewa uwanjani.

“Pale uwanjani tulikwenda kwa ajili ya burudani, sasa baada ya kuona wananchi wanaanza kuleta masuala ya kisiasa nikaona ni busara kuacha kuhutubia. kuepusha shari,” alisema Nape.

Pamoja na Nape, tamasha hilo pia lilihudhuriwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira na Muungano), January Makamba, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella na Mabula.

Ukiachilia mbali dosari hizo, tamasha hilo lilikonga nyoyo za wapenzi wa sanaa ya muziki waliokesha uwanjani hapo hadi saa 11:00 alfajiri wakiburudishwa na wasanii nguli.

Wasanii wengine waliopata nafasi ya kutumbuiza ni Juma Nature, Ney wa Mitego, Ruby na Fid Q.

CUF Waitupia Lawama Serikali kwa Kushindwa Kuwajibika na Kuruhusu Uingizwaji wa Simu FEKI

$
0
0

Jumuiya ya Vijana CUF (JUVICUF) imeitaka Serikali kubeba mzigo wa kushindwa kuwajibika ipasavyo kwa kuruhusu uingizwaji wa simu feki nchini.

Kauli ya jumuiya hiyo imekuja wakati imebaki mwezi mmoja kwa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), kuzima simu feki zote.

Akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam jana, Katibu Mtendaji wa JUVICUF, Mahamoud Mahinda Ally alisema Serikali ilishindwa kutimiza wajibu wake wa kuhakikisha simu hizo haziingizwi nchini, hivyo inapaswa kuwajibika.

Ally alisema Serikali ilipaswa kuziba mianya hiyo tangu mwanzo na kwamba inachofanya sasa ni kukosa huruma kwa watu wake.

Alisema kitendo cha wananchi kuachwa wakinunua simu feki siku za nyuma bila ya kudhibiti uingizwaji wake nchini ni kutozingatia matakwa ya haki za binadamu.

“Kuruhusu simu feki ziingie nchini, kisha kuzizima ni mapambano ambayo Serikali inapambana dhidi ya wananchi wake,” alisema Ally.

Akizungumzia kuhusu hilo, Meneja Mawasiliano wa TCRA, Innocent Mungy alisema mamlaka hiyo ilianza kutoa elimu kuhusu ya matumizi ya simu feki tangu mwaka 2010.

Alisema bado TCRA inaendelea na kampeni hiyo kwa wananchi juu ya madhara ya matumizi ya simu feki. Pia, alisema TCRA iliamua kufanya hivyo kutokana na majangili wanaotumia njia za panya kupitisha simu hizo na bila kulipa kodi.

Alisema wafanyabishara hao wasio waaminifu ndiyo wamechangia kuwapo kwa uingizaji wa simu feki nchini, licha ya Serikali kupiga marufuku.

Mungy alisema kutokana na wimbi la uingizwaji wa simu feki kuwa kubwa, waliamua kutumia teknolojia ya kuzima simu feki, ambayo itatumika kuanzia mwezi ujao ili kuwaepusha wananchi na bidhaa hizo kama zinazofanya nchi mbalimbali duniani.

Katibu Mtendaji wa Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano Tanzania (TCRA-CCC), Mary Msuya alisema simu feki kuingizwa nchini ni tatizo la wafanyabiashara wasio waaminifu.

Alisema kuna baadhi ya wafanyabiashara wanaotumia njia za panya kuingiza bidhaa feki nchini. “Siyo simu tu hata bidhaa nyingine.”

Alisema ofisi yake ambayo ni washauri wa watumiaji wa huduma za mawasiliano nchini, imekuwa ikitoa elimu kwa wananchi kuhusu simu feki.

Alisema wananchi wamekuwa wishauriwa kuhakikisha kuwa wananunua simu katika maduka ya simu na wahakikishe wanapewa risiti ya dhamana ya muda wa matumizi ya bidhaa usiopungua miezi 12.

“Mteja asiponunua bidhaa feki hata mfanyabaishara atakosa soko,” alisema.Aliwataka wananchi kuzingatia mafunzo wanayopewa.

Mhifadhi Mwandamizi wa TANAPA, Genes Shayo anashikiliwa na Kikosi cha kupambana na ujangili kwa tuhuma za kujihusisha na ujangili.

$
0
0


Vita dhidi ya ujangili inazidi kushika kasi baada ya kikosi kazi maalumu cha kupambana na ujangili kumnasa Mhifadhi Mwandamizi wa Shirika la Hifadhi za Taifa (Tanapa) kwa tuhuma za ujangili.

Pia, kikosi hicho kimemtia mbaroni Mchungaji wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG), wilayani Arumeru kwa tuhuma za kukutwa na jino la tembo wakati akisaka mnunuzi.

Waziri wa Utalii na Maliasili, Profesa Jumanne Maghembe alisema jana kuwa vyombo vya ulinzi na usalama vimeongeza kasi ya kupambana na majangili katika mapori yote ya akiba.

Meneja Uhusiano wa Tanapa, Paschal Shelutete katika taarifa yake jana alisema kuwa Mei 14, mwaka huu, shirika hilo lilipokea taarifa za siri kuwa mchungaji huyo alikuwa akimiliki jino hilo.

“Tuliambiwa mchungaji huyo alikuwa akihitaji mtu wa kufanya naye biashara. Baada ya kupata taarifa tuliwasiliana na kikosi kazi maalumu cha kitaifa ili wafuatilie,” alisema Shelutete.

Shelutete alidai kuwa Mei 15, mchungaji huyo alikamatwa na kumtaja ofisa wa Tanapa kuwa ni mmoja wa washirika wake katika biashara hiyo.

“Alipokamatwa na kuhojiwa alimtaja mhifadhi huyo kuwa anataarifa za yeye kuwa na jino hilo ndipo Mei 16 naye alikamatwa,” alisema Shelutete.

Tanapa imewaomba raia wema kuendelea kufichua vitendo vya ujangili na haitasita kuchukua hatua dhidi ya watumishi wake watakaobainika kujihusisha na ujangili.

Mwishoni mwa wiki iliyopita, Waziri Maghembe alisema majangili sasa wamehamishia ujangili wao katika mapori ya akiba baada ya kudhibitiwa kwa kiasi kikubwa katika Hifadhi.

Profesa Maghembe alionya kuwa hakuna jangili hata mmoja ambaye atasalimika katika msako unaoendelea na kwamba, salama yao ni kujisalimisha pamoja na silaha zao.

Kukamatwa kwa ofisa huyo mwandamizi wa Tanapa kumekuja miezi michache baada ya kufikishwa mahakamani kwa Mkuu wa Kitengo cha Intelijensia cha Mamlaka ya Ngorongoro kwa tuhuma za ujangili. 

Mtuhumiwa huyo, Iddy Mashaka (49), anadaiwa kuwa Januari 6 na Februari Mosi wilayani Meatu alimshauri mshtakiwa namba mbili, Shija Mjika (38) kuua wanyama wasioruhusiwa.

Watuhumiwa wengine ambao wanashitakiwa pamoja na Mkuu huyo wa Kitengo cha Intelijensia, wao wameshitakiwa kwa kutungua helkopta na kumuua rubani wake, Rogers Gower huko Maswi.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images