Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Haya Hapa Majina Ya Kambi Zote 11 Ya Wanafunzi Kidato Cha 6 Waliopangiwa JKT 2016


Zitto Kabwe kuisaliti kambi ya ukapera...Amchumbia mrembo huyu

$
0
0
Kambi maarufu mjini ya Ukapera inatarajia kupata pigo la mwaka pale member wake mahiri na wa muda mrefu, mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe atakapoigika kibuti rasmi.

Zitto amemchumbia msichana mrembo anayetarajia kumbadilisha jina soon kuwa ‘Mrs Kabwe.’

Picha za mbumbe huyo akimvisha pete msichana huyo mbele ya ndugu na jamaa zimesambaa mtandaoni wiki hii.

Kuna picha moja inayoonesha kuwa ni post ya Instagram aliyoiweka Zitto ambapo aliandika: So Beautifu and full of love. I love you.

Kabla ya kufutwa post hiyo ilikuwa imefikisha comments 216 na likes 3,257. 

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatano ya May 25

Mkoa wa Mwanza Unategemea Kupokea Tani 500 za Sukari

$
0
0

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella, amesema mkoa wa Mwanza unategemea kupokea Tani 500 za Sukari zitakazo ingia katika mkoa huu zikitokea kiwanda cha sukari cha Kagera Sugar tarehe 24, Mei, 2016, ambazo zinaingizwa mkoani hapo na muagizaji na Msambazaji P.H  Shah.

Hata hivyo mkuu wa mkoa ameonya watu watakao uza sukari hiyo kinyume na bei elekezi kuchukuliwa hatua za kisheria ikiwa ni pamoja nakufikishwa katika vyombo vya dola.

Mongella amesema pia kwamba, kupitia kamati yakushughulikia sukari, tayari wametoa maelekezo kwa Wakuu wa wilaya jinsi yakushughulikia suala la sukari na kwamba wasambazaji wote katika Wilaya lazima wazingatie maelekezo bila kuvunja utaratibu utakao wekwa.

Mahitaji ya sukari katika mkoa wa Mwanza ni Tani 1,500 kwa wiki kwa matumizi ya kawaida kwa wananchi wake, hivyo kuwasili kwa tani 500 itasaidia kupunguza uhaba wa sukari  unao ukabili  mkoa huu kwa sasa..

Hata hivyo mkuu wa mkoa amewatoa wanachi hofu juu ya sukari kwakusema, tayari viwanda vya hapa nchini vimekwisha anza uzalishaji wa sukari na kwamba muda si mrefu tatizo la sukari litapungua kama sio kuisha kabisa.

Imetolewa na Atley J. Kuni
Afisa habari na Mahusiano, Ofisi ya mkuu wa Mkoa
MWANZA -24, Mei 2016

Waziri Mkuu: Serikali Kuiuzia Umeme Zambia

$
0
0

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Tanzania ina mpango wa kujenga njia ya umeme kutoka Mbeya hadi Zambia kupitia Tunduma ili kupunguza tatizo la umeme linaloikabili nchi hiyo.

“Serikali ya Tanzania inajenga njia ya umeme ya msongo wa KV 400 kutoka Iringa – Dodoma – Singida – Shinyanga ambayo ni sehemu ya mradi mkubwa wa umeme unaolenga kuunganisha Zambia, Tanzania na Kenya,” amesema.

Amesema  upembuzi yakinifu kwa ajili KV400 kutoka Iringa hadi Mbeya umekwishakamilika tangu mwaka 2012, na hivi sasa Serikali inatafuta fedha kwa ajili kuunganisha kipande cha kutoka Mbeya na gridi ya Taifa ya Zambia.

Waziri Mkuu ambaye anahudhuria mkutano huo kwa niaba ya Mheshimiwa Rais, Dk. John Pombe Magufuli, ametoa ufafanuzi huo jana mchana (Jumanne, Mei 24, 2016) wakati akichangia hoja kwenye mjadala wa wakuu wa nchi na Serikali uliohusu Nishati na Mabadiliko ya TabiaNchi kwenye ukumbi wa mikutano cha kimataifa wa Mulungushi.

Alisema ili kukabiliana na changamoto ya nishati barani Afrika, nchi za bara hili zinahitaji kuwa na fedha ama mitaji, teknolojia ya kisasa na wataalamu wenye ujuzi wa kutosha jambo ambalo amesema ni gumu kulikamilisha kila nchi peke yake.

Alisema ili kukaribisha wawekezaji kwenye sekta ya umeme, Tanzania inafanyia marekebisho sheria zake ili kuruhusu uwekezaji kwenye sekta hiyo.

Akizungumzia kuhusu hali ya nishati Tanzania, Waziri Mkuu alisema Tanzania imebarikiwa kuwa na gesi asilia yenye ujazo wa futi trilioni 57.25 (tcf), makaa ya mawe yenye uhjazo wa tani bilioni 1.9 (asilimia 25 imevumbuliwa), umeme wa nguvu ya maji wa gigawati 4.7 ambazo ni asilimia 12 tu ndiyo inatumika. Pia alisema Tanzania ina deposits za urani yenye ujazo wa ratili milioni 200 (200 million pounds), joto la ardhini (geothermal) linaloweza kuzalisha umeme wa megawati zaidi ya 5,000. “Hivyo ni mbali na vyanzo vya umeme utokanao ua upepo na jua,” alisema.

Akizungumzia kuhusu usambazaji wa umeme vijijini, Waziri Mkuu alisema Tanzania kupitia REA imefanikiwa kusambaza umeme kwenye asilimia 52 ya vijiji vyote na inatarajia kufikia asilimia 90 ifikapo mwaka 2025.

Akishiriki mjadala huo, Makamu wa Rais wa Nigeria, Bw. Yemi Osinbajo alisema bara la Afrika linahitaji kuwa na vyanzo vikubwa vya umeme kama kweli linataka kufanikiwa kukamilisha kuwa na viwanda vya kutosha.

“Hatuwezi kuwaza kuwa na viwanda vingi wakati tukitegemea umeme wa nguvu ya jua peke yake… huu unahitaji uwekezaji mkubwa na eneo kubwa la kuweka mitambo,” alisema.

Naye Waziri Mkuu wa Msumbiji, Bw. Carlos Agostinho do Rosário

Akishiriki mjadala huo, Makamu wa Rais wa Nigeria, Bw. Yemi Osinbajo alisema bara la Afrika linahitaji kuwa na vyanzo vikubwa vya umeme kama kweli linataka kufanikiwa kukamilisha kuwa na viwanda vya kutosha.

“Hatuwezi kuwaza kuwa na viwanda vingi wakati tukitegemea umeme wa nguvu ya jua peke yake… huu unahitaji uwekezaji mkubwa na eneo kubwa la kuweka mitambo,” alisema.

Naye Waziri Mkuu wa Msumbiji, Bw. Carlos Agostinho do Rosário alisema masuala ya nishati yanahitaji uwekezaji mkubwa kwa hiyo akashauri makampuni kuungana kwenye uwekezaji na kuibua miradi ambayo ina tija (feasible and viable).

Waziri Mkuu amefuatana na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Asantu Kijaji, wachumi kadhaa pamoja na wataalamu wa sekta ya fedha.

14 Wakamatwa Mauaji ya watu Watatu Msikitini Jijini Mwanza

$
0
0

Jeshi la Polisi Nchini linawashikilia watuhumiwa 14 kufuatia tukio la mauaji ya watu watatu lililotokea katika msikiti wa Rahman eneo la Ibanda relini mkaoni Mwanza, Mei 18 mwaka huu.

Akiongea na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini Kamishna Msaidizi Advera Bulimba alisema kuwa msako wa kuwakamata watuhumiwa wengine unaendelea katika maeneo mbalimbali nchini.

Hivyo amewaomba wananchi kutoa ushirikiano mkubwa kwa jeshi hilo ili kufanikisha kuwakamata wale wote wanaotuhumiwa kuhusika na tukio hilo.

“Nitoe wito kwa wananchi kushirikiana kikamilifu na vyombo vya usalama katika kufichua wahalifu kwa kuwa ni watu tunaoishi nao, hivyo hakuna budi kutoa taarifa zao ili usalama na mali zetu uendelee kuimarika”, aliongeza Kamishna Msaidizi Bulimba.

Hata hivyo, alieleza kuwa hali ya usalama nchini iko shwari na kuwatoa hofu wananchi kwamba jeshi hilo limejipanga kikamilifu katika kuhakikisha hali ya usalama inaendelea kuwepo.

“Niwaombe wananchi kuondoa hofu juu ya hali ya usalama na wasiwasi na watoe ushirikiano kwa vyombo vya dola ili kuhakikisha kwamba wote wanaojihusisha na uhalifu wanakamatwa haraka”, alisema Kamishna Msaidizi  Bulimba.

Aliongeza kuwa uchunguzi zaidi wa matukio ya uhalifu nchini unaendelea ikiwemo matukio ya mkoani Tanga, Dar es Salaam na mikoa mingine ili kubaini na kuwakamata wahusika na kufikishwa katika vyombo vya sheria.

Hivi karibuni kumeripotia matukio mbalimbali ya uvunjifu wa amani katika mikoa mbalimbali  ikiwemo mauaji ya watu watatu waliouawa wakiwa msikitini jijini Mwanza.

Wamiliki wa silaha watakiwa kuhakiki silaha zao kabla ya Juni 30

$
0
0

Jeshi la Polisi nchini limetoa wito kwa wamiliki wa silahi  kujitokeza na kuhakiki silaha zao katika Wilaya wanazoishi kabla ya kumalizika kwa zoezi hilo mnamo Juni 30 mwaka huu.

Hayo yalisemwa na Msemaji wa Jeshi hilo Kamishna Msaidizi Advera Bulimba alipokuwa  akiongea na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam.

“Serikali imetoa muda wa miezi mitatu kukamilisha zoezi hili muhimu na tayari miezi miwili imepita hivyo wale ambao bado hawajahakiki silaha zao kuzikakiki sasa kabla ya Juni 30 ili kuepukana na usumbufu” alisema Kamshna Msaidizi Bulimba na kuongeza kuwa:

“Natoa wito kwa watu wote wanaomiliki silaha kinyume na sheria kusalimisha silaha hizo katika vituo vya polisi, ofisi za serikali na kwenye nyumba za ibada  na watakaofanya hivyo ndani ya muda ulipangwa hawatachukuliwa hatua zozote za kisheria”.

Aliongeza kuwa baada ya muda ulipangwa na Serikali kupita na wamiliki hawajahakiki silaha zao Jeshi la Polisi  nchini litaendesha operesheni kali kuwakamata  wale ambao hawakujitokeza katika zoezi la uhakiki na hatua kali zitachukuliwa ikiwemo kufutiwa leseni na silaha zao kutaifishwa na kuwa mali ya Serikali.

Aliwaomba ndugu wa wale walikuwa wakimiliki silaha ambao wamefariki au ni wagonjwa wasalimishe silaha hizo katika vituo vya Polisi kwa niaba ya ndugu zao ndani ya kipindi cha uhakiki wa silaha.

Zoezi la uhakiki wa silaha lilianza Machi 21 mwaka huu kufuatana na sheria ya usimamizi wa silaha na risasi ya mwaka 2015, ambapo kifungu cha 66 cha sheria hiyo kinamtaka kila mmiliki kuhakiki kumbukumbu za silaha yake au risasi  pale anapoamriwa na mamlaka.

Lengo la kuhakiki kumbukumbu za wamiliki wa silaha ni kupata taarifa sahihi za wamiliki hao zitakazosaidia kubaini wale wote wanaomiliki kinyume na sheria, kuwafahamu wamiliki waliohama na kuhamia makazi mapya, kuwafahamu wamiliki waliofariki ili kuzuia vitendo vya uhalifu na uvunjwaji wa amani nchini.

CBE Yatolea Ufafanuzi dhidi ya Tuhuma za Ufisadi chuoni Hapo.

$
0
0

CHUO cha Elimu ya Biashara (CBE) kimetoa ufafanuzi kuhusu tuhuma za ufisadi zilizotolewa dhidi yake na kudai si za kweli, zinalenga kuharibu sifa za chuo hicho pamoja na uongozi wake.

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam Mkuu wa chuo hicho, Profesa Emanuel Mjema alisema kimembaini mfanyakazi wake anayedaiwa kutoa taarifa hizo katika vyombo vya habari na ametakiwa kujieleza huku taratibu nyingine zikifuatia.

Mjema alisema chuo kimesikitishwa na habari hizo zilizochapishwa na magazeti mawili ya kila siku , zikidai upo ufisadi mkubwa katika chuo hicho.

Alisema wamekuwa wakifanyiwa ukaguzi na Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG) na hakukuwahi kubainika uchafu na kimepatiwa hati safi.

“…niseme tu tutawashitaki waandishi hawa kwa kutoa taarifa ambazo hazina ukweli wowote,” alisema Mjema na kusema kimetaka magazeti husika kukanusha taarifa hizo."

Milioni 392 Zajenga Barabara HEWA Dar es Salaam

$
0
0

Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Boniface Jacob amebaini matumizi ya Sh392 milioni zilizoandikwa kwenye taarifa ya manispaa hiyo kuwa zimetumika kwa ajili ya ukarabati wa barabara ya Sinza - Igesa ambao haukufanyika.

Katika taarifa ya manispaa hiyo, fedha hizo zilidaiwa kutumika kwa ajili ya matengenezo ya mara kwa mara ya barabara hiyo.

Akizungumza kwenye ziara ya Kamati ya Uchumi na Fedha ya Manispaa hiyo, Jacob alisema ni ajabu kuona hakuna matengenezo yoyote yaliyofanyika kama taarifa hiyo inavyoelezwa huku fedha zikionekana kulipwa.

Alisema hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa yeyote atakayebainika kuhusika kwenye matumizi hayo huku akiiomba Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (Takukuru) kuchunguza matumizi ya fedha hizo. 

“Fedha hizi zinaonekana zimelipwa kwa mkandarasi Skol Building Contract Ltd wakati barabara ina mahandaki na mashimo makubwa, ikionyesha kwamba haijakarabatiwa,” alisema.

Alisema kama wasingeamua kukagua thamani ya fedha za halmashauri hiyo zinavyotumika kwenye miradi hiyo katika kipindi cha Jaruari hadi Machi mwaka huu wasingegundua udanganyifu huo.

Meya huyo aliyeonyesha kukasirishwa na hali hiyo, aliwataka wataalamu wa halmashauri hiyo waliohusika kuandika ripoti hiyo kutoa maelezo ya kina kuhusu udanganyifu huo.

“Hivi kama tungenyamaza tusiamue kukagua miradi hii nani angesimama kueleza hayo? Mnaleta hadithi wakati tayari mmeshalidanganya Baraza la Madiwani kwamba fedha hizi zimetumika kukarabati barabara hii?” alisema.

Akitetea matumizi ya fedha hizo, mchumi wa manispaa hiyo, Huruma Eugen alisema zilizoandikwa kwenye taarifa hiyo zimetumika kwa ajili ya kulipa madeni ya nyuma.

Huku kukiwa na mabishano baina yake na Meya, Eugen alisema awali, ujenzi wa barabara hiyo ulifanyika kwa kukopa kutoka fedha za Mfuko wa Barabara, jambo lililowafanya watumie fedha za mapato ya ndani ya halmshauri kulipa deni hilo. 

“Hela ilitoka kwenye mfuko wa barabara na imerudishwa kwenye akaunti, japo huku imeandikwa imelipwa kwa mkandarasi aliyejenga barabara hii,” alisema Eugen.

Hata hivyo, Meya huyo alisema kama fedha hizo zimetumika kwa ajili ya kulipa madeni zingeonyesha wazi kwenye taarifa hiyo badala ya kuandikwa kwamba zimeelekezwa kwenye ukarabati wa barabara, wakati jambo hilo halijafanyika.

Diwani wa Sinza, Godfrey Chindaweli alieleza kushangazwa na taarifa inayoonyesha ukarabati wa barabara hiyo wakati ni miongoni mwa barabara zenye mashimo kwenye kata yake.

Alisema mara kadhaa amepokea malalamiko kutoka kwa wananchi kuhusu ubovu wa barabara hiyo na kuahidi kuikarabati akidhani ipo kwenye mpango.

“Nimeshangaa kuona miongoni mwa miradi iliyotumia fedha za robo ya tatu ya mwaka huu wa fedha, barabara ya Sinza ambayo haijaguswa ipo kwenye orodha, jambo hili linahitaji majibu ya haraka,” alisisitiza.

Diwani wa Makongo, Ndeshukuru Tungaraza aliwataka wataalamu wa halmashauri hiyo kueleza ilikuwaje fedha ziandikwe kwamba zimetumika kwa ajili ya ukarabati wa barabara wakati hazikutumika kwa kazi hiyo.

Tungaraza alisema hakuna sheria ya matumizi ya fedha inayoelekezwa kufanya kama ambavyo manispaa hiyo imefanya, jambo ambalo madiwani hawatakubaliana nalo.

Katika eneo la Mwananyamala kwenye Barabara ya Akachube inayoelekea kwenye kituo cha daladala cha Makumbusho, Meya huyo aliwaagiza wahandisi aliowakuta wakiendelea na ujenzi kukamilisha haraka ili kuondoa usumbufu kwa watumiaji wa barabara hiyo.

Alisema malalamiko mengi ya wananchi kuhusu ubovu wa barabara yanatokana na uzembe wa kutosimamia kwa ukamilifu miradi iliyopo.

Hata hivyo, mkandarasi wa kampuni ya Delmonto, Rajab Athman alisema wanashindwa kukamilisha kwa wakati barabara hiyo kutokana na kupasuka kwa mabomba ya maji.

“Maji yanamwagika mengi, hivyo tunawasubiri Dawasco wakishakamilisha kutengeneza mabomba yaliyopasuka tutaendelea kujenga,” alisema.

Katika ujenzi wa Jengo la Bima ya Afya, katika Hospitali ya Mwananyamala linaloendelea kujengwa, Meya Jacob alionyesha wasiwasi wa jengo hilo kukamilika mapema kabla mpango wa matumizi ya bima kwa wananchi wote kuanza.

“Mpango huu unatarajia kuanza Julai lakini mpaka sasa hali inaonyesha halitakamilika kwa wakati, jambo hili linanipa wasiwasi,” alisema.

Lowassa azungumzia tuhuma za kukwapua ardhi ya wananchi, Lukuvi aahidi kumnyang’anya

$
0
0
Baada ya Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi kueleza Bungeni kuwa Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa alijimilikisha ardhi iliyotolewa kwa wananchi wilayani Monduli mkoani Arusha na kuahidi kuirejesha, Mwanasiasa huyo amejibu tuhuma hizo.

Lowassa amesema kuwa halijui shamba alilolizungumzia Waziri huyo na kwamba hakuna ardhi ambayo anaimiliki kinyume cha taratibu.

Alisema kuwa hana taarifa kamili kuhusu maelezo ya Waziri Lukuvi na kwamba ameomba Mbunge wa Jimbo la Monduli, Julius Kalanga (Chadema) kulifuatilia kwa karibu na kumpa taarifa ili aweze kulitolea ufafanuzi.

“Nashindwa kutoa maelezo kuhusu taarifa hizo kwa sababu sifahamu lolote kuhusu shamba hilo,” Lowassa anakaririwa na gazeti la Jambo Leo lililofanya nae mahojiano kwa njia ya simu. 

“Mimi sipo Bungeni, nimesikia hizo habari, lakini sijui zimetolewa lini na nani. Mbunge wangu analifanyia kazi kwa sababu sina shamba nilalolimiliki ambalo liko kinyume na taratibu,” aliongeza.

Akijibu hoja ya Mbunge wa Monduli kuhusu umiliki na uporaji wa ardhi unaofanywa na vigogo jimboni humo, Waziri Lukuvi alieleza kuwa kuna shamba ambalo lilidhaminiwa na Rais Benjamin Mkapa ili wapewa wananchi jimboni humo, lakini  Lowassa alijimilikisha.

“Lile Shamba la Makuyuni lilitolewa kwa wananchi litarudi kwao na ukae ukijua litakuwa kwao kwa sababu aliyejimilikisha ni Edward Lowassa,” alisema Lukuvi na kuahidi kulirejesha mikononi mwa wananchi hao.

Vodacom Tanzania kugawa bonasi ya Tsh bilioni 25 kwa wateja wake kupitia huduma ya M-Pesa

$
0
0

Wateja wapatao milioni 11 wa Vodacom Tanzania wanaotumia huduma ya M-Pesa kuanzia leo wataanza kupatiwa mgao wa bonasi kutoka kwenye fungu la shilingi bilioni 25 zilizohifadhiwa kwenye akaunti maalumu ya M-Pesa kwenye mabenki mbalimbali nchini.
 
Mkurugenzi Mkuu wa Vodacom Tanzania, Ian Ferrao alisema, “Mgao wa fedha hizi kwa wateja wetu ni mwendelezo wa kugawa fedha za bonasi ya M-pesa ambao ni utaratibu wetu. Hapo awali tuligawa takriban bilioni 20; awamu hii inayoanza leo tutagawa bilioni 25 na kuanzia sasa tutakuwa tunatoa gawio kila baada ya kipindi cha miezi mitatu” alisema Ferrao.

Ferrao alisema “kiasi cha fedha atakachopata mteja kwenye mgao wa fedha hizi utategemea matumizi yake ya huduma hii katika kufanya miamala mbalimbali ya malipo ikiwemo kutuma fedha. Natoa wito kwa wateja wetu ambao wameacha kutumia kadi zetu za simu wakati waliwahi kutumia huduma hii wajiunganishe tena kwenye mtandao wetu ili fedha za mgao wao zisipotee bure. Pia wateja wetu wanaotumia huduma hii kuanzia leo wanaweza kuangalia fedha watakazojipatia kwa kutuma ujumbe wa maneno kwa kuandika neno KIASI na kuutuma kwenda namba 15300”

Aliongeza kusema kuwa wateja wa huduma ya M-Pesa wakiwemo mawakala wakubwa na wadogo wanao uhuru wa kutumia fedha zao za mgao watakazopata ambapo wanaweza kuzitumia kununulia huduma mbalimbali za Vodacom kama muda wa maongezi,kujiunga na vipurushi mbalimbali ikiwemo  kifurushi cha DABO BANDO kinachomuwezesha mteja kununua muda wa maongezi na vifurushi vya internet moja kwa moja kwa kutumia M-Pesa, wanaweza kuzituma fedha hizo kwa ndugu na marafiki, kulipia ankra zao mbalimbali au kujiwekea akiba kwenye akaunti za M-Pawa kwenye simu zao. Vodacom pia imetangaza kuwa itaendelea kuboresha huduma za M-Pesa ili utumiaji wake ulete unafuu kwa wateja pia kuwanufaisha mawakala wake.

Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa M-Commerce wa Vodacom Tanzania, Sitoyo Lopokoiyit, amesema kuanzia mwezi uliopita imepunguza viwango vya makato kwa watumiaji wa huduma  ya M-Pesa kwa miamala ya hadi shillingi 40,000 kwa asilimia 40% hali inayoleta unafuu kwa wateja na mawakala kuendelea kujipatia faida ya kutoa huduma “M-Pesa imeleta mapinduzi makubwa ya  huduma za kifedha nchini ikiwa na mtandao wa mawakala zaidi ya 85,000.

Bunge Latolea Ufafanuzi Madai ya Kitwanga Kujibu Swali Bungeni Huku Akiwa Amelewa

$
0
0

BUNGE limekanusha taarifa inayosambazwa katika mitandao ya kijamii na watu wanaodaiwa kuwa ni madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza.

Taarifa hiyo inadai kuwa video iliyomuonesha aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga akijibu swali bungeni Mei 20 mwaka huu, ilihaririwa na kusambazwa na maafisa wa Bunge.

Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano cha Bunge kilitoa taarifa ya ufafanuzi kuhusu madai ya kuhaririwa kwa video hiyo, mjini Dodoma jana.

Taarifa hiyo ilieleza kuwa taarifa hizo, si za kweli na zina lengo la kuupotosha umma, kwani ukweli ni kwamba kipindi cha maswali na majibu bungeni, hurushwa moja kwa moja na hupatikana kupitia vituo vyote vya televisheni, vinavyopokea matangazo ya bunge.

Ilisema matangazo hayo, yanaweza pia kurekodiwa na mtu yeyote mwenye uwezo huo popote alipo, kadri anavyoweza kuyapokea matangazo.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Akutana Na Watanzania Waishio Zambia

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Watanzania waishio Zambia kwenye ubalozi wa Tanzania uliopo Lusaka Mei 24, 2016. Majaliwa alikwenda Zambia kumwakilisha  Rais John Magufuli kwenye Mkutano wa Benki ya Maendeleo ya Afrika- ADB uliofanyika kwenye Kituo cha Mikutano cha Mlungushi. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Baadhi ya Watanzania  waishio Zambia wakimsikiliza Waziri  Mkuu, Kassim Majaliwa wakatia lipozungumza nao kwenye ubalozi wa Tanzania uliopo Lusaka.  Majaliwa  alikwenda Zambia kumwakilisha Rais John Magufuli kwenye  mkutano wa Benki ya Maendeleo ya Afrika – ADB, Mei 24, 2016. (Picha na  Ofisi ya Waziri Mkuu)
Baadhi ya Watanzania  waishio Zambia wakimsikiliza Waziri  Mkuu, Kassim Majaliwa wakatia lipozungumza nao kwenye ubalozi wa Tanzania uliopo Lusaka.  Majaliwa  alikwenda Zambia kumwakilisha Rais John Magufuli kwenye  mkutano wa Benki ya Maendeleo ya Afrika – ADB, Mei 24, 2016. (Picha na  Ofisi ya Waziri Mkuu)
Baadhi ya Watanzania  waishio Zambia wakimsikiliza Waziri  Mkuu, Kassim Majaliwa wakatia lipozungumza nao kwenye ubalozi wa Tanzania uliopo Lusaka.  Majaliwa  alikwenda Zambia kumwakilisha Rais John Magufuli kwenye  mkutano wa Benki ya Maendeleo ya Afrika – ADB, Mei 24, 2016. (Picha na  Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Akutana Na Kagame Lusaka

$
0
0
Waziri Mkuu, Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Rais wa Rwanda, Paul Kagame  kwenye  Kituo cha Mikutano cha Mlungushi kilichopo Lusaka Zambia ambako walihudhuria mkutano wa Benki ya  Maendeleo ya Afrika – ADB, Mei 24, 2016, Majaliwa alimwakilisha Rais John Magufuli kwenye mkutano huo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Upinzani Burundi Wataka AU,EU wasishiriki mazungumzo ya kutafuta amani

$
0
0
Mzunguko wa kwanza wa mazungumzo ya Burundi umemalizika, huku kukiwa na mvutano kuhusu kualikwa kwa chama cha CNARED, kinachojumuisha wanasiasa wanaoishi nje ya Burundi. 

Msuluhishi wa mgogoro huo, Rais mstaafu wa Tanzania, Benjamin Mkapa alisema mzunguko wa kwanza ulijikita zaidi katika ‘mazungumzo binafsi’ na Serikali. 

Alisema mzunguko wa pili utaanza mwishoni mwa mwezi ujao na kwamba atakutana na vikundi ambavyo havikuhudhuria mzunguko huo, akiamini vitakuwa na mchango wenye masilahi. 

Burundi imekuwa kwenye mgogoro huo baada ya uchaguzi uliopita na zaidi ya watu 450 wameuawa tangu Rais Pierre Nkurunziza alipogombea kipindi cha tatu cha urais na kushinda. 

Wapinzani wake wanadai kugombea kwake kumevunja Katiba inayotamka vipindi vya urais ni viwili. Mzunguko wa kwanza wa mazungumzo hayo ulianza mwishoni mwa wiki jijini Arusha, baada ya majadaliano ya mwaka jana kabla ya Mkapa kuteuliwa, yaliyofanyika kwa nyakati tofauti katika nchi za Burundi na Uganda kushindikana. 

Hata hivyo, baadhi ya vikundi vya upinzani kikiwamo cha CNARED, kinachojumuisha wanasiasa na maofisa wa zamani wa Serikali wanaoishi uhamishoni, walisema mazungumzo hayo yanahitaji kujumuisha wapinzani wote.

“Mazungumzo lazima yawe kati ya upande wa Nkurunziza na vyama vyote vya upinzani na vikundi vya kijamii wanaopinga muhula wa tatu.” alisema msemaji wa CNARED, Pancrace Cimpaye. 

Wakati huohuo; vyama tisa vilivyoshiriki uchaguzi wa Burundi wa mwaka 2015 , vimetaka wawakilishi wa umoja wa Ulaya na Umoja wa Afrika kutoshiriki katika mazungumzo ya amani ya Burundi. 

Katika taarifa yao iliyotiwa sahihi na viongozi wote tisa wa vyama hivyo, walisema kutokana na lugha na misimamo ya wawakilishi hao wa taasisi za juu, ni wazi wataharibu mchakato huo unaoendelea wa kutafuta amani ya Burundi.

Viongozi hao wamemtaka msuluhishi wa mgogoro huo, Rais mstaafu Mkapa kutokubaliana na wawakilishi hao na kushirikisha pande zote zenye masilahi na mgogoro wa Burundi.

Jeshi la Polisi Zanzibar Lawatahadharisha Viongozi wa CUF

$
0
0
Jeshi la Polisi Zanzibar, limesema kuwa vitendo vya kihalifu vya uvunjifu wa amani vinavyotokea kisiwani Pemba vinachochewa na viongozi wakuu wa chama cha Wananchi CUF.

Akizungumza na waandishi wa habari visiwani hapa, naibu mkurugenzi wa upelelezi na Makosa ya jinai wa Jeshi hilo, Salum Msangi alisema kuwa viongozi wakuu wa CUF wamekuwa wakiwatuma wafuasi wao kufanya vitendo vya hujuma kisiwani Pemba kwa madai kuwa serikali iliyopo madarakani sio halali.
 
Alisema kuwa jeshi la polisi linataarifa za uhakikia kuhusu viongozi wa CUF wakiwapongeza wafuasi wao na kuwapa zawadi ya fedha kwa kuweza kufanya vitendo vya hujuma kisiwani humo ikiwemo uchomaji moto wa majengo mbalimbali na kuhujumu mikarafuu na mazao mbalimbali.
 
“Tunao ushahidi viongozi wa CUF wamewakusanya wafuasi wao na wanawapa pongezi wale ambao wameza kufanikiwa kufanya vitendo vya hujuma dhidi ya wananchi”alisema.
 
Alisema kuwa jeshi hilo halitamvumilia mtu yoyote atakaehusika kufanya vitendo vya uvunjifu wa amani na wala halitakua na muhali katika kuchukua hatua za kisheria bila ya kujali cheo cha mtu.
 
Aidha alisema kuwa jeshi hilo linawashikilia watu zaidi ya 20 kisiwani Pemba ambapo wanahusishwa na vitendo vya uvunjifu wa amani na upelelezi utakapokamilika watafikishwa mahakamani.
 
Akizungumzia kuhusu ripoti ya Chama cha wananchi CUF waliyoitoa juzi ya kulipeleka Jeshi hilo mahakama ya kihalifu ya kimataifa (ICC),alisema jeshi hilo haliogopi kupelekwa huko na kusema kuwa taarifa zilizomo katika ripoti hiyo zinazohusu jeshi la polisi ni za uongo.
 
“Kama ICC tutaanza kuwapeleka wao viongozi wakuu wa CUF ambao wao ndio wachochezi wakubwa wa uvunjifu wa amani ya nchi na taarifa zao zote tunazo”alisema Msangi.
 
Hata hivyo alisema jeshi la polisi linaendelea kuwaita watu mbalimbali na kuwahoji akiwemo Katibu mkuu wa CUF Maalim Seif Sharif Hamad na viongozi wengine waandamizi wa chama hicho.
 
Jeshi hilo liliwapa tahadhari viongozi na wafuasi wa vyama vya siasa kuacha tabia ya kuwashawishi wafuasi wao kufanya vitendo vya hujuma wakati wao wametulia majumbani mwao.

TANESCO Yawataka Wateja wake Kuunganishiwa Umeme na Mafundi Waliosajiliwa.

$
0
0

Shirika la Umeme Tanzania Nchini (TANESCO) limewataka wateja wake kuhakikisha wanaunganishiwa umeme na mafundi au wakandarasi waliosajiliwa na shirika hilo ili kupunguza ajali za moto.

Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es Salaam na Meneja wa Afya na Usalama kazini wa TANESCO, Mhandisi Majige  Mabulla alipokua akiongea na waandishi wa habari juu ya vyanzo vya ajali za moto vinavyosababishwa na umeme.

Mhandisi Mabulla alisema kuwa matukio ya moto yanayosababishwa na umeme hutokea kutokana na kuzalishwa kwa joto kali ndani ya nyaya kunakosababishwa na umeme kuwa mkubwa kuliko uwezo, kulegea kwa maungio ya nyaya pamoja na radi au nyaya za umeme kuangukia juu ya paa la nyumba.

Kwa mujibu wa Mhandisi Mabulla aliongeza kuwa ajali za moto zinazosababishwa na umeme huanza kama unavyoanza moto wa kiberiti au viwashio vinginevyo vya moto na husambaa haraka kwa kutegemea na aina ya vitu vilivyopo kwenye eneo husika kwa kuwa baadhi ya vitu hushika moto haraka na kuenea kwa kasi.

“Ajali za moto zinazosababishwa na umeme ni ngumu kutokea kama umeme utasukwa na mtaalam aliyebobea kwenye fani hiyo, TANESCO tunatoa wito kwa wateja wetu kuhakikisha wanafungiwa umeme na fundi au mkandarasi aliyesajiliwa na kampuni yetu,”alisema Mabulla.

Pia Mhandisi Mabulla alisema ili kuepukana na ajali za moto zinazotokana na hitilafu za umeme wateja wanapaswa ;kuepuka kupitisha nyaya za umeme juu ya paa za nyumba, kutokuunganisha umeme kutoka nyumba moja kwenda nyingine bila kupata maelekeza kutoka TANESCO.

Aidha Mhandisi Mabula alisema wateja pia wanapaswa kuhakikisha mfumo wa umeme unapitiwa upya kila baada ya miaka mitano pamoja na kuwa makini katika utumiaji wa vifaa vinavyotumia umeme kama vile pasi, hita za umeme.

Makampuni 52 Yajitokeza Kuwekeza Sekta Ya Umeme

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema hadi sasa Serikali imekwishapokea maombi 52 kutoka makampuni mbalimbali ambayo yanataka kuwekeza kwenye sekta ya umeme nchini Tanzania.

Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo jana jioni (Jumanne, Mei 24, 2016) wakati akizungumza na Watanzania waishio Zambia katika mkutano uliofanyika kwenye Ubalozi wa Tanzania jijini Lusaka, Zambia.

“Haya maombi yamekwishapokelewa na wenye makampuni wamekwishahojiwa kuangalia uwezo walionao katika suala zima la uwekezaji wanaotaka kuufanya, na tukiwapata wenye uwezo na wenye nia ya dhati watapatiwa miradi ya kuiendesha,” alisema.

Aliwataka Watanzania hao waishio Zambia watumie fursa ya uwepo wao huko kutafuta marafiki ambao wanaweza kuja kuwekeza kwenye miradi mbalimbali nchini kwani Serikali peke yake haiwezi kufanya kila kitu wakati wananchi wanahitaji kupatiwa huduma muhimu.

“Serikali peke yake haiwezi kufanya kazi ya uwekezaji kwa hiyo tunahitaji kushirikiana na sekta binafsi, taasisi za kifedha na washirika wa maendeleo na ndiyo maana kule kwenye mkutano nimewaeleza washiriki kwamba milango ya uwekezaji Tanzania iko wazi."

Alisema kupatikana kwa umeme wa uhakika kutawezesha wananchi wengi zaidi kujiingiza katika shughuli za kiuchumi na hivyo kuinua uchumi wa nchi na maendeleo ya Taifa kwa ujumla.

Alisema malengo ya Serikali ya awamu ya tano ni kuona kuwa nchi inakuwa na mitambo mingi ya kuzalisha umeme na umeme wote unaozalishwa na mitambo hiyo inaunganishwa na gridi ya Taifa ili kuondokana na tatizo la mgao wa umeme nchini.

Alisema Tanzania ina vyanzo vingi vya nishati vikiwemo gesi asilia, makaa ya mawe, madini ya urani, maji, upepo, nishati ya joto kutoka ardhini (geothermal energy) na nishati inayotokana na vinyesi vya mifugo (biomass) ambayo alisema vinatumika kwa watu wachache (siyo kitaifa).

Alisema kupatikana kwa gesi asilia nchini kumeleta neema ambapo mabomba ya gesi yamekwishajengwa kutoka Mtwara hadi Kinyerezi na kutoka Kilwa-Songosongo hadi Dar es Salaam. 

“Sasa hivi kuna utafiti unaendelea juu ya uwezekano wa kusambaza gesi ya kupikia majumbani. Tumeanza pale Mikocheni (DSM) na sasa hivi wanafanya utafiti mwingine kule Mtwara ili wananchi waweze kutumia gesi hii kupikia badala ya mkaa,” alisema.

Akielezea kuhusu uwekezaji kwenye makaa ya mawe, Waziri Mkuu alisema Serikali imelenga kutumia makaa ya mawe ili kuendeshea mitambo ya kwenye viwanda vikubwa badala ya kutumia umeme au mafuta ya dizeli kama inavyofanyika sasa.

 “Baadhi ya wenye viwanda wanabadilisha mifumo ya kuendeshea mashine zao ili iweze kuendana na teknolojia ya makaa ya mawe pindi tu uchimbaji ukishika kasi,” alisema.

Akifafanua kuhusu juhudi za Serikali katika kusambaza nishati ya umeme, Waziri Mkuu alisema tangu kuanzishwa kwa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), vijiji zaidi ya 3,000 katika ya vijiji 12,000 vilivyopo nchini vimefikiwa na nishati ya umeme.

“Tulianza na REA awamu ya kwanza, awamu ya pili na sasa tunaenda awamu ya tatu. Hata mkipiga simu kwa ndugu zenu vijijini, mtakuta katika kila kata kuna vijiji kati ya vinne hadi vitano ambavyo vimefikiwa na nishati ya umeme kupitia mradi wa REA,” alisema.

Waziri Mkuu amerejea nchini leo (Jumatano, Mei 25, 2016).

Viongozi Wa Afrika Wataka Ushirikiano Zaidi

$
0
0

WAKUU wa nchi za Afrika wametaka kuwepo na juhudi za pamoja katika kukabiliana na majanga yatokanayo na mabadiliko ya tabiachi yanayolikumba bara hilo.

Kauli hiyo ilitolewa jana mchana (Jumanne, Mei 24, 2016) wakati wa majadiliano baina ya viongozi kutoka Zambia, Chad, Nigeria, Msumbiji na Tanzania mara baada ya ufunguzi wa Mkutano wa 51 wa Mwaka wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano cha kimataifa wa Mulungushi, jijini Lusaka, Zambia.

Wakishiriki kwenye mjadala wa Wakuu wa Nchi na Serikali uliohusu Nishati na Mabadiliko ya Tabianchi, viongozi hao walisema bara la Afrika linahitaji kupata maendeleo zaidi licha ya tatizo la nishati linalolikumba bara hilo hivi sasa.

Akichangia mjadala huo, Rais wa Zambia, Bw. Edgar Lungu alisema nchi yake imepania kuboresha hali ya upatikanaji wa umeme vijijini lakini imekuwa ikikabiliwa na tatizo la uhaba wa mvua kwa zaidi ya miaka miwili hali ambayo alisema imechangia kukosekana kwa umeme katika maeneo mengi nchini humo.

“Uhaba wa mvua umepunguza kiwango cha maji katika bwawa la Kariba ambalo hutumika kuzalisha umeme nchini mwetu. Na hapa kwetu, karibu asilimia 80 ya umeme wetu, unategemea uzalishaji wa umeme kutokana na vyanzo vya maji,”  alisema.

Rais wa Chad, Bw. Idriss Deby Itno aliitaka benki ya AfDB ichukue nafasi ya mdau mkuu kwenye uwekezaji wa sekta ya nishati na kuzisadia nchi za bara hili kupata mitaji ya uwekezaji na ushauri wa kitaalamu.

“Tunahitaji kutumia fursa ambazo benki yetu inazo katika kukabilianana changamato za ukosefu wa nishati. Tukiweza kutekeleza jambo hilo, tutafanikiwa kuwa na miradi ambayo ni makini na kwa maana hiyo tutaweza kuliangaza bara letu la Afrika kwa kupata mwanga wa uhakika,” alisema.

Kwa upande wake, Makamiu wa Rais wa Nigeria, Prof, Yemi Osinbajo alisema bara la Afrika halina budi budi kuweka kipaumbele kwenye masuala ya maendeleo yake wakati likitafuta suluhisho la kukabiliana na athari za mazingira.

“Tunapaswa kutafuta njia za kubalance mahitaji makubwa ya umeme ambayo bara letu linakabiliwa nayo dhidi ya athari za kimazingira ambazo zinapigiwa kelele na mataifa makuna na zinahatarisha kutunyima fursa ya kuendelea haraka kama ilivyokuwa kwao,” alisema na kuongeza:

“Kama nchi zilizoendelea zinataka sana kupunguza athari zitokanazo na mabadiliko ya tabianchi, zinatakiwa zitupatie fedha, teknolojia na wataalamu ambao watasaidia kuendesha mitambo ili tupate nishati safi kutokana na mafuta ya petroli na dizeli sababu ni rasilmali ambazo tunazo.”

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alisema ili kuondokana na tatizo la nishati, kuna haja ya kuwa na viongozi wenye utashi wa kisiasa ambao watakuwa tayari kuruhusu uwekezaji mkubwa kwenye sekta ya nishati na kuongeza kuwa Tanzania inapitia upya sheria zake ili kuruhusu miradi mikubwa ya uwekezaji kwenye sekta hiyo.

Aliwaambia washiriki wa mkutano huo kwamba milango ya uwekezaji Tanzania iko wazi kwa ajili ya wawekezaji walio tayari kuwekeza kwenye sekta hiyo na kutaja fursa ambazo Tanzania inazo kwenye sekta ya nishati ikiwemo gesi asilia, makaa ya mawe, madini ya urani, maji, upepo na nishati ya joto kutoka ardhini (geothermal energy).

Naye Waziri Mkuu wa Msumbiji, Bw. Carlos Agostinho do Rosário alisema kuna haja ya kuwa na taasisi ya uzalishaji na ugawaji umeme ya pamoja (electricity pool) ambayo itaruhusu wazalishaji wa umeme wawauzie wanunuzi wakubwa.

Waziri Mkuu ambaye yuko Lusaka kuhudhuria mkutano huo wa ADB kwa niaba ya Mheshimiwa Rais, Dk. John Pombe Magufuli, amerejea nchini leo (Jumatano, Mei 25, 2016).

Mtoto wa Wilson Kabwe AGOMA Kupokea Mkono wa Pole Toka Kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda

$
0
0

Anna Kabwe, binti wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, Wilson Kabwe amegoma kumpa mkondo Paul Makonda, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam

Tukio hilo la aina yake lilimfika Makonda aliposhiriki shughuli ya kuaga mwili wa Kabwe katika Viwanja vya Karimjee alipokuwa akitoa mkono wa pole kwa familia ya Kabwe.

Wakati Makonda akimpa mkono, Anna aliendelea kuchezea simu yake huku akipuuza mkono wa kiongozi huyo. Anna alifanya hivyo akiwa amekaa huku ndugu zake wengine wakiwa wamesimama wakati wakipokea mkono huo wa pole.

Kitendo hicho kimetafsirika kwamba, Anna alikumbuka tukio lililofanywa Aprili 19 mwaka huu wakati wa uzinduzi wa Daraja la Kigamboni ambapo Makonda alimtuhumu marehemu Kabwe (baba yake) kwamba amehusika na kusaini mikataba iliyoikosesha mapato serikali.

Kabwe alifariki tarehe 19 Mei mwaka huu kutokana na tatizo la ini. Mauli yalimkuta akiwa katika Hospitali ya Mama Ngoma jijini Dar es Salaam alipokuwa akipatiwa matibabu. Ameacha mjane na watoto watano; wanne wa kiume na mmoja wa kike.

Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images