Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Kigogo Kenya Matatani kwa Kuhudhuria Sherehe za Kuapishwa Rais Magufuli Dar

$
0
0
Gavana wa Jimbo la Siaya, nchini Kenya, Cornel Rasanga ameingia matatani akidaiwa kutumia Sh20 milioni za nchi hiyo (karibu Sh400 milioni) kutoka katika mfuko za Serikali kwa ajili safari ya kuhudhuria sherehe za kumwapisha Rais John Magufuli. Dk Magufuli alipishwa Novemba 5, kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam baada ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kumtangaza mshindi wa uchaguzi wa urais

Mchakato wa Kuanzisha Mahakama ya MAFISADI Waanza

$
0
0
Utekelezaji wa ahadi za Rais John Magufuli unazidi kushika kasi baada ya kuanza kwa mchakato wa kuanzisha mahakama maalumu ya kuwashughulikia mafisadi. Jaji Kiongozi, Shaban Lila alisema jana kuwa tayari wadau mbalimbali wa haki jinai wameanza kukutana kuangalia namna ya kuanzisha mahakama hiyo kama sehemu ya utekejezaji wa ahadi ya Rais. Akizungumza katika hafla ya kuhitimisha mafunzo ya

Dawa ya Jiko Yathibitishwa Na Mkemia Mkuu wa Serikali

$
0
0
JIKO  ni  dawa  asilia  inayo  tolewa  na  duka  la  kuuza  dawa  za  asili  liitwalo  NEEMA  HERBALIST  &  NUTRITIONAL  FOODS  CLINIC.  Dawa  hii  ni ya   asili  kabisa isiyo  na  kemikali  za  viwandani na   ambayo  inatibu  na  kuponyesha  kabisa  tatizo  la  ukosefu  na  upungufu  wa  nguvu za  kiume  ndani  ya  siku  thelathini. DAWA  YA  JIKO  IMETHIBITISHWA  NA  MKEMIA  MKUU  WA 

Jaji wa Escrow Kusikiliza Kesi ya Ubunge wa David Kafulila

$
0
0
Kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi iliyofunguliwa na aliyekuwa Mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR-Mageuzi), David Kafulila, kupinga matokeo ya uchaguzi itaanza kusikilizwa leo na Jaji John Utamwa katika Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Tabora. Kafulila aliyekuwa Mbunge kinara katika kuibua ufisadi wa sakata la uchotwaji wa zaidi ya Sh. bilioni 306 katika akaunti ya Tegeta Escrow iliyokuwa

Wabunge Mtegoni: Rais Magufuli Aombwa Kufuta Posho za Zisizo na Umuhimu

$
0
0
RAIS John Magufuli ametakiwa kufuta posho zote zisizokuwa za lazima kwa wabunge huku watunga sheria hao wakitakiwa kueleza waziwazi msimamo wao kuhusu kukataa posho hizo ili fedha zitakazookolewa zitumike kwa kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi katika majimbo yao. Hayo yalisemwa Dar es Salaam jana na Mwenyekiti wa Jukwaa Huru la Wazalendo, Ally Hapi wakati akizungumza na

Hapa Kazi Tu: Serikali Yapiga Marufuku Utengenezaji na Uchapishaji Kadi za Xmass na Mwaka Mpya kwa Gharama Zake

$
0
0
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue amepiga marufuku utengenezaji na uchapishaji wa kadi za Christmas na Mwaka Mpya kwa gharama za serikali/umma, kwa mwaka huu. Balozi Sefue, ameelekeza kuwa yeyote anayetaka kutengeneza ama kuchapisha kadi hizo, afanye hivyo kwa gharama zake mwenyewe. Badala yake Balozi Sefue ameagiza fedha zilizopangwa kugharamia utengenezaji na uchapishaji wa

CHADEMA Yashinda Kesi......Mahakama Yatoa Kibali Mwili wa Marehemu Alphonce Mawazo Kuagwa na Kuzikwa

$
0
0
Mahakama kuu kanda ya Mwanza imetoa hukumu ya kuondoa zuio la kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza la kuinyima familia ya aliyekuwa mwenyekiti wa chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) kibali cha kuuaga mwili wa marehemu Alphonce Mawazo katika jiji la Mwanza. Hukumu ya kesi hiyo iliyovuta umati mkubwa wa wakazi wa jiji la Mwanza na mikoa jirani ya kanda ya ziwa, imetolewa leo mchana na jaji

Lowassa, Sumaye na Freeman Mbowe Kuongoza Maelfu Ya Wafuasi wa Chadema Jijini Mwanza Leo Kuuaga Mwili wa Marehemu Alphonce Mawazo

$
0
0
Leo  Siku ya Ijumaa, Novemba 27 saa 2 asubuhi, mwili wa Alphonce Mawazo utachukuliwa Hospitali ya Bugando kuelekea nyumbani kwa Baba yake mdogo, eneo la Nyegezi-Swea kwa ajili heshima za familia kabla ya kuelekea Viwanja vya Furahisha ambapo Viongozi waandamizi wa UKAWA, wakiongozwa wa Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe, Mgombea Urais Edward Lowassa, Waziri Mkuu Mstaafu Fredrick

Rais Magufuli Afika ofisini kwa Waziri Mkuu, Majaliwa ......Wateta Kwa Zaidi Ya Saa Moja

$
0
0
Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Waziri Mkuu Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa wakati alipomtembelea Ofisini kwake jijini Dar es salaam jana Novemba 26, 2015 na kuzungumza nae kwa takribani saa moja. Rais John Pombe Joseph Magufuli akitia saini kitabu cha wageni wakati alipomtembelea Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa ofisini kwake jijini Dar es salaam jana

Rais Magufuli "Amaliza Kazi".......Baraza La Mawaziri Kutangazwa Muda Wowote Kuanzia Sasa

$
0
0
RAIS John Magufuli ambaye tangu Novemba 17, mwaka huu alikuwa katika Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma kwa majukumu mbalimbali, amerejea Dar es Salaam jana na wakati wowote inaelezwa kwamba anaweza kutangaza Baraza la Mawaziri linalosubiriwa kwa hamu na Watanzania. Dk Magufuli alitua Ikulu ya Chamwino, Novemba 17 kwa kutumia usafiri wa barabara akisafiri kwa zaidi ya kilometa 300 kwenda

Rais Mstaafu Jakaya Kikwete Aendelea na Kazi za Chama Ofisini Kwake Mtaa wa Lumumba

$
0
0
Mwenyekiti wa CCM Taifa Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Katibu wa Itikadi na Uenezi  Nape Nnauye mara baada ya kuwasili kwenye Makao Makuu ya Chama Ofisi Ndogo Lumumba.   Mwenyekiti wa CCM Taifa Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa ofisini kwake Makao Makuu ya  CCM Ofisi Ndogo Lumumba .

CUF Yakanusha Taarifa za Kukubaliana na CCM Kurudia Uchaguzi wa Zanzibar

$
0
0
KWA VYOMBO VYA HABARI Tumepokea taarifa kwamba Balozi Seif Ali Iddi amehojiwa na Idhaa ya Kiswahili ya Radio France International (RFI) na kusema kwamba eti viongozi wa CCM na CUF WAMEKUBALIANA UCHAGUZI ZANZIBAR URUDIWE, na kinachojadiliwa hivi sasa ni NANI ASIMAMIE UCHAGUZI WA MAREJEO kwa sababu ZEC ya JECHA INAONEKANA KUTOAMINIKA. Tunapenda kuwawekea wazi Wazanzibari wote kwamba

Bunge Kuondoa Ajira za Kudumu Serikalini.....Kudumu Kwa Ajira Ya Mfanyakazi Kutategemea Juhudi Zake Kazini

$
0
0
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania litafanyia mabadiliko makubwa sheria za utumishi wa umma kwa kuondoa ajira za kudumu serikalini, ili kuwezesha mabadiliko yaliyokusudiwa na Rais Dk. John Magufuli. Katika mabadiliko hayo, mfumo sasa wa ajira za serikali kuwa za kudumu utabadilishwa na badala yake, kudumu kwa ajira ya mfanyakazi kutategemea juhudi na bidii yake kazini, ili kuondoa

Sherehe 30 za Maadhimisho ya Kitaifa Mikononi mwa Magufuli

$
0
0
Sherehe 30 za maadhimisho ya kitaifa zinazofanyika nchini kila mwaka huenda ‘zikachinjwa’ kutokana na kasi ya Rais wa Awamu ya Tano, Dk John Magufuli ya kupunguza gharama na kubana matumizi ya Serikali yasiyo ya lazima. Wasiwasi wa kufutwa kwa maadhimisho hayo ya kitaifa umekuja baada ya Rais Magufuli juzi kufuta maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani iliyopangwa kuadhimishwa Desemba Mosi

Marekani Yaipa Kibano Tanzania .....Yaitaka Serikali itoe Maelezo Uchaguzi Zanzibar na Sheria ya Mtandao , Yatishia kusitisha Msaada wa Trilioni

$
0
0
Mfuko wa Changamoto za Milenia (MCC) wa Marekani umeonya kuwa hali ya kisiasa Zanzibar na tukio la hivi karibuni la watu kukamatwa chini ya sheria mpya ya uhalifu mtandaoni yanaweza kuathiri vigezo vya kuiwezesha Tanzania kupata msaada. Katika barua ya MCC ya Novemba 19, ambayo imesainiwa na Naibu Makamu wa Rais wa Idara ya Operesheni ya Miradi kwa Afrika, Jonathan O. Bloom kwenda kwa

Kesi ya Ubunge wa David Kafulila Yaahirishwa Hadi Jumatatu Novemba 30 Baada ya Mlalamikiwa Kutofika Mahakamani

$
0
0
Kesi iliyofunguliwa na aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kusini, David Kafulila, kupinga matokeo ya ubunge yaliyomtangaza mshindi Husna Mwilima, katika jimbo hilo, imeahirishwa hadi Novemba 30, mwaka huu.   Kesi hiyo ipo mbele ya Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Tabora, John Utamwa. Jaji Utamwa alisema mlalamikiwa (Mwilima), katika madai hayo, hakupelekewa wito wa mahakama, hivyo anaamuru

Dk. Manyaunyau Ahukumiwa Jela Miaka 3 Kwa Kushindwa Kufufua Maiti

$
0
0
Mkazi  wa Dar es Salaam, Dunia Salumu maarufu kwa jina la Dk. Manyaunyau, amehukumiwa kutumikia kifungo cha miaka mitatu jela pamoja na kulipa fidia ya Sh milioni 10 baada ya kupatikana na hatia ya kujipatia fedha Sh milioni 29.6 kwa njia ya udanganyifu. Manyaunyau anadaiwa kujipatia kiasi hicho cha fedha kutoka kwa mlalamikaji, Tekra Modesta kama malipo ya kazi ya kumfufua marehemu kaka

Waziri Mkuu Majaliwa Afanya Ziara ya Kushtukiza Bandarini.....Awafuta Kazi na Kuamuru Kukamatwa Kwa Maofisa Kibao wa TRA

$
0
0
WAZIRI MKUU Majaliwa Kassim Majaliwa amewasimamisha kazi maafisa watano na watumishi watatu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kutokana na upotevu wa makontena 349 yenye thamani ya zaidi ya sh. bilioni 80/-. Akizungumza na viongozi wa Mamlaka ya Bandari pamoja na viongozi wa TRA katika ziara ya kushtukiza leo mchana (Ijumaa, Novemba 27, 2015), Waziri Mkuu amewataka Kamishna Mkuu wa

Serikali Yakanusha Hazina Kuachwa Tupu na Rais Kikwete

$
0
0
Serikali imekanusha taarifa zinazosambazwa na baadhi ya vyombo vya habari kuwa Rais mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kuwa amekomba fedha hazina na kuiacha Serikali bila fungu lolote. Hayo yamesemwa jijini dare es salaam na Kamishina wa Bajeti kutoka Wizara ya Fedha Bwa. John Cheyo huku akiwataka wananchi kupuuza habari hiyo kwani hazina ukweli wowote. “Hazina inazo pesa

Rais Magufuli Amfuta Kazi Kamishna Mkuu wa TRA Kwa Upotevu wa Makontena 349 Bandarini

$
0
0
Rais wa Jamuhuri ya Mungano wa Tanzania, Mh. Dkt John Pombe Joseph Magufuli amemsimamisha kazi kuanzia leo tarehe 27 Nov. 2015, Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ndugu Rished Bade kufuatia ziara ya kushtukiza ya Waziri Mkuu, Mh. Majaliwa Kasimu Majaliwa mapema leo asubuhi Bandarini jijini Dar es salaam. Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akizungumza na
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images

<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>
<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596344.js" async> </script>