Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Kutimiza agizo la Rais: Maelekezo ya Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje kwa Balozi zote

0
0
Kufuatia maagizo ya Mhe. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aliyoyatoa hivi karibuni ya kusitisha safari za nje kwa Wizara, Idara na Taasisi za Serikali, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa imeanza kutekeleza maagizo hayo kwa kutoa maelekezo mahsusi kwa Balozi zake nje. Wizara imezielekeza Balozi zote zilizopo maeneo mbalimbali duniani

Biashara ya Maduka ya Dawa Baridi Muhimbili Yavurugwa

0
0
BIASHARA ya maduka ya dawa baridi katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili imeingia shubiri, huku maduka mengine katika hospitali za Serikali yakitakiwa kuwa tayari baada ya agizo la Rais John Magufuli, kuanza kutekelezwa.    Dk Magufuli alipoingia madarakani tu, moja ya maagizo yake alitaka Bohari ya Dawa (MSD) kufungua maduka ya dawa za Serikali kwenye hospitali za rufaa na za kanda,

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Apiga Marufuku Kuuza na Kunywa Pombe Saa za Kazi

0
0
MKUU wa Mkoa wa Dodoma, Chiku Galawa amepiga marufuku uuzaji na unywaji wa pombe wakati wa saa za kazi. Amri hiyo ameitoa jana katika taarifa yake aliyoisambaza kwa vyombo vya habari. Gallawa alisema kwamba amechukua uamuzi huo kwa kuzingatia mamlaka aliyonayo kwa mujibu wa Katiba, Ibara ya 61, Ibara ndogo ya 4.    Alisema kutokana na amri hiyo itakuwa marufuku kwa wakazi na

"Dili Limebumbulika".....Magogo ya Milioni 300 Yakamatwa Bandarini Yakipelekwa Nchini China Kinyemela

0
0
Kontena 37 zenye shehena ya magogo aina ya mninga yenye thamani zaidi ya Sh. milioni 300 zimekamatwa zikiwa zinasafirishwa kuelekea nchini China bila kibali. Katika shehena hiyo, kontena 31 zimekamatiwa katika Bandari ya Dar es Salaam, kati ya hizo mbili zimekamatwa mkoani Mbeya,  na mikoa ya Rukwa na Pwani katika maeneo ya Kibaha na Kongowe, kontena moja kila sehemu na Mbezi ya jijini

Zitto Kabwe 'Akaabwa Koo' Zanzibar......Apewa Siku 14 za Kuomba Radhi Kwa Kumhusisha Dr. Shein na Makosa ya Uhaini

0
0
Mbunge wa Kigoma Mjini  kwa tiketi ya Chama cha ACT-Wazalendo,  Zitto Kabwe, amepewa siku 14 kufuta kauli yake na kuomba radhi kwa kumhusisha rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein na makosa ya uhaini. Msimamo huo ulitolewa na wagombea wawili wa nafasi ya urais wa Zanzibar, Juma Ali Khatib (Tadea) na Soud Said Soud, walipokuwa wakizungumzia kauli ya Zitto kudai haikuwa sahihi kwa Rais wa

Majipu Matano SUGU Anayotakiwa Kuyatumbua Rais Magufuli

0
0
Wasomi, wanasiasa na watu kutoka makundi mengine ya jamii wamesema Rais John Magufuli atapimwa katika miaka mitano ijayo kwa mambo makubwa matano yaliyoonekana kuwa ‘majipu sugu’ na changamoto kwa mtangulizi wake, Jakaya Kikwete. Majipu (mambo matano) hayo ni; 1.Kudhibiti mtandao wa wafanyabiashara wa dawa za kulevya. 2.Kukomesha rushwa na ufisadi. 3.Kufumua mtandao wa majangili. 4.

Papa Francis Kumfufua Nyerere.....Mama Maria Nyerere Atangulia Uganda

0
0
ZIARA ya Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Francis nchini Uganda imetajwa kuwa itafufua mchakato wa kumtangaza Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere kuwa mtakatifu. Kwa mujibu wa mtandao wa ETN wa nchini Uganda, ziara hiyo ya kitume ya Papa Francis itamfikisha katika eneo la Namugongo ambalo mashahidi wa imani ya dini ya Kikristu walichomwa moto. Ni katika eneo hilo la

Watumishi Wengine Watatu Wasimamishwa Kazi TRA

0
0
SERIKALI imewasimamisha kazi watumishi watatu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ambao jana iliamriwa kwamba watahamishiwa mikoani. Watumishi hao ni Bw. Anangisye Mtafya, Bw. Nsajigwa Mwandengele na Bw. Robert Nyoni. Uamuzi huo umetolewa leo (Jumamosi, Novemba 28, 2015), na Waziri Mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa ili kupisha uchunguzi zaidi wa tuhuma zinazowakabili.    Kama ilivyo kwa

Maamuzi Mapya ya Rais Magufuli Kuhusu Serikali Kupunguza Matumizi ya Fedha Ikiwemo za Kalenda na Diaries

0
0
Katibu  Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue ametoa ufafanizi wa maagizo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John  Pombe Magufuli kuhusu kupunguza matumizi yasiyo ya lazima katika Wizara,idara na Taasisi za serikali. Katika ufafanuzi huo,Balozi Sefue amemtaka kila Mtendaji Mkuu ama Afisa Masuhuli wa serikali kujiuliza mwenyewe ni kwa kiasi gani anatekeleza kwa vitendo nia ya Rais

Waraka wa Kufuta Ada Elimu ya Sekondari ( Kidato cha 1 Hadi 4) na Michango yote Elimu ya Msingi

0
0
Serikali imeamua kutoa elimu pasipo malipo kwa elimumsingi kuanzia elimu ya awali hadi kidato cha nne,kuanzia mwaka wa masomo wa 2016. Azima hii ya serikali ni katika kutekeleza sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 2014 ambayo ina lengo la kuhakikisha kwamba watoto wote wa Tanzania wanapata Elimu bila kikwazo ikiwemo ada au malipo. Katika kutekeleza maamuzi hayo,ada zote zilizokuwa

Marehemu Alphonce Mawazo Aagwa Rasmi Jijini Mwanza......Lowassa Atoa Tamko Zito, Mbowe Aapa Kumfungulia Kesi ya Madai RPC -Mwanza

0
0
Aliyekuwa mgombea Urais wa Chadema, Edward lowassa, amelitaka jeshi la Polisi nchini kuwachukulia hatua wale wote wanadaiwa kumuua, aliyekuwa Mwenyekiti wa chama hicho mkoa wa Geita, Alphonce Mawazo na kwamba kama hawatafanya hivyo, watachukua hatua wao wenyewe. Kauli hiyo ameitoa ikiwa ni siku mbili sasa tangu Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza, kutoa hukumu kwa chama hicho kikuu cha upinzani

Viongozi Waliojiuzulu Chadema Warejea Tena

0
0
Viongozi wa Chadema Mkoa wa Rukwa waliotangaza kujiuzulu nyadhifa zao ndani ya chama hicho hivi karibuni, wamesitisha uamuzi wao na kurejea madarakani. Mratibu wa Chadema Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Frank Mwaisumbe alisema hayo juzi wakati akizungumza na mwandishi wetu  kwa njia ya simu kutoka mkoani Mbeya. Mwaisumbe alisema wamekubaliana na viongozi hao kurejea katika nyadhifa zao

IKULU: Katibu Wa Wizara ambaye ni Goigoi Ajiondoe Mapema

0
0
Joto la utawala wa Rais John Magufuli limebadili utendaji kazi wa makatibu wakuu wa wizara mbalimbali waliozoea kukaa ofisini na sasa wanafanya kazi nje ya ofisi na kusikiliza kero za wananchi kwenye maeneo yao. Wakati hilo likifanyika, Ikulu jijini Dar es Salaam imesema katibu mkuu au mtumishi yeyote wa umma atakayeshindwa kwenda na kasi na mabadiliko ya utendaji kazi katika serikali ya

Bakharesa Ajibu Tuhuma za Makontena 349 Yaliyopita Bandarini bila Kulipiwa Kodi

0
0
Kumekuwa na taarifa zinazosambazwa katika mitandao ya kijamii kuwa kampuni ya Bakhresa inahusika na upotevu wa Makontena 349 yaliyoripotiwa hivi karibuni kuwa yametolewa bandarini bila kulipiwa ushuru. Taarifa hizo zilitolewa na Waziri Mkuu wakati wa ziara yake ya Bandari ya Dar es salaam hivi karibuni. Uchunguzi wetu umeonyesha kuwa si kweli kuwa kuna makontena yenye bidhaa zilizoingizwa

Waziri Mkuu: Tumedhamiria Kuwatumikia Watanzania...Tutahakikisha Mapato Ya Taifa Yanatumika Kwa Maslahi ya Watanzania Wote

0
0
WAZIRI MKUU Majaliwa Kassim Majaliwa amesema Serikali ya Awamu ya Tano imedhamiria kuhakikisha kila kinachokusanywa kama mapato ya nchi kinatumika kwa maslahi ya Watanzania wote na si kwa manufaa ya wachache. Alitoa kauli hiyo jana mchana (Jumapili, Novemba 29, 2015) wakati akifunga maadhimisho ya miaka 20 ya Dayosisi ya Pwani ya Kanisa la African Inland Church Tanzania (AICT) kwenye

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatatu ya Leo Tarehe 30 Novemba

Lowassa, Mbowe Watua Alipouawa Alphonce Mawazo

0
0
Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe  na aliyekuwa mgombea urais wa chama hicho Mhe. Edward Lowassa pamoja na viongozi mbalimbali wakitazama eneo ambalo Alphonce Mawazo alifanyiwa kitendo ya kinyama cha kukatwakatwa mapanga na watu wanaosemekana ni wafuasi wa CCM ikiwa ni umbali mchache kutoka kutuo cha polisi na ofisi za CCM katika barabara kuu inayoelekea Geita kutokea Busanda.

Moto Wa Magufuli Watua Kwa Bakhresa.......TRA Yazuia Makontena Yake Bandari Kavu, Kampuni Yake Yahusishwa na Ukwepaji Kodi

0
0
KAMPUNI ya Said Salim Bakhresa (SSB) inachunguzwa na vyombo vya dola kwa tuhuma za kushiriki kukwepa kodi na hivyo kuikosesha serikali mabilioni ya fedha kutokana na makontena yaliyohifadhiwa kwenye bandari yake ya nchi kavu (ICD) ‘kupotea’ bila kulipiwa kodi.  Tayari Mamlaka ya Mapato (TRA) imepiga marufuku SSB kuingiza makontena katika bandari hiyo kavu ambako ndiko kunadaiwa kufanyika

Chadema Yateua Meya Manispaa ya Kinondoni

0
0
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Mkoa wa Konondoni, kimempitisha Diwani mteule wa Ubungo, Boniface Jacob (Chadema), kuwa mgombea umeya wa Manispaa ya Kinondoni, huku akiwakilisha mwamvuli wa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa). Mgombea huyo alikuwa akiwania nafasi hiyo huku akipambana na diwani mwenzake mteule wa Kata ya Mbweni, Abdunel Elibariki (Chadema)

Serikali Yazungumzia Tishio la Marekani Kusitisha Misaada Tanzania

0
0
Serikali imezungumzia tishio la Serikali ya Marekani la kusitisha misaada kwa Serikali ya Tanzania kutokana na mgogoro wa kisiasa Zanzibar na kukamatwa kwa maofisa wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu. Ofisi ya Ikulu jana ilisema masharti yaliyotolewa na Serikali ya Marekani yanatekelezeka na yatamalizwa kabla ya kikao cha Bodi ya Shirika la Maendeleo ya Milenia (MCC) kukaa Desemba,
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images