Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Serikali yahimizwa kuhamishia makao makuu Dodoma

$
0
0
SERIKALI imesisitiza agizo lake la kusitisha ujenzi wa ofisi za wizara na taasisi zake katika jiji la Dar es Salaam badala yake uelekezwe mjini Dodoma, ikiwa ni hatua ya kuhamishia makao makuu mjini Dodoma.   Naibu Waziri , Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Aggrey Mwanri alisema hayo wakati akijibu swali la Mbunge wa Chilonwa, Ezekiah Chibulunje (CCM)

Wafanyabishara Mwanza waazimia kugoma siku za kesi ya Mwenyekiti wao

$
0
0
Siku chache baada ya mwenyekiti wa jumuiya ya wafanyabiashara Tanzania Johnson Minja kufikishwa katika mahakama ya hakimu mkazi wilaya ya Dodoma akikabiliwa na kesi ya kudaiwa kushawishi wafanyabiashara kutenda kosa la jinai la kutolipa kodi na kudaiwa kuzuia ukusanyaji wa kodi kwa kutumia mashine za kodi za kielektroniki (EFD’s ), wafanyabiashara wa kati na wadogo zaidi ya 600 wenye

Afisa Elimu Mbinga avuliwa madaraka

$
0
0
BARAZA la madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma limemvua madaraka afisa elimu msingi wa wilaya hiyo Daniel Mkali baada ya kufanyiwa uchunguzi kwa muda kwa tuhuma mbalimbali zilizotajwa na baadhi ya madiwani pamoja na viongozi wa idara hiyo ya elimu msingi na kuelekea kutishia kuibuka kwa mgogoro wilayani humo.   Akitangaza uamuzi huo wa kumvua wadhifa huo pamoja na

Bunge lataka mawaziri wazembe wawajibike

$
0
0
Baadhi ya wabunge wamechachamaa na kuwashukia baadhi ya mawaziri na watendaji wa serikali kwa kuzembea katika utendaji wao jambo linalosababisha upotevu wa mabilioni ya shilingi na kulisababishia taifa hasara. Wabunge hao wameongeza pia kuwa umasikini na ugumu wa maisha kwa wananchi kwa kuongezewa kodi na tozo mbalimbali kunasababishwa na uzembe wa viongozi wachache wa serikalini.

Mume Amcharanga Mapanga Mkewe, kisa Kachelewa Kupata Ujauzito

$
0
0
Mtu mmoja mwanamume, aliyetajwa kwa jina la John Weghai amemjeruhi vibaya mke wake, Anastazia John (18) kwa kumkatakata na mapanga kwa kile kinachodaiwa kuchelewa kwake kupata ujauzito, katika maisha ya wawili hao waliyoanza Februari mwaka jana. Tukio hilo la kinyama lilitokea katika Kijiji cha Mariba, Kata ya Mriba, wilayani Tarime mkoani Mara na majeruhi huyo amelazwa katika

Unyama: Mume Amchinja Kikatili Mkewe ndani ya Hoteli jijini Dar......Ampasua mbavu na kutoa maini na Moyo

$
0
0
Huu ni ukatili namba moja kwa wanandoa duniani! Bado picha haijatoka kichwani kwa wakazi wa Manzese jijini Dar kufuatia kifo cha kuchinjwa cha  Josephine Ndengaleo Mushi kinachodaiwa kufanywa na mume wake wa ndoa, Remy Joseph (35). Tukio hilo la kutisha kusimuliwa achilia mbali kuona, lilijiri saa 9: 10 alasiri ya Januari 29, mwaka huu ndani ya chumba kimoja kilichopo ghorofa ya pili ya

Mahakama ya Kadhi bado "pasua kichwa"

$
0
0
Umoja wa Wainjilisti wa Kikisto Tanzania (Uwakita), umemtaka Waziri Mkuu, Mizengo Pinda (pichani) kuuondoa Muswada wa Mabadiliko ya Sheria vinginevyo utazunguka nchi nzima kuwahamasisha waumini wake kuipigia kura ya hapana Katiba Inayopendekezwa.   Wiki hii, Serikali inakusudia kuwasilisha bungeni muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria mbalimbali wa Mwaka 2014 unaopendekeza,

Kituo kingine cha polisi chavamiwa.....Majambazi Yapora Bunduki, Risasi 30 na vitu vingine kibao

$
0
0
Kundi la watu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi, wamevamia na kuvunja stoo ya Kituo kidogo cha Polisi Mngeta, Kilombero na kuiba bunduki aina ya SMG ikiwa na risasi 30.   Majambazi hao pia wanadaiwa kuiba jenereta, redio, viti, betri ya gari na spika ya redio.   Akizunguzia tukio hilo jana, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Leonard Paul alisema uporaji huo ulitokea usiku wa Februari

Serikali: "Tanesco haiwezi kushusha bei kwa sasa"

$
0
0
KUSHUKA kwa bei ya mafuta katika soko la dunia hakujawapa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) unafuu wa kuwafanya washushe bei ya umeme.   Aidha, serikali imesema haifumbii macho suala hilo na imeziagiza Mamlaka husika za Tanesco na Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (EWURA), kuangalia inapotokea fursa, ili iweze kwenda kwa wananchi.   Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles

Wajawazito wajifungulia sakafuni kijiji cha Msisi-Dodoma

$
0
0
WAJAWAZITO katika Kijiji cha Msisi wilayani Bahi, mkoani Dodoma wanajifungulia sakafuni kwenye jengo la wazi, hali inayosababisha kukosa faragha.   Kutokana na kadhia hiyo, Mkuu wa Wilaya hiyo, Betty Mkwasa ameahidi kutoa Sh 500,000 kwa ajili ya kuchangia ujenzi za chumba cha kujifungulia akinamama hao.   Hayo yalibainishwa hivi karibuni wakati wa kikao cha Baraza la Madiwani wa

Kupe Wakubwa Watumika kukabiliana na Ukeketaji

$
0
0
Wanawake  wa Kimasai wanaopinga suala la tohara kwa watoto wamegundua njia nyingine ya kukabiliana na ukeketaji kwa kutumia kupe wakubwa. Hayo yalielezwa katika warsha ya kujipanga kupokea mradi wa kijiji cha dijitali, iliyofanyika katika kijiji cha Ololosokwan hivi karibuni.   Wakijadili changamoto ya ukeketaji kama sehemu ya shida kubwa ya jamii kiafya, wanawake wamesema kwamba

Fedha Zakwamisha kukamilika Mradi wa DART

$
0
0
Mradi wa Mabasi yaendayo Haraka Dar es Salaam (DART) unakabiliwa na changamoto ya kifedha katika ujenzi wa miundombinu,  kutokana na ongezeko la mahitaji ya fedha za kuukamilisha. Bunge lilielezwa kwamba ongezeko la mahitaji ya fedha za kukamilisha mradi huo ni Sh bilioni 64.7, ambazo kati yake Sh bilioni 20.6 ni ongezeko la mishahara na Sh bilioni 44.1 ni ongezeko la kazi na madai

Kipindupindu chaua Watano Kigoma, 170 Taabani

$
0
0
Mlipuko wa kipindupindu ulioukumba mkoa wa Kigoma, umesababisha vifo vya watu watano, huku wengine zaidi ya 170 wakilazwa hospitalini. Hayo yalithibitishwa mjini hapa na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Leonard Subi (pichani) akisema Manispaa ya Kigoma/Ujiji imeathirika kwa kiasi kikubwa na ugonjwa huo, na kwamba tayari hatua mbalimbali zimechukuliwa kukabiliana na hali hiyo.   Alisema

Bei ya MAFUTA Yazidi Kuporomoka

$
0
0
Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), imetangaza kushuka zaidi kwa bei za bidhaa za mafuta hapa nchini kuanzia leo, kutokana na bei katika soko la dunia kuendelea kuporomoka. Mwezi uliopita, kwa mara ya kwanza baada ya muda mrefu, bei ya petroli, dizeli na mafuta ya taa ilishuka kwa kiasi kikubwa, mathalani bei ikifikia chini ya Sh 2,000. Na jana, bei ya juu kabisa ya

Bunge Lamshambulia Mkurugenzi wa Mashitaka Nchini (DPP) kwa kukwamisha Juhudi za TAKUKURU

$
0
0
Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka Nchini (DPP) imetajwa kudhoofisha juhudi za Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), kutokana na ama kuchelewesha au kutokutoa vibali vya kufikisha mahakamani kesi kwa makosa makubwa ya rushwa. Bunge limeambiwa kwamba gharama nyingi za serikali, zimekuwa zikitumika katika kufanya uchunguzi wa tuhuma za rushwa, lakini majalada yanapowasilishwa

Mwanasheria Mkuu wa Serikali amesema Mahakama ya Kadhi itakayoanzishwa Kisheria haitahudumiwa na Serikali.

$
0
0
Mwanasheria mkuu wa serikali Mh. George Masaju amesema mahakama ya kadhi itakayoanzishwa kisheria haitahudumiwa na serikali na itakuwa ya hiari kwa waumini wa dini ya kiislamu watakaoiridhia katika masuala ya ndoa, talaka, mirathi pamoja na wakfu na kutaka wanasiasa kuacha kukuza mijadala ya suala hilo kwa maslahi yao binafsi.   Akizungumza katika mahojiano maalum na vyombo vya habari

Polisi Tabora yamkamata mtuhumiwa sugu wa Ujambazi

$
0
0
Jeshi la polisi mkoani Tabora limefanikiwa kumkamata mtuhumiwa wa matukio ya uhalifu katika kata ya Ngambo manispaa ya Tabora, akiwa na risasi 356 za silaha za SMG/SAR, zinazosadikiwa kuwa, zilikuwa zitumike, katika matukio ya  uharifu katika mikoa ya Tabora, Kigoma, Mbeya, na Njombe.   Kaimu kamanda wa polisi mkoani Tabora ACP Juma Bwire amemtaja mtuhumiwa huyo kwa jina la Warfram

Shamsa Achukia Kuitwa Mshamba

$
0
0
Mrembo na mwigizaji wa filamu, Shamsa Ford amewabwatukia baadhi ya watu ambao wanapenda kumsema kuwa yeye ni mshamba kwa kushindwa kutoka misele nyakati za usiku.   Akizungumza na GPL, Shamsa alisema anawashangaa watu hao kumsema na kumjadili kwa watu wengine kuwa yeye ni mshamba kitu ambacho hakipendi kwani kila mtu ana aina yake ya maisha aliyoyachagua kuishi.   “Mimi sijawahi

Rais Kikwete Afichua SIRI Kipigo cha Lipumba.....Asema sheria za nchi lazima Zifuatwe

$
0
0
SIKU chache baada ya Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba na wafuasi wake kupigwa na polisi, Rais Jakaya Kikwete amesema tukio hilo limetokea kwa sababu nchi inaongozwa kwa sheria na atakayekiuka atakumbana na mkono wa sheria.   Rais Kikwete alitoa kauli hiyo jana Ikulu jijini Dar es Salaam, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari baada ya kufanya

Rugemalira wa IPTL sasa ‘mikononi’ mwa Takukuru

$
0
0
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) imesema imemhoji na inaendelea kumchunguza mmiliki mwenza wa zamani wa Kampuni ya Kufua Umeme ya Independent Power Tanzania Ltd (IPTL), James Rugemalira.   Akizungumza na Mwananchi jana, Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Dk Edward Hoseah alisema vigogo wote waliohusika na sakata la uchotwaji wa fedha katika Akaunti ya Tegeta Escrow, ya
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images