Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

EWURA yatakiwa kufanya upya ukokotoaji na kupunguza bei ya mafuta ili kumnusuru mwananchi wa kawaida

0
0
KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, imeitaka Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) kufanya ukokotoaji upya wa bei ya mafuta ili kumsaidia mlaji wa mwisho wa bidhaa hiyo kunufaika na punguzo la bei ya mafuta duniani.   Akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa shughuli za kamati hiyo, Mbunge wa Tandahimba, Juma Njwayo (CCM) kwa niaba ya mwenyekiti wa kamati hiyo

JWTZ yaapa kupambana na majambazi wanao pora silaha za askari

0
0
Jeshi la wananchi nchini (JWTZ) kwa kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama nchini limeahidi kukabiliana na makundi ya watu wanaodaiwa kuwa majambazi sugu ambao wanapora silaha za askari huku wengine wakiuawa hatua ambayo imeanza kutishia usalama wa nchi.    Akizungumza jijini Tanga kufuatia hivi karibuni makundi hayo kupora silaha na kisha kuua askari huko Rufiji mkoani Pwani na

"Tupige kura ya NDIYO Katiba inayopendekezwa"- Rais Kikwete

0
0
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Jakaya Kikwete amewataka watanzania wote kujitokeza na kuipigia Kura ya Ndiyo Katiba Inayopendekezwa muda utakapofika. Dkt Kikwete ameyasema hayo katika sherehe za maadhimisho ya miaka 38 ya chama hicho zilizofanyika katika uwanja wa Majimaji mjini Songea, ambapo amesema kuwa Katiba

Prof. Lipumba Awataka Wananchi Kutowachukia Polisi

0
0
Chama cha Wananchi CUF kimewataka wananchi kutowachukia polisi kufuatia kitendo cha kutotenda haki kwa raia ikiwemo kuwabambikizia kesi mbalimbali na kuwashushia vipigo bila sababu zozote. Hayo yalisemwa na mwenyekiti wa taifa wa chama hicho Profesa Ibrahim Lipumba alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari mapema jana  jijini Dar es Salaam.   Hata hivyo Profesa Lipumba amesema

Rais ajaye Asipotoka CCM Nchi Itayumba - Kikwete

0
0
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Dkt Jakaya Kikwete amewaagiza viongozi wa chama hicho kuhakikisha Chama cha Mapinduzi kinashinda katika uchaguzi ujao unaotarajiwa kufanyika mwezi Oktoba mwaka huu. Dkt Kikwete ametoa agizo hilo katika uwanja wa Majimaji mjini Songea ambapo zimefanyika sherehe za maadhimisho ya miaka 38 ya chama hicho.   Akimnukuu mwalimu Nyerere, amesema kuwa Rais

Mbowe Asimikwa UTEMI wa Kabila la Wasukuma.....Asisitiza msimamo wa CHADEMA Kutoshiriki Kupiga Kura Ya Maoni Katiba Mpya

0
0
Chama cha demokrasia na maendeleo (Chadema) kimesisitiza msimamo wake wa kutoshiriki kwenye mchakato wa kupiga kura ya maoni ya katiba mpya inayopendekezwa na badala yake kimewataka wanachama wake na watanzania kwa ujumla kuelekeza nguvu kwenye maandalizi ya uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwezi Oktoba mwaka huu.   Kikisisitiza msimamo huo uliotolewa hivi karibuni na

Hoteli Zafungwa Arusha kwa Kukosa Watalii

0
0
Baadhi ya hoteli za kitalii mjini Arusha zimefungwa, huku mishahara ya wafanyakazi ikipunguzwa kwa asilimia 25, kutokana na kukosa watalii. Akizungumza wakati wa tafrija ya kuukaribisha mwaka mpya 2015, zilizoandaliwa na Chama  cha Mawakala wa Watalii Nchini (TATO), Mwenyekiti wa chama hicho, Willy Chambulo alisema hali ya biashara kwa miezi hii mbaya na kusababisha kufungwa kwa  baadhi ya

Watanzania Wahimizwa Kula Mayai ya Kwale

0
0
Watanzania wamehimizwa kutumia mayai ya ndege aina ya kwale na nyama yake kwa kuwa ni chakula bora chenye virutubisho mbalimbali. Ushauri huo ulitolewa na mfugaji wa kwale ambaye ni mkazi wa Tegeta, Dar es Salaam, Susan Magibo alipokuwa akizungumza na Mpekuzi.   Magibo alisema ndege hao hivi sasa ni gumzo hapa nchini, kwani inasadikiwa kuwa ni dawa ya magonjwa mbalimbali kama pumu,

Wabunge Waomba Wanaume Wafungwe Kizazi

0
0
Wabunge wametaka kuwepo na udhibiti wa ongezeko la watu nchini kwa  kutaka wanaume wadhitibiwe katika uzazi, kama ilivyo kwa wanawake huku wengine wakitaka serikali kuboresha rasilimali bila kudhibiti uzazi. Miongoni mwa waliotaka wanaume wafungwe kizazi kama inavyofanyika kwa wanawake ni Mbunge wa Jimbo la Ulanga Mashariki, Celina Kombani ambaye pia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais

RUSHWA: Magufuli Awafukuza Kazi Wafanyakazi 400 wa Mizani, Asema huo ni mwanzo tu

0
0
Waziri wa Ujenzi Dk John Magufuli amevitaka vyombo vya dola kuingilia kati suala la rushwa kwenye vituo vya mizani za kupimia uzito wa magari yanayosafirisha mizigo, akisema rushwa hiyo imekithiri. Magufuli alitoa agizo hilo alipotembelea na kukagua kituo cha mizani cha Mpemba wilayani Momba, ambapo alipita kituoni hapo kwa kushtukiza, alipokuwa katika ziara yake ya kukagua barabara

Mahakama ya Kadhi, Ripoti ya Msola Kutikisa Bunge

0
0
Bunge linaendelea na mkutano wake wa 18, ambao kamati mbalimbali zitaendelea kuwasilisha taarifa kwa ajili ya majadiliano. Licha ya kamati za kisekta na zisizo za kisekta, kabla ya Bunge kuahirishwa wiki hii, pia Kamati Teule iliyoundwa kuchunguza na kuchambua Sera mbalimbali zinazohusu masuala ya ardhi, kilimo, mifugo, maji na uwekezaji kubaini kasoro zilizomo katika matumizi ya ardhi,

Wanafunzi wajawazito kuendelea na masomo wakijifungua

0
0
Serikali imeruhusu wanafunzi wa shule za msingi na sekondari waliopata ujauzito kuendelea na masomo wanapojifungua. Mratibu wa Masuala ya Jinsia wa  Wizara ya Elimu na Mafunzo ya  Ufundi, Chimpaye Marango, wakati wa mjadala wa sababu za kuongezeka kwa idadi ya watoto ya  mabinti wanaokosa elimu baada ya kupata mimba. Mjadala huo ulioitishwa na  asasi ya kiraia ya uchambuzi wa sera ya

Polisi achomoka lindo na bunduki kwenda Kuua Raia

0
0
Jeshi la Polisi Wilaya ya Ludewa mkoani Njombe, limeingia katika kashfa baada ya askari wake kutuhumiwa kumuua raia. Raia huyo ambaye ni mkazi wa mtaa wa Mdonga, fundi wa magari, Januari Mtitu (20), inadaiwa kuwa aliuawa kwa risasi na askari mwenye namba G 6352, Abduel Nyuki. Tukio hilo lilitokea Januari 23, mwaka huu, saa 7:00 usiku, na mtuhumiwa anafanya kazi katika Kituo cha Polisi

Mahabusu Afia Kituo cha Polisi Ubungo- Urafiki baada ya Kujitundika na Kunyinyonga

0
0
Mahabusu mmoja Shabani Ramadhani (28), amekutwa amejinyonga katika choo cha Kituo cha Polisi Ubungo- Urafiki, jijini Dar es Salaam. Tukio hilo lilitokea jana baada ya mahabusu huyo kufikishwa katika kituo hicho juzi akituhumiwa kufanya tukio la unyang’anyi. Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Augustino Senga, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kueleza kuwa marehemu

Je, unasumbuliwa na tatizo la nguvu za kiume?? Unataka kuimarisha mishipa yako ili uweze kwenda Raundi mbili na kuendelea??....Bofya hapa ukutane na JIKO

0
0
Neema  Herbalist  & Nutritional  Foods  Clinic  ni  wauzaji wa dawa  mbalimbali  za  asili. Tunapenda  kuwatangazia  wateja  wetu  kuwa  tunayo  dawa nzuri  ya  asili  inatibu na  kuponyesha  kabisa  tatizo  la ukosefu  na  upungufu  wa  nguvu  za  kiume.  Dawa  hii iitwayo  JIKO  ni  ya  asili  kabisa  (PURE HERBAL) na inaponyesha  na  kumaliza  kabisa  tatizo  la  nguvu  za kiume

Kanngi Lugola ( CCM ) Awasha moto bungeni.....Awataka wananchi Wasiichague CCM

0
0
MBUNGE wa Mwibara, Kangi Lugola (CCM), amewasha moto bungeni akifunguka kuwa atawaambia wananchi wake wasiipigie kura CCM pamoja na yeye mwenyewe kama maji hayatapatikana jimboni mwake wakati akichangia katika majiadiliano ya hoja za kamati bungeni leo.   Pia Lugola amehoji kwa nini nguvu zinazotumika kuwapiga watu kama akina Profesa Lipumba zisitumike kupambana na wawekezaji

Francis Cheka Ahukumiwa Miaka Mitatu Jela

0
0
Bondia maarufu nchini wa ngumi za kulipwa Francis Cheka amehukumiwa kifungo cha miaka 3 jela na kutakiwa kulipa fidia ya shilingi millioni 1 kwa kosa la kumpiga na kumjeruhi meneja wa baa yake iliyopo huko Morogoro Meneja huyo ajulikanaye kwa jina la Bahati inaelezwa alienda kudai fedha zake alizokuwa hajalipwa na bondia huyo wakati akifanya kazi ya umeneja katika baa yake hiyo ndipo

Zitto Kabwe Amtaka Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu AJIUZULU Ifikapo leo jioni

0
0
MBUNGE wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe amemtaka Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu ifikapo leo jioni awe ametoa tangazo katika gazeti la serikali ili kuruhusu tozo mpya za mahoteli kwenye hifadhi la sivyo ajiuzulu cheo chake. Zitto ameyasema hayo leo wakati akichangia kwenye majadiliano ya hoja za kamati bungeni.   Zitto amesema kuwa serikali inapoteza shilingi bilioni

Mahakama kuandika hukumu kwa Kiswahili

0
0
WIZARA ya Katiba na Sheria imesema iko haja ya hukumu zinazotolewa katika Mahakama nchini, ziandikwe katika Kiswahili kuwezesha haki kutendeka na ionekane imetendeka.   Naibu Waziri, Ummy Mwalimu alisema hayo jana wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu, Amina Mwidau (CUF) aliyeshauri serikali kuangalia uwezekano wa hukumu kutolewa kwa lugha hiyo.   “Ni kweli kwamba kuna haja

"Mabilioni" ya Kikwete bado hayajarejeshwa

0
0
FEDHA zilizotolewa na serikali kwa ajili ya kuwezesha wananchi kiuchumi maarufu kama mabilioni ya Kikwete, imeelezwa sehemu hazikutumika huku nyingine zilizokopwa hadi sasa hazijarejeshwa.   Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Uwekezaji na Uwezeshaji, Christopher Chiza alitoa taarifa hiyo jana bungeni wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Viti Maalumu, Maryam Salumu Msabaha (Chadema).
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images