Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Serikali Kupitia Kwa Waziri wa Fedha Dokta Mpango Yaiomba AFDB Kujenga Barabara Njia Nne Morogoro Hadi Dodoma

$
0
0
Na Benny Mwaipaja, Dodoma
WAZIRI wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango ameiomba Benki ya Maendeleo ya Afrika kuipatia Tanzania mkopo nafuu kwa ajii ya kujenga barabara ya njia Nne kuanzia Morogoro hadi Dodoma ili kuboresha usafiri na usafirishaji wa abiria na mizigo

Dkt. Mpango ametoa ombi hili Jijini Dodoma alipokutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Wakurugenzi ya Benki hiyo anayewakilisha nchi nane za ukanda wa Afrika Mashariki Bw. Amos Cheptoo.

“Barabara hii ilijengwa muda mrefu miaka ya 80, malori mengi yanapita hapa kwenda Mwanza, Kigoma na nje ya nchi ikiwemo Burundi, Rwanda, na unaona kabisa imeelemewa na imeanza kuharibika” Alisema Dkt. Mpango

Alisema amemwomba Mkurugenzi Mtendaji huyo wa AfDB waanze kuliweka jambo hili kwenye miradi itakayogharimiwa na Benki hiyo baadae ili barabara hiyo itakayo kuwa na uwezo wa kuelekeza magari mawili kwenda upande mmoja na mengine mawili kupita upande mwingine iweze kujengwa.

“Baada ya Dodoma kuwa Makao Makuu ya nchi, tunahitaji usafirishaji kwa njia ya barabara uwe na tija zaidi, uende haraka zaidi lakini pia kupunguza ajali. Hivi sasa kuna ajali nyingi sana kwa sababu magari yanayokwenda Dar es Salaam na yanayokuja Dodoma au kwenda Mwanza yanapishana kwenye haka kanjia kamoja” alisisitiza Dkt. Mpango

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji huyo wa Bodi ya Wakurugenzi ya Benki ya Maendeleo ya Afrika Bw. Amos Cheptoo aliyeko nchini kwa ziara ya kikazi ya siku mbili, alisema Benki yake itahakikisha Tanzania inapata mikopo ya miradi yake ya kimkakati na ya kipaumbele ukiwemo huo wa barabara ya Morogoro hadi Dodoma.

Katika hatua nyingine Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika- AfDB, Bw. Cheptoo Amos Kipronoh, ameitaka Sekta Binafsi nchini Tanzania kuchangamkia fursa za mikopo nafuu zilizopo katika Benki hiyo.

Bw. Kipronoh alisema kuwa Sekta Binafsi nchini Tanzania ina nafasi nzuri ya kupata mikopo na utaalam utakaoiwezesha kujikwamua kiuchumi kwa lengo la kutokomeza umasikini katika Bara la Afrika.

“Sekta Binafsi hapa Tanzania haijatumia vizuri dirisha la mikopo ya Sekta hiyo ikilinganishwa nan chi nyingine za ukanda huu wa Afrika na ninakuomba Mhe. Waziri wa Fedha na Mipango uihamasishe Sekta Binafsi ikope fedha hizo ili kukuza mitaji yao na kuongeza tija” alisema Bw. Cheptoo

Aidha, alisema kuwa Benki ya AfDB ipo katika hatua za mwisho za kutoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Msalato Dodoma na tayari benki hiyo imetoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa barabara za mzunguko mjini Dodoma pamoja na miradi mipya ya kuzalisha Nishati ya umeme ambayo iko mbioni kuwasilishwa katika vikao vya Bodi ya Benki hiyo hivi karibuni.

Mkurugenzi huyo amempongeza Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli, kwa kuwa kiongozi mwenye maono ambaye amesaidia katika mabadiliko makubwa ya  uchumi na kuzitaka nchi nyingine barani Afrika kujifunza kutoka Tanzania.

“Nilipotua nimeona jengo la abiria la III katika Uwanja wa Ndege  wa Kimataifa wa Julius Nyerere, daraja la juu la Mfugale na ujenzi wa Reli ya Kisasa unaoendelea kwa kasi, miundombinu ambayo miaka miwili iliyopita sikuikuta nilipotembelea hapa nchini” alisema Bw. Cheptoo.

Aidha, amempongeza Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango kwa kusimamia na kuhakikisha uchumi unaendelea kuwa imara ikiwa ni moja ya lengo la Benki hiyo katika jitihada za kuifanya Afrika kuwa na uchumi imara.

Kwa upande Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango, amewataka watanzania kujivunia hatua za maendeleo zinazoonekana kwa kuwa hata wageni wanaona mabadiliko makubwa ya kiuchumi nchini.

Ameishukuru Benki ya AfDB kwa kukubali kufadhili miradi ya barabara za mzunguko Jijini Dodoma na pia miradi mbalimbali ya kilimo ambayo inaajiri watu wengi, huku akibainisha kuwa kwa kipindi cha miaka minne miradi mbalimbali imetekelezwa kwa msaada wa AfDB na kuifanya Tanzania kukua kwa kasi kiuchumi.

Dkt. Mpango amewataka watendaji wa Wizara yake kuhakikisha wanawakutanisha viongozi wa Sekta Binafsi na Watendaji hao wa AfDB kabla ya kumaliza ziara yao nchini, ili kufanya mazungumzo yatakayosaidia kutumia fursa zilizopo katika Benki hiyo.

Aidha, Dkt. Mpango amewataka watanzania wenye vigezo kuchangamkia nafasi mbalimbali za kazi zinazotangazwa katika Benki hiyo ili kuongeza uwakilishi wa wananchi hasa kutoka Afrika Mashariki, ikizingatiwa nafasi zinazotangazwa ni za ushindani.

Benki ya Maendeleo ya Afrika-AfDB imefadhili miradi 23 hapa nchini ikiwemo miradi 21 ya umma na miwili ya Sekta Binafsi, katika Nyanja za Nishati, miundombinu ya barabara, usafiri, kilimo, maji na usafi wa mazingira, yote kwa pamoja ikiwa na thamani ya dola za Marekani bilioni 2 nuta 1

MWISHO

TAKUKURU Mkoa Wa Dodoma Yawakamata Viongozi Watatu Chama Cha Ushirika Matumaini Saccos .

$
0
0
Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa [TAKUKURU]mkoa wa Dodoma  inawashikilia  watu watatu waliokuwa viongozi   wa chama cha Ushirika cha Akiba na Mikopo  cha Matumaini[Matumaini SACCOS] Kilichopo kata ya Msanga Wilaya ya Chamwino  kwa kosa la matumizi mabaya ya Mamlaka  kinyume na kifungu cha 31 cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa  sura ya 329  Marejeo ya 2018.
 
Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Nov.19,2019 Ofisini kwake,Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Dodoma Bw.Sosthenes Kibwengo amewataja  ,Watuhumiwa hao kuwa ni Bw.Charles Yohana Chilongani mwenye Umri wa miaka 51 ambaye alikuwa meneja ,Bw.Isaya Noah Chigalila [54]ambaye alikuwa Mhasibu  na Bi.Mwanahamis Moshi Kaisi [33] ambaye alikuwa karani wa SACCOS hiyo  ,wote wakazi wa kata ya Msanga Chamwino .
 
Bw.Kibwengo amesema uchunguzi wa TAKUKURU Umeonesha kuwa kati ya Mwaka 2011 na 2013  kwa pamoja walichakata   bila kupata idhini ya Mrajisi wa vyama vya Ushirika na kuwezesha SACCOS hiyo kupata bila kustahili mkopo wa Tsh.Milioni mia moja arobaini na nane[148,000,000/=] kutoka benki ya Uwekezaji Tanzania [TIB] Kinyume na Matakwa ya Sheria  ya vyama vya Ushirika  Na.20 ya Mwaka 2003  na kanuni zake za Mwaka 2004.
 
Katika hatua nyingine Bw.Kibwengo amesema TAKUKURU Kwa Kushirikiana na Ofisi ya Mashtaka ya Taifa Mkoa wa Dodoma leo Nov.19,2019 itamfikisha Mahakamani Bw.Ibrahim Hassan Kahogo  mwenye umri wa Miaka arobaini na tatu[43] mkazi wa Area A jijini Dodoma kwa Makosa ya Kughushi ,kujifanya mtu Mwingine ,kutoa taarifa za Uongo  yote yakiwa ni kinyume cha sharia ya kanuni za Adhabu  Sura ya 16 marejeo ya Mwaka 2002.

Mkuu huyo wa TAKUKURU amesema Ofisi yake ilipokea taarifa Mwezi Juni 2019 kwamba Mtuhumiwa akiwa katika ofisi za Kamishina  wa Kazi jijini Dodoma alitumia njia za Udanganyifu ili kumwezesha kuomba na kuchukua vibali vya kufanya kazi[working Permits]kwa wageni ambao wameajiriwa  na Taasisi ya One Acre Fund ya Mjini Iringa.
 
“Uchunguzi wetu umethibitisha kwamba Mtuhumiwa alighushi nyaraka mbalimbali zikiwemo barua na vitambulisho na kujifanya ni mwajiriwa wa kampuni hiyo na kwamba ana ridhaa yao ya kufuatilia vibali hivyo kwa ajili ya waajiriwa wa kigeni,jambo ambalo sio kweli.Uchunguzi umebaini pia kwamba ,mtuhumiwa amekuwa mara kwa mara akitumia vitambulisho vyenye picha yake  na majina ya watumishi wa Taasisi hiyo  kudanganya na kumwezesha kupata huduma  katika ofisi ya Kamishina wa Kazi”amesema Bw.Kibwengo.
 
Pia Bw.Kibwengo amesema  Mahakama ya Wilaya Ya Kondoa jana Nov.17,2019 ,imetoa hukumu  ya shauri la jinai Na.101/2019 na kuwatia hatiani washtakiwa wawili ambao ni Bw.Shaban Maulid Simpi aliyekuwa Mwenyekiti wa kijiji cha Soera na Bw.Abdi Ramadhani Tutupa ambaye ni diwani wa kata ya Soera wilaya ya Kondoa katika makosa ya matumizi mabaya ya Mamlaka na Ubadhilifu  kinyume  na Sheria ya kuzuia na kupambana na Rushwa  Sura 329 Marejeo ya 2018.
 
Bw.Kibwengo amesema TAKUKURU iliwafikisha Washtakiwa hao mahakamani hapo Mwezi Machi,2019 na kuwafungulia mashtaka matatu  baada ya  uchunguzi wa Ofisi ya TAKUKURU kuonesha kuwa walitumia madaraka yao vibaya  kwa kuingia mkataba na kampuni ya China Railway Seventh Group iliyokuwa ikitengeneza barabara ya Kondoa-Bonga kwa ajili ya kupata eneo la kuchimba mawe  pasipo kushirikisha serikali ya Kijiji,na baadaye kufanya ubadhilifu  wa Tsh.Milioni moja ,laki tisa na sabini na nne elfu[1,974,000/=] walizopokea kutoka kampuni hiyo.
 
Mkuu huyo wa TAKUKURU ameendelea kufafanua kuwa,Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Kondoa Mhe.Masao amemtia hatiani Mshitakiwa  Simpi katika Makosa yote matatu  na kumhukumu kifungo cha Miaka mitatu jela kwa makosa yote  au kulipa faini ya Tsh.Laki tisa[900,000/=] huku akitakiwa kulipa Tsh.1,974,000/=alizofuja.
 
Bw.Tutupa alishtakiwa katika Makosa mawili  na ametiwa hatiani kwenye kosa moja  na kuhukumiwa kwenda jela mwaka mmoja  au kulipa faini ya Tsh.laki tatu[300,000/=]
 
Sanjari na hayo Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Dodoma Bw.Sosthenes Kibwengo amesema TAKUKURU inaendelea kuwaasa wananchi kuwa,rushwa ni adui wa Haki na Maendeleo hivyo waendelee kushiriki kwa vitendo  kuikataa na kuikemea.
 
Aidha,Bw.Kibwengo ameitaka jamii kutumia Fursa ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa kuchagua viongozi wanaoichukia rushwa kwa Matendo yao ili wawe chachu ya Maendeleo .

Uteuzi Mpya Uliofanywa na Rais Magufuli Leo

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Dkt. Buruhani Salum Nyenzi kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA).

Dkt. Nyenzi (Tanzania Bara) anashika wadhifa huo kwa kipindi cha pili.

Wakati huo huo, Rais Magufuli amemteua Dkt. Makame Omar Makame kuwa Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya TMA.

Dkt. Makame (Zanzibar) ni Mhadhiri Mwandamizi wa Jiografia katika Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA).

Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi imeeleza kuwa uteuzi wa viongozi hao umeanza tarehe 18 Novemba, 2019.

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumatano November 20

Rais Magufuli Kuanza Ziara Dodoma Kesho

$
0
0
ZIARA YA KIKAZI YA MHE. DKT. JOHN POMBE JOSEPH MAGUFULI RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MKOANI DODOMA

Ndg. Waandishi wa Habari
Natumia fursa hii kuwatangazia wananchi wote wa Mkoa wa Dodoma na umma wa Tanzania kuwa, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, imempendeza kufanya ziara ya kikazi katika Mkoa wa Dodoma, Makao Makuu ya nchi, kuanzia tarehe 21 hadi 25 Novemba, 2019.

Katika ziara yake Mkoani Dodoma, Mhe. Rais atatembelea miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa kwenye Mkoa wa Dodoma. Vilevile, atatumia ziara yake kuzungumza na wananchi wa Mkoa wa Dodoma na Watanzania kwa ujumla kupitia Mikutano kadhaa ya hadhara ambayo  hotuba hizo zitarushwa moja kwa moja (mubashara) kupitia vyombo vya habari na mitandao ya kijamii.

Ndg. Waandishi wa Habari

Miongoni mwa shughuli atakazofanya ni kama ifuatavyo:-

Alhamisi Novemba 21, 2019, Mhe. Rais atakuwa ni Mgeni Rasmi katika Mahafali ya kumi (10) ya Chuo Kikuu cha Dodoma – UDOM yatakayofanyika kwenye ukumbi wa Chimwaga, Chuoni hapo.
 
Ijumaa Novemba 22, 2019 Mhe. Rais atatembelea na kuweka mawe ya msingi kwenye miradi ya Hospitali ya Uhuru, Wilayani Chamwino; ujenzi wa nyumba 118 za Askari Polisi katika maeneo ya FFU Nzuguni na Medeli East; Ujenzi wa Stendi Kuu ya mabasi iliyopo Nzuguni; na Soko Kuu linalojengwa katika eneo la Nzuguni na kuzungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara utakaofanyika katika stendi ya mabasi Nzuguni. 
 
Jumatatu Novemba 25, 2019 Mhe. Rais ataweka mawe ya msingi kwenye miradi ya ujenzi wa Makao Makuu ya Jeshi la Wananchi Tanzania Kikombo; ujenzi wa Ofisi ya Makao Makuu ya Idara ya Uhamiaji na Ujenzi wa jengo la Makandarasi katika eneo la National Capital City.

Ndg. Waandishi wa Habari

Maandalizi yote yamekamilika na Sisi wana Dodoma, kama ilivyo kwa watanzania wote, tunaelewa fika wingi na uzito wa majukumu aliyonayo Mhe. Rais ya kujenga Tanzania mpya na yenye matumaini makubwa kimaendeleo na ustawi wa Jamii. Hivyo, kupata nafasi ya kufanya ziara kwenye Mkoa wa Dodoma, licha ya majukumu hayo, ni upendeleo usiokuwa na kifani. Hivyo kwa niaba ya wananchi wa Mkoa wa Dodoma, nitumie fursa hii kumshukuru sana Mhe. Rais kwa upendeleo anaotupatia daima.

Ziara hii ya Mhe. Rais kwetu ni fursa ya kumwonesha hatua tulizofikia katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo aliyotupatia na kupokea maelekezo ya namna ya kusonga mbele kwa uhakika katika hatua mbalimbali za utekelezaji wake. Aidha, atatumia ujio huu kuelekeza yale atakayoona kuwa yatazidi kuboresha utendaji wetu na yatakayotupa shime na hamasa zaidi ya kusonga mbele zaidi kimaendeleo. Hivyo, wananchi wa Dodoma tujitokeze kwa wingi kuungana na Rais wetu mpendwa na hivyo, kufanikisha ziara yake.

AHSANTENI SANA KWA KUNISIKILIZA!

Dkt. Binilith S. Mahenge
MKUU WA MKOA
NOVEMBA 20, 2019

Rais Magufuli: Watu wanataka kusajili laini zao lakini zoezi la vitambulisho linacheleweshwa

$
0
0
Rais Magufuli amemuagiza Mkurugenzi Mkuu wa NIDA kufika Mkoani Morogoro leo na ikiwezekana akae Mkoani humo hata siku tatu ili kushughulikia tatizo la Watu wengi kukosa vitambulisho vya Taifa huku Mkoa mzima ukiwa na Ofisi moja pekee ya NIDA.

Rais Magufuli ametoa agizo hilo akiongea na wananchi wa Msamvu, Morogoro akiwa njiani akielekea mkoani Dodoma

“Nimemtaka Mkurugenzi Mkuu NIDA afike hapa Morogoro ashughulikie hii changamoto ya vitambulisho na nataka huduma hii iende kila Wilaya, haiwezekani Watu wasafiri kutoka Wilayani kuja Mjini au muwape nauli na hela ya Gesti,na hili litazamwe Nchi nzima Watu wapewe vitambulisho” amesema.

"Watu wanataka kusajili laini zao za simu na mambo mengine lakini zoezi la vitambulisho linacheleweshwa na Watu wachache, suala la NIDA linaenda polepole sana, Mkurugenzi Mkuu wa NIDA nitahitaji unipe na tathmini ya zoezi lote Nchi nzima".

Aidha, Rais Magufuli amesisitiza kuwa katika kipindi chake cha uongozi hatopanga bei ya mkulima kuuza mazao yake.

“Wengine wanalalamikia bei ya mahindi kupanda, nataka wakulima washangilie kama bei ya mahindi imepanda, biashara hii lazima iwe huru, bei ya mahindi itajipanga yenyewe, wakati wa kuwapangia bei wakulima kwenye mazao yao umekwisha,” amesema Rais Magufuli.

Amnesty: Zaidi ya waandamanaji 100 wameuwawa Iran

$
0
0
Shirika la Kutetea Haki za Binadamu la Amnesty International limesema zaidi ya watu 100 wameuwawa kwenye miji 21 nchini Iran wakati wa machafuko yaliyozuka wiki iliyopita kupinga kupanda kwa bei ya mafuta.

Katika taarifa iliyochapishwa jana, shirika hilo limesema polisi wa kulenga shabaha walifyetua risasi kuelekea makundi ya waandamanaji kutoka juu ya majengo na katika kisa kimoja kutoka ndani ya helikopta.

Shirika hilo lenye makao yake mjini London limesema taarifa yake ni kutoka duru za kuaminika na vyanzo vingine ikiwemo mashuhuda, kanda za video na maelezo ya watetezi wa haki za raia.

Amnesty imesema vikosi vya polisi na intelejensia havikurudisha miili ya waliuwawa kwa familia zao na vimelazimisha baadhi ya miili kuzikwa haraka bila kufanyiwa uchunguzi wa kitababu.

Taarifa hiyo imefichua jinsi vikosi vya usalama nchini Iran vinavyoendesha mauaji ya raia kinyume na sheria ikiwa ni pamoja na kutumia mbinu katili na nguvu iliyopindukia.

Raha Behreini, ambaye ni mwanasheria na mtafiti wa Amnesty International amesema "Mamlaka za Iran zina historia ya kutumia ukatili na nguvu kubwa dhidi ya wale wanatimiza haki yao ya kujieleza na kuandamana kwa amani. Hata hivyo inaonekana mara hii, wamezidisha zaidi ukandamizajai kwa sababu hawataki maandamano hayo yawe makubwa"

Iran yenyewe haijatoa taarifa ya idadi ya watu waliokamatwa, kujeruhiwa au kuuliwa wakati wamaandamano hayo yaliyosambaa haraka kwenye karibu majiji na miji 100.

Mamlaka nchini humo zimezima huduma za mtandao wa intaneti tangu siku ya Jumamosi na hali hiyo imeendelea hadi jana jumanne.

Kukosekana kwa upatikanaji taarifa kumevifanya vyombo vya habari vya Iran na maafisa wa nchi hiyo pekee kuwa na uwezo wa kutoa taarifa kuhusu kinachoendelea.

Afisa mmoja nchini Iran amesema maandamano hayo yamepungua nguvu baada ya kikosi cha ulinzi wa mapinduzi cha jeshi la Iran kutishia kuchukua hatua kali iwapo yataendelea.

Credit:DW

Nafasi 37 za Kazi Tanzania Institute of Accountancy (TIA) | Deadline 29 November 2019

$
0
0
The Tanzania Institute of Accountancy (TIA) is an Executive Agency under the Ministry of Finance and Planning which was established on 1st July, 2002 by the Government Notice No. 489 of 1st November, 2001 and officially launched on 24th January, 2002 as per Act No. 30 of 1997.

As an Executive Agency, TIA is operating ‘semi’ autonomously and commercially in providing quality education in the field of Accountancy, Procurement & Supplies and other Business related disciplines so as to become a self-sustainable Institute. TIA is accredited by NACTE as an Institute of Higher Learning Education.

The Institute is looking for qualified and dedicated personnel to fill the post of Tutorial Assistants on contract basis. The table below provides details on a particular fields/ professionals one should apply against.

==>>Kujua Namna Ya Kutuma Maombi;<< Ingia Ha>>



Makusanyo Kodi Ya Ardhi Gairo Hayamfurahishi Naibu Waziri Mabula

$
0
0
Na Munir Shemweta, WANMM GAIRO
Kasi ndogo ya ukusanyaji mapato ya Kodi ya pango la ardhi katika halmashauri ya wilaya ya Gairo mkoa wa Morogoro imemsononesha Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ta Makazi Dkt Angeline Mabula na kuagiza halmashauri hiyo kuongeza kasi ili kufikia lengo la mapato ya kodi ya ardhi.

Akiwa katika ziara yake ya siku moja katika wilaya hiyo jana tarehe 19 Novemba 2019 Dkt Mabula alielezwa na Afisa Ardhi katika halmashauri ya Gairo Nicolaus Matsuva kuwa halmashauri hiyo katika kipindi cha mwaka 2018/2019 imekusanya shilingi milioni 12.3 na mwaka huu kufikia Novemba imekusanya milioni 10 ya kiwango ilichopangiwa cha milioni 55.

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi alisema, kiwango hicho cha makusanyo katika halmashauri ya Gairo ni kidogo na hakijafikia hata nusu ya makadirio ya shilingi milioni 55 iliyowekewa halmashauri hiyo kukusanya kwa mwaka na makadirio hayo hayalingani na uhalisia wa makusanyo ya halmashauri.

Aliitaka halmashauri ya Gairo kupitia idara yake ya ardhi kuongeza kasi ya makusanyo ya maduhuli ya kodi ya pango la ardhi kwa kuwa kodi hiyo ndiyo inayoisaidia serikali kutekeleza miradi mikubwa aliyoieleza kuwa mingi inataegemea kodi ya ndani.

‘’Msipokusanya kodi ya ardhi mjue mnamkwamisha Mhe Rais kutekeza miradi mikubwa kama vile mradi wa kufufua umeme wa Mwl. Nyerere maarufu kama stiglers hivyo ni lazima tuongeze kasi ya makusanyao’’ alisema Dkt Mabula.

Sambamba na hilo Dkt Mabula aliitaka halmashauri ya wilaya ya Gairo kuhakikisha kufikia Desemba 2019 inarejesha fedha shilingi milioni 31 ilizopatiwa mwezi Juni 2019 kama mkopo kwa ajili ya upimaji viwanja katika halmashauri hiyo.

Hatua hiyo inafuatiwa Naibu Waziri Mabula kuhoji kuhusiana na marejesho ya fedha za mkopo huo na kuelezwa na Afisa Ardhi kuwa, halmashauri hiyo hajarejesha kiasi chochote cha fedha za mkopo iliopatiwa kwa ajili ya upimaji viwanja na kuomba kuongezewa muda wa kurejesha hadi mwezi Machi 2019.

‘’ Toka mwezi Juni hadi leo Desemba hamjarejesha wakati ulitakiwa kurejeshwa ndani ya miezi mitatu, Mkopo huu unazunguka kwa nini hamjarejesha hadi leo? Kazi mliyopewa hamjamaliza naagiza hadi kufikia Desemba fedha hiyo iwe imerejeshwa’’ alisema Mabula.

Aidha, Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi ameshangazwa na idara ya ardhi katika halmashauri ya Gairo kuingiza viwanja 155 kati ya 1,198 kwenye mfumo wa makusanyo ya kodi ya ardhi kwa njia ya kielektroniki jambo alilolieleza linaikosesha serikali mapato yataokanayo na kodi ya pango la ardhi sambamba na kushindwa kutoa ilani kwa wadaiwa sugu wa kodi ya ardhi ingawa ilani hizo zilizndaliwa tangu mwezi Machi 2019.

Dkt Mabula alielezwa na Afisa Ardhi wa Halmashauri ya wilaya ya Gairo Nicolaus Matsuva kuwa, baadhi ya wadaiwa sugu wa kodi ya ardhi walishindwa kupatiwa ilani hizo kutokana na maeneo wanayomiliki kukutwa wakiishi watu wengine tofauti na wamiliki waliopo kwenye kumbukumbu zao jambo lilimfanya Naibu Waziri kumuagiza Kaimu Kamishna wa Ardhi Msaidizi Kanda Maalum ya Morogoro Erick Makundi kufuatilia suala hilo kwa kwenda uwandani na kupatiwa taarifa kufikia Desemba mwaka huu.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Gairo Sirieli Mchembe alisema, wilaya yake ina changamoto kubwa ya ujenzi holela na kubainisha kuwa hata zoezi la urasimishaji katika wilaya hiyo linakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo sebule za baadhi ya nyumba kuelekezwa kwenye vyoo vya nyumba nyingine.

Hata hivyo, alimuahidi Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi kuwa ofisi yake itayafanyia kazi maagizo yote aliyoyatoa ikiwemo uandaaji wa Mpango Kabambe katika wilaya hiyo iweze kupangika kimji sambamba na kuwa na Mji wa Serikali utakaojumuisha taasisi zote za serikali zilizopo katika wilaya hiyo.

Ktika hatua nyingine Naibu Waziri wa Ardhi nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula alitembelea hifadhi ya Msitu wa Ukaguru uliopo Tarafa ya Nongwe kata ya Mandege wilaya ya Gairo mkoa wa Morogoro na kukagua maendeleo ya ujenzi wa nyumba na ofisi za Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) unaofanywa na Shirika la nyumba la Taifa (NHC).

Akiwa kwenye ukaguzi wa ujezi huo, Dkt Mabula alipata malalamiko ya baadhi ya vibarua wanaojenga ofisi hiyo kutopatiwa malipo kwa wakati jambo walilolieleza kuwa linawakatisha tamaa kuendelea na kazi hiyo. Hata hivyo, Naibu Waziri Mabula aliwataka vibarua hao kuendelea kufanya kazi kwa bidii na kuahidi kulifuatialia suala hilo haraka ili vibarua hao walipwe fedha kwa wakati.

Aidha, Dkt Mabula alipata fursa ya kutembelea Maporomoko katika hifadhi ya shamba la Miti la Ukaguru ambapo alijionea namna eneo hilo linavyoweza kuwa moja ya vyanzo vya umeme sambamba na kuwa kivutio kikubwa cha utalii kinachoweza kuingizia serikali mapato yatokanayo na sekta hiyo.

Mkuu wa Wilaya ya Gairo Sirieli Mchembe alielezea ziara ya Naibu Waziri Mabula kwenye Maromoko hayo kuwa ni ya kwanza kufanywa na Waziri na kubainisha kuwa ziara hiyo inaweza kuwa chachu ya hifadhi ya Msitu huo kutumika kwa shughuli mbalimbali kama vile za kitalii.

Wabunge Wanne CHADEMA Wanusurika Kwenda Gerezani....Mahakama Yawapa Onyo

$
0
0
Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche, Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa, Mbunge wa Kawe, Halima Mdee na Mbunge wa Bunda, Esther Bulaya wamenusurika kwenda gerezani baada ya mahakama kuridhia ombi la kutowafutia dhamana zao.

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba leo Jumatano Novemba 20, saa saba mchana imetoa uamuzi kuhusu maombi ya Jamhuri ya kutaka washtakiwa hao wafutiwe dhamana kwa kushindwa kufika Mahakamani Novemba 15 mwaka huu.

“Baada ya kupitia hoja za pande zote mbili na hoja za washtakiwa mahakama inaona kwamba maelezo yao hayana mashiko na kuwafutia dhamana ni hatua kali sana badala yake mahakama inawapa onyo kali wasirudie tena,” amesema Hakimu Simba.

Hakimu Simba amesema walifanya makusudi na kwamba hatua ya kujisalimisha polisi ni uoga wa jambo ambalo lingewatokea.

Kutokana na hali hiyo, amesema mahakama imewaachia kwa dhamana zao za awali na kuwataka wafuate masharti ya dhamana ya kuwa na wadhamini wawili.

Katika kesi ya msingi, washtakiwa hao wanadaiwa kuwa kati ya Februari Mosi na Februari 16, mwaka huu Mbowe na wenzake wakiwa Kinondoni, Dar es Salaam kwa pamoja walikula njama na  wengine ambao hawapo mahakamani ya kutenda kosa la jinai ikiwamo kuendelea na mkusanyiko isivyo halali na kusababisha chuki na uchochezi wa uasi.

Infinix YAZINDUA Infinix S5 SIMU YA KWANZA YENYE 32 CLEAR SELFIE NA Infinity-O Display.

$
0
0
Infinix YAZINDUA Infinix S5 SIMU YA KWANZA YENYE 32 CLEAR SELFIE NA Infinity-O Display.

Infinix, baada ya kuliteka soko na toleo pendwa la Infinix S4, Infinix imezindua rasmi Infinix S5, kinamara wa toleo la S series kwa sasa ikiwa na Infinity-O Display na 32MP. Ujio wa Infinix S5 umeambatana msimu wa sikukuu za Christmas na Mwaka mpya hivyo Infinix kusheherekea msimu huu kwa kuzindua rasmi promotion itayoanza rasmi tarehe 25/11/2019 na zawadi mbalimbali kama vile Vacuum Cleaner, Deep Flyer, Subwoofer Radio. 
 
Akizungumza na vyombo vya habari wakati wa uzinduzi wa Infinix S5, Afisa wa mahusino wa kampuni ya Infinix, Aisha Karupa alisema, “Infinix ikiwa ni kampuni yenye ushawishi mkubwa katika mfumo wa kidigitali tunawahakikishia wateja wetu bidhaa zenye teknolojia ya hali ya juu kwa bei Rafiki”,
 
Vile vile Aisha aligusia kuhusiana na sifa za simu hiyo kwa kusema, “na pamoja ya kuwa na selfie kali yenye 32MP lakini pia inasifa lukuki kama vile teknolojia ya Artifficial Intelligence kwenye kamera 4 za nyuma ambazo ni 16MP+5MP+2MP+AI Lens, lakini pia Infinix S5 ina memory card ya ukubwa wa GB 4  kwa GB64 yenye uwezo wa kutunza kumbukumbu nyingi pasipo huitaji ya memory card ya ziada na kwa upande wa design Infinix S5 imekuja katika muonekano wa kitofauti wenye kuvutia kutokana na namna kamera ya mbele ilivyopachikwa ndani ya Display kwa jina la kitaalamu Infinity-O Display  na kwa wale wenye matumizi mengi Infinix S4 inauwezo wa kukaa na chaji kwa muda mrefu kutokana na ujazo mkubwa wa Battery wenye mAh40,000”.
 
Pia Infinix wametumia nafasi hiyo kutambulisha rasmi promotion ya msimu wa sikukuu inayoenda sambamba na uzinduzi wa Infinix S5. 

Akizungumza meneja wa mauzo wa Infinix Bwana Fredy Kadilana alisema kwamba, katika msimu huu wa sikukuu za Christmas na mwaka mpya Infinix imezindua rasmi promotion itakayompa nafasi mteja wa Infinix S5 au mteja wa simu yoyote ya Infinix kujishindia zawadi mbalimbali kama vile Vacuum Cleaner, Deep Flyer, Subwoofer Radio na nyengine nyingi lakini pia Infinix haijasahau wadau wake wa wanaotembelea kurasa @infinixmobiletz kwa kuitambulisha challenge ya #S5showitoff itayoanza rasmi mwishoni mwa wiki hii”.
 
Kwa maelezo zaidi tembelea www.infinixmobility.com

Rais Magufuli Kutunukiwa shahada ya heshima ya udaktari wa falsafa na Chuo Kikuu cha Dodoma Kesho

$
0
0
Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) kesho kitamtunukia Rais Dk. John Magufuli Shahada ya Heshima ya Daktari wa Falsafa (Honorary PhD) kwa uongozi wake hususani katika ujenzi wa uchumi wa viwanda, kuwekeza kwenye elimu, miundombinu, kuimarisha utawala bora, na mapambano dhidi ya rushwa.

Akizungumza leo Jumatano Novemba 20, 2019 makamu mkuu wa chuo hicho, Profesa Faustine Bee amesema shahada hiyo itatolewa kesho katika mahafali ya 10 ya chuo hicho.
 
Profesa Bee amesema wahitimu 6,488 watatunukiwa astashahada, shahada, stashahada ya juu, shahada ya umahiri, na shahada ya uzamivu.

Benki ya Maendeleo ya Afrika – AfDB Yaridhishwa Na Ujenzi Wa Mradi Wa Kituo Cha Kupoza Umeme Cha Zuzu Mkoani Dodoma

$
0
0
Na Peter Haule, WFN, Dodoma
Benki ya Maendeleo ya Afrika – AfDB imeridhishwa na kasi ya maendeleo ya mradi wa Kituo cha kupoza umeme cha Zuzu kinachofadhiliwa na Benki hiyo kwa kushirikiana na Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Japan- JICA.

Hayo yameelezwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya AfDB, Bw. Amos Cheptoo, alipofanya ziara ya  kukagua maendeleo ya Kituo hicho kilichopo katika eneo la Zuzu Mkoani Dodoma.

Bw. Cheptoo alisema kuwa amejionea kazi nzuri inayofanywa na Mkandarasi ya  kuhakikisha mradi huo unakamilika Februari, 2020 na kutumika kikamilifu katika kupoza na kusambaza umeme kwa manufaa ya Tanzania na nchi jirani.

Alisema kuwa mradi huo utakua na tija zaidi baada ya kukamilika kwa mradi mkubwa wa umeme wa Julius Nyerere unaotarajia kuzalisha zaidi ya Megawati 2000, hivyo kuifanya miundombinu ya kupoza umeme kutumika kimailifu.

Mkurugenzi huyo wa  AfDB  alisema  umeme ndio nyenzo muhimu katika  ukuzaji wa uchumi na uendelezaji wa viwanda katika nchi za Afrika, kukamilika kwa miradi ya umeme kutasaidia uwepo wa umeme wa kutosha hasa katika nchi za Afrika mashariki na kusini mwa Afrika.

Serikali ya Tanzania imechukua hatua nzuri za kuboresha miundombinu wezeshi ya uzalishaji hasa Dodoma ambapo ndio Makao Makuu ya nchi.

Kwa upande wake mratibu wa mradi huo Mhandisi Peter Kigandye alisema kuwa, mradi huo utakuwa na uwezo wa kushusha umeme kwa Kilovoti 400 na kupoza umeme wenye uwezo wa takribani megawati 400 kisha kusambaza umeme katika maeneo mbalimbali mkoani Dodoma.

Gharama ya mradi huo unajumuisha mradi mwingine uliopo Singida na gharama zake ni dola za Marekani milioni 53 ambazo zimetolewa kwa ushirikiano wa Serikali ya Tanzania, Benki ya AfDB na Shirika la JICA ambapo Kituo cha Kupozea Umeme cha Zuzu kinagharimu takribani dola za Marekani milioni 22.

Aidha Kamishna Msaidizi wa masuala ya Nishati ya Umeme kutoka Wizara ya Nishati Mhandisi Innocent Luoga, ameishukuru Benki ya AfDB kwa kusaidia uboreshaji wa miundombinu hasa ya umeme kwa kuwa miradi hiyo itakapokamilika, utazinufaisha pia nchi za Zambia, Botswana na hata Afrika ya Kusini, kupitia mtandao wa umeme wa kusini

Amewataka wawekezaji walio na nia ya kuwekeza Dodoma kutumia fursa ya upatikanaji wa umeme wa uhakika kuwekeza hasa katika viwanda vikubwa na vidogo kwa kuwa mazingira ya uwekezaji yapo vizuri.

Mhandisi Luoga ameiomba Benki ya AfDB kusaidia upatikanaji wa fedha kwa ajili ya usambazaji zaidi wa umeme katika Mkoa wa Dodoma na viunga vyake ili kuchochea ukuaji wa uchumi na kulifanya jiji kuwa na hadhi stahiki.

Mwisho

Tanzania Ina Utoshelevu Wa Chakula Cha Ziada Takriban Tani Mil.2.5 Sawa Na Asilimia 109%

$
0
0
Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
SERIKALI imesema kwa sasa nchi ina utoshelevu wa chakula cha  ziada takriban tani milioni 2.5 sawa na asilimia 109%   ambapo katika kipindi cha miezi mitatu kuanzia Julai hadi Septemba imeuza tani za mahindi elfu 84.5 nje ya nchi.
 
Akifungua mkutano wa kupokea tafiti kuhusu kuimarisha usalama wa chakula ndani na nje ya Nchi  Nov,19,2019  jijini Dodoma,Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo,Profesa  SIZA TUMBO amesema pia katika kipindi cha miezii mitatu Mihogo tani elfu tano ilipelekwa nchini Burundi na tani elfu 2000 za Mtama zilipelekwa nje ya nchi.
 
Aidha Profesa TUMBO amesema kwa mujibu wa taarifa rasmi ya Benki ya Dunia tayari Tanzania imeshafikia kwenye uchumi wa kati.

Kwa Upande wake,Mkuu wa Idara ya Ushauri Elekezi kutoka Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF) VIVIAN KAZI Kazi amesema  utafiti huo una malengo sita ikiwemo kuboresha uzalishaji wa taarifa ili kuhamasisha mauzo ya mazao ndani na nje ya nchi.

ESRF ilianzishwa mwaka 1994 kama taasisi ya utafiti ikiwa imejikita kufanya kazi zake katika kutoa ushauri elekezi  wa kisera katika nyanja za uchumi na jamii ndani na nje ya nchi na imefanya utafiti huo kwa kushirikiana na ofisi ya Rais TAMISEMI,Uvuvi na Mifugo,Viwanda na Biashara,Kilimo na Ofisi ya Taifa ya Takwimu.

Mwanamke Atuhumiwa Kumchinja Mwanae na Kumla Nyama Ludewa

$
0
0
LUDEWA -NJOMBE
Mwanamke mmoja anaejulikana kwa jina la Christina Mlelwa(38) mkazi wa Kijiji cha Mavanga kata ya Mavanga kitongoji Cha mji mwema wilayani Ludewa mkoa wa Njombe anashikilikiwa na jeshi la polisi kwa tuhuma za kumchinja mwanae Joseph Gumbilo(4) mwenye ulemavu wa viungo na kumla nyama

Awali akizungumzia tukio hilo mkuu wa wilaya ya Ludewa Andrew Tsere anasema mapema baada ya kufikishiwa taarifa za tukio hilo alilazimika kufika eneo la tukio na kumhoji mtuhumiwa ambaye alikiri kutekeleza mauaji ya mwanae na kisha kumkata viongo vyake  na kumla huku viungo vingine kuvitupa porini na chooni.

Tukio hilo linaleta mshituko kwa kamati ya ulinzi na usalama mkoa na kumsukuma mkuu wa mkoa wa Njombe Christopher Olesendeka kufika katika kijiji hicho kuzungumza na wananchi na kisha kutoa agizo kwa wakuu wote wa  wilaya za mkoa huo kukamata kijiji kizima na kuweka lockup endapo watagoma kutoa ushirikiano kwa vyombo vya ulinzi na usalama kuhusu matukio ya mauaji

Katika hatua nyingine Olesendeka ameliagiza jeshi la polisi kusaka ukweli wa tukio hilo haraka na wahusika kufikishwa mahakamani kama ambavyo katiba inalinda haki ya kuishi ya kila binadamu bila kujali ulemavu wake.

Katika mahojiano ya awali na  jeshi la polisi, mama huyo ambaye anaonekana kuwa na matatizo ya akili amekiri kuua na kukata vipande vipande na kumla nyama huku masalia mengine ikiwemo fuvu la kichwa na miguu akiyatupa porini hatua ambayo ililazimu kamati ya ulinzi kuvamia pori na kukuta vitu hivyo.

Lakini Mume wake bwana Daniel Gumbilo anasema mke wake alisha wahi kufanya jaribio kama hilo miaka ya nyuma kwa mototo wao mwingine anaesoma ambapo majirani walinusuru maisha ya mototo wao .

Nae kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Njombe Hamisi Issa anasema jeshi linaendelea kuchunguza kwa kina zaidi kuhusiana na tukio hilo ili wahusika wapewe haki yao ya hukumu ya uovu wao.

Kwa upande wa mtendaji wa kijiji cha Mavanga Fadhiri Tajiri alisema ni kweli tukio hilo limetokea na kwamba taarifa zaidi anasubiri muongozo kutoka kwa viongozi wake.

"Ni kweli Hilo tukio lipo lakini viongozi wangu wamesema wapo njiani wanakuja nasubiri muongozo wa kutoka kwao"alisema Tajiri.


Rais Magufuli avitaka Vyombo vya Usalama kutowanyanyasa Wananchi kwa kuwasingizia makosa ya Uzururaji

$
0
0
Vyombo vya Usalama nchini vimeonywa kutowaonea Wananchi kwa kuwashitaki kama Wazururaji, wakati wana shughuli zao kufanya.

Onyo hilo limetolewa na Rais John Magufuli ambaye amesisitiza kuwa, yeye hawatetei Wazururaji, na kama kweli kuna Mzururaji sheria ziko wazi kwa ajili ya kumshitaki na wala sio kumnyanyasa.

Rais Magufuli ametoa onyo hilo akiwa njiani kuelekea jijini Dodoma, baada ya baadhi ya Wakazi wa mkoa wa Morogoro kudai kuwa, wamekua wakikamatwa na vyombo vya Usalama kama Wazururaji wakati wana shughuli zao za kuwaingizia kipato.

"Vyombo vya usalama ambavyo vinadili na hawa wazururaji, wasiwaonee watu, Umemkuta anauza mahindi ndio yake, unamshika unamuambia mzururaji, haya ya uonevu yasiwepo" -Rais Magufuli.

Amerejea kauli yake ya kutaka kutobughudhiwa kwa Wafanyabiashara wadogo ambao wamekua wakihangaika kufanya shughuli mbalimbali ili kujiingizia kipato.

Pia Rais Magufuli amesisitiza kuwa, wakati akiomba ridhaa ya kuongoza nchi, aliahidi kulinda haki za Watanzania wote na kuhakikisha sheria zinafuatwa, hivyo hatoruhusu mtu ama chombo chochote kuvunja sheria na kumuonea mwingine.

Wimbo UNO wa msanii Harmonize Wafutwa Youtube

$
0
0
Wimbo UNO wa msanii Harmonize umeondolewa kwenye mtandao wa YouTube baada ya mtayarishaji Magix Enga wa nchini Kenya kudai kuwa Harmonize ameiba Beat katika  wimbo aliotayarisha uitwao Dundaing wa King Kaka feat. Kristoff.

Novemba 17, 2019  Enga alimuomba Harmonize kuufuta wimbo huo katika mtandao huo na kumpa wiki moja na kuahidi kuwa asipofanya hivyo, atachukua jukumu hilo mwenyewe.

Kupitia ukarasa wake kwenye mtandao wa Instagram, Magix ameandika;  “Week Imeisha and The song Uno is no longer on YouTube Don’t sample magix Enga Beats. I repeat, dont! Like I said i’m not going to allow this to happen not in 254 🇰🇪.”

Jinsi Punyeto Inavyo Sababisha Kusinyaa Na Kudumaa Kwa Maumbile Ya Kiume

$
0
0
Wanaume  wanao  jihusisha  na  upigaji  wa  punyeto  kwa  muda  mrefu  husalia  kuwa  na  maumbile  ya  kiume  yaliyo  sinyaa  na  kudumaa.

Kwa mujibu  wa  tafiti  mbalimbali  za  kitaalamu, kufanya  punyeto  kwa  muda  mrefu  huathiri  na  kuharibu  mishipa  na  misuli  ya  uume na  hivyo kusababisha  kujengeka  kwa  mafuta na  tishu  zisizo vutika  kwenye  mishipa  ya  ateri na  hivyo  kuzuia  mishipa ya  ateri  kupanuka na  kuongezeka  pamoja  na  damu  kutiririka  kwenda  kwenye  misuli  ya  uume.

Mambo  hayo  mawili yanapotokea  huathiri  uzalishaji  wa homoni muhimu  zinazo  husika  na ukuaji wa misuli ya  uume, na hatimaye  hufanya  uume  wa  mhusika  kudumaa, kusinyaa, kunywea  na  kurudi ndani  kiasi  cha  kuufanya  uonekane  kama wa  mtoto.

 Homoni  hizo hujulikana   kitaalamu kama  HGH  na  huzalishwa  kwenye  ini.

Sababu nyingine   inayo  tajwa  na  wataalamu  ni kwamba, mtu  anaye fanya punyeto   hutumia  akili,  nguvu na  nishati  nyingi sana, jambo ambalo  huathiri utendaji  wa  ogani  nyingine  muhimu  katika  mwili , likiwemo  ini.

Na kwamba  ini  linapo kosa  nishati   ya kutosha  hushindwa  kufanya kazi  zake  vizuri  na  moja  kati  ya  kazi kubwa  za  ini  ni  pamoja  na  uzalishaji  wa  homoni  zijulikanazo  kitaalamu kama  HGH  ambazo  kama  ilivyo andikwa  hapo juu, zinahusika na  kuchochea  ukuaji  wa  sehemu mbalimbali  katika  mwili  wa  mwanadamu  ikiwemo   misuli  ya  uume.

Mbali na  kuathiri  utendaji  wa  ogani  nyingine  mwilini, upigaji  punyeto  husababisha  athari nyingine  kwenye  mwili wa  mwanadamu  kama  vile uchovu  sugu  wa mwili  pamoja na kunyonyoka kwa  nywele.

Athari nyingine  za  upigaji punyeto  ni  pamoja  na  kupoteza  kumbukumbu, kuwahi  kufika  kileleni  ambako  husababishwa  na  kulegea  kwa  mishipa  ya  ateri, kushindwa  kurudia  tendo  la  ndoa, kukosa  hamu  ya  tendo  la  ndoa, uume  kusimama  katika  hali  ya  ulegelege,   maumivu  wakati  wa  tendo  la  ndoa  husuani  wakati  wa  kurudia  tendo  la pili na    mara  baada  ya  tendo  la  ndoa  la  kwanza.

KWANINI   WATU WENGI  WANAO  JIHUSISHA  NA  UPIGAJI  PUNYETO  WANA  MAUMBILE  MADOGO  YA  KIUME YALIYO  DUMAA, SINYAA  NA  KURUDI NDANI.

Uzeofu  unaonyesha  kuwa,  asilimia  kubwa  ya  wanaume  ambao  wamewahi  kufanya  punyeto  kwa  muda  mrefu, wanakabiliwa  na  tatizo  la kuwa  na  maumbile  ya  kiume yaliyo dumaa, sinyaa  na  kurudi ndani.

SABABU  KUBWA   NI  HII  HAPA
Sababu  kubwa  ni kwamba   vijana wengi  wa  kiume, huanza  kujihusisha  na  punyeto   wakiwa  na  miaka  kumi  na sita , kumi na  saba  au  chini  ya  hapo.

Hiki ni  kipindi  ambacho  vijana  hawa  ndio  wanakuwa  wamebalehe.

Na kwa mujibu  wa  tafiti  za kisayansi, katika  kipindi  hiki cha  balehe  ndio  kipindi  ambacho  homoni za  HGH  ambazo huhusika  na  ukuaji  wa  sehemu  mbalimbali  za  mwili  ikiwemo  maumbile ya  kiume, huzalishwa  kwa wingi.

Kama  tulivyo ona  hapo  juu, upigaji  punyeto  huathiri  uzalishwaji  wa   homoni  hizo.

Mwisho wa  siku  maumbile  ya  kiume  ya  wahusika, hushindwa  kukua  na  kuishia  kudumaa na  kusinyaa.

Na  hii ndio  sababu  kubwa  wanaume  wanao  kabiliwa  na  tatizo  hili  husalia  kuwa  na  maumbile yenye  ukubwa  ule  ule  walio kuwa  nao wakati wa  kubalehe

NINI  TIBA  ASILIA  YA  TATIZO  LA  KUDUMAA, KUSINYAA  NA  KURUDI NDANI KWA  MAUMBILE  YA  KIUME.
Kama uume wako  umedumaa, sinyaa, legea, nywea  na  kurudi ndani  kwa  sababu  ulifanya  punyeto  kwa  muda  mrefu  na  unataka  kuondokana  na  hali  hiyo. HII  NI HABARI NJEMA  SANA  KWAKO! 
 
Ipo dawa  ya ASILI   ambayo  HUTIBU  na  KUPONYESHA  KABISA  tatizo la  KUDUMAA, KUSINYAA, KUNYWEA  NA  KURUDI NDANI  KWA MAUMBILE  YA  KIUME kunako  tokana  na  ufanyaji  punyeto  wa  muda  mrefu.
 
Ni  dawa  ya  asili  kabisa ambayo  hutibu  na  kuponyesha  kabisa  tatizo  la kudumaa  na  kusinyaa  kwa  uume  ndani ya siku thelathini.

JINSI YA  KUPATA  TIBA  HII : Kupata  tiba  hii  fika  ka6ika  duka  la  kuuza  dawa  za  aslili  la  NEEMA  HERBALIST.  Tunapatikana  UBUNGO  jijini  DAR  ES  SALAAM  jirani  na  SHULE  YA  MSINGI  UBUNGO  NATIONAL  HOUSING  nyuma  ya  jengo  la  UBUNGO  PLAZA.

Kwa wateja  waliopo  jijini  Dar  Es  Salaam  ambao  hawana  nafasi  ya  kufika  ofisini  kwetu  watapelekewa  dawa  mahali  walipo  ( HOME & OFFICE  DELIVERY )  na kwa  wateja  waliopo  nje  ya  mkoa  wa  Dar  Es  Salaam  watatumiwa  dawa  kwa  njia  ya  usafiri  wa  mabus  au  boti  kwa  waliopo  Zanzibar.

Wasiliana  nasi  kwa  simu  namba  :    0693  005 189.

Scholarships for Tanzanian Students| Ufadhili wa Kusoma Nje ya Nchi (Unalipiwa Kila Kitu) | Deadline ni Mwakani 2020

$
0
0
📚 FURSA ZA UFADHILI  WA KUSOMA NJE YA NCHI

▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬

    🎓Tanzanian Scholarships


Kama wewe ni Mtanzania mwenye Ndoto ya Kusoma nje ya Nchi lakini hukuwa na uwezo, basi hii ni Nafasi yako. Kuna Nafasi Nyingi sana za Ufadhili zimetangazwa (Scholarships)


 Zote Hizo ni Full Funded( Unalipiwa kila Kitu) Japo kuna zingine utachangia kidogo 

_______________________ 

Bado hujachelewa, Deadline ni kuanzia Mwezi huu wa  kumi na moja  hadi Mwakani-2020
._______________________ 


1.Global Scholars Program- Clark University USA 

2.Hong Kong PhD Fellowship Scheme for International Students

3.Clarendon Fund Scholarships, University of Oxford, UK

4.Holland Scholarship for Non EEA International Students

5.Justus & Louise van Effen Excellence Scholarships in Netherlands

6.Oxford Pershing Square Graduate Scholarships in UK

7.Emile-Boutmy Scholarship in France for Non EU Students

8.Karen McKellin International Leader of Tomorrow Award, University of British Columbia

9.Weidenfeld-Hoffman Scholarships and Leadership Program

10.Radboud Scholarship Programme | Netherlands

11.Global Minds Doctoral Scholarships Programme at KU Leuven

12.Chalmers IPOET Scholarships for International Students

13.ETH Zurich Excellence Masters Scholarships

14.Maastricht University Holland High Potential Scholarships for International Students

15.Uppsala University Global Scholarships

16.University of Twente Scholarships (UTS)

Bofya hapo chini kujua zaidi
👇👇👇👇👇👇👇👇


http://ajirazote.com/scholarship/

Rais Magufuli Aagiza Majengo Yote Ya Ofisi Za Tanroad Dumila Yawe Kituo Cha Afya....Asema Serikali Haiwezi Kuingilia Kupanda Bei Ya Mahindi

$
0
0
Rais Magufuli ameagiza majengo yote yaliyokuwa ya Ofisi za Wakala wa Barabara Tanzania(TANROAD)eneo la eneo la Dumila mkoani Morogoro yakabadilishwe na kuwa Kituo cha Afya Dumila.

Ametoa maagizo hayo leo Novemba 20,mwaka 2019 wakati akizungumza na wananchi wa Dumila akiwa safari kuelekea mkoani Dodoma. Akiwa hapo wananchi hao kupitia diwani wao walitoa maombi yao kadhaa kwa Rais ambayo kwao yamekuwa changamoto ikiwemo ya kukosa kituo cha afya, uhaba wa maji safi na salama na umeme.

Hivyo wakati anajibu changamoto hizo, Rais amesema kuanzia leo hii, majengo hayo ya ofisi za TANROAD yatakuwa Kituo cha afya Dumila na nyumba 11 za ofisi hizo ziwe nyumba za watumishi wa kituo hicho.

"Hoja zote ambazo zimetolewa na diwani wenu hapa ni za msingi na zitafanyiwa kazi, hili la kituo cha afya, naagiza majengo ya ofisi ya Tanroad yawe kituo cha Afya, kuhusu madaktari, dawa na vifaa tiba hilo nitatoa maagizo kwa Wizara ya Afya.

"Kesho Diwani mje mfungue kituo cha afya na andika jina lako kwa niaba yangu, nimekuruhusu.Yale majengo yalijengwa kwa fedha za Serikali, kuna nyumba 11 nazo zote ziwe za kituo cha afya Dumila,"amesema Rais Magufuli.

Pia Rais amesema changamoto nyingine ambazo zimeelezwa na wananchi hao zitafanyiwa kazi huku akitumia nafasi hiyo kutoa ruhusa ya wananchi hao kuchimba mchanga katika daraja la Mto Dumila ingawa ametaka kuwepo na utaratibu mzuri ambao uchimbaji huo hautaharibu daraja hilo.

"Nawaruhus mchimbe mchanga, lakini tukubaliane kwa utaratibu mzuri, tusiharibu hili daraja.Ikitoke mkachimba mchanga na kuharibu daraja matipa yote nitayakamata,"amesema Rais Magufuli.

Wakati huo huo Rais Magufuli amewataka viongozi wa Mkoa wa Morogoro wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa huo kutafuta ufumbuzi wa migogoro kati ya wakulima na wafugaji ambao ametumia nafasi hiyo kueleza anayo matumaini makubwa kuwa ufumbuzi utapatikana.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images

<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>
<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596344.js" async> </script>