Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

TAKUKURU yamkamata Muweka hazina wa kikundi

$
0
0
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Arusha inamshikilia Muweka hazina wa kikundi cha ujasiriamali cha Imani kwa tuhuma za kutafuna Tsh.Million 39 za Wanakikundi na kudai zimeyeyuka kishirikina.

Wanakikundi 28 juzi walikesha wakilia nyumbami kwa Muweka hazina huyo Halima Mwidadi Mkazi wa Osunyai Arusha baada ya kuambiwa fedha hizo ambazo walitakiwa kugawana zimepotea katika mazingira ya kutatanisha.

Wengine waliokamatwa na TAKUKURU ni Katibu wa Kikundi Deogratius Seif na Mwenyekiti wake Aisha Saidi ambao walikamatwa jana na kuachiwa kwa dhamana huku Muweka hazina akiendelea kusota Mahabusu kwa sababu za kiupelelezi.

Waziri Mkuu Amtaka Mtendaji Mkuu TBA Ajitathmini ...Awasimamisha Kazi Wakurugenzi Watatu

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemtaka Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), Arch. Daud Kondoro ajitathmini kuhusu utendaji kazi wake huku akiwasimamisha kazi wakurugenzi watatu wa wakala huo.

“TBA tunaihitaji lakini watu wake wana shida. Hatuwezi kuwaacha, TBA wasipewe miradi kwa sababu hawawajibiki na wanadhani kwa kuwa ni taasisi ya Serikali ndio wataachwa wafanye mambo ya hovyo.”

Waziri Mkuu amewasimamisha kazi wakurugenzi hao leo (Jumatatu, Novemba 18, 2019) wakati alipotembelea mradi wa ujenzi wa Ofisi ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) eneo la Njedengwa jijini Dodoma.

Wakurugenzi waliosimamishwa kazi ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ujenzi, Arch.Humphrey Killo, Kaimu Meneja wa Miradi, Abdallah Awadh na Kaimu Mkurugenzi Idara ya Ushauri Arch. Hamis Kileo.

Waziri Mkuu amechukua hatua hiyo baada ya kutoridhishwa na utendaji kazi wa TBA katika miradi mbalimbali waliyopewa na Serikali ukiwemo ujenzi wa jengo la NEC ambalo ujenzi wake ulianza Julai, 2017 na ulitakiwa ukamilike Juni 2018 kwa gharama ya sh. bilioni 13. Hata hivyo mradi huo bado haujakamilika na ujenzi wake umesimama.

Akiwa katika eneo la mradi wa ujenzi wa ofisi ya NEC Waziri Mkuu alihoji sababu za mradi huo kutokamilika kwa wakati ambapo Kaimu Mkurugenzi wa Ujenzi alisema jengo hilo limeshindwa kukamilika kwa sababu wakati walipokuwa wanaanza kazi walibaini kuwa kuna vitu vilisahaulika wakati wa uandaaji wa Bill of Quantities(BOQ). TBA ndio waandaaji wa ramani ya jengo hilo na ndio wajenzi.

“Bajeti ya awali ilikuwa sh. bilioni 10 wakati wa uandaaji wa michoro ya ujenzi gharama ziliongezeka na kufikia sh. bilioni 13 ambazo ndizo tulikubaliana katika mkataba. Wakati tunaendelea na kazi tuligundua kuna vitu vimesahaulika kwenye BOQ jambo lililoongeza bajeti ya ujenzi na kufikia sh. bilioni 32.” Amesema Arch. Killo.

Waziri Mkuu akahoji tena “kutoka sh. bilioni 13 hadi kufikia sh. bilioni 32 je unaona inakuja vizuri hiyo” sh. bilioni 10 hadi sh. bilioni 13 tena hadi sh. bilioni 32 inazungumzikaje hii na je mwenye jengo mlikubaliana naye? Awali mwenye mahitaji alisema ana sh. bilioni 10 sasa imefikaje 32 je mlimshauri muhusika kuhusu ongezeko hili?

Kaimu Mkurugenzi wa Ujenzi Arch. Killo alipotakiwa kueleza sababu za kuongezeka kwa gharama za ujenzi huo amesema waligundua tofauti wakati wakiwa kwenye eneo la ujenzi kwamba kuna kazi zilitakiwa zifanyike lakini katika mkataba hazipo na hawakuwasiliana na muhusika.

Miongoni mwa vitu vilivyosahaulika katika BOQ ya mradi huo ni pamoja na kutokuwepo kwa ghorofa ya nne katika jengo moja wanalolijenga katika mradi huo ambalo ni la ghorofa nane, pia hapakuwa na paa la jengo la kuhifadhia vifaa mbalimbali vya NEC.

Waziri Mkuu amesema miradi mingi inayojengwa na TBA katika maeneo mbalimbali imeshindwa kukamilika kwa wakati, hivyo amemwagiza Waziri wa NchiOfisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Jenista Mhagama asitishe mkataba huo wa ujenzi na atafutwe mkandarasi mwingine aje amalizie.

“Jengo la TAMISEMI lililopo katika mji wa Serikali limejengwa kwa gharama ya sh. bilioni 1.7, nyie wataalamu gani na kwa nini tuendelee kuwaacha ndani ya taasisi? TBA hamfanyi kazi vizuri wakuu wa mikoa na wilaya wanalalamika majengo hayakamiliki ni Serikali gani itakayowavumilia, mmeshindwa kutambua majukumu yenu.”

Waziri Mkuu ameagiza mkandarasi atakayepatikana ahakikishe mradi wa ujenzi huo unakamilika katika kipindi cha miezi sita kuanzia sasa na lijengwe kwa kutumia mfumo wa force account.

(mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,

Taaluma Ya Maendeleo Na Ustawi Wa Jamii Iwe Chachu Ya Mabadiliko Katika Jamii: Dkt. Jingu

$
0
0
Na Mwandishi Wetu Morogoro
Katibu Mkuu Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu amevitaka Vyuo na Taasisi za Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii nchini kutoa elimu itakayowasaidia wahitimu kuleta mabadiliko katika jamii zao na kuweza kujiajiri na kuajiri watu wengine kuliko kutegemea kuajiriwa.

Dkt.John Jingu ameyasema haya leo mkoani Morogoro wakati akifungua kikao kazi cha wakuu wa Vyuo na Taasisi za Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii nchini kilicholenga kubadilishana uzoefu kwa wakuu hao wa vyuo katika utendaji kazi na kujengeana uwezo ili Taasisi na Vyuo viweze kufanikisha malengo ya Taifa.

Dkt. Jingu amesema kuwa taaluma ya Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii  lazima iwe nyenzo ya kutatua changamoto zilizopo katika jamii ikiwemo tatizo la ajira kwa vijana kwa kutoa taaluma itakayowapa fursa wahitimu kujiajiri kutokana na taaluma waliyopata.

“Umefika wakati sasa Taasisi na Vyuo kuja na Mpango Mkakati wa namna ya kutekeleza dhana ya kujiajiri  kwa lengo la kuzalisha wahitimu mahiri " alisema Dkt. Jingu.

Ameongeza kuwa Vyuo vya Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii vimetoa mchango mkubwa sana katika kutatua changamoto za jamii na hivyo jamii kuthamini uwepo wa vyuo katika jamii na mafanikio yaliyoonekana  kwa vyuo hivyo yaonekane kwa kila chuo.

Aidha Dkt. Jingu amevitaka Vyuo hivyo kuanzisha Vituo vya kielektroniki vya ubunifu na maarifa (Digital Innovation Centre) ambao utarahisisha upatikanaji wa maarifa na ujuzi kwa haraka zaidi kuliko kusoma vitabu na itatoa fursa ya kupata maarifa katika muda mfupi.

“Natumaini ushiriki wetu katika kikao kazi hiki utatuongezea ari na ubunifu wa kazi katika maeneo yetu na mtazingatia mafunzo na maelekezo yatakayotolewa katika kuhakikisha vyuo vinatoa matokeo chanya kwa kuzalisha wataalam wenye ujuzi na maarifa ya kazi.   

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Jamii nchini Patrick Golwike amesema kuwa ili kujipambanua katika jamii umuhimu wa Kada ya Maendeleo ya Jamii inatakiwa kuwa na mbinu ya namna ambayo Vyuo vya Maendeleo ya Jamii itatoa wataalam wakaosaidia kuleta mabadiliko kwa jamii.

Naye Kamishna wa Ustawi wa Jamii nchini Dkt. Naftali Ng’ondi amesema kuwa Kada ya Ustawi wa Jamii ni moja kati ya Kada ambazo zina uwanda mpana wa kujiajiri na kuajiriwa hivyo Vyuo na Taasisi ya Ustawi wa Jamii zijikite katika kutoa elimu itakayowasaidia wahitimu hasa kujiajiri.

Wakuu wa Vyuo na Taasisi za Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii wamekutana mkoani Morogoro katika kikao kazi kilicholenga kutafuta namna bora ya taaluma ya Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii katika kuleta mabadiliko katika jamii.

MWISHO.

Waziri Mkuu Amtaka Mtatiro Awashughulikie Waliokula Fedha Za Korosho Tunduru

$
0
0
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amemuagiza Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Bw. Julius Mtatiro ahakikishe anaondoka na Mkurugenzi wa Bodi ya Korosho hadi Tunduru ili wakahakiki ni kwa nini wakulima hawajalipwa.

"Nimefurahi kusikia minada ya korosho inakwenda vizuri. Lakini sijafurahia habari ya Tunduru. Mheshimiwa Rais aligiza sh. milioni 40 zipelekwe kwa wakulima. Na ninajua kwamba zimeshalipwa. Sasa ni kwa nini wakulima bado wanadai?, alihoji.

"Ukitoka hapa kwenye mkutano nenda pale jengo la Bodi ya Korosho. Ondoka na Mtendaji Mkuu wake, mwende Tunduru akafuatilie ni kwa nini malipo ya mwaka jana hayajalipwa hadi sasa." Bw. Mtatiro ni Mkuu wa Wilaya ya Tunduru.

"Nataka afuatilie fedha zimekwama kwa nani. Kaimu Mkuu wa Mkoa ukigundua wanaokwamisha ni viongozi wa ushirika, shughulika nao hukohuko kama ambavyo umekuwa ukifanya," amesisitiza.

Ametoa agizo hilo leo mchana wakati akifungua kongamano la siku moja la Wakandarasi na Wazabuni wa mikoa ya Kusini lilioandaliwa na benki ya CRBD kwenye ukumbi wa Benki Kuu (BoT) mjini Mtwara.

Akizungumzia kuhusu kongamano hili ambalo kaulimbiu yake ni "Pamoja nawe kukuza uchumi", Waziri Mkuu amewataka wakandarasi hao baada ya kupata elimu kidogo kuhusu shughuli za benki hiyo, anataraji kuwa wataenda kwenye Halmashauri zao na kutafuta ........

"Serikali inajenga miradi mikubwa kama vile bwawa la kuzalisha umeme kwa nguvu ya maji la Mwalimu Nyerere, bomba la mafuta la kutoka Hoima hadi Tanga na miradi ya maendeleo kama ile ya barabara, reli, ujenzi wa  hospitali, madarasa na nyumba za walimu. Miradi yote hii inawatarajia ninyi wakandarasi mkaijenge."

Alisema Serikali imeendelea kuimarisha na kusogeza karibu kwa wananchi huduma za jamii ikiwemo ukarabati wa miundombinu ya kufundishia na kujifunzia katika ngazi zote za elimu. "Katika kipindi cha Januari hadi Juni 2019, kwa shule za msingi, Serikali imejenga madarasa 473, matundu ya vyoo 1,405, nyumba za walimu 24 na kukamilisha maboma ya madarasa 2,760. Kwa shule za sekondari, Serikali ilijenga madarasa 465, matundu ya vyoo 736, nyumba za walimu 23 na kukamilisha maboma ya madarasa 2,392," alisema.

Waziri Mkuu alitumia fursa hii kutoa wito kwa viongozi na watendaji wazingatie utekelezaji wa Sheria ya Ununuzi wa Umma kwa kutenga zabuni zenye thamani ya chini ya shilingi bilioni 10 kwa ajili ya wazabuni Watanzania ili kuwajengea uwezo na kushiriki katika zabuni. Alisema Serikali kwa upande wake itaendelea kusimamia utekelezaji wa Sheria ya Ununuzi ili kufikia malengo yaliyokusudiwa.

Alimpongeza Mkurugenzi Mkuu wa CRDB kwa kubuni programu hiyo ya tofauto ambayo imelenga kuwainua wakandarasi wadogo na wa kati.

Mapema, akimkaribisha Waziri Mkuu kuzungumza na washiriki qa kongamano hilo, Mkuu wa Mkoa wa Mtwara,  Bw. Gelasius Byakanwa alisema hadi sasa jumla ya tani 67,000 za korosho zimeuzwa mkoani humo kupitia minada mitatu.

Oktoba 30, mnada wa kwanza ulipofanyika bei ilikuwa sh. 2,468/- kwa kilo na mnada wa tarehe 15 Novemba, ulishihudia bei ikipanda na kufikia sh. 2,890/- kwa kilo, alisema.

Alisema katika msimu huu, korosho zimeingiza sh. Bilioni 1.75  ambapo kati ya hizo, sh. Bilioni 1.20 zimeshaingizwa kwenye akaunti na kupelekwa kwa wakulima.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa benki ya CRDB, Bw. Abdulmajjid Nsekela alisema bei hiyo inamsaidia mteja kwa kutoa ushauri, kumwezesha na  kushirikiana naye kuijenga nchi.

"Leo tuko Mtwara,  lakini tumeshaendesha makongamano kama haya katika mikoa ya Dar es Salaam, Arusha, Mbeya, Mwanza. Na hapa Mtwara tumejumuisha pia mikoa ya Lindi na Ruvuma," alisema.

Alisema benki hiyo ina hisa trilioni 6.3 ambazo ni sawa na asilimia 20 ya hisa za mabenki yote na kwa upande wa amana, Mkurugenzi Mkuu huyo alisema amana za benki hiyo zinafikia trilioni 4.9 ambazo ni sawa na asilimia 23 ya amana za benki zote nchini.

(mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,

Mkapa Aweka Wazi Rostam Aziz alivyochangia kuanzishwa NHIF

$
0
0
Rais mstaafu, Benjamin Mkapa ameweka wazi kuwa uamuzi wa kuwa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), ni mpango ulioasisiwa na mfanyabiashara maarufu nchini Rostam Aziz.

Katika kitabu chake cha ‘My Life, My Purpose’ alichokizindua wiki iliyopita jijiji Dar es Salaam, Mkapa ameeleza alijifunza mpango huo wakati mfanyabiashara huyo alipokuwa Mbunge wa Jimbo la Igunga alikouasisi mwaka 1996 kabla ya kutangazwa rasmi kuwa wa kitaifa.

“Njia nyingine ya moja kwa moja ya kuwasaidia masikini ni kupitia Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), ambao umejitolea kuzipatia familia hizo bima za afya.

“Nilijifunza kuhusu mpango huu kutoka kwa Rostam Aziz, Mbunge na mmoja kati ya wafanyabiashara wakubwa waliofanikiwa.

“Mwaka 1996 alianzisha mpango wa bima ya afya kwa wananchi wake wa Jimbo la Igunga kwa kiwango kidogo cha fedha ya Sh 10,000 ambacho kilisaidia familia yenye watoto wanne kutumia bima hiyo kwa kipindi cha mwaka mzima. Tuliamua kuutangaza mpangohuu kitaifa,” ameeleza Mkapa katika kitabu chake hicho.

Amesema ingawa mpango huo ulipoanzishwa haukueleweka vizuri kwa watu kwani wengine walisema “sitaumwa sasa kwanini nitoe fedha yangu kwenye mfuko huu,” lakini waliendelea kusisitiza juu ya mpango huo.

Yaliyojiri Leo Mahakamani Katika Kesi Ya Aliyemchoma Moto Mkewe Kwa Magunia Ya Mkaa

$
0
0
Upande wa mashtaka katika kesi ya tuhuma za mauaji inayomkabili mfanyabiashara Khamis Luwonga anayedaiwa kumuua mkewe Naomi Marijani kwa kumchoma moto kwa kutumia magunia mawili ya mkaa, umeieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu  kuwa upelelezi wa kesi hiyo kuwa jarada la shauri hilo lipo kwenye hatua ya uchapaji.

Wakili wa Serikali Mwandamizi Wankyo Simon amedai hayo leo Novemba 18, mwaka 2019 mbele ya Hakimu Mkazi Salum Ally, wakati kesi hiyo ilipokuja kwa ajili ya kutajwa.

Amedai shauri hilo lilikuja kwa ajili ya kutajwa, na kwamba upelelezi umekamilika na  jarada lipo kwenye hatua ya uchapaji kwa ajili ya maandalizi ili lipelekwe kwa  Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini (DPP) hivyo wanaomba tarehe nyingine ili waweze kufatilia suala hilo.

Hakimu Ally amearisha kesi hiyo hadi Desemba 2, mwaka huu. 
 
Mshitakiwa anadaiwa Mei 15, 2019 katika eneo la Gezaulole Kigamboni Dar es Salaam alimuua mkewe Naomi Marijani kisha kumchoma moto kwa kutumia magunia mawili ya mkaa ambapo alichukua majivu ya marehemu na kwenda kuyafukia shambani kwake Mkuranga.

 

Askari Polisi, Mtumishi wa Mahakama Kortini Wakituhumiwa Kupokea Rushwa

$
0
0
Watu wawili akiwamo askari polisi ambaye ni mwendesha mashtaka wa Mahakama ya Wilaya ya Temeke, Dar es Salaam nchini Tanzania, Leslie Koini wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi kisutu wakikabiliwa na kosa la kuomba rushwa ya Sh200, 000.

Pia,  upande wa mashtaka umedai mshtakiwa ambaye ni karani wa mahakama hiyo Itialy Omary hakuwepo mahakamani hapo hivyo wameiomba mahakama hiyo hati ya kukamatwa mshtakiwa huyo.

Akizungumza leo Mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Augustina Mmbando, Wakili wa Serikali kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Odessa Horombe amedai Mei 8, mwaka 2018 mshtakiwa Omary na Koini kwa pamoja walipokea rushwa ya Sh. 200,000 kutoka kwa Mussa Abdallah ikiwa kama kishawishi ili asikutwe na we na hatia katika kosa namba 211/2018 la usalama barabarani.

Baada ya kusomewa mashtaka hayo mshtakiwa  alikubali kutenda kosa hilo na upande wa mashtaka ulidai bado haujajiandaa hivyo wanaomba ahirisho la muda kwa ajili ya kujiandaa.

Hata hivyo, Hakimu Mmbando alitoa masharti ya dhamana kwa mshtakiwa ambapo alitakiwa kuwa na mdhamini mmoja mwenye barua na vitambulisho halali atakayesaini bondi ya Sh. 500,000.

Mshtakiwa ametimiza masharti ya dhamana, nje kwa dhamana.Kesi hiyo itatajwa tena Novemba 21 mwaka huu.

Familia ya Marehemu Daudi Balali Yamuomba Rais Magufuli Awasaidie Kurejesha Mali Zao

$
0
0
Familia ya Marehemu Daudi Balali imemuomba Rais Magufuli kuisaidia kuokoa mali za Gavana huyo wa zamani wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) ambazo inadai zimechukuliwa na Wajanja wa Mjini.

Balali aliyeripotowa kufariki Dunia Marekani Mei 16, 2008 alikuwa Gavana wa BOT katika Utawala wa Serikali ya Awamu ya Tatu chini ya Rais Mkapa.

Wakizungumza na Wanahabari Boko nje kidogo ya Dar, baadhi ya Ndugu wa Balali wakiwamo Kaka na Dada zake wamedai kupokwa mali za Ndugu yao kulianza 2012 baada ya watu wasiojulikana kuvamia kwa Mama yake (Rahel Balali) Boko na kuiba sanduku lililokuwa na nyaraka mbalimbali za marehemu ikiweno hati za mashamba, nyumba na viwanja.

"Tunaomba Rais atusaidie kuna mambo yanakwamishwa na baadhi ya Watumishi wa Serikali, tunapoona watu wa nje wanafanya uamuzi wa kubeba kila kitu tunaadhirika, tunateseka"

Mikoa 3 kutopiga kura serikali za mitaa

$
0
0
Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) imesema mikoa mitatu haitafanya uchaguzi wa serikali za mitaa kwa kuwa wagombea kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) wamepita bila kupingwa.

Naibu Waziri wa wizara hiyo, Mwita Waitara amesema jana  jijini Dar es Salaam kuwa, kati ya halmashauri za wilaya 184 nchini, 90 hazifanyi uchaguzi huo Novemba 24 mwaka huu kwa kuwa wagombea wamepita bila kupingwa.

“Katika mikoa 26 ya hapa bara, kwa taarifa ambazo tumeshapokea mpaka leo asubuhi mikoa mitatu inaonekana kwamba wagombea wa Chama Cha Mapinduzi wamepita bila kupingwa kwa hiyo kuanzia siku ya uteuzi wao ni viongozi halali na wasimamizi wameshawateua, hakuna haja ya kampeni katika eneo hilo” ameyasema hayo wakati anazungumza kwenye kipindi cha Asubuhi  kinachorushwa na kituo cha redio cha TBC Taifa cha Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC).

Waitara ameitaja mikoa ambayo haitafanya uchaguzi kabisa kuwa ni Katavi, Tanga, na Ruvuma.

“Mahalali ambako mgombea alikuwa peke yake na amepita bila kupingwa kazi ya msimamizi ni kumtangaza na baada ya hapo atasubiri baada ya tarehe 24 ataapishwa na ataanza majukumu yake kwa hiyo hakuna habari ya kampeni lakini mikoa 23 itakuwa na mchakato wa uchaguzi”amesema Waitara.

Kwa mujibu wa kiongozi huyo hata katika mikoa hiyo 23 uchaguzi utafanyika kwenye baadhi ya maeneo.

IGP Sirro: Tundu Lissu ameshindwa kutoa ushirikiano kuhusu tukio lake la kupigwa risasi

$
0
0
Mkuu wa Jeshi la polisi nchini Tanzania(IGP) Simon Sirro amesema uchunguzi juu ya kupotea kwa mwandishi wa habari za Uchunguzi Azory Gwanda wa gazeti la mwananchi unaendelea kwani wameshafungua jalada la uchunguzi, huku akiwataka watu kama wana taarifa kuhusu tukio hilo kuzifikisha polisi na si kuishia mitandaoni kwani haziwezi kusaidia.

Akizungumza katika kipindi maalum cha Konani kinachorushwa na ITV kupitia Mitandao yake ya Youtube na Facebook, IGP Sirro amesema suala la watu kupotea halijaanza leo huku akitolea mfano wa wazee wa kizanaki wengi walikuwa wanasemekna wamepotea lakini baadae wanaonekana.

Katika hatua nyingine IGP Sirro amezungumzia suala la aliyekuwa mbunge wa Singida Mashariki kwa tiketi ya CHADEMA, Tundu Lissu kupigwa risasi ambapo amesema mpaka sasa bado hawajambaini mtu aliyefanya tukio hilo, huku akieleza kwamba Tundu Lissu ameshindwa kutoa ushirikiano kwa jeshi hilo jambo ambalo linachukua muda.

"Sisi tunamsubiri Mhe.Tundu Lissu aje afungue kesi, kitu gani kimemtokea, mazingira gani na yule dereva wake, dereva tumemtafuta imekuwa shida, yeye mwenyewe alipopata matatizo yupo nje hatujamuona, tunamuona tu kwenye mitandao"IGP Sirro.

IGP Sirro ameweka bayana kwamba kesi ya jinai mara nyingi haifi hata ikichukua miaka kumi bado ni kesi ya jinai, "Kimsingi ni kwamba kesi ipo tunamsubiri Bwana Lissu aje atupe taarifa ilikuwaje na yule shahidi yake nafikiri tutapata sehemu ya kuanzia.

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumanne November 19

Uchaguzi Mkuu CHADEMA Kufanyika Desemba 18, 2019

$
0
0
Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema kimetangaza ratiba ya uchaguzi wa viongozi wake ngazi ya Taifa.

Mchakato huo unaanza na uchukuaji na urejeshaji fomu kuanzia  Novemba 18 hadi Novemba 30, 2019 huku mkutano mkuu ukifanyika Desemba 18, 2019.

Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Vicent Mashinji akizungumza na wanahabari makao makuu ya chama hicho, Kinondoni jijini Dar es Salaam alisema uchaguzi huo utaanza kwa kuchagua viongozi ngazi ya mabaraza na kufuatiwa na viongozi wakuu wa chama ngazi ya Taifa.

"Tutakuwa na Mkutano Mkuu wa Taifa itakuwa December 18, 2019, tushapeleka mialiko kwa watu mbalimbali, miongoni mwa mambo tutakayoyafanya siku hiyo ni kuchagua Viongozi Wakuu wa Chama

"Mchakato tunaoanza nao ni kuchukua na kurudisha fomu za Wagombea, huu mchakato unaanza November 18, 2019, wote ambao wangependa kugombea nafasi mbalimbali wanakaribishwa kuja kuchukua fomu, kujaza kwa ufasaha na kwenda kugombea" Amesema 
Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Vicent Mashinji

Amesema baada ya kupitia majina ya wote walioomba, Desemba 8, 2019 kamati tendaji ya baraza la vijana na wazee watakutana na kufuatiwa na mkutano mkuu wa uchaguzi wa viongozi wa mabaraza hayo Desemba 9, 2019.

Dk Mashinji amesema Desemba 10, 2019 kamati tendaji ya baraza la wazee na vijana itakutana ambapo ni vikao vinavyofanyika kufuatiwa na mkutano mkuu.

Wabunge Watatu CHADEMA Washikiliwa Polisi Baada ya Kujisalimisha....Kufikishwa Mahakamani Leo

$
0
0
Wabunge  watatu wa CHADEMA wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kufuatia amri ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu iliyotaka wabunge wanne wa chama hicho wakamatwe kwa kukiuka masharti ya dhamana.
 
Wabunge waliokamatwa jana Novemba 18, 2019 ni mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche na Mbunge wa Iringa Mjini, Peter Msigwa huku  Mbunge wa Kawe, Halima Mdee yeye alishakamatwa wiki iliyopita
 
Heche na Msingwa walikamatwa jana mara baada ya kujisalimisha katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ili kuonana na Hakimu Mkazi Mkuu anayesikiliza kesi inayowakabili, Thomas Simba.
 
Wabunge hao wameunganishwa na Mbunge wa Kawe, Halima Mdee katika kituo hicho cha Osterbay huku Mbunge wa Bunda mjini Ester Bulaya akidaiwa kuwa anaumwa na amelazwa.
 
Novemba 15, mwaka huu 2019 Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu iliamuru wabunge hao wanne wakamatwe na kufikishwa mahakamani hapo baada ya kutokufika mahakamani hapo bila ya kutolewa taarifa yoyote wakati kesi yao ya uchochezi ilipokuja kwa ajili ya kusikilizwa.
 
Kesi hiyo inatarajia kuendelea leo Novemba 19, 2019 kwaa ajili ya kuendelea na hatua ya usikilizwaji.

Serikali yalifunga Kanisa la Mfalme Zumaridi Jijini Mwanza

$
0
0
Uongozi wa Wilaya ya Nyamagana Mkoani Mwanza umepiga marufuku ibada zinazoendeshwa na kiongozi wa kanisa la Mfalme Zumaridi lililoko mtaa wa Iseni kata ya Butimba hadi hapo Serikali itakapojiridhisha kuwa ibada hazikinzani na sheria za nchi.
 
Agizo la kupiga marufuku limetolewa  jana Novemba 18, 2019 na Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Mkoani Mwanza Daktari Philis Nyimbi akiwa ameongozana na kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya hiyo katika eneo la kanisa hilo.

Amesema kanisa hilo limekuwa likitumia katiba ya kanisa lingine ambalo ni Pentecoste Christian Church of Tanzania  na pia limekuwa likitembea na Katiba ya Kanisa hilo.

DC Nyimbi amesema kiongozi wa Kanisa hilo la Mfalme Zumarid amekuwa akiendesha kanisa hilo bila kufuata sheria za nchi wala maandiko matakatifu kwa kujiita Mungu wa Dunia, Mfalme wakati yeye ni Mwanamke.

Waziri wa Katiba na Sheria Aitaka Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora kuimarisha utawala bora

$
0
0
Na Mbaraka Kambona,
Waziri wa Katiba na Sheria, Balozi Dkt. Augustino Mahiga ameitaka Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) kuimarisha misingi ya utawala bora nchini ili kuboresha utoaji wa huduma za Serikali kwa jamii.

Waziri Mahiga alitoa kauli hiyo Novemba 18, 2019 jijini Dodoma katika kikao kilichofanyika kwenye ofisi za Wizara ya Katiba na Sheria baina yake na Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Mheshimiwa Mathew Mwaimu.

Akiongea katika kikao hicho, Waziri Mahiga alieleza kuwa tume ni chombo muhimu ambacho kimepewa mamlaka ya kusimamia mambo mawili ambayo ni  haki za binadamu na utawala bora.

Waziri Mahiga aliendelea kusema  kuwa tume katika kipindi chote cha utekelezaji wa majukumu yake imekuwa ikifanya kazi kubwa katika masuala ya haki za binadamu zaidi ya utawala bora, na hivyo, kuwataka katika awamu hii ya tano wawekeze nguvu zaidi katika kuimarisha misingi ya utawala bora.

“Tume ni chombo muhimu katika kujenga ustawi wa jamii, hususani kujenga jamii yenye utamaduni wa kuheshimu haki za binadamu nchini, lakini msisahau kujenga utawala bora”, alisema Mahiga

“Mheshimiwa Rais anaposema serikali hii ni ya wanyonge, anataka wale watu walio kwenye mamlaka walijue hilo na wazingatie utawala bora katika kuhudumia jamii, na nyie ndio wenye jukumu la kuhakikisha misingi ya utawala bora inaimarika nchini”aliongeza Maiga

Katika hatua nyingine Waziri Mahiga aliitaka tume kuieleza na kuifafanulia jamii utekelezwaji wa haki za binadamu  unavyotekelezwa kwa vitendo na serikali ya awamu ya tano.

Mahiga alisema pamoja na changamoto zinazopigiwa na kelele na wadau wa masuala ya haki za binadamu, lakini ni ukweli uliowazi kuwa serikali ya awamu ya tano imetekeleza na inaendelea kutekeleza haki mbalimbali kwa vitendo na kuhakikisha haki hizo wananchi wanazipata.

Alieleza kuwa serikali ya awamu ya tano imetekeleza kwa vitendo haki ya kupata elimu kwa kutoa elimu bure kwa wanafunzi kuanzia shule za msingi mpaka sekondari.

Pia, alieleza kuhusu haki ya afya ambapo wazee wameanza kupata matibabu bure, na upatikanaji wa bima ya afya kwa wananchi.

“Hizi jitihada zote za serikali katika kuwapatia huduma wananchi bado hazijaelezwa vya kutosha, tume tumieni nafasi yenu kuyaeleza haya kwa jamii iweze kuelewa”alisisitiza Mahiga

Naye, Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Profesa Sifuni Mchome alimueleza Mwenyekiti wa tume kuwa masuala ya haki za binadamu yanafanywa na taasisi nyingi na hivyo kipindi hiki wawekeze nguvu zao katika kuimarisha utawala bora na utawala wa sheria nchini.

“Tume ni lazima muonekane mnachukua hatua, wekeni mkakati wa viashiria vya kubaini haraka changamoto  zinazoelekea kuathiri utawala bora na kuzifanyia kazi”, alisema Mchome

Akizungumza mapema, Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala bora, Mheshimiwa, Jaji Mstaafu Mathew Mwaimu alimueleza Waziri Mahiga dhamana waliyopewa wataitumia vyema katika kusaidia serikali kutimiza lengo lake la kuifikisha nchi katika uchumi wa kati.

“Tume itaendelea kuunga mkono jitihada za serikali na tutatekeleza majukumu yetu kwa kuzingatia taratibu, sheria na katiba ya nchi”alisema Mwaimu

Mwenyekiti huyo wa Tume alikwenda kutembelea Wizara ya Katiba na Sheria kwa lengo la kujitambulisha kwa Waziri Mahiga ikiwa ndio mara yake ya kwanza tangu alipoapishwa Novemba 4, 2019.

Katika ziara hiyo Mwenyekiti aliongozana na  Makamu Mwenyekiti, Mohamed Khamis Hamad, na Makamishna wengine watano ambao ni  Mheshimiwa, Dkt. Fatma Rashid Khalfan, Mheshimiwa Thomas Masanja, Mheshimiwa Amina Talib Ali, Mheshimiwa Khatib Mwinyi Chande  na Mheshimiwa Nyanda Josiah Shuli.

Freeman Mbowe Alazwa Hospitali ya Aga Khan jijini DSM

$
0
0
Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo, Freeman Mbowe, ameshindwa kufika mahakamani kutokana na kulazwa katika Hospitali ya Aga Khan jijini DSM akiwa anapatiwa matibabu.

Mbowe aliyelazwa  tangu  Novemba 17, 2019b ni miongoni mwa viongozi tisa wa CHADEMA wanaokabiliwa na kesi ya uchochezi namba 112/2018 inayoendelea leo Jumanne Novemba 19, 2019  na alitakiwa kuendelea kujitetea leo lakini mdhamini wake,  Greyson Selestine ameieleza mahakama  kuwa anaumwa.

Kinachoendelea kwa sasa Mahakamani ni washtakiwa wanne; John Heche; Ester Bulaya, Mchungaji Peter Msigwa na Halima Mdee  kujitetea kwanini wasifutiwe dhamana.
 

Novemba 15, 2019, mahakama hiyo ilitoa amri ya kukamatwa kwa washtakiwa hao kutokana na kukiuka masharti ya dhamana baada ya kutofika  mahakama kusikiliza kesi hiyo.

Mbinu Za Wizara Ya Maji Zimekuja Na Utatuzi Wa Huduma Ya Maji Miji Mikuu Ya Mikoa

$
0
0
Na Ismail Ngayonga, MAELEZO
Maji ni hitaji muhimu sana katika ukuaji wa uchumi  na hii inatokana na ukweli kuwa maendeleo ya kiuchumi ya nchi yoyote duniani  yawe ya viwanda, kilimo na kadhalika yanategemea maji.

Aidha Maji ni hitaji muhimu sana katika uhai wa mwanadamu na viumbe wengine na ndio maana maji hayana  mbadala na pia bila maji hakuna uhai na hivyo serikali inaendelea kutekeleza miradi mikubwa ya maji ili kuimarisha uendeshaji na utoaji wa huduma ya maji kwa wananchi.

Huduma za maji mijini hutolewa kupitia Mamlaka za Maji na Usafi wa Mazingira kwenye Miji Mikuu ya Mikoa 23 pamoja na Dar es Salaam; Miji Mikuu ya Wilaya 99, Miji Midogo 14; na miradi 8 ya maji ya Kitaifa ili kufikia malengo yaliyopo ya kuboresha huduma hiyo katika Miji Mikuu ya Mikoa kutoka asilimia 86 hadi kufikia asilimia 95 mwaka 2020

Taarifa ya Serikali kupitia Wizara ya Maji inaonesha kuwa mwaka 2016, Uzalishaji wa majisafi maeneo ya mijini umeongezeka kutoka lita milioni 385 kwa siku mwezi Aprili 2015 hadi kufikia lita milioni 470 kwa siku mwezi Machi, 2016 sambamba na ongezeko la idadi ya wateja waliounganishiwa huduma ya maji kuongezeka kutoka kutoka 362,953 mwezi Aprili, 2015, hadi wateja 405,095 mwezi Machi, 2016 ambapo wateja 392,942 sawa na asilimia 97 wamefungiwa dira za maji.

Aidha makusanyo ya maduhuli kwa mwezi yatokanayo na yatokanayo na mauzo ya maji yameongezeka kutoka Tsh. Bilioni 7.28 mwezi Aprili, 2015 hadi kufikia Tsh. Bilioni 8.50 mwezi Machi 2016 sawa na ongezeko la asilimia 17.

Katika kukabiliana na changamoto mbalimbali zilizojitokeza katika sekta ya maji nchini, Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Uongozi wa Rais Dkt. John Magufuli, imeendelea kuboresha hali ya upatikanaji wa huduma ya maji katika Miji Mikuu ya Mikoa ili kufikia asilimia 95; na Miji Mikuu ya Wilaya, Miji Midogo na Miradi ya Kitaifa kufikia asilimia 90 ifikapo mwaka 2020.

Akiwasilisha Hotuba ya Makadirio ya Bajeti ya Mapato na Matumizi kwa mwaka 2019/2020, Waziri wa Maji, Prof. Makame Mbarawa anasema katika mwaka 2018/2019, Serikali imeendelea kuboresha hali ya upatikanaji wa huduma ya maji mijini kwa kujenga, kukarabati na kupanua miundombinu ya majisafi na majitaka pamoja na kuzijengea uwezo Mamlaka za Maji Mijini.

Akbainisha baadhi ya Miradi inayotekelezwa na Serikali katika Miji Mikuu ya Mikoa, Waziri Mbarawa anasema katika Manispaa ya Kigoma Serikali kwa kushirikiana na  na Serikali ya Ujerumani na Umoja wa Ulaya inatekeleza mradi wa usambazaji wa huduma ya majisafi na usafi wa mazingira kwa gharama ya Euro milioni 16.32, ambapo hata hivyo mwaka 2018 Serikali imesitisha mkataba na mkandarasi wa mradi huo kutokana na uwezo mdogo wa mkandarasi.

‘’Hadi kuvunjwa kwa mkataba, utekelezaji wa mradi ulikuwa umefikia asilimia 87 na mradi ulikuwa umeanza kutoa huduma ya maji kwa wananchi, kutokana na hali hiyo, Wizara imechukua jitihada za kuhakikisha huduma iliyokuwa ikitolewa kwa wakazi wa Mji wa Kigoma inarejeshwa kwa kuajiri mkandarasi wa kuweka mitambo ya muda ya kusukuma maji’’ anasema Waziri Mbarawa.

Kuhusu Jiji la Arusha,, Waziri Mbarawa anasema Serikali kwa kushirikiana na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) inatekeleza mradi wa ujenzi wa miundombinu ya usambazaji majisafi na uboreshaji wa huduma ya uondoaji wa majitaka katika Jiji la Arusha kwa gharama ya Dola za Marekani Milioni 233.9.

Anaongeza kuwa Kazi zinazotekelezwa ni pamoja na uchimbaji wa visima virefu 56, ujenzi wa matanki 10; ujenzi wa mtambo wa kutibu na kusafisha maji, upanuzi na ukarabati wa mtandao wa mabomba ya majisafi, upanuzi na ukarabati wa mtandao wa majitaka, ujenzi wa mabwawa mapya 18 ya majitaka, ujenzi wa ofisi ya Mamlaka; ununuzi wa vitendea kazi na kutoa mafunzo mbalimbali kwa watumishi.

Akifafanua zaidi Waziri Mbarawa anasema hadi mwezi Aprili 2019, utekelezaji wa mradi umefikia asilimia 30 na unatarajiwa kukamilika mwaka 2020, ambapo kukamilika kwa mradi huo kutaongeza uzalishaji wa maji kutoka lita milioni 40 kwa siku za sasa hadi kufikia lita milioni 200 kwa siku na muda wa upatikanaji wa huduma ya majisafi utaongezeka kutoka wastani wa saa 12 za sasa kwa siku hadi saa 24.

Waziri Mbarawa anasema katika Manispaa ya Lindi, Serikali kwa kushirikiana na Serikali ya Ujerumani na Umoja wa Ulaya inatekeleza mradi wa majisafi na usafi wa mazingira katika Manispaa ya Lindi unaogharimu Euro milioni 11.7 ambao ulitarajiwa kukamilika mwaka 2017 lakini haukukamilika kutokana na uwezo mdogo wa kiutendaji wa mkandarasi.

Anasema kuwa Serikali ilichukua hatua ya kuvunja Mkataba na Mkandarasi huyo mwezi Oktoba 2018 ambapo utekelezaji wa mradi ulikuwa umefikia asilimia 92.3 na unatoa huduma ya maji kwa wakazi wapatao 81,343 wa Mji wa Lindi, ambapo kazi zilizobaki ni kufunga mfumo angalizi wa uzalishaji maji, ununuzi wa gari la uondoaji majitaka na kurekebisha maeneo yenye mapungufu katika mradi huo.

Aidha Waziri Mbarawa anasema katika mpango wa muda mfupi wa kuboresha huduma ya maji katika Mji wa Njombe, Serikali imekamilisha ujenzi wa mradi wa maji wa chemchemi ya Kibena uliogharimu Tsh. bilioni 1.1, ukihusisha  ujenzi wa kidakio cha maji, ulazaji wa bomba kuu lenye urefu wa kilomita 2.2 na ufungaji wa pampu mbili za kusukuma maji zenye uwezo wa kuzalisha lita 72,000 kwa saa.

Kukamilika kwa mradi huo kumeongeza uzalishaji wa maji kutoka lita 480,000 hadi lita 864,000 kwa siku na kuboresha upatikanaji wa huduma ya maji katika Hospitali ya Kibena, Chuo cha Uuguzi, na Ofisi za Makao Makuu ya Mkoa na hivyo kuongeza upatikanaji wa huduma ya maji katika Mji wa Njombe kutoka asilimia 69 mwaka 2016 hadi asilimia 87 za sasa.

Ili kufanikisha malengo yaliyopo, ni wajibu wa Mamlaka za Majisafi na Usafi wa Mazingira katika miji mikuu ya Mikoa kuimarisha hali ya Uzalishaji wa majisafi pamoja na kupunguza kiwango cha upotevu wa maji pamoja na kuongeza ufanisi wa utoaji wa huduma iliyo bora na endelevu kwa wananchi.

MWISHO

Nafasi Mpya 16 za Kazi Benki ya CRDB | Deadline ni November 21, 2019

$
0
0
Background
CRDB Bank Plc is an African bank and a leading Financial Services Provider in Tanzania with current presence in Tanzania and Burundi, East Africa. The Bank was established in 1996 and was listed on The Dar Es Salaam Stock exchange (DSE) in June 2009.
 
Over the years, CRDB Bank has grown to become the most innovative and preferred financial services partner in the region. Supported by a robust portfolio and uniquely tailored products, CRDB Bank remains the most responsive bank in the region.

CAREER OPPORTUNITIES
We are a collection of individuals who believe in excellence. We are always on the look out for fresh talent and we hiring people who have the drive to succeed and the will to implement the discipline required to succeed. We focus on nurturing our team and providing our team with an environment that is conductive to creative thought.

==>>Bonyeza Tangazo husika la Kazi hapo chini kupata maelekezo zaidi na namna ya kutuma Maombi
 
TITLE                                                          
 ▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬   

1. Contact Center Agent (5 Positions)   


3. Internal Audit (5 Posts) |  20th, November 2019 
4. Department of Human Resources (5 Posts) | 21st , November 2019 
  1.   Manager; Wellness, Diversity Inclusion & Empowerment
  2.     Senior Specialist; Labour & Trade Union Relations
  3.     Manager; Learning & Development
  4.  Learning & Development Partner- Quality Assurance
  5.     Learning & Development Specialist
▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬   
 
Kwa Nafasi Zingine Kama Hizi <<INGIA HAPA>>

    Wabunge Wanne CHADEMA Warudishwa Mahabusu....Hatima Yao Kujulikana Kesho

    $
    0
    0
    Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imepanga kesho Jumatano Novemba 20, 2019 kutoa uamuzi dhidi ya wabunge wanne wa Chadema waliokiuka masharti ya dhamana kwa kutofika mahakamani bila taarifa yoyote.

    Hayo yameelezwa leo Jumanne Novemba 19, 2019 na hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama hiyo, Thomas Simba baada ya washtakiwa hao kumaliza kujitetea kwa nini  wasifutiwe dhamana baada ya kukiuka masharti.

    Ijumaa iliyopita Novemba 15, 2019 mahakama hiyo iliamuru wabunge hao, Mchungaji Peter Msigwa; John Heche ; Halima Mdee  na Ester Bulaya  kukamatwa baada ya kukiuka masharti ya dhamana kwa kutofika mahakamani kusikiliza kesi ya uchochezi inayowakabili.

    Wabunge hao wamerudishwa mahabusu na kutakiwa kufikishwa mahakamani hapo kesho saa 4:30 asubuhi ili mahakama hiyo itoe uamuzi.

    Amri ya kukamatwa ilitolewa na Hakimu Simba baada ya washtakiwa hao kutokuwepo mahakamani bila taarifa yoyote wala wadhamini wao.

    Wakijieleza kwanini wasifutiwe dhamana kwa nyakati tofauti akianza Msigwa aliomba radhi kwamba haikuwa nia yake kuidharau mahakama, tangu kesi ianze hajawahi kuchelewa, hajawahi kukaidi amri ya mahakama na kwamba anaheshimu kiti cha hakimu.

    Amedai alitokea Dodoma alidhani kesi ni saa nne na nusu kama kawaida akiwa na Heche lakini walipofika walikuta kesi imeisha na jitihada za kumuona hakimu kumaliza tatizo hilo zilishindikana.

    Kwa upande wake Mdee pia ameomba radhi, ameonyesha jinsi anavyoiheshimu mahakama na kwamba alichelewa kwa kuwa alipitia kupima presha zahanati na alipofika kesi ikawa imeisha na amri imeshatolewa na wadhamini wake waliwahi lakini hawakufanikiwa kumaliza tatizo hilo Novemba 15 kwa kuwa waliambiwa amri ilishatolewa.

    Heche amedai aliomba asifutiwe dhamana, anadai anaheshimu mahakama, hajawahi kuidharau, siku ya kesi ilikuwa Dar es Salaam lakini alijua kama kawaida kesi yao inasikilizwa saa nne na nusu hivyo alipofika alikuta imeahirishwa.

    Akijitetea Bulaya amedai Novemba 14 alienda msibani Singida kumzika mama yake mdogo lakini aliwapa taarifa wadhamini wake ambao siku ya kesi walikuwepo katika eneo la mahakama.

    CHADEMA Yapata Pigo.....Ni Baada ya Meya wa Arusha Kalisti Lazaro Kujiunga CCM

    $
    0
    0
    Wakati kampeni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa zikiendelea nchini, aliyekuwa Meya wa Jiji la Arusha Kalisti Lazaro amejiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kupokelewa na Ndg. Humphrey Polepole Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM.

    Ndugu Kalisti Lazaro aliyefika katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM Lumumba jijini Dar es Salaam ameeleza amefikia uamuzi huo baada ya kupitia wakati mgumu akiwa katika Wadhifa wake wa Meya wa Jiji la Arusha.

    Ndugu Kalisti amesema amepokea barua za maonyo mara kadhaa kutoka Uongozi wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ambazo zilimtaka kutokutoa ushirikiano na Viongozi wa Serikali ambao anatakiwa kufanya nao kazi ngazi ya Mkoa na Wilaya na kutompongeza hadharani Ndg. John Pombe Joseph Magufuli Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kazi nzuri ambayo ameifanya Nchini ikiwamo katika Mkoa wa Arusha.

    Vitisho vya mara kwa mara ikiwamo dhidi ya uhai wake ndio vimepelekea kujivua nafasi zake zote katika Chadema na kujiunga na CCM, Chama ambacho kinashughulika na utatuzi wa kero za wananchi. 

    Ndg. Lazaro pia amechukizwa na Chama chake kujitoa katika uchaguzi huku akiita kitendo hicho uvunjaji wa demokrasia ambacho ndani ya masaa mawili uamuzi wa Kamati Kuu ya Chadema iliwanyima mamilioni ya wapenda demokrasia haki ya kushiriki katika Uchaguzi huu wa Serikali za Mitaa, Vijiji na Vitongoji.

    Ndg. Kalisti Lazaro amesema sasa yuko tayari kuchapa kazi ya wananchi akiwa ndani ya Chama ya Mapinduzi na kwamba yuko tayari kwa maelekezo ya kazi kutoka Uongozi wa CCM.

    Ndg. Kalisti kwa kujiunga na CCM amejiuzuru nafasi ya Udiwani, Umeya wa Jiji la Arusha, Uenyekiti wa Mameya na Madiwani wote wa Chadema Nchini na Ujumbe wa Kamati Kuu ya Chadema.

    Ndugu Kalisti Lazaro atapokelewa rasmi na wanachama wa CCM Mkoa wa Arusha katika tarehe itakayopangwa hivi karibuni.

    Imetolewa na,
    IDARA YA ITIKADI NA UENEZI
    CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM)
    Viewing all 45270 articles
    Browse latest View live




    Latest Images