Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Serikali Yawataka Wananchi Wapuuze Ujumbe Unaotumia Jina La Waziri Mkuu Majaliwa

$
0
0
Ofisi ya Idara ya Habari Maelezo, imesema kwamba, taarifa zinazosambazwa kwenye mitandao ya kijamii ikiwepo Whatsapp kuhusu kampuni ya mikopo iliyosajiliwa kwa jina la Waziri Mkuu, 'Kassim Majaliwa Foundation' haihusiki na kiongozi huyo.
 
Taarifa hiyo iliyotolewa siku ya leo imesema kwamba ujumbe huo umekuwa ukiwataka wajasiriamali watume pesa  ili waweze kupatiwa pesa ndani ya saa 24.

Wananchi wameaswa kupuuza ujumbe huo huku hatua kali za kisheria zikiwa zinachukuliwa kwa wahalifu hao wanachafua jina la Waziri Mkuu.

Hata hivyo taarifa hiyo imesisitiza kwamba, Waziri Mkuu hamiliki, hausiki wala hajasijili kampuni ya aina hiyo ya utoaji mikopo.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Ijumaa ya March 22

Migogoro Mikubwa 14 Kati Ya 29 Yatatuliwa Na Wizara Ya Mifugo Na Uvuvi

$
0
0
Na. Edward Kondela
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega amesema wizara kupitia timu yake maalum ya kushughulikia migogoro, hadi sasa imetatua migogoro mikubwa 14 kati ya 29 inayohusisha wakulima na wafugaji pamoja na hifadhi na wawekezaji.

Naibu Waziri Ulega amebainisha hayo alipokuwa akizungumza na Mkuu wa Wilaya ya Hai Mkoani Kilimanjaro Mhe. Lengai Ole Sabaya pamoja na viongozi wengine wa wilaya hiyo, mara baada ya kuarifiwa kuwepo kwa mgogoro wa wakulima na wafugaji katika Wilaya ya Hai na kubainisha kuwa ni hatari kwa jamii inayoishi pamoja kuwa na mgogoro wa aina hiyo.

“Nitamsisitiza katibu mkuu mifugo aliangalie kwa karibu sana hili kwa sababu ni hatari sana kwa jamii inayoishi pamoja kutokuwa na maelewano ya kuachiana maeneo kwa ajili ya shughuli zao za kiuchumi.” Alisema Mhe. Ulega

Mhe. Ulega ametoa kauli hiyo baada ya Mkuu wa Wilaya ya Hai Mhe. Lengai Ole Sabaya kumuarifu kuwa baadhi ya maeneo yenye migogoro ni Kata ya KIA ambapo wafugaji wamekuwa wakiingiza mifugo yao katika maeneo ya uwanja wa ndege wa KIA, pamoja na wakulima wilayani humo kutotaka kuwaachia wafugaji maeneo wasiyoyatumia kwa kilimo hususan yenye magadi kwa ajili ya malisho kwa wafugaji hivyo kutengeneza chuki dhidi yao.

Naibu Waziri Ulega amemshauri pia mkuu huyo wa wilaya kutumia Chuo cha Mifugo Tengeru na Kituo cha Uhimilishaji cha Taifa (NAIC) vilivyopo Mkoani Arusha ili kuleta mabadiliko kwa wafugaji katika Wilaya ya Hai Mkoani Kilimanjaro kwa kuwa na ng’ombe wachache na wenye tija ukizingatia ukanda huo kuna kiwanda cha maziwa cha Tanga Fresh ambacho kinahitaji maziwa kwa wingi katika uzalishaji wao.

“Ukanda huu kuna kiwanda cha maziwa cha Tanga Fresh ambacho kinahitaji lita laki moja ya maziwa kwa siku na bado hayatoshelezi hadi inawalazimu kuchukua maziwa kutoka mikoa ya Iringa na Njombe ni vyema mkashirikiana na wizara kutoa elimu ili wafugaji wa wilaya hii wabadilike kwa kufuga kisasa hususan ng’ombe wa maziwa badala ya kuwa na ng’ombe wengi wasio na tija kiuchumi.” Alisema Mhe. Ulega

Naibu Waziri Ulega amemshauri pia mkuu wa wilaya Mhe. Sabaya kuwa na kampeni maalum ya kutoa elimu kwa wafugaji pamoja na kushirikiana na wataalam ili wilaya hiyo iwe ya mfano katika kubadilisha fikra za wafugaji.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya Hai Mhe. Lengai Ole Sabaya amesema changamoto kubwa zilizopo wilayani hapo ni mgogoro kati ya wakulima na wafugaji ambao tayari upo katika hatua mbalimbali za kutatuliwa pamoja na wafugaji kutokuwa tayari kubadilika kutoka kwenye ufugaji wa zamani wa kuwa na makundi makubwa ya mifugo isiyo na tija.

Kufuatia mazungumzo baina yake na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Ulega, mkuu huyo wa wilaya amesema atazidi kushirikiana na wizara hiyo ili kuhakikisha changamoto hizo zinatatulika na kuifanya wilaya hiyo kuzidi kunufaika na mifugo iliyopo.

Mwisho.

Waziri Mkuu Mgeni Rasmi Mechi Ya Taifa Stars Na The Uganda Cranes Jumapili Taifa

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, atakuwa mgeni rasmi katika mechi ya kuwania tiketi ya kufuzu Fainali za Afrika kati ya wenyeji Timu ya Taifa (Taifa Stars) dhidi ya Uganda (Cranes) itakayochezwa keshokutwa Jumapili kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Akizungumza jijini jana, Mwenyekiti wa Kamati ya Ushindi ya Taifa Stars, Paul Makonda ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam alisema kuwa wanaamini ujio wa kiongozi huyo utaongeza morali kwa wachezaji kwa ajili ya kusaka ushindi katika mchezo huo.

Makonda alisema kuwa kamati yake inawaomba wazalendo kujitokeza kushangilia katika mechi hiyo, ambayo Tanzania inajiandaa kuweka historia nyingine ya kufuzu fainali hizo baada ya kukosa kwa miaka 39.

"Mgeni rasmi katika mechi hii kubwa na muhimu kwa nchi yetu atakuwa ni Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, tunaamini kila kitu kitakwenda vema na ili tuweze kutimiza ndoto zetu, kila shabiki anatakiwa kufika uwanjani kuishangilia Taifa Stars," alisema Makonda.

Wakati huo huo, wasanii wa bongo flava, filamu, watangazaji na watu wengine mbalimbali maarufu akiwamo mrembo wa Tanzania wa mwaka 2006, Wema Sepetu walijitokeza jana kuhamasisha Watanzania kujitokeza kuishangilia Taifa Stars katika mchezo huo wa mwisho wa hatua ya makundi.

Video: Queen Darleen - Muhogo

Video: Tid X Q Chief - Najidai

$
0
0
Video:  Tid X Q Chief - Najidai

CUF Zanzibar kukagua ofisi zake Zilizobadilishwa Rangi

$
0
0
Makamu mwenyekiti wa CUF Zanzibar,  Abass Juma Muhunzi amesema chama hicho kitafanya ziara katika ofisi zake zote Zanzibar baada ya kumalizika kile alichokiita ‘vurugu’ alizodai kufanywa na wanachama wa chama cha ACT-Wazalendo.

Ametoa kauli hiyo jana Alhamisi Machi 21, 2019 katika mkutano wake na waandishi wa habari kuzungumzia vitendo vya ofisi za CUF kubadilishwa kuwa na ACT, baada ya aliyekuwa Katibu Mkuu wa chama hicho, Maalim Seif Sharif Hamad kujiunga na ACT.

Alisema licha ya kuwa na mpango wa kuyatembea matawi hayo ili kupanga mikakati kichama, lakini wakati huu hawawezi kufanya hivyo kutokana na wanachama wa ACT kupaka rangi za chama hicho ofisi za CUF.

Mafundi Umeme Kortini kwa Rushwa la Laki 1

$
0
0
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Wilaya ya Kondoa, mkoani hapa imewafikisha mahakamani mafundi umeme, Ally Manyundo na Ibrahim Seleman kwa kosa la kuomba rushwa ya Sh 100,000.

Kati ya fedha hizo tayari walipokea Sh 60,000 ili waweke nguzo za umeme karibu na nyumba ya mtoa taarifa.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana na Kamanda wa Takukuru Mkoa wa Dodoma, Sostenes Kibwengo, Manyundo ni fundi umeme na mwajiriwa wa Kampuni ya MF Electrical Engineering Company Limited na Selemani ni kibarua kwenye kampuni hiyo.

Akiwasomea mashtaka mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Kondoa, Lucas Jang’andu baada ya kufunguliwa kesi ya jinai Namba 56/2019, Mwendesha Mashtaka wa Takukuru, Leonard Haule aliiambia mahakama hiyo kuwa washtakiwa wametenda kosa la kuomba na kupokea rushwa kinyume na Kifungu cha 15 (1) (a) na (2) ya Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Na. 11 ya mwaka 2007.
 
Mwendesha Mashitaka huyo alidai kuwa washtakiwa hao kati ya Machi 8 na Machi 10 mwaka huu, wakiwa katika Kijiji cha Kiteo Wilaya ya Kondoa Mkoa wa Dodoma waliomba Sh 100,000 na kupokea kiasi cha Sh 60,000 kama rushwa kwa ajili ya kuweka nguzo ya umeme karibu na nyumba ya mtoa taarifa.

Alisema washtakiwa hawakukidhi masharti ya dhamana, hivyo walipelekwa rumande hadi Machi 22 mwaka huu kesi hiyo itakaposikilizwa.

Wavamizi Shamba La Miti Biharamulo Wapewa Miezi 3

$
0
0
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu ametoa muda wa miezi mitatu kwa wananchi waliovamia na kuanzisha shughuli za kibinadamu ndani ya Shamba la miti la Biharamulo kuondoka mara moja kwa hiari yao bila shuruti kabla ya mwezi Juni mwaka huu.

Ametoa muda huo ili wananchi  waliolima   mazao mbalimbali yakiwemo  mahindi na pamba  waweze kuvuna mazao yao  kabla ya kuanza kwa oparesheni maalum ya kuwaondoa, iliyopangwa kufanyika mwanzoni mwa mwezi Julai mwaka huu itakayofanywa na Wakala wa Huduma ya Misitu Tanzania ( TFS) kwa kushirikiana na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya wilaya hiyo.

Mhe.Kanyasu  ametoa agizo hilo wakati wa ziara yake ya kikazi ya   kutembelea shamba la miti Biharamulo lililopo katika wilaya ya Chato mkoani Geita.

Amesema Oparesheni hiyo haitasubiri taarifa ya Wizara tano inayoendelea kufanyiwa kazi kwa kuwa eneo hilo halihusiani na vile vijiji 366  vilivyokutwa ndani ya Hifadhi.

Amesema  haiwezekani wananchi waliovamia eneo hilo waendelee kuachwa kwa kisingizio cha Kauli ya Rais aliyoitoa Januari 15 mwaka huu kuhusiana na vijiji 366 vilivyokutwa ndani ya maeneo ya Hifadhi.

Amebainisha kuwa wananchi waliovamia eneo hilo wameitafsiri visivyo Kauli hiyo na kuongeza kuwa baada tu ya tamko la Mhe. Rais , baadhi ya wananchi hata wale waliokuwa wakiishi  katika maeneo mengine nje ya hifadhi waliendelea  kuvamia na kuanza kujimilikishia  maeneo makubwa  wakidai kuhalalishwa na tamko la Rais.

Amefafanua kuwa taarifa inayoendelea kufanyiwa kazi  na timu ya Mawaziri na Makatibu Wakuu kutoka Wizara tano imebainisha kuwa mpaka sasa zaidi ya vijiji 700 vimekutwa ndani ya Hifadhi badala 366 vilivyoripotiwa awali.

Kufuatia hali hiyo amesema baadhi ya wavamizi wa Hifadhi katika maeneo mbalimbali wataendelea kuondolewa bila kusubili kukamilika kwa zoezi linaloendelea kwa kuwa walieendelea kuvamia maeneo ya Hifadhi kwa kisingizio cha tamko la Rais huku maeneo hayo yakizidi kuharibiwa kwa miti kukatwa na shughuli nyingi za kibinadamu

Katika hatua nyingine, Mhe.Kanyasu ameiagiza Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania ( TFS) kutenga Bajeti ya kugharamia operesheni ya kuwaondoa  wavamizi ndani ya Shamba hilo.

Ameitaka TFS kuendesha oparesheni za mara kwa mara ili wavamizi hao wajue Serikali ipo kazini kulinda rasilimali za Taifa muda wote.

Awali, Mkuu wa Wilaya ya Chato,  Mtemi Simeoni akizungumza katika ziara hiyo  alisema kuwa  baadhi ya wananchi kutoka nje ya wilaya hiyo wamekua wakivamia na kuanzisha shughuli za kibinadamu ndani ya Shamba hilo, suala ambalo ni kinyume cha sheria.

Mkuu huyo wa wilaya amebainisha kuwa wananchi katika maenro hayo wana mahitaji makubwa ardhi na kuiomba Wizara iangalie  namna ya kuwasaidia  hekari 5000 ili wapate maeneo ya kulima na kuchungia mifugo yao.

Kwa upande wake Meneja wa Shamba hilo Bw. Thadeus Shirima  amemweleza Naibu Waziri huyo kuwa hadi sasa zaidi ya hekari 900 zimepandwa miti licha ya Shamba hilo  kukabiliwa  na changamoto ya uhaba wa watumishi pamoja na vitendea kazi.

CUF yatoa msimamo, kuhusu wabunge wanaomuunga mkono Maalim Seif

$
0
0
Katibu Mkuu mpya wa Chama Cha Wananchi CUF, Khalifa Suleiman Khalifa amesema chama chao hakina haja ya kuungwa mkono na wabunge wake ambao walikuwa upande wa Maalim Seif kwa kile alichokidai hata wakati wa mgogoro huo walikuwa hawaungwi mkono.

Khalifa Suleyman ametoa kauli hiyo wakati akizungumza kwenye kipindi cha East Africa Breaks cha East Africa Radio ambapo amesema kwa sasa wapo kwenye ujenzi wa chama chao hivyo hawahitaji tena migogoro na wako tayari kufanya kazi na Mbunge yeyote akiomba msamaha.

"Sisi hatuwahitaji wabunge kiasi hicho, kwa sababu tulienda kipindi cha mgogoro hawajatusaidia chochote walitutukana na walitudhalilisha ila sisi tunasema yameshaisha, tujenge chama.

"Watu wenye mtihani mkubwa kwa sasa ni wabunge wa CUF, mimi nafikiri wanapaswa kuwa na busara sana, kwa upande wetu wabunge wametuumiza sana, wabunge wametumia pesa zao kutuumiza sana sisi tunaomuunga mkono Lipumba." amesema Khalifa

Mgogoro wa Chama Cha Wananchi (CUF) umedumu kwa zaidi ya miaka 3, mpaka pale Mahakama ilipotoa uamuzi kuwa Profesa Ibrahim Lipumba ndiye Mwenyekiti halali wa chama hicho na kupelekea aliyekuwa Katibu Mkuu wa CUF Maalim Seif kuhamia ACT - Wazalendo.

Seikali yasimamisha biashara chuma chakavu

$
0
0
Serikali  imezuia biashara ya kuingiza na kusafirisha nje  ya nchi taka zenye madhara vikiwamo vyuma chakavu, betri zilizotumika na taka za  eletroniki mpaka utaratibu mpya utakapotolewa.

Taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Makamu wa Rais   Dar es Salaam jana, imewataka watu wanaojihusisha na biashara ya ukusanyaji, usafirishaji, urejerezaji wa vyuma chakavu, taka za  elektroniki, taka za kemikali, mafuta machafu, taka zitokanazo na huduma za afya na betri zilizotumika kujiandikisha upya Baraza ka Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira na kupata vibali vipya kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais.

Utaratibu huo mpya utajumuisha ukaguzi wa uwezo wa waombaji wa kufanya shughuli hizo huku wafanyabishara wakionywa kutopokea taka hizo kutoka kwa mtu asiyekuwa na kibali kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais.

Taarifa hiyo ilitolewa   baada ya ziara ya ghafla ya Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), January Makamba, katika Bandari ya Dar es Salaam.

Makamba  alitoa maelekezo na maagizo kuhusu utaratibu mpya wa biashara ya taka zenye madhara, baada ya kuwapo ukiukwaji wa Sheria ya Mazingira ya Mwaka 2004, kanuni za sheria hiyo na Mkataba wa Kimataifa wa Basel kuhusu taka zenye madhara.

Alisema Ofisi ya Makamu wa Rais inakusudia kubadilisha Kanuni za Usimamizi wa Mazingira za Mwaka 2009 na kuandika kanuni mpya za taka za  elekroniki kuweka udhibiti bora zaidi.

Wakati serikali ikitoa agizo hilo, tayari kuna makontena 44 ya vyuma chakavu katika Bandari ya Dar es Salaam na   Waziri Makamba na ujumbe wake wamekuta makontena 10.

“Lazima jambo hili lifuatiliwe kujua nani waliohusika na jambo hili wakati taarifa ya kusimamisha usafirishaji imekwisha kutolewa,” alisema.

Ilibainika kuwapo mzigo wa vyuma chakavu ulioingizwa nchini kwa majahazi  kama “loose cargo” kutoka Comoro kupitia Zanzibar.

“Tunawasihi wananchi wote pia kutoa taarifa haraka kwa mamlaka husika, ikiwamo NEMC na Ofisi ya Makamu wa Rais,  wanapohisi au kuona mtu au kampuni yoyote inaingiza nchini taka za aina yoyote kutoka nje ya nchi au ukusanyaji wa vyuma  chakavu, taka za elektroniki na betri zilizotumika na utupaji wa taka za hospitali unafanyika kinyume cha utaratibu,” alisema Makamba katika taarifa hiyo.

Katika ziara hiyo, Waziri Makamba aliambatana na Mkurugenzi Mkuu wa NEMC, Dk. Samuel Gwamaka na maofisa waandamizi wa baraza hilo.

Rais wa zamani wa Brazil Temer akamatwa

$
0
0
Aliyekuwa rais wa Brazil Michel Temer amekamatwa katika Operesheni ya uchunguzi wa rushwa inayoendelea Brazil kwa jina la Operation Car Wash. Temer analengwa katika uchunguzi wa kesi kadhaa za ufisadi. 

Anatuhuiwa kwa kuwa kiongozi wa kundi la uhalifu linalojihusisha na utakatishaji fedha na ubadhirifu. 

Rais huyo wa zamani pia anatuhumiwa kwa kupokea hongo, ikiwa ni pamoja na inayohusishwa na ujenzi wa kiwanda cha nyuklia cha Angra dos Reis katika jimbo la kusini mwa Rio de Janeiro. 

Temer ni rais wa zamani wa tatu mfululizo nchini Brazil kukabiliwa na mashtaka ya uhalifu, baada ya Luiz Inacio Lula da Silva na mwanafunzi wake Dilma Rousseff. 

Uchunguzi huo wa ufisadi, ulioanza Mei 2014, umewanasa wanasiasa wengi wa Brazil pamoja na makampuni kadhaa makubwa, kama vile kampuni kubwa ya ujenzi ya Odebrecht na hasa kampuni ya mafuta ya Brazil inayomilikiwa kwa sehemu na serikali ya Petrobas. 

Michel Temer alichukua madaraka Agosti 2016, baada ya mtangulizi wake Dilma Rousseff kuvuliwa madaraka.

Askari wanne wasimamishwa kazi kwa kuingiza simu na dawa za kulevya gerezani

$
0
0
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni amemuagiza Kamishna Jenerali wa Magereze, Phaustine Kasike kuwasimamisha kazi Askari wanne wa Gereza la Ruanda jijini Mbeya kwa tuhuma za kushirikiana na wafungwa kuingiza simu na dawa za kulevya ndani ya Gereza.

Masauni alitoa agizo hilo jana alipokuwa anazungumza na wandishi wa Habari kwenye Ofisi ya Kamanda wa Polisi wa Mkoani wa Mbeya ambapo alisema alibaini ukiukwaji huo wa sheria na maadili ya magereza alipofanya upekuzi kwa kushirikiana na baadhi ya maofisa wa Gereza hilo.

Alisema katika upekuzi huo waliwakuta wafungwa wakiwa na simu Tisa pamoja na dawa za kulevya aina ya bangi ambazo ziliingizwa gerezani kwa ushirikiano wa maaskari na wafungwa hao.

Aliwataja askari waliohusika kwenye tukio hilo ambao wanatakiwa kusimamishwa kuwa ni Inspecta Longino Mwemezi, WDR Ramadhan Mhagama na wengine Sajinitaji Alexander Mwijano na Benjamini Malango wote wenye cheo cha Sajintaji.

Taarifa ya Jeshi la Polisi Toka Mkoani Mbeya

$
0
0
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linawashikilia watu watatu kwa tuhuma mbalimbali.

KUINGIA NCHINI BILA KIBALI,
Mnamo tarehe 21.03.2019 saa 16:30 jioni huko eneo na Kata ya Lupa Tingatinga, Tarafa ya Kipambawe. Wilaya ya Chunya, Mkoa wa Mbeya. Polisi walimkamata OMARY JUMA @MWAMI [21] raia wa nchi ya Burundi akiwa ameingia nchini bila kibali na kufanya shughuli za kilimo cha Tumbaku. Upelelezi unaendelea.

UNYANG’ANYI WA KUTUMIA NGUVU
Mnamo tarehe 21.03.2019 saa 00:30 usiku huko maeneo ya Veta Kata ya Ilemi, Tarafa ya Iyunga ndani ya Jiji na Mkoa wa Mbeya. IMAN ANDISON [20] Dereva bodaboda na mkazi wa Simike alinyang’anywa pikipiki yake yenye namba za usajili MC 833 BVS aina ya Kinglion na watu watatu wasiofahamika.
Mbinu iliyotumika ni kwamba muhanga akiwa amepaki pikipiki yake maeneo ya Kiwira Motel alitokea abiria mmoja na kutaka apelekwe Veta na ndipo alipomfikisha maeneo hayo walijitokeza watu wengine wawili na kumvamia kisha kumjeruhi kichwani na watu hao kutokomea na pikipiki hiyo. Majeruhi amelazwa Hospitali ya Rufaa Mbeya. Uchunguzi/upelelezi unaendelea kuwabaini waliohusika katika tukio hilo.

KUINGIZA NCHINI BIDHAA BILA KULIPIA USHURU.
Mnamo tarehe 22.03.2019 saa 07:00 asubuhi huko Uwanja wa Siasa uliopo Kata ya Mbugani, Tarafa ya Unyakyusa, Wilaya ya Kyela, Mkoa wa Mbeya, Polisi wakiwa Doria walimkatama mtu mmoja aitwaye ZACHARIA MWANGUKULU [28] Mkazi wa Mbugani akiwa ameingiza nchini bidhaa mbalimbali bila kulipia ushuru.

Bidhaa alizokamatwa nazo mtuhumiwa ni:-
Mipira ya kiume [Condoms] aina ya Chishango Boksi 45.
Juisi aina ya BAK’S Boksi 27
Mafuta ya Kula aina ya Cook Well ndoo moja yenye ujazo wa lita 10
Mifuko ya Plastiki aina ya Soft vifurushi 03

Bidhaa hizo zilikuwa zikisafirishwa kwenye gari lenye namba za usajili T.532 CGU aina ya Toyota Noah iliyokuwa ikiendeshwa na dereva aitwaye ABRAHAM MWARABU [32] Mkazi wa Njisi Kasumulu Kyela ambaye naye amekamatwa.
Bidhaa hizo zimeingizwa nchini zikitokea nchi jirani ya Malawi kwa kutumia njia na vivuko visivyo halali. Taratibu za kuzikabidhi bidhaa hizo Mamlaka ya Mapato Tanzania zinafanyika.

Imetolewa na:
[ULRICH O. MATEI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA

Chadema kupinga Sheria Vyama vya Siasa mahakamani

$
0
0
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema kitafungua kesi mahakamani kupinga Sheria ya Vyama vya Siasa Sheria ambayo wamedai ni mbaya kutokana na vifungu vyake kukiuka Katiba, misingi ya utawala bora na mikataba mbalimbali  ya kimataifa ambayo Tanzania imetia saini.     
                   
Mkurugenzi wa Itikadi, Mawasiliano na Mambo ya Nje wa Chadema, John Mrema, katika taarifa yake kwa vyombo vya habari aliyoitoa leo Ijumaa Machi 22, amesema dhamira yao hiyo iko palepale ambapo wanaendelea kushauriana na vyama vingine na wadau mbalimbali njia nzuri zaidi ya kufungua shauri hilo mahakamani mapema iwezekanavyo.

“Sheria hii imeenda kufanya shughuli za kisiasa nchini kuwa ni jinai kwani kila kifungu cha sheria hii kimeweka adhabu ya faini,  kifungo au vyote kwa pamoja kwa  wanasiasa, ila Msajili na Serikali na vyombo vyake hakuna kifungu hata kimoja ambacho kinawagusa kama wakikiuka utekelezaji wa sheria hii.

“Mathalani kifungu cha 3 (b), kimempa Msajili wa Vyama vya Siasa jukumu la kusimamia chaguzi za ndani ya Vyama ikiwa ni Pamoja na teuzi za wagombea wa nafasi mbalimbali.

“Hii inampa Msajili mamlaka ya kuingilia vyama na kuviamulia ni nani awe kiongozi wa chama husika au mgombea wa nafasi ya kiserikali kama mgombea urais na ubunge,  hii ni kinyume na Katiba ya nchi ambayo imetoa fursa na haki ya kujumuika kwa wananchi wake,” imesema taarifa hiyo.   


Bunge Laitakia Ushindi Mnono Taifa Stars Dhidi Ya Uganda Jumapili,machi 24.

$
0
0
Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Katibu    wa timu ya Bunge La Jamhuri ya Muungano wa Tanzania [Bunge sports],Mhe.William Ngeleja amewahakikishia Watanzania kuwa Bunge litakuwa pamoja  na Watanzania katika kuitakia ushindi mnono timu ya Taifa Stars dhidi ya Uganda hapo Jumapili Machi 24 katika kujiweka  vyema katika mashindano ya AFCON 2020. 

Mhe.Ngeleja ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Sengerema mkoani Mwanza ameyasema hayo leo  Machi 22 wakati akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa kitengo cha habari bungeni  jijini  Dodoma. 

Ngeleja amesema kuwa Bunge lina imani kubwa na timu ya taifa Stars pamoja na benchi la ufundi lililoteuliwa na waziri wa Habari,Sanaa,Utamaduni na Michezo Dokta Harrison Mwakyembe.
 
Amesema kila mtanzania kwa imani yake anatakiwa kuiombea timu ya Taifa Stars kushinda  katika Mchezo huo ili iweze kusonga mbele zaidi. 

Naye kocha mkuu wa timu ya Bunge[Bunge Sports] Mhe.Venance Mwamoto ambaye ni mbunge wa  Kilolo Mkoani Iringa amewaasa watanzania kuwa na uzalendo na timu yao kwa kuvaa jezi za Taifa la Tanzania wakati wakishangilia popote pale . 

Aidha Mhe.Mwamoto amewaasa watanzania kushangilia Mwanzo mwisho ili kuipa hamasa ya Kushinda timu hiyo.
Hata hivyo  Mhe.Ngeleja na Mhe.Mwamoto wameiahidi Timu ya Taifa Stars kuwa Bunge lipo tayari kuwasaport  pindi wafanyapo vizuri  la litaishauri serikali kuongeza bajeti kwenye timu ya Taifa.

Waziri Mkuu Azindua Kiwanda Cha Kuchakata Muhogo......Awataka wakulima kuchangamkia fursa kwa kulima kwa wingi

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka wananchi katika mikoa ya Lindi na Mtwara watumie fursa ya uwepo wa kiwanda cha kuchakata muhogo katika kijiji cha Mbalala, kata ya Nyengedi mkoani Lindi kwa kulima zao hilo kwa wingi ili waweze kujiongezea kipato.

“Kama unataka pesa nenda kalime muhogo kwani kuna soko la uhakika na pia zao hili ni la muda mfupi na kilimo chake ni rahisi. Kwa sasa hatuna muda wa kukaa vijiweni vijana jiungeni katika makundi na muanzishe mashamba ya mihogo soko lipo tena mwenye kiwanda atawafuata hukohuko shambani.”

Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Ijumaa, Machi 22, 2019) wakati akifungua kiwanda cha kuchakata muhogo cha Kampuni ya Cassava Starch of Tanzania Corporation Limited (CSTC) kilichopo katika kijiji cha Mbalala, kata ya Nyengedi mkoani Lindi.

Amesema lengo la Serikali ya Awamu ya Tano, inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli la kuhamasisha ujenzi wa viwanda ni kusaidia katika kuongeza thamani ya mazao mbalimbali yanayolimwa na wakulima nchini kabla ya kuuzwa.” Mbali na kuongeza tija kwa wakulima pia viwanda vinatoa ajira nyingi”.

Kadhalika, Waziri Mkuu amekipongeza kituo cha utafiti wa mazao ya kilimo cha Naliendele kilichopo mkoani Mtwara kwa kazi nzuri ya utafiti wa mbegu za mazao mbalimbali wanayoifanya. Amesema kituo hicho ndicho kilichotafiti mbegu bora za muhogo zenye uwezo wa kuzalisha tani 20 hadi 50 kwa hekta.

Kwa upande wake, Balozi wa ufaransa nchini, Balozi Frederic Clavier amesema Serikali ya Ufaransa ipo tayari kumuunga mkono Rais Dkt. Magufuli katika mkakati wake wa kukuza uchumi hadi kufikia uchumi wa kati kwa kupitia sekta ya viwanda ifikapo 2025.

Amesema ujenzi wa kiwanda hicho ni ushuhuda tosha wa ushirikiano mzuri uliopo baina ya Serikali ya Tanzania na Serikali ya Ufaransa na kilimo ni miongoni mwa mikakati ya kuinua uchumi wa Tanzania.

Nae, Naibu Waziri wa Kilimo Omary Mgumba amewashukuru wawekezaji hao kwa uamuzi wao wa kujenga kiwanda cha kuchakata muhogo nchini kwa kuwa wamewezesha wakulima wa zao hilo kupata soko la uhakika na vijana wengi kupata ajira.

Kwa upande wake,Mbunge wa jimbo la Mtama, Nape Nnauye amemshukuru Rais Dkt. Magufuli kwa msukumo alioutoa wa kuhamasisha ujenzi wa viwanda nchini kwa kuwa umechangia kuboresha maendeleo ya wananchi katika maeneo mbalimbali.

Mbunge huyo amesema uwekezaji katika sekta ya viwanda umesaidia kupunguza changamoto ya ajira hususani kwa vijana. “Tunamshukuru Mheshimiwa Rais Dkt. Magufuli kwa juhudi zake, kwani hatukutarajia kuwa na kiwanda katika eneo hili”.

Awali,Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya CSTC, Christophe Gallean alisema kiwanda hicho ambacho kilianza kujengwa mwaka 2012 kinazalisha unga wa muhogo wenye kiwango cha juu cha ubora na kinauza unga huo katika nchi za Afrika Mashariki, Kusini, Mashariki ya Kati, Ulaya na Marekani.

Alisema kiwanda hicho chenye wafanyakazi zaidi ya 420 ambapo Watanzania ni asilimia 97 kina uwezo wa kuchakata tani 60 za muhogo mbichi kwa siku, ambao ni sawa na tani 25 za unga bora wa muhogo kwa siku.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumamosi ya March 23

Viwanja vya Makazi Vinauzwa Mapinga Kimere

$
0
0
VIWANJA VYA MAKAZI MAPINGA KIMERE
Viwanja vya makazi vinauzwa MAPINGA, KIMERE Mingoi.Viwanja vipo Mtaa wa Kimere ni Km 5 kutoka Bunju( Km 3 tu kutoka Mainroad Bagamoyo)


Vipo viwanja vinane(8)......Vipo viwanja vya ukubwa na bei tofauti kama ifuatavyo:
Sqm 400(20×20)kwa bei ya mill 3.5
Sqm 540(20×27)kwa bei ya mill 5

Luksa kulipa kwa Cash au kwa Awamu (anza na 50% maliza na 50% ndani ya miezi 3)

Miundo mbinu ya  barabara ipo vizuri sana,maji na umeme vipo karibu sana na viwanja.

Piga Simu kwa muhusika
0713909842/0759463410

Ukipata ujumbe huu mjurishe ndugu,Jamaa na Marafiki.

Waziri wa Afya Ummy Mwalimu Awataka NHIF Kuwalipa Watoa Huduma Ndani ya Siku 30

$
0
0
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, ameuagiza Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), kulipa madeni ya hospitali zinazotoa huduma za bima ndani ya mwezi mmoja.

Ummy alitoa agizo hilo jana, jijini Dar es Salaam, baada ya Ofisa Mtendaji Mkuu wa Hospitali ya CCBRT, Brenda Msangi, kusema hiyo ni changamoto wanayokutana nayo katika utoaji wa huduma kwenye jengo la huduma binafsi lililozinduliwa hospitalini hapo.

Mtendaji mkuu huyo alieleza changamoto hiyo wakati wa uzinduzi wa jengo la kutoa huduma binafsi za kibingwa kwa wagonjwa wa nje.

Msangi alisema miongoni mwa changamoto wanazokabiliana nazo kwenye utoaji wa huduma binafsi ni ongezeko la wagonjwa, hivyo mifuko ya bima ya afya, ukiwamo NHIF usipotoa malipo kwa wakati husababisha shida kwao.

Kutokana na changamoto hiyo, Waziri Ummy, wakati akizindua jengo hilo, alisema alishaielekeza NHIF kwamba kama mtu ameshatoa huduma kwa wateja, alipwe ndani ya mwezi mmoja.

“NHIF mpo hapa? Nataka ndani ya mwezi mmoja muwe mmewalipa watoa huduma kwa wanachama wenu. Kama mtu amefanya kazi mjitahidi mumlipe, maana mnajificha kwenye kivuli cha kuhakiki. Mnahakiki kitu gani kisichoisha?” Alihoji.

“Nanawaomba na nyie watoa huduma mpeleke madai yenu kwa wakati ili wayahakiki mapema,” alisema.

Katika mkutano huo, Waziri Ummy alibaini kwamba tatizo hilo haliko kwa watoa huduma bali NHIF kutokana na CCBRT kueleza kuwa madai ya mwezi uliopita yameshapelekwa NHIF.

“Kumbe tatizo liko kwetu NHIF. Nawaelekeza tusiwe kikwazo cha huduma bora kwa sababu mtoa huduma anategemea hizi fedha kulipa mishahara, kununua vifaa, kulipa umeme na maji. Tunataka watu waone raha ya kuwa na NHIF, sitaki mwisho wa siku watoa huduma waseme hatuzipokei bima kwa sababu malipo hawayapati kwa wakati,” alisisitiza.

Waziri Ummy pia aliwataka Watanzania waone umuhimu wa kuwa na bima kwa sababu ndiyo njia rahisi ya kupata huduma bila kikwazo cha fedha.

Alisema alikutana na kijana ambaye analipa fedha taslimu Sh. 50,000 ili kumwona daktari, gharama ambayo haihusishi vipimo na dawa.

“Nimemwambia NHIF kwa watu sita ni Sh. milioni 1.5, ukiigawa ni kama 250,000 kwa hiyo sisi tumeangalia mkiwa watu sita hawawezi kuumwa wote, kwa hiyo tunakamilisha utaratibu tuwe na bima ya afya ya mtu mmoja mmoja ili kila mtu ajipimie kifurushi chake,” alisema.

Alisema ndani ya wiki tatu, serikali itatangaza vifurushi vya mtu mmoja mmoja ambavyo vitawezesha Watanzania kupata huduma bora za afya.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images