Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

CHADEMA Kuwashitaki Mawaziri Waliopiga Kampeni Monduli

$
0
0
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHEDEMA) kanda ya Kaskazini, kimelalamikia kitendo cha mawaziri kujitokeza na kufanya kampeni za uchaguzi mdogo jimbo la Monduli na kimeeleza kitawafikisha kwenye kamati ya maadili ya taifa.

Katibu wa chama hicho kanda ya Kaskazini ambaye pia ni mwenyekiti wa chama mkoa wa Arusha, Amani Golugwa amesema mbali na malalamiko yao ya kutotendewa haki katika uchaguzi uliofanyika jana lakini watawashtaki mawaziri waliopiga kampeni.

''Sisi kama viongozi tulijipanga vyema kuanzia kampeni tumeona uvunjivu wa sheria mwingi na tumerekodi kila kitu ikiwemo mawaziri kuja kufanya kampeni huku wakiahidi utekelezaji wa miradi kitu ambacho ni kinyume na sheria ya uchaguzi hivyo tutawafikisha kwenye kamati ya taifa ya maadili'', amesema.

Amani Golugwa amewataja baadhi ya mawaziri waliofika jimboni Monduli wakati wa kampeni na kutoa ahadi ni pamoja na waziri wa Ardhi William Lukuvi, Naibu Waziri wa Maji Jumaa Aweso, pamoja na Naibu waziri wa Madini Mhe. Doto Mashaka Biteko.

Aidha Golugwa amefafanua kuwa katika kipindi hicho cha kampeni walishuhudia mawaziri hao wakitoa ahadi na kufanya baadhi ya mambo ambayo kimsingi yapo kinyume na sheria na taratibu za uchaguzi.

Tazama Hapa Mfanyakazi wa Hoteli Alivyojipatia 500,000 Kirahisi Kabisa

$
0
0
Manford Mtwango mkazi wa Kitunda Dar es Salaam, alivutiwa na Mojaspesho tu baada ya kusikia matangazo akaamua na yeye ajiingize kwenye hii fursa. Baada ya muda wa miezi minne ya kucheza mpaka kieleweke, kweli kimeeleweka mwezi huu wa tisa.

Manford ni kijana wa miaka 39 tu, ni muajiriwa kwenye hoteli moja kubwa jijini Dar es Salaam ambaye kajishindi mshiko wa papo hapo wa laki tano.
 

“Sikuamini huu mchezo mpaka pale nilipo pigiwa simu nimeshinda. Mojaspesho ni mchezo wa kweli na mrahisi, ushindi ni wa kweli na mkubwa”  
 
Manford alipata ushindi wake baada ya kucheza namba zake spesho 164 kwenye droo za dakika kumi. Ushindi unanukia, usikate tama kwani hauwezi kujua bahati yako imejificha tarehe gani.

Nawe pia unaweza kuwa mshindi kila siku na jackpot ya kila wiki. Jinsi ya kucheza Mojaspesho ni rahisi
1. Nenda kwenye menu yako ya #Mpesa, #TigoPesa, #AirtelMoney au #Halopesa;
2. Chagua lipia bili
3. Ingiza kampuni namba 123255
4. Ingiza kumbukumbu namba zako 3 za bahati zikifuatiwa na neno SEE mf. 123SEE
5. Weka kiasi kuanzia sh 1000 na utakua umecheza #Mojaspesho.

Mke na Mume Wauawa....Miili yao Yatupwa Mtoni

$
0
0
Watu watatu wakiwamo mume na mke wake, wakazi wa Mji mdogo wa Mlowo wilayani Mbozi Mkoa wa Songwe wamekutwa wameuawa na kisha miili yao kutupwa chini ya daraja la Mto Mlowo.

Waliofariki ni Luka Humri, Bahati Mohamed na mwingine ametambulika kwa jina maarufu la Mama Dina.

Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Nicodemas Mwangela amesema tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia   Septemba 17, 2018 na mtu wa tatu ni jirani wa mume na mke waliouawa.

Alisema wauaji hao baada ya kutekeleza tukio hilo wamewachukua kisha kwenda kuwatupa kwenye daraja la mto huo.

Mwangela amewaomba wakazi wa Mlowo kuwa watulivu wakati jeshi la Polisi likiendelea na uchunguzi wa tukio hilo.

“Niwaombe sana ndugu zangu hebu kuweni watulivu kutokana na tukio hilo baya kabisa. Lakini wakati vyombo vya ulinzi na usalama vikiendelea na uchunguzi wa kiini juu ya watu hawa kuawa, niwaombe tena toeni ushirikiano kwa vyombo hivi kwa yoyote kutoa taarifa zinazohitajika ili kuwabaini waliotekeleza mauaji haya,” amesema.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe, Mathias Nyange amesema wanandoa hao walikuwa wafanyabiashara katika Soko la Sokowo  na chanzo cha mauaji hayo bado hakijafahamika lakini upelelezi umeanza ikiwa ni pamoja kuwatambua kwa majina marehemu hao.

Lukuvi Amnyang'anya Hati ya Viwanja Mwekezaji

$
0
0
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Mendeleo ya Makazi, William Lukuvi  ameitaka kampuni ya Magarya engineering kurejesha haraka kwake hati ya umiliki wa viwanja vitano katika eneo la uwanja wa ndege wilayani Tarime ili eneo hilo liweze kukabidhiwa  kwa watu wengine kwaajili ya shughuli za maendeleo.

Agizo hilo amelitoa leo Septemba 18,2018 alipofika katika eneo hilo na wananchi kumuomba awasaidie ili waweze kumiliki viwanja hivyo na kufanya shughuli za maendeleo ikiwemo ujenzi wa shule ya msingi kwaajili ya wakazi wa eneo hilo.

Waziri Lukuvi alisema kutokana na mmiliki wa eneo hilo kushindwa kuliendeleza eneo lake japokuwa anamiliki hati kwa zaidi ya miaka 20 huku akishindwa kulipia kodi ya zaidi ya Sh40 milioni.

Amemtaka mmiliki wa kampuni hiyo aliyejulikana kwa Magarya Mwita Manko kuwasilisha hati hiyo kwake kabla hajaondoka wilayani Tarime leo na kuwaagiza viongozi wa halmashauri ya mji wa Tarime kuhakikisha mtu huyo anapatikana.

"Hatuwezi kumuangalia tu huyo mtu amepewa kiwanja zaidi ya miaka 20 bila kuliendeleza na hata kodi halipii halafu tunamuangalia tu ni lazima tuchukue hatua, " amesisitiza waziri huyo

Mwenyekiti wa mtaa wa Uwanja wa Ndege, Musa Mukunye amesema wameishi katika eneo hilo kwa muda mrefu na kwamba tayari wananchi wameanza ujenzi wa shule ya msingi kwaajili ya watoto wao lakini hivi karibuni mtu huyo alijitokeza na kuwazuia kufanya shughuli yoyote katika eneo hilo kwa madai kuwa eneo hilo  ni mali yake.

Alisema tayari wamejenga madarasa saba kwa ajili ya shule ya msingi kutokana na watoto wao kutembea umbali mrefu kwenda shule na kumuomba waziri huyo kuingilia kati ili waweze kuendelea na shughuli zao ikiwemo ujenzi wa shule hiyo.

Polepole Ampinga Makonda Kuwapongeza Polisi Dar

$
0
0
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Humphrey Polepole amesema  mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam,  Paul Makonda hakupaswa kufanya sherehe na Polisi kwa sababu kuna mahali hali haikuwa shwari na wao walikaa kimya.

Polepole ameyasema hayo leo Septemba 18,2018 alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ofisi ndogo ya CCM Lumumba jijini Dar es salaam akielezea sababu za ushindi wa majimbo mawili ya Monduli na Ukonga.

Amesema Chadema wanasema Jeshi la  Polisi linawasaidia CCM ilihali aliyekuwa mgombea ubunge wa chama chao kwenye Jimbo la Ukonga  Asia Msangi alimkwida msimamizi wa uchaguzi mbele ya Polisi na walikuwa wametulia.

"Makonda hakupaswa kufanya sherehe nao kwa sababu kuna mahali sheria ya tume ilikuwa inakiukwa na wao wapo wametulia" amesema Polepole.

Amesema pamoja na yote CCM inathamini uwepo wa vyama vya upinzani na wanataka wakosolewe na kupewa mawazo mbadala.

"Kwa bahati mbaya hawa wenzetu kazi yao ni kukosoa tu" amesema

Pia, Katibu huyo aliutaka upinzani utambulike kwa itikadi za vyama vyao badala ya kuonekana mtu zaidi ya chama.

"Kama chama kinachojinasibu kuwa ni mpinzanii mkuu na ninachelea kukiita mpinzani na ninashukuru wameshindwa vibaya, ukimtoa yule kiongozi wao na wapambe wake wa karibu Kinabaki nini, ACT Wazalendo ukimtoa mjomba kinabaki nini.”

"Wajenge kwanza itikadi ya vyama vyao itambulike, CCM ni taasisi inayotambulika kiitikadi" amejinasibu Polepole.

Lukuvi Atatua Mgogoro wa Bibi Aliyemwaga Machozi Mbele ya Rais Magufuli

$
0
0
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi, ametekeleza ahadi aliyoitoa kwa Rais Magufuli Jumatano ya Septemba 5, 2018, ya kwenda kusikiliza na kutatua kero ya ardhi ya bibi Nyasasi Masige mkazi wa wilaya ya Bunda aliyedai kuporwa eneo lake.

Lukuvi jana ameanza ziara mkoani Mara akiwa na lengo la kusikiliza kero zote zilizoelezwa na wananchi wakati wa ziara ya Rais Magufuli mkoani humo. Ziara yake imeanzia wilayani Bunda na kufika moja kwa moja hadi nyumbani kwa bibi Nyasasi Masige kusikiliza kero yake.

Waziri Lukuvi ameutatua mgogoro huo kwa kuzikutanisha pande zote mbili ambazo ni bibi Nyasasi Masige na mfanyabiashara mmoja ambaye jina lake halijatambulika mara moja anayedaiwa kujimilikisha eneo zaidi ya lile alilouziwa awali na bibi Nyasasi.

''Nimewasikiliza vizuri na kutokana na kwamba eneo hili halijapimwa, nimeagiza mamlaka kulipima na kisha kumpatia viwanja viwili bibi Nyasasi'', alisema Lukuvi.

Aidha Waziri ameitaka mamlaka ya ardhi wilayani Bunda kuhakikisha zoezi la kupima eneo hilo linafanyika ndani ya siku nne na bibi Nyasasi amilikishwe viwanja hivyo viwili bila kutozwa gharama yoyote ya malipo ya Hati ya viwanja.

Katika ziara ya Rais Magufuli, bibi Nyasasi alieza kuwa alikuwa anamiliki eneo kubwa ambalo alilazimika kuuza kipande kwaajili ya kupata pesa ya matibabu na baada ya kwenda mjini Musoma kwa matibabu mtu aliyemuuzia alijimilikisha na eneo lililobaki bila maelewano.

Lukuvi Amnyang'anya Hati ya Viwanja Mwekezaji

$
0
0
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Mendeleo ya Makazi, William Lukuvi  ameitaka kampuni ya Magarya engineering kurejesha haraka kwake hati ya umiliki wa viwanja vitano katika eneo la uwanja wa ndege wilayani Tarime ili eneo hilo liweze kukabidhiwa  kwa watu wengine kwaajili ya shughuli za maendeleo.

Agizo hilo amelitoa leo Septemba 18,2018 alipofika katika eneo hilo na wananchi kumuomba awasaidie ili waweze kumiliki viwanja hivyo na kufanya shughuli za maendeleo ikiwemo ujenzi wa shule ya msingi kwaajili ya wakazi wa eneo hilo.

Waziri Lukuvi alisema kutokana na mmiliki wa eneo hilo kushindwa kuliendeleza eneo lake japokuwa anamiliki hati kwa zaidi ya miaka 20 huku akishindwa kulipia kodi ya zaidi ya Sh40 milioni.

Amemtaka mmiliki wa kampuni hiyo aliyejulikana kwa Magarya Mwita Manko kuwasilisha hati hiyo kwake kabla hajaondoka wilayani Tarime leo na kuwaagiza viongozi wa halmashauri ya mji wa Tarime kuhakikisha mtu huyo anapatikana.

"Hatuwezi kumuangalia tu huyo mtu amepewa kiwanja zaidi ya miaka 20 bila kuliendeleza na hata kodi halipii halafu tunamuangalia tu ni lazima tuchukue hatua, " amesisitiza waziri huyo

Mwenyekiti wa mtaa wa Uwanja wa Ndege, Musa Mukunye amesema wameishi katika eneo hilo kwa muda mrefu na kwamba tayari wananchi wameanza ujenzi wa shule ya msingi kwaajili ya watoto wao lakini hivi karibuni mtu huyo alijitokeza na kuwazuia kufanya shughuli yoyote katika eneo hilo kwa madai kuwa eneo hilo  ni mali yake.

Alisema tayari wamejenga madarasa saba kwa ajili ya shule ya msingi kutokana na watoto wao kutembea umbali mrefu kwenda shule na kumuomba waziri huyo kuingilia kati ili waweze kuendelea na shughuli zao ikiwemo ujenzi wa shule hiyo.

Raia Wa Nigeria Kizimbani Kwa Kusafirisha Dawa za Kulevya

$
0
0
Raia wa nchini Nigeria, Martine Ike (46) mfanyabiashara na Mkazi wa Mbezi Salasala, amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na shtaka la kusafirisha gramu 647.7 za dawa za kulevya aina ya Heroin.

Wakili wa Serikali, Faraja Nguka akisoma hati ya mashtaka, leo Septemba 18,2018 mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Augustine Rwizile amedai kuwa mshtakiwa ametenda kosa hilo Julai 6,2018.

Imedaiwa, siku ya tukio, mshtakiwa huyo akiwa katika ofisi ya basi la kampuni ya Tahmeed iliyopo Mwembe Tayari Mombasa nchini Kenya, alikamatwa akisafirisha dawa hizo za kulevya zenye uzito wa gramu 647.7.

Hata hivyo, baada ya mshtakiwa huyo kusomewa shtaka lake, hakuruhusiwa kujibu chochote kwa sababu Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu haina mamlaka ya kuisikiliza kesi hiyo hadi Mahakama Kuu au kwa kupata kibali kutoka kwa DPP.

Kwa mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi bado haujakamilika na kesi imeahirishwa hadi Septemba 26 mwaka huu kwa ajili ya kutajwa na kuangalia kama upelelezi utakuwa umekamilika ama la.

Mwili wa Mtangazaji Dr Misanya Bingi Waagwa na Kusafirishwa Kuelekea Dodoma Kwa Mazishi

$
0
0
Mwili  wa aliyekuwa mtangazaji mahiri nchini na Mhadhiri wa Shule ya Habari na Mawasiliano ya Umma (SJMC) iliyo chini ya Chuo Kikuu Dar es Salaam (UDSM), Dkt Misanya Bingi (47) umeagwa leo katika Kanisa Katoliki la Makongo Juu liliopo Dar es Salaam na kusafirishwa kuelekea Miuji jijini Dodoma kwa ajili ya mazishi siku ya kesho.

Dkt Misanya Bingi alifariki dunia siku Jumapili katika Hospitali ya Taifa Muhimbili na wakati wa uhai wake alifanya kazi kwenye kituo cha Radio One ambapo alitangaza vipindi mbalimbali.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatano ya Septemba 19

Hamissa Mobetto Kaachia Video ya Madam Hero Ambayo Ndani yake Kaigiza Akifukuzwa na Ndugu wa Mwanaume

$
0
0
Mwanamitindo na muimbaji, Hamisa Mobetto ameachia video ya wimbo wake  ‘Madam Hero’ huku ndani ikiwa na matukio yasiokuwa yakawaida. 

Mrembo ambaye amezaa mtoto mmoja na Diamond, kupitia video ya wimbo huo ameigiza anafukuzwa na ndugu wa mume akiwa na mtoto mdogo, tukio ambalo limeanza kuwa gumzo mitandaoni kutokana na mrembo huyo kutokuwa na mahusiano mema na mzazi mwenzake, Diamond.

==>>Itazame video hapo chini

Video Mpya ya Masanja Mkandamizaji - Kemea Pepo

$
0
0
Masanja Mkandamizaji anakukaribisha kusikiliza wimbo wake mpya unaokwenda kwa jina la Kemea Pepo. Usikilize hapa.

Kwa Nini Matukio ya Watu Kujiua Yanazidi Kuongezeka? Nini Chanzo? Nini Suluhu Yake?...Bofya Hapa Kusoma kila Kitu

$
0
0
Msongo wa mawazo na kuvunjika moyo kunauhusiano na kukata tamaa ya kuishi. 

Mtu anapofikia hatua hii haoni tena thamani na furaha ya kuishi na hivyo huweza kuchukua maamuzi ya kutoa uhai wake mwenyewe ama wa mtu mwingine. 

Ndani ya kitabu hiki, msomaji atajifunza kuuona upendo wa Mungu katika hali zote, upendo unaoweza kumpa nguvu mpya na sababu ya kufurahia maisha katikati ya maumivu, kukata tamaa ama kuvunjika moyo.
 
Kitabu hiki kinapatikana/kinauzwa katika mtandao wa Amazon.com kwa gharama za TSh. 7000/- (2.99 USD ebook) na TSh. 11000/- (5.50 USD paperback). 

Kununua kitabu hiki “search code” hizi B07H6JR5X2 (ebook) au 1720166846 (paperback) ama unaweza ku-search jina la kitabu (YOU CAN DO BETTER THAN MURDER-SUICIDE: The Love of God is Sufficient)

Au  <<INGIA HAPA>> Kukinunua

China, Marekani wazidi kukabana koo

$
0
0
China imesema italipiza kisasi kwa kutoza ushuru wa dola bilioni sitini kwa bidhaa za kutoka Marekani, baada ya rais Donald Trump kutangaza kiwango cha ushuru wa ziada kwa bidhaa zinazoingia kutoka China.

China ilitangaza hivyo baada ya kutangazwa kuwa ushuru wa ziada kuwa dola bilioni 200.

Mvutano huu ni matokeo ya vita ya kibiashara kati ya nchi hizi mbili zenye uchumi mkubwa.

Wizara ya fedha ya China imesema inalipiza kile alichokiita ajenda ya Marekani ya kutazama upande mmoja na biashara yenye ushindani usio wa usawa.

Rais Trump ametahadharisha kuwa atalipa kisasi ikiwa wakulima, wafugaji na wafanyakazi wa kimarekani watalengwa kwenye maamuzi ya China. Amesema milango iwazi iwapo China itataka kuzungumza.

Trump amesema China imepatiwa fursa nyingi na sasa China inataka kufanya mazungumzo.

'' Tumekuwa na biashara isiyo na uwiano sawa na China, mwaka jana tulipoteza kiasi cha zaidi ya dola bilioni mia tano kwa China, hatuwezi kufanya hivyo''
 

Credit: BBC

Ahukumiwa Miaka 30 Jela Kwa Kumbaka Mtoto Bubu

$
0
0
Mahakama  ya Wilaya ya Mpanda mkoani Katavi, imemhukumu Ramadhani Shaban (24), Mkazi wa Mtaa wa Majengo B, kifungo cha miaka 30 jela, baada ya kumtia hatiani kwa kosa la kumbaka mtoto mwenye umri wa miaka 15, bubu ambaye pia ana upungufu wa akili.

Hukumu hiyo ilitolewa jana na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa mahakama hiyo, Gosper Luoga, baada ya mshtakiwa kukiri kosa.

Awali, Mwendesha Mashtaka wa Serikali wa Mkoa wa Katavi, Flaviana Shio, alidai mahakamani hapo kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo Septemba 9, mwaka huu majira ya saa 12 jioni katika Mtaa wa Majengo B.

Alidai kuwa siku ya tukio mshtakiwa alikwenda maeneo ya Mtaa wa Mjimwema alikokuwa akiishi mtoto huyo na mjomba wake, Ernest Chambala na kumpakia kwenye baiskeli yake.

Alisema alikwenda naye hadi kwenye chumba chake alichokuwa amepanga na kumbaka.

Aliendelea kuiambia mahakama kuwa baada ya tukio hilo mtoto huyo alitoka nje na kuanza kuwaonyesha watu kwa ishara kuwa amebakwa.

Mjomba wa mtoto huyo alianza jitihada za kumsaka mbakaji huyo kwa kumchukua mpwa wake huyo ambaye alimwongoza hadi kwenye nyumba alikofanyiwa unyama huo.

Alieleza kuwa majirani wa nyumba hiyo walipoulizwa kama walimuona mtoto huyo akiingizwa kwenye chumba cha mshtakiwa walikiri kumuona.

Baada ya kukamatwa alichukuliwa na kupelekwa kituo cha polisi na katika maelezo yake alikiri kutenda kosa hilo na taarifa za daktari zilithibitisha kuwa mtoto huyo alikuwa ameingiliwa na mwanaume kwa kuwa sehemu zake za siri zilikuwa na mbegu za kiume.

Mshtakiwa alikiri kutenda kosa hilo kwa kile alichodai amekuwa akifanya naye mapenzi mara kwa mara kwa sababu ni mpenzi wake.

Katika utetezi wake, mshtakiwa aliiomba mahakama impunguzie adhabu kwa kuwa mama yake mzazi anamtegemea na baba yake alishafariki.

Hakimu Luoga baada ya kusikiliza utetezi huo aliiambia mahakama kuwa mshtakiwa amepatikana na hatia imemhukumu kwenda kutumikia jela miaka 30.

Alisema katika hukumu hiyo mahakama pia imezingatia ongezeko la matukio ya ubakaji wilayani humo.


Mwanafunzi Darasa la Tatu Apewa Mimba.....Serikali Yaagiza Wazazi Wake Wakamatwe

$
0
0
Serikali wilayani Nkasi mkoani Rukwa, imeagiza kukamatwa kwa wazazi wa mwanafunzi wa darasa la tatu katika Shule ya Msingi Mkinga aliyepata ujauzito kwa kosa la kuandaa mpango wa kumuoza mwanafunzi huyo.

Agizo hilo lilitolewa jana na Mkuu wa Wilaya hiyo, Said Mtanda, wakati akikabidhi pikipiki 28 zenye thamani ya Sh. milioni 98 zilizotolewa na Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, kwa kushirikiana na Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi).

Fedha hizo zilitolewa kwa ajili ya mpango wa kukuza stadi za kusoma, kuandika na kuhesabu kwa waratibu kata wa wilaya hiyo.

Alisema katika kijiji cha Mkinga kuna mwanafunzi wa darasa la tatu amepata ujauzito na wazazi wake walikuwa wanaandaa mkakati wa kumuozesha, lakini walishindwa baada ya Mwalimu Mkuu wa shule hiyo kuingilia kati na kuvuruga mpango huo.

"Naagiza wazazi wote wa mwanafunzi huyo wakamatwe mara moja, mwanafunzi huyo pamoja na aliyempa mimba wafikishwe katika vyombo vya dola, ili sheria ichukue mkondo wake na ninyi waratibu elimu kata tambueni mna jukumu kubwa la kuhakikisha mimba hizi zinakwisha, " alisema.

Mtanda alisema hali hiyo inaonyesha kuwa bado tatizo la mimba ni kubwa kwa sababu katika mwezi uliopita jumla ya wanafunzi 27 walipata ujauzito, hivyo bado kuna kazi kubwa ya kufanya.

Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Misana Kwangula, alisema lengo la serikali kuwapatia pikipiki hizo ni kuwawezesha kutembelea shule zilizopo katika kata zao kwa kuwa walikuwa wanalalamika kuwa hawana vitendea kazi vya kuwawezesha kufanya ukaguzi katika shule wanazozisimamia.

Irene Uwoya: Nimeamua Kutafuta Mwanaume wa Rika Langu maana Mlisema Dogo Janja Ni Mtoto

$
0
0
Muigizaji wa Bongo movie Irene Uwoya ametoa kauli ambayo imethibitisha kuachana  kwake na mume wake staa wa Bongo fleva Dogo Janja.

Kwa mwezi sasa kumekuwa na tetesi kuwa Irene Uwoya ameachana na Dogo Janja huku tetesi hizo zikichangiwa na Safari aliyoifanya Uwoya wiki chache zilizopita nchini Dubai ambako ilisemekana alikuwa na mwanaume mwingine.

Ingawa wawili hao walishawahi kukataa tetesi za kuachana Lakini sasa inaonekana kama wameamua kuweka mambo hadharani kwani Uwoya ameandika maneno ambayo yanaashiria kamuacha Dogo Janja.

Kupitia page yake ya instagram, Uwoya ameweka comment kwa shabiki mmoja aliyemhoji Kuhusu Dogo Janja ambapo ameandika kuwa ameamua kumuacha Dogo Janja na kutafuta mwanaume anayeendana naye kiumri.

Irene Uwoya aliandika maneno  haya: "Simlisema wenyewe nitafute wa umri wangu yeye bado mdogo? Sasa nimefata ushauri jamani…..au keshakuwa”.

Mwanafunzi auawa kwa kisu kwenye kigodoro akigombea mwanamke

$
0
0
Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro linamshikiliwa mwanafunzi anayetuhumiwa kumuua mwenzake mwenye umri wa miaka kumi na tisa wote wakiwa wanasoma Shule ya Sekondari Mteule akituhumiwa kumchoma kisu sehemu kifuani wakiwa kwenye kigodoro.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro Wilbroad Mutafungwa amemtaja aliyeuawa ni Abdulrahiman Daud aliyeshambuliwa kwa kile kinachodaiwa ugomvi wa kugombea mwanamke.

==>>Msikilize Kamanda Mutafungwa akongea hapo chini 


Credit: Azam Tv

Ashitakiwa Kwa Kujiita Mtoto wa CAG na Kisha Kubaka

$
0
0
Mkazi wa Mwananyamala, Ahmed Mudhihiri (26), amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Wilaya Kinondoni,   Dar es salaam akikabiliwa na mashtaka matatu yakiwamo ya ubakaji na kufanya udanganyifu kuwa yeye ni mtoto wa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).

Akisomewa mashtaka yake mbele ya Hakimu Caroline Kiliwa, Mwendesha Mashtaka, Neema Moshi, alidai Julai 6  katika eneo la Hoteli ya White Sands  Mbezi Africana   Dar es Salaam, mshitakiwa alimbaka binti (jina limehifadhiwa).

Shitaka la pili ni kuwa  kati ya Juni 17 na Julai 7 mwaka huu   Dar es Salaam, alidanganya kuwa yeye ni Mwamvita Makamba.

Katika shitaka la tatu, mshitakiwa alidaiwa kati ya Juni 18 na Julai 7 mwaka huu, Dar es Salaam, alijitambulisha kuwa yeye ni Edd mtoto wa   CAG.

Benki Kuu ya Tanzania (BOT) Yasema ni kosa la jinai kudhihaki au kukejeli noti na sarafu za Tanzania.

$
0
0
Benki Kuu ya Tanzania imewataka wananchi kuheshimu fedha ya Tanzania kwani ni moja ya alama ya taifa.

Kauli hiyo imekuja kufuatia matukio ya hivi karibuni ya baadhi ya wananchi kutoziheshimu, kuzifanyia dhihaka na kebehi noti za Jamhuri ya Mungano wa Tanzania.
 
Taarifa ya BoT kwa vyombo vya habarI ambayo inasema utunzaji mzuri wa fedha zetu utapunguza uwezekano wa fedha hizo kuchakaa mapema na kupunguza gharama za uchapishaji.

"Kwa mujibu wa Sheria ya Benki Kuu ya Tanzania ya mwaka 2006, kifungu cha 26, BoT ndiyo taasisi pekee yenye mamlaka ya kutoa noti na sarafu katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania," imesema taarifa hiyo.

Pia imesema noti na sarafu hizo zina alama muhimu inayolitambulisha taifa la Tanzania ambayo ni nembo ya Bwana na Bibi. Imefafanua alama hiyo inapaswa kuheshimwa kama zilivyo alama nyingine kwa mfano Bendera ya Taifa.

Pia noti na sarafu zote zimetengenezwa kutoa thamani ya kisheria (legal tender) kama ilivyoandikwa juu ya noti au sarafu husika na pia Benki Kuu pekee ndiyo yenye mamlaka ya kuharibu noti na sarafu.

Taarifa hiyo imefafanua kuhusu hilo kupitia kifungu cha  28 kikisomwa pamoja na kifungu cha 30 cha Sheria ya Benki Kuu ya Tanzania ya mwaka 2006.

"Benki Kuu inatoa rai kwa wananchi kuzitunza fedha zetu kwa kuwa ni mojawapo ya tunu na alama muhimu ya uchumi wa nchi yetu.

"Vilevile, utunzaji mzuri wa fedha zetu utapunguza uwezekano wa fedha hizo kuchakaa mapema na kupunguza gharama za uchapishaji," imesema taarifa hiyo ya BoT.

==>>Hapo chini ni taarifa ya BoT
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images