Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Serikali Yasema Ushrikiano Wa umoja wa mashirika ya kuzalisha umeme (SAPP) Unaharakisha Miundombinu Ya Umeme

$
0
0
Na Ahmed Mahmoud Arusha
SERIKALI imesema kuwa ushirikiano  wa nchi za umoja wa mashirika ya kuzalisha umeme kusini mwa jangwa la Sahara SAPP, unatoa msukumo  wa nchi wanachama  kuharakisha kujengwa na kukamilika kwa miundo mbinu ya mfumo wa umeme wenye gharama nafuu .

Hayo yameelezwa jana na Waziri wa Nishati Dakta Medad  Kalemani,alipokuwa akifungua mkutano wa 51 wa mashirika ya umeme ya nchi za kusini mwa afrika SAPP, na kusema kuwa lengo la mkutano huo ni kuimarisha ushirikiano uliopo ili kuwezesha nchi zote kunufaika na miundo mbinu imara ya kusafirisha umeme.

Waziri Dakta Kalemani alisema Tanzania, Malawi na Angola, ambazo hazijakamilisha  miundo mbinu  hiyo zinapata uzoefu ambao unawezesha kuharakisha ukamilishaji wa  miundo mbinu ya umeme na hivyo kunufaika na ushirikiano huo.

 Alisema ushirikiano huo unawezesha kuwepo na mpango madhubuti wa kuzalisha na kuuza na kununua umeme wa gharama nafuu kwa nchi wanachama.

Waziri Kalemani,amlisema miradi ya umeme itawezesha kuinua na kuboresha uchumi wa nchi husika kutokana na kutekeleza miradi hiyo mikubwa ya uzalishaji umeme.

Amlisema mradi huo wa miundo mbinu ya umeme unaunganisha nchi wanachama ambazo ni kumi na moja na unakwenda  hadi kufikia Cairo nchini Misiri..

Waziri,amesema hivi sasa Tanzania tunazalisha umeme mwingi, katika maporomoko ya Mto Rufiji ,Somanga, pamoja na kuzinduliwa mradi wa gesi asili wa Kinyerezi na hivyo tunaweza kuuza umeme nje ya nchi na pia tunaweza kununua ueme toka nje kwa gharama nafuu zaidi .

Alisema kuwa mbali na kujiunga kwenye ushirikiano huo wa SAPP pia Tanzania imejiunga na mashirika ya umeme ya nchi wanachama wa Jumuia ya afrika mashariki lengo ni kuwezesha wananchi kupata umeme wa gharama nafuu na wa uhakika.

Alisema Tanzania sasa ina ziada ya umeme mega wati 200  baada ya kuzinduliwa kwa mradi wa gas wa Kinyerezi ,ambapo uzalishaji ni mega wati 161 1 na mahitaji ni mega wati 1537 .

Kwa upande wake mkurugenzi mtendahji wa shirika la umeme nchini ,mhandisi, Michael Tito ,alisema Tanesco imejipanga kuhakikisha umoja huo unafanya kazi kikamilifu pamoja na kuboresha miundo mbinu ya umeme ambayo itaungwanishwa kwenye gradi ya taifa.

Alisema kuwa maeneo yote ya mipakani yatapata umeme kutoka kwenye nchi wanachama kwa gharama nafuu  na hivyo kuwawezesha kuboresha maisha yao.

Mwisho................

Dawa Asilia Ya Kurefusha Na Kunenepesha Uume Ulio Sinyaa Kwa Punyeto.

$
0
0
Umefanya  punyeto kwa  muda  mrefu  na  kuishiwa nguvu  za  kiume ? Maumbile  yako  ya  kiume  yamesinyaa  na  kunywea  kiasi  cha kuyafanya  yaonekane  kama  ya  mtoto ? Umejaribu  kutumia  dawa mbalimbali  bila  mafanikio ?  Unahitaji  kupata  tiba  itakayo kurejeshea  nguvu  zako za  kiume  na  kuyarejesha  maumbile  yako katika  hali  yake  ya  awali ?
 
Kama  jibu  lako  ni  NDIO  basi hii  ni  HABARI  NJEMA  SANA  kwako. Tunayo  dawa  ya  asili  ambayo  inasaidia  kurejesha  nguvu  za kiume  kwa  mwanaume  aliye  athirika  na  punyeto . Mbali  na kurejesha  nguvu  za  kiume, dawa  hii  pia  inarefusha  na kunenepesha  maumbile  ya  kiume  yaliyo  sinyaa  kwa  punyeto  na kuyarejesha  katika  hali  yake  ya  kawaida  ndani  ya  siku thelathini.

Kupata  dawa  hii  fika  katika  duka  la  kuuza  dawa za  asili  la NEEMA  HERBALIST.  Tunapatikana  UBUNGO  jijini  DAR  ES  SALAAM jirani  na  SHULE  YA  MSINGI  UBUNGO  NATIONAL  HOUSING  nyuma  ya jengo   la  UBUNGO  PLAZA.
 
Kwa  wateja wetu  wa  jijini  DAR  ES  SALAAM  ambao  hawana  nafasi ya  kufika  dukani  kwetu  tunayo  huduma ya  kuwapelekea  dawa mahali  popote  walipo  jijini  Dar  Es  Salaam  na  kwa  wateja waliopo  nje  ya  Dar  Es  Salaam  tunawatumia  dawa   kwa  ma bus mbalimbali  na  kwa  wale  wa  Zanzibar  tunawatumia  dawa  kwa usafiri  wa  boti.

WASILIANA  NASI  KWA  SIMU  NAMBA  : 0693  005 189  AU  0766  538384.
 
Na  kwa  taarifa  zaidi  kuhusu  tiba  mbalimbali  za  asili,
tutembelee  kupitia  blogu  yetu :

Baada Ya Kutisha Kwenye Uzinduzi Sasa Filamu Ya Bahasha Kuanza Kuonekana Sinema Leo

$
0
0
Ukisikia neno Rushwa unapata picha gani kwenye fikra zako? Unadhani Rushwa inahusisha pesa kubwa kubwa tu!! Leo hii katika Kumbi za Sinema za Mlimani City unaletea Filamu ya “Bahasha”iliyozinduliwa wiki iliyopita katika Ukumbi wa Sinema wa Mlimani City.

Filamu hii ya BAHASHA imeandaliwa na Ubalozi wa Uswisi na Uholanzi kwa kushirikiana na Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (TAKUKURU) inayozungumzia madhara yanayojitokeza katika sehemu mbalimbali inayosababishwa na rushwa. 

Kupitia filamu hii tunamuona mwenyekiti wa mtaa wa Mtakuja, Kitasa akichukua fedha kwa ajili ya kuwashawishi kamati yake watie saini na kuuza eneo la wazi kujengwa eneo ambalo watoto wamekuwa wanalitumia kwa ajili ya michezo, likiwa karibu na shule ambapo katika jengo hilo walilojenga liliweza kuleta madhara ya uharibufu ya miundo mbinu ya maji, kubakwa kwa mtoto wake wa kike Hidaya na changamoto zingine. Tizama kipande kuifupi hapa chini na usikose kuifuatilia filamu hii.

Ratiba ya filamu hii kuonesha ni kama inavyoonekana kuanzia leo Septemba 7 kuanzia saa 6 mchana, saa 10 jioni na saa 2 usiku katika Kumbi za Century Cinemax Mlimani City.

CHADEMA Wapinga Ongezeko la Vituo vya Kupigia Kura Ukonga

$
0
0
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Jimbo la Ukonga, kimesema uchaguzi katika jimbo hilo unanyemelewa na jinamizi kutokana na sintofahamu ya idadi ya vituo vya kupigia kura.

Mkurugenzi wa Operesheni wa Uchaguzi Jimbo la Ukonga, Singo Kigaila, akizungumza na waandishi wa habari katika ngome ya jimbo hilo, alisema mwaka 2015 kulikuwa na vituo 659 na watu waliojiandikisha walikuwa 293,000.

“Tangu mwaka 2015 hakuna uandikishaji wa wapigakura uliofanyika, haitegemewi idadi iongezeke, inawezekana kupungua kwa sababu wanaweza kuwepo waliofariki dunia.

“Vituo vinatakiwa kubakia 659 na si 675 vilivyotangazwa kuwepo katika Jimbo la Ukonga, kwa idadi hiyo kuna vituo 16 vilivyoongezeka,” alisema Kigaila.

Alisema wana wasiwasi mkubwa na vituo hivyo  vilivyoongezeka sababu wanajua matatizo yaliyowahi kutokea katika chaguzi mbalimbali zilizofanyika.

Kigaila alisema chama hicho kimekatia rufaa majibu waliyopewa na Tume ya Maadili kuhusu malalamiko waliyowasilisha, kwamba mgombea ubunge wa jimbo hilo kupitia CCM, Mwita Waitara aliandika maneno katika mtandao akihamasisha waliyodai kuwa ni mauaji.

Alisema Tume iliwajibu kwamba wafuatilie Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kujua kama namba hiyo iliyotumika ilikuwa ya Mwita na aliyetafsiri lugha iliyotumika kwenye mtandao awe mkalimani anayetambulika.

“Sisi kama chama hatuwezi kuiamuru TCRA kuchunguza na kutoa majibu ya namba iliyotumika kama ya Waitara ndani ya saa 48, hata tukipeleka sasa hivi, uchaguzi utamalizika na majibu hayatapatikana,” alisema.

Alisema kutafsiri lugha iliyotumika hakuhitaji mkalimani na wala kujua kama namba ya simu iliyotumika kama ni ya Waitara pia hakuhitaji uchunguzi huo kwani yeyote anaweza kujua.

Uhamiaji: Wachungaji Acheni Kualika Wahubiri Kutoka Nje Ya Nchi

$
0
0
Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Afisa uhamiaji katika jijini la Dodoma Edwin Mwasota amewataka wachungaji na viongozi mbalimbali wa madhehebu ya Kikristo mkoani Dodoma kuacha tabia ya kualika wachungaji kutoka nje ya Tanzania na kufanya mahubiri katika jiji hilo bila kibali Maalum.
 
Bwana Edwin ameyasema hayo  Septemba 5 katika moja ya Ziara ya mkuu wa wilaya ya Dodoma mjini Patrobass Katambi kwenye mikutano ya hadhara iliyofanyika katika kata za Ipagala na Mnadani jijini Dodoma.
 
Afisa Uhamiaji huyo amesema kuwa wahubiri wazawa wana uwezo wa kuhubiri hivyo kufanya mialiko ya kualika wahubiri kutoka nje ni kujidhihisha kuwa wao hawawezi na kubainisha kuwa katika jiji la Dodoma pamekuwepo na wimbi la mabango ya matangazo ya wahubiri kutoka nje ya Tanzania ikiwemo Kenya bila Uhamiaji kujulishwa juu ya ugeni huo.

"Hivi nyie wachungaji hamjiamini  kuhubiri?sasa kumeibuka wimbi la wahubiri kutoka nje ya nchi.Ukifuatilia mtu huyo kaingiaje hapa jijini Dodoma hauwezi kuelewa mwanzo wala mwisho.Ukienda kila mtaa  hususan kwenye nguzo za TANESCO utakuta kuna mabango ya matangazo  ya Ujio wa
wahubiri kutoka nje ya nchi mfano Kenya,Uganda.Sasa unajiuliza huko anakotoka hakuna watu wa kuhubiriwa mpaka aje Tanzania."Alisema 
 
Pia Bwana Edwin aliongeza kuwa"Nimeamua kusema haya kwa sababu Nimewahi kushuhudia mchungaji wa Kanisa Fulani kutoka nje ya nchi alikuja hapa kwa lengo la kuhubiri ,baada ya mkutano wa mahubiri kumalizika kama ilivyopangwa aling'ang'ania kukaa hapa nchini.Ndipo ujue kuwa Tanzania ni kuzuri watu wanatamani Kukaa"
 
Aidha Afisa huyo wa uhamiaji amewataka wananchi wa jiji la Dodoma kushirikiana na idara ya uhamiaji kuwabaini watu wanaofanya  kazi za majumbani kutoka nje ya nchi bila kibali maalum  ili hatua za kisheria ziweze kuchukuliwa.
 
Alisema"Kuna baadhi ya watanzania wamekuwa wakiwatumikisha  kazi za ndani wasichana wadogo kutoka nje ya nchi kwa kigezo cha gharama nafuu.Naomba tushirikiane ili tuweze kuwabaini "
 
Kwa upande Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya Dodoma mjini ambaye ni mkuu wa wilaya hiyo  Mhe:Patrobass Katambi amesema kuwa suala la ulinzi na usalama ni la kila mtu hivyo jamii inapaswa kulinda mali ya mwenzake.
 
"Suala la ulinzi na Usalama ni la kila mtu ,wana Dodoma tushirikiane kulinda mali ya mwenzake"Alisema .
=========================================
MWISHO.

Makanga 3 Power; Dawa Bora Nguvu Za Kiume

$
0
0
Kutibu nguvu za kiume dakika(10) na kupona muda wa siku tatu tuu. Kuimarisha misuli ya uume uliolegea, pia ipo Dawa ya kurefusha uume mfupi inchi NNE hadi saba na kunenepesha uume mfupi sentimita NNE.

Tiba ya kudumu kutibu maumivu ya mgongo,kiuno, tumbo kuunguruma na kujaa gesi, kupata choo vizuri, na kutibu uzazi, kutibu busha bila operesheni, kisukari, presha ,miguu kuuma, uzazi, fangas sugu, vidonda vya tumbo.

Ni docta bingwa wa kutibu magonjwa sugu, kutoa ndagu za utajiri kwa kutumia Pete, kazi ,cheni, mikufu maalumu ya bahati, una kesi umedhulumiwa Mali au pesa? Zitarudi muda wa Masaa matatu tuu.

Onana na Dr shilindes shida zako zote zitakwisha, anatoa Dawa za utajiri kwa wafanyakazi, wakulima, na wafugaji, wafanyabiashara na wachimba madini kwa kutumia pete, kazi kwa yeyote anaetaka kuwa na pesa nyingi.

Pia anaboresha akili kwa wanafunzi darasani, masomo na kufaulu mitihani pia kushinda bahati nasibu yeyote.

Pia tunatoa Dawa kumrudisha Mume, mke, mpenzi, hawara, kwa muda wa SAA moja tuu, na kuomba msamaha kwa kukupigia magoti na yeyote yule, unaemtaka kimapenzi au kuoana, utampata na kumfunga asitoke nje ya ndoa daima na kutekeleza shida zako zote. Kupunguza unene, kupunguza matiti makubwa, tumbo na nyama uzembe muda wa siku sita unapata saizi uipendayo.

Kutoa makovu mwilini, chunusi, upele na mabaka, pia tunayo Dawa ya kuongeza hipsi, makalio, mguu wa bia na kupata shepu safi kwa muda wa siku saba tuu.

Wa mikoani mtapata huduma popote mlipo.
Tupo dar es salam mbagala rangi tatu.

Mawasiliano simu namba: 0784 460 348. Au 0659 103 360.

LIVE | Wizara ya Maji yawekeana saini ya makubaliano na Benki ya Dunia

$
0
0
Wizara ya Maji yawekeana saini ya makubaliano na Benki ya Dunia

TCRA yataka wateja wa DSTV, AZAM na ZUKU waliolipishwa kuwasilisha taarifa zao

$
0
0
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania TCRA imewataka wateja visimbuzi vya DSTV, ZUKU na AZAM kutuma taarifa zao zinazoonesha na kuthibitisha kuwa wamekuwa wakilipia chaneli za ndani jambo ambalo ni kinyume na sheria.

TCRA imewataka wateja wa ving’amuzi hivyo kutoa taarifa juu ya majina yao kamili yaliyosajiliwa katika king’amuzi, aina ya king’amuzi anachotumia, namba ya kadi ya king’amuzi chake, eneo alipo, kiasi cha pesa ambacho amekuwa akilipia kutazama chaneli hizo na idadi ya miezi aliyolipia.

Taarifa hiyo ni maalumu kwa mtazamaji aliyekuwa anatozwa kutazama chaneli za televisheni ya TBC 1, ITV, STAR TV, CHANNEL TEN, EAST AFRIKA TV, na CLOUDS TV.

TCRA imewataka wahanga hao kutoa taarifa hizo ofisini kwao kupitia barua pepe au barua ya kawaida kwenye anuani yao ya dg@tcra.go.tz au kupitia kwa Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Mawasiliano kwa sanduku la Posta 474.

Mnamo Agosti 7, 2018 Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania iliziamuru Kampuni za DSTV, AZAM TV na ZUKU kuondoa cheneli za kutazamwa bila kulipia baada ya kukiuka sheria na masharti ya leseni zao kwa kuwatoza watazamaji ada za viwango mbalimbali kutazama chaneli hizo ambazo kisheria zinapaswa kutazwa bure.

Huna Sababu Ya Kuaibikatena............ Jipatie Dawa Bora Ya Nguvu Za Kiume, Maumbile Madogo Na Mvuto Wa Mapenz

$
0
0
Usikate tamaa ondoa maradhi yako, maana matatizo haya yamekua yakiasili watuwengi kisaikolojia hasa baada ya kujiona wako tofauti sana na wengine kawaida mwanaume anatakiwa awe na uume kuanzia (6-8) vinginevyo mtuhuyo anamapunguvu katika mwiliwake.

Kunasababu nyingi sana zinazosababisha matatizo haya, chango hushambulia never ambayo huasili misuli ya uume, Ngili :- hii huleta maumivu ya tumbo chini ya kitovu na kufanya tumbo kuunguluma na kujaa gesi, kolodani moja kuvimba au kuingia ndani pamoja na kutopata choo vizuli. Sababuhizi na nyingine hufanya uume kulegea na kusinyaa na kuwa mfupi na mwembamba na marakwamara husababisha kukosa hamu ya kuludia tendo la ndoa na baadae kushindwa kabisa

MASISA 3POWER :- nidawa ya mitishamba iliyotengenezwa kwa mfumo wa vidonge, huongeza nguvu za kiume maradufu kuanzia umri wa miaka 15-90 , inakomaza mbegu zisizo na viini vya uzazi (manii) inaimalisha mishipa iliyolegea wakati wa tendo la ndoa, itakufanya uludie tendo la ndoa zaidi ya mara nne (4) birahamu kuisha wara kuhisi kuchoka na itakufanya uchelewe kufika kileleni zaidi ya dk (20-30 )

YONINANI:- hurefusha na kunenepesha maumbile madogo ya uume uliosinyaa inchi 6-8 na unene wa sm 3-4 kwa mda mfupi sana,

SUPER MORINA :- nidawa inayotibu ama kutatua tatizo la kisukali kwawaliohangaika bila mafanikio, huondoa tatizo la kisukali na kupona kabisa, vilevile ninadawa ya magonjwa sugu km vile presha, vidondo vya tumbo, miguu kuwakamoto, muwasho mwilin, kaswende,uzazi nk.

LUGIMBA :- nidawa ya mvuto wa mapenzi, humtuliza mke, mme, mchumba, hawara au mtu yoyote umpendae na kumfanya akutimizie chochotekile unachokitaka kutoka kwake na kumfunga asiwe na mtu yoyote zaidi yako.

WASILIANA NA DR CHIPUPA NAPATIKANA DAR ES SALAAM KUMBUKA HUDUMAHII ITAKUFIKIA POPOTE ULIPO  0759208637 / 0622344969

Wabunge Wamzomea Waziri Mwijage

$
0
0
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage leo Ijumaa Septemba 7, 2018 amejikuta katika wakati mgumu bungeni mjini hapa baada ya  kuzomewa na wabunge kutoka Zanzibar.

Alikumbwa na mkasa huo wakati akijibu swali la nyongeza la mbunge wa Baraza la Wawakilishi (BLW), Jaku Hashim Ayoub aliyetaka kujua sababu za Serikali kuendelea kuzuia sukari ya kiwanda cha Mahonda kuuzwa Tanzania Bara.

Katika swali lake, Jaku amesema haiingii akilini kuona bidhaa kutoka Zanzibar kuwa ngumu kuingia katika soko la Tanzania Bara, wakati zile za Tanzania Bara zinaingia  kirahisi Zanzibar.

Katika majibu yake, Mwijage amesema katika kipindi cha uongozi wake hawezi kuruhusu sukari kutoka kiwanda cha Mahonda kuletwa Tanzania Bara kwa maelezo kuwa bado kuna vitu vya kuhoji ndani ya kiwanda hicho.

Kauli hiyo ilizua mvutano mkali bungeni na wabunge wa Zanzibar walianza kupiga kelele kwa sauti za juu wakipinga majibu hayo.

“Mheshimiwa mwenyekiti naomba nikuelekeze wewe majibu yangu na wabunge wanaotaka kunisikiliza, lakini wale wasiotaka waache waendelee kupiga kelele tu,” amesema Mwijage.

“Mimi ninasimamia kuwa kiwanda cha Mahonda kinazalisha tani 4,000 wakati mahitaji ya wananchi wa Zanzibar ni tani 20,000, je hiyo wanayotaka kuuza huku wanaitoa wapi? Siko tayari kukubali hata wakizomea.”

Kuhusu sukari iliyorundikana kwenye viwanda, Mwijage amesema vyombo vya dola viko kazini na tayari wamegundua ndani ya uchunguzi huo kuna jinai hivyo kuna watu ambao watashughulikiwa.

Pigo: Wenyeviti 20 wa CHADEMA katika jimbo la Hai Wamkimbia Mbowe na Kutimkia CCM

$
0
0
Wenyeviti 20 wa vijiji wa Chadema katika jimbo la Hai mkoani Kilimanjaro wamehamia CCM leo Alhamisi Septemba 6, 2018.

Mbunge wa Hai ni Freeman Mbowe ambaye ni mwenyekiti wa Chadema na Kiongozi wa Kambi Rasmi za Upinzani Bungeni.

Majina ya wenyeviti hao na vijiji vyao katika mabano ni, Hendry Kimaro (Lukani), Josephat Joseph (Mbosho), Comred Munuo (Kyuu), Elibariki Mbise (Rundugai), Nassor Mushi (Wari Sinde), Erasto Mushi (Kyeeri), Iddy Mtambo (Chemka), Seth Munisi (Uraa), Issa Kisanga (Kware) na Paradiso Munisi (Uswaa).

Wengine ni  Emanuel Mbowe (Nshara), Simbo Mbasha (Mungushi), Bethuel Swai (Isawerwa), Godfrey Kivuyo (Jiweni), Joel Kalungwana (Nerere), Emanuel Laizer (Mlima Shabaha), Michael Kiwelu (Kambi ya Raha), Godfrey Maimu (Umoja), Witness Mwanga (Sonu).

Mkurugenzi wa halmshauri ya Hai, Yohana Sintoe amethibitisha kupokea barua za kujiuzulu za wenyeviti hao.

Amesema kulikuwa na wenyeviti 19 lakini baadae akaongezeka mmoja na kufikia 20. Hata hivyo mwenyekiti huyo wa  20 jina lake halijapatikana.

Mkuu wa wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya amesema anawapongeza viongozi hao kwa kutumia haki yao kidemokrasia na kujiuzulu.

Sabaya amesema kwa sasa hakuna Mtanzania ambaye haoni kazi nzuri za Rais John Magufuli hivyo viongozi hao kujiuzulu wameonesha heshima kwa Rais.

Serikali Kuongeza Fedha Katika Mradi Wa Tasaf Ili Ziwafikie Walengwa Wote

$
0
0
SERIKALI imesema ina mpango wa kuongeza fedha katika Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini (TASAF) ili kuongeza idadi ya wananchi watakazonufaika na mradi huo.

Hayo yamesemwa leo tarehe 7 Septemba, 2018 jijini Dodoma katika kipindi cha maswali na majibu, na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Nkuchika.

Waziri Nkuchika ameeleza kuwa, malengo ya TASAF ni kufikia walengwa wote na kwamba hadi sasa asilimia 70 ya walengwa wamefikiwa na mradi huo, hivyo serikali imedhamiria kuongeza fedha.

“Malengo ya TASAF ni kufikia walengwa wote wanaokubali kusaidiwa, mpaka sasa tumefikia walengwa asilimia 70. TASAF kwenye awamu ya tatu B, malengo ya serikali ni kufikia walengwa wote na ili tuwafikie walengwa wote lazima serikali iongeze fedha,” amesema.

Aidha, Waziri Nkuchika ameahidi kufanyia kazi changamoto zinazoikabili mradi huo ikiwemo malalamiko ya upendeleo katika utolewaji wa fedha hizo.

“…Nakubali rai yake yale maeneo yenye malalamiko nitayafanyia kazi, naomba mbunge yoyote mwenye ushahidi kwamba mahali fulani hizi fedha zina upendeleo nitalifanyia kazi. Kwa kuwa TASAF inafanya kazi nzuri hapa nchini, na kufanya kazi maeneo mengi, upande wa afya elimu, sasa hivi inasimamia elimu bure kwa watoto wa masikini, lakini mwenyekiti nasema hivi TASAF haibagui chama, TASAF iko tayari kuwaongezea fedha ili ihudumie watu wengi.” Amesema Waziri Nkuchika.

Mradi wa TASAF ulianza rasmi mwaka 2013 na unatarajiwa kumalizika mwaka 2023 ambapo unatekelezwa katika kipindi cha miaka kumi mfululizo ambapo vimegawanyika kwa awamu mbili. Fedha za utekelezaji wa mradi huo ni za mkopo kutoka Benki ya Dunia (WB)

Mbunge CHADEMA Aitaka Serikali Itatua Matatizo ya Maji Badala ya Kutumia Hela Nyingi Kununua Ndege

$
0
0
Mbunge wa Momba, David Silinde (Chadema), amesema badala ya serika kutumia fedha nyingi kununua ndege kwa nini fedha hizo zisielekezwe katika miradi ya maji sehemu mbalimbali nchini.
 
Silinde amesema hayo bungeni jijini Dodoma leo wakati akiuliza swali la nyongeza ambapo amesema maji yanayotumiwa katika vyoo maeneo ya mijini yanaonekana ni safi kuliko maji yanayotumiwa kwa matumizi ya nyumbani katika maeneo ya vijijini.
 
Katika swali lake msingi, Silinde alihoji “tatizo la maji Momba halijapatiwa ufumbuzi wa kudumu hadi sasa, je serikali itamaliza tatizo hilo Wilaya ya Momba,”
 
Akijibu swali hilo, Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso amesema kwa kiasi kikubwa tatizo la maji limetatuliwa sehemu nyingi nchini na pia ndege ina umuhimu wake.
 
“Mheshimiwa Mwenyekiti naomba nimwambie mbunge kuwa serikali inatambua tatizo la maji  katika Wilaya ya Momba ambapo katika utekelezaji wa Awamu ya Kwanza ya Programu ya Maendeleo ya Sekta ya Maji (WSDP), seikali pia imekamilisha ujenzi wa vijiji vya Namtambala, Iyendwe, Itumbula, Mnyuzi, Chilulumo na Kamsamba katika jimbo la Momba.
 
“Pia serikali imetenga Sh bilioni moja katika jimbo hilo lakini pia kwa kuwa kazi ya Mbunge ni kusimamia, nitaomba asimamie fedha hizo zitumike vizuri katika mradi kusudiwa,” amesema Awe

LIVE: Fuatilia Matangazo Ya Moja Kwa Moja Rais Magufuli anazungumza na Wananchi Tarime – Tarehe 7 septemba 2018

$
0
0
Rais Magufuli anazungumza na wananchi kwenye mkutano wa hadhara katika viwanja vya chuo Ualimu

==>>Msikilize hapo chini

Tundu Lissu Leo Katimiza Mwaka Mmoja Tangu Ashambuliwe Kwa Risasi

$
0
0
Mnamo tarehe 7 Septemba 2017, aliyekuwa Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) na Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki, Mhe. Tundu Lissu akiwa maeneo ya Area D mjini Dodoma alishambuliwa kwa risasi na watu wasiojulikana.

Tundu Lissu baada ya tukio hilo alipelekwa katika Hospitali ya General na baadae kusafirishwa jijini Nairobi kwa kupatiwa matibabu zaidi.

Hata hivyo, Tundu Lissu baadae alitolewa tena nchini Kenya na kwenda kutibiwa nchini Ubelgiji huku sababu za  kiusalama zikitajwa kusafirishwa kwake

Kwa mujibu wa waraka wake alioundika ikiwa leo ametimiza mwaka mmoja tangu ajeruhiwe kwa risasi na watu wasiojulikana, Lissu amesema mwaka mmoja umekuwa mrefu na mgumu sana kwangu kwake kwa sababu ya majeraha ya mwili na pia amei-miss Tanzania na Watanzania.

“Nime-miss sana Bunge, licha ya matatizo yote ya Bunge la Spika Ndugai. Nimewa-miss sana watu wangu wa Jimbo la Singida Mashariki na mikutano yetu ya hadhara, kazi zangu za chama, viongozi wenzangu, wanachama wetu na wafuasi wetu katika mamilioni yao.

“Nime-miss sana mapambano ya utetezi wa haki za watu wetu ndani na nje ya Mahakama, Mawakili wa Tanzania Bara (TLS) walionipa heshima ya kuwaongoza katika kipindi kigumu sana katika historia ya TLS,” amesema Lissu.

Amesema katika huo mwaka mmoja wa kukaa nje ya nchi, wa kutokuonana moja kwa moja na watu wake, familia, ndugu, jamaa, majirani na marafiki zake, kufuatilia mapambano ya kudai haki na demokrasia mitandaoni badala ya kuwa mshiriki kwenye uwanja wa mapambano, sasa ameelewa maana hasa ya kuwa ‘uhamishoni.’

Aidha, Lissu amemzungumzia dereva wake ambaye alidaiwa kutoroshwa kwa madai ya kushiriki njama za kumjeruhi akisema dereva huyo amekuwa mwaminifu kwake tangu akiwa na miaka 19, hawezi kushiriki njama hizo.

Hata hivyo, Lissu pia amehoji kuhusu ulipofikia uchunguzi wa polisi kuhusu tukio la kujerushiwa kwake na kuongeza kuwa hadi sasa hakuna mtu yeyote anayeshukiwa kumshambulia.

“Hakuna yeyote anayetuhumiwa, hakuna yeyote aliyehojiwa na wapelelezi wa polisi kama shahidi. Hata waathirika wa shambulio lenyewe, mimi na dereva wangu, hatujahojiwa,” amesema Lissu huku akiwatoa hofu Watanzania kwamba atarejea salama wakati wowote.

Kwa upande wake Mkuu wa Idara ya Uenezi ya Chadema, Hemed Ally, ambaye alikuwapo kipindi chote ambacho Lissu alikuwa amelazwa katika Hospitali ya Nairobi, amesema aliyopitia Lissu ni mapito yanayompambanua katika mapambano ya ukombozi.

“Kaka yangu, Lissu unafahamu njia yetu, maisha yetu, upendo na udugu wetu tumshukuru Mungu kwa haya mapito.

“Naamini kesho yetu ya vita hii ni neema na ndoto ya Watanzania na ndiyo maana Mungu amekupitisha. Endelea kuugua pole na nyumbani Watanzania wanakusubiri kwa hamu isiyo kifani,” amesema.

Binti amfanya Rais Magufuli achangishe fedha Baada ya Kumtajia Matatizo ya Shule yao

$
0
0
Akiwa katika mwendelezo wa ziara yake katika mikoa ya kanda ya ziwa ambapo kwasasa yupo Mkoani Mara Rais Magufuli, leo ameendesha harambee ndogo katika eneo la Nyamongo ya kuchangia fedha kwa ajili ya kutatua kero katika shule ya Ingwe, huku akiwataka wanaume katika eneo hilo kuacha mawazo

Akiongea na wananchi katika eneo hilo la Nyamongo wilayani Tarime mkoani Mara, Rais alimruhusu binti aitwaye Monica Bernad mwanafunzi wa kidato cha tano, katika shule ya Ingwe kueleza kero zilizopo katika shule hiyo.

Alipokabidhiwa kipaza sauti, Monica alianza kwa kusema kuwa shule hiyo inakumbana na changamoto nyingi ikiwamo upungufu wa walimu pamoja na vitabu.

“Shule yetu imeanza mwezi wa saba tarehe 30 kama High School lakini shule yetu ina upungufu wa walimu na vitabu kwa o-level na advanced level,” alisema mwanafunzi huyo.

Pia alieleza kuwa wana uhaba wa mabweni, hali inayosababisha wanafunzi kuchangia vitanda.

“Tuna bweni moja ambalo ‘tunashea’ wanafunzi wa o-level na advanced wa kike, katika bweni hilo tuna vitanda vichache ambapo inasababisha kitanda cha futi mbili na nusu tunalala wanafunzi watatu,” amesema.

Pia ametaja mambo mengine kuwa ni upungufu wa vyumba vya madarasa, viti, maji, umeme na ukosefu wa gari la wagonjwa.

“Tunakosa vitabu rejea kwa kidato cha tano na cha sita na inatufanya kutumia kitabu kimoja kwa kuchangia na vitabu hivi shuleni havipo. Mheshimiwa Rais tunatoka katika familia maskini tunaomba ututatulie tatizo hili,” amesema.

Baada ya kusikiliza kero hizo, Rais Magufuli alisema;

''Kwanza Monica nikushukuru sana lakini si ajabu vijana wa kiume wa Nyamongo wameshaanza kumwangalia angalia na pengine kufikiria kumtorosha, washindwe kabisa wasimsogelee Monica ambaye ameongea kwa niaba ya wanafunzi na vijana wengi'', alisema Magufuli.

Aidha katika kutatua kero za shule hiyo Rais aliendesha harambee ndogo katika mkutano huo wa hadhara ambapo viongozi mbalimbali wakiwemo Madiwani, Wabunge na Mawaziri walichangia na kuwezesha kupatikana kwa takribani shilingi milioni 24.

Mwisho Rais Magufuli yeye alichangia kiasi cha shilingi milioni 5, hivyo kufikisha zaidi ya milioni 29 ambazo amewaagiza Mkuu wa mkoa na RPC kuhakikisha zinakusanywa na kwenda kutumika kama ilivyokusudiwa ili wanafunzi katika shule ya Ingwe wasome bila shida.

Rais Magufuli Kuanza Ziara Mkoani Simiyu Kesho Septemba 08

$
0
0
Na Stella Kalinga, Simiyu
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli atafanya ziara ya siku tatu (03) Mkoani Simiyu, kuanzia kesho tarehe 08/09/2018 hadi tarehe 10/09/2018, Mkoani Simiyu.

Akizungumza na Waandishi wa habari ofisini kwake Mkuu wa Mkoa Mhe. Anthony Mtaka amesema Mhe. Rais akiwa mkoani Simiyu atapata nafasi ya kutembelea miradi mbalimbali ya maendeleo, kuweka mawe ya msingi, kufungua pamoja na kuzungumza na Wananchi kupitia mikutano ya hadhara.

Mtaka amesema siku ya Jumamosi tarehe 08/09/2018, Mhe. Rais atakagua na kuweka jiwe la msingi Ujenzi wa Mradi wa Maji wa Lamadi uliopo wilayani Busega na baadaye, ataelekea wilayani Bariadi.

Aidha, amesema Mhe. Rais akiwa katika Wilaya ya Bariadi, atafungua Jengo la Wagonjwa wa Nje(OPD) Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Simiyu, atakagua na kufungua barabara za lami (kilomita 6.9) zilizojengwa chini ya mradi wa kuboresha Miundombinu ya Miji (ULGSP).

“Siku hiyo pia atakagua maendeleo ya Ujenzi wa  barabara ya Bariadi-Maswa inayojengwa kwa kiwango cha lami na kuweka jiwe la msingi. Mhe.Rais atapokea salamu za Chama Cha Mapinduzi, salamu za Wilaya, Mkoa, taarifa ya mradi wa ujenzi wa barabara na baadaye kuzungumza na Wananchi wa Mkoa wa Simiyu na Watanzania wote kwa ujumla, katika Mtaa wa Salunda kwenye Viwanja vya Shule ya Msingi Salunda.”

“Tarehe 09/09/2018 Mhe. Rais atazungumza na wananchi wa wilaya ya Itilima eneo la Makao Makuu ya Wilaya (Lagangabilili) na kuelekea wilayani Meatu. Akiwa njiani kuelekea Meatu Mhe. Rais atapata fursa ya kusalimia wananchi wa Kijiji cha Mwandoya na baadaye atafungua Miundombinu ya Uboreshaji wa Huduma za Afya Hospitali ya Wilaya ya Meatu na kuzungumza na wananchi katika Viwanja vya Stendi ya Mwanhuzi” alisema Mtaka.

Ameongeza kuwa Siku ya Jumatatu tarehe 10/09/2018 Mhe. Rais Magufuli atahitimisha ziara yake Mkoani Simiyu kwa kuweka jiwe la msingi ujenzi wa daraja la Mto Sibiti linalounganisha Mkoa wa Simiyu na Singida na baadaye  kuwasalimia wananchi.

Katika hatua nyingine Mtaka ametoa wito kwa wananchi wote mkoani Simiyu hususani katika Miji ya Lamadi, Bariadi, Lagangabilili, Mwanhuzi na vitongoji vyake kujitokeza kwa wingi katika maeneo yote ambayo Mhe. Rais Magufuli atapita na kufanya mikutano ya hadhara.

MWISHO

Rais Magufuli: Tumelaliwa Vya Kutosha, Ngoja Na Sisi Tuwalalie

$
0
0
RAIS John Magufuli amekemea tabia ya baadhi ya  kampuni za uchimbaji madini zinazokwepa jukumu la kusaidia shughuli za kijamii katika maeneo wanayochimba madini, ikiwemo kuchangia fedha katika utekelezaji wa miradi ya maji, afya na elimu. Amapo amesema kampuni hizo zina wajibu wa kurudisha faida wanayopata katika jamii.

Rais Magufuli wakati akizungumza na akizungumza na Wananchi katika kijiji cha Nyamongo wilayani Tarime mkoa wa Mara leo tarehe 7 Septemba, 2018 amesema baadhi ya kampuni za uchimbaji madini zimekuwa zikiilalia serikali na wananchi kwa ujumla, na kwamba safari hii ni zamu yao kulaliwa.

“Lakini bahati nzuri sasa hivi tumepitisha sheria nzuri ya madini, palikuwa na sheria ya hovyo hovyo ndiyo maana nikasema, tumelaliwa vya kutosha ngoja na sisi tuwalalie, wametugeuza vya kutosha ngoja na sisi tuwageuzie, wametuchezea vya kutosha na sisi lazima tuwachezee, hii mali tumepewa na Mungu na Mungu ndiye alitaka hii mali iwe nyamongo kwa hiyo wale walitakiwa kuyafanya nataka kuwambia watayafanya, kwa hiyo huu mradi wa maji kwa vile ulikuwa ni mradi wao, nitamtuma waziri wa maji akazungumze nao.”

Kauli hiyo imetolewa na Rais Magufuli baada ya kupokea taarifa kuhusu kukwama kwa mradi wa maji unaojengwa na kampuni ya uchimbaji madini ya Acacia wilayani Tarime mkoa wa Mara unaogharimu kiasi cha Sh. Milioni 700.

Rais Magufuli amesema haiwezekani kampuni hiyo ikapata faida kutokana na uchimbaji madini, halafu ikashindwa kutoa sehemu ya faida hiyo kwa ajili ya kusaidia wananchi husika katika kutatua kero ya maji.

“Huu mradi wa milioni 700 ambao walisema wataleta na hawajaleta, mimi mwenyewe nitadili nao, kwa sababu hakuna mwekezaji aliyekuja kutangaza dini huku. Wote wamekuja kuwekeza kwa sababu ya kutafuta faida, sasa hawawezi wakataka faida, hata ile faida kidogo tunayoitaka na yenyewe waichukue, kwa sababu milioni 700 ni kiasi gani kwa mgodi mkubwa unaochukua matrilioni ya fedha? Maji tukose, wao wanakunywa maji ya chupa, hawataki kutupa maji miaka yote wanachukua dhahabu sisi kutupa maji hapana, nasema hili tutalisimamia,” amesema na kuongeza Rais Magufuli.

Benki Ya Dunia Yaipa Tanzania Mkopo Wa Trilioni 1.8

$
0
0
Benki ya Dunia (WB), imeipatia Tanzania mkopo wa masharti nafuu wa Sh trilioni 1.8 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi wa nishati na maji nchini.

Akizungumza le jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Dotto James, alisema kuwa mkopo huo wa masharti nafuu utakuwa na manufaa kwa nchi.

Alisema katika fedha hizo Wizara ya Nishati kupitia Tanesco itapewa Sh trilioni 1.04 kwa ajili ya kutekeleza mradi wa umeme unaounganisha Tanzania na Zambia na sehemu ya Magharibi mwa nchi.

“Na upande wa maji wao watapata Sh bilioni 800 ili kuweza kutekeleza miradi ya maji vijijini. Kwa mjini maeneo mengi tumefanya vema na sasa serikali kupitia Hazina kazi yetu ni kutafuta fedha kama hivi ili kuweza kufikia malengo ya serikali na kutekeleza miradi ya maendeleo,” alisema James.

Pamoja na hali hiyo, alisema kwa sasa serikali imedhamiria kusimamia kwa vitendo utekelezaji wa miradi yote ya maendeleo kama ilivyopangwa.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Profesa Kitila Mkumbo, alisena fedha hizo zinakwenda kutekeleza miradi kwenye mikoa 17 kwa kuimarisha huduma za maji, vyanzo.

“Pia fedha hizi zitakwenda kuimarisha taasisi zinazozimamia vyanzo vya maji pamoja na kuimarisha usafi ikiwamo zahanati na shule kwa kuwa na maji ya uhakika,” alisema Profesa Kitila

Alisema anaishukuru serikali kupitia Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, ambaye akuwa akitafuta fedha za miradi ya maji.

Akidi ya wabunge yakwamisha upigaji kura ya uamuzi

$
0
0
Kutotimia kwa akidi ya wabunge katika kikao cha nne cha Bunge la 12  leo Ijumaa Septemba 7, 2018 kimekwamisha kufanyika kura ya uamuzi ya kuupitisha au kuukataa  muswada wa marekebisho ya sheria mbalimbali  namba mbili wa mwaka 2018.

Kabla ya Bunge kukaa kama kamati ya Bunge zima, mbunge wa Kawe (Chadema), Halima Mdee aliomba kuhusu utaratibu kwa mujibu wa kanuni ya uendeshaji wa chombo hicho cha Dola , akieleza kuwa idadi ya wabunge bungeni haifiki nusu ya idadi ya wabunge wote.

Amesema wabunge wote ni 393 lakini waliopo bungeni mpaka muda huo wa mchana leo walikuwa 67, kubainisha kuwa idadi yao hiyo ni ndogo na hawawezi kufanya uamuzi kuhusu muswada huo.

Akijibu kuhusu utaratibu huo, mwenyekiti wa Bunge, Najma Giga amesema watakapofika wakati wa kufanya uamuzi, watazingatia idadi ya wabunge waliopo bungeni.

Hata hivyo, baada ya Kamati ya Bunge zima kumaliza shughuli yake ya kupitia kifungu hadi kifungu, bado idadi  ya wabunge bungeni ilikuwa ndogo na kumfanya Halima kunyanyuka tena, kukumbushia jambo hilo.

“Mheshimiwa mwenyekiti utoe maelekezo kengele ipigwe walioko nje waje, kwa makatibu wahesabu wabunge walioko bungeni halafu utaratibu wa kikanuni ufuatwe,”amesema Mdee.

Wakati Halima akieleza hayo naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Stella Manyanya, ameshauri kuwakata posho wabunge ambao hawakuwepo bungeni kwa wakati huo isipokuwa waliokwenda msikitini na wale wenye ruhusa.

“Mwenyekiti ukiwatoa wale walioenda msikitini na wale walioomba ruhusa kuna wale wazembe wa kutohudhuria Bunge. Ninashauri wakatwe posho ya siku ya leo,” amesema Manyanya.

Katika ufafanuzi wake Najma amesema, “natoa dakika tatu kengele ipigwe ili waingie waliokuwepo nje.”

Licha ya tangazo hilo idadi ya wabunge bado haikutimia na hivyo kuamua kuahirisha Bunge hadi Septemba 10, 2018 saa 3:00 asubuhi.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images