Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumamosi ya Septemba 8


Kiwanda cha Kagera Sugar Chatoa Kodi ya bilioni 44 kwa Miaka mitatu

0
0
Na Jacquiline Mrisho –Maelezo
Kiwanda cha Sukari cha Kagera kimeilipa Serikali kodi ya jumla ya shilingi 44,461,815,798 katika kipindi cha miaka mitatu tangu 2015 hadi 2018.

Takwimu hizo zimetolewa jana na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Jimbo la Nkenge, Balozi Dkt. Diodorus Kamala lililohoji manufaa ya kiwanda cha Sukari cha Kagera kwa wananchi wa Wilaya ya Misenyi, Mkoa wa Kagera na Taifa kwa ujumla.

Waziri Mwijage amesema kuwa tangu kiwanda hicho kibinafsishwe,faida na michango mbalimbali imepatikana ikiwemo ya kuongezeka kwa uzalishaji wa sukari kutoka tani 15, 362 zilizozalishwa mwaka 2004/05 hadi kufikia tani 75, 568 mwaka 2017/18 ambapo uzalishaji huo umesaidia kuokoa fedha za kigeni ambazo zingetumika kuagiza bidhaa hiyo toka nje ya nchi.

“Mpaka sasa kuna wakulima 500 wanaolima eneo la hekari 5, 019 za miwa ambapo kwa Mwaka wa Fedha 2017/18 wakulima hao waliweza kuzalisha tani 60,000 za miwa zilizowapatia kipato cha shilingi bilioni kuwepo kwa kiwanda hiki ni faida kwetu hivyo natoa rai kwa wafanyabiashara wa sukari kuendelea kuzingatia sheria za kuendesha biashara hiyo,”alisema Mwijage.

Waziri Mwijage ameongeza kuwa hadi kufikia mwaka 2018, kiwanda kimetoa jumla ya ajira 6,000, kimejenga hospitali yenye vitanda 78, kimechangia vifaa vya ujenzi wa madarasa, kimechimba visima vya maji, kujenga vyoo, nyumba za walimu pamoja na madawati.

Vile vile kiwanda hicho kimechangia ujenzi wa maabara na kutoa vifaa vya kufundishia kwa shule 23 katika Wilaya ya Misenyi, kimepanda jumla ya miti 20,000 katika eneo la kiwanda hicho pia kimejenga mtandao wa barabara zenye urefu wa Kilomita 1,250.

Aidha, Waziri Mwijage amefafanua kuwa kiwanda hicho kina utaratibu wa kuwatumia wakulima wa nje katika kulima miwa inayotumia hivyo inawaletea manufaa wakulima nchini kwa kulima mazao bora yenye tija.

Kiwanda cha Sukari cha Kagera ni kati ya Viwanda vilivyobinafsishwa katika miaka 90 kikiwemo cha  Kilombero kilichopo mkoani Morogoro. Hivi karibuni Mhe. Rais John Pombe amekuwa akisisitiza kuwa viwanda vilivyobinafsishwa na  hadi sasa havifanyi kazi virudishwe Serikalini.

Rais Magufuli ataja sababu kumg’oa bosi TAKUKURU

0
0
Rais, John Magufuli, amesema sababu za kumtumbua Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Valentino Mlowola, ni kutokana na kushindwa kushughulikia jalada lililomfikia mezani kwake na madhambi mengine ya nyuma.

Rais Magufuli alitoa sababu hiyo jana katika mkutano wa hadhara uliofanyika viwanja vya Chuo cha Ualimu Tarime, mkoani Mara ikiwa ni siku moja tangu amwondoe kwenye nafasi hiyo na kumteua kuwa balozi.

Nafasi ya Mlowola ambaye ni Kamishna wa Polisi, imechukuliwa na kamishna mwingine wa jeshi hilo, Diwani Athumani, ambaye alikuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera.

Akizungumza na wananchi waliokuwa wamefurika kwenye mkutano huo, Rais Magufuli alisema alikwenda Musoma, mkoani Mara na kukuta mtu aliyeinunua hoteli ya Musoma haiendelezi na kila kandarasi anayopewa haiendelezi.

Alisema hata Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, alipita na kutoa maagizo Takukuru walishughulikie tatizo hilo hilo la mnunuzi wa hoteli ya Musoma lakini hakuna kilichofanyika.

“Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Mara alilishughulikia, akalishughulikia na kulipeleka Makao Makuu ya Takukuru na kuweka mapendekezo yake yote. Makao makuu tangu Aprili hadi mwezi huu hawajalishughulikia.

"Nikaona Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru akae pembeni akafanye kazi nyingine.Nikaangalia na madhambi mengine yakajitokeza nikasema kazi ya kushughulikia rushwa haiwezi,” alisema.

“Nilikaa usiku nafikiria hadi kichwa kikauma, ilipofika saa 11 alfajiri nikafanya kazi. Muda huo ndipo ilitumwa taarifa ya Ikulu kuwa uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru umetenguliwa,”alisema.

Aliongeza kuwa: “Nataka kuwaeleza kuwa watu wangu ninaowateua mshughulikie shida za wanyonge. Ambaye hawezi kufanya hivyo aandike barua ya kuacha kazi. Huwezi kazi lakini mshahara unalipwa. Usafiri unao wananchi maskini kama hawa huwashughulikii wakati wangu hili haliwezekani,” alisisitiza.

Rais Magufuli alimtangazia msamaha Mkuu wa Wilaya ambaye alishindwa kushughulikia tatizo la mama mwenye ulemavu wa macho kuwa, amemsamehe siku hiyo lakini akirudia mara ya pili hatamsamehe.

Akizungumzia kuhusu mwanamke huyo mwenye ulemavu wa macho, Rais Magufuli alisema alikwenda katika kijiji kimoja na kumkuta mwanamke huyo ambaye amedhulumiwa mazao yake na tajiri mmoja mwenye zaidi ya ng’ombe 3,000.

Alisema mama huyo alikuwa anahangaika kila siku na wakati mwingine alikuwa anaanguka kwenye mitaro kwa sababu haoni.

“Amekwenda hadi mahakamani, amekwenda hadi kwa Mkuu wa Wilaya ambaye anamamlaka makubwa lakini hakufanya hivyo na ameendelea kulalamika mpaka nilipofika mimi,” alisema

Aliongeza kuwa: “Nimeumia mno kwamba Watanzania hatumuogopi hata Mungu nilitamani kumfukuza Mkuu wa Wilaya leo, Roho wa Bwana akaniambia tunatakiwa kusamehe saba mara sabini na mimi huwa sijali natumbua tu.”

Katika hatua nyingine, Rais Magufuli alimwagiza Waziri wa Madini na Mkuu wa Mkoa Mara wamhoji mtu aliyetajwa kwa jina moja la King’anya ambaye ndiye aliyesaini mkataba wa Mfuko wa Fedha wa North Mara (NMRF) ambao fedha zake hazijulikani zipo wapi.

“Palikuwa na malipo ya vijiji kati ya vitano au sita ambavyo viliingia mkataba na mgodi tangu ukiitwa North Mara kabda haijaja kampuni ya Acacia,” alisema.

Alisema vijiji hivyo viliingia mkataba kwamba vingekuwa vinalipwa fedha ndipo ukafungulia mfuko huo lakini akaja mtu mjanja akauanzisha ili ziingizwe humo.

Alisema fedha hizo zimeingizwa kwenye mfuko na zilivyokuwa nyingi ukasimamishwa hivyo Acacia hawawezi kuingiza fedha humo na licha ya hali hiyo viongozi wa serikali wapo lakini hawajafanya chochote.

“Huyu King’anya ndiye anayetakiwa atuambie mfuko una kiasi gani. Waziri wa Madini na Mkuu wa Mkoa mshughulikie suala hili, mumuite King’anya mjue huo mradi una kiasi gani mumueleze huyo King’anya ni kiasi gani cha fedha ambacho hakijalipwa,” alisema.

Rais alisema fedha hizo zingekuwepo hata wangetaka maji ya bilioni tano zingetosha kwa sababu vile vijiji vilikubali.

“Nilitegemea Mbunge, diwani na watendaji wengine Mkuu wa Wilaya, Mkuu wa Mkoa wangeshughulikia suala la mfuko huu na kujua fedha hizi zimekwenda wapi na Acacia inatakiwa kulipa kiasi gani lakini hawayashughulikii haya na hawajui mfuko una shilingi ngapi,” alisema.

Alisema mfuko huo umeshikiliwa na matapeli na viongozi kuanzia ngazi ya chini hawajui una kiasi gani.

Diwani wa eneo hilo alipohojiwa na Rais kuhusu fedha za mfuko huo alisema hadi sasa hawajui ni shilingi ngapi zipo na kumtaja King’anya kuwa ndiye anayefanya mahesabu kwa kushirikiana na Acacia.

Rais Magufuli alisema anataka kupata taarifa za fedha hizo zilizopo tangu mfuko ulivyoanza, zilizotumika na zilizobaki.

“Kama hamjui King’anya ndiye mtia saini, wanaofaidika ni wengine ambao ndio watia saini, wananchi hawafaidiki ni sawa na kufuga ng’ombe maziwa wanywe wengine,” alisema.

Rais Magufuli alisema anataka kuijenga Tanzania ili wazulumaji, majizi wote washughulikiwe na ndiyo maana alianza kwa kuwaondoa watumishi hewa, mafisadi wakubwa kwa kuwapeleka mahakamani.

Alisema wote waliosaini katika mkataba huo akiwamo King’anya lazima watoe maelezo fedha za Nyamongo ziko wapi.

Magufuli alisema wapo baadhi ya wananchi ambao wanatakiwa kulipwa fidia ya nyumba na mashamba yao yaliyofanyiwa tathmini lakini baadhi wanategesha ili nao walipwe.

“Tatizo lililopo Nyamongo wajuaji ni wengi maarifa mengi kupoteza njia wamekuja watu wakafanya tathmini wakaja wengine wanategesha, niwaambie wanaotegesha hakuna atakayelipwa, tegesha hata kwenye maji hutalipwa,” alisema.

Alisema orodha ya watu wanaostahili kulipwa fidia ipo na hao wanaotegesha ndio wanaowacheleweshea wanaostahili kulipwa.

Rais Magufuli alisema kuwa aliyekuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi eneo hilo alikuwa hafai ndiyo maana alitolewa.

“Nataka kuwaeleza ukweli nayafahamu ya hapa, mkoa wa Mara umejaa migogoro kila ukifika kuna migogoro, nimefika pale kwenye daraja Nyasurura nimekuta mama amedhurumiwa ni kipofu, akaenda kwa viongozi wote wanamzungusha mpaka amekwenda kwa Mkuu wa Wilaya (DC).

“Nilitamani leo nifukuze DC lakini ana bahati sana. Sitaki watu wanyanyaswe, mimi ni Rais wa wananchi wanyonge na mimi nimetoka familia maskini,”alisema na kuongeza:

“Niwaombe wananchi muendelee kushirikiana na serikali na nyinyi mkubali kusikiliza maelekezo yanayotolewa na serikali,” alisema Katika ziara hiyo, Mwanafunzi wa Kidato cha Tano katika Shule ya Sekondari Ingwe, Monica Dunde, alimgusa Rais Magufuli baada ya kupewa nafasi na kueleza changamoto za shule yao zilizosabababisha, atoe fedha taslimu Sh. milioni tano 5 na viongozi wengine kuchangia.

Fedha zilizotolewa ahadi na taslimu ni zaidi ya shilingi milioni 18 ambazo zitakwenda kutatua changamoto za shule hiyo ikiwemo upungufu wa madawati, vyumba vya madarasa, vitabu, vitanda na mabweni.

Ajali Yaua Watu 11 Jijini Mbeya

0
0
Watu 11 wamefariki dunia  na wengine kadhaa kujeruhiwa katika ajali ya barabarani iliyohusisha magari manne ikiwemo gari ndogo ya abiria aina ya Toyota Hiace iliyotokea  jana eneo la Mlima Igawilo Kasoko Jijini hapa.

Kwa majibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Ulrich Matei amesema ajali hiyo imetokea majira ya saa kumi na moja za jioni ambapo chanzo cha ajali hiyo inadaiwa ni kufeli kwa Lory lenye namba T334 DJN lililokuwa limebaba ndizi likitokea Wilayani Rungwe.

Amesema, waliofariki dunia  ni watu ni  na idadi ya majeruhi bado haijapatikana kwani watu waliokuwepo kwenye magari hayo walikimbizwa hospital kwa ajili ya matibabu.

Aidha amesema baada ya Lory namba T334 DJN likitokea Tukuyu, kufeli brek hivyo kugonga  gari Dogo ya abiria Hiace namba T883 ABS ambalo nalo liligonga Lory lingine lililopakia ndizi nalo kugonga Lory la mafuta. 

Amesema , majeruhi wa ajali hiyo walikimbizwa hospitali ya Rufaa ya Mbeya kwa ajli ya matibabu.

 Baadhi wa mashuhuda wa ajali hiyo, walisema kuwa dereva wa lory lililosababisha ajali alifanya makosa kwani alipoona gari hilo limeferi brek alikuwa na uwezo wa kulichepusha pembeni ili kuepusha ajali hiyo ambayo ni kubwa.

Rais Magufuli Atuma Salamu za Rambirambi.....“Nimeshtuka watu 11 kufariki tena kwa ajali mkoani Mbeya”

0
0
“Nimepokea kwa mshtuko taarifa ya vifo vya watu 11 vilivyotokea leo jioni huko Mbeya, kwa mara nyingine tumewapoteza Watanzania wenzetu katika ajali ya barabarani na wengine wameumia, nimesitishwa sana na vifo hivi.
 
“Nawapa pole wanafamilia wote waliopoteza ndugu zao katika ajali hii na pia nawapa pole majeruhi wote, nawaombea watibiwe na kupona haraka ili waweze kuungana na familia zao na kuendelea na shughuli zao za kila siku”

Ni salamu za rambirambi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli alizozitoa kupitia kwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Albert Chalamila kufuatia ajali ya barabara iliyosababisha vifo vya watu 11 na wengine 15 kujeruhiwa.

Ajali hiyo imetokea  jana katika mteremko wa mlima wa Igawilo Jijini Mbeya baada ya Lori lililokuwa na shehena ya viazi, likitokea Tukuyu kwenda Mbeya Mjini kuyagonga magari matano likiwemo basi dogo lililokuwa na abiria.

Pamoja na kutoa pole kwa wafiwa wote, ndugu, jamaa, marafiki na wote walioguswa na vifo hivyo Rais Magufuli amewaombea Marehemu wote wapumzike mahali pema peponi.

Tanzania Yaikabidhi Seychelles Uongozi Wa Mapambano Dhidi Ya Utakasishaji Fedha Haramu Na Ufadhili Wa Ugaidi

0
0
Na Benny Mwaipaja, WFM, Mahe, Seychelles
TANZANIA imekabidhi uongozi wa mwaka mmoja wa Umoja wa Udhibiti wa Fedha Haramu wa Nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika (ESAAMLG) kwa nchi ya Seychelles, huku ikijivunia mafanikio makubwa ya kuhakikisha kuwa nchi wanachama wa umoja huo zinakuwa na sera, sheria, taasisi na mifumo imara inayowezesha mapambano dhidi ya vitendo vya utakasishaji fedha haramu na  ufadhili wa ugaidi.

Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, amekabidhi uongozi huo kwa niaba ya Serikali ya Tanzania kwa Waziri wa Fedha, Biashara, Uwekezaji na Mipango ya Kiuchumi wa Seychelles Balozi Maurice Lousteau – Lalanne, wakati wa Mkutano wa 18 wa Baraza la Mawaziri wa Umoja huo, uliofanyika Mjini Mahe, nchini Seychelles na kushuhudiwa na Rais wa Nchi hiyo, Mhe. Danny Faure.

Miongoni mwa mafanikio yaliyofikiwa katika kipindi hicho cha mwaka mmoja, ni kufanyika kwa tathimini ya mifumo ya kudhibiti utakasishaji wa fedha haramu na ufadhili wa ugaidi wa nchi tatu wanachama wa umoja huo za Mauritius, Madagascar na Seychelles, na kwamba zoezi la kuzitathmini nchi nyingine mbili za Zambia na Malawi, linaendelea.

"Rasilimali za nchi zetu zinahitaji kutumika  vizuri, kwa sababu zinapotumika vibaya zinapunguza uwezo wa nchi zetu kuchochea maendeleo haraka, pale zinapo hatarisha sekta yetu ya fedha, matumizi adili ya rasilimali hizi na usalama wa nchi zetu" alisema Dkt. Mpango

Aidha, Dkt. Mpango amesema kuwa utakasishaji wa fedha haramu unazuiwa kwa sababu unamadhara makubwa kiuchumi, kijamii na kiusalama kwa nchi wanachama..

"Fedha ambazo zinakuja kuja tu hivi! Hujui kama zinakwenda kugharamia ugaidi, au ni fedha za wananchi wetu lakini wanazitorosha ambapo badala ya kuzitumia ipasavyo wanazitumia kufanya mambo haramu" aliongeza Dkt. Mpango

Kwa upande wake, Katibu Mtendaji wa Umoja wa nchi za Mashariki na Kusini Mwa Afrika ESAAMLG, Dkt. Elliawony  Kisanga amesema kuwa tangu umoja huo uanzishwe miaka 19 iliyopita, yamekuwepo mafanikio makubwa na kazi iliyopo mbele ya uongozi mpya ni kuanza na kuendelea kufanyika kwa tathmini ya mifumo ya udhibiti ya nchi za Zambia, Malawi na Tanzania.

Mwenyekiti Mpya wa ESAAMLG, Waziri wa Fedha, Biashara, Uwekezaji na Mipango ya Kiuchumi wa Seychelles Balozi Maurice Lousteau – Lalanne, ameipongeza Tanzania chini ya Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, kwa uongozi wake mahili na kuuwezesha umoja huo kutekeleza majukumu yake ipasavyo na msukumo wake utakuwa kuwezesha nchi wanachama kuendelea kusimamia utekelezaji wa sheria.

Aidha  Mkutano wa Baraza la Mawaziri wa ESAAMLG ulitanguliwa na Mkutano wa 36 wa Kikosi Kazi cha Maafisa waandamizi wa ESAAMLG, ambapo Bw. Onesmo Makombe alikabidhi kwa niaba ya Tanzania Uenyekiti wa Kikosi Kazi hicho kwa Bw. Philip Moustache wa Jamhuri ya Seychelles.

Tanzania ilipokea uongozi wa Umoja huo Septemba 7 mwaka jana wakati wa Mkutano wa 17 wa Baraza la Mawaziri wa Nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika uliofanyika Zanzibar, ikipokea majukumu ya uongozi huo kutoka nchi ya Zimbabwe ambapo Umoja huo unaundwa na nchi 18 ambazo ni Angola, Botswana, Eswatini, Ethiopia, Kenya, Lesotho, Madagascar, Malawi, Mauritius, Mozambique, Namibia, Rwanda, Seychelles, South Africa, Tanzania, Uganda, Zambia na Zimbabwe.

Mwisho

Kalulumila:Dawa Bora ya Nguvu za Kiume na Maumbile Madogo

0
0
 BORA YA NGUVU ZA KIUME NA MAUMBILE MADOGO KALULUMILA.
----------------------------------------
Ni dawa pekee iliyojipatia umaarufu nchini na nje ya nchi kwa kufanya kazi mara 3, kwa wakati mmoja 1, kurefusha uume na kunenepesha saizi uipendayo kuongeza nguvu za kiume na inatibu matatizo na gerentii miaka 30. Na kuendelea haina madhara, inaimarisha mishipa ya uume iliyoregea na udhalishaji wa mbegu za kiume. 


---------NINI HUCHANGIA MATATIZO HAYA--Ngiri ni chanzo kikubwa cha matatizo haya ili kujua kwamba una ngiri ni chanzo kikubwa cha matatizo haya, ili kujua kama unangiri dalili zake ni kufika haraka kileleni wakati wa tendo la ndoa, 2)kushindwa kurudia tendo la ndoa. 3)kutoa choo kama cha mbuzi. 4)tumbo kujaa gesi na kuunguruma. 5)kukosa choo kabisa. 6)maumbile kuingia ndani na kuwa mafupi. 7) korodani moja kuvimba 8)kutosikia hamu ya tendo la ndoa na maumivu ya kiuno wakati wa tendo la ndoa. 9)maumivu ya kiuno na mgongo pia tunatibu kisukari kwa siku7, presha, busha, bila kupasuliwa na magonjwa mbalimbali. 

---------------------------------------
TUPO TEGETA KWA NDEVU KARIBU NA MACHINJIO YA NGOMBE UTAONA OFSI IMEANDIKWA KALULUMILA HERBALIST CLINIC HOSPITAL SIMU .
----------------------------------------
-0655-557-182.
-0755-557182.
-0784-557-182.
PIA UTAWEZA KULETEWA POPOTE ULIPO.
---------------------------------------
KARIBUNI SANA.
----------------------------------------

Majambazi Wavamia Kijiji na Kuiba Mali

0
0
Watu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi wamemvamia mfanyabiashara, Burugu Mahanghija (44), mkazi wa Kijiji na Kata ya Lyabukande Shinyanga vijijini na kumpora fedha taslimu na mali yenye thamani ya zaidi ya Sh3 millionI.

Diwani wa Kata hiyo ya Lyabukande Joseph Misri, amesema baada ya kupora fedha na mali katika duka hilo, watuhumiwa hao waliwavamia wananchi wengine waliokuwa wakiangalia taarifa ya habari katika moja ya baa za eneo hilo na kuwapiga huku wakiwapora fedha na simu.

“Kelele za kuomba msaada ziliwafanya watuhumiwa hao waliokuwa na silaha kufyatua risasi hewani kutishia wananchi kabla ya kutokomea gizani,” amesema Misri.

Serikali yawasilisha bungeni marekebisho sheria ya TLS.....Watumishi wa umma, madiwani, wabunge ni Marufuku

0
0
Serikali imewasilisha marekebisho ya Sheria ya Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS) sura namba 307 ambapo sasa watumishi wa umma, madiwani, wabunge na viongozi wa vyama vya siasa hawataruhusiwa kugombewa ujumbe wa Baraza la TLS.

Akiwasilisha maoni ya Kamati ya Katiba na Sheria bungeni jana  Septemba 7 2018, mjumbe wa kamati hiyo Dk Damas Ndumbaro alisema marekebisho hayo yanalenga pia kuongeza vifungu vidogo na kuboresha mtiririko wake.

Alisema vifungu vinavyoongezwa katika muswada huo vinaweka sifa za mtu kuchaguliwa kuwa mjumbe wa baraza hilo ambapo mjumbe husika anatakiwa kuwa raia wa Tanzania, amethibitishwa kuwa na akili timamu.

Sifa nyingine zinazoongezwa ni kuwa hajatangazwa kuwa mufilisi na amethibitishwa na kamati ya uteuzi kuwa na weledi.

“Marekebisho yanayopendekezwa yanakusudia kutoruhusu mtumishi wa umma, diwani, mbunge ama kiongozi wa chama cha siasa kugombea ujumbe wa baraza hilo,”alisema.

Alisema pia muswada huo unapendekeza kuongeza kifungu kinachohusu kuzuia mjumbe wa baraza kujihusisha na shughuli za kisiasa na sheria.

Muswada huo umeainisha shughuli za kisiasa kuwa zinazokatazwa na sheria hiyo ni pamoja kugombea nafasi za kisiasa katika chama cha siasa, kupiga kampeni za kumuunga mkono au kumpiga mgombea yeyote chaguzi za kisiasa.

Shughuli nyingine ni kutoa hotuba za kampeni, kukusanya michango au kufanya harambee kwa ajili ya chama chochote cha siasa na kupanga au kusimamia maandamano ya kisiasa au mikutano au kuwa na nafasi ya madaraka katika vyama vya siasa.

“Inapendekezwa na ibara hii kuwa iwapo mjumbe atakiuka masharti atakuwa amefanya makosa makubwa ya kimaadili na ikitokea, mwanasheria mkuu wa Serikali anaweza kupeleka maombi katika kamati ya mawakili ili mhusika aondolewe kwenye orodha ya mawakili,”alisema Ndumbaro.

Pia muswada huo unapendekeza utungaji wa kanuni ufanywe na baraza kwa kushauriana Mwanasheria Mkuu wa Serikali na kisha kanuni hizo zitatatikiwa kuchapishwa kwenye gazeti la Serikali.

Dk Ndumbaro amesema kamati hiyo imeridhia mapendekezo ya Serikali kwasababu yana lengo la kuimarisha misingi ya nidhamu, vigezo na mipaka ya kitaaluma kwa mawakili wa kujitegemea.

Makanga 3 Power; Dawa Bora Nguvu Za Kiume

0
0
Kutibu nguvu za kiume dakika(10) na kupona muda wa siku tatu tuu. Kuimarisha misuli ya uume uliolegea, pia ipo Dawa ya kurefusha uume mfupi inchi NNE hadi saba na kunenepesha uume mfupi sentimita NNE.

Tiba ya kudumu kutibu maumivu ya mgongo,kiuno, tumbo kuunguruma na kujaa gesi, kupata choo vizuri, na kutibu uzazi, kutibu busha bila operesheni, kisukari, presha ,miguu kuuma, uzazi, fangas sugu, vidonda vya tumbo.

Ni docta bingwa wa kutibu magonjwa sugu, kutoa ndagu za utajiri kwa kutumia Pete, kazi ,cheni, mikufu maalumu ya bahati, una kesi umedhulumiwa Mali au pesa? Zitarudi muda wa Masaa matatu tuu.

Onana na Dr shilindes shida zako zote zitakwisha, anatoa Dawa za utajiri kwa wafanyakazi, wakulima, na wafugaji, wafanyabiashara na wachimba madini kwa kutumia pete, kazi kwa yeyote anaetaka kuwa na pesa nyingi.

Pia anaboresha akili kwa wanafunzi darasani, masomo na kufaulu mitihani pia kushinda bahati nasibu yeyote.

Pia tunatoa Dawa kumrudisha Mume, mke, mpenzi, hawara, kwa muda wa SAA moja tuu, na kuomba msamaha kwa kukupigia magoti na yeyote yule, unaemtaka kimapenzi au kuoana, utampata na kumfunga asitoke nje ya ndoa daima na kutekeleza shida zako zote. Kupunguza unene, kupunguza matiti makubwa, tumbo na nyama uzembe muda wa siku sita unapata saizi uipendayo.

Kutoa makovu mwilini, chunusi, upele na mabaka, pia tunayo Dawa ya kuongeza hipsi, makalio, mguu wa bia na kupata shepu safi kwa muda wa siku saba tuu.

Wa mikoani mtapata huduma popote mlipo.
Tupo dar es salam mbagala rangi tatu.

Mawasiliano simu namba: 0784 460 348. Au 0659 103 360.

Mgambo wa Makonda wanaodaiwa kupiga raia wapandishwa kizimbani, Wanyimwa Dhamana

0
0
Askari Mgambo wawili na Afisa mtendaji wa kata ya Bunju,
wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na shtaka la kumjeruhi kwa kutumia Rungu mkazi wa Bunju Robinson Olotho.

Wakili wa Serikali, Mwanaamina Kombakono amewataja washtakiwa hao kuwa ni askari Mgambo Kelvin Sawala (25) na Goodluck Tarimo (30) ambao wanashtakiwa pamoja na Ofisa Mtendaji wa Kata ya Bunju Ibrahim Mabewa (39).

Wakisomewa hati ya mashtaka mbele ya Hakimu Mkazi, Maira Kasonde imedaiwa August 30, 2018 huko  Bunju Wilayani Kinondoni, washtakiwa hao walimpiga Olotho kwa kutumia rungu sehemu mbalimbali za mwili wake na kumsababishia majeraha makali

Hata hivyo washtakiwa wamekana kosa hilo na wamerudishwa rumande baada ya wakili wa serikali, Nassoro Katuga kuieleza mahakama kuwa, licha ya kesi hiyo kudhaminika lakini wanaiomba mahakama isubirishe dhamana ya washtakiwa hao kwa sababu kuu mbili.

Alizitaja sababu hizo  kuwa kuna suala la kiusalama ambapo washtakiwa walionekana kwenye video zilizosambaa katika mitandao ya kijamii na vyombo vya habari, hivyo kama watapatiwa dhamana usalama wao utakuwa shakani kwa sababu wananchi na ndugu wa mjeruhiwa watakuwa na hasira.

Pia akadai sababu nyingine ni kwamba mjeruhiwa bado yupo hospitali na hali yake ya kiafya sio nzuri.

Hakimu Kasonde alipowauliza washtakiwa hao kuhusu hoja hizo walidai hali ya afya ya mjeruhiwa walionana naye jana na anaendelea vizuri wala hayupo hospitalini na kuwa suala la usalama wao liko vizuri, hivyo wanaomba dhamana,

Hata hivyo, Hakimu Kasonde alisema mahakama imekubali hoja za upande wa mashtaka kuhusu usalama wa washtakiwa hao, hivyo wananyimwa dhamana hadi hapo itakapojiridhisha kuhusu usalama wao.

Upelelezi katika kesi hiyo bado haujakamilika na imeahirishwa hadi September 20,2018.

Hamisa Mobetto kusimamia Show Miss Tanzania 2018

0
0
Mwanamitindo Hamisa Mobetto ndiye atasimama kama host wa shindano la Miss Tanzania ambalo litafanyika usiku wa leo September 08, 2018.

Mrembo huyo anachukua nafasi huyo akiwa na uzoefu wa kutosha na mashindano kama hayo kwa kuwa ameshashiriki hadi Miss Univeristy Afrika.

Utakumbuka mwaka 2010 alitwaa taji la Miss XXL, After School Bash, mwaka uliofuata Hamisa alishiriki mashindano ya Miss Dar Indian Ocean na kushika nafasi ya pili, pia aliwahi kufanikiwa kuingia nusu fainali ya Miss Tanzania. 

Magufuli aagiza uchunguzi madai ya maji yenye sumu

0
0
Rais , John Magufuli, ameagiza kufanyika upya kwa uchunguzi wa madai ya maji yenye sumu yanayotiririka kutoka mgodi wa Acacia North Mara kwenda kwenye vyanzo vya maji baada ya ripoti ya kwanza kujaa udanganyifu.

Agizo hilo limetolewa ikiwa ni zaidi ya miaka 10 tangu wananchi wa vijiji vinavyozunguka mgodi huo kudai kuwa maji hayo yamekuwa yakisababisha madhara makubwa kwa binadamu ikiwemo vifo vya watu, mifugo na kuathiri vyanzo vya maji.

Rais Magufuli aliyasema hayo jana akiwa kwenye ziara ya kikazi na kuagiza Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kufanya upya uchunguzi huo kwenye Mto Tigiti.

“Maji wanayokunywa watu na wanyama kwenye mto huo kwenye ripoti ya kwanza iliyoundwa nikiwa bado Waziri waliichezea, ng’ombe walikuwa wanakufa, watu walikuwa wakioga wanaungua mikono ripoti ikachezewa,” alisema na kuongeza:

“Mimi ni mkemia ninafahamu. Nataka mfanye uchunguzi vizuri na hiyo ripoti iwe wazi. watu wa Nemc waje wachunguze haya maji yanayotoka mgodini,” alisema.

Rais Magufuli alisema kama kuna kitu wamefanya cha kuharibu mazingira na kuyaharibu maisha ya watu, lazima walipe kwa sababu “mshahara wa dhambi unajulikana”.

“Watu wanateseka wanakunywa maji ya ajabu. Hili ninataka mlifuatilie. NEMC waje wachunguze maji yote yanayonywewa na wananchi wa hapa, wachunguze mito yote waangalie mchanganyiko wa kemikali zote zilizomo humo.

“Lazima wananchi hawa watendewe haki ninaifahamu ile ripoti ng’ombe wanaungua, watu walikuwa wanaoga wanabadilika rangi ripoti waliichezea,” alisema.

“Kwa sababu sikuwa na madaraka nikanyamaza, leo nina madaraka ninayasema hadharani. Ripoti ile ileteni NEMC ifanye kazi na wakiichezea wanaondoka wote,” alisisitiza.

Katika hatua nyingine, Rais Magufuli alisema mwaka 2015 alikwenda kuomba kura na walimpa nyingi na aliwaahidi atawafanyia kazi.

“Leo nimekuja na gari kuwashukuru hapa, hapa- kupangwa mkutano lakini nilipoona ni Nyamongo nimesimama mwenyewe ili kusudi nizungumze na nyinyi,” alisema.

Rais Magufuli aliwaeleza wananchi hao kuwa yapo mengi ambayo wamejipanga kuyashughulikia.

“Suala la umeme halikuwepo lakini sasa unapita na utasambazwa vijijini vingi, tunafanya hivi kwa heshima kubwa wananchi wa Nyamongo, Tarime na Serengeti wana haki ya kula matunda ya nchi hii.

“Mimi ni Rais wa Watanzania wote nisingekuwa na upendo hapa nisingepita kwa sababu niliwaomba mnichagulie mbunge mkamgeuka hamkumchagua lakini nikaja nikajua ile halikuwa kosa lenu, lilikuwa kosa la wana CCM. Waliwaletea mtu ambaye hakubaliki, tumeshajifunza siku nyingine tutawaletea mtu anayekubalika kweli kweli,” alisema.

Huna Sababu Ya Kuaibikatena............ Jipatie Dawa Bora Ya Nguvu Za Kiume, Maumbile Madogo Na Mvuto Wa Mapenz

0
0
Usikate tamaa ondoa maradhi yako, maana matatizo haya yamekua yakiasili watuwengi kisaikolojia hasa baada ya kujiona wako tofauti sana na wengine kawaida mwanaume anatakiwa awe na uume kuanzia (6-8) vinginevyo mtuhuyo anamapunguvu katika mwiliwake.

Kunasababu nyingi sana zinazosababisha matatizo haya, chango hushambulia never ambayo huasili misuli ya uume, Ngili :- hii huleta maumivu ya tumbo chini ya kitovu na kufanya tumbo kuunguluma na kujaa gesi, kolodani moja kuvimba au kuingia ndani pamoja na kutopata choo vizuli. Sababuhizi na nyingine hufanya uume kulegea na kusinyaa na kuwa mfupi na mwembamba na marakwamara husababisha kukosa hamu ya kuludia tendo la ndoa na baadae kushindwa kabisa

MASISA 3POWER :- nidawa ya mitishamba iliyotengenezwa kwa mfumo wa vidonge, huongeza nguvu za kiume maradufu kuanzia umri wa miaka 15-90 , inakomaza mbegu zisizo na viini vya uzazi (manii) inaimalisha mishipa iliyolegea wakati wa tendo la ndoa, itakufanya uludie tendo la ndoa zaidi ya mara nne (4) birahamu kuisha wara kuhisi kuchoka na itakufanya uchelewe kufika kileleni zaidi ya dk (20-30 )

YONINANI:- hurefusha na kunenepesha maumbile madogo ya uume uliosinyaa inchi 6-8 na unene wa sm 3-4 kwa mda mfupi sana,

SUPER MORINA :- nidawa inayotibu ama kutatua tatizo la kisukali kwawaliohangaika bila mafanikio, huondoa tatizo la kisukali na kupona kabisa, vilevile ninadawa ya magonjwa sugu km vile presha, vidondo vya tumbo, miguu kuwakamoto, muwasho mwilin, kaswende,uzazi nk.

LUGIMBA :- nidawa ya mvuto wa mapenzi, humtuliza mke, mme, mchumba, hawara au mtu yoyote umpendae na kumfanya akutimizie chochotekile unachokitaka kutoka kwake na kumfunga asiwe na mtu yoyote zaidi yako.

WASILIANA NA DR CHIPUPA NAPATIKANA DAR ES SALAAM KUMBUKA HUDUMAHII ITAKUFIKIA POPOTE ULIPO  0759208637 / 0622344969

Tundu Lissu Kudai Stahiki zake Mahakamani

0
0
Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu, amesema atalifikisha Mahakama Kuu suala la gharama za matibabu yake ili iweze kutoa tafsiri sahihi baada ya Bunge kushindwa kumlipia.

Lissu aliyasema hayo kupitia andiko lake lililoanza kusambaa jana akiwa anatimiza mwaka mmoja tangu alipopigwa risasi Septemba 7, mwaka jana eneo la nyumbani kwake jijini Dodoma.

Katika andiko  lake hilo ambalo pia  ameelezea tukio zima la kujeruhiwa kwake,  mwenendo wa matibabu katika kipindi chote cha mwaka mmoja na kile alichodai kiini cha kuumizwa kwake, kuhusu suala la matibabu ambalo amelifafanua kwa kina  Lissu ametoa sababu za kimazingira na kisheria  ambazo ndio msingi wa yeye kuamua kulifikisha suala hilo mahakamani.

“Kwa upande wetu, njia pekee iliyobaki sasa ni kulipeleka suala hili mahakamani ili Mahakama Kuu itoe tafsiri sahihi ya jambo hili. Maandalizi ya kwenda mahakamani yanaendelea,” alisema Lissu.

Akirejea mvutano kuhusu Bunge kukataa kulipia gharama za matibabu yake,  Lissu aliuelezea kama ‘mgogoro wa kutengenezwa’ ambao katikati yake yumo Spika wa Bunge, Job Ndugai na Katibu wa chombo hicho, Steven Kagaigai ambao wamekuwa wakidai alikiuka taratibu za matibabu ya wabunge kwa kupelekwa Nairobi badala ya Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwanza.

Katika hilo Lissu alisema utaratibu huo hautambuliki kisheria jambo linaloonekana Spika Ndugai amekubali kuingiliwa na kupokwa madaraka ya Bunge kuendesha shughuli zake kama mhimili huru wa dola.

Akifafanua kuhusu sheria hiyo inayohusika na matibabu ya Wabunge alisema ni Sheria ya Uendeshaji wa Bunge ya mwaka  2008 ambayo inaeleza kwa kifupi kwamba kila mbunge atakuwa na haki ya kutibiwa ndani au nje ya Tanzania kwa gharama ya Bunge.

“Utaratibu wa kupata kibali cha Muhimbili, au cha Katibu Mkuu Afya, au cha Rais haupo kwenye Sheria hiyo.

Lissu alisema kama utaratibu huo ungekuwepo kisheria, bado ulikuwa haukidhi na usingeweza kukidhi mahitaji ya dharura iliyotokana na kushambuliwa kwake.

“Kwa majeraha niliyokuwa nayo na kwa hali ya kiusalama iliyokuwepo, hakukuwa na uhakika kwamba nikipelekwa Muhimbili nitakuwa salama dhidi ya watu walionishambulia.

“Na hakukuwa na muda mrefu wa kusubiri hali itulie ndio taratibu zinazosemwa zifuatwe. Ilibidi uamuzi ufanywe haraka ili nikapatiwe matibabu katika hali ya dharura ya kiafya na kiusalama iliyokuwepo”, linasomeka andiko lake hilo.

Alisema uamuzi na taratibu zote za kumpeleka hospitali ya Nairobi haukufanywa na uongozi wa juu wa Chadema peke yao bali ulihusisha viongozi wengine wa Bunge na Serikali  na hivyo kuhoji utaratibu aliokiukwa.

Alisema baada ya kukimbizwa Hospitali ya Mkoa wa Dodoma kilifanyika kikao kilichowahusisha viongozi wa Chadema, Bunge na Serikali kuhusu hatua za kuchukua.

Alisema upande wa Chadema uliongozwa na Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, na  Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe na wabunge kadhaa na upande wa Bunge uliongozwa na  Spika Ndugai, Naibu Spika Tulia Akson na Katibu wa Bunge wakati huo, Dk. Thomas Kashililah wakati upande wa serikali alikuwepo Waziri wa Afya Ummy Mwalimu, Katibu Mkuu wake Dk. Ulisubisya Mpoki na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba.

“Kikao hicho ndicho kilichoamua nipelekwe Nairobi. Ndio maana katika msafara ulionipeleka Nairobi Hospitali, alikuwepo pia Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dodoma”, alieleza Lissu.

Kutokana na hayo alisema ndio maana ndege iliyompeleka Nairobi iliruhusiwa kuruka Uwanja wa Ndege wa Dodoma saa sita usiku.

“Ningekuwa nimepelekwa Nairobi kwa utaratibu binafsi, kama inavyodaiwa sasa, nisingesindikizwa na Mganga Mkuu wa Mkoa na wala Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA) isingeruhusu ndege kuondoka Dodoma saa sita usiku.

“Na wala maafisa wa uhamiaji wasingegonga muhuri passport zetu na kuturuhusu kutoka nje ya nchi”, alieleza.

Alisema baada ya kuwa ameshapokelewa hospitali ya Nairobi na maisha yake  kuokolewa, Spika Ndugai na Katibu wa Bunge Kashililah walikutana na ndugu zake kwenye Ofisi ya Bunge Dar es salaam  na kuwashauri waandike barua rasmi ya maombi ili Bunge liweze kutoa fedha za matibabu yangu.

Lissu alieleza kuwa Waziri wa Afya, Ummy naye alishauri hivyo hivyo, tena hadharani kwenye mkutano na wandishi habari.

Alieleza kuwa Ummy alisisitiza jambo hilo kwa kutoa mfano wa Spika wa zamani wa Bunge, marehemu Samuel Sitta, ambaye inasemekana aliomba msaada wa kutibiwa na Bunge wakati hakuwa Mbunge tena, na tayari alikuwa hospitalini London, Uingereza.

“Barua zikaandikwa na ndugu zangu kama walivyoelekezwa na uongozi wa Bunge. Lakini mara Katibu wa Bunge Kashililah akaondolewa madarakani na Rais Magufuli, na Steven Kagaigai akateuliwa kushika nafasi hiyo”, alieleza.

Alieleza kuwa inavyoonekana Kagaigai alikwenda na maelekezo ya yeye kutopewa fedha yoyote ya matibabu na Bunge.

Rais Magufuli Akerwa na Ugomvi wa DC na Mkuu wa Mkoa

0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli amekemea tabia ya wakuu wa wilaya na mikoa kugombana wakati wanapotumikia wananchi.

Ameyasema hayo wakati akihutubia wananchi wa wilaya ya Tarime mkoani Mara wakati wa ziara yake ya kikazi, ambapo kuna mgogoro mkubwa kati ya DC wa wilaya Glorius Luoga na mwenyekiti wa CCM wa wilaya hiyo Daud Ngicho na mkuu wa mkoa huo Adam Malima.

Rais Dkt. Magufuli ameonyesha kukerwa na misiguano ya viongozi wa mkoa wa Mara unaofanya hata miradi mbalimbali ya maendeleo kukwama kufuatia DC Luoga na RC Malima kutofautiana.

“Kwanini mnagombana, wewe DC uko chini ya RC Malima, umheshimu na si kugombana kila wakati mpaka shughuli za maendeleo zinakwama,”amesema JPM

Hivi karibuni  Rais pia alikemea mgogoro kati ya mkuu wa wilaya ya Chemba na Naibu waziri wa Fedha, Dkt. Ashatu Kijaji na viongozi wa wilaya hiyo wakati wa kuzindua barabara inayounganisha Afrika.

Waliofariki Kwa Ajali Jijini Mbeya Wafika 15

0
0
Idadi ya watu waliofariki dunia katika ajali iliyohusisha magari matano eneo la Mlima Igawilo jijini Mbeya imefikia 15.

 Muuguzi Mkuu wa Hospitali  ya Rufaa Kanda ya Mbeya, Dk Petro Seme, alisema jana walipokea majeruhi 15 wa ajali hiyo lakini wawili walifariki wakati wakiendelea kupatiwa matibabu.

Alisema majeruhi wanne walitibiwa na kuruhisiwa na wengine wanaendelea na matibabu.

“Pia tulipokea maiti 13, lakini majeruhi wawili walifariki dunia hapa hospitali. Majeruhi wengine wawili waliopo hapa wapo ICU (chumba cha uangalizi maalum)  na mmoja hali yake si nzuri.” amesema

Ajali hiyo ilitokea jana saa 11 jioni ikihusisha magari mawili yaliyokuwa yamebeba mafuta, mengine mawili yalikuwa yamebeba viazi na ndizi pamoja na daladala iliyokuwa imebeba abiria kutoka Igoma kwenda Mbeya mjini.

Makontena ya Makonda Yakosa Wateja kwa Mara ya Tatu

0
0
Mamlaka ya Mapato nchini (TRA), leo imefanya mnada tena kwa mara ya tatu mfululizo wa makontena 20 yaliyoingizwa nchini na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, lakini yameshindwa kuuzika kutokana na wateja kushindwa kufika bei.

Mnada huo umefanyika bandari kavu ya Dar es salaam (DICB), ikiwa ni mwendelezo wa minada miwili iliyofanyika huko nyuma lakini hakuna hata kontena moja ambalo limefanikiwa kununuliwa.

TRA imepanga bei ya shilingi milioni 60 kwa kila kontena lakini wateja wameshindwa kufikia bei hiyo, wengi wakifika shilingi milioni 20 hadi 30.

Kwa upande wake Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya udalali ya Yono, Scolastica Kivela amesema wao kama madalali wanafanya jukumu lao kwa mujibu wa maelekezo waliyopewa na TRA hivyo hawawezi kupunguza bei bila maelekezo ya mamlaka ya mapato.

“Kila mnada wateja wanajitokeza lakini wanaishia bei zilezile za milioni 20 mpaka 30 kwahiyo mzigo huu wa samani haununuliki labda mpaka tupate maelekezo mapya kutoka TRA'', amesema.

Rais Magufuli Asema Mkuu wa mkoa wa Simiyu Antony Mtaka Ndo Anayeongoza Kwa Kuchapa Kazi Vizuri Tanzania Nzima

0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, amemtaja mkuu wa mkoa wa Simiyu Mh. Anthony Mtaka, kuwa ndiye mkuu wa mkoa kinara anayepiga kazi na kwamba hana mfano licha ya kupuuzwa kabla  hajamteua.

Hayo ameyasema leo mkoani Simiyu wakati akihutubia wananchi wa mkoa huo kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika jioni hii ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya siku 7 katika mikoa ya kanda ya ziwa.

Rais Magufuli ameeleza kuwa, wakati anajaribu kutafuta wakuu wa Wilaya na wakuu wa mikoa aliambiwa na vyombo vyake kuwa Mtaka hafai hata U-DC lakini yeye akaamua kumteua kuwa mkuu wa mkoa kwasababu anajua watu wazuri huwa wanapingwa vita sana.

''Nilipotaka kumteua niliuliza vyombo vyangu nikaambiwa hafai kabisa lakini nimeuliza ripoti ya Wakuu wa Mikoa wanaofanya kazi vizuri, wakaniletea Mtaka ndio namba moja na namba mbili ni yeye kwa kifupi hana mfano'', amesema.

Aidha Rais Magufuli ambaye atakamilisha ziara yake katika mikoa hiyo siku ya Jumatatu Septemba 10, 2018 amemtaka Mtaka kuendelea kuchapa kazi wala asiyumbishwe kwasababu yeye anajua watu wanaopigwa vita na kuwekewa maneno ya ajabu ndio wazuri.

Mavunde Aipongeza Kampuni Ya Mafuta Puma

0
0
NAIBU Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Ajira na Wenye Ulemavu, Antony Mavunde, ameipongeza Kampuni ya Mafuta ya Puma Tanzania, kwa kuunga mkono juhudi za serikali kwa kujali usalama wa wanafunzi kwa kutoa mafunzo kwa wanafunzi.

Kauli hiyo ameitoa leo jijini Dar es Salaam wakati akifunga mafunzo ya uchoraji kwa wanafunzi wa shule za msingi za mkoa huo.
 
Amesema tangu mwaka 2013, kampuni hiyo ilipoanzisha kampeni ya usalama barabarani ambayo imekuwa na lengo la kupunguza ajali za usalama barabani na sasa mafanikio yanaonekana.

“Tangu ilipozinduliwa kampeni hii tunaona kuna mafanikio na katika awamu ya kwanza ya mafunzo haya wanafunzi 9,152, wamepewa mafunzo usalama barabarani ikiwamo kushiriki katika michoro hongereni sana Puma.
 
“….na la kufurahisha zaidi ni hatua ya kuzishirikisha na shule za wanafunzi wenye ulemavu ikiwamo ya shule mojawapo ya Mkoani Ruvuma,” amesema Mavunde.

Awali Meneja Mkuu wa Puma Tanzania, Philippe Corsaletti, alisema mafunzo hayo ni mwendelezo wa kuwaelimisha wanafunzi kuhusu usalama barabarani tangu mwaka 2013 ilipozinduliwa kampeni hiyo.

“Tangu ilipoanza kampeni hii tumetoa mafunzo kwa wanafunzi wapatao 68,000 katika shule 63 za mikoa ya Dar es Salaam, Arusha, Geita, Kilimanjaro na Ruvuma,” amesema
 
Alisema madhumuni ya kuwahusisha wanafunzi wa shule za msingi imetokana na kuamini kwamba mafunzo ya salama barabarani yanatakiwa kutolewa kwa watto wadogo ili waweze kukua wakiwa na uelewa kuhusu usalama barabarani.

“Tumeamua kuweka mkazo katika mafunzo haya kwa wanafunzi tukielewa kuwa wanakabiliwa na hatari nyingi za barabarani.

Na kuyafanya mafunzo haya kuwa kipaumbele chetu cha kwanza,” amesema Philippe
 
Meneja huyo alisema kuwa kwa mwaka huu wamefundisha wanafunzi 9,152 wa shule za msingi 16 za Mkoa wa Dar es Salaam na Ruvuma pamoja na kuendesha mafunzo hayo kwa shule za walemavu na kuwa kampuni ya kwanza ya mafuta kuendesha mafunzo hayo.

Katika mashindano hayo mshindi wa kwanza aliibuka mwanafunzi Francisco Salvatory wa Shule ya Msingi Upanga ambaye alinyakua kitita cha Sh 500,000 wa pili ni Magreth Andrew wa Shule ya Msingi Maktaba, ambaye alivyakua kitita cha Sh 300,000 na wa tatu ni pia alikuwa mwanafunzi wa shule ya Msingi Upanga ambaye alizwadiwa Sh 150,000.
Mwisho
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images