SERIKALI inaendelea na jitihada mbalimbali za uboreshaji wa maji safi na salama ili maji yanayotoka bombani yaweze kunywewa moja kwa moja bila kuchemsha.
Taarifa hiyo imetolewa bungeni leo na Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Maria Hewa (CCM).
Katika swali lake Maria Hewa alitaka kujua lini wananchi wataruhusiwa kunywa maji ya bomba
↧