Wakazi
wa kijiji cha Ayalabe kata ya Ganako wilaya ya Karatu wameiomba
serikali isikie kilio chao kwa kuchukua hatua kwa watendaji wa
halmashauri waliohusika katika kuuza hekari 30 za ardhi ya shule ya
msingi Ayalabe pamoja na kuuza mlima pekee wa kijiji kwa mwekezaji huku
wakigawana zaidi ya shilingi milioni 500 za chama cha ushirika cha
kijiji hicho bila kuwashirikisha wananchi.
↧