ALIYEKUWA mgombea nafasi ya Uenyekiti wa Serikali ya kitongoji cha Idodomiya kijiji cha Kanoga na mfanyakazi wake kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wilaya ya Kaliua mkoani Tabora, wameuawa kwa kupigwa kwa mapanga.
Katibu wa chama hicho Wilaya, Rajabu Hamisi alisema kuwa mauaji hayo yalitokea juzi nyumbani kwake katika kijiji cha Kanoga wilayani Kaliua mkoani hapa.
↧