Watu saba wamefariki Igunga, mkoani Tabora, ambapo wengi
wamejeruhiwa baada ya basi la Mohammed Trans lililokuwa likitoka Mwanza
kuelekea Dar es Salaam, kukatika 'steering power' na kuacha njia na
kisha kupinduka.
Basi hilo limepinduka jana majira ya saa nane mchana, ambapo maiti
na majeruhi walipelekwa katika Hospitali ya Wilaya ya Igunga.
↧