Chama cha Mapinduzi CCM kimesema hakioni sababu ya suala la waliohusika
kusababisha dosari zilizojitokeza wakati wa zoezi la upigaji kura
kuundiwa tume au kuchunguzwa wakati wanajulikana.
Chama
hicho kimesema kuwa badala ya hatua hizo, watu hao wachukuliwe hatua,
huku kikieleza kusikitishwa na mapungufu yaliyojitokeza ambayo wamedai
yalitokana na uzembe wa watendaji wachache.
↧