Kundi la watu wanaodhaniwa ni majambazi, wamevamia na kupora fedha taslimu na vitu mbalimbali katika Kanisa Katoliki la Kilema, Jimbo la Moshi Vijijini mkoani Kilimanjaro.
Tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia Desemba 14, mwaka huu, ambapo watu hao wakiwa na vifaa maalumu vya kuvunja milango, walivunja lango kuu la kanisa hilo, kuvunja sanduku la sadaka na kupora vifaa vya kufanyia ibada
↧