Mchakato wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wa kupata wagombea katika nafasi mbalimbali unaanza leo ambapo mikutano ya ngazi ya wilaya/majimbo itapiga kura za mapendekezo kati ya leo na kesho.
Upigaji wa kura unaoanza leo unahusisha kura za maoni za kuwapata wagombea katika nafasi za ubunge, uwakilishi, udiwani (Tanzania Bara) na usheha kwenye wadi visiwani Zanzibar.
Baada ya mikutano hiyo, Julai 30 kutakuwa na vikao vya kamati za siasa za majimbo kuwajadili wagombea na kutoa mapendekezo kwenye kamati za siasa za wilaya.