Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all articles
Browse latest Browse all 45270

TAKUKURU Yawaonya Wafanyabiashara Kufadhili Gharama za Uchaguzi za Wagombea

$
0
0
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), imewataka wafanyabiashara kujiepusha na vitendo vya rushwa kwa dhana ya kufadhili gharama za uchaguzi ndani ya vyama vya siasa.


Hayo yameelezwa na Brigedia Jenerali, John Mbungo, Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, wakati anafungua warsha ya wadau wa uchaguzi, kujadili namna ya kudhibiti vitendo vya rushwa kwenye Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2020, jijini Dar es Salaam.

Brigedia Jenerali Mbungo alisema gharama za uendeshaji wa uchaguzi ndiyo chanzo cha vitendo vya rushwa na baadhi ya wafanyabiashara hutumia mwaya huo kujinufaisha baada ya wagombea waliowafadhili, kupata uongozi serikalini.

"Mara nyingi chanzo kikuu cha rushwa katika uchaguzi ni gharama za uchaguzi, jambo hili husababisha wagombea au watia nia kutumia ushawishi pamoja na nguvu ya fedha ili kurubuni wapiga kura wawachague, mgombea au wagombea wenye uwezo wa kifedha, hutumia kigezo hicho cha fedha kuwarubuni wananchi ili wawachague," alisema Brigedia Mbungo.

Brigedia Jenerali Mbungo alisema vitendo hivyo vinasababisha viongozi kufanya uamuzi wa kisera wenye maslahi kwa watu wachache.

Alisema TAKUKURU iliamua kukutana na wadau wa uchaguzi kwa lengo la kuunga mkono azma ya Rais John Magufuli ya kutaka uchaguzi huo ufafanyike kwa haki, huru na usawa.

Alisema Juni 26 mwaka huu wakati Rais Magufuli anavunja shughuli za Bunge la 11, alisisitiza wadau wa uchaguzi kuepuka vitendo vya rushwa katika uchaguzi huo.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 45270

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>