Mtia nia wa Urais kupitia tiketi ya Chama cha Demokrasia na maendeleo Chadema ambaye pia ni mwenyekiti wa kanda ya kati Lazaro Nyalandu amesema chama hicho kitaibuka na ushindi mkubwa katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Octoba mwaka huu kwakuwa kimetengeneza muunganiko mzuri baina ya mgombea Urais,Ubunge,Udiwani na wananchi.
Kauli hiyo aliitoa jana baada ya kufanyika kwa mdahalo wa kuwachuja watia nia wa nafasi ya ubunge jimbo la Njombe mjini ambapo ametumia fursa hiyo pia kuomba udhamini kwa wajumbe ili kupeperusha bendera ya nafasi ya Urais
Nyalandu alisema kwa kuwa Chadema kimezidi kufanya mambo yenye mvuto kwa umma, wana imani kitaibuka kidedea katika nafasi mbalimbali za uongozi katika uchaguzi mkuu.
Nyalandu alisema kwa kuwa Chadema kimezidi kufanya mambo yenye mvuto kwa umma, wana imani kitaibuka kidedea katika nafasi mbalimbali za uongozi katika uchaguzi mkuu.
“Kama unagombea Udiwani,Ubunge naomba ujiandae kufanya kampeni tena ufanye kampeni kweli kweli kama unategemea utakuja kutangazwa unapoteza muda wako hata tangazwa mtu atatangazwa mshindi”alisema Nyalandu
Awali watia nia wakimwaga sera katika mdahalo huo ulioongozwa na kauli mbiu ya "Njombe Tuitakayo" Akiwemo Sigrada Mligo, Emmanuel Masonga na Rose Mayemba wameweka bayana vipao mbele vyao endapo watapata ridhaa ya chama kugombea.
“Chadema ndicho chama ambacho kina wabunge wenye hoja thabiti na niwachache lakini wanapambana”Alisema Lusia Mlowe aliyekuwa mbunge wa Viti Maalumu mkoa wa Njombe
Katika uchaguzi wa kura za maoni ushindani mkubwa umekuwa kwa mgombea wa 2015 wa jimbo hilo Emmanuel Masonga pamoja na Rose Mayemba lakini chaguo la wanachama likamwangukia Emmanuel Masonga ambaye ametoa shukrani kwa wajumbe kumchagua kupeperusha bendera ya chama kwa nafasi ya ubunge katika uchaguzi mkuu na kuahidi kutokiangusha chama hicho.