Quantcast
Channel: MPEKUZI

TICTS yatajwa kuwa chanzo cha matatizo kwa wafanyabiashara bandari ya Dar

$
0
0


Na Kidawa Hamza, Dar
Kushindwa kujiendesha kwa ufanisi kwa Kampuni ya Kimataifa ya Kuhudumia Makasha (TICTS) kumesababisha msongamano wa makasha hayo bandari ya Dar es Salaam na kuathiri shughuli muhimu za kiuchumi nchini.

Mojawapo ya maeneo yaliyoathiriwa ni usafirishaji wa zao la parachichi ambapo wafanyabiashara wa zao hilo wanakimbia kusafirisha kupitia bandari ya Dar es Salaam na badala yake hutumia bandari za nchi jirani.

Kusuasua kwa TICTS, kumeongeza gharama ya kusafirisha zao la parachini  nchini na kulikosesha Taifa mapato ya matrilioni ya fedha, kutokana na wafanyabiashara kuikwepa bandari wakikimbilia bandari ya Mombasa, Afrika Kusini na Namibia zenye ufanisi zaidi.

Kutokana na udhaifu wa TICTS, gharama za kuhudumia shehena na makasha zinazopita bandarini zimeongezeka na hivyo kufanya wawekezaji ambao walikua na nia ya kuja kuweza nchi kughahiri na kwenda nchi nyingine.

Kwa mujibu wa takwimu, Tanzania inashika nafasi ya tatu kwa uzalishaji wa parachichi ikitanguliwa na Afrika Kusini na Kenya, lakini inaweza kuwa ya kwanza endapo mageuzi yatafanyika na kuipa tenda kampuni nyingine itakayo fanya kazi kwa ufanisi bandarini ili kuwapa ari wakulima kulima kwa wingi zao hilo.


Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo July 23

Rais Samia Akutana Na Kuzungumza Na Rais Wa Burundi Ndayishimiye Ikulu Jijini Arusha

$
0
0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mwenyekiti Mpya wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) ambae pia ni Rais wa Burundi Mhe. Évariste Ndayishimiye alipowasili Ikulu ndogo ya Arusha

Waziri Mkuu Akagua Maandalizi Ya Siku Ya Mashujaa Dodoma

$
0
0

 


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan atakuwa Mgeni Rasmi katika maadhimisho ya siku ya Mashujaa, yatakayofanyika kitaifa Julai 25, 2022 Mkoani Dodoma.

Amesema hayo leo (Jumamosi, Julai 23, 2022), baada ya kukagua maandalizi ya maadhimisho hayo, katika viwanja vya Mashujaa Mkoani Dodoma. Waziri Mkuu amesema ameridhishwa na maandilizi yaliyofanywa na kamati ya maadhimisho kitaifa kwa kushirikiana na vyombo vya Ulinzi na Usalama.

“Sherehe hii itafanyika kitaifa mkoani Dodoma na itaongozwa na Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dkt. Hussein Ali Mwinyi, Viongozi wastaafu na viongozi wengine wa kitaifa.”

Waziri Mkuu amesema, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan aliridhia maadhimisho hayo yafanyike kitaifa mkoani Dodoma, lakini akaelekeza yafanyike nchi nzima kwa Wakuu wa Mikoa kuadhimisha siku hiyo kwa kwenda kwenye maeneo muhimu ya kumbukumbu kwenye mikoa yao.

“Kamati ya maadhimisho imefanya kazi yake vizuri sana kwa kushirikiana na vyombo vyote vya Ulinzi na Usalama, eneo linafafana na tukio lenyewe, lakini maandalizi ya vikundi mbalimbali ikiwepo vyombo vya ulinzi na usalama vimeleta askari kwa ajili ya gwaride, na mwaka huu  Jeshi la Uhamiaji limeanza kushiriki kikamilifu kwenye gwaride kuanzia kwenye tukio hili muhimu la mashujaa”

Aidha, Waziri Mkuu amevipongeza vyombo vya habari kwa namna ambavyo vimekuwa vikishiriki katika kutoa hamasa kwa wananchi kushiriki katika matukio mbalimbali ya kitaifa na kwamba Serikali inathamini mchango huo.

“Serikali inawashukuru sana wananchi kwa namna ambavyo wanajitokeza katika matukio haya ya kitaifa na kujanza viwanja, tunaamini pia Julai 25 watajitokeza kwa wingi.”

Serikali Yatoa Maelekezo Hatua Ya Kudhibiti Ajali Barabarani

$
0
0


 Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Baraza la Taifa la Usalama Barabarani imetoa maelekezo yatayosaidia kudhibiti ajali za barabarani nchini. Serikali imesema kuwa hairidhishwi na takwimu za ajali barabarani zilizotokea hivi karibuni na kutoa maelekezo matano kwa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, LATRA pamoja na watumiaji vyombo vya moto na abiria kwa ujumla.

Akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi na Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Jumanne Sagini amesema kuwa Serikali ambayo inadhamana ya kulinda usalama wa raia na mali zao isingependa kuona matukio ya vifo na uharibifu wa mali za raia yakiendelea.

Naibu Waziri Sagini alielekeza LATRA na Kikosi cha Usalama Barabarani kupitia idadi ya magari madogo yaliyopewa leseni, kuendelea kufanya operesheni za kukamata magari yanayokiuka Sheria za Barabarani, kutoa elimu kwa abiria na wafanyabiashara wenye uwezo kuomba leseni za usafirishaji wa abiria kutoka LATRA kwenye maeneo ya uhitaji yakiwemo Mikoa ya Simiyu, Kagera, Kigoma, Mara na Geita.

“Serikali ambayo ina dhamana ya kulinda Usalama wa Raia na mali zao isingependa kuona matukio ya vifo na uharibifu wa mali za raia wake yakiendelea. Ni kwa msingi huo, tumemsikia mara kadhaa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akikemea na kulitaka Jeshi la Polisi kuchukua hatua madhubuti kudhibiti ajali za barabarani.

Naibu Waziri Sagini ameyasema hayo leo kwenye mkutano na waandishi wa Habari kuzungumzia masuala ya usalama barabarani uliofanyika jijini Dar es Salaam.

Aidha ameipongeza Kamati ya Usalama ya Mkoa wa Simiyu chini ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. David Kafulila kwa kuchukua hatua za kudhibiti matumizi ya magari yaliyosajiliwa kama teksi yanayokukiuka Sheria na kubeba abiria wengi na kwa masafa marefu.

“ Kamati hiyo ilichukua hatua hizo baada ya kujiridhisha kuwa magari hayo yamekuwa yakikiuka kwa kiwango kikubwa Sheria ya Usalama barabarani ikiwemo kubeba abiria wengi kuliko uwezo wa gari hizo, kuendesha magari kwa mwendo kasi kuliko inavyoruhusiwa” alisema.

Hatahivyo aliagiza Jeshi la Polisi, Kikosi cha Usalama Barabarani kuchukua hatua kwa askari Polisi mkoani Simiyu na nchini kwa ujumla watakaobainika wanamiliki tesksi hizo.

Habari Zilizopo Katika mgazeti ya Leo july 25

Ummy Azindua Bodi Ya Wadhamini MSD

$
0
0


WAZIRI wa Afya, Mhe.Ummy Mwalimu  Julai 25,2022 amezindua Bodi Mpya ya Wadhamini ya Bohari ya Dawa (MSD) ambapo ameiagiza kuhakikisha inaendelea kufanya kazi kwa weledi.

Akizungumza wakati akizindua Bodi hiyo leo katika Ofisi za MSD Jijini Dar es Salaam amesema bodi hiyo inatakiwa ifanye kazi kuzingatia sheria huku wakisimamia uwekaji wa mifumo mizuri ya usimamizi na usambazaji wa dawa nchini.

Waziri Ummy ameipa jukumu la kuhakikisha inasimamia suala la kupangua safu ya uongozi pamoja na wafanyakazi wa MSD ili utendaji kazi uimarike.

Amesema kuwa MSD ilifanya kazi vizuri na kuaminiwa na nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), hivyo ameagiza kurudishwa kwa mifumo ya TEHAMA iliyosaidia kudhibiti mianya ya ubadhirifu ndani ya taasisi hiyo.

“Watu wanategemea kuona ufanisi wake,sisi tutawapima bodi kwa utendaji wenu kama dawa zinawafikia wananchi maeneo yanayotakiwa.Ila pia muangalia kama ni kuifumua nyie mtaangalia tunachotaka ni kuona mabadiliko ya kiutendaji ndani ya MSD,”Amesema Waziri Ummy.

Nae Mwenyekiti mpya wa Bodi ya Wadhamini ya Bohari ya Dawa Tanzania (MSD), Bi.Rosemary Silaa ameahidi bodi hiyo mpya kuwa bodi hiyo inaanza kazi rasmi ya kuisuka upya MSD.

Ajali Yaua Watu 10 Mtwara

$
0
0


Watu kumi wamefariki dunia katika ajali ya gari iliyotolea mapema hii leo katika eneo la Mjimwema manispaa ya Mtwara – Mikindani mkoani Mtwara.

Taarifa za awali kutoka mkoani Mtwara zinaeleza kuwa miongoni mwa watu waliofariki dunia ni wanafunzi nane wa shule ya msingi ya King David,
dereva wa basi dogo la shule pamoja na mama mmoja anayedaiwa kuwa aliomba lifti kwenye basi hilo.

Wanafunzi wengine 19 wamejeruhiwa katika ajali hiyo, huku watano hali zao zikielezwa kuwa ni mbaya.

Habari zaidi zinaeleza kuwa, chanzo cha ajali hiyo huenda ni kushindwa kufanya kazi vizuri kwa mfumo wa breki wa basi hilo la shule.


Tamko La Serikali Kuhusu Tishio La Mgomo Wa Madereva

$
0
0


Ndugu Wanahabari; Kama mnavyokumbuka mnamo tarehe 22 Julai, 2022 Serikali ilitoa taarifa kwa Vyombo vya Habari kuhusu hatua zilizochukuliwa katika kushughulikia Hoja na Malalamiko yaliyowasilishwa na Viongozi wa Vyama vya Wafanyakazi Madereva na Wamiliki wa Vyombo vya Usafirishaji nchini.

Kufuatia kutolewa kwa taarifa hiyo, wapo baadhi ya Madereva ambao wameipokea kwa mtazamo tofauti.

Kutokana na hali hiyo, wamekuwa wakipotosha taarifa hiyo na kuchochea ama kuhamasisha Madereva wenzao kugoma.

Uchochezi wa mgomo wao umejikita katika viwango vya posho ambavyo Madereva, Wamiliki wa Vyombo vya Usafiri na Serikeli waliafikiana katika vikao vya majadiliano.

Ndugu Wanahabari; Viwango walivyokubaliana ni viwango vya chini vya posho za
safari (Minimum allowances) ambapo waajiri hawaruhusiwi kulipa chini ya viwango
hivyo.

Kwa wale Waajiri ambao walikuwa wanalipa viwango ambavyo viko juu ya viwango vya chini vya posho za safari vilivyowekwa, hawaruhusiwi kushusha viwango hivyo kwani kufanya hivyo ni kosa kwa mujibu wa Sheria.

Ndugu Wanahabari; Serikali kwa kutambua umuhimu wa sekta ya usafirishaji kwa uchumi wa nchi, inasisitiza kuwa nafasi ya majadiliano bado ipo wazi na hivyo Wafanyakazi Madereva ambao wana hoja na malalamiko zaidi ya yale yaliyofanyiwa kazi, wayawasilishe rasmi katika mamlaka zinazohusika ili yaweze kupatiwa ufumbuzi.

Ndugu Wanahabari; Ninawasihi Wafanyakazi Madereva wapokee kwa mtazamo chanya
taarifa ya Serikali kuhusu hatua zilizochukuliwa katika kushughulikia Hoja na Malalamiko yaliyowasilishwa na Vyama vyao na Wamiliki wa Vyombo vya Usafirishaji.

Ninawasihi Wafanyakazi Madereva wote kuendelea kutekeleza majukumu yao kama kawaida. Natoa rai
kwa makundi yanayojihusisha kuchochea migomo ya Madereva kuacha mara moja, kwanikufanya hivyo ni kukiuka Sheria.

Hivyo, Serikali haitasita kuchukua hatua stahiki kwa wale wote watakaoendelea kuchochea migomo ya Madereva.
IMETOLEWA NA
Prof. Joyce Lazaro Ndalichako (MB)
WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU
(KAZI, VIJANA, AJIRA NA WENYE ULEMAVU)

Majeshi ya Ukraine yashambulia daraja la kimkakati litumiwalo na Urusi

$
0
0


Jeshi la Ukraine limefanya mashambulizi katika daraja moja la kimkakati linalotumiwa na Urusi kwa ajili ya kuyasambazia majeshi yake yaliyoko kusini mwa nchi hiyo silaha. 

Haya yamefanyika wakati ambapo Urusi imeshambulia maeneo kadhaa nchini Ukraine kwa maroketi na makombora. 

Naibu mkuu wa serikali ya Kherson aliyeteuliwa na Urusi Kirill Stremousov amesema jeshi la Ukraine limeishambulia daraja la Antonivskyi katika mto Dnieper. 

Stremousov amesema daraja hilo halikuanguka ila lina mashimo yanayowia magari vigumu kupita. 

Ameongeza kwamba majeshi ya Ukraine yametumia silaha za kutoka Marekani za HIMARS kurusha maroketi. 

 Mapema katika vita hivyo, majeshi ya Urusi yaliliteka kwa haraka eneo la Kherson lililoko kaskazini mwa rais ya Crimea ambayo Urusi iliiteka katika uvamizi wa mwaka 2014.

Dkt. Magembe Atoa Siku Mbili Kuwasilisha Taarifa Ya Ukaguzi Wa Bidhaa Za Tiba

$
0
0

 


OR - TAMISEMI

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Afya), Dkt. Grace Magembe ametoa siku mbili kwa Mganga Mkuu wa hospitali ya Mtwara kuwasilisha taarifa ya ukaguzi wa dawa , vitendanishi pamoja na vifaa tiba katika Kituo cha Afya cha Ufukoni kilichopo katika Manispaa ya Mtwara Mikindani.
 
 Agizo hilo limetolewa tarehe 26 Julai, baada ya Dkt. Magembe kutembelea kituo hicho na kubaini mapungufu katika leja za mapokezi na matumizi ya dawa , vifaa tiba na vitendanishi vya maabara.
 
Pia amemtaka kushirikiana na mkaguzi wa ndani wa Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara Mikindani katika kutekeleza ukaguzi huo.
 
“ Haiwezekani dawa zitumike bila rekodi, TAMISEMI ilishatoa maelekezo na nyenzo ya ukaguzi wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi, ni swala la utekelezaji tu,” amesema Dkt. Magembe
 
Pia amewaekekeza Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mtwara na wa Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara kufanya mabadiliko ya uongozi katika Kituo cha Afya Ufukoni ikiwemo kumpangia majukumu mengine Mganga Mfawidhi wa kituo hicho. 
 
Aidha, Dkt. Magembe ametumia fursa hiyo kuwahimiza Wakurugenzi wa Halmashauri za Mtwara na Nanyamba kuongeza kasi ya ujenzi unaoendelea katika Hospitali za Halmashauri.

Pia amewataka kuhakikisha wanatenga fedha za kumalizia kazi kwa haraka na ubora ili huduma zianze kutolewa.

Tanzania Na Kituo Cha Kudhibiti Magonjwa Nchini Marekani (CDC ) Kuendelea Kushirikiana

$
0
0

 


Na. WAF Dar es Salaam

Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu amesema kuwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano Tanzania chini ya Rais Samia Suluhu Hassan itaendelea kushirikiana na Kituo cha Kudhibiti Magonjwa kutoka Marekani katika mapambano dhidi ya magonjwa mbalimbali.

Waziri Unmy amesema hayo mara baada kukutana na Mkurugenzi wa Kituo cha Udhibiti wa Magonjwa cha Marekani (CDC) Dkt. Rochelle Walensky na kufanya nae mazungumzo.

Waziri Ummy ameishukuru CDC kwa kuendelea kushirikiana na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuanzia Mwaka 2001 katika kudhibiti magonjwa ya kuambukiza hususani ugonjwa wa UKIMWI, Kifua Kikuu na Malaria.

“Tumeshirikiana na CDC katika maneo mbalimbali yakiwemo; kuimarisha huduma za ufuatiliaji wa magonjwa, huduma Za maabara, kuwajengea uwezo wataalam kupitia mafunzo ya muda mfupi na mrefu na kuanzisha mfumo wa kidijitali katika kutoa mafunzo na kutafasiri majibu ya uchunguzi unaofanywa katika vituo vya ngazi ya msingi” amesema Waziri Ummy.

Aidha Mhe Ummy alimfahamisha Dkt Walensky kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan, ameweka kipaumbele katika masuala ya usalama wa afya hususani katika kujikinga, kufanya utambuzi na kukabiliana na mlipuko wa magonjwa na majanga.

Kuhusu UVIKO-19 Mhe Ummy ameipongeza CDC kwa kushirikiana na Serikali katika kukabiliana na mlipuko wa UVIKO-19 ikiwemo kuchangia katika kuongeza kasi ya uchanjaji wa chanjo ya UVIKO-19.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa kituo cha kudhibiti magonjwa cha Marekani (CDC) Dkt. Rochelle Walensky Ameishukuru Serikali kupitia Wizara ya Afya kwa kuendelea kushirikiana kwa muda mwingi na kuahidi wataendelea kushirikiana kwa kujali Afya za watanzania pamoja na kuongeza msaada kwa Tanzania katika kudhibiti magonjwa na kulinda usalama wa watu duniani kote.

Dkt. Walensky amesema Kituo hicho hutumia ushahidi wa kisayansi katika kukabiliana na magonjwa hivyo ameishauri Serikali kupitia Wizara ya Afya kuongeza jitihada katika kufanya tafiti za kisayansi zinazohusiana na magonjwa na njia zinazotumika kukabiliana nayo.

Wizara Ya Maliasili Na Utalii Kuboresha Kanuni Za Uwindaji

$
0
0

Wizara ya Maliasili na Utalii imesema kuwa imepokea maoni yatakayosaidia kuboresha mapendekezo ya marekebisho ya Kanuni za Uwindaji wa Wenyeji nchini kupitia mifumo ya Kisheria iliyopo.

Akifungua kikao cha Wawindaji Wenyeji, Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe Balozi Dkt. Pindi Chana (Mb) amesema kuwa Serikali kwa kutambua umuhimu wa wenyeji kunufaika na rasilimali za wanyamapori kama ilivyoainishwa katika Sera ya Wanyamapori ya mwaka 2007, iliamua kuanzisha utaratibu wa uwindaji wa wenyeji ili kuwawezesha wenyeji na wageni wakazi kupata kitoweo cha nyamapori kwa utaratibu rahisi na kwa bei nafuu bila kuathiri dhana nzima ya uhifadhi endelevu.

“Serikali ilitenga maeneo ya wazi yatumike kwa ajili ya shughuli za uwindaji wa wenyeji kupitia utaratibu maalum ambao uliwekwa katika Kanuni za mwaka 2010” Amesema Mhe. Balozi Dkt Chana

Aidha, Waziri Balozi Dkt. Chana amewataka wadau hao kutumia fursa hiyo kutoa maoni ya kujenga na ambayo yatazingatia mahitaji na malengo ya uwindaji wa wenyeji kwa kuzingatia mustakabali mzima wa uhifadhi kwa manufaa na kizazi cha sasa na kijacho

Kikao kazi hicho kilichofunguliwa Jijini Arusha, kimejumuisha wataalam kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii, TAWA, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Wadau wa uwindaji wa wenyeji.

TECNO CAMON 19 Pro Yaongoza..... Yaishinda Vikali Infinix Note 12 VIP Katika Vipengele Vya Kamera, Kioo Na Muundo.

$
0
0

Mapema Julai, Kampuni ya Simu ya TECNO ilitangaza uzinduzi wa simu yake ya CAMON 19 iliyo na ubunifu wa picha kali za usiku kwa camera yake ya 64MP, bezel nyembamba ya 0.98mm na vipengele vingine vya kuvutia vinavyopendwa na mashabiki.



Muonekano wa TECNO CAMON 19 Pro

TECNO, kampuni ya simu inayotambulika kimataifa sasa imekuwa chapa ya simu mahiri inayoongoza kwa kufanya uzinduzi wa matoleo yake mbalimbali kwa kutumia teknolojia bora kwa watazamaji wake. TECNO pamoja na mawazo yake ya kibunifu na teknolojia ya hali ya juu inatoa mpambano mkali kwa washindani wake.


Sifa kuu za TECNO CAMON 19 Pro 5G

TECNO CAMON 19 PRO Vs INFINIX NOTE 12 VIP

KAMERA

Ikiwa na kamera yake kuu ya 64MP yenye lensi ya glasi ya RGBW iliyotengenezwa kwa ushirikiano na Samsung, kamera ya usiku ya CAMON 19 Pro inaweka viwango vipya vya kunasa kwa usahihi picha angavu katika mazingira ya mwanga hafifu. Hili linakamilishwa kwa kutumia mfumo ambao unaiga mwelekeo wa jicho la mwanadamu na kuruhusu uchakataji wa mwanga wa kipekee, pamoja na lenzi ya kioo ambayo huongeza upokeaji wa mwanga kwa zaidi ya asilimia 208 na kuongeza mwangaza wa picha kwa kiasi kikubwa. Sifa hii imemuacha mbali mpinzani wake Infinix Note 12 VIP yenye camera ya 108MP.


KIOO

TECNO imeendelea na umahiri wake wa kuthibitisha sifa kabambe katika simu zake kwa watumiaji. TECNO CAMON 19 Pro imekuja na bezel nyembamba zaidi yenye inchi 6.8 FHD+, ili kutoa utumiaji wa kina usio na kifani wakati Infinix Note 12 VIP ina kioo chenye 6.7 inches.


MUUNDO

Hata hivyo, TECNO CAMON 19 Pro inajulikana kwa muundo maridadi unaothaminiwa sana. Hapo awali, CAMON 19 pro ilishinda tuzo za IF Design kuwashinda washindani wake wote ikiwemo Infinix Note 12 VIP kwa muundo bora wa bidhaa kwa kuwa na fremu nyembamba sana na muundo mzuri wa kamera tatu za pete mbili na mipako inayofanana na almasi milioni 200 unaosaidia kuepuka uchafu wa alama za vidole. Hii ni tuzo ya kwanza ya TECNO katika shindano la kimataifa la ubunifu, na kuthibitisha kujitolea kwa kampuni hiyo katika uvumbuzi wa kiteknolojia na mafanikio endelevu.




BEI ya kununua

TECNO CAMON 19 Pro inauzwa kwa bei rafiki zaidi ya Tsh 660,000ikilinganishwa na Infinix Note 12 VIP ambayo inauzwa Tsh 820,000.




TECNO CAMON 19 Pro

Bei na Upatikanaji wa TECNO CAMON 19 Series

TECNO CAMON 19limekuja katika matoleo matatu ya CAMON 19, CAMON 19 Pro na CAMON 19 Pro 5G ambayo itawasili mwishoni mwa mwezi Julai. Bei ni Tsh 450,000 kwa CAMON 19 (128+4GB), Tsh 510,000 kwa CAMON 19 (128+6GB), Tsh 660,000 kwa CAMON 19 Pro, na Tsh 790,000 kwa CAMON 19 Pro 5G. Tembelea duka lolote la TECNO au duka la Vodacom ili kujipatia simu hii.

Agiza mtandaoni kupitia INALIPA;https://www.inalipa.co.tz/stores/tecno#/

Kwa maelezo zaidi piga namba;0744 545 254 or 0678 035 208.

 

Habari Zilizopo Katika Magazeti yaLeo July 28


Rais Samia Afanya Uteuzi wa Wakuu Wapya 9 wa Mikoa na Kuwahamisha Vituo Wengine

Rais Samia Afanya Uteuzi Makatibu Tawala wa Mikoa ( 7 ni Wapya, 10 Wamehamishwa)

Malalamiko ya TUCTA yawasilishwa serikalini

$
0
0


Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Nchini (TUCTA),  limewasilisha rasmi serikalini malalamiko yake ya kutoridhishwa na nyongeza ya mishahara kwa watumishi wa umma.

Malalamiko.hayo yamewasilishwa serikalini kwa njia ya maandishi.

Wakizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma, viongozi wa TUCTA wakiongozwa na Rais wa Shirikisho hilo Tumaini Nyamuhokya
wamesema, wameamua kuwasilisha malalamiko hayo baada ya kuwepo kwa sintofahamu katika nyongeza ya mishahara waliyolipwa watumishi mwezi huu wa Julai.

Wameongeza kuwa katika nyongeza hiyo baadhi ya kada na taasisi za umma hazijaguswa.

Shirikisho hilo la Vyama vya Wafanyazi Nchini limependekeza kuwa nyongeza ya mishahara kwa watumishi wa umma ni vema ikazingatia zaidi asilimia kuliko kiwango cha fedha.

Mei 14 mwaka huu Rais Samia Suluhu Hassan alitangaza ongezeko la mishahara kwa watumishi wa umma kwa asilimia 23.3.

Hata hivyo, baadhi ya wafanyakazi wamelalamikia kiasi cha fedha walichoongezwa, hatua ambayo imeilazimu TUCTA kuwasilisha rasmi serikali malalamiko hayo.

Tanzania Ni Mwenyekiti Na Mwenyeji Wa Mkutano Wa Tatu Wa Dharura Wa Baraza La Mawaziri Wa Nchi Zinazozalishwa Almasi Afrika.

$
0
0

Na Mwandishi wetu - Arusha

Tanzania Kama mwenyekiti na mwenyeji wa mkutano wa tatu wa dharura wa baraza la mawaziri wa nchi zinazozalisha almasi (ADPA) itakuwa na mkutano wa baraza la mawaziri kesho tarehe 29 julai 2022 katika kituo cha mikutano cha kimataifa cha Arusha.

Waziri wa Madini Dkt Doto Biteko amezungumza hayo leo jijini Arusha katika mkutano na wanahabari wakati akieleza nia na dhumuni la mkutano huo.

Waziri Dkt Biteko amesema kikao hicho kitatanguliwa na kikao cha kamati ya wataalamu ambacho kinakaa Leo kupitia taarifa na nyaraka na kabla ya kuwasilisha kwenye baraza.

"Lengo la mkutano huu pamoja na mambo mengine ni kuidhinisha nyaraka muhimu za ADPA zilizofanyiwa marekebisho ambazo ni katiba, kanuni na miongozo ya umoja huo na kuteua viongozi watatu wa Sekretarieti ambao ni katibu Mtendaji na manaibu wake wawili" - amesema Dkt Biteko.

Dkt Biteko amesema Jumuiya ya wazalishaji wa almasi afrika (ADPA) ilianzishwa kwa mujibi wa azimio la Luanda, Angola mnano  November 2006 na lengo kuu la kuundwa kwa ADPA ni kuzipatia nchi zinazozalisha Almasi Afrika jukwaa la kuzikutanisha nchi zote za Afrika katika kusudi moja la kuhakikisha rasilimali za madini hayo zinanufaisha nchi wanachama pia zinapokutana nchi wanachama zinazhirikiana uzoefu na ushirikiano katika nyanja anuwai za Sekta ya almasi.

Aidha Dkt Biteko amesema kuwa katika kipindi hicho chote Tanzania ni mwenyeji wa Jumuiya hiyo imekuwa ni heshima kubwa kwa kuwajibika kwa ajili ya marndeleo ya nchi, hususani katika usimamizi wa madini ya almasi ambapo kama ilivyoahidi nchi ya Tanzania Wakati ikikabidhiwa nafasi hiyo imewezesha kupitiwa Kwa mfumo wa jumuiya hiyo ikiwepo marekebisho ya katiba na kanuni pia miongozo mbalimbali ya jumuiya.

Aidha Dkt Biteko amebainisha kuwa Kama nchi imejifunza zaidi kuhusu usimamizi wa sekta hususani Kwa madini ya Almasi ambapo pia nchi wanachama na hata wasio wanachama walipata nafasi ya kuja kujifunza kuhusu namna Tanzania ilivyofabikiwa kuwaendeleza wachimbaji wadogo wakiwepo wa madini ya almasi na madini ya dhahabu na namna ambavyo Serikali ilivyoweza kusimamia mifumo inayohusisha mnyororo mzima wa shughuli za madini.

Waziri Mkuu Atoa Agizo Kwa Wakuu Wa Mikoa Ya Mipakani

$
0
0

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka wakuu wa mikoa iliyopo mipakani watekeleze maelekezo ya Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan ya kufanya ufuatiliaji wa watu waliounda vikundi visivyo rasmi vinavyosababisha migogoro katika sekta ya usafirishaji.

Amesema kuwa Serikali haitomvumilia mtu yeyote anayejihusisha na vitendo hivyo vilivyo tofauti na sheria na taratibu za nchi. “Ukifanya vitendo viovu utajiingiza kwenye migogoro, kuwa makini usijeingia kwenye mgogoro kwa kutumwa tu, tunazo sheria za nchi.”

Amesema hayo  Jumatano Julai 27, 2022 alipofanya ziara ya kawaida ya Kukagua mwenendo na shughuli za usafirishaji katika Halmashauri ya Mji wa Tunduma Mkoani Songwe.

Mheshimiwa Majaliwa amesema kuwa iwapo kuna changamoto yoyote katika sekta ya usafiri inayowahusisha madereva na waajiri wao wasisite kuziwasilisha Serikalini. “Kama zipo shida njooni sisi tutawapokea na kuwasikiliza ili kutatua shida zenu, malori yanayotoka na kuingia nchini yaachwe, tusijihusishe na migogoro ambayo inatatulika.”

Aidha, Waziri Mkuu amewapongeza madereva kwa kuamua kuisikiliza Serikali na kurejea kwenye shughuli za usafirishaji kama awali.

“Taifa linakua kiuchumi katika sekta nyingi ikiwemo sekta ya usafirishaji, kuzuia wengine kufanya kazi ya usafirishaji ni uhujumu uchumi, magari haya yanatuletea fedha, kwani yanahudumiwa na wananchi wengi ambao kwa kufanya hivyo wanajipatia fedha na kuendesha maisha yao”

Ameongeza kuwa sekta binafsi inashamiri zaidi nchini na kuwa ni sehemu ya ukuaji wa uchumi. “Serikali inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan inatambua na itaendelea kuweka mazingira mazuri ili Watanzania waendelee kunufaika, lengo ni kupanua uchumi kutoka kwa mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla”

Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, David Silinde amesema kuwa katika kipindi cha mwaka mmoja wa Rais Samia, Serikali imejenga shule katika kata 466 mpaka sasa na ujenzi wa vituo vya afya 234 nchi nzima”

habari Zilizopo Katika Magazeti yaleo August 1

Asilimia 97 Ya Watoto Wanaozaliwa Hunyonyeshwa Maziwa Ya Mama

$
0
0


Na.Catherine Sungura,Ikungi
Asilimia 97 ya watoto wanaozaliwa hunyonyeshwa maziwa ya mama, ikiwa asilimia 92 ya watoto hunyonyeshwa kwa kipindi cha mwaka mmoja na kuendelea.
Hayo yamebainishwa leo na Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu Mhe. Mwanaidi Khamis wakati akimwakilisha Waziri wa Afya Mhe Ummy Mwalimu kwenye uzinduzi wa maadhimisho ya wiki ya unyonyeshaji maziwa ya mama kwa watoto kitaifa yanayofanyika kwenye halmashauri ya Ikungi Mkoani Singida.
Mhe. Mwanaidi ameendelea kusema kuwa 43% tu ya watoto  ndio hunyonyeshwa hadi kipindi cha miaka miwili na kuendelea huku takwimu zikionesha 57% tu ya watoto ndiyo hunyonyeshwa maziwa ya mama pekee bila kuchanganya na chakula kingine wala maji ndani ya kipindi cha miezi 6.
 
“Tafiti zinaeleza kuwa mtoto akizaliwa na kuanza kunyonyeshwa maziwa ya mama ndani ya saa moja kunaweza kuokoa uhai wake kwani kuchelewa kumnyonyesha mtoto kuna changia kwa kiwango kikubwa vifo vya watoto wachanga ndani ya siku 28.” Aliongeza.
Aidha, amesema hapa nchini unyonyeshaji wa watoto wachanga ndani ya saa moja umefikia 90% hivi sasa ikilinganishwa na 54% iliyokuwa mwaka 2018 wakati utoaji wa Vitamini A kwa watoto wa miezi 6-59 nao umeongezeka kutoka 64% mwaka 2018 hadi kufikia 97% hivi sasa.
 
Hata hivyo Naibu Waziri huyo aliwahimiza wahudumu katika vituo vya kutolea huduma za afya kutoa huduma kwa wakati husika na kuwaasa wazazi kuendelea kuhudhuria Kliniki kama inavyoagizwa pia wazazi kuwanyonyesha watoto wachanga maziwa ya mama pekee kwa kipindi cha miezi sita bila kumlisha chakula kingine wala maji pamoja na kuwanyonyesha watoto kwa kipindi cha miaka miwili na zaidi. 
 
“Kunyonyesha maziwa ya mama kuna faida nyingi kwa mama na mtoto kwa kuwa kunaimarisha afya na ustawi wa mama na mtoto, vilevile unyonyeshaji watoto maziwa ya mama huzuia aina zote za utapiamlo kwa vile kuna kuwa na uhakika wa chakula kwa watoto wachanga na wadogo”. Alisisitiza
Vile vile amesema ili kuimarisha na kuendeleza juhudi za kulinda Afya ya watoto kupitia unyonyeshaji maziwa ya mama, Serikali itaendelea kufuatilia utekelezaji wa sheria, kanuni na miongozo iliyopo juu ya unyonyeshaji watoto maziwa ya mama, kuendelea kutenga fedha za kutekeleza afua za kuboresha ulishaji wa watoto ikiwemo elimu ya Afya, lishe na huduma za msingi kwa wanawake wajawazito na wanaonyonyesha pamoja na kutoa miongozo na taarifa sahihi kuhusu unyonyeshaji na namna ya kujikinga na magonjwa hasa ya mlipuko.
Naye, Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe. Jerry Muro amewataka wakurugenzi na watoa huduma ya Afya wa halmashauri yake kuendelea kutoa elimu juu ya unyonyeshaji na kuwasihi wananchi kuepukana na mimba za utotoni.
 
“Changamoto zinazopelekea wazazi kutonyonyesha watoto zao ni pamoja na mimba za utotoni kwakuwa hawajui umuhimu wa kunyonyesha na wengine kuwa bize na kazi na hivyo kuacha kunyonyesha watoto zao.” Amesema DC Muro
 
Aidha, Mkuu huyo wa Wilaya ametoa rai kwa Serikali kuongeza muda wa ruhusa kwa wazazi wanaofanya kazi ili kupata muda mwingi wa kuwanyonyesha watoto zao.
Maadhimisho hayo ya wiki ya unyonyeshaji maziwa ya mama kwa watoto kitaifa yanayofanyika kwenye halmashauri ya Ikungi Mkoani Singida kuanzia 1-7 Augusti 2022 yenye kauli mbiu isemayo CHUKUA HATUA ENDELEZA UNYONYESHAJI: ELIMISHA NA TOA MSAADA

Mnadhimu Mkuu Wa Jwtz Ajitambulisha Kwa Rais Dk.hussein Ali Mwinyi

$
0
0

 


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi (kulia) alipokuwa akizungumza na Mnadhimu  Mkuu wa  JWTZ (Chief of Stuff) Luteni Generali  Salum Haji Othman,alipofika Ikulu Jijini Zanzibar kujitambulisha  akiwa na ujumbe aliofuatana nao .[Picha na Ikulu] 01/08/2022

Rais Samia Azitaka Halmashauri Kusimamia Mapato

Kesi ya Zumaridi yapangiwa hakimu mpya

$
0
0


Hakimu Monica Ndyekobora ameondolewa kusikiliza shauri la jinai namba 12/2022 linalomkabili Diana Bundala maarufu kama Mfalme Zumaridi na wenzake 83 badala yake shauri hilo litasikilizwa na Hakimu Mkazi, Clescensia Mushi.

Jumatatu Agosti Mosi 2022 kesi hiyo imeitwa kwa ajili ya kusikiliza hoja kutoka kwa mawakili wa utetezi jambo ambalo halikufanikiwa baada ya Hakimu Mkazi, Clescensia Mushi kupanda mahakamani hapo na kutangaza kwamba shauri hilo limepangwa chini yake kuanzia leo huku akiitaarifu mahamakama kwamba atasikiliza shauri hilo kwa siku tatu mfululizo kuanzia Agosti 15 mwaka huu.

Bila kutaja sababu za Ndyekobora kuondolewa, Mushi aliagiza upande wa Jamhuri kupeleka mashahidi watatu siku hiyo ili kuendelea na usikilizaji wa ushahidi baada ya shahidi mmoja kati ya 20 wa Jamhuri kumaliza kutoa ushahidi wake chini ya Hakimu Ndyekobora.





Latest Images